Qatar Air Yanunua Hisa 25% Za South African Air Link

Kituko kikubwa zaidi ni pale wanapo fananisha ATCL (state owned) to Airlink ambayo ni kampuni binafsi. Wanafananisha machungwa na tufa.
Sawa na leo hii Precisoin Air Tanzania, wauze 50% kwa Qatar Air, ni wangapi watapiga kelele?
Siyo kituko biashara ni biashara tu, iwe private au public, ukiishiwa maarifa au mtaji unauza tu kuingiza maarifa na mtaji mpya.

Ya nini ung'ang'anie kuendesha biashara inayokupa hasara? Kwa mfano MWENDOKAKASI ya Tanzania kwa situation iliyonayo ? Kama ni mtaji tafuta? Kama siyo mtaji bali management, nayo unaweza kuitafuta kwa njia nyingi tu
 
Shida inaanzia kwenye udini,unadhani bandari ingepewa kampuni ya ulaya kungekua na kelele
 
Mkamdarasi kutoka UAE ankuja kuendesha Mwendokasi
 
Wewe hata kama una umri mkubwa bado mbumbumbu tu
Ungekuwa una fikiria vizuri usingefafanisha mkataba wa kampuni ambao uko wazi kwenye umiliki na usimamizi
Ambao uko clear 25% share

Na kituko Cha mkataba wenye Kona Kona nyingi haijulikana ni wanamilki Asilimia ngapi mipaka yao ya usimamizi haiko clear
 
Kwa hiyo wewe kipimo chako ni mdomo au kelele za watakao kuuliza kwa nini wauza shirika la umma? Kama unaogopa kelele za watu badala ya ubora wa maamuzi then wewe hufai kuwa entrepreneur!!

Vigezo vya kuendesha taasisi yeyote ya biashara ni profitability, period

Model ya BRT (Bus Rapid Transit) ni product ya World Bank na ilifanikiwa sana huko South America kupunguza congestion kwenye urban transport.

Tunachopaswa kufanya ni kuichukua wholly kama ilivyo na siyo kuchakachua
 
Unataka asilimia za nini kwenye model ya TPA ? Kwani Net Group Solutions alipokuwa anaendesha TANESCO miaka ya 2000-2006 kwa mfumo wa management contract Tanzania ilikuwa na share ngapi?

Sisi bado TPA ni mali ya Tanzania kwa 100% ila tumekodisha menejimenti ya operations za port, period
 
Ndo maana nikakuambaia kulinganisha mkataba wa Bandari na huu wa Qatar Airways ni
Dalili za kushindwa kufikiria vizuri

Hapo wenzenu wametafuta wawekezaji na sio wanyampara

Tpa imetafuta wanyampara wa mataifa mengine kuja kuwasimamia wao na watanzania wengine na watawalipa pia
Tena bila aibu walitaka kipengele Cha kutokuvunja mkataba
Pili hawakutaka mahakama za NDANI ziamue kesi zao

Usilazimishe mikataba ya watu wenye akili na vitu vya aibu
Tafuta mifano mingine
 
Wape jina lolote lakini wamekuzidi maarifa, mtaji, teknolojia na mzigo.. Ndiyo maana wanafanya biashara dunia nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…