SEHEMU YA 31
“Its just a joke Austin” akasema Job
huku akicheka
“Job nadhani tumeongea mengi na
ninahitaji kuondoka kwani natakiwa
kumuhoji Dr Marcelo usiku huu.Kuna
mambo ambayo nahitaji kuyafahamu toka
kwake.Kabla sijaondoka kuna jambo
nataka nikuombe”
“ Jambo gani Austin?
“ Kwa hali ya mambo inavyokwenda
nahitaji kuhamisha makazi yangu na vile
vile natakiwa kumlinda pia Marcelo na
Monica.Pale mahala ninapoishi kwa sasa
tayari pamekwisha julikana kwa kuwa
katika nyumba hii hakuna mtu yeyote
anayeishi unaonaje endapo nitaweka
makazi ya muda humu mimi na Marcelo?
Hii ni sehemu salama na inaweza kunifaa
sana”
“Hakuna tatizo lolote katika jambo
hili Austin.Hata mimi nilikuwa nafikiria
jambo kama hilo Karibu tuishi sote hapa.Ni
nyumba kubwa ina vyumba vya kutosha
na usalama ni mkubwa.Hata hivyo kuna
jambo nataka ulifahamu” akanyamaza
kidogo na kusema
“ Sintarejea tena katika maisha yangu
ya uwazimu.Nimechoka kuishi maisha
yale.Nimeteseka sana Austin na
ninashukuru kwa ujio wako ambao
umenipa nguvu ya kuweza kuweka nukta
katika maisha yale magumu.Sikuwahi
kufikiri eti mtu kama mimi siku moja
nitaweza kuokota chakula majalalani,laini
imenilazimu kufikia hali hiyo ili
kuwakimbia
wanaonitafuta
waniue.Mwanzoni hawakuamini na
walikuwa nawaona wakinifuata na
kunichunguza ili wapate uhakika kweli
nimekuwa kichaa .Walinifuatilia kwa
miaka miwili ndipo walipokata tamaa
wakiamini kuwa kweli nimekuwa
kichaa.Uchungu nilio nao siwezi kuuelezea
Austin” Job akasema kwa hisia kali huku
machozi yakimtoka
“It’s ok brother,they‘ll all pay”
akasema Austin
“Sure they must pay.Kikubwa
ninachokitaka kwa sana ni kufahamu aliko
mwanangu kwani mateso yote haya
ninayavumilia kwa ajili yake.”
“Nakuhakikishia Job kati kati ya
sinema hii utafahamu alipo mwanao”
akasema Austin na wote wakacheka
“By the way,umewezaje kujenga
nyumba kubwa namna hii Job? Umepata
wapi pesa? Akauliza Austin.Job
akatabasamu na kusema
“Niliwahi kushiriki katika operesheni
moja huko Darfur kumtafuta mtu aliyeitwa
Hussein Hafidh Abdullah.Huyu ni kiongozi
wa ukoo mmoja na alikuwa anatafutwa
kwa kuchochea watu wa ukoo wake
kuvamia na kuwachinja kikatili watu wa
ukoo mwingine.Hussen alikuwa ni mtu
tajiri sana na ilituchukua muda kufahamu
maficho yake.Tulivamia nyumba yake na
yakatokea mapambano makali baina yetu
na walinzi wake,kati kati ya mapambano
hayo
Hussein
akafanikiwa
kutoroka.Tulipoipekua nyumba yake
tulikuta kuna chumba kimejazwa fedha
.Hatukuacha hata senti moja.Tulikuwa
watu kumi na tano,tukagawana fedha zote
na ndizo ambazo nilizitumia kujenga
jumba hili kwa siri bila ya mke wangu
kujua.Amarachi
ndiye
aliyekuwa
akisimamia ujenzi wa jumba hili wakati
nikiwa Darful hadi lilipokamilika kwa hiyo
hakuna mtu wangu yeyote wa karibu
anayefahamu kuwa jumba hili ni langu
zaidi ya Amarachi.Hii ni siri yako Austin
hatakiwi mtu mwingine kufahamu kwani
tulichokifanya haikuwa sahihi” akasema
Job na wote wakacheka.Job akamtembeza
Austin sehemu mbali mbali za jumba lile
kisha wakaagana
“Usiku wa leo nitakuwa na kazi moja
tu ya kufanya usafi humu ndani na kuweka
mazingira safi kabla hamjahamia humu”
akasema Job ,Austin akaondoka