Quality ya nguo za GSM na Waikiki siyo nzuri

Wazeee wa Karume na Kkoo bila shaka hii 3d haituhusu!

Hapo wala haituhusu wazee wa karume, memorial moshi, kahama, Mbeya Baba lao kwa mtumba mkali anzia jinzi, kadet, formsix, mashati, na wale wa mtumba wa viatu vya ulaya vya nairobi na wale wazee wa mtumba grade wa kampala sisi tunapita kimya kimya tu,
 
ComputersDAR fuata huu ushauri.

Kuongezea usinunue Nguo za Gsm nunua Nguo za Brand fulani ndani ya maduka Ya Gsm ama ndugu zake hao Gsm.

Mfano Msasani Mall ni wakala wa Brand nyingi za South kama Babyshop, Max, Splash, Anta, Ipanema etc so kinachofanyika pale Ingia Duka la Brand husika kununua. Ikiwa ni Duka la Gsm mwenyewe ina maana anaweza weka nguo yoyote ila ukiingia Max ama Babyshop ama Brand yoyote inayojulikana wanabanwa na mikataba kuweka Exactly Nguo za Standard fulani. Ni kama Cocacola ama Kfc mfano wake.
 
Hapo umepigwa sana kwa hiyo bei unapata 3-5
Unashangaa jeans ya mtumba kuuzwa 40K?ipo mitumba classical na hizo ronya za buku 10 10

Ipo suruali ya mtumba unakuta mtu ameishika unampa 60K anakataa wakati unalia akupunguzie anakuja mtu kitendo cha kuishika kujua material yake akianziwa 85 analipa 80k unabaki umeduwaa.
 
Nyie ndo mnapigwa afu mnajifanya wajanja
 
Acha ushamba unafuliaje nguo jik
Jik ni kwa ajili ya choo tu.
Eti zinachanika:
Maji ya chumvi
Sabuni za jik
Tena unaloweka
Unategemea zisichanike kweli
 
Nyie ndo mnapigwa afu mnajifanya wajanja
Tatizo letu binadamu ni kujifanya tunajua kila kitu.

Tukubaliane vipo unavyovijua wewe vipo ninavyovijua mimi mfano huwezi kukuta Levi's Jeans mtumba fresh from USA muuzaji amenunua balo Nairobi 2.7mill ukauziwa suruali Tsh 40,000/=

Na hiyo 80K nimekupa kama mfano tu kama wewe mtoto wa mjini hapa Dar miaka ya 2008 wakati mtaa wa Lumumba unawika kwa kuuza magari na kuwepo wale jamaa waliokuwa wanaimbwa imbwa kwenye bands mbalimbali nilishawahi kumuona jamaa akiitwa Kizaizai ananunua jeans moja kwa 150K na hababaiki huyo mtu anayemuuzia wewe mwenyewe unaogopa kumsogelea kwa vitu alivyobeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…