SEHEMU YA 16: SEASON 5
Saa nne za asubuhi ,Austine
akiwa na wenzake,Job,Amarachi na
Marcelo walikuwa wakijadili namna
kumpata Yasmin Esfahani.Walijitahidi
kwa kadiri walivyoweza usiku mzima
uliopita kutafuta mahala ambako
Yasmin alitumia simu ya rais
kuzungumza na mwanae Maria lakini
hawakufanikiwa.
“Jana tulifanya kila tuliloweza ili
kufahamu mahala aliko Yasmin
hatukufanikiwa.Kuna jambo moja tu
ambalo tunaweza kulifanya ili
kumpata yasmin.Nitampa simu Maria
ampigie rais na aombe kuzungumza
na mama yake.Hilo likifanikiwa
nitazungumza na Yasmin na
atatueleza kile kilichopo kati yake na
rais” akasema Austin
“ Maria atakuwa tayari kufanya
hivyo? Tayari amekwisha hakikishiwa
uhuru na rais sidhani kama
aataonyesha tena ushirikiano
kwetu.”Akasema Amarachi
“Tutamfanya akubali kufanya
tunavyotaka” akasema Austin na bila
kupoteza muda wakaenda wote
chumbani kwa Maria isipokuwa
Marcelo.
“Maria ule wakati wa mzaha
umekwisha na nimekuja kikazi zaidi
kwa hiyo nitakuomba utekeleze kila
kile nitakachokuamuru
ukifanye”akasema Austin na sura
yake haikuonyesha masihara hata
kidogo.Siku hii alikuwa na nafuu
kubwa.Akatoa simu mfukoni na
kuiweka mezani.
“Nataka umpigie simu rais na
umwambie kwamba unataka
kuzungumza na mama yako mara
moja.” Akasema Austin.Maria
akatabasamu na kusema
“ Austin nimekueleza toka jana
kwamba usipoteze muda wako
kuhusu mimi au mama
yangu.Nadhani umekwisha pigiwa
simu na rais akikutaka uniachie huru
kwa hiyo siwezi kufanya hicho
unachoniamuru nikifanye.”akasema
kwa dharau na kuinamisha kichwa
“Maria nilikueleza awali
kwamba sihitaji mzaha siku ya leo
kwa hiyo chukua simu hiyo na
umpigie rais.”
“ No ! I cant do that!! Akasema
Maria kwa ukali.Sura ya Austin
ikazidi kujikunja kwa hasira
akamgeukia Amarachi
“ Bring Boaz here”
Amarachi akatoka kwenda
kumelata Boaz
“ If you do anything to my father
I swear I’ll kill you all!! Akasema
Maria kwa hasira.Baada ya dakika
tatu Boaz akaletwa mle
chumbani.Kwa sekunde kadhaa
akatazamana na mwanae Maria na
wote machozi yakawatoka
“ Austin kwa nini umetufanyia
hivi ? Tumekukosea nini? akauliza
Boaz kwa uchungu baada ya
kumuona mwanae namna
alivyoumizwa.
“Sit !!! akaamuru Austin na Boaz
akaketi kitini.Akawatazama kwa
zamu na kusema
“ Kwa miaka kadhaa nimeishi
nanyi kwa upendo mkubwa kama
familia moja.Niliamini ninyi ni watu
wema na wenye upendo wa kweli
kwangu lakini Mungu amenionyesha
kuwa watu nilioamini ni wazuri
kwangu nimashetani waliovaa miili ya
wanadamu.”
“ Unatuita sisi mashertani? Bila
ya sisi ungekuwa kaburini hivi sasa
.Kwa haya yote tuliyokutendea
unadiriki kutuita sisi mashetani?
Akauliza Boaz
“ Shut up !! akafoka Austin.
“ You are the family of
devils.Siku chache zilizopita huyu
mwanao amenipiga risasi nne na
nusura ningepoteza maisha.Look at
her.Ukimtazama huwezi kudhani
kama amewahi hata kuigusa silaha
lakini ni mtu hatari sana.Ana uwezo
mkubwa wa kutumia silaha.Ni
Mungu tu ameninusuru na kifo kwa
sababu anajua kunakazi kubwa
ninaifanya.”akanyamaza akamtazama
Boaz na kusema
“ Wewe na mwanao mliniambia
kwamba mama yake Maria alifariki
dunia angali maria akiwa mdogo.kwa
nini mkanidanganya wakati mama
yake Maria yupo hai?
“ That’s not true.She’s dead”
“ No ! She’s not dead.She spoke
with your daughter last night.Muulize
mwanao kama ninasema uongo”
akasema Austin na sura ya Boaz
ikabadilika
“ Maria ! akaita
“Her name is not Maria.She’s
Shamim” akasema Austin na kuzidi
kumchanganya Boaz
“ Shamim? Akauliza Boaz
“Ndiyo.Hufahamu kama
mwanao ana majina zaidi ya moja?
“hapana sifahamu
chochote.Mimi nalifahamu jina moja
nililompatia mimi wakati alipozaliwa
la Maria hayo mengine siyafahamu.”
Akasema Boaz na kumgeukia Maria
“ Maria my love tell me what this
man is saying is not true”
Maria akainamisha kichwa
“Nijibu Maria kama ni kweli
anachokisema Austin.Ni kweli mama
yako yuko hai?
“It’s true dady” akasema Maria
“Oh my God !!! akasema Boaz
“Umefahamuje kama mama yako
yuko hai ? akauliza Boaz
“ Ukweli ni huu” akasema
Austin
“Yasmin Esfahani ambaye
uliwahi kuishi naye na mkajaliwa
kupata mtoto mmoja ambaye ni Maria
ni gaidi wa kimataifa toka kikundi cha
kigaidi cha IS.Alikuja hapa Tanzania
kwa lengo la kutanua mtandao wao
katika eneo la afrika mashariki na
kabla hajafanikisha lengo lake
akakamatwa na kufungwa mahala pa
siri kwa zaidi ya miaka kumi
sasa.Mwanao Maria alikuwa
anafahamu suala hili kwa muda mrefu
na hakukueleza.Tumefuatilia
mawasiliano yake ya barua pepe na
mtu mmoja anaitwa Bin Omar na
alimtaarifu kuwa anakuja Tanzania
kwa lengo la kumtafuta mama yake na
alitegemea kunitumia mimi ili
kumpata mama yake.Sina shaka
yoyote kuwa Maria naye ni mmoja wa
wafuasi wa IS lakini anayefanya
mamboyake kwa siri kubwa.Nadhani
mpaka hapo tayari umekwisha pata
picha halisi ya mwanao “ akasema
Austin.
Uso wa Boaz uliloa
jasho,akamtazama mwanae kwa
hasira na kusema
“Maria ni kweli hayo anayosema
Austin?
Maria hakujibu kitu akainamisha
kichwa.Austin akamgeukia Maria
“ Maria it’s time now to pick the
damn phone and call mr President!!
Akasema Austin.Bado Maria hakujibu
kitu.
“Job give me the gun” akasema
Austin na Job akampa bastora
“Boaz nilikuheshimu kama baba
yangu lakini pamoja na heshima hiyo
kubwa niliyokupa bado ukadiriki
kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
mdogo wangu ambaye ni sawa na
mwanao,ukamuingiza katika biashara
ya dawa za kulevya na mwisho
akafungwa gerezani.Hilo limeniumiza
sana.It’s your time to pay.Kama
nilivyokueleza awali kwamba ukiingia
katika anga zangu mimi ni mkatili
kuliko hata Simba na leo nitakuondoa
uhai wako lakini ni jambo moja tu
litakalokuokoa .Ni pale mwanao
atakapochukua simu na kumpigia
rais.Asipofanya hivyo ninakifumua
kichwa chako” akasema Austin na
kuielekeza bastora kichwani kwa Boaz
“ Maria you have one minute to
decide either your father to die or call
president” akasema Austin
“Austin please don’t do that to
my father.Dont kill him” akasema
Maria huku machozi yakimtoka
“ Three !!! akahesabu Austin
“ Austin please don’t do that
“ Two..!! take the phone and call
president !!! akasema Austin lakini
Maria alionyesha wazi kuwa hayuko
tayari kufanya alichoamriwa na
Austin na mara ukasikika mlio wa
risasi.Kila mmoja akafumba macho
.Baada ya sekunde kadhaa Maria
akafumbua macho na kumuona baba
yake ameketi kitini huku akitetemeka
mwili.
“Hilo lilikuwa ni onyo kwamba
huwa sifanyi utani na ndiyo maana
nimepiga risasi pembeni.Kama
utaendelea na kiburi chako nitafanya
kweli”akasema Austin
“ok ! ok ! Nitampigia rais.”
Akasema Maria na Austin akawasha
simu akazitafuta namba za rais
akapiga na kumpa simu Maria
“ Hallow Austin.Habari yako?
Nimekutafuta toka asubuhi bila
mafanikio .Kuna tatizo lolote?
Akasema rais baada ya kupokea simu
“ Shikamoo mzee.Unaongea na
Maria hapa”
“ Oh ! Maria habari yako. Tayari
umefika ikulu?” akasema rais
“ Mheshimiwa rais naomba
nizungumze na mama yangu
tafadhali”
“Kabla ya kuzungumza na mama
yako nataka kwanza kufahamu je
tayari umeshafika ikulu?
“ Mheshimiwa rais bado sijafika
Ikulu”
“ Uko karibu na Austin? Nahitaji
kuzungumza naye”
“ hapana mzee siko naye
karibu.Niko peke yangu” akasema
Maria
“ Sawa Maria naomba unisubiri
baada ya dakika tano utazungumza na
mama yako.Naelekea mahala alipo ila
mwambie Austin nahitaji sana
kuzungumza naye” akasema rais
“ Austin nadhani ametoka
pamoja na wenzake na sijui
wameelekea wapi.Waliniachia simu
hapa kwa ajili ya mawasiliano na
mama” akasema Maria
“ Ok Maria nitakupigia baada ya
muda mfupi” akasema rais na kukata
simu
“ Good.Umefanya vizuri.Wakati
mwingine usitake
kunijaribu.Nikikuamuru kufanya
jambo Fulani ,lifanye bila kusita!!
Akasema Austin huku akimtazama
Boaz ambaye alikuwa amejisaidia haja
ndogo kwa woga uliompata baada ya
kukoswa na risasi
“ Take him away” akasema
Austin na Amarachi akamchukua
Boaz akamrejesha katika chumba
chake. Baada ya dakika tano kama
alivyoahidi rais akapiga simu.Monica
akaipokea na kuanza kuzungumza
kiarabu baada ya kufahamu
aliyekuwa anaongea ni mama yake.
“ Give me that phone” akasema
Austin na Maria akampa simu
“ hallo Yasmin” akasema Austin
kwa lugha ya kiarabu
“ wewe ni nani na unataka nini?
Kwa nini haujamuachia huru
mwanagu hadi sasa ? Akauliza
Yasmin kwa kiarabu
“ naomba unisikilize vizuri
Yasmin.Binti yako Shamin pamoja na
mumeo Boaz ,wote ninawashikilia
hapa na usalama wao utategemea
sana namna utakavyotii maelekezo
yangu”
“ Nini unahitaji? Akauliza
Yasmin
“ Kwanza nahitaji kufahamu
kuna kitu gani kinachoendelea kati
yako na rais?
“ rais ameniachia huru na
tumeweka makubalino kuwa siwezi
kuondoka bila ya mwanangu Shamin
na ndipo alipokupigia simu akakupa
maelekezo kuhusu kumuachia
Shamim.Leo saa nane mchana
ninaondoka kwa hiyo namuhitaji
mwanangu kabla ya muda huo bila
hivyo makubaliano yetu na rais
yatakuwa yamekufa” alasema Yasmin
“ Kwani mmekubaliana jambo
gani? Rais amefanya makubaliano
gani na mtu ambaye anafahamu kuwa
ni mfuasi wa IS? Akauliza Austin
“ Rais hajafanya makubaliano na
mimi wala IS bali amefanya
makubaliano na Alshabaab na moja
kati ya jambo walilokubaliana ni mimi
kuachiwa huru.Kwa hiyo sifahamu
wamekubaliana mambo gani ila mimi
na yeye tumekubaliana kuwa lazima
nimpate mwanangu kabla sijaondoka
leo”
“ Sikiliza Yasmin,mwanao
Shamim niko naye mimi na hataweza
kuachiwa hata kwa amri ya
rais.Hautamuona tena katika maisha
yako “
Shamim akasikika akivuta pumzi
ndefu kisha akasema
“ Ni vipi iwapo mimi na wewe
tutafanya makubaliano? Kuna kitu
cha thamani sana ambacho
nitakukabidhi ili unipe mwanangu”
“ Kitu gani hicho?
“ Kuna kitu kikubwa sana
nitakupatia lakini endapo utakuwa
tayari kwa mambo yafuatayo.Kwanza
utanikabidhi mwanangu Shamim na
pili utanisaidia niweze kupata hati
mpya ya kusafiria itakayoniwezesha
niende mbali kabisa mimi na
mwanangu.Ukinifanikishia hayo
nitakupa kitu hicho kikubwa kwa
ajiliya usalama wa nchi yenu.Uko
tayari kwa hilo” akauliza Yasmin, na
kukawa kimya.
“ hallo, uko tayari kwa hilo
nililokueleza? Akauliza Yasmin
“ Siwezi kufanya maamuzi hadi
hapo utakaponieleza ni kitu gani
hicho chenye thamani ambacho
unataka kunipatia”
“ Siwezi kukueleza sasa hivi ni
kitugani hadi hapo nitakapokuwa
nimekabidhiwa.Niambie kama uko
tayari ili nianze kuweka mipango ya
kukutana nawe”
“ Niko tayari ” akajibu Austin
“ Vizuri.Kaa tayari nitakupigia
simu muda wowote baadae nitakupa
maelekezo ila tafadhali naomba
mwanangu asiendelee kuteswa”
akasema Yasmin na kukata
simu.Austin na wenzake wakatoka
mle ndani wakarejea sebuleni.
“ Pole Austin it wasn’t easy”
akasema Amarachi
“ Thank you”akajibu Austin na
kuvua fulana yake kwani aliokuwa
anatokwa na jasho akanywa glasi ya
maji na kusema
“Nyote mmefuatilia
mazungumzo yangu na Yasmin.Kuna
jambo hapa linaendelea kati ya rais na
Alshabaab kiasi cha kufanya
makubaliano ya kumuachia huru
Yasmin.Kitu gani kinaendelea kati ya
rais na Alshabaab? Hiki ni kikundi cha
kigaidi rais anawezaje kufanya
makubaliano na kikundi hiki? Kuna
siri kubwa imejificha hapa.Lazima iko
sababu iliyomplekea rais akafanya
makubaliano na hawa jamaa huku
akifahamu ni watu hatari” Akasema
Job
“Niliwaeleza jana kwamba
mwenendo wa rais si mzuri kwa hiyo
inatupasa kuwa na jicho la tatu ili
tuweze kuona zaidi mambo
anayoyafanya.Alikana kumfahamu
Yasmin lakini anamfahamu na
amefanya makubalianao na Alshabaab
ya kumuachia mtu huyu hatari kabisa
.Kwa nini akaamua kukubaliana na
Alshabaab kumuachia mtu huyu
hatari ndilo swali tunalopaswa
kujiuliza.Nadhani itatulazimu kuweka
pembeni mambo mengine yote na
kuanza kushughulika na rais kwanza
ili tumfahamu vyema kutokana na
mambo yake anayoyafanya.Huyu ni
mtu ambaye bado hatumfahamu
vizuri. Vita na Alberto’s inamtegemea
sana yeye lakini hatuwezi kufanikiwa
endapo mtu tunayemtegemea
anakuwa na ndimi mbili.Kama
ameweza kutudanganya kuhusu
Yasmin tutamuaminije mtu kama
huyu? Tunachopaswa kufanya ni
kuweka pembeni mipango yote ili
kwanza tujiridhishe na mtu ambaye
tunashirikiana naye kama tunapaswa
kuendelea naye au vipi.Kitendo cha
kuwa na mawasiliano na Alshabaab
kinatosha kabisa kutufanya tuwe na
mashaka kwamba huyu sio mtu
mwema hata kidogo.Wakati
tukiendelea kumsubiri Yasmin apige
simu na kutupatia hicho kitu cha
muhimu na chenye thamani
anachokisema ,Amarachi utakwenda
kufuatilia majibu ya kile kipimo cha
vinasaba kwani waliahidi leo majibu
yatakuwa tayari.Job tutaendelea
kumuhoji Maria ili kumfahamu kwa
undani zaidi.” Akasema Austin
SEHEMU YA 17: SEASON 5
Inakaribia saa tano za
asubuhi,Ernest Mkasa rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania tayari
alikuwa katika nyumba walimolala
Tariq na Yasmin.Kikubwa
kilichomleta hapa ni kumkabidhi
Yasmin hati ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar kama
walivyokubaliana na Habib mkuu wa
kikundi cha Alshabaab.
Akaufungua mkoba wake na
kutoa bahasha ya khaki ambayo ndani
yake akatoa hati ya muungano
akaitazama na kisha akamkabidhi
Yasmin.
“Hii ndiyo hati halisi ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.Ninakukabidhi kama
tulivyokubaliana na wakuu wako”
akasema Ernest.Yasmin hakujibu kitu
akaifungua akaitazama kurasa
mojamoja halafu akampatia Tariq
naye akaipitia na kumrudishia.
“Nadhani nyote mmeiona na
kuridhika nayo” akasema Ernest
“Tumeiona lakini bado
wataalamu wetu wataipitia tena ili
kuhakiki kama kweli ni halisi ingawa
kwa macho ya kawaida inaonekaan ni
halisi” akasema Yasmin.Rais
akachukua simu yake na kumpigia
Habib
“ Habari za asubuhi mheshimiwa
rais.Nadhani utakuwa na taarifa
njema za kunipatia ” akasema Habib
“Ndiyo habib ninazo taarifa
nzuri kwako.Ni kwamba tayari
nimempatia Yasmin ile hati halisi ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar kama tulivyokubaliana.”
“Nafurahi kusikia hivyo.Naomba
nizungumze na Yasmin” akasema
Habib na rais akampa simu Yasmin
wakaanza kuzungumza kwa lugha ya
kiarabu.Walizungumza kwa zaidi ya
dakika kumi halafu Yasmin akampa
simu rais azungumze na Habib
“Mheshimiwa rais ahsante kwa
kutekeleza ahadi yako ,kinachofuata
sasa ili makubaliano yetu yatimie
nataka Yasmin na Tariq waondoke
hapo nchini Tanzania haraka
iwezekanavyo.Nataka kablaya saa
kumi na moja jioni ya leo wawe tayari
wamefika Mogadishu.” Akasema
Habib
“Kila kitu kimekwisha andaliwa
Habib na ndege watakayoondoka
nayo iko tayari .Kitu ninachokuomba
ni kuyaheshimu makubaliano yetu”
“ Usijali kuhusu hilo.Kila kitu
kitafanyika kama tulivyokubaliana”
akasema Habib na kukata simu.Rais
akafuta jasho usoni na kusema
“ Kila kitu kimekwenda vizuri na
tayari ndege inawasubiri kwa ajili ya
kuwapeleka Mogadishu.Vijana wangu
watawapeleka uwanja wa ndege
tayari kwa kuondoka hapa
nchini.Ndege ni salama na haina
tatizo lolote.” Akasema rais.
“Tunashukuru rais kwa kukubali
kutuachia huru na kwa huduma nzuri
tulizopata kuanzia jana.Lakini kabla
hatujaondoka kuna vitu ningeomba
umtume mmoja wa vijana wako
akaninunulie.Sina mavazi ,sina
vipodozi naonekana kama mzimu”
akasema Yasmin na rais akainuka kwa
ajili ya kuondoka.Yasmin akampa
Tariq ile hati ya muungano aendelee
kuipitia wakati akimsindikiza rais.
“Mheshimiwa rais,jana ulitaka
kufanya makubaliano na mimi
kuhusu kurejeshewa mwanangu
.Nitafanya kama unavyotaka kwa ajili
ya mwanangu lakini kuna kitu
nitakiomba.” Akasema Yasmin
wakiwa nje .Ernest akatabasamu kwa
mbali an kuuliza
“ Unahitaji nini?
“ Nahitaji kijana utakayemtuma
aniletee mavazi na vipodozi aniletee
pia bastora mbili ,simu na fedha
taslimu shilingi milioni
kumi.Ukinipatia hivyo viwili basi
ukae ukisubiri simu yangu ili unipatie
mwanangu na mimi nikupatie hati
yako ya muungano.Uko tayari kwa
hilo?
“Sina tatizo na hilo hata
kidogo.Nitaongozana na kijana mmoja
nitampatia vitu hivyo atakuletea ila
tafadhali naomba uwe mkweli.”
“Namuhitaji sana mwanangu
kuliko kitu chochote kwa hiyo niko
tayari kufanya jambo lolote
kumpata.Huyo kijana utakayemtuma
aniletee vitu hivyo aweke vitu hivyo
katika begi sitaki Tariq afahamu
chochote ” akasema Yasmin na kurejea
ndani ,rais na walinzi wake
wakaondoka.Wakiwa garini rais
akajaribu tena kupiga simu ya
Austin.Simu ikaita bila
kupokelewa,akapiga tena simu ya Job
nayo ikaita bila kupokelewa
“ Hawa vijana wana tatizo gani
leo? Namuhitaji sana Maria ili pindi tu
Yasmin atakapopiga simu basi niwe
tayari kwa mabadilishano .Ngoja
kwanza nimalize suala kubwa la leo
halafu nitawatafuta” akawaza rais.
Alirejea ikulu na moja kwa moja
akaenda chumbani kwake na
kuwasiliana na Jenerali Lameck
Msuba akamtaarifu kuwa tayari
amekwisha ikabidhi hati ya
muungano kwa Yasmin kwa hiyo
maandalizi ya tukio la jioni yaendelee.
“Zimebaki saa chache sana kwa
Tanzania kutikisika.Kuna wakati hofu
inaniingia lakini sina namna nyingine
lazima nifanye hivi.Lazima niisafishe
nchi.Lazima Alberto’s wote niwafagie
,na mwisho wao ni leo.” Akaendelea
kuwaza huku akinywa mvinyo mkali