QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Next tyme msifanye hizi mambo. Kama stori ni ya kulipia mseme kuanzia mwanzo wasio na uwezo wasihangaike nayo.Muweke tangazo mwanzoni mwa stori kuwa kuna kulipia kuliko hali hii ya kutesa watu. Binafsi nimeshaisoma ila natoa angalizo kwa stori zitakazofuata. Kama lengo ni kuitangaza nendeni fb au humu muiweke jukwaa la matangazo

Naunga mkono hoja kwa aslilimia mia moja.
 
Sio kweli mkuu ukisemacho bali kujua kwingi mbele kiza..nishaweka peniela humu hakuna aliyelipia hata shilingi 5 lkn kwenye hii story ya queen monica watu wameleta ujuaji mwingi sana.mwishowe imekuwa shida nilikuwa naweka angalizo mara nyingi kuwa wakienda jikoni wasiseme mambo ya huku jf kuwa ipo.

Mwishowe haya ndio matokeo yake.wanajiona kama wajanja lkn ndio wametuharibia.

Mkuuu Lege nakubaliana na wewe kuwa kuna watu walichoma lkn usisahau hii ni Jf je una uhakika gani kama mwenye story hapiti humu kusoma au pengine ni member wa Jf pia.sina hakika kama kupelekea kulipia sisi wasomaji ni chanzo cha hayo yakuvujisha nadhani hii elf3 ilikuwa kwenye utaratibu wenu tu ikifika wakati member tulipie sio dili saana.kikubwa kama ni biashara basi ianzie mwanzo na sio kutuzunguuuusha kama watoto wadogo,binafsi nimetoa elf3 nanimeshasoma season 6 yote.
 
SEASON 6: SEHEMU YA 11

Ilimlazimu rais kuomba
radhi kwa mara nyingine tena
na kutoka nje ya kikao kwa ajili
ya kupokea simu muhimu.Safari
hii simu ilitoka kwa Habib.Rais
Ernest uso wake uliloa
jasho.Akavuta pumzi ndefu na
kuipokea simu ile ya Habib
“ Halow” akasema
“ Mheshimiwa rais
nimekupigia kutaka taarifa
kama tayari umefanikiwa
kumpata Yasmin” akasema
Habib .
“ Nimetuma kikosi maalum
Zanzibar kikiongozwa na
mkurugenzi wa idara ya
usalama wa taifa muda mfupi tu
baada ya kunipa taarifa zile na
tayari wamefika katika hoteli ile
uliyoelekeza.Hawajafanikiwa
kumkuta Yasmin lakini Tariq
amekutwa ameuawa.”
“ Tariq ameuawa? !!
akauliza Habib kwa mstuko
“ Ndiyo.Amekutwa katika
chumba chao akiwa amepigwa
risasi.Hatujui amepigwa risasi
na nani .Hivi sasa uchunguzi
unaendelea kubaini nini
kimetokea na wakati huo huo
tunaendelea na msako mkali
sana kumtafuta
Yasmin.Tunaamini bado yuko
kisiwani Zanzibar kwa hiyo njia
zote za kuingilia na kutokea
Zanzibar zimefungwa hakuna
kuingia wala kutoka.Hivi sasa
tumeshirikisha pia vikosi vya
jeshi la polisi katika kumsaka
Yasmin.Nakuhakikishia Habib
mpaka kufika asubuhi nitakuwa
na jibu zuri la kukupa kuhusu
Yasmin kama amepatikana au
bado” akasema Rais
“ Mheshimiwa rais
ninaamini Tariq ameuawa na
Yasmin ili apate nafasi ya
kutoroka akiwa na ile hati .Hata
hivyo swali ninalojiuliza haraka
haraka alipata wapi silaha
aliyotumia kumuulia Tariq?
Alitoka gerezani akiwa hana kitu
chochote imewezekanaje
akapata silaha na kumuua
Tariq? Kuna kitu kinafanyika
hapa mheshimiwa rais ambacho
kitasababisha matatizo
makubwa sana.Inaonekana wazi
kwamba wakati ameondoka Dar
es salaam Yasmin alikuwa na
silaha kwani kwa mujibu wa
maelezo ya Tariq aliyoyatoa kwa
Aziz ni kwamba Yasmin alikuwa
na bastora mbili ndani ya ndege
ambazo alizitumia kuwatishia
marubani ndipo wakabadili
uelekeo na kwenda
Zanzibar.Silaha hizi alitoa wapi?
Akauliza Habib.
“ Habib siwezi kuwa na jibu
la haraka la kukupa kuhusiana
na jambo hili.Nipe muda wa
kufanya uchunguzi kwanza ili
tubaini kama kweli Yasmin
ndiye aliyemuua Tariq na kama
ni yeye hizo silaha alizipataje?
Nitakupigia asubuhi na mapema
iwapo nitakuwa nimepata jibu
lolote toka kwa watu wangu
wanaoendelea na msako mkali
kule Zanzibar.”
“ Rais hii ni mara ya mwisho
ninazungumza nawe.Nataka
asubuhi unipigie simu na
kunijulisha kuwa tayari
umempata Yasmin.Ukumbuke
haya yalikuwa ni makubaliano
na tayari nimekwisha timiza
upande wangu.Nataka na wewe
utumize upande wako kwa
kunipatia kile
tulichokubaliana.Endapo
utashindwa kufanya kile
tulichokubaliana nakuonya
mheshimiwa rais athari zake ni
kubwa sana.Damu ya
watanzania itaendelea
kumwagika kila
uchao.Tunaipenda Tanzania na
hatujawahi kufikiria hata siku
moja kufanya shambulio lolote
lakini unatulazimisha kuanzisha
vita na nchi yako.”akasema
Habib
“ Habib nimekuomba unipe
muda nilishughulikie hili suala
kwani hakuna yeyote
anayefahamu hadi sasa nini
hasa kilichotokea .Hata mimi pia
nilifanya sehemu yangu nilitoa
kila kile ulichokitaka lakini ni
Yasmini mwenyewe aliyefanya
haya yanayotuumiza
vichwa.Nilitoa ndege ya
kuwapeleka Mogadishu na
Yasmin akaibadili uelekeo na
kwenda Zanzibar.Mimi sihusiki
kabisa na hili kwa hiyo naomba
tusiendele kulumbana tusubiri
vijana wafanye uchunguzi na
watupe majibu nini hasa
kilichotokea” akasema rais na
Habib akakata simu kwa hasira.
“ Uuphhh !!! rais akaegemea
ukuta na kushusha pumzi.
“ Mambo yanazidi kuwa
magumu.Bila kumpata Yasmin
tutaingia katika vita kali na
hawa jamaa.Naamini mpaka
kesho lazima Yasmin
atapatikana.” Akawaza rais na
kurejea tena ndani ya kikao
ambako mkuu wa jeshi la polisi
alimpa taarifa kwamba
amepokea ripoti muda mfupi
uliopita kwamba kuna ndege
imetua katika daraja la Nyerere.
“ Ndege imetua katika
daraja la Nyerere? Rais
akashangaa
“ Ndiyo mheshimiwa rais”
akasema mkuu wa polisi
“ Imekuaje hadi ndege hiyo
imetua darajani badala ya
uwanja wa ndege? Akauliza rais
“ Ripoti niliyoipokea
inasema kwamba ndege hiyo
ilikuwa inatokea Zanzibar na
ilikuwa na watu ndani yake
ambao walitakiwa kushikiliwa
kwa mahojiano na ndege
ilipogusa ardhi ya uwanja wa
ndege wa Julius Nyerere
walikuta vikosi vimewekwa
tayari vikiwasubiri hivyo
wakairejesha ndege hewani na
kwenda kutua katika daraja la
Nyerere.”
“ Oh my God !! akasema rais
na kushika kichwa
“ Wote waliokuwamo ndani
ya hiyo ndege wametoka
salama? Hakuna aliyepata
matatizo? Hakuna uharibifu
wowote ulitokea? Akauliza rais
kwa wasiwasi
“ Ndege imefanikiwa kutua
salama kwani kwa usiku huu
hakukuwa na magari hapo
darajani na baada ya kutua
watu hao waliokuwa wanatakiwa
kuhojiwa walifanikiwa kutoka
haraka na kutokomea
kusikojulikana.Aliyeumia ni
rubani mmoja aliyepigwa risasi
ya bega na watu hao wakati
wakiwalazimisha kutua katika
daraja la Nyerere ambaye kwa
sasa tayari amekwishakimbizwa
hospitali kwa matibabu.”
Akasema mkuu wa polisi.Rais
akainama kwa muda akafikri na
kuinua kichwa akawatazama
wajumbe wa kikao kile.Uso wake
ulionyesha hasira
“ Nani aliyetoa agizo la
kukamatwa kwa watu
waliokuwamo katika ndege hiyo
? Akauliza rais kwa ukali
“ Ni mimi mheshimwa
rais”akasema Jenerali Lameck
Msuba.
“ You ?!! akasema rais kwa
mshangao.Kukawa kimya kwa
muda kisha rais akasema
“ Ndugu zangu tuko katka
kipindi kigumu sana hivi sasa
kwa hiyo tunapaswa kuwa kitu
kimoja .Kuanzia sasa hakuna
yeyote atakayetoa agizo lolote
bila ya kupata ruhusa yangu
kwanza.Jambo lolote
linalotakiwa kufanywa lazima
lipitie kwanza
kwangu.Tumeelewana? akauliza
rais na wajumbe wote wakaitika
kisha kikao kikaendelea.
“ Kwa nini Lameck
akanipuuza na kuagiza Monica
akamatwe na ahojiwe? Sipendi
kuwa na ushirika na watu kama
hawa.Akiendelea na tabia yake
hii nitalazimika
kumuondoa.Napenda kuwa na
ushirika na watu watii..” Rais
akatolewa mawazoni baada ya
kupata taarifa nyingine toka
kwa mku wa jeshi la polisi
kwamba mzee Pantaleo Mgela
ambaye ni mfanyakazi wa ikulu
amekutwa amejinyonga karibu
na nyumbani kwake.Sura ya
rais ikaonyesha mstuko
“ Pantaleo amejinyonga?
Akasema rais na kuweka
mikono yake kichwani
“ Good job.Vijana
wamefanya kazi nzuri.Sasa
hakuna yeyote atakayejua kama
hati ile ni mimi ndiye
niliyeichukua.Ninachotakiwa
kufanya ni kuongeza nguvu
zaidi kumtafuta Yasmin na
kuipata hati ile.” Akawaza rais
Kikao kizito bado kiliendelea
kujadili hali ya usalama wa nchi
na hatua za kuchukua.Wajumbe
wakapewa dakika tano za
mapumziko na kisha warejee
kwa ajili ya kuendelea na
kikao.Rais akaitumia nafasi hiyo
kumuita Jenerali Lameck
wakaelekea katika chumba cha
maongezi ya faragha
“ Jeneral Lameck wewe ni
mshirika wangu na tuko katika
suala hili pamoja lakini kwa nini
ukanizunguka na kuyapuuza
maagizo yangu? Akauliza rais
kwa ukali
“ Utanisamehe mheshimiwa
rais lakini lengo langu lilikuwa
zuri .Nilitaka kufahamu sababu
za walinzi wale wote wanne
kupotezwa fahamu” akasema
Lameck
“ Tulilizungumza hilo na
nikakwambia tuachane nalo
kwani ndani ya ndege ile yuko
mwanangu lakini wewe
ukanipuuza na kutoa maagizo
yako.Kwa nini Lameck? Una
nguvu zaidi kunishinda mimi?
Akauliza rais
“ Nisamehe mheshimiwa
rais.Sintorudia tena” akasema
Lameck.Rais akamtazama kwa
muda kisha akasema
“ Sitaki jambo kama hili
lijirudie tena.Nikitoa maelekezo
naomba yafuatwe
tafadhali.Sipendi mtu
anayekwenda kinyume na
mimi.Tuko katika wakati
mgumu hivi sasa naomba
tusijaribu kuanzisha mtafaruku
mwingine baina
yetu.Tunatakiwa kuwa kitu
kimoja .Umenielewa Lameck?
Akauliza rais
“ Nimekuelewa mzee”
akasema Lameck na kutoka
katika kile chumba.Rais akatoa
simu na kumpigia Monica lakini
simu yake
haikupatikana.Akampigia Austin
lakini naye simu yake
haikupatikana.Akampigia simu
Janet.
“ Hallo Ernest.Habari
yako.Pole sana na tukio la leo.”
Akasema Janet baada ya
kupokea simu
“ Ahsante Janet.Samahani
sana kwa kukusumbua usiku
huu.Nahitaji msaada wako.”
“Sema Ernest unahitaji
msaada gani?
“ Nahitaji kuonana na
Monica usiku huu.”
“ Monica?!! Janet
akashangaa
“ Ndiyo Jane.Nataka
kuonana na Monica usiku huu
ni muhimu mno” akasema
Ernest
“ Ernest kuna nini hadi
utake kuonana na Monica usiku
huu?akauliza Janet
“ Kuna jambo limetokea
usiku huu ambalo natakiwa
nilitatue kabla
hakujapambazuka kwani
linaweza kumletea matatizo ”
Akasema rais na kumstua sana
Janet
“ Kuna nini kimetokea
Ernest?Monica amefanya nini?
“Nitakueleza baadae Jane
lakini naomba unisaidie niweze
kuonana naye hapa ikulu usiku
huu .Ninatuma kwako vijana
waje uwaelekeze mahala
anakoishi Monica.Usihofu ni
suala ambalo liko ndani ya
uwezo wangu na nitalimaliza”
akasema Ernest
“ Ernest umenistua sana
.Kuna nini kimetokea?akauliza
janet
“ Tutazungumza baadae
Jane .Vijana watakuja hapo
muda sim refu.Tafadhali nisaidie
nionane na Monica” akasema
Ernest na kukata simu.Kwa
dakika mbili Janet mwamsole
mama yake Monica alibaki
ameduwaa asijue cha
kufanya.Taarifa ile ya rais
ilimstua sana.Alijaribu kumpiga
simu ya Monica lakini
haikupatikana.Akawapigia simu
walinzi wa getini
akawafahamisha kwamba kuna
watu watakuja wanatoka ikulu
wakifika wamjulishe.Akarejea
chumbani kwake na kumkuta
mumewe bado amelala.Akakaa
kitandani akiwa na mawazo
mengi.
Baada ya dakika kumi na
tano simu ya mezani ikaita
akaipokea ilitoka kwa walinzi wa
getini wakamtaarifu kwamba
wale watu wamekuja .Akatoka
bila kumuaga mumewe akaenda
kuonana nao kisha
wakaongozana wote kuelekea
kwa Monica
 
SEASON 6: SEHEMU YA 12
Monica aliingia chumbani
kwake na kukaa kitandani
akaanza kumwaga machozi.
“ Ahsante Mungu kwa
kunirejesha salama” akasema
huku akilia
“ Austin !! akasema kwa sauti
ndogo na kushika kichwa
“ Yule Austin
niliyemshuhudia akifanya
mambo yale usiku huu ni yeye
kweli au ni Austin mwingine
anayefanana naye? Akajiuliza
“ Lakini ni yeye mwenyewe
.Ni yule yule Austin
ninayemfahamu.Ni Yule Yule
Austin ambaye ilibaki kidogo
nijitoe kwake.Sikujua kama
yuko namna hii.Who is he?
Akajiuliza na kuvuta pumzi
ndefu
“ Mambo niliyoyashuhudia
leo yanaogopesha .Wale si watu
wa kawaida na sitaki tena
ukaribu nao .Sikuamini
kumuona Amarachi akifanya
mambo kama yale.” Akaendelea
kuwaza Monica na picha ya
tukio zima ikamrudia kichwani
akatetemeka mwili.
“ Kuanzia sasa natakiwa
kuwa makini sana na marafiki
wapya.Nilipokutana na Austin
niliamini ni mtu mzuri na
anafaa kuwa mtu wangu wa
karibu lakini kumbe ni mtu wa
namna hii!! Nahisi Yule atakuwa
ni mpelelezi au ni jambazi.Lakini
jambazi hapana nahisi atakuwa
ni mpelelezi na ndiyo maana
anafahamiana na rais.Kama ni
mpelelezi kwa nini alikuja
kwangu na kuanzisha urafiki na
mimi? Kuna nini alikuwa
anakichunguza kwangu?
Akawaza Monica na kuanza
kuogopa.
“ Alikuja kwa kigezo cha
kushirikiana nami katika miradi
ya kijamii na kutokana na
muonekano wake nilimkubali na
kumuamini mara moja,kumbe
nilikaribisha nyoka.Nini alikuwa
anakichunguza kwangu? Halafu
nakumbuka alisema kwamba
kuna kitu anataka kunieleza
kuhusu mimi ni kitu gani hicho?
Alisema ananifahamu zaidi ya
ninavyojifahamu.Inawezekana
kuna jambo silifahamu
.Nilifanya kosa kutompa nafasi
ya kumsikiliza.Yawezekana kweli
ana jambo kubwa na la muhimu
alitaka kunieleza.” Akawaza
Monica
“ Hata hivyo sitaki kabisa
ukaribu na naye na sitaki
kumuona tena.Sasa naanza
kuona umuhimu wa kuwa na
walinzi kama alivyotaka
David.Itanilazimu kumuomba
ulinzi kwani tayari nimeanza
kuhisi hatari katika maisha
yangu.” Akawaza na kupanda
kitandani akajifunika,alihisi
baridi.
“ Monica I promised to tell
you something very important
about you.Please Monica it’s
important”
Maneno haya aliyoyatamka
Austin yakaendelea kujirudia
kichwani kwake.
“ Jambo gani Austin alitaka
kuniambia ambalo alisisitiza
kuwa ni la muhimu? Je kuna
umuhimu wakumtafuta na
kulifahamu? Akajiuliza
“Hakuna ulazima wowote wa
kufahamu lolote kutoka kwa
Austin.Ni mtu ambaye sitaki
kabisa kumuona kwa hili
alilolifanya leo.Ameniweka
katika hatari kubwa.Nivipi iwapo
ndege ile ingeshindwa kutua
katika daraja lile au
ingegongana na gari? Oh gosh !
sitaki hata kulikumbuka jambo
hili.Ni jambo baya kabisa
kuwahi kunitokea katika maisha
yangu na sina hakika kama
linaweza kufutika kwa haraka
katika kichwa changu.” Akawaza
“ Halafu sikuamini
niliposhuhudia Amarachi naye
akifanya mambo ya
hatari.Kumbe wote wako kitu
kimoja .Dah ! tukio hili la leo
litanitesa sana.Halafu Yule
mwanamke waliyekwenda
kumchukua ni nani? Nilisikia
wanamuita Shamim.Ana
umuhmu gani kwao hadi
wahatarishe maisha yao kiasi
kile? Akaendelea kujiuliza
maswali
“Swali lingine ninalojiuliza
Austin na rais ni watu wa karibu
sana ,kwa nini hakutaka
kuzungumza na rais moja kwa
moja na akanifuata mimi
nizungumze na rais ili niombe
kupatiwa usafiri? Kwa nini iwe
mimi? Halafu mbona rais
alikubali kirahisi sana
kunisaidia? Viwanja vyote vya
ndege vilikuwa vimefungwa
lakini rais akatumia uwezo wake
na ndege
ikapatikana.Inaonekana Austin
alifahamu kabisa kwamba rais
hawezi kunikatalia suala lile
nitakalomuomba na ndiyo
maana akaja kwangu.Whats
going on? Sasa naanza kupata
picha ya kile alichokuwa
anakisema Austin kuwa kuna
jambo anataka kuniambia
ambalo silielewi.” Monica
alikuwa na mawazo mengi mno.
Akiwa bado katika mawazo
mengi mara mlango wake
ukagongwa.Alistuka sana kwani
haikuwa kawaida ya watumishi
wake kumgongea kwa usiku
ule.Akavuta pumzi ndefu na
kuinuka akaenda kuufungua
mlango akakutana na mmoja wa
watumishi wake.
“Madam nimetaarifiwa na
walinzi kwamba mama
amekuja”akasema Yule
mtumishi
“ Mama ?!! Monica akastuka
akaingia tena chumbani akavaa
vizuri na kutoka kuelekea getini
.Ni kweli mama yake alikuwa
amekuja akiwa ameongozana na
watu wawili.Monica
akamkumbatia mama yake na
kutoa machozi
“ Mama nashukuru
umekuja” akasema Monica
mama yake akambembeleza
akanyamaza
“ Mama mbona uko hapa
usiku huu? Akauliza Monica
“ Monica nimelazimika kuja
hapa usiku huu baada ya
kupigiwa simu na rais.”
“ Rais amekupigia simu? !!
Monica akashangaa
“ Ndiyo amenipigia simu na
akanieleza kwamba kuna jambo
limekutokea nikastuka
sana.Nini kimetokea Monica?
Akauliza Janet
“ Mama ni hadithi
ndefu.Sina hakika kama
ninaweza kuliongelea hilo kwa
sasa.” Akasema Monica na
machozi yakamtoka
“ Monica hawa watu
nilioongozana nao wanatokea
ikulu wametumwa na rais
anataka kuonana nawe usiku
huu.”
“ Rais anataka kuniona?
Akauliza Monica huku macho
yake yakionyesha woga mkubwa
“ Ndiyo anataka kuonana
nawe”
Monica akainamisha kichwa
akafikiri kidogo na kusema
“ Mama sidhani kama niko
tayari kuonana na rais muda
huu.Kichwa changu nahisi
kama kimechanganyikiwa”
“ Monica rais ana lengo zuri
la kutaka kuliweka sawa jambo
lililotokea kabla
hakujapambazuka ili kusiwe na
tatizo lolote kwa upande wako”
akasema Janet na Monica
akainama akatafakari kisha
akasema
“ Sawa mama “ akaenda
ndani na kuvaa halafu
akaongozana na mama yake na
wale walinzi wakaelekea ikulu.
Walifika ikulu na rais
akataarifiwa kwamba wageni
wake tayari
wamewasili.Akawaacha
wajumbe wakiendelea na kikao
akaenda kuonana na
Monica.Aliwakaribisha vizuri
kisha akamchukua Monica
wakaenda katika chumba cha
maongezi ya faragha.
“Monica samahani sana kwa
kukusumbua usiku huu.Vile vile
napenda nikupe pole kwa
matatizo yote yaliyotokea usiku
wa leo.” Akasema rais
“Ahsante sana mzee”
akajibu Monica na kufuta
machozi
“ Nilistuka sana nilipopata
taarifa za kilichotokea “ akasema
rais na kunyamza kidogo halafu
akaendelea
“ Uliponipigia simu ukataka
usafiri nilituma watu wawili toka
usalama wa taifa waje
wakuchukue wakupeleke
Zanzibar na kuhakikisha
unamaliza shughuli zako na
kurejea salama.Kule Zanzibar
pia nikaagiza vijana wawili toka
usalama wa taifa waongezeke ili
kuimarisha zaidi ulinzi
wako.Baadae nikapata taarifa
kwamba wale walinzi
niliowatuma uongozane nao toka
hapa Dar es salaam wamekutwa
katika gari lao wakiwa
wamefungwa miguu na mikono
.Vile vile wale walinzi wawili wa
kule Zanzibar nao wamekutwa
hawana fahamu katika gari
lao.Hizi ni taarifa za kushangaza
sana na wakuu wa vyombo vya
usalama wakataka ndege
mliyopanda izuiliwe uwanja wa
ndege , mshikiliwe kwa
mahojiano lakini nilizuia hilo
lisifanyike kwa kujua kwamba
uko ndani ya ile ndege.Kuna
kiongozi mmoja akapuuza agizo
langu na kuamrisha
mtakaposhuka mkamatwe na
vikosi vikawekwa tayari uwanja
wa ndege jambo lililopelekea
mkaenda kutua katika daraja la
Nyerere.Thanx God mmetoka
salama.Nimekuita hapa ili
kufahamu nini hasa
kilichotokea? Naomba unieleze
ukweli wote Monica ili
nikusaidie kwani hivi
tunavyoongea mipango
inapangwa kuanza msako mkali
kuwatafuta na hasa wewe kwani
ndiye unayejulikana zaidi”
akasema rais.
Monica aliogopa sana
akalazimika kumsimulia rais
kila kitu toka alivyokuja Austin
na kumtaka ampigie simu
rais,walivyoondoka hadi
walivyofika Zanzibar na hadi
walivyorudi na kutua katika
daraja.Ernest Mkasa alihisi
mwili wake wote umeloa jasho
.Alihisi woga uliochanganyika na
hasira.Alitaka kuzungumza kitu
akashindwa midomo
ikamtetemeka.Monica
akashangaa
“ Mheshimiwa rais” akaita
Monica lakini rais hakujibu kitu
akabaki anamtazama.Baada ya
muda akatamka
“ Oh my God ! This is
another war!! Akasema kwa
sauti ndogo
“What war Mr president?
Akauliza Monica akishangazwa
na kauli ile ya rais
“ Sorry !Kichwa changu
kimekuwa na mambo mengi
sana siku ya leo” akasema rais
na kuinamisha kichwa kwa
muda kisha akasema
“ Monica suala hili
lililotokea si suala dogo lakini
nitahakikisha hakuna
atakayekugusa na jambo hili
litaisha kimyakimya.Mimi ndiye
rais wa nchi na nitakaloamua
hakuna wa kunipinga.Pamoja na
hayo ninahitaji msaada wako”
“Msaada gani mheshimiwa
rais?
“ Unafahamu anapoishi
Austin? Akauliza rais
“ Anapoishi Austin ?!!!
Monica akashangaa
“ Ndiyo umewahi kufika
mahala anakoishi Austin?
“ Austin ana makazi
mangapi? Nafahamu pale
tulipokutana siku ile kwa
chakula cha usiku.Sifahamu
kama ana makazi mengine”
“ Ile ni nyumba yangu
nilimpa kwa ajili ya makazi ya
muda na alihama na sijui kwa
sasa anaishi wapi.Nahitaji sana
kuonana naye usiku huu.”
Akasema rais
“ Austin aliniambia kwamba
wewe ni mtu wake wa karibu
inakuaje usifahamu mahala
anakoishi? Akauliza Monica
“ Alihama pale mahala
nilipomuweka aishi na sijui
alikohamia.Nataka nizungumze
naye kama nilivyozunguma
nawe.Yule ni kijana wangu na
sitaki yamkute matatizo
yoyote.Kama unafahamu mahala
aliko tafadhali naomba
unijulishe.” Akasema rais
“ Hapana sifahamu
mheshimiwa rais.” Akajibu
Monica
“ Nimejaribu kumpigia simu
hapatikani.Naomba kesho
asubuhi na mapema umpigie
simu na umueleze kwamba
unataka kuonana n aye na
akuelekeze mahala alipo ili
ukamuone kisha unipigie simu
na mimi nitatuma vijana wangu
watakufuatilia kwa nyuma hadi
u takapofika kwa
Austin.naomba sana Monica
unisaidie kwa hilo. Uko tayari
kunisaidia Monica? Akauliza
rais
“ Ndiyo mheshimiwa
rais.NItafanya hivyo” akajibu
Monica.Ukapita ukimya mfupi
rais akasema
“ Monica nashukuru sana
kwa kuitika wito wangu
japokuwa ni usiku mwingi
,nashukuru pia kwa maelezo
uliyonipa yamenipa picha kamili
ya kilichotokea.Nakuhakikishia
tena hakuna tatizo lolote
litakalokupata kwa hiyo kuwa
na amani. Endelea na shughuli
zako kama kawaida ila naomba
endapo utakuwa na tatizo lolote
usisite kunieleza na
nitakusaidia” akasema rais na
kuhitimisha maongezi yao na
kutoka katika kile chumba cha
maongezi ya faragha akaagana
na Janet wakaondoka kurejea
nyumbani.
Baada ya Monica kuondoka
rais akamuita Jenerali Lameck.
“Lameck kuna taarifa
nimezipata toka kwa Monica
ambaye ametoka hapa muda si
mrefu zimenipa mstuko mkubwa
sana”
“ Ni taarifa gani hizo
mheshimiwa rais? Akauliza
Lameck.Rais akavuta pumzi
ndefu na kumueleza Lameck
mambo yote aliyoelezwa na
Monica.
“ Mhh !! Lameck akaguna
“ mambo sasa yanataka
kuharibika.Kwa hiyo tunafanya
nini mheshimwia rais?
“ Hii ni vita mpya
imeanza.Kama tayari Austin
amempata Yasmin basi lazima
atafahamu kila kitu
kilichofanyika.Atafahamu
kuhusu makubaliano yangu na
Alshabaab na atafahamu
kuhusu hati ya muungano
niliyompa Yasmin.Lameck
tumetengeneza tatizo
kubwa.Austin ni tatizo kubwa
.Ni bomu ambalo tunapaswa
kulitegua haraka sana kabla
halijaleta madhara.Endapo
likilipuka litatuua sisi sote.Yule
kijana ni hatari najuta kwa nini
nilimtafuta.” Akasema rais.
“ Mheshimiwa rais
tunatakiwa kuelekeza nguvu
nyingi katika kumsaka hadi
tumpate Austin na wenzake
ndani ya muda mfupi ujao.”
Akasema Lameck
“ Kumpata Austin inaweza
isiwe kazi nyepesi sana na suala
hili linatakiwa kufanyiks kwa
haraka sana usiku huu kwani
tukichelewa hadi kesho asubuhi
tayari atakuwa amefahamu kila
kitu.Kilichobaki kwa sasa ni kitu
kimoja tu.Kumuua.Hana
thamani yoyote kwetu tena”
akasema rais na kunyamaza
baada ya mlinzi wake kutokea
na kumtaarifu kuwa anahitajika
kwenye kikao kuna jambo la
dharura linalohitaji uwepo
wake.Akaongozana na Lameck
kurejea katika ukumbi wa
mikutano.
“ Kuna taarifa gani
mmeipata? Akauliza rais baada
ya kuingia katika chumba cha
mikutano
“ Mheshimiwa rais tumepata
taarifa kutoka kwa vikosi
vilivyoko eneo la tukio
vikiendelea na jitihada za uokozi
kutafuta endapo kuna
manusura
wowote.Tumetaarifiwa kwamba
tayari wamefanikwia kulifikia
eneo la ukumbi wa mikutano
ambako wamezipata maiti
nyingi.Wamefanikiwa kupata
mwili wa makamu wa rais”
akasema kamishna jenerali wa
polisi na rais akainamisha
kichwa.Baada ya muda akauliza
“ Hakuna taarifa zozote
kuhusu mke wangu kwa sababu
naye alikuwamo ndani ya
ukumbi huo” akauliza rais
“ Mpaka sasa
hakuna.Tunaendelea kusubiri
taarifa zaidi.Tumepata pia
taarifa za Dodoma.Mpaka sasa
wamefanikiwa kupata maiti za
wabunge 207 na zoezi la
kuondoa vifusi ili kuwatafuta
maiti na mejeruhi zinaendelea”
akasema Mkuu wa jeshi la polisi
 
SEASON 6: SEHEMU YA 13
Monica hakutaka kurejea
tena nyumbani kwake usiku ule
akaelekea moja kwa moja
nyumbani kwa wazazi wake.
“ Monica nini hasa
kilichotokea? Nahitaji kufahamu
tafadhali” akasema mama yake
baada ya kufika nyumbani
“ Mama kichwa changu
hakiko sawa sawa.Naomba
funguo nikapumzike chumbani
kwangu nitawaeleza kila kitu
kesho asubuhi nitakapokuwa
nimetulia.” Akasema
Monica.Mama yake akamletea
funguo akaenda chumbani
kwake kulala.Akakaa kitandani
na kushika kichwa,alikuwa na
mawazo mengi.
“ Umekuwa ni usiku mbaya
sana katika maisha
yangu.Nahisi kichwa changu
kizito kama nimebeba
tofali.Mambo yaliyotokea usiku
wa leo ni mambio mazito
sana.Nashukuru rais
amenihakikishia kwamba
sintapata tatizo lolote.” Akawaza
na kukumbuka maongezi yake
na rais
“ Rais ameniuliza kama
ninafahamu mahala anakoishi
Austin.Yeye ndiye mtu wake wa
karibu ameshindwaje kufahamu
mahala alipo Austin hadi
anitumie mimi? Halafu
nilipomtajia kwamba nilikuwa
na Austin na ndiye niliyekwenda
naye Zanzibar alistuka mno hadi
jasho nikaliona usoni
pake.Kama haitoshi alionyesha
pia mstuko mkubwa pale
nilipomtajia kwamba Austin
alikwenda Zanzibar kumchukua
Yule mwanamke anaitwa
Yasmin.Alishindwa kuzungumza
na midomo ikamcheza.Kuna nini
kinaendelea hapa? Yasmin ni
nani? Akajiuliza
“ Rais ameonyesha kunijali
sana wakati nimefahamina naye
kwa siku chache tu.Leo
hakuonyesha hata kumjali
mama yeye lengo lake lilikuwa ni
kwangu tu.Ana nini na mimi
Yule mzee?
Alikosa majibu ya maswali
yake akapanda kitandani na
kujilaza.
“ Amenitaka nimpigie simu
Austin halafu nimtaarifu ili ili
atume vijana
wakamchukue.Kwa nini
anitumie mimi kumpata Austin?
Kwa nini yeye mwenyewe
asimpigie wakaongea kwa
sababu ni watu wa karibu?
Kuna tatizo gani kati yao?Jambo
hili naona halijakaa vizuri .Yeye
mwenyewe anatakiwa afanye
juhudi za kumtafuta Austin
kama alivyofanya juhudi za
kunitafuta mimi.Kuna kitu hapa
hakinipi picha nzuri
.Nilipokwenda kumtembelea
hospitali ,Austin alinihakikishia
kwamba rais ni mtu wake wa
karibu sana ambanye alikuwa ni
rafiki wa karibu wa baba yake
na amekuwa ni kama mlezi
wake. Kwa ukaribu huo walio
nao kwa nini alishindwa
kumpigia simu na kumuomba
amsaidie usafiri wa kwenda
Zanzibar hadi anitumie mimi?
Kwa nini aliamini akinitumia
mimi rais atanisikiliza na
kunipatia huo usafiri? Kuna
jambo gani alitaka kumficha rais
asijue? Halafu rais naye hataki
kumtafuta Austin anataka
kunitumia mimi kumpata
Austin,kwa nini? Akaujiuliza
“ Sintaweza kupata majibu
ya maswali haya hadi
nitakapoonana na Austin na
anieleze ukweli kitu gani
kimetokea kati yake na rais hadi
wameanza kukwepana.Kila
mmoja hataki kuwasiliana na
mwenzake moja kwa moja.Kesho
asubuhi nitajitahidi kwa kila
niwezavyo kumtafuta Austin na
nitahakikisha ninampata”
akawaza Monica .Akajaribu
kufumba macho kutafuta
usingizi lakini picha ya ndege
ikitua katika daraja la Nyerere
ikamjia na kufumbua macho
“ Kumbukumbu hii itanitesa
mno kwa muda mrefu .Ni tukio
ambalo sintalisahau katika
maisha yangu yote yaliyobaki.”
akawaza Monica

SEASON 6: SEHEMU YA 14

Janet aliingia chumbani
kwake na kumkuta mumewe
mzee Benedict amekaa
kitandani.Wakatazamana kwa
muda Benedict akasema
“ Umetoka wapi usiku huu?
Akauliza Ben ambaye sura yake
ilionyesha ukali
“ Samahani Ben nilipata
dharura nikatoka mara moja”
akasema Janet
“ Dharura? Ni Dharura ipi
hiyo ya usiku huu? Halafu kwa
nini ukaondoka bila kuniaga?
Nitaaminije kama kweli ulipata
dharura ? akauliza Benedict
“ Ben naomba
uniamini,ilitokea dharura
nikaondoka.Monica alipata
matatizo”
“ Matatizo?!! Akauliza Ben
“ Ndiyo alipata tatizo usiku
huu”
“ Alipata tatizo gani? Kwa
nini hukuniamsha na kunieleza
kama kuna tatizo? Akauliza Ben
“ Hata mimi
nilichanganyikiwa nilipopewa
taarifa hizo na ndiyo maana
nikaondoka hapa kama kichaa”
“ Nani alikupa taarifa hizo
?akauliza Ben.Janet akabaki
kimya
“Mbona hunijibu Janet ?
Ulizipata wapi taarifa hizo za
Monica? Nani alikutaarifu?
Akauliza Ben
“Ernest alinipigia simu”
akasema Janet na uso wa Ben
ukazidi kubadilika
“ Ernest alikupigia simu?
Akauliza kwa ukali
“ Ndiyo alinipigia
akanitaarifu kuwa kuna tatizo
limetokea linalomuhusuMonica
na anahitaji kuonana naye
usiku huu ikulu ili kulimaliza
suala hilo kabla ya
kupambazuka.”
“ Ernest amefahamuje kama
Monica ana tatizo? Ameanza lini
ukaribu na Monica? Kwa nini
alimtaka aende ikulu? Akauliza
Ben na Jane akabaki kimya
“ Jane naomba unieleze
ukweli,umemueleza Ernest
kuhusu Monica? Akauliza
Ben.Janet akabaki kimya
“ Oh my God ! umevunja
makubaliano yetu.Kwa nini
ukamueleza kuhusu suala hili?
Tulikubaliana usimueleze kitu
chochote lakini umeendelea
kukutana naye kwa siri na
umemueleza kila kitu.Kwa nini
Janet?akauliza Ben
“ Ilinilazimu nimueleze
ukweli kwani ana haki ya
kufahamu kama baba wa
Monica.Utanisamehe Ben lakini
nilifikiria sana na nikaona
sintakuwa namtendea haki
Monica endapo nitaendelea
kuificha siri hii.Anastahili
kumfahamu baba yake ambaye
ni Ernest.Najua hayakuwa
makubaliano yetu lakini baada
ya kutafakari nimeshindwa
kuvumilia na imenilazimu
kumueleza ukweli Ernest”
akasema Janet
Benedict akamtazama kwa
hasira na kuuliza
“ Monica naye umekwisha
mueleza kuhusu suala hili?
Akauliza
“ Hapana bado.Monica
sijamueleza chochote.”
“ You’ll pay for this
Janet.Tutaongea baadae suala
hilo lakini nieleze kwanza
Monica amepatwa na tatizo gani
hadi Ernest akamuita ikulu?
“ Hata mimi sifahamu nini
kimempata Monica kwani
hakuwa tayari kunieleza
chochote hata tulipofika ikulu
walikaa katika chumba cha
maongezi ya faragha na Ernest
wakaongea bila
kunishirikisha.Monica nimekuja
naye hapa yuko chumbani
kwake amelala.Anaonekana
hayuko sawa sawa kuna jambo
lazima limetokea.Ameahidi
kunieleza asubuhi kilichotokea”
akasema Janet .Ukapita ukimya
wa dakika zipatazo tano kisha
Janet akasema
“ Ben kuna jambo lingine
nataka nikutaarifu kuhusu
Monica” akasema Janet.Ben
akastuka na kumtazama Janet
“ Monica alinipigia simu na
kunieleza jambo Fulani ambalo
lilinistua kidogo” akanyamaza
tena.
“ Nieleze Jane ni jambo gani
hilo? Akasema Ben kwa shauku
ya kutaka kufahamu
“ Monica alinieleza kwamba
hajaziona siku zake na kwa
maelezo aliyonipa kuna kila
dalili kwamba atakua mjamzito”
Ben akahisi kama nyundo
kubwa imekipiga kichwa chake .
“ Ni ya kweli haya
unayonieleza Janet? Akauliza
Ben
“ Ni kweli kabisa.Hata yeye
mwenyewe jambo hili
lilimchanganya sana ikamlazimu
kunipigia simu kunieleza na
kuniomba ushauri” akasema
janet
“ Dah !! hili ni pigo kubwa
sana” akasema Ben .Alihisi
miguu kumtetemeka akakaa
kitandani.
“ Mipango yangu yote sasa
imeharibika.Hakuna
kitakachoendelea tena iwapo
David atagundua kwamba
Monica ana mimba.Kwa
niniMonica akafanya hivi.Tayari
amekwisha mpata bwana
mwenye mali nyingi,ni rais na
tajiri mkubwa afrika lakini kwa
nini ameshindwa kujituliza ili
aolewa na David ? Akajiuliza
Ben halafu akamtazama mkewe.
“Sikiliza janet tena naomba
unisikie kwa makini.Kama kweli
Monica ana ujauzito lazima
utolewe haraka sana.lazima
aolewe na David
Zumo.Tumepiga hatua kubwa
hadi hapa tulipofika na
tukishindwa kufikia malengo
itakuwa ni aibu kubwa sana
kwetu.Sitaki hilo litokee na
ndiyo maana nasema kwamba
hiyo mimba itatolewa na Monica
ataolewa na David Zumo.That’s
my order na hakuna wa
kulipinga hilo.Umenielewa Janet
!!! akauliza Ben kwa ukali na
kumtazama Janet kwa hasira
hadi akaogopa
“Ben jaribu kupunguza
hasira.Nafahamu jambo hili
limekustua sana na hata mimi
nilistuka hivyo hivyo kama
ulivyostuka wewe lakini bado
halijaishia hapo.Subiri nimalizie
kukueleza hadi mwisho”
akasema Janet na Ben
akamtazama kisha akaketi
kitandani
“ Monica aliniambia
kwamba alipokwenda Kinshasa
kumtembelea David walifanya
mapenzi na hii ilikuwa ni mara
ya kwanza kwake kufanya
mapenzi.Anasema kwamba yeye
na Ben hawakutumia kinga
yoyote na kwa hiyo kama kweli
atakuwa na mimba basi itakuwa
ni mimba ya David Zumo.Jambo
tunalopaswa kulifanya kwa sasa
si kumshawishi aitoe hiyo
mimba kwa kuwa muhusika
yupo na yuko tayari kumuoa
.Tunatakiwa kuhakikisha David
naMonica wanaoana kabla ya
mimba hiyo haijawa kubwa na
kugundulika” akasema Janet na
Ben akahisi mzigo mzito
uliokuwa kichwani kwake
ukishushwa
“ Amekwisha mueleza David
suala hili? Akauliza Ben
“ hapana bado.Nilimshauri
asimueleze kwanza hadi hapo
atakapokuwa na uhakika kuwa
kweli ana mimba kwani kukosa
kuona siku zake kunaweza
kuchangiwa na mambo mengine
pia lakini baada ya siku saba
anaweza akapime na kujua
iwapo ana mimba au vipi”
akasema Janet
“ Hizi ni taarifa zilizonistua
sana lakini kwa sasa angalau
nina ahueni.Nina uhakika
mkubwa kwamba David Zumo
akizipata taarifa hizi atakuwa na
furaha kubwa kwani hajawahi
kuwa na mtoto na mke wake
aliyefariki dunia.Ili kuongeza
msukumo wa ndoa yake na
David anatakiwa kumfahamisha
David mapema
zaidi.Ikiwezekana tunapokwenda
kuhudhuria mazishi ya mke
wake atafute nafasi na
kumueleza” akasema Ben
“ Nitamshauri hivyo.Ben
tunakwenda kumpata mjukuu
wetu wa kwanza” akasema Janet
huku akitabasamu.
“ Ni jambo la faraja sana
kumpata mjukuu lakini furaha
yangu yote yakumpata mjukuu
imeharibniwa na kitendo chako
cha kumwambia Ernest kwamba
Monica ni mwanae.Ulifanya kosa
kubwa sana Janet”
“ Ben najua nimekukosea
sana lakini sintomtendea haki
Ernest kama nisingemueleza
ukweli kuhusu Monica.Muda
utafika ambao mambo yote
lazima tuyaweke wazi.Siwezi
kwenda kaburini na siri hii
lazima niiweke wazi.Najua ni
jambo zito litakalomuumiza
sana Monica lakini hatuna
namna lazima ukweli
ujulikane.Hapo awali niliogopa
sana nini kitatokea iwapo
Monica akifahamu kuwa wewe si
baba yake.Niliogopa kumuumiza
kiakili ila baada ya kutafakari
kwa kina nimeamua ni bora
endapo nitamueleza ukweli
potelea mbali kama ataumia
lazima ajue kila kitu.Ben
utanisamehe sana kwa
hili,lakini nakuhakikishia
kwamba hata kama ikitokea
Monica akaufahamu ukweli
ataendelea kukutambua wewe
kama baba yake.Umemlea kwa
mapenzi makubwa toka akiwa
mdogo na hadi sasa bado
unaendelea kumpenda .Mpaka
anaingia kaburini wewe utabaki
kuwa ni baba yake.She’ll never
choose him over you.” Akasema
Janet.
“ Nafahamu ataendelea
kuwa mwanangu na
atanichagua mimi badala ya
Ernest but it’ll never be the
same again.Haitakuwa kama
awali.Mambo yatabadilika
akiufahamu ukweli.Umeniingiza
katika vita na Ernest .” Akasema
Ben
“ Ben tafadhali naomba
jambo hili lisiwe chanzo cha
ugomvi kati yako na
Ernest.Hakuna sababu ya wewe
na yeye kuingia katika vita kwa
sababu ya Monica.Huyu ni
mwanenu wote.Mkiingia katika
vita mtamsababishia matatizo
makubwa Monica.Nakuomba
Ben usiwe na hasira na
Ernest.Mnatakiwa mkae kama
watu wazima mmalize tofauti
zenu.Hii ni kwa ajili ya Monica.”
Akasema Janet.Ben akainuka
na kumtazama Janet kwa hasira
“ Mimi nikae na Ernest?
Nikae na mtu anayenisaliti na
mke wangu? That wont happen
!! me and him we’re enemies !!
akasema Ben.Janet naye
akasimama
“ Ben unamaanisha nini
unaposema kwamba Ernest
anakusaliti na mke wako? Una
maanisha kwamba mimi
ninatembea na Ernest? Akauliza
Janet kwa ukali na wote wawili
wakatazamana kwa hasira
“ Unajaribu kujitetea?
Akauliza Ben na Janet akataka
kumnasa kibao Ben akamshika
mkono
“ Usithubutu kuninasa
kibao shetani wewe.Unadhani
sifahamu mambo
unayoyafanya? Janet
ninafahamu kila kitu
unachokifanya.Nimeweka watu
wa kukufuatilia kila
unachokifanya.Ninafahamu kila
kitu kuhusu wewe na
Ernest.Bado mnaendelea
kukutana kwa siri katika hoteli
yake na hadi chumba na tarehe
ambazo mmekutana ninaweza
kukutajia.Hivi juzi tu
mmekutana tena
hospitali,unakataa na hayo?
Tafadhali usitake kunitibua akili
yangu nikakuingiza na wewe
katika orodha ya maadui
zangu.Ernest atabaki kuwa adui
yangu milele .!! akasema Ben na
macho ya mkewe Janet yalijaa
machozi.
“ Ben I’m sorry.” Akasema
Janet
“ You are sorry ? akauliza
Ben
“ I’m sorry Ben.Naomba
nikueleze ukweli.Nimekuwa
nikikutana na Ernest kwa
siri.Naomba unisamehe sana
kwa hilo.Nakuahidi sintorudia
tena kufanya kosa kama hilo la
kukosa uaminifu.Mimi ni
binadamu na kila binadamu
anakosea.Sote tumekosea na
tunatakiwa kujifunza
kusameheana pale
tunapokoseana.Mambo mangapi
umenikosea Ben lakini
nimekusamehe. Ningekuwa
nataka kulipiza kisasi kwa yale
uliyoyafanya tusingefika hapa
tulipofika sasa hivi.Umezaa
watoto kadhaa nje ya
ndoa,ninawafahamu lakini
nimekusamehe kwa hilo na
ndiyo maana ndoa yetu
imeendelea kustawi.Naomba
nisamehe na mimi katika hili
.Tumekwishakuwa watu wazima
na hatutakiwi kuanzisha
malumbano yanayoweza
kuibomoa familia yetu.Tumepitia
mambo mengi katika safari yetu
hadi leo hii,tumevuka vikwazo
vingi mno na hata hili tunaweza
kulivuka pia” akasema Janet na
kwenda kupiga magoti mbele ya
Ben
“ Ben tafadhali naomba
unisamehe sana kwa jambo hili
la kuisaliti ndoa yetu.Nakuahidi
kwamba utakuwa ni mwisho
wangu kuonana tena na Ernest
.Nimekosa sana Be……………”
Janet akaangua kilio.Ben
akamtazama na kumshika
mkono akamuinua akamfuta
machozi.
“ Umeomba msamaha kwa
machozi na
nimekusamehe.Naomba
ulichokiongea hapa kiwe kitu
cha kweli na hautarudia tena
kufanya kosa hili.Nakuweka
wazi kwamba bado nitaendelea
kufuatilia mienendo yako na
endapo nitagundua kwamba
bado unaendelea na tabia zako
chafu nitakachokifanya naomba
usinilaumu.!! Akasema Ben
“ Ben nakuhakikishia
kwamba sintorudia tena
kufanya jambo hili
tena.Nimetubu na sintorudia
tena” akasema Janet
“ Nimekusamehe.” Akasema
Ben na kukumbatiana na
mkewe
“ Ahsante Ben.Ahsante sana
my King.” Akasema Janet huku
machozi yakiendelea kumtoka
“ Janet usiku huu naomba
uwe ni mwanzo wetu
mpya.Tuyafurahie maisha yetu
yaliyobaki badala ya kuongeza
matatizo.Tujiandae kumpokea
mjukuu wetu tutakayempata.”
Akasema Ben.Baada ya muda
wa sekunde kadhaa kupita Ben
akasema
“ Nieleze tatizo lililompata
Monica usiku huu.Nini
kimetokea? Nina wasi wasi
sana”
“ Kaman nilivyokueleza
awali kwamba hata mimi
sifahamu chochote hadi sasa
kwani Monica hajafunguka
chochote.Kila nilipojaribu
kumuomba anieleze kilichotokea
aliniambia nisubiri na
atakapokuwa tayari atanieleza
kila kitu.Nadhani lipo jambo
kubwa limetokea na tumpe
muda ili atakapokaa sawa
atueleze kwa ufasaha zaidi nini
kimetokea.Kwa sasa
anaonekana
kuchanganyikiwa.Namuonea
huruma sana Monica.Sijawahi
kumuona akiwa katika hali
ile.Tusubiri hadi asubuhi
atueleze kile kilichomtokea”
Akasema Janet
 
SEASON 6: SEHEMU YA 15
Imetimu saa nane za
usiku,bado rais alikuwa katika
kikao na wakuu wa vyombo
mbalimbali vya ulinzi na
usalama wakijadiliana kile
kilichotokea ,hatua za kuchukua
na vile vile waliendelea kupokea
taarifa kutoka kwa vikosi
vilivyoendelea na kazi ya
kufukua vifusi katika majengo
yaliyolipuliwa kutafuta maiti na
watu walionusurika .Mjini
Dodoma mpaka kufikia muda
huyo tayari jumla ya maiti 346
zilikuwa zimepatikana na zoezi
liliendelea kutafuta maiti
wengine kama wapo.Jijini Dar es
salaam maiti zaidi ya mia tatu
zilikuwa zimepatika.Katika
ukumbi uliokuwa wa mikutano
maiti zaidi ya maiti mia mbili
zilipatikana na nyingi zikiwa
zimeharibika vibaya sana kiasi
cha kushindwa kutambulika.
Mjadala mkubwa uliokuwa
ukiendelea katika kikao kile ni
hatua za kuchukua baada ya
Alshabaab kujitangaza kuwa
walihusika na shambulio
lile.Kulikuwa na mabishano
ambapo baadhi ya wajumbe
walitaka uchunguzi wa kina
ufanyike kabla ya kuchukua
hatua zozote.Wengine walitaka
hatua za haraka sana
zichukuliwe dhidi ya wale
waliotekeleza shambulio lile
baya.Mvutano ulikuwa mkali
sana ndani ya kikao kile.Mkuu
wa majeshi akasimamana
kuwatuliza wajumbe waliokuwa
wakivutana kisha akasema
“Mheshimiwa rais,mimi
kama mkuu wa majeshi nina
haya ya
kusema.Tumeshambuliwa.Adui
aliyetushambulia anafahamika
na tayari amejitokeza hadharani
akakiri kuhusika na unyama
huu mkubwa uliotokea na kama
haitoshi bado anaendelea kutoa
vitisho vya mashambulio zaidi
iwapo hatutakuwa tayari
kutekeleza matakwa yake.Mimi
kama mkuu wa majeshi
napendekeza kwamba
tusikubaliane na matakwa yake
kwani huo ni ushindi kwake.Sisi
ni nchi yenye nguvu,sisi
tunajeshi kubwa lenye nguvu na
linaloogopeka afrika kwa nini
tusumbuliwe na kikundi kidogo
kama Alshabaab? Hatuwezi
kukulbali hilo.Kwa kuwa
Alshabaab wametangaza vita
kazi yetu ni kuwaonyesha sisi ni
nani.Dunia inapaswa kutambua
kwamba Tanzania ni nchi ya
amani lakini ikichokozwa kipigo
chake hakina
mfano.Tuwaonyeshe kazi hawa
Alshabaab” akasema Jenerali
Lameck Msuba.Watu wote mle
ndani ya chumba wakabaki
kimya wakisubiri maamuzi ya
rais.
“ Ndugu wajumbe
,nimeyasikia mawazo yenu
kuhusiana na jambo hili na
kama alivyosema Jenerali
Lameck kwamba hiki
kilichofanywa na Alshabaab ni
tangazo la vita.Sisi kama taifa
hatutaweza kukubaliana na
uchokozi huu na ninakubaliana
na mkuu wa majeshi kwamba
hakuna muda wa kupoteza
kufanya uchunguzi wakati tayari
adui tunamfahamu na
anatamba.Mimi kama rais natoa
ruhusa ya kuwaonyesha kazi
hawa mashetani.Nataka mpaka
kutakapopambazuka tayari niwe
nimesikia jeshi letu limeanza
kuwafundisha adabu
maharamia hawa.Hatuwezi
kuishi kwa wasiwasi na kikundi
kidogo kama hiki.Mkuu wa
majeshi kaa na makamanda
wako na mpange namna ya
kuanza kuwafunza adabu hawa
jamaa lakini kabla ya kufanya
shambulio lolote naomba
kwanza nijulishwe.” Akasema
rais kisha akainuka akatoka mle
ndani ya chumba akatoa simu
na kuzitafuta namba za Habib
akampigia
“ Mheshimiwa rais,kuna
taarifa nzuri unataka kunipa?
Akauliza Habib baada ya
kupokea simu
“ Habib kuna jambo nataka
kukutaarifu.Kwanza kuna
taarifa za kutia moyo kuhusiana
na mahala aliko Yasmin.Kuna
kila dalili kwamba anaweza
akapatikana hadi kufikia
asubuhi.Jambo la pili nataka
kukujulisha kwamba kwa saa
kadhaa sasa nimekuwa na kikao
na wakuu wa vyombo vya
usalama na kufuatia lile tamko
lako kuwa Alshabaab ndio
wanaohusika katika
mashambulio yale mawili,kikao
kimeamua kwamba yafanyike
mashambulio katika kambi za
Alshabaab .Nimeona nikujulishe
hilo ili uwataarifu watu wako
wote watoke katika kambi hizo
zitakazoshambuliwa” akasema
rais
“Mnataka kutushambulia?
Mnataka kuharibu kambi zetu
na kuua watu wetu? Akauliza
Habib kwa mshangao
“ Habib lengo la kufanya
hivyo ni kuzuia kutokufanyika
kwa uchunguzi wowote
kuhusiana na mashambulio
yaliyotokea na ndiyo maana
nimeamua kukupigia ili
kushauriana nawe kuhusu
jambo hili.Nakuahidi kwamba
nitagharamia mimi mwenyewe
ujenzi wa kambi hizo baada ya
kuharibiwa.Nitatoa fedha nyingi
katika suala hili.Naomba
tukubaliane katika hilo Habib”
akasema rais na wakajadiliana
na Habib kwa muda wa zaidi ya
dakika kumi kisha wakaagana
kisha akampigia simu Jenerali
Lameck na kumtaka waonane.
“Nimezungumza na Habib
muda mfupi
uliopita.Nimemtaarifu kwamba
tunataka kufanya mashambulio
mawili katika kambi
zake.Haikuwa rahisi lakini
tumekubaliana na amenipa
namba za simu za mmoja wa
makamanda wake ambaye
mtawasiliana na atakupa
maelekezo yote.” Akasema
rais.Wakati akijadiliana na
Lameck simu yake
ikaita,zilikuwa ni namba ngeni
katika simu yake.Akasogea
pembeni na kuipokea
“Hallow”akasema
“Hallow Mr president”
ikasema sauti ya mwanamke
upande wa pili na Ernest
akastuka sana.Akatazama kama
kuna mtu yeyote pale karibu
yake kisha akauliza
“Nazungumza na nani?
Mwanamke Yule akatoa
kicheko kidogo kisha akasema
“Ni kweli umeisahau sauti
hii au umechanganyikiwa baada
ya kuisikia? Akauliza Yule
mwanamke
“ tell me who are you or I’ll
hang up !! akafoka rais
“ Fine .Yuu want to know
who I am? Its me Agatha your
wife”
Ernest akashusha
pumzi.Alikosa neno la kuongea
akabaki ameishikilia simu
sikioni
“ I’m not dead mr
President.I’m still alive.”
Akasema Agatha.Bado rais
aliendelea kukaa
kimya.Hakuamini kile
alichokisikia.
“Mr president samahani
kwa kukusumbua usiku huu
najua una mambo mengi
kuhusiana na shambulio
lililofanywa na
Alshabaab.Nitakupigia tena siku
nyingine kwa sasa nakuacha
umalize kwanza shughuli za
msiba huu mkubwa wa taifa.”
Rais akavuta pumzi ndefu
na kusema
“ Where are you?
“ Just wait for my call mr
president anytime soon”
akasema Agatha na kukata
simu.Ernest akachanganyikiwa.
MPENZI MSOMAJI
USIKOSE SEASON 7
ITAKAYOKUWA SEHEMU YA
MWISHO YA SIMULIZI HII ILI
UFAHAMU MWISHO
UTAKUAJE.
 
Mbududa, hongera na Asante maana wengine tulishakata tamaa.

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom