Qatar Airways route za Dar/KIA analeta mikangafu!

 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa huwa hawana Sajesheni boksi?,nadhani haya malalamiko ungehakikisha yanaufikia uongozi wa hilo shirika ungekuwa umetisha sana kwani ungewasaidia wengi!
Ukiingia kwenye website yao na uandike malalamiko yako ndio hakuna zaidi, ukipiga simu inakwenda Doha na huko hakuna msaada wowote, najua watu tunalalamika ukipiga simu ATC ( Air Tanzania )hakuna majibu lakini Qatar ndio wazembe kuliko ATC, ukifika Doha bora ukutane na wa Kenya wanaweza kukupa msaada lakini desk nyingi utakuta wa Hindi na ukitoa Pass ya Tanzania hesabu maumivu
 

Ethiopia hiihii ninayoijuwa mimi au nyingine. Hata bure hunipandishi.
 
Nimepanda mashirika mengi ila sijaona linalozudi SQ- Singapore airline- hawa Jamaa huduma zao, usafi wao, na chakula ndani ya Ndege ni full masinonda…
Changi airport pia ni safi sana - ni 5 start airport na Kwa kweli- nilitembelea ma super market Yao kujionea tu bila kuwa na nia ya kununua chochote, Ila nilivyotoka nilikuwa na lundo la shopping- hawa wa Singapore wanajua nini maana ya customer services/ care Kwa kweli… inabidi watu wetu wakajifunze huko…
 
Tatizo wachangiaji wengi ni wa economy ujue
 
Mleta mada nisaidie kidogo. Ndani ya Oman air wanatoa huduma za chakula na vinywaji kama Qatar airways au. Sababu napenda Qatar Kwa ajili ya beer za heinken za kopo.
 
Hawa wamanga wanatuchukulia poa Siku ya kuondoka tulipandishwa kwenye Ngalangala (chata la Oman Air) siti mbovu, in-flight entertainment hamna, Ila Doha-New York full chuma, siku narudi nako DOHA-Dar full kangafu limepauka mpaka rangi. Hii Imekaaje?
Umefika hujafika?
 
Huduma pale doha ni kweli 0,wako wahindi na wapakistani wengi sana.
Nilipata problem wakati wa kwenda na kurudi late.
Airport is too big,but no information.
Nimeenda kuboard naambiwa hatuna ticket yako nikaambiwa your flight is after us aisee.
Wakati iliyoandikwa ni hii na nikiikosa ina maana deal lote linakufa huko nnakoenda.
Ilibidi wapate attention baada ya kwenda customer service na kuwaambia kwamba kesho mtakua responsible na haya mambo .
Ndio nikapewa seat ndege ingine niunge night kwa night yaani nikafika kikao cha kwanza niko hoii.
Hiyo ni Qatar airways.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…