SEASON 6: SEHEMU YA 13
Monica hakutaka kurejea
tena nyumbani kwake usiku ule
akaelekea moja kwa moja
nyumbani kwa wazazi wake.
“ Monica nini hasa
kilichotokea? Nahitaji kufahamu
tafadhali” akasema mama yake
baada ya kufika nyumbani
“ Mama kichwa changu
hakiko sawa sawa.Naomba
funguo nikapumzike chumbani
kwangu nitawaeleza kila kitu
kesho asubuhi nitakapokuwa
nimetulia.” Akasema
Monica.Mama yake akamletea
funguo akaenda chumbani
kwake kulala.Akakaa kitandani
na kushika kichwa,alikuwa na
mawazo mengi.
“ Umekuwa ni usiku mbaya
sana katika maisha
yangu.Nahisi kichwa changu
kizito kama nimebeba
tofali.Mambo yaliyotokea usiku
wa leo ni mambio mazito
sana.Nashukuru rais
amenihakikishia kwamba
sintapata tatizo lolote.” Akawaza
na kukumbuka maongezi yake
na rais
“ Rais ameniuliza kama
ninafahamu mahala anakoishi
Austin.Yeye ndiye mtu wake wa
karibu ameshindwaje kufahamu
mahala alipo Austin hadi
anitumie mimi? Halafu
nilipomtajia kwamba nilikuwa
na Austin na ndiye niliyekwenda
naye Zanzibar alistuka mno hadi
jasho nikaliona usoni
pake.Kama haitoshi alionyesha
pia mstuko mkubwa pale
nilipomtajia kwamba Austin
alikwenda Zanzibar kumchukua
Yule mwanamke anaitwa
Yasmin.Alishindwa kuzungumza
na midomo ikamcheza.Kuna nini
kinaendelea hapa? Yasmin ni
nani? Akajiuliza
“ Rais ameonyesha kunijali
sana wakati nimefahamina naye
kwa siku chache tu.Leo
hakuonyesha hata kumjali
mama yeye lengo lake lilikuwa ni
kwangu tu.Ana nini na mimi
Yule mzee?
Alikosa majibu ya maswali
yake akapanda kitandani na
kujilaza.
“ Amenitaka nimpigie simu
Austin halafu nimtaarifu ili ili
atume vijana
wakamchukue.Kwa nini
anitumie mimi kumpata Austin?
Kwa nini yeye mwenyewe
asimpigie wakaongea kwa
sababu ni watu wa karibu?
Kuna tatizo gani kati yao?Jambo
hili naona halijakaa vizuri .Yeye
mwenyewe anatakiwa afanye
juhudi za kumtafuta Austin
kama alivyofanya juhudi za
kunitafuta mimi.Kuna kitu hapa
hakinipi picha nzuri
.Nilipokwenda kumtembelea
hospitali ,Austin alinihakikishia
kwamba rais ni mtu wake wa
karibu sana ambanye alikuwa ni
rafiki wa karibu wa baba yake
na amekuwa ni kama mlezi
wake. Kwa ukaribu huo walio
nao kwa nini alishindwa
kumpigia simu na kumuomba
amsaidie usafiri wa kwenda
Zanzibar hadi anitumie mimi?
Kwa nini aliamini akinitumia
mimi rais atanisikiliza na
kunipatia huo usafiri? Kuna
jambo gani alitaka kumficha rais
asijue? Halafu rais naye hataki
kumtafuta Austin anataka
kunitumia mimi kumpata
Austin,kwa nini? Akaujiuliza
“ Sintaweza kupata majibu
ya maswali haya hadi
nitakapoonana na Austin na
anieleze ukweli kitu gani
kimetokea kati yake na rais hadi
wameanza kukwepana.Kila
mmoja hataki kuwasiliana na
mwenzake moja kwa moja.Kesho
asubuhi nitajitahidi kwa kila
niwezavyo kumtafuta Austin na
nitahakikisha ninampata”
akawaza Monica .Akajaribu
kufumba macho kutafuta
usingizi lakini picha ya ndege
ikitua katika daraja la Nyerere
ikamjia na kufumbua macho
“ Kumbukumbu hii itanitesa
mno kwa muda mrefu .Ni tukio
ambalo sintalisahau katika
maisha yangu yote yaliyobaki.”
akawaza Monica
SEASON 6: SEHEMU YA 14
Janet aliingia chumbani
kwake na kumkuta mumewe
mzee Benedict amekaa
kitandani.Wakatazamana kwa
muda Benedict akasema
“ Umetoka wapi usiku huu?
Akauliza Ben ambaye sura yake
ilionyesha ukali
“ Samahani Ben nilipata
dharura nikatoka mara moja”
akasema Janet
“ Dharura? Ni Dharura ipi
hiyo ya usiku huu? Halafu kwa
nini ukaondoka bila kuniaga?
Nitaaminije kama kweli ulipata
dharura ? akauliza Benedict
“ Ben naomba
uniamini,ilitokea dharura
nikaondoka.Monica alipata
matatizo”
“ Matatizo?!! Akauliza Ben
“ Ndiyo alipata tatizo usiku
huu”
“ Alipata tatizo gani? Kwa
nini hukuniamsha na kunieleza
kama kuna tatizo? Akauliza Ben
“ Hata mimi
nilichanganyikiwa nilipopewa
taarifa hizo na ndiyo maana
nikaondoka hapa kama kichaa”
“ Nani alikupa taarifa hizo
?akauliza Ben.Janet akabaki
kimya
“Mbona hunijibu Janet ?
Ulizipata wapi taarifa hizo za
Monica? Nani alikutaarifu?
Akauliza Ben
“Ernest alinipigia simu”
akasema Janet na uso wa Ben
ukazidi kubadilika
“ Ernest alikupigia simu?
Akauliza kwa ukali
“ Ndiyo alinipigia
akanitaarifu kuwa kuna tatizo
limetokea linalomuhusuMonica
na anahitaji kuonana naye
usiku huu ikulu ili kulimaliza
suala hilo kabla ya
kupambazuka.”
“ Ernest amefahamuje kama
Monica ana tatizo? Ameanza lini
ukaribu na Monica? Kwa nini
alimtaka aende ikulu? Akauliza
Ben na Jane akabaki kimya
“ Jane naomba unieleze
ukweli,umemueleza Ernest
kuhusu Monica? Akauliza
Ben.Janet akabaki kimya
“ Oh my God ! umevunja
makubaliano yetu.Kwa nini
ukamueleza kuhusu suala hili?
Tulikubaliana usimueleze kitu
chochote lakini umeendelea
kukutana naye kwa siri na
umemueleza kila kitu.Kwa nini
Janet?akauliza Ben
“ Ilinilazimu nimueleze
ukweli kwani ana haki ya
kufahamu kama baba wa
Monica.Utanisamehe Ben lakini
nilifikiria sana na nikaona
sintakuwa namtendea haki
Monica endapo nitaendelea
kuificha siri hii.Anastahili
kumfahamu baba yake ambaye
ni Ernest.Najua hayakuwa
makubaliano yetu lakini baada
ya kutafakari nimeshindwa
kuvumilia na imenilazimu
kumueleza ukweli Ernest”
akasema Janet
Benedict akamtazama kwa
hasira na kuuliza
“ Monica naye umekwisha
mueleza kuhusu suala hili?
Akauliza
“ Hapana bado.Monica
sijamueleza chochote.”
“ You’ll pay for this
Janet.Tutaongea baadae suala
hilo lakini nieleze kwanza
Monica amepatwa na tatizo gani
hadi Ernest akamuita ikulu?
“ Hata mimi sifahamu nini
kimempata Monica kwani
hakuwa tayari kunieleza
chochote hata tulipofika ikulu
walikaa katika chumba cha
maongezi ya faragha na Ernest
wakaongea bila
kunishirikisha.Monica nimekuja
naye hapa yuko chumbani
kwake amelala.Anaonekana
hayuko sawa sawa kuna jambo
lazima limetokea.Ameahidi
kunieleza asubuhi kilichotokea”
akasema Janet .Ukapita ukimya
wa dakika zipatazo tano kisha
Janet akasema
“ Ben kuna jambo lingine
nataka nikutaarifu kuhusu
Monica” akasema Janet.Ben
akastuka na kumtazama Janet
“ Monica alinipigia simu na
kunieleza jambo Fulani ambalo
lilinistua kidogo” akanyamaza
tena.
“ Nieleze Jane ni jambo gani
hilo? Akasema Ben kwa shauku
ya kutaka kufahamu
“ Monica alinieleza kwamba
hajaziona siku zake na kwa
maelezo aliyonipa kuna kila
dalili kwamba atakua mjamzito”
Ben akahisi kama nyundo
kubwa imekipiga kichwa chake .
“ Ni ya kweli haya
unayonieleza Janet? Akauliza
Ben
“ Ni kweli kabisa.Hata yeye
mwenyewe jambo hili
lilimchanganya sana ikamlazimu
kunipigia simu kunieleza na
kuniomba ushauri” akasema
janet
“ Dah !! hili ni pigo kubwa
sana” akasema Ben .Alihisi
miguu kumtetemeka akakaa
kitandani.
“ Mipango yangu yote sasa
imeharibika.Hakuna
kitakachoendelea tena iwapo
David atagundua kwamba
Monica ana mimba.Kwa
niniMonica akafanya hivi.Tayari
amekwisha mpata bwana
mwenye mali nyingi,ni rais na
tajiri mkubwa afrika lakini kwa
nini ameshindwa kujituliza ili
aolewa na David ? Akajiuliza
Ben halafu akamtazama mkewe.
“Sikiliza janet tena naomba
unisikie kwa makini.Kama kweli
Monica ana ujauzito lazima
utolewe haraka sana.lazima
aolewe na David
Zumo.Tumepiga hatua kubwa
hadi hapa tulipofika na
tukishindwa kufikia malengo
itakuwa ni aibu kubwa sana
kwetu.Sitaki hilo litokee na
ndiyo maana nasema kwamba
hiyo mimba itatolewa na Monica
ataolewa na David Zumo.That’s
my order na hakuna wa
kulipinga hilo.Umenielewa Janet
!!! akauliza Ben kwa ukali na
kumtazama Janet kwa hasira
hadi akaogopa
“Ben jaribu kupunguza
hasira.Nafahamu jambo hili
limekustua sana na hata mimi
nilistuka hivyo hivyo kama
ulivyostuka wewe lakini bado
halijaishia hapo.Subiri nimalizie
kukueleza hadi mwisho”
akasema Janet na Ben
akamtazama kisha akaketi
kitandani
“ Monica aliniambia
kwamba alipokwenda Kinshasa
kumtembelea David walifanya
mapenzi na hii ilikuwa ni mara
ya kwanza kwake kufanya
mapenzi.Anasema kwamba yeye
na Ben hawakutumia kinga
yoyote na kwa hiyo kama kweli
atakuwa na mimba basi itakuwa
ni mimba ya David Zumo.Jambo
tunalopaswa kulifanya kwa sasa
si kumshawishi aitoe hiyo
mimba kwa kuwa muhusika
yupo na yuko tayari kumuoa
.Tunatakiwa kuhakikisha David
naMonica wanaoana kabla ya
mimba hiyo haijawa kubwa na
kugundulika” akasema Janet na
Ben akahisi mzigo mzito
uliokuwa kichwani kwake
ukishushwa
“ Amekwisha mueleza David
suala hili? Akauliza Ben
“ hapana bado.Nilimshauri
asimueleze kwanza hadi hapo
atakapokuwa na uhakika kuwa
kweli ana mimba kwani kukosa
kuona siku zake kunaweza
kuchangiwa na mambo mengine
pia lakini baada ya siku saba
anaweza akapime na kujua
iwapo ana mimba au vipi”
akasema Janet
“ Hizi ni taarifa zilizonistua
sana lakini kwa sasa angalau
nina ahueni.Nina uhakika
mkubwa kwamba David Zumo
akizipata taarifa hizi atakuwa na
furaha kubwa kwani hajawahi
kuwa na mtoto na mke wake
aliyefariki dunia.Ili kuongeza
msukumo wa ndoa yake na
David anatakiwa kumfahamisha
David mapema
zaidi.Ikiwezekana tunapokwenda
kuhudhuria mazishi ya mke
wake atafute nafasi na
kumueleza” akasema Ben
“ Nitamshauri hivyo.Ben
tunakwenda kumpata mjukuu
wetu wa kwanza” akasema Janet
huku akitabasamu.
“ Ni jambo la faraja sana
kumpata mjukuu lakini furaha
yangu yote yakumpata mjukuu
imeharibniwa na kitendo chako
cha kumwambia Ernest kwamba
Monica ni mwanae.Ulifanya kosa
kubwa sana Janet”
“ Ben najua nimekukosea
sana lakini sintomtendea haki
Ernest kama nisingemueleza
ukweli kuhusu Monica.Muda
utafika ambao mambo yote
lazima tuyaweke wazi.Siwezi
kwenda kaburini na siri hii
lazima niiweke wazi.Najua ni
jambo zito litakalomuumiza
sana Monica lakini hatuna
namna lazima ukweli
ujulikane.Hapo awali niliogopa
sana nini kitatokea iwapo
Monica akifahamu kuwa wewe si
baba yake.Niliogopa kumuumiza
kiakili ila baada ya kutafakari
kwa kina nimeamua ni bora
endapo nitamueleza ukweli
potelea mbali kama ataumia
lazima ajue kila kitu.Ben
utanisamehe sana kwa
hili,lakini nakuhakikishia
kwamba hata kama ikitokea
Monica akaufahamu ukweli
ataendelea kukutambua wewe
kama baba yake.Umemlea kwa
mapenzi makubwa toka akiwa
mdogo na hadi sasa bado
unaendelea kumpenda .Mpaka
anaingia kaburini wewe utabaki
kuwa ni baba yake.She’ll never
choose him over you.” Akasema
Janet.
“ Nafahamu ataendelea
kuwa mwanangu na
atanichagua mimi badala ya
Ernest but it’ll never be the
same again.Haitakuwa kama
awali.Mambo yatabadilika
akiufahamu ukweli.Umeniingiza
katika vita na Ernest .” Akasema
Ben
“ Ben tafadhali naomba
jambo hili lisiwe chanzo cha
ugomvi kati yako na
Ernest.Hakuna sababu ya wewe
na yeye kuingia katika vita kwa
sababu ya Monica.Huyu ni
mwanenu wote.Mkiingia katika
vita mtamsababishia matatizo
makubwa Monica.Nakuomba
Ben usiwe na hasira na
Ernest.Mnatakiwa mkae kama
watu wazima mmalize tofauti
zenu.Hii ni kwa ajili ya Monica.”
Akasema Janet.Ben akainuka
na kumtazama Janet kwa hasira
“ Mimi nikae na Ernest?
Nikae na mtu anayenisaliti na
mke wangu? That wont happen
!! me and him we’re enemies !!
akasema Ben.Janet naye
akasimama
“ Ben unamaanisha nini
unaposema kwamba Ernest
anakusaliti na mke wako? Una
maanisha kwamba mimi
ninatembea na Ernest? Akauliza
Janet kwa ukali na wote wawili
wakatazamana kwa hasira
“ Unajaribu kujitetea?
Akauliza Ben na Janet akataka
kumnasa kibao Ben akamshika
mkono
“ Usithubutu kuninasa
kibao shetani wewe.Unadhani
sifahamu mambo
unayoyafanya? Janet
ninafahamu kila kitu
unachokifanya.Nimeweka watu
wa kukufuatilia kila
unachokifanya.Ninafahamu kila
kitu kuhusu wewe na
Ernest.Bado mnaendelea
kukutana kwa siri katika hoteli
yake na hadi chumba na tarehe
ambazo mmekutana ninaweza
kukutajia.Hivi juzi tu
mmekutana tena
hospitali,unakataa na hayo?
Tafadhali usitake kunitibua akili
yangu nikakuingiza na wewe
katika orodha ya maadui
zangu.Ernest atabaki kuwa adui
yangu milele .!! akasema Ben na
macho ya mkewe Janet yalijaa
machozi.
“ Ben I’m sorry.” Akasema
Janet
“ You are sorry ? akauliza
Ben
“ I’m sorry Ben.Naomba
nikueleze ukweli.Nimekuwa
nikikutana na Ernest kwa
siri.Naomba unisamehe sana
kwa hilo.Nakuahidi sintorudia
tena kufanya kosa kama hilo la
kukosa uaminifu.Mimi ni
binadamu na kila binadamu
anakosea.Sote tumekosea na
tunatakiwa kujifunza
kusameheana pale
tunapokoseana.Mambo mangapi
umenikosea Ben lakini
nimekusamehe. Ningekuwa
nataka kulipiza kisasi kwa yale
uliyoyafanya tusingefika hapa
tulipofika sasa hivi.Umezaa
watoto kadhaa nje ya
ndoa,ninawafahamu lakini
nimekusamehe kwa hilo na
ndiyo maana ndoa yetu
imeendelea kustawi.Naomba
nisamehe na mimi katika hili
.Tumekwishakuwa watu wazima
na hatutakiwi kuanzisha
malumbano yanayoweza
kuibomoa familia yetu.Tumepitia
mambo mengi katika safari yetu
hadi leo hii,tumevuka vikwazo
vingi mno na hata hili tunaweza
kulivuka pia” akasema Janet na
kwenda kupiga magoti mbele ya
Ben
“ Ben tafadhali naomba
unisamehe sana kwa jambo hili
la kuisaliti ndoa yetu.Nakuahidi
kwamba utakuwa ni mwisho
wangu kuonana tena na Ernest
.Nimekosa sana Be……………”
Janet akaangua kilio.Ben
akamtazama na kumshika
mkono akamuinua akamfuta
machozi.
“ Umeomba msamaha kwa
machozi na
nimekusamehe.Naomba
ulichokiongea hapa kiwe kitu
cha kweli na hautarudia tena
kufanya kosa hili.Nakuweka
wazi kwamba bado nitaendelea
kufuatilia mienendo yako na
endapo nitagundua kwamba
bado unaendelea na tabia zako
chafu nitakachokifanya naomba
usinilaumu.!! Akasema Ben
“ Ben nakuhakikishia
kwamba sintorudia tena
kufanya jambo hili
tena.Nimetubu na sintorudia
tena” akasema Janet
“ Nimekusamehe.” Akasema
Ben na kukumbatiana na
mkewe
“ Ahsante Ben.Ahsante sana
my King.” Akasema Janet huku
machozi yakiendelea kumtoka
“ Janet usiku huu naomba
uwe ni mwanzo wetu
mpya.Tuyafurahie maisha yetu
yaliyobaki badala ya kuongeza
matatizo.Tujiandae kumpokea
mjukuu wetu tutakayempata.”
Akasema Ben.Baada ya muda
wa sekunde kadhaa kupita Ben
akasema
“ Nieleze tatizo lililompata
Monica usiku huu.Nini
kimetokea? Nina wasi wasi
sana”
“ Kaman nilivyokueleza
awali kwamba hata mimi
sifahamu chochote hadi sasa
kwani Monica hajafunguka
chochote.Kila nilipojaribu
kumuomba anieleze kilichotokea
aliniambia nisubiri na
atakapokuwa tayari atanieleza
kila kitu.Nadhani lipo jambo
kubwa limetokea na tumpe
muda ili atakapokaa sawa
atueleze kwa ufasaha zaidi nini
kimetokea.Kwa sasa
anaonekana
kuchanganyikiwa.Namuonea
huruma sana Monica.Sijawahi
kumuona akiwa katika hali
ile.Tusubiri hadi asubuhi
atueleze kile kilichomtokea”
Akasema Janet