Qatar Airways route za Dar/KIA analeta mikangafu!

1. Aisee, Emirates analeta A380? Kuanzia lini?

2. A800 ni toleo jipya? Sijawahi kuisikia
 
Korea na Lufthansa ndio operator wakubwa waliobakia. KLM naona anazo ila sijajua kama ni cargo au abiria pia.
 
Duh Jamii forum shikamoo! Nimepitia comments zote nimebaki nacheka hovyo yani wote humu mmepanda ndege!!! Mam*e kuna jitu linasema eti tulipanda dubai mpaka Barcelona tena inaweka na kwenye bracket "BNC", jingine eti lilienda China ikaongezeka na 800k aisee amkeni mtakojoa nendeni mkalime magimbi acheni kuota 🤣🤣🤣🤣🤪
 
Nakumbuka nililipa 800k zaidi Ili nipande A380 from Dubai tu Guangzhou and it was worth it. Ile ndege achana nayo
Wako vizuri ukiwa nje huko,Nilitoka Heathrow huduma ,misosi,pombe mule hamnaga uisilamu unatwanga whisky njia nzima na lile dege huwa halijai utakuta siti ya mtu tatu umekaa mwenyewe na hata kuhama unaruhusiwa.
Sasa umefika doha unakimbizwa mkuku kwenye vile vi atr vingalangala kwenda bongo.
Humo ndo unakutana na kila aina ya ukhanisi.
Na abiria km wa mbagala.
Nikakuta muhudumu mkenya kumwambia lete whisky alipiga kelele huyo utafkiri naiba.
Baadae anakuja kuambiwa huyo mpe tu katoka mbali huko kila kitu kimelipiwa.
Ndo katoa macho.
 
Yeah tiketi za kampuni nyengine zilikua bei rahisi lakini Emirates bei yao iliongeza Kwa 800k. Nililipa Ile nipande ndege kubwa kabisa Duniani A380 jumbo kmmk. Sema mbona ndege zinapandwa sana Mzee hata siku hizi ndege za Dodoma na mwanza zinajaaa kinoma
 
Hahah sio Atr mkuu ni Boeing zile narrowbody.
 
Jamaa huwa hawana Sajesheni boksi?,nadhani haya malalamiko ungehakikisha yanaufikia uongozi wa hilo shirika ungekuwa umetisha sana kwani ungewasaidia wengi!
 
Nilikuwa natania tu, hizo a380 nimeziona duabi international airport (DXB) japo sijawahi kuzipanda nilipanda fly Dubai kwenda Dubai then Kuwait 2016 Ila kwa kipindi hicho sikuwa mkubwa wa kuweza kufuatilia aina ya ndege ila ndege ya dubai to Kuwait imetulia sana nafkiri pia kwa sababu ya idadi ya abiria maana ndege za kuja huku abiria ni wachache sana hasa wengine wanashuka Zanzibar mpka unajiuliza ivi hizi kampuni hazipati hasara kweli
 
Jamaa huwa hawana Sajesheni boksi?,nadhani haya malalamiko ungehakikisha yanaufikia uongozi wa hilo shirika ungekuwa umetisha sana kwani ungewasaidia wengi!
Haisaidii lolote,wwakikufikisha doha shughuli imeisha utafika unakokwenda hasa Africa.
Watu weupe wakipanda Qatar ujue anaishia hapo hapo Doha haendi mbali.
 
Alipata isolated incident. Hii huwa inatokea kama ndege iliyopangiwa route inakuwa ina matatizo mnaletewa ya dharura...na huwa wanasema.

Nilipanda Boeing 777 ya Qatar kutoka JFK mpaka Doha dah! Siti pana, ndani kuzuri, entertainment safi na chakula cha kueleweka. Hata mimi ukiniambia nichague nitachagua KLM na Qatar always japo na wengine akina BA wapo....

By the way, mashirika ya ndege ya Kimarekani niliyowahi kupanda - Delta, United, NWestern, American...yote hayafai. Viti vimerundikwa, huduma mbovu ikiwemo chakula. Haya kama mtu una vihela afadhali hukoo Business class kama una lisafari lirefu!

Nasubiri siku nikipanda ndege za mashirika ya Asia - Indonesian Airlines, Thai, Korean, Malaysian, Japanese....nasikia wao wako level nyingine kwenye design na hospitality...
 
Hahaha wamerekani wenyewe hawayapendi hayo mashirika.
 
Mkuu nadhani point ya mtoa mada ni kuwa ndege zinazokuja Afrika (ukitoa Cairo, Johannesburg na Cape town) Ni mangalangala. Nimeshuhudia kupakizwa kwenye Ngalangala la Oman Air kutokea KIA-Dar-DOHA wakati tiket Ni Qatar. Kuanzia DOHA-LHR nikapanda pipa la maana. Business class ilikua full
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…