6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 3,952
- 8,807
- Thread starter
- #61
Ni maajab unashauri watu wavue bias, wakati wewe mwenyewe umeshindwa japo kiunafiki tu kuivua hiyo biazVua bias zote,
Ndomaana nasema wew binafsi umeshindwa kupretend japo hata kiunafiki tu ili usijulikane kama umeandika comment hii kwa lengo la kuipa Israel ubora isiokuwa nao hata chembe.jadili uwezo wa Israel na uhodari wake kwenye vita ya siku 12, namna Taifa dogo kama Israel lilivoendesha operation ngumu kama kuishambulia Iran na vituo vyake vya Nyuklia alafu replace Iran weka nchi yoyote ya Kiarabu
Kwanza usijifanye haujui kwamba Marekani nayo ilituma ndege ya kuisaidia Israel kushambulia vinu vya nyuklia vya Iran. Na hii ni baada ya Marekani kuona Israel yenyewe ilishindwa kufikia malengo ya shambulizi kutokana na ubora wa vinu na mahali vilipowekwa.
Pili unajifanya haujui kwamba Israel iliendesha vita vyake kwa msaada mkubwa wa kijeshi kutoka Marekani na kwa washirika wake wa Magharibi kama vile UK, Ufaransa, Ujerumani, Italy nk. Hata wakati wa makabiliano ya vita, hizo nchi nlizotaja hapo juu zikishirikiana na Saudia, Qatar yenyewe, vikosi vya kambi za Marekani vilivyopo Iraq na Jordan kwa pamoj zilishiriki kwa kiwango kikubwa kuilinda Israel ili kuhakikisha mashambulizi ya Iran hayafiki Israel, lakin walifeli pakubwa na kusababisha miji mingi ya Israel ikiwemo miji mikuu, ofisi za serikali na kambi za jeshi kushambuliwa kama vile hakuna mfumo wa Iron Dome wala THAAD.
Na kumbuka hiyo nchi ambayo Marekani, UK, Ufaransa na washirika wengine walipambana kuizuia ina vikwazo vya zaidi ya miaka 70! Je ingekuwa haina vikwazo vya kiuchumi, silaha na teknolojia kama Israel hali ingekuaje?
Au jiulize kama Israel ingewekewa vikwazo vya kiuchumi, na silaha japo kwa miaka 5 tu halaf iingie vitani na Iran ambayo ingekuwa haina vikwazo vya kiuchumi na silaha hali ingekuaje?
Kama tukiacha bias kama ulivyosema, tunawaza kusema ile ilikuwa vita ya Iran pekee yenye vikwazo vya kiuchumi na kijeshi, dhidi ya Israel isiokuwa na vikwazo vyovyote iliyoshirikiana na Marekani kisilaha na kijeshi kupambana na nchi moja, na bado wenyewe wakakimbilia kuomba poo bila lengo lao kubadilisha regime ya Iran kutimia.