QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 34



kutoa ruhusa ya kumuua mtu ambaye
amekwenda kinyume na jumuiya na ndiyo
maana nataka nishike nafasi ya uenyekiti
ili kusitokee mkwamo wa aina yoyote .Kwa
hiyo Boaz nitafutie huyo mtu wa kuifanya
hiyo kazi yangu” akasema Jeremiah halafu
wakaendelea na maongezi mengine na
baadae Boaz akaondoka kwenda
kupumzika
“Mhh !! hili jambo linakoelekea
limeanza kunitisha.Hii ni kama filamu ya
usaliti.Dr Richard ametusaliti wenzake na
kutuuza kwa mwanae Marcelo,Ernest
Mkasa amewasaliti Alberto’s na sasa
Jeremiah na wenzake wanataka kufanya
usaliti mwingine kwa kwenda kinyume na
makubaliano ya kikao chao cha
pamoja.Sifahamu nini mwisho wa filamu
hii lakini huko tunakoelekea si kuzuri hata
kidogo.Watu
wamechanganyikiwa
hawafikiri sawasawa.Mimi nadhani suluhu
pekee hapa ni kumuua rais ambaye ndiye
anayeonekana kuwa kikwazo.Tukiendelea
kumuacha hai hatujui nini malengo
yake.I’m confused!! Akawaza Boaz.Kwa
upande wangu nadhani nisijiingize sana
katika mambo haya ya Alberto’s bali
nijikite katika kujihakikishia usalama wetu
mimi na wenzangu.Tuhakikishe kitabu
kinapatikana na papo hapo tuanze kubuni
mikakati ya kuifanya biashara yetu
iendelee endapo mambo hayatakuwa
mazuri.Tunatakiwa tujenge uwezo wa
kuendesha mambo yetu bila ya
kuwategemea sana Alberto’s.Hata hivyo
nina uhakika mkubwa Alberto’s
hawatakubali kushindwa na Ernest.Nina
imani huko makao makuu yao hivi sasa
watakuwa wanapanga mikakati mikubwa
namna ya kufanya” akawaza Boaz na
kukumbuka kuwa alihitaji kuongea na
Wilson Mukasha.Akachukua simu na
kuzitafuta namba za Mukasha akapiga
“Boaz !! akasema Mukasha kwa
mshangao
“Hallo Wilson”
“Hallo Boaz.Nimestuka kidogo
,sikutegemea kama ungenipigia mida hii”
akasema Mukasha.
“Usistuke Mukasha.Unafahamu mimi
huja na kuondoka kama mvua.Samahani
kwa kukupigia mida hii .Bado uko kazini?
“Hapana nimefika nyumbani muda
huu”
“Poleni sana kwa mambo yaliyotokea
na yanayoendelea kutokea”
“Ahsante Boaz.Ni kweli kuna upepo
mbaya unavuma sasa hivi na hali si nzuri
sana” akasema Mukasha
“Hicho ndicho hasa kilichonirudisha
nyumbani haraka.Kwa namna mambo
yanavyokwenda unadhani yanaweza
yakatulia hivi karibuni? Akauliza Boaz
“Hapana sina uhakika Boaz.Hii ni vita
ngumu.Ernest amejipanga sana kwa
mapambano.Ni wakati wa kuwa
waangalifu mno”
“Nalifahamu hilo Wilson na tayari
tumekwisha
anza
kuchukua
tahadhari.Wilson kilichonifanya nikupigie
usiku huu ni kutaka kufahamu jambo
moja”
“ Jambo gani Boaz?
 
SEHEMU YA 35


Ni
kuhusu
Ernest
na
Austin.Unaweza kufahamu Ernest amempa
Austin kazi gani? Boaz akauliza
“Ernest ni mtu wangu wa karibu sana
na siri zake nyingi amekuwa ananieleza ila
kwa hili amekuwa mgumu kidogo
kunieleza.Ni siri yake na Austin pekee
kwani hata wanapozungumza hawataki
mtu mwingine awe karibu na asikie
wanachokiongea.Ninachoweza
kuhisi
lazima kuna jambo kubwa ambalo Austin
analishugulikia kwani ilimlazimu Ernest
kulipa ujira mkubwa ili Austin aweze
kumfanyia kazi yake.Kwa hiyo naweza
kusema kazi ambayo Austin anamfanyia
Ernest ni kazi yenye umuhimu mkubwa
sana kwa Ernest” akasema Mukasha
“Umesema kuna ujira Ernest
ametoa? Ni kiasi gani amemlipa Austin?
“Ndiyo kuna ujira ametoa lakini si
pesa ila kuna kitu kikubwa amemfanyia
Austin na ndicho kilichomfanya Austin
akubali kuifanya kazi hiyo ya Ernest”
“Alimfanyia jambo gani? akauliza
Boaz.Mukasha akavuta pumzi ndefu na
kusema
“ Alimtoa Linda mdogo wake Austin
gerezani nchini China.”
Boaz akahisi kama vile amemwagiwa
maji ya barafu ghafla gari likayumba
kidogo kwa mstuko alioupata ikamlazimu
kuegesha pembeni.
“Boaz are you there? Akauliza
Mukasha
“ Wilson I’m....I’m just shocked.Hii ni
taarifa ambayo imenistua sana.Amewezaje
kumtoa Linda?
“He’s a president kwa hiyo
ametumia madaraka yake kufanya hilo
liwezekane.Amebadilishana wafungwa na
seriali ya China.Kwa hiyo hivi sasa Linda
yuko huru” akasema Mukasha.Boaz
akavuta pumzi ndefu
“Wilson nimestuka sana.Sikutegemea
kabisa kama lingetokea jambo kama
hili.Yule binti anafahamu mambo yangu
mengi na anaweza akamueleza kaka yake
kila kitu kuhusu mimi kuwa ndiye
niliyemuingiza katika biashara hii ya dawa
za kulevya .Kwa hivi sasa yuko wapi?
“Kwa hivi sasa anaishi kwa balozi wa
Tanzania nchini China” akasema Mukasha.
“Wilson tafadhali naomba unishauri
nifanye nini? Linda hapaswi kuwa huru.Ni
hatari mno kwangu.Austin hapaswi
kufahamu chochote kuhusu mimi na
mambo yangu.Endapo atafahamu mambo
yangu basi tutakuwa maadui wakubwa na
kazi zangu nilizompa azifanye
hazitafanyika.Hiki ni kipindi ambacho
ninamuhitaji mno Austin.Kuna kazi nyingi
ambazo nahitaji azifanye” akasema Boaz
“Boaz kitu pekee ambacho unaweza
kukifanya hapa ni kumuua Linda”
“Wilson hilo si jambo rahisi hata
kidogo kwani kuingia katika ubalozi wetu
na kumuua Linda si jambo dogo.Hata hivyo
niachie mimi nitajua nifanye
nini.Ninahitaji kujua kitu kimoja ambacho
kinaweza kunipa picha .Wewe ndiye
uliyenitambulisha kwa rais.Mimi na yeye
hatukuwa tukifahamiana.Ilikuaje hadi
akafahamu kuwa mimi niko na Austin?
“Boaz I don’t think that’s
necessary.Kuna mambo mengi ambayo
tunapaswa tuyajadili kwa sasa na si suala
hilo” akasema Mukasha
“Wilson jambo hili ni muhimu sana
kwangu.I want to know the bottom of this.I
want to know how it started?
Wilson akavuta pumzi ndefu na
kusema
“ Ernest met with this woman...”
“ What woman? Boaz akauliza
“ Anaitwa Janet mwamsole.Huyu ni
rafiki wa siku nyingi wa Ernest na huwa
wanakutana mara kwa mara .Ni watu
wanaofahamiana kwa miaka mingi toka
wakiwa shuleni.Baada ya kutoka kuonana
na na Janet ndipo alipotaka nimtafutie mtu
mwenye sifa maalum amfanyie kazi yake
na ndipo nilipomkumbuka Austin.”
Akasema Mukasha
“Unadhani huyo mwanamke
alimueleza nini Ernest? Unahisi anaweza
kuwa na mahusiano na hiki alichokifanya
Ernest?
 
SEHEMU YA 36



Siwezi kuwa na uhakika sana wa
hilo labda tufanye uchunguzi” akasema
Mukasha
“Hakuna haja.Tujikite katika masuala
ya msingi.Kuna jambo nataka
kukufahamisha.Unamkumbuka marehemu
Dr Richard?
“Ninamkumbuka
uliwahi
kunikutanisha naye ukatutambulisha
lakini si kuwahi kuwa na ukaribu naye.”
“Usingeweza kuwa na ukaribu naye
kwa kuwa wewe si mwanachama wa
Alberto’s.Dr Richard alikuwa anahusika na
wafuasi wa Alberto’s pekee.Leo hii
nimeipata barua ambayo kabla hajafa
alimuandikia mwanae Marcelo.Katika
barua hiyo alimueleza kila kitu kuhusu
Alberto’s na sisi pia.Mwisho wa maelezo
yake akamtaka ahakikishe anapambana
kufa na kupona kuwafyeka Alberto’s na
sisi pia tunaojihusisha na biashara ya
dawa za kulevya.Alimuachia kitabu Fulani
ambacho kina orodha ya wafanya biashara
wote wa dawa za kulevya hapa nchini
,mahala walipo ,mali zao na hadi mtiririko
wao mzima wa fedha.Dr Marcelo
ametoroshwa na watu wasiojulikana na
mpaka
sasa
hatujui
yuko
wapi.Tunachofahamu ni kuwa hayuko
peke yake kuna watu anaoshirikiana
nao.Kwa hiyo hivi sasa ninajiandaa kwa
operesheni nzito kuhakikisha ninampata
Austin na hicho kitabu .Bila kumpata
Austin au hicho kitabu basi hatutakuwa
salama.Kuna watu ambao wanajipanga
kutuzimisha kabisa” akasema Boaz
“ Hizo ni taarifa za kustusha sana.Una
sehemu yoyote ya kuanzia kufanya
uchunguzi huo? Akauliz Mukasha
“Ninazo tetesi Fulani ambazo
ninazifanyia kazi .Nina imani ndani ya siku
mbili nitakuwa na jibu la uhakika
.Ninachokuomba Mukasha endelea
kufanya uchunguzi ufahamu ni kazi gani
ambayo rais amempa Austin.Ni muhimu
sana kwangu”
“Sawa Boaz mimi nitajaribu kufanya
uchunguzi wangu na chochote
nitakachokipata nitakutaarifu”
“Ahsante Mukasha.Kuwa makini sana
hasa katika nyakati hizi.Jitahidi kadiri
uwezavyo kuendelea kuwa karibu na rais
ili asigundue upande wako wa pili”
“Ahsante Boaz nitajitahdi” akasema
Wilson Mukasha na kukata simu.Boaz
aliyekuwa ameegesha gari pembeni ya
barabara akawasha gari akaendelea na
safari ya kurejea hotelini
“Habari ya Linda kutolewa gerezani
ni habari ambayo naweza kusema ni
mbaya zaidi.Yule binti anafahamu mambo
yangu mengi kwani nilikuwa namtumia
kimapenzi na kumuingiza katika biashara
ya dawa za kulevya.Endapo akipata nafasi
ya kumueleza Austin mambo anayoyajua
kuhusu
mimi
sijui
nini
kitatokea.Ninachotakiwa kufanya kwa sasa
ni kumuhimiza Austin anifanyie kazi zangu
haraka haraka na baada ya kumaliza I’ll
have to kill him.Sitaki apate nafasi ya
kuonana na Linda.Nikiruhusu hilo litokee
basi nimekwisha na Austin ataniua kwani
nmaamini lazima Linda amueleze kila kitu
wakionana .Austin must die” akawaza
Boaz
 
SEHEMU YA 37



ustin alirejea katika makazi yake
tayari ilikwisha timu saa saba za
usiku.Mara tu alipoingia ndani akaenda
moja kwa moja kubisha hodi katika
chumba
cha
Marcelo.Mlango
haukufunguliwa akaingiwa na wasi wasi
akaitoa bastora yake na kukinyonga kitasa
mlango
ukafunguka
akaingia
ndani.Marcelo alikuwa amelala usingizi
mzito
sana.Austin
akashusha
pumzi,akamfuata Marcelo na kumuamsha.
“Austin you are back” akasema
Marcelo kwa uchovu huku akipiga
mwayo.Austin akamtazama kwa makini na
kusema
“Marcelo huu si muda wa kulala
namna hiyo.Huu ni muda wa mapambano
ni muda wa kukesha macho .Ni muda wa
kujilinda .Si muda wote utakuwa na mimi
kwa hiyo unapokuwa peke yako unapaswa
kujilinda .Ni vipi endapo ni adui ndiye
aliyegonga mlango na akaufungua bila hata
ya kustuka? Don’t do that next time”
akasema Austin
“Nimekuelewa Austin.Hii imetokana
na hizi dawa ninazotumia zina nguvu
sana.I’m sorry it wont happen again”
akasema Marcelo
“Good!!! Akasema Austin na kwenda
kuketi katika kochi dogo lililokuwamo mle
chumbani
“Nilikuahidi kwamba tutaongea
nitakaporejea kwa hiyo naomba unisikilize
kwa makini sana.” Akasema Austin na
kumtazama Marcelo kwa makini sana
akasema
“Naitwa Austin January.Ni mtanzania
mwenye uraia wa Afrika kusini.Nimerudi
Tanzania kwa ajili ya kazi maalum”
akatulia kidogo halafu akaendelea
“Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa
nafanya kazi katika idara ya usalama wa
taifa kitengo cha ujasusi wa kimataifa
.Nimefanya kazi nyingi na za hatari
nilizotumwa na nchi yangu.Kazi ya
mwisho niliyoifanya ilikuwa kuongoza
kikosi
maalum
kilichokwenda
kuwakomboa watanzania waliotekwa na
wanamgambo wa Alshabaab nchini
Somalia.Katika operesheni hiyo nilipigwa
risasi na mmoja wa wenzangu
nilioongozana nao nikatelekezwa hapo na
kuchukuliwa
na
Alshabaab.Kilichosababisha nitake kuuawa
ni baada ya kugundua mpango wa kumuua
rais Ferdinand uliosukwa na watu ndani
ya serikali” akatulia na kumeza mate
akaendelea
“ Nilikombolewa toka kwa Alshabaab
na mtu mmoja anaitwa Boaz ambaye ni
baba wa mpenzi wangu Maria.Kwa msaada
wake nimefanikiwa kuanza maisha mapya
na yeye ndiye sababu mimi kuwa hapa
nilipo leo.Sikuwahi kurejea tena Tanzania
hadi hivi sasa nilipoitwa na rais kwa kazi
maalum.Jioni ya leo kama utakumbuka
nilikuomba uende chmbani kwako kwa
kujua kuwa rais amekuja.Hakuwa rais
kama nilivyotegemea bali alikuwa mlinzi
wake aliyekuwa ametumwa kuwaleta
wageni ambao ni Boaz na mpenzi wangu
Maria.Nilistuka sana kwani sikuwa
nimewatarajia kabisa.Boaz aliniomba
tuongee pembeni na akanieleza
kilichomleta.Amekuja kuniomba nimfanyie
kazi yake moja.Alinieleza kwamba aliwahi
kuwa na rafiki yake anaitwa Dr Richard
ambaye kwa sasa ni marehemu”
“Dr Richard ?!! ..Dr Marcelo akastuka
sana
“Ndiyo Dr Richard .Alisema kwamba
walikuwa na mahusiano ya kibiashara
.Walikuwa na miradi ambaye Dr Richard
walikuwa na miradi kadhaa ya pamoja
ambayo Dr Richard ndiye aliyekuwa
msimamizi mkuu.Alipofariki Dr Richard
alimuachia majukumu yote mwanae
anaitwa Dr Marcelo .”
“What??!! Dr Marcelo akazidi
kushangaa
“Subiri nimalize Marcelo” akasema
Austin
“Dr Macelo ndiye aliyekuwa
msimamizi mkuu wa miradi yote baada ya
 
SEHEMU YA 38



baba yake kufariki.Kwa mujibu wa
maelezo ya Boaz ni kwamba Marcelo
alibadilika na kutaka kujimilikisha miradi
ile ya ubia jambo ambalo
halikumfurahisha.Anadai
kwamba
Aliwatuma vijana wake wakamuhoji lakini
akawafyatulia risasi na wao ikawalazimu
wajibu na kumjeruhi kwa risasi akaenda
kulazwa hospitali lakini ghafla akatoweka
hapo hospitali alikokuwa amelazwa na
hajulikani yuko wapi .Boaz anadai kwamba
kuna kitabu ambacho Dr Richard
alimkabidhi Marcelo ambacho ndicho kina
maelekezo yote kuhusiana na miradi hiyo
ya ubia baina yao.Marcelo ametoweka na
kitabu hicho.Kazi aliyonipa Boaz ni
kumsaka Marcelo na kuhakikisha
ninampata
yeye
na
hicho
kitabu.Kunirahisishia kazi zaidi amenipa
majina ya watu wawili ambao ana uhakika
mkubwa kuwa wanafahamu mahala
ulipo.Ametaka niwateke ,niwatese
waonyeshe mahali alipo kisha
niwaue.Watu hao ni Daniel Swai na
mwingine anaitwa Monica Benedict”
“No!!...No!!...noo !! akasema Marcelo.
“Let me finish Marcelo” akasema
Austin.Uso wa Marcelo ulikuwa umeloa
jasho
“Nilimkubalia kufanya kazi yake kwa
hiyo hivi sasa niko katika zoezi la kumsaka
Marcelo.Natumai Marcelo ambaye Boaz
anamtafuta si wewe...”
“Austin please dont do it! Mimi
ndiye Marcelo ambaye huyo Boaz
anamtafuta.Dr Richard ni baba yangu na
kweli amekwisha fariki” akasema Dr
Marcelo .Kwa dakika mbili Austin na
Marcelo wakabaki wanatazamana
“Please don’t do it” akasema Marcelo
huku macho yake yakichuruzika machozi
“Boaz alipomtaja Dr Marcelo
nilistuka sana na nilifahamu moja kwa
moja kuwa ni wewe ila sikumueleza
chochote
kama
ninakufahamu.Ninachotaka unieleze kwa
ufasaha kabisa historia yako na mahusiano
yako na Boaz na kama alichokizungumza
Boaz ni kitu cha kweli .I need to hear the
truth..”
Dr Marcelo akafuta machozi na
kusema
“ Baba yangu marehemu Dr Richard
alikuwa ni daktari bingwa wa saratani na
vile vile alikuwa na uwezo mkubwa katika
mambo ya upasuaji.Ni daktari aliyejizolea
sifa kubwa kutokana na umahiri katika
kazi yake.Alinivutia sana kwa kazi zake na
mimi nikajikuta nikivutiwa kuwa daktari
.Naweza kusema kwamba sikutumia muda
mwingi kuwa na baba kwani mara nyingi
alikuwa ni mtu wa kusafiri katika nchi
mbali mbali mimi muda mwingi nilikuwa
masomoni.Nikiwa masomoni China
nilipigiwa simu kuwa baba ni mgonjwa
sana na anahitaji kuniona.Nilirudi haraka
sana kuonana naye.Hakuwa na matumaini
ya kupona hivyo akanieleza mambo
kadhaa ya muhimu ambayo alitaka
niyatekeleze baada ya yeye
kufariki.Alinipa vile vile kitabu
alichokisema ni mwongozo katika kazi
zangu za kitabibu.Alisema kwamba kila
nitakapokuwa na tatizo lolote katika kazi
yangu basi nitampata ufumbuzi wake
katika kitabu hicho.Alinipa vile vile namba
za simu akasema kwamba nizipige kabla
sijaanza kukitumia kitabu hicho ili niweze
kupewa maelekezo na huyo mtu aliyenipa
namba zake.Alinitaka nisikifungue kitabu
kile hadi atakapokuwa amefariki.Hata
baada ya baba kufariki sikuwahi
kukifungua kitabu kile wala kumpigia simu
huyo
mtu
aliyenielekeza
nimpigie.Nilikihifadhi kitabu kile katika
kasiki na sikuwahi kukigusa hadi hivi
majuzi nilipokuta kasiki langu
limefunguliwa na baadhi ya nyaraka zangu
zikachukuliwa likiwemo faili langu la
matibabu.Nilipochunguza
vizuri
nikagundua kwamba hata kitabu hicho
alichonipa baba nacho kilikuwa
kimechukuliwa.Jioni ya siku hiyo
nikapigwa risasi na watu nisiowafahamu
nashukuru madaktari walifanikiwa kuokoa
maisha yangu.Nikiwa hospitali nilimuona
mtu mmoja aliyewahi kuwa na urafiki na
baba na ambaye aliwahi kunionya kwamba
nisiwe na mazoea naye kabisa .Niliogopa
sana nikajua tayari maisha yangu yako
 
SEHEMU YA 39



hatarini ikanilazimu kuomba msaada kwa
mtu ambaye ninamuamini naye ni Monica
Benedict ambaye Boaz anataka umtafute
umpate.”
“Monica Benedict ? akauliza Austin
“Ndiyo” akajibu Marcelo
“Ok endelea” akasema Austin
“Nilimuomba Monica anisaidie
niweze kutoka pale hospitali bila mtu
mwingine yeyote kueleza sikutaka hata
ndugu zangu wafahamu.Monica aliahidi
kunisaidia lakini ghafla akapotea na
sikuonana naye tena hadi leo hii.Sielewi
nini kilitokea hadi David Zumo akapata
taarifa zangu akamuomba rais wa
Tanzania ambaye alikutuma wewe ukaja
kunitoa pale hospitali.Kwa hiyo Austin
simfahamu Boaz ,sijawahi kumuona na
wala baba hakuwahi kunieleza au kunitajia
jina kama hilo.Mambo yote aliyokueleza
siyafahamu na ninaweza kusema kwamba
si ya kweli.Nakuomba tafadhali usifanye
alichokuomba
ufanye.Usiwafanye
chochote Daniel na Monica,hawafahamu
chochote kuhusu mahali nilipo na zaidi ya
yote ni watu wangu wa karibu
mno.Naomba uniamini Austin” akasema Dr
Marcelo.Austin akamkazia macho Marcelo
kwa muda kidogo na kusema
“Ofcourse I believe you”
“Ahsante sana Austin kwa
kuniamini” akasema Marcelo
“Nilifahamu toka awali Boaz alikuwa
ananidanganya.Hapa lazima kuna jambo
linaendelea
ambalo
Marcelo
halifahamu.Kuna jambo limefichwa katika
hicho kitabu ambacho Boaz anaonekana
kukihitaji kwa gharama zozote.Boaz
asingeweza kufunga safari kuja kuniomba
nimfanyie kazi yake hii kama haina
umuhimu mkubwa kwake” akawaza
Austin akiendelea kumtazama Dr Marcelo
“Marcelo unadhani ni nani aliingia
chumbani kwako akafungua kasiki na
kuchukua kitabu na nyaraka zako
nyingine? Unaweza kumuhisi mtu yeyote?
Akauliza Austin
“Toka lilipotokea tukio lile
nimekuwa najiulza sana nani anaweza
akafanya kitendo kile? Nimetafakari mno
lakini mpaka sasa sina yeyote niyaweza
kumuhisi.
“Unahisi na nani nyumbani kwako?
“Ninahisi peke yangu ila ninaye
mfanyakazi wa ndani ambaye ni mtu
mzima anayejiheshimu na hawezi kufanya
kitu kama hicho.Huja asubuhi na
kuondoka saa kumi jioni.Hajawahi kuingia
chumbani kwangu hata mara moja.”
“Huna mke?
“Hapana sina”
“Je mpenzi ambaye huja na kuondoka
mara kwa mara?
“Hata mpenzi sina”
Austin akaonekana kushangaa
“ Marcelo nitafurahi endapo utakuwa
mkweli kwangu ili nitafute namna ya
kukusaidia.Right now I’m your only help.
So tell me the truth” akasema Austin
“Nimekueleza ukweli Austin,sina
mke wala mpenzi.Mbona unaonekana
kushangaa?
“Inashangaza kidogo kwa mtu kama
wewe kukosa mke au hata mpenzi.
“Sikiliza Austin ,sababu ya mimi
kukosa mke au mpenzi ni kwa kwamba
mimi ni mgonjwa.Ninasumbuliwa na kansa
ya damu kwa hiyo sitaki kujiingiza katika
mahusiano yoyote.Ila niliwahi kuwa katika
mahusiano na msichana mmoja anaitwa
Lily wakati fulani” akasema Marcelo
“Nini kilitokea?
“It didn’t work”
“Where is she now? Akauliza Austin
“I don’t know.Tulipoachana
hatukuwahi tena kuwasiliana “
Aliwahi
kuingia
chumbani
kwako?Anazifahamu namba za siri za
kufungulia kasiki?
“Tulikuwa wapenzi kwa hiyo
chumbani kwangu kulikuwa ni kama
chumbani kwake.Alikuwa akija mara kwa
mara.Kuhusu namba za kufungulia kasiki
hazifahamu”
Austin akafikiri kidogo na kusema
“Tell me about Monica Benedict.Una
mahusiano gani naye? Are you two dating?
“Mimi na Monica ni marafki wa
kawaida na hatuna mahusiano ya
 
SEHEMU YA 40


kimapenzi.Nimefahamiana na Monica siku
si nyingi .Daniel ndiye aliyenitambulisha
kwake na toka tulipoonana tumekuwa
watu wa karibu sana.” Akajibu Marcelo
“Inavyoonyesha Boaz anazo taarifa
zako zote.Kila unachokifanya anakifahamu
na ana uhakika mkubwa kwamba mmoja
kati ya hawa watu wawili Daniel na
Monica
anafahamu
mahala
ulipo.Inaonekana amekuwa anakufuatilia
au ameweka watu wa kukufuatilia kila
ukifanyacho bila wewe kufahamu.
Inaonekana anachokitafuta toka kwako ni
kitu kikubwa na ninahisi miongoni mwa
watu wako wa karibu kuna mtu
kapandikizwa ili kukuchunguza.Unapaswa
uchekeche akili na ujue ni nani ambaye
unahisi anaweza akawa ni pandikizi la
Boaz?
“Austin nakubaliana nawe kwamba
inawezekana katika watu wangu wa
karibu kuna mtu anayenichunguza lakini
nakuomba ufanye kila uwezalo kuwalinda
Daniel na Monica.Dont let anybody hurt
them especially Monica” akasema Marcelo
kwa msisitizo
“Nitajitahdi kadiri niwezavyo
kuwalinda hao rafiki zako lakini kuna
mambo mawili ninajiuliza .Kwanza kitabu
ulichopewa na baba yako ambacho Boaz
anakitafuta ambacho kimeibwa kwako
lakini Boaz hajakipata nani anacho?
Ninahisi aliyekichukua kitabu hicho hana
mahusiano na Boaz na ndiyo maana Boaz
hafahamu kama kitabu hicho
kimeibwa.Nini kilichomo ndani ya hicho
kitabu na kukifanya kiwe na thamani
kubwa namna hii? Jambo la pili najiuliza
rais wa Cngo David Zumo ameingiaje
katika suala hili? Marc......” Austin
akakatishwa na mlio uliotoka katika saa
yake ya mkononi
“Somebody is at the door” akasema
na wote wakashangaa
“ Una miadi ya kuonana na mtu usiku
huu ? akauliza Marcelo
“Hapana ni usiku mwingi tayari na
sitegemei mgeni yeyote.” Akasema Austin
na kuchukua kile kifaa kidogo mithili ya
simu ya mkononi alichokuwa amemuachia
Marcelo akakibonyeza na picha kutoka
katika
kamera
zikaanza
kuonekana.Kamera ya getini ilionyesha
kulikuwa na mtu amesimama,alikuwa ni
mwanamke.Austin akastuka na kuongea
kwa sauti ya mshangao
“ Maria?!!
“ You know her? Akauliza Marcelo
“ Amekuja kutafuta nini usiku huu?
Akajiuliza Austin halafu akamgeukia
Marcelo
“ Marcelo ujio wa Maria usiku huu
unanipa mashaka sana.Chukua bastora ile
niliyokupa na utajificha katika maua
karibu na mlango mkubwa wa kuingila
sebuleni.You are going to cover me.”
Akasema Austin wakatoka mle ndani na
kuelekea nje.Marcelo akajificha katika
maua kama alivyoelekezwa na Austin na
kwa tahadhari Austin akaelekea
getini.Akachungulia katika kijitundu
kidogo akamuona Maria akiwa
amesimama akisubiri kufunguliwa
geti.Hakukuwa na mtu mwingine hapo
 
SEHEMU YA 41



karibu.Taratibu na kwa tahadhari kubwa
Austin akaufungua mlango mdogo wa geti
na kutoka bastora ikiwa mkononi
“Austin don’t shoot!! its me Maria !!
akawahi kujitambulisha Maria baada ya
kuona namna Austin alivyotoka pale getini.
“Are you lone?
“Yes I’m alone.Nililetwa na gari ya
hotelini lakini tayari imeshaondoka”
akasema Maria .Austin akamtaka aingie
ndani haraka na kufunga geti
“I’m sorry Austin” akasema Maria
kwa sauti ya woga
“Twende ndani” akaamuru Austin na
Maria akamfuata .Dr Marcelo aliyekuwa
amejibanza katika maua kama alivyokuwa
ameelekezwa na Austin alihisi mwili
kuingiwa baridi baada ya kumtazama
mwanamke Yule aliyekuwa ameongozana
na Austin
“Lilian??!! Akajiuliza
“Sidani kama ninaota.Japokuwa ni
muda mrefu hatujaonana lakini macho
yangu hayanidanganyi that’s Lily.What is
she doing here? Amefahamianaje na
Austin? Ama kweli milima haikutani
binadamu hukutana.Baada ya miaka hii
yote kupita hatimaye leo ninakutana tena
na Lily! Akawaza Marcelo .Austin na Maria
walipoingia sebuleni,Marcelo akatoka
katika maua na kusogea mlangoni
akajibanza
kusikia
walichokuwa
wanakizungumza Austin na Maria
“Maria why are you here? Why are
you back? akauliza Austin mara tu
walipoingia sebuleni.
“Maria !!!...Her name is Maria? Mbona
mimi namfahamu kwa jina la Lilian?
Halafu ana jina lingine anaitwa Shamim”
Dr Marcelo akazidi kushangaa.
“Nisamehe Austin lakini imenilazimu
kurudi tena.I need answers.What are you
doing here and why you don’t want me to
be here with you? What are you hiding?
akauliza Maria huku macho yake
yakiingiwa machozi.Kabla Austin hajajibu
kitu Marcelo akaingia pale sebuleni.Austin
na Maria wakastuka wote wakageuka na
kumtazama.
“Lilian !! akasema Marcelo
“Marcelo !! akasema Maria kwa sauti
yenye kitetemeshi.Alionekana kustuka na
kuogopa sana.
“Do you know him? Austin akauliza
kwa mshangao.Maria akaitika kwa kutikisa
kichwa.Wote
watatu
wakabaki
wanatazama
“Habari yako Lily.Habari za miaka
mingi?Akasema Dr.Marcelo huku
akitabasamu kwa mbali.Kabla Maria
hajafumbua mdomo wake kujibu chochote
Austin akauliza kwa mshangao
“ Lilian ?
Austin na Marcelo wakatazamana
kisha Marcelo akasema
“Austin tunaweza kuzungumza
pembeni tafadhali?
“Sure” akajibu Austin kisha
wakaingia katika chumba cha pembeni
chenye mlango wa kioo
“Marcelo umefahamiana wapi na
Maria? Akauliza Austin
“Ni hadithi ndefu kidogo lakini mimi
na Maria tuliwahi kuwa na mahusiano ya
kimapenzi.Huyu ndiye mwanamke ambaye
nilikueleza kuwa niliwahi kuwa naye
katika
mahusiano
lakini
tukaachana.Ninamfahamu kwa jina la
Lily.Ni muda mrefu hatujaonana hadi
nilipomtia machoni usiku huu.Anafanya
nini hapa? Akasema Marcelo.Austin
alionekaa kushanagzwa na habari ile ya
Marcelo.
“Huyu haitwi Lilian anaitwa
Maria.Huyu ni mtoto wa Boaz mtu
anayekutafuta kwa udi na uvumba na
ndiye mpenzi wangu kwa sasa.Huyu ndiye
aliyemshawishi baba yake anikomboe toka
Alshabaab kwa kiasi kikubwa cha fedha”
akasema Austin na wote wakaendelea
kutazamana.Marcelo akasema
“Umesema anaitwa Maria”
“Ndiyo anatwa Maria”
“Hii imenishangaza kidogo kwani
mimi ninamfahamu kwa jina la
Lilian.Ninazihamu nyaraka zake zote zina
jina la Lilian Bakile.Pasi zake za kusafiria
,kadi zake za benki,na vyeti vyake
mbalimbali vyote vinaonyesha kwamba
jina lake ni hilo.Kitu ambacho
 
SEHEMU YA 42


kilisababisha mimi na Lily kushindwa
kuelewana na hatimaye kutengana ni pale
nilipogundua kuwa ana pasi nyingine ya
kusafira yenye jina la Shamim.Nilipohoji
kuhusu hilo ukaibuka mkwaruzano na
tukatengana.Nimestuka kidogo kusikia
anaitwa Maria. ” Akasema Marcelo
Austin akainama akafikiri kidogo na
kusema
“Nimeshangaa sana kwanza
sikufahamu kama wewe na Maria
mnafahamiana na kwamba mpenzi wangu
aliwahi pia kuwa mpenzi wako.Mimi
ninamfahamu kwa jina la Maria .Nyaraka
zake zote zinaonyesha anaitwa Maria Boaz
Abrahams. Kwa hili uliloniambia kuna taa
nyekundu
imewaka
kichwani
kwangu.Kuna kitu Maria anakificha.Kwa
nini awe na majina zaidi ya moja? Nadhani
kuna ulazima wa kumfahamu
vizuri.Nadhani bado sijamjua vizuri mtu
ninayedhani ni mpenzi wangu.Ahsante
Marcelo kwa kunifumbua macho” akasema
Austin
“Tutafanya nini Austin? Huyu ni
mtoto wa Boaz na tayari amekwisha niona
na akitoka hapa lazima ataenda kumueleza
baba yake kuwa niko hapa.Naomba
unisaidie Austin”
“Usijali Marcelo.She wont get out of
here”
Austin akafungua mlango na kutoka
akamuendea Maria na bila kupoteza hata
sekunde akatoa bastora na kumuelekezea
Maria
“Nataka unieleze what’s your real
name? Are you Maria,Lilian or Shamim?
Akauliza Austin kwa ukali.Maria hakujibu
kitu akabaki anamtazama Austin kwa
woga.
“Answer me !! what’s your real
name? akauliza tena Austin kwa ukali
lakini Maria hakujibu kitu akabaki
anatetemeka .Austin aliyekuwa amefura
kwa hasira akamnasa kibao kikali Maria
“Answer me !! akasema Austin.Maria
hakujibu kitu akaendelea kulia.Austin
akamuinamia pale sofani
“Nafahamu unanidanganya kuhusu
mambo yako mengi lakini leo ni siku yako
ya kunieleza ukweli, wewe ni nani? I don’t
care how much you love me but I want to
hear the truth.Kwa nini uwe na jina zaidi
ya moja? Kwa nini una pasi zaidi ay moja
za kusafiria? Jina lako halisi ni
lipi?Usiponieleza ukweli nakuhakikishia
nitakufanyia kitu kibaya sana.Look at me !!
Look at me ! akasema Austin kwa ukali na
kumlazimisha Maria amtazame usoni
“Right now,I’m not Austin you
know.I’m at work and when I’m doing my
job I become a monster so if you don’t tell
me the truth I’ll do smething very painfull
to you.Usinilazimishe nikufanyie hivyo
Maria tell me who are you ?Kwa nini
ubadilishe majina ? akauliza Austin lakini
Maria hakujibu kitu akaendelea kulia
“Maria tafadhali usinilazimishe
nikufanyie jambo ambao sikuwa
nimekusudia kulifanya.Niambie ukweli
kuhusu wewe.”
“Austin give her a chance to expl....”
Marcelo akataka kusema kitu lakini Austn
akamzuia
“Marcelo nenda chumbani kwako
kajiandae.We’re leaving this place”
akasema Austin halafu akachukua waya
akamfunga Maria mikono na miguu na
kumfunga kitambaa usoni.
“Austin why are you doing this to
me? Akauliza Maria huku akilia
“I warned you don’t come to Dar es
salaam because I didn’t want this to
happen to you.Now I don’t have a choice I
have to do this.Wewe utakuwa chanzo cha
kupata kile ninachokihitaji”
“Nani kakubadilisha namna hii
Austin hadi ukanifanyia haya? Nini
unakitafuta toka kwangu?
“The ruth !! akasema Austin kwa
ukali
“I want to know who you real are?
Kwa kuwa umekuwa mgumu wa kunieleza
ukweli unanifanya niamini kwamba kuna
mambo mengi ambayo bado umenificha
kuhusu wewe .Inaniuma kukufanyia hivi
lakini hata kama angekuwa ni mama yangu
mzazi lazima ningemfanyia hivi.I don’t
have a soul whem I’m doing my job”
akasema Austin na kupanda kwa hasira
ghorofani akakusanya vitu vake vyote vya
muhimu akavipakia katika gari halafu
akambeba Maria na kumpakia katika gari.
Akamuamuru Dr Marcelo aingie garini
wakaondoka
Austin akaongeza sauti ya muziki
hakutaka kusikia Maria alivyokuwa akilia.
“ I hate this job.Sikufikiria kama siku
moja nitamfanyia hivi mwanamke
ninayempenda .Maria ni sababu ya mimi
kuwa hapa nilipo leo lakini hayo yote
lazima niyaweke pembeni kwanza kuna
vitu ambavyo natakiwa kuvifahamu toka
kwake.Kwa nini awe na majina
matatu?Kwa nini hajawahi kunieleza
kuhusu majina yake mengine? Kuna kitu
gani anakificha na ambacho hataki
kukiweka wazi? Ninahisi kuna jambo
haliko sawa hapa.Ngoja nitaufahamu
ukweli kabla hakujapambazuka” akawaza
Austin
 
SEHEMU YA 43


Wilson Mukasha alishindwa kupata
usingizi akainuka na kwenda kusimama
kibarazani.Alionekana kujawa na mawazo
“Rais amempa kazi gani Austin? Si
kawaida yake kunificha jambo lolote lakini
katika hili ameniweka pembeni.Kwa nini
hataki nifahamu kazi aliyompa Austin?
Amehisi nini hadi asinishirikishe katika
jambo hilo wakati mimi ndiye
niliyemsaidia akampata Austin? Sina
hakika kama atakuwa amehisi kitu juu
yangu kwani endapo angekuwa amehisi au
kusikia kitu chochote basi asingefikiria
kunichagua kuwa waziri mkuu wa
Tanzania.” Akawaza Mukasha
“ Ujio wa Austin umekuwa kama na
mkosi kwani ni baada ya yeye kuja ndipo
rais alipobadilika ghafla.Sifahamu nini
kinaendelea kati yao lakini nahisi lazima
Austin atakuwa anahusika katika
mabadiliko haya ya ghafla ya rais.Jambo
hili si la kupuuzia kwani bila kuchukua
tahadhari mambo mengi yanaweza
yakafichuka hapa.Nimeanza kuwa na wasi
wasi sana na Austin.Nitachunguza nijue
kazi anayoifanya hapa Tanzania na
nikitaka kujuia ni kazi gani natakiwa
kumuhoji Janet kwani baada tu ya rais
kutoka kuongea naye ndipo alipoanza
kumtafuta mtu mwenye sifa kama za
Austin.Nina hakika Janet kuna kitu
atakuwa anakifahamu” akawaza Mukasha
*********************
Austin aliwasili katika makazi ya Job.
“Job imenilazimu kuja mapema zaidi
ya nilivyotegemea” akasema Austin baada
ya kushuka garini
“Hakuna tatizo Austin.Hapa
unakaribishwa muda wowote.Nini hasa
kimetokea?
“Something happened Job.Tutaongea
baadae lakini ndani ya gari kuna watu
wawili ambao nitakuwa nao hapa”
akasema Austin na kuufungua mlango wa
gari na kumtaka Marcelo ashuke
“Huyu anaitwa Dr Marcelo” Austin
akamtambulisha Marcelo kwa Job halafu
akamfungua Maria kitambaa usoni na
waya aliomfunga miguuni akamuamuru
ashuke
“Huyu anaitwa Maria” akasema kwa
ufupi kisha wakaingia ndani
“Austin you are a devil.Sikutegemea
kama siku moja ungeweza kunifanyia
hivi.Yaani kukupenda kwangu kumbe
nilifanya kosa na leo hii unanifanya mimi
kama mhalifu? Nilifanya kosa kubwa sana
kukupenda shetani kama wewe.I swear
Austin you’ll pay for this..!!!! akasema kwa
hasira Maria
“Shut up !!! Austin akafoka
Austin akawataka Maria na Marcelo
waketi pale sebuleni halafu yeye na Job
wakapanda ghorofani.
“Austin what’s going on? Who is that
woman? Job akauliza.Austin akavuta
pumzi ndefu na kusema
 
SEHEMU YA 44



Anaitwa Maria.Ni mtoto wa Boaz na
ndiye mpenzi wangu niliyekueleza awali”
“Your girlfriend? Nini kimetomkea
hadi akawa katika hali ile?
Austin akamsimulia Job kila kitu
kilichotokea
“ Dah ! Austin una akili nyepesi sana
ya kutambua mambo.Ninakubaliana nawe
kuwa hapa kuna kitu kimejificha.Haiingii
akilini awe na majina mawili tofauti,awe
na pasi zaidi ya moja?.Kuna kitu gani
anakificha? Ni vipi endapo atakuwa na
majina zaidi ya hayo matatu? Tunapaswa
tumchunguze huyu mpenzio.Inawezekana
yeye na baba yake kuna mambo
wanayafanya.” Akasema Job
“ Boaz ndiye pekee ambaye anaweza
akatupa taarifa tunazozitaka kuhusiana na
Mukasha na ili kumfanya Boaz atupe
tunachokitaka tunatakiwa kumtumia
Maria .Anampenda mno mtoto wake na
hatakubali jambo lolote limtokee Maria
kwa
hiyo
atatueleza
kile
tunachokitaka.Kesho nitampata Boaz na
atatueleza kila kitu.” Akasema Austin
Job akamtazama Austin kwa makini
na kusema
“Austin are you sure about this?
What we’re going to do is not easy so you
must be sure that you are going to hurt the
woman you real love.”
Austin akavuta pumzi ndefu na
kusema
“ Yes ! I’m sure”
Job akamuongoza katika chumba
maalum cha mahojiano kilicho ndani ya
jumba lile.Ni chumba kilichojengwa kisasa
sana kiasi kwamba ukiwa nje unaweza
kumuona mtu aliyemo ndani kupitia kioo
maalum bila ya yeye kukuona.
Sebuleni Dr Marcelo alikuwa ameketi
akitazamana na Maria.Hakuna aliyekuwa
akimsemesha mwenzake.Bastora ambayo
Marcelo alipewa na Austin kwa ajili ya
kujilinda ilikuwa mezani.
“Marcelo
nimefurahi
sana
kukuona.Ni
muda
mrefu
hatujaonana.Nimekuwa nakukumbuka
sana lakini sikujua ningekuona vipi.kwa
sasa mimi makazi yangu ni afrika ya kusini
na huja mara chache hapa Dar es salaam
kibiashara.Umefahamiana vipi na Austin?
Maria akauvunja ukimya uliokuwepo pale
sebuleni
“ Shut up lily !! akasema Marcelo
“ Marcelo tafadhali usinifanyie
hivi.Usiwe kama Austin .Tena nakushauri
Marcelo usiwe na urafiki na huyu mtu he’s
a monster.Siamini kama anaweza
akamfanyia jambo kama hili mwanamke
anayempenda.Kwa taarifa yako mimi
ndiye sababu ya yeye kufika hapa alipofika
leo lakini ameyasahau hayo yote na
ananifanyia hivi.Sintomsamehe kamwe
katika maisha yangu” akasema Maria huku
akilia machozi.Marcelo akaonekana
kuguswa na kumuonea huruma.
“Lilian pole sana .Lakini kwa nini
usimueleze ukweli kuhusu wewe na
mkayamaliza mambo haya? Anakupenda
sana na haachi kukuzungumzia kila dakika
lakini umemchanganya wewe mwenyewe
kutokana na utata wa majina yako.Hata
mimi umenishangaza sana.Who you real
are? Akauliza Marcelo
 
SEHEMU YA 45


akati nikiwa nawe nilikufahamu
kama Lilian baadae nikagundua jina lako la
Shamim na sasa unaitwa Maria ,what’s
your real name? Did you change your
name? haya ndiyo mambo ambayo Austina
anahitajiku yafahamu .Funguka na mambo
haya yatamalizika amani itakuwepo.Hata
mimi sifurahi kukuona katika hali hii”
akasema Marcelo.Maria akamtazama kwa
huruma na kusema
“Fine.Nitawaeleza kila kitu .Mnataka
ukweli basi mtaujua lakini naomba
kwanza unifungue nikajisaidie.Nimebanwa
sana” akasema Maria huku akiibana miguu
kuonyesha namna alivyobanwa.
“ Siwezi kufanya hivyo.Wasubiri
akina Austin wanakuja sasa hivi” akasema
Marcelo
“Marcelo
nimebanwa
sana
tafadhali.Usiniache nikajisaidia hapa .Mimi
si mhalifu na sistahili kufanyiwa
hivi.Nimesema nitawaeleza kila kitu kwa
hiyo basi naomba unifungua Marcelo
nikajisaidie.Una bastora hapo ,itume
endapo nitafanya jambo lolote la
kipuuzi.Ninakwenda kujisaidia na
nikimaliza utanifunga kamba zenu.”
Akasema Maria.Marcelo akamtazama kwa
wasi wasi mwingi
“Amebanwa sana na halitakuwa
jambo jema kumuacha akajisaidia
hapa.Ngoja nimfungue akajisaidie”
akawaza Marcelo na kwenda kumfungua
Maria waya aliofungwa mikononi.
“Thank you Marcelo for this.You are
real a gentleman.Show me the toilet”
akasema Maria na Mara tu Marcelo
alipogeuka bila kutarajia akajikuta
amepigwa pigo zito kichwani lililompeleka
chini na kumpoteza fahamu. Haraka
haraka akaichukua bastora iliyokuwa juu
ya meza.
“Its my turn now.He wants to know
who I am and now the time has come to
know who I real am” akasema Maria kwa
sauti ndogo na kwa tahadhari akaenda
kuchungulia dirishani
“Sioni mtu yeyote nje.What is this
place? I need to get out of this place now
before these monsters comes down”
akasema Maria kwa kunong’ona na kwa
haraka akaenda mlangoni akakinyonga
kitasa kwa lengo la kuufungua mlango
“Stop right there !! ikasema sauti kali
ya Austin aliyekuwa amesimama katika
ngazi akitokea ghorofani.
“Slowly put your gun down and push
it to me !!!.akasema Austin kwa sauti kali
Taratibu Maria akaushusha chini
mkono uliokuwa na bastora kwa lengo la
kuiweka chini kama alivyoamriwa lakini
kabla bastora ile haijagusa chini kukatokea
kitendo ambacho Austin hakuwa
amekitarajia.Kwa wepesi wa aina yake
Maria akageuka na kuvurumisha risasi
upande aliokuwa amesimama Austin
ambaye alianguka huku akivuja
damu.Bastora yake ikifuka moshi Maria
akamuendea Austin aliyekuwa amelala
akivuja damu,machozi yakamtoka
“I’m sorry my love.Sikutegemea
kama siku moja tungefika hapa.Ni afadhali
nikuue kuliko kukupa nafasi ya
kunifahamu mimi ni nani.I love you Austin
and God will forgive me for what I’m going
to do” akaema Maria kwa sauti ndogo na
kuelekeza bastora katika kichwa cha
Austin na ukasikika mlio wa risasi.






AUSTIN ANAPIGWA RISASI NA
MPENZI WAKE MARIA,NINI HATIMA
YAKE? MARIA NI NANI NA KWA NINI
HATAKI AUSTIN AMFAHAMU?
MCHAKATO WA NDOA YA RAIS
DAVID ZUMO NA MONICA BENEDICT
UMEANZA ..JE WATAFANIKIWA LENGO
LAO?
MPENZI MSOMAJI KUPATA MAJIBU
HAYA NA MENGINE MENGI USIKOSE
QUEEN MONICA SEASON 4
 
NILIKUWEPO AHADI YANGU NIMEIKAMILISHA MABOSS ZANGU PAMOJA SANA WACHA TUIVUTIE SUBIRA SEASON 4.
Salute LEGE nisipokushukuru nitakuwa very selfish.... Keep it up mkuu!!!!!!!!!!!!!!
 
Shukrani sana mkuu.
Hiyo ya 4 sijui ndo mpaka link.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…