SEHEMU YA 13 : SEASON 5
Macho ya Ernest Mkasa rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania
yaliekezwa katika saa ya ukutani
akihesabu dakika na sekunde
zilizobaki kufika saa kumi na mbili za
jioni.Ilipotimu saa kumi na mbili na
dakika mbili simu ikaita haraka
haraka akaipokea
“ Hallow Habib” akasema rais
“ Mheshimiwa rais nilikuahidia
kukupigia simu leo saa kumi na mbili
nimetimiza ahadi yangu.Nilikupa
muda wa kutosha wa kutafakari ombi
langu na nina imani hivi sasa tayari
unalo jibu la kunipa”
“ Habib nimetafakari sana na
nimefanya maamuzi” akasema rais na
kunyamaza
“ Nakusikiliza mheshimiwa rais”
“Nitawapa kile mnachokihitaji”
“ Vizuri sana.Navihitaji vitu
vyote kesho.Nataka kabla ya saa kumi
za jioni Yasmin na Tariq wawe
wametua katika uwanja wa ndege wa
Aden Adde Mogadishu.Watakapotua
Yasmin awe na hati ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar
mkononi.Wataalamu wetu
wataifanyia kazi ili kuhakikisha ni
halisi na nitakupa jibu kama ni halisi
na kisha tutaendelea na mipango
yetu.Endapo haitakuwa hati halisi
makubaliano yetu yatakuwa
yamekufa na utakuwa umetangaza
vita na sisi na nchi yako itamwagika
damu kwa miaka mingi.Kama
ujuavyo mheshimiwa rais kwamba sisi
tukiingia katika vita na taifa fulani
basi vita hiyo hudumu kizazi hadi
kizazi kwa hiyo ni vita
isiyokwisha.Tafadhali usithubutu
kutufanyia uhuni wa aina yoyote.”
Akasema Habib
“ Usihofu Habib nitawapa hati
halisi na hakuna uhuni wowote
utakaofanyika.Tafadhali naomba
makubaliano yetu yaheshimiwe”
“ Hilo halina tatizo mheshimiwa
rais.Ukienda sawa na makubaliano
yetu basi hakuna
kitakachoharibika.Nitaarifu pindi
Yasmin na Tariq watakapokuwa
huru” akasema Habib na kukata
simu.Rais akachukua kitambaa na
kujifuta jasho
“I’m not sure if I’m doing the
right thing but I have to do
it.Nitawapa Alshabaab wanachokitaka
ili mipango yangu iende kama
ninavyotaka.Lazima Alberto’s wote
niwafagie hapa nchini na hii ndiyo
itakuwa gharama yake.Potelea mbali
litakalotokea na litokee tu lakini
lazima nihakikishe mashetani hawa
wanafutika hapa Tanzania.Baada ya
hapo nitawashughulikia akina Austin
kwani mpaka muda huo tayari
nitakuwa nimepata majibu ya kipimo
cha vinasaba na hawatakuwa na
msaada tena kwangu.Siwezi
kuwaacha hai kwani walikofika ni
mahala wasikotakiwa
kufika.Nawashukuru wamenisaida
sana lakini siwezi kusubiri kuona
msaada walionisaidia unageuka
shubiri kwangu” akawaza rais
“ Jioni hii Austin amenitaarifu
kwamba tayari wanafahamu
aliyemvamia Mukasha kuwa ni
Evans.Hii tayari imekaa vibaya kwa
upande wangu .Evans alifanya
uzembe mkubwa na ambao unataka
kunigharimu .Wale vijana lazima
wajiulize maswali mengi kuhusiana
na kitendo cha Evans kumvamia
Mukasha” akawaza rais
“ Kuna nyakati ninajikuta
ninajuta kwa nini nilimtafuta Austin
kwani ameanza kuninyima usingizi na
kunifanya nifanye mamo mengine
ambayo sikuwa nimefikiria
kuyafanya.Japokuwa amenisaidia kwa
kiasi kikubwa kupata nguvu za
kupambana na Alberto’s lakini siwezi
kabisa kumuacha .” akawaza rais na
kuchukua simu yake akampigia Evans
“ Hallow mzee” akasema Evans
“ Evans uzembe ulioufanya sasa
unaanza kuniletea matatizo.Mtu yule
ambaye alimuokoa Mukasha anaitwa
Job na ni mshirika mkubwa wa
Austin.Nimepigiwa simu usiku huu
na Austin akanitaarifu kuwa tayari
wanafahamu kuwa wewe ndiye
uliyemvamia Mukasha
.Nimewaambia kwamba sifahamu
chochote na wanipe muda nilifuatilie
suala hilo.Unachotakiwa kufanya ni
kuondoka nchini haraka sana kabla
hawa jamaa hawajakutia mikononi
kwani wakibahatika kukupata
watakutesa mno na utatoa siri.You’ll
go out of country for three
months.Utakaporejea mambo yote
yatakuwa yametulia na hakutakuwa
na kitisho chochote tena.Umenielewa
Evans? Akauliza rais.
“ Nimekuelewa mzee.Nitafanya
kama ulivyonielekeza” akajibu Evans
“ Good” akasema rais na kukata
simu
“ Sasa ni wakati wa kwenda
kumchukua Yasmin .Lakini kabla
sijaenda huko lazima nihakikishe
mipango yote ya kumtoa Tariq usiku
huu kule gerezani inakwenda
vizuri.Nataka usiku wa leo niwapate
wote wawili Yasmin na Tariq halafu
kesho asubuhi nikaichukue hati ya
muungano na kuwapatia kisha
niwaondoe hapa nchini ili jioni ya
kesho moshi mweusi utande katika
anga la Tanzania.” Akawaza rais na
kuchukua simu akazungumza na
mkuu wa magereza kwa dakika
kadhaa halafu akaondoka na walinzi
wake wakaelekea kule mahala
walikomuacha Silvanus Kiwembe
mkurugenzi wa idara ya usalama wa
taifa.
Rais aliwasili katika majengo yale
na moja kwa moja akaelekea
alikokuwa amefungwa Silvanus
Kiwembe
“ Vipi maendeleo yako Silva?
Akauliza rais
“ Mheshimiwa rais mimi na
wewe ni watu ambao tunaelewana na
hata siku moja sijawahi kudharau
maelekezo yako ,kwa nini lakini
unanifanyia hivi? Akauliza Silva
“ Silva wewe mwenyewe ndiye
uliyesababisha haya yakakupata.Kwa
nini umenificha mambo haya wakati
mimi ndiye mkuu wako?
“Mheshimiwa rais kuna mambo
mengine hata mkuu wa nchi hapaswi
kuyafahamu.Ni kwa ajili ya usalama
wa nchi”akasema Silva
“ Hilo ndilo kosa lako
linalosababisha nikuharibu .Ulitakiwa
uwe muaminifu kwangu na kunieleza
kila kitu kuhusu jambo hili.Tuachane
na hayo ni wakati sasa wa kwenda
kumchukua Yamsin” akasema
rais.Silva akainuka wakaongozana na
rais katika gari na kuondoka
wakaelekea katika gereza la siri
alimofungwa Yasmin Esfahani.
Iliwachukua dakika arobaini
kulifikia jumba moja kubwa lenye
ghorofa zaidi ya tano .Juu ye geti la
kuingilia katika jengo lile kulikuwa na
bango kubwa lililoandikwa kwa
maandishi makubwa Mazwa Rest
house”
“ Tumefika mheshimiwa rais”
akasema Silva na rais akashangaa
“ Ni hapa?
“ Ndiyo mzee ni hapa”
“ This is a rest house!! akasema
rais
“ Ndiyo mzee hii ni nyumba ya
kupumzika wageni lakini chini ya
jengo hili kuna gereza hilo.Ni gereza
la aina yake ambalo limejengwa ndani
ya bahari kwa hiyo si rahisi kwa mtu
yeyote anayefungwa humo kutoroka”
akasema Silva.
“ Naona jumba linawaka taa
mnaruhusu wageni kulala hapa?
Akauliza rais
“ Ndiyo mzee.Tunaruhusu
wageni kulala ili siri ya eneo hili
isijulikane hata hivyo wageni
wanaoruhusiwa kulala hapa ni wale
wageni wa serikali na mabalozi wan
chi mbali mbali mtu yeyotye ambaye
analala hapa tunamfanyia uchunguzi
wa kutosha kujiridhisha kuwa si mtu
hatari” akasema Silva
“ Karibu mheshmiwa rais lakini
walinzi wako naomba wabaki nje
ndani tutaingia mimi na wewe pekee”
akasema Silva
“ Hapana ninaingia na walinzi
wangu wote” akasema rais
“ Haitawezekana mzee.Utaingia
na walinzi wawili” akasema Silva na
kuwaongoza rais na walinzi wake
kuingia ndani ya jengo lile lililokuwa
kimya na cha kushangaza ndani
hakukuwa na mlinzi hata mmoja.
“ Sioni mlinzi yeyote hapa.Ulinzi
unapaswa kuwa mkali sana eneo hili”
akasema rais
“ Ulinzi ni mkali na wa hali ya
juu mno.Huku kote tunakotembea
tunaonekana na kama mtakumbuka
kuna mahala niliweka kadi yangu ya
utambulisho na ndiyo maana mpaka
sasa mko salama kwani bila hivyo
msingeweza kufika hadi hapa
tulipofika mkiwa peke yenu.Kuna
silaha zimefichwa kila mahala na
endapo kunatokea kitisho chochote
cha usalama silaha hujifungua na
hatari huondolewa haraka sana.”
Akasema Silva na kuendelea
kutembea kimya kimya hadi
walipofika katika mlango mkubwa
Silva akapitisha kadi yake katika
sehemu ya kadi pembeni ya
mlango,ukafunguka wakaingia katika
chumba kidogo kisha mlango
ukajifunga na Silva akabonyeza vitufe
kadhaa wakaanza kushuka chini.
“ Sasa tunaelekea chini umbali
wa mita elfu mbili na mia saba”
akasema Silva.Baada ya muda mfupi
mlango ukafunguka wakashuka na
kuingia katika gari dogo
“ Kutoka hapa hadi gerezani
kuna umbali wa kilometa tano na
tunatumia magari haya kufika
gerezani” akasema Silva.Akawasha
gari wakaondoka.Kulikua na barabara
nzuri yenye taa nyingi usingedhani
uko mita kadhaa chini ya ardhi.Hali
ya hewa ilikuwa ya ubaridi mzuri
kutokana na mitambo yakusambazwa
hewa safi inayotumika.
Hatimaye waliwasili katika
gereza lenyewe na Silva
akamzungusha rais sehemu mbali
mbali halafu akamuacha rais na
walinzi wake katika chumba fulani na
baada ya muda akarejea na kumtaka
rais waongozane wakaeleka katika
chumba alimo Yasmin
“ Yasmin anahifadhiwa katika
chumba hiki “ akasema Silva halafu
kwa kutumia kifaa cha mawasiliano
akawasiliana na mtu aliyefungua
mlango wa chumba alimo Yasmin
wakaingia ndani.Kilikuwa ni chumba
kikubwa chenye kitanda na meza ya
kulia chakula .Pia kulikuwa na
mlango wa choo kilichotengenezwa
kwa teknolojia ya hali ya juu ambacho
hakiruhusu maji ya bahari kuingia
ndani.Silva na walinzi wa rais
wakatoka wakamuacha rais peke yake
na Yasmin
Habari yako Yasmin” akasema
rais lakini Yasmin hakumjibu kitu
“ Naitwa Ernest Mkasa rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Yasmin akatumia sekunde
kadhaa kumsaili rais na kisha akauliza
“ Unataka nini hapa? .Rais
akavuta pumzi ndefu na kusema
“Nimekuja hapa kuhitimisha
kifungo chako.Nimekuja kukuachia
huru”
“Kuniachia huru? Bado siamini
kama usemayo ni ya kweli.Mnataka
kuniua? Nimekuwa ndani ya chumba
hiki sifahamu ni kwa muda gani na
toka nimewekwa humu sijawahi hata
kuliona jua kwa miaka yote
niliyofungwa,adhabu yote hii haitoshi
hadi mniue?
“ Hapana Yasmin,hatuendi
kukuua.Nimekuja kukuachia huru.”
Akasema rais.Yasmin akamtazama
kwa sekunde kadhaa na kuuliza
“ Kwa nini niachiwe huru.Kwa
nini umekuja mwenyewe kuniachia
huru?
“ Nimefanya makubaliano na
Habib na moja ya makubaliano ni
kukuacha huru wewe na Tariq hivyo
nimekuja mimi mwenyewe kukutoa
humu” Yasmin akastuka kidogo.
“Umesema umefanya
makubaliano na Habib? Ni nani huyo
Habib? Huyo Tariq naye ni nani?
Akauliza Yasmin
“Humfahamu Habib? Yeye ndiye
aliyenipa taarifa zako zote kwani
sikuwa nikifahamu chochote
kuhusiana na kushikiliwa kwako hapa
Tanzania.Habib ni kiongozi wa
Alshabaab”
“Alshabaab?!! Yasmin
akashangaa
“ Mimi si mfuasi wa
Alshabaab.Kwa nini Alshabaab
watake niachiwe huru?
Wamenifahamuje? Wanataka nini toka
kwangu? Nimeanza kuwa na wasi
wasi kwa hiyo humu
sintatoka”Akasema Yasmin.
“ Yasmin makubaliano tayari
yamekwisha fanyika kati yangu na
Habib na usiku wa leo wewe na Tariq
mtaachiwa huru na kesho mtaondoka
hapa nchini kuelekea Mogadishu”
“ Nimesema sitoki humu
ndani.Siendi kokote.Simfahamu huyo
Habib na sijui nini lengo lake kwangu
kwa hiyo mwambie kwamba Yasmin
amekataa kutoka gerezani!! Akasema
Yasmin kwa ukali.Ukimya ukatanda
mle chumbani Ernest akasema
“ Yasmin hii ni nafasi pekee
umeipata .Hakuna anayefungwa
katika gereza hili anatoka
hai.Ukifungwa humu utaishi hadi
kufa kwako na hakuna yeyopte
atakayejua kama uko hapa kwani
gereza hili liko ndani ya
bahari.Tafadhali ipokee fursa hii
iliyojitokeza na utoke humu
ukaendelee na maisha yako.Nafahamu
vile vile unaye mtoto ambaye naye
huko aliko ana hamu sana ya kutaka
kukuona.Itumie fursa hii utoke na
umtafute mwanao ambaye hajakutia
machoni kwa miaka zaidi ya kumi.”
Akasema Ernest.Yasmin akatumia
kama dakika tatu kutafakari na
kusema
“ Sawa nimekubali kuondoka
lakini kabla ya kutoka humu nahitaji
kuzungumza na Habib.Lazima
nimfahamu mtu huyo ambaye
umefanya makubaliano nawe .”
akasema Yasmin
“ Hapa tulipo tuko chini ya
bahari kwa hiyo utawasiliana na
Habib baada ya kutoka humu”
akasema rais na kugonga mlango
ukafunguliwa.Silva na walinzi wa rais
wakaingia.Kupitia redio ndogo za
mawasiliano Silva akatoa maelekezo
kuwa kamera zote zigeuzwe uelekeo
halafu wakamtoa Yasmin na
kumpeleka moja kwa moja katika gari
la rais.Kabla hawajaondoka rais
akamwambia Silva
“ Ahsante sana Silva lakini
kuanzia sasa gereza hili litakuwa chini
yangu.Mimi ndiye nitakayekuwa na
maamuzi ya mwisho ya kila
kinachofanyika hapa.Nataka kesho
saa nne asubuhi nipate ripoti yote
kuhusiana na gereza hili ofisini
kwangu.Umenielewa Silva? Akauliza
rais
“ Nimekuelewa mheshimiwa
rais” akajibu Silva
“ Good.Get in the car” akasema
rais ,Silva akaingia garini wakaondoka
“ Jambo lingine Silva ,nataka
ufahamu kuwa nimeweka watu wa
kukufuatilia kila unachokifanya na
kila kinachofanywa na familia yako
kwa hiyo tafadhali usijaribu kufanya
kitu chochote cha kipuuzi.What
happened tonight will remain between
us.Ukifumbua mdomo wako
nitakumaliza wewe na familia yako
.Tunaelewana Silva? Akauliza rais.
“Nimekuelewa mzee”
Safari ikaendelea na safari hii
hawakurejea tena katika yale majengo
mfano wa kiwanda bali walifuata
maelekezo ya rais na walipofika katika
kituo kimoja cha mafuta gari
zikasimama na Silva akaruhusiwa
kushuka ili amuite dereva wake aje
kumchukua.Rais hakutaka Silva
afahamu ni wapi alikuwa anampeleka
Yasmin.
Safari iliishia katika nyumba
fulani iliyokuwa inalindwa na askari
wane wenye silaha ambao walifungua
geti haraka na gari zile tatu zikaingia
ndani.Rais na Yasmin wakashuka na
kuingia ndani.Rais akawataka walinzi
wasubiri nje.Walipoingia sebuleni
akachukua simu na kumpigia mkuu
wa magereza wakazungumza kwa
dakika kadhaa halafu rais akamuita
kiongozi wa wale jamaa wenye suti
akampa maelekezo fulani akaondoka
akiongozana na wenzake .
Rais akazitafuta namba za simu
za Habib akampigia
“ Habari za usiku huu
mheshimiwa rais? Akauliza Habib
baada ya kupokea simu
“ Habari nzuri.Nimekupigia
kukujulisha kuwa tayari nimempata
Yasmin na Tariq nitampata muda
mfupi ujao.Zungumza na Yasmin”
akasema rais na kumpa simu Yasmin
azungumze na Habib.Wakaanza
kuzungumza kiarabu ambacho Ernest
hakuelewa chochote.Maongezi yao
yalichukua zaidi ya dakika
kumi,Yasmin akaweka simu mezani
na kumtazama rais na kusema
“ Bado kuna mtu nahitaji
kuzungumza naye ,atanipigia baada
ya dakika chache”
Zilipita dakika nne simu ya rais
ikaita,Yasmin akaitazama na
kubonyeza kitufe cha kupokelea kisha
akaanza kuzungumza kwa lugha ya
kiarabu kwa takribani dakika
ishirini.Alipomaliza maongezi
akamtazama rais
“ Tayari nimeelekezwa kila
kitu.Nimeambiwa kwamba utanipatia
mzigo fulani kesho ambao tayari
mmekubaliana na Habib” akasema
Yasmin
“ Ndiyo kuna mzigo nitakupatia
kesho kama tulivyokubaliana na
Habib” akasema Ernest
“Pamoja na makubaliano ambayo
mmekubaliana na Habib kuna jambo
lingine ambalo nataka tukubaliane
mimi na wewe na liiingizwe katika
makubaliano ya jumla.”
“Jambo gani hilo ? akauliza
Ernest akionekana kuwa na wasi wasi
“ Wakati ninakamatwa zaidi ya
miaka kumi iliyopita nilikuwa na
mahusiano na mwanaume mmoja
mtanzania ambaye nilizaa naye mtoto
mmoja.Nimefahamishwa na
wenzangu walionipigia simu muda
mfupi uliopita kwamba mwanangu
yuko hapa Tanzania na jina
analotumia ni Maria Boaz
Abrahams.Nataka ufanye kila lililo
ndani ya uwezo wako ili mwanangu
apatikane kabla sijaondoka
kesho.Ukishindwa kulitekeleza hilo
,makubaliano yote yatavunjika na
mipango yako itashindikana”
akasema Yasmin.Ernest Mkasa
akastuka na kumtazama Yasmin
“ Umesema mwanao anaitwa
nani?
“ Anaitwa Shamim lakini jina
analotumia sasa ni Maria Boaz
Abrahams”
“ Oh my God!! Akasema Ernest
“ Mbona umeshangaa
unamfahamu?
“ Ndiyo ninamfahamu na ninajua
mahala alipo lakini mimi na wewe
lazima tuwe na makubaliano ili
niweze kukuunganisha tena na
mwanao”
“ Unataka makubaliano na mimi?
Kwa sasa mimi ndiye ninayekupa
maelekezo kwa hiyo hakuwezi kuwa
na makubaliano yoyote kati
yetu.Ukishindwa kutekeleza maagizo
ujue na mipango yako yote
itashindikana” akasema Yasmin
“ Sikiliza Yasmin.Hivi
tuongeavyo mwanao yuko mahali
fulani ameshikiliwa na watu fulani
hatari wanamtesa.Ninao uwezo wa
kumtoa mwanao hapo na ukaungana
naye endapo utakuwa tayari kufanya
nitakachokuamuru” Yasmin akafikiri
kidogo na kusema
“ Siwezi kufanya makubalino
yoyote na wewe.Namtaka mwanangu
kesho kabla sijaondoka Tanzania.”
Akasema Yasmin.Rais akachukua
simu na kumpigia Austin
“Hallow mheshimiwa rais”
akasema Austin baada ya kupokea
simu
“ Austin nahitaji kuzungumza na
Maria” akasema rais
“ Maria? Austin akashangaa
“ Ndiyo.Naomba umpe simu
nizungumze naye.Naomba aachwe
peke yake nina jambo la muhimu sana
la kuzungumza naye.” Akasema
rais.Bado Austin aliendelea kushangaa
“ Austin” akaita rais baada ya
kuona kumekuwa kimya
“ Mheshimiwa rais” akasema
Austin
“ Naomba tafadhali nizungumze
na Maria halafu baadae nitakupa
maelekezo muhimu “ akasema
rais.Baada ya dakika mbili simu ya
rais ikapigwa ,alikuwa ni Austin.
“ Hallow Austin” akasema rais
“ Hallow nazungumza na nani?
Akauliza Maria
“ Unazungumza na rais”
“Shikamoo mheshimiwa rais.”
“Marahaba.Maria uko peke yako
hapo ulipo?
“Ndiyo mzee niko mwenyewe”
“kuna mtu anataka kuzungumza
nawe” akasema rais na kumpa Yasmin
simu akaanza kuzungumza na Maria
kwa lugha ya kiarabu.Maongezi yao
yalichukua zaidi ya dakika ishirini
kisha wakaagana.Yasmin akafuta
machozi yaliyokuwa yanamtoka na
kumtazama rais usoni
“ Nini unahitaji toka kwangu ili
nimpate mwanangu? Akauliza
Yamsin.Rais akavuta pumzi ndefu na
kusema
“ Kesho nitakupatia hati ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.Hii ni nyaraka kubwa sana
na muungano huu uliodumu kwa
miaka mingi upo shakani endapo hati
hii haitakuwepo.Ninataka ufanye kila
lililo ndani ya uwezo wako kuirudisha
hati hii mara tu Alshabaab
watakapotoa tamko la kuhusika na
matukio mawili yatakayotokea
kesho,kisha unirudishie hati hiyo na
nitakukabidhi mwanao.Uko tayari
kwa……” Rais akastuka kidogo baada
ya mlango kugongwa
“ Tariq amewasili .Fikiria hilo
nililokuambia endapo unahitaji tena
kumuona mwanao” akasema Ernest
“ Nitaangalia namna ya kufanya
lakini naomba uwazuie hao
wanaomshikilia mwanangu
wasiendelee kumtesa.” Akasema
Yasmin na rais akaelekea mlangoni
.Wale jamaa wenye suti nyeusi
walikuwa wamerejea wakiwa na Tariq