Tempus Fugit
JF-Expert Member
- Jun 22, 2016
- 850
- 2,212
Niliitwa na jamaa yangu mmoja....akawa ananiambia kuna siku ataniita nije nione ujasiriamali aufanyao. Nikawa najaribu kudadisi nijue anajihusisha na nini katika biashara yake mpya? Jamaa akawa hataki kusema, akidai nitajua tu siku nikienda.
Kichwani nikaanza kujiuliza inawezekanaje kama mtu amefungua biashara na hataki watu waijue? Hapo tayari nikachezwa chale.siku ikawadia akanipigia simu jioni akanielekeza, nikafika ofisini.
Kwa nje inaonekana ni nyumba tu ya kuishi watu, kumbe ndani ni ofisi. Nikapokelewa na zile goodmorning etc...kuona mabango tayari nikawa nimewatambua. Qnet.
Kwenye semina nikasikiliza stori za mamilioni...then nikauliza swali kuwa toka nimeingia humo kwao sijaona Certificate of incorporation ya kampuni yao, sijaona TIN ya kampuni, sijaona leseni ya biashara n.k ktk mazingira hayo nawezaje kuwekeza kwenye entity ambayo haitambuliki?
Wakaanza kujikanyaga, mara walionyeshwa kwenye taarifa ya habari, mara waziri alikuja kuzindua ofisi yao, mara sijui gazeti liliwaripoti,...tayari nikahitimisha kuwa these people are after my hard earned money. Nilipoondoka sikurudi kwa semina ya pili.