QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: FINAL SEASON
SEHEMU YA 8

Mlango wa chumba alichokuwamo
Irene ukafunguliwa akaingia jamaa
mmoja mrefu mwenye ndevu
nyingi.Alikuwa amevaa koti refu la
rangi ya kahawia.Akavuta kiti na kuketi
mbele ya Irene
“Habari yako Irene” akasema yule
jamaa mwenye sauti ya
kukwaruza.Monica akamtazama na
kusema
“Nahitaji kwanza kuwaona wazazi
wangu.Nionyesheni waliko wazazi
wangu”
“Usihofu Irene wazazi wako wako
salama na wanapata huduma
nzuri.Baba yako anapumzika hivi sasa
huku akiendelea na matibabu.Yupo
daktari tumempa kazi ya
kumuhudumia kwa hiyo sisi si watu
wabaya.Utawaona wazazi wako muda si
mrefu sana lakini kwanza kuna jambo
ambalo tumekuitia hapa.Naomba utupe
ushirikiano tafadhali” Akasema Yule
jamaa halafu akainuka akaufungua
mlango na kuwakaribisha ndani watu
wawili mle chumbani na Irene
akapatwa na mshangao mkubwa sana.
“Madam Agatha?!! Akasema kwa
mshangao
“Hallo Irene” akasema Agatha
“Siamini macho yangu.Ni wewe
ndiye unayenifanyia hivi?akauliza
Irene
“Irene tafadhali naomba utulie na
utoe ushirikiano na kama utakuwa
jeuri utapata matatizo makubwa sana
na kuna hatari hata wazazi wako
ukawapoteza kwa hiyo tulia ,jibu vizuri
maswali utakayoulizwa na baada ya
hapo utaachiwa wewe na wazazi wako
mtandao.Hakuna mwenye lengo la
kukudhuru lakini endapo utaonyesha
ukaidi utatulazimisha tutumie nguvu”
Akasema Agatha
“Siamini madam Agatha.Kumbe na
wewe ni mtu mbaya namna hii.Una sura
nzuri kama malaika lakini kumbe ni
shetani mkubwa.kwa nini umenifanyia
hivi ? kwa nini umewatesa wazazi
wangu? Kwa nini mmemuua Flora?
Kama mlikuwa na shida na mimi kwa
nini msingenichukua mimi peke yangu
hadi muwachuikue na wazazi wangu na
kumuua Flora? Akauliza Irene.Agatha
akaletewa kiti akaketi na kumtazama
Irene
“Irene tumalize maongezi yetu na
tukuachie wewe na wazazi wako
muondoke.Kuna kitu kimoja tu
ninachotaka kukifahamu toka
kwako.Ulinipigia simu jana ukanitaka
nitoke katika lile jengo la hoteli
nilimokuwamo kwani kuna jambo baya
litakwenda kutokea hapo.Nilikusikia na
nikaondoka na baadae jengo
likalipuliwa.Taarifa hizi za kutokea
mlipuko katika lile jengo ulizipata
wapi?Ulijuaje kama niko ndani ya ile
hoteli? Nijibu maswali hayo na
nitakuachia uende zako” akasema
Agatha.
“Irene ,Irene !! Kupitia kile kifaa
alichokiweka sikioni ,Irene akasikia
sauti ya Job ikimuita
“Usimjibu hicho
alichokuuliza.Mjibu chochote ili
kupoteza muda kwani sisi tuko nje ya
jengo hili ulimo tunaingia ndani
kukufuata” akasema Job
“Irene umesikia nilichokuuliza?
Akauliza Agatha
“Umekosea madam Agatha si mimi
niliyekupigia simu.Sijawahi kukupigia
simu,sina namba zako na wala
sifahamu chochote kuhusiana na
mlipuko uliotokea.Mtafute mtu
aliyekupigia na si mimi” akasema
Irene.Sura ya Agatha ikaanza kubadlika
“Irene tafadhali usinilazimishe
nikuharibu binti yangu.Ninakupenda
sana na tafadhali nijibu maswali
niliyokuuliza” Akasema
“Madam Agatha una sura nzuri
lakini kumbe moyoni ni
shetani.Unawezaje kunifanyia hivi
halafu ukasema eti
unanipenda?Unawezaje kuwatesa
wazazi wangu kiasi hiki ilihali sina kosa
lolote? Akauliza Irene kwa kujiamini
“Irene hii ni mara ya mwisho
ninakuomba ujibu maswali
niliyokuuliza” akasema Agatha kwa
ukali.Irene hakumjibu kitu wakabaki
wanatazamana.Agatha akainuka na
kumsogelea Irene
“Irene tafadhali usijaribu kutaka
kucheza na mimi.Nitakufanyia kitu
kibaya sana.kama kweli unawapenda
wazazi wako nijibu maswali yangu ama
sivyo utawapoteza ndani ya muda
mfupi ujao.Mimi ni mtu mbaya sana
kama ukinifanyia kiburi.Naomba
usinilazimishe nikufanyie kitu kibaya
Irene.Nijibu maswali yangu nikuachie
uende zako” akasema Agatha.Irene
akamtazama kwa macho yalioyojaa
dharau na kwa ujasiri mkubwa
akamtemea Agatha mate usoni.Kitendo
kile kilimkasirisha mno akaanza
kumchapa makofi.Mdomoni mwa Irene
ilianza kuonekana damu kutokana na
makofi aliyopiga.
Job na Daniel walifanikiwa
kuwadhibiti wale watu wawili
waliokuwa nje ya ile nyumba na
kuwapoteza fahamu kisha kuwaficha
chini ya uvungu wa gari wakaingia
ndani kwa tahadhari kubwa
sana.Walitembea kwa kunyata na
nyumba ile ambayo ilionekana kama
ofisi ilikuwa kimya kabisa .Sauti za
watu wakuiongea zilisika kwa
mbali.Wakatokeza katika varanda na
Job akachungulia akawaona watu
wawili wakiwa wamesimama nje ya
mlango mmoja.Akawachunguza kwa
haraka namna walivyokaa
“Daniel tunawaondoa wale jamaa
waliosimama pale kwenye ule mlango
ili tuweze kuingia ndani ya kile
chumba.Nadhani kuna kitu cha muhimu
ndani ya kile chumba ndiyo maana
wanalinda” akasema Job na kisha
akahesabu moja hadi tatu na kama
umeme wakajitokeza katika lile
varanda na kuwamiminia risasi wale
jaama wawili kwa kutumia bastora zao
zilizofungwa viwambo vya sauti na wale
jamaa wawili ambao hawakuwa
wamejua kama watashambuliwa
wakaanguka chini.Haraka haraka Job
na Daniel wakakimbia kuelekea katika
mlengo ule ambao wale jamaa
walikuwa wamesimama na kabla
hawajaufikia mlengo ule ukafunguliwa
akatoka mtu mmoja akiwa na koti
jeupe na alipowaona akina Job wakiwa
na bastora akataka kupiga kelele lakini
Job akamuwahi akamfanyia ishara
asithubutu kupiga kelele.Wakawavuta
wale jamaa na kuwaingiza ndani ya kile
chumba.
“Jamani naombeni msiniue
tafadhali” akasema Yule jamaa huku
akitetemeka
“Irene yuko chumba gani?
Akauliza Job
“Simfahamu Irene.Mimi ni daktari
nimeletwa hapa kuja kumtibu
mgonjwa”
“Mgonjwa yupi? Yuko wapi?
Akauliza Daniel
“Yuko ndani ya chumba hicho”
akasema Yule jamaa na kuwaelekeza
akina Job mlango.Job akaufungua
mlango ule alioelekeza Yule jamaa na
kuwakuta watu wawili.Mmoja
mwanaume mwenye umri kati ya miaka
sitini hivi akiwa amekaa kitandani
ametundikiwa chupa ya maji na
pembeni yake akiwa amekaa
mwanamke mmoja ambaye mavazi
yake yalikuwa yameloa damu.Mara
moja Job akawatambua watu wale
kuwa ni wazazi wa Irene kwani
aliwaona katika video ile
aliyoonyeshwa na Daniel.
“ Ninyi ni wazazi wa Irene?
Akauliza Job
“Ndiyo baba” akajibu yule mama
kwa woga
“Naitwa Job ni rafiki wa Irene
tumekuja hapa kuwaokoeni” Akasema
Job halafu akamuita Daniel ambaye
alitambuliwa mara moja na mama yake
Irene
“Oh Daniel !! akasema mama yake
Irene kwa mshangao.Daniel
akamfanyia ishara akae kimya.
“Tunawatoa nje watu hawa.Please
cover my back” akasema Job
akamuamuru Yule daktari aishike
chupa ya maji aliyokuwa ametundikiwa
baba yake Irene halafu akambeba
begani na kwa tahadhari kubwa
wakaanza kutoka nje ya kile chumba
kuelekea nje
Kitendo cha Irene kumtemea mate
Agatha kilimchefua sana mama Yule
ambaye aliendelea kumshambulia
Irene kwa makofi hadi pale
alipozuiliwa na Silvanus Kiwembe
aliyekuwa ameambatana naye
“Imetosha Agatha.Utamuumiza na
tukashindwa kupata taarifa za
muhimu” akasema Silva
“Huyu mtoto ana kiburi sana
Silva.Niacheni nimfundishe adabu.!!
Akasema kwa ukali Agatha huku
akihema kwa haraka haraka
“kwa kuwa amenichefua nenda
kawalete wazazi wake.Sina huruma
naye tena.Nitawateketeza wazazi wake
mmoja baada ya mwingine na
asiponieleza ninachokitaka hata yeye
mwenyewe nitammaliza!! Akasema
Agatha na kumuamuru Yule jamaa
mwenye koti refu akawalete wazazi wa
Irene.
Job na Daniel wakisaidiwa na Yule
daktari walifanikiwa kuwatoa nje
wazazi wa Irene na kuwaficha nyuma
ya banda moja lililokuwa karibu halafu
Yule daktari akafungwa kamba miguu
na mikono akajazwa vitambaa
mdomoni kisha wakarejea ndani kwa
tahadhari kubwa.
Yule jamaa aliyetumwa kuwaleta
wazazi wa Irene alistuka sana alipokuta
michirizi ya damu katika mlango wa
kuingilia chumba walimokuwamo
wazazi wa Irene.
“Eddy !! akaita lakini
hakujibiwa.Akachomoa bastora
“Eddy !! akaita tena lakini
hakujibiwa akasogea taratibu hadi
mlangoni.Kabla hajaufungua
akatazama huku na huku kama kuna
mtu nyumba yote ilikuwa kimya
akakizungusha kitasa na mlango
ukafunguka akapatwa na mstuko
mkubwa.Wenzake wawili walikuwa
wamekwisha uawa.Akaubamiza mlango
na kuanza kukimbia lakini akina Job
tayari walikwisha muona na Daniel
akamuwahi kumpiga risasi ya bega la
kushoto akanguka chini kisha
akageuka kwa kasi ya ajabu na kwa
kutumia mkono wake wa kulia
uliokuwa na bastora akavurumisha
risasi kuelekea upande ule
waliokuwepo akina Job.Bastora yake
haikuwa na kiwambo hivyo mlio
mkubwa wa risasi ukasikika.Job kwa
shabaha ya aina yake akamlenga Yule
jamaa risasi mbili na kummaliza.
Mlio ule wa risasi uliwastua
Agatha na Silva waliokuwa katika
chumba alimokuwamo Irene
“Stay here.Ngoja nikaangalie kuna
nini” akasema Silva
“Silva hapana.Siwezi kubaki peke
yangu hapa” akasema Agatha kisha
akamfuata Silva kwa nyuma wakatoka
ndani ya kile chumba.Silva akafungua
mlango akatoka na kwenda
kuchungulia katika Varanda akawaona
watu wawili wakiwa wanamshachi yule
jamaa mwenye koti refu akahisi nguvu
zinamuishia akamgeukia Agatha na
kumtaka waondoke haraka sana kwani
kuna watu wamewavamia.
“Vipi kuhusu Irene? Amekwisha
tuonana anatufahamu kwa hiyo
tukimuacha hai anaweza akawa ni
tatizo kubwa kwetu.Kill her !! akasema
Agatha.
“Agatha leave her.We don’t have
time.” Akasema Silva na kumshika
mkono Agatha ,wakazima taa ye eneo
lile walilokuwapo kukawa na mwanga
hafifu wakaitumia nafasi hiyo kuingia
katika chumba kingine kilichokuwa
karibu na kile alichokuwamo Irene.
“Agatha na mwenzake
wanatoroka.fanyeni haraka”Irene
akawaambia akina Job kupitia kifaa
kile wanachokitumia kuwasiliana
Job na Daniel wakaenda kwa
haraka upande ule uliokuwa
umezimwa taa na mara wakasikia sauti
ya Irene akiita .Haraka haraka
wakaifuata sauti ile na kumkuta Irene
katika chumba akiwa amefungwa
katika kiti
“wafuateni haraka watatoroka”
akasema Irene kisha Job na Daniel
wakatoka mbio wakaanza kufuatilia
chumba kimoja na wakasikia watu
wakiongea katika moja wapo ya
chumba.Wakapeana ishara na Daniel
akaufungua mlango wa chumba kile
taratibu na kwa tahadhari lakini ghafla
Silva akageuka na kuanza kuvurumisha
risasi.Silva alikuwa anamsaidia Agatha
kupenya katika dirisha.Job akampa
ishara Daniel aupige teke mlango na
kisha kwa kasi ya aina yake
akavurumisha risasi zilizompata Silva
akaanguka chini.Akaachia tena risasi
mbili na kwa mtu yule aliyekuwa
akimalizia kupenya dirisahni na moja
ikampata Agatha katika mguu wa
kushoto wakati akimalizia kutoka
katika dirisha akaanguka chini.Job
akamtuma Daniel atoke nje amfuate
Yule mwanamke aliyeruka nje.Job
akamfuata Irene katika kile chumba
akamfungua kamba alizokuwa
amefungwa.
“Thank you Job.Wazazi wangu
wako wapi? Akauliza Irene baada ya
kufunguliwa
“Wazazi wako salama tayari
tumekwisha wakomboa.Let’s………….”
Job akastuka na kunyamaza baada ya
kusikia sauti ya Daniel akizungumza na
mtu
“Don’t shoot me !! ikasema sauti
ya mwanamke
“Who are you? Akauliza Daniel
“I’m Agatha mkasa the first lady!!
“First lady ?? What are you doing
here? akauliza Daniel
“Tafadhali nisaidie kijana.What’s
your name?
“Daniel..Daniel swai”
“ Daniel swai.Please help me.Let
me out of here” akasema Agatha.
Baada ya muda Daniel akasikika
akimwambia Agatha
“ Go !! go !!
“Wamekuumiza? Job akamuuliza
Irene
“Wamenipiga piga na kuniumiza
mdomoni” akasema Irene
“Wazazi wangu wako wapi?
Akauliza Irene
“wako nje.Tuondoke mahala
hapa” akasema Job akamshika mkono
Irene akamuongoza kutoka nje ambako
walikutana na Daniel
“Yule mtu aliyeruka dirishani
sijafanikiwa kuonana naye
katoroka.Tusipoteze wakati twendeni
tuondoke .Kuna gari liko hapo nje
tunaweza kulitumia kwenda hadi
mahala tulikoliacha gari letu.Ngoja
nikawasachi wale jamaa kule ndani
nione kama nitapata funguo.” Akasema
Daniel.Job akampeleka Irene mahala
walipokuwapo wazazi wake.Irene
akawakumbatia kwa furaha wazazi
wake huku akilia machozi
“Hallo Mukasha” Daniel akasikika
akiongea simuni
“Niko katika operesheni Fulani na
kumetokea mapambano hapa ya
kurushiana risasi na mmoja kati ya
watu ambao nimegundua wamefariki ni
Silvanus Kiwembe” akasema Daniel
baada ya muda akasikika tena
“Nikitoka hapa
nitakujulisha,lazima nionane nawe
leo.Kuna mambo mazito ninataka
kukueleza.” akasema Daniel
“This traitor !! akasema kwa
hasira Job na kuingia ndani akamfuata
Daniel
“Tumemuua Silvanusi Kiwembe
mkuu wa idara ya usalama wa
taifa.Siamini kama naye alikuwemo
katika jambo hili ” akasema Daniel
“He was a traitor to his country jut
like you!! Akasema Job kwa
hasira.Daniel aliyekuwa ameinama
akimkagua Silvanus akainua kichwa na
kujikuta akitazamana na bastora ya Job
“Job !! akasema Daniel
“Shut up you traitor!! Akafoka Job
“Job what’s the meaning of this??
Akauliza Daniel huku akitaka kuinuka
“Daniel tafadhali usijaribu
kuinuka.Weka silaha yako chini na
isukume ije kwangu!! Akasema
Job.Daniel akatii na kuisukuma silaha
yake ikamuendea Job ambaye aliipiga
teke ikaenda mbali
“Sasa nataka uniambie who do you
work for? Akauliza Job
“Mbona sikuelewi Job?
Unamaanisha nini unaponiuliza swali
kama hilo wakati unafahamu kazi
yangu? Akauliza Daniel
“Daniel I swear I’ll kill you.Please
answer my question!!! akasema Job
“Job unataka nikujibu nini? Sina
chochote cha kukujibu.Unafahamu kazi
yangu kwa hiyo hupaswi kuniuliza
swali kama hilo” akasema Daniel huku
midomo ikimtetemeka kwa mbali
kwani sura ya Job haikuonyesha
masihara
“Vua hiyo fulana haraka” akasema
Job na Daniel akavua fulana aliyokuwa
amevaa isiyopenya risasi aliyopewa na
Job.Huku akiwa bado amemuelekezea
bastora,Job akatoa kifaa Fulani toka
katika ile fulana na kumuonyesha
Daniel
“You are so fool Daniel.Fulana hii
niliweka hiki kifaa kidogo cha kunasa
maongezi yako yote na hukuweza
kustuka.Sikuwa nakuamini toka
mwanzo kwani nimewahi kuzisikia sifa
zako wewe ni msaliti
mkubwa.Umewekwa kwa ajili ya
kufanya kazi Fulani fulani za wakubwa
ndiyo maana nikakuwekea kifaa hiki
.Kile kifaa nilichokuwekea sikioni
ulikitupa kwa kuogopa nisiyasikie
maongezi yako lakini hukujua kwamba
ninayasikia kupita kifaa hiki
kilichokuwapo katika hii
fulana.Nilikuuliza kama unamfahamu
Mukasha ukasema humfahamu na
hujawahi kumsikia lakini kumbe una
mawasiliano naye.Kama haitoshi
umeendeleza usaliti wako kwa
kumuachia mke wa rais
aondoke.Nimekusikia ukimruhusu
aondoke na ukanidanganya kwamba
ametoweka.How could you do that
Daniel? kwa nini unakuwa msaliti kwa
nchi yako? Unafahamu kitu
wanachokifanya kwa wananchi hawa
watu unaowafanyia kazi? Answer me
Daniel!! Akasema Job kwa hasira.Daniel
akakosa la kusema
“ hauna jibu Daniel? Akauliza Job
“ Job my friend,give me a chance to
explain this” akasema Daniel
“ Explain what ?!! akauliza Job
Ghafla Daniel akaruka mzima
mzima na kumrukia Job wote
wakaanguka chini.Bastora ya Job
ikamponyoka mkononi na kuanguka
pembeni.Daniel akampiga Job ngumi
mbili kali zilizomfanya aone nyota
nyota.kwa kasi ya aina yake Daniel
akachomoa kisu toka kiunoni akataka
kukizamisha shingoni mwa Job lakini
akamuwahi na kumshika mkono.Job
akauvuta pembeni mkono ule wenye
kisu kwa nguvu na Daniel akakosa
uelekeo na Job akaitumia fursa hiyo
akampiga Job ngumi kali ya uso kwa
mkono wa kushoto akaanguka upande
wa pili.Job akasimama na kumtandika
Daniel teke kali sana maeneo ya ikulu
na kumfanya atoe ukelele wa maumivu
makali.Job akataka kuiokota bastora
yake lakini pamoja na maumivu Daniel
alikiona kitendo kile akaruka mzima
mzima na kumtandika Job teke kali la
uso akaruka na kujigonga ukutani na
Daniel akatambaa ili kuiwahi bastora
“Huyu Daniel yuko vizuri sana
katika karate na nisipofanya juhudi
anaweza kunizidi nguvu” akawaza Job
na kabla Daniel hajaishika bastora Job
akaokota pande la kioo kilichokuwa
kimevunjwa na akina Silva na kwa
nguvu kubwa akakirusha kioo kile
kikatua shingoni kwa Daniel.Akainuka
haraka na kumfuata akakichomoa kioo
kile kilichokuwa kimezama shingoni na
damu nyingi ikatoka na kumrukia.Job
akamgeuza akamtazama Danel
aliyekuwa akitapa tapa na kuchukua
bastora yake yenye kiwambo cha
kuzuia sauti
“Tulidhani ni rafiki na msaada
kwetu kumbe ni msaliti mkubwa”
akasema Job na kumchakaza Daniel
kwa risasi.
“ Hii ni kwa usaliti ulioufanya kwa
taifa lako.I hope you are burning in hell
right now!! Akasema na kumsachi
Daniel akachukua simu yake na
kuondoka akaenda nje kuwafuata akina
Irene ambao walistuka baada ya
kumuona akiwa amechafuka damu
“Twendeni tuondoke mahala
hapa” akasema Job
“Where is Daniel?
“Irene twendeni tuondoke.Forget
about Daniel !! akasema Job na
kumbeba baba yake Irene kisha
akawaongoza akina Irene kuondoka
eneo lile la bustani kuelekekea mahala
waliokuwa wameacha gari lao.Job
alichoka sana kwa uzito aliokuwa nao
yule mzee lakini akajitahidi hadi
wakafika mahali waliokoacha
gari,wakaingia na kuondoka.
“Toka nilipomuona Daniel
nilistuka sana kwani ninamfahamu
vyema si mtu mzuri.Ninazifahamu sifa
zake za usaliti na kuuza
taarifa.Sikupata nafasi ya kumstua
Austin kuhusu Daniel hadi
akamjumuisha katika operesheni
zetu.Mwanaharamu yule naamini huko
aliko atakuwa anaungua hivi sasa kwa
usaliti alioufanya.Kumbe yeye na
Mukasha wanafahamiana.Nilisikia
anamwambia Mukasha kwamba
amepata taarifa ya muhimu anayotaka
kumpatia.Nahisi alitaka kumpatia
taarifa kuhusiana na operesheni
yetu.Mukasha amejificha
wapi?Nitamsaka hadi nihakikishe
ninampata kwani yeye ndiye
atakayetuongoza kuelekea kwa Don
ambaye ndiye anayefahamu mahala
waliko mke na mtoto wangu.Lengo
langu mimi ni kumpata mwanangu
Mileen.Mama yake sina haja naye
kwani aliniacha na kukimbia”akawaza
Job na kumgeukia Irene
“Irene mnaelekea wapi muda huu
niwapeleke? Akauliza Job
“Sifahamu tunaelekea wapi.Kwa
mambo yaliyonitokea sina hamu ya
kwenda tena nyumbani.Nahisi hawa
jamaa wanaweza wakaendela kutufuata
hata nyumbani.I’m confused” akasema
Irene
“ Msijali tutakwenda nyumbani
kwangu.Nina nyumba kubwa yenye
vyuma vya kutoshana ni sehemu
salama.Halafu ninaye daktari pale
atasaidia matibabu kwa mzee wako”
akasema Job
“Ahsante sana Job.Sikutegemea
kabisa kama wazazi wangu
watakombolewa.Watu wale ni wabaya
sana na kama si jitihada zenu wazazi
wangu wangeuliwa” akasema Irene na
kuanza kulia
“Usilie Irene.You have to be strong
for your parents” akasema Job
“Job ninahisi uchungu mkubwa
sana moyoni hasa nilipogundua
kwamba madam Agatha ndiye
aliyenifanyia haya.Mimi ndiye
niliyemuopoa kutoka katika shambulio
lile lakini shukrani yake ni
hii.!!Binadamu sikuhizi hawana
shukrani kabisa.Ukimtendea wema
yeye anakulipa ubaya.Wamewatesa
wazazi wangu na hata kumuua dada wa
kazi.Ninaumia sana Job, sina namna ya
kuelezea uchungu ninaousikia”
akasema Irene
“Usijilaumu Irene.Dunia hii imejaa
wasaliti kila kona.Unamuamini mtu
kwa moyo wako wote lakini baadae
mtu huyo huyo anakuja kukugeuka na
kukusaliti kama ulivyomuamini Agatha
ukamuokoa kutoka katika lile
shambulio lakini badala ya
kukushukuru tazama kitu
alichokufanyia.Huu ni unyama
mkubwa.Hapa tunajifunza somo kubwa
kwamba usimuamini mtu
kupindukia.Yule yule unayemuamini
leo ndiye atakayekuangamiza
kesho.Usimuamini mtu yeyote katika
dunia hii ya sasa.Trust only God “
akasema Job
“Usemayo ni sawa Job.Mungu
pekee ndiye wa kumuamini.” Akasema
Irene na kugeuka akawatazama wazazi
wake halafu akamtazama Job.
“Agatha alifanikiwa kutoroka?
Akauliza.Job hakumjibu kitu
“ Job Agatha aliwezaje kutoroka?
Akauliza tena
“Agatha hakutoroka bali
alitoroshwa? Daniel let her go”
akasema Job huku akisikitika
“He let her go !! Irene naye
akashangaa
“Yes he let her go!!
“Why?? Yule mwanamke ni hatari
sana hakutakiwa kuachiwa hata kama
ni mke wa rais lakini hayuko juu ya
sheria na alitakiwa apatikane ajibu
kosa la utekaji na mauaji.Wamewateka
wazazi wangu wakawatesa na kama
haitoshi wakamuua dada wa kazi.Yote
haya yamefanyika kwa amri yake.Kwa
nini Daniel akamuachia aende?
Tutampata wapi tena? Akauliza Irene
na kuinama akashika ikchwa
“Irene I’m sorry to say this but
Daniel wasn’t on our side.”
“Kivipi Job? Irene akauliza
“ He wa a traitor!! Akasema Job na
kuuma meno kwa hasira
“Traitor?!! Irene akauliza
“Ndiyo.Alijifanya yuko upande
wetu kumbe ana malengo yake”
akasema Job
“Hebu nieleweshe Job
nikuelewe.Daniel aliniokoa toka kwa
watu waliokuwa wananisaka na
akanifahamisha kwamba yeye ni
mpelelezi kazi anayofanya kwa siri na
kumbe hata ninyi nyote
mnafahamu.Amepambana nawe bega
kwa bega mpaka wazazi wangu
wakafanikiwa kuokolewa.Iweje ageuke
msaliti? Amefanya jambo gani? Kwa
nini amebaki? Akauliza Irene
“Tutaongea tukifika nyumbani.Ni
suala ambalo natakiwa nikueleze kwa
utulivu kidogo” akasema Job
“Job napenda nichukue nafasi hii
kukushukuru kwa kazi kubwa
uliyoifanya wewe na Daniel ya
kuwakomboa wazazi wangu.Bila ninyi
mimi na wazazi wangu wote
tungepoteza maisha.Watu wale
walikuwa na malengo mabaya sana
kwetu.Nitaendelea kuwashukuru
katika siku zote za uhai wangu.
Mmeyatoa maisha yenu kwa ajili ya
familia yangu.Sina kitu cha kuwalipa ila
nitwaombea kwa Mungu azidi kuwapa
uhai mrefu na muendelee kuwasaidia
watu wengi zaidi” akasema Irene na Job
hakujibu kitu.
Walifika nyumbani kwa
Job.Marcelo akastuka sana kwa namna
Job alivyochafuka damu.Wakasaidiana
kumshusha mzee Maboko baba yake
Irene wakamuingiza ndani na Job
akamueleza Marcelo aanze
kumshughulikia mara moja kwani hali
yake haikuwa nzuri.Job akamuita Irene
wakaenda juu kabisa ghorofani.
“Job ahsante sana kwa msaada
wako mkubwa.Sipati picha bila wewe
sijui nini kingetokea leo.Bila shaka hivi
sasa tayari mimi na wazazi wangu
tungekuwa ni marehemu kwani
nilikwisha ziona kila dalili za
kutokutoka hai katika lile
jengo.Sinoacha kukushukuru kwa hilo”
akasema
“Irene operesheni ile ilifanikiwa
kutokana na ujasiri wako na kufuata
maelekezo uliyopewa.Endapo
ungekwenda kinyume na maelekezo au
ungeonyesha uoga basi tungepata
wakati mgumu sana hivyo shukrani
nyingi zikuendee wewe kwani kwa
asilimia kubwa umeifanya operesheni
ile iwe rahisi tofauti na tulivyokuwa
tumefikiria.Una ujasiri mkubwa
sana.Ungefaa sana kama ungekuwa
mpelelezi” akasema Job na kwa mara ya
kwanza akaliona tabasamu katika sura
ya Irene
“Nimeona namna mnavyofanya
kazi zenu,hapana nisingeweza kuwa
mpelelezi.Ni kazi ngumu sana.By the
way nieleze kuhusu Daniel amefanya
nini? Akauliza Irene
“Adrian hakuwa mwenzetu.”
Akasema Job
“Ninamfahamu vyema kwa muda
mrefu niliwahi kusikia sifa zake
kwamba ni mtu mwenye tamaa ya pesa
na amekuwa na tabia ya kuuza
taarifa.Ni wakala wa mashirika kadhaa
ya ujasusi ambayo humlipa pesa nyingi
ambazo huzitumia kwa starehe.Ni mtu
anayefahamika sana hapa mjini kwa
starehe na kubadili
wanawake.Nilipomuona leo pale
nyumbani kwa Monica nilistuka sana
lakini sikupata nafasi ya kumfahamisha
Austin kuhusu Daniel.Tukiwa njiani
tukielekea kule walikokuwa wazazi
wako nilimuuliza kama anamfahamu
Wislon Mukasha akasema hamfahamu
na hajawahi kumsikia hata mara
moja.Tukiwa katika pori lile
linalozunguka ile bustani ya wanyama
aliniomba apige simu .Kwa kuwa
nilikuwa ninamfahamu vizuri sikuwa
nimemuamini moja kwa moja kwa hiyo
niliweka kifaa fulani cha kunasa
maongezi yake yote.Nilisikia maongezi
yake na Mukasha simuni nikastuka
sana” akasema Job na kumstua Irene
“Daniel anafahamina na
Mukasha??
‘”Ndiyo wanafahamiana na
alimueleza kwamba ana taarifa za
muhimu sana amezipata.Nahisi taarifa
aliyotaka kumuuzia Mukasha ni
kuhusiana na taarifa ile uliyomrekodi
rais na Jenerali Lameck kwani
alimtaarifu kwamba amepata taarifa
nzito sana na akamtaka aandae pesa za
kutosha.Hii ni tabia ya Daniel kuuza
taarifa nyeti na ndiyo maana amekuwa
akitumiwa na wakuu mbalimbali
kutafuta taarifa muhimu” akasema Job
“Dah ! sikulijua hilo.Nilimuamini
sana Daniel na hata niliwahi kuwa naye
katika mahusiano na baadae
tukatengana” akasema Irene.Job
akaendelea
“Baadae nilimsikia akizungumza
tena na Mukasha akamtaarifu kwamba
Silvanus Kiwembe amefariki dunia”
“Namfahamu Silva.Nilistuka sana
nilipomuona akiwa na Agatha pale
ndani” akasema Irene
“Silva ni mshirika mkubwa wa
Agatha kwani wote ni wafuasi wa
Alberto’s.Daniel naye alikuwa mshirika
wa Mukasha” akasema Job
“Daniel amekimbilia wapi?
Akauliza Irene
“Daniel hajakimbia.He’s dead”
akasema Job na Irene akashindwa
kujizuia kulia
“I think you need to be alone”
akasema Job
“Hapana Job.Please I need
someone with me right now.Please stay
with me” akasema Irene
“Irene I still have an important job
to do tonight ” akasema Job
“ Kazi nyingine? Irene akauliza
“ Ndiyo nina kazi ya muhimu sana
ambayo natakiwa kuikamilisha usiku
huu kabla ya jua kuchomoza
kesho.Usihofu hapa kwangu ni sehemu
salama kabisa na baba yako yuko
katika mikono salama ya Marcelo
ambaye ni daktari mzuri” Akasema Job
“ Job nina jambo nataka kuuliza.”
Akasema Irene
“Flora yule mtumishi wetu
aliuawa na watu hawa waliowateka
nyara wazazi wangu na hivi sasa
naamini kwamba tutakuwa
tunatafutwa sana na ndugu na nina
imani hata taarifa zetu tayari zitakuwa
zimefika polisi,nini itakuwa hatima
yetu? Lini tutatoka hapa katika nyumba
yako? Nini kitafuata baadaya hapa?
Tutaeleza nini endapo tutahojiwa na
polisi kuhusu kifo cha Flora? Je
tukihojiwa niweke wazi kwamba ni
mke wa rais ndiye aliyekuwa nyuma ya
tukio lile la utekaji? Na je nikisema
hivyo tutaelewekaje bila ya kuwa na
ushahidi wa kutosha ? Job I’m
confusewd I don’t know what to do”
akasema Irene.
“Irene kuwakomboa wazazi wako
si mwisho wa hatari kwa familia
yako.Bado mko katika hatari tena kwa
sasa hatari imeongezeka zaidi baada ya
Agatha kukimbia.Hatujui nini
atakifanya na ninaamini huko aliko
atakuwa anapanga kufanya jambo
lolote ili kukufumba mdomo .Vile vile
endapo rais atagundua kwamba wewe
ndiye uliyempa Agatha taarifa zile za
shambulio atakusaka kwa udi na
uvumba.Kwa hiyo mtaendelea kuishi
hapa wewe na baba yako wakati
tukiendelea kulishughulikia suala
lenu.Kuna mambo mazito
tunayoendelea kuyashughulikia kwa
sasa yanayohsu usalama wa nchi na
yanamuhusu hata rais kwa hiyo
tutakapomaliza masuala hayo
tutalishughulikia suala lako pia”
“Vipi kjuhgusu baba yangu? Hali
yake inazidi kuwa mbaya kwani
anatakiwa apelekwe nje ya nchi kwa
matibabu”
“Kuhusu mzee wako tutaangalia
namna ya kufanya ili aweze kupata
nafuu kwa wakati huu hadi hapo hali ya
mambo yatakapokuwa yametulia ndipo
tutakusaidia ipi mzee wako aelekee nje
ya nchi kwa matibabu” akasema
Job.Irene akashika kichwa alionekana
kuchanganyikiwa.
“Mambo yote haya niliyasababisha
mimi.Kama nisingedukua simu ya rais
na kusikia maongezi yale ya rais na
Lameck nisingekuwa katika hatari
kubwa hivi sasa.Nisingeiweka familia
yangu katika hatari.Najuta kwa hii
nililolifanya na endapo ikitokea baba
akapoteza maisha hii itakuwa
imetokana na uzembe wangu and I’ll
never forgive myself for that” akasema
Irene
“Irene tafadhali usijilaumu kwa
hili ulilolifanya.Japo ni jambo a hatari
lakini la muhimu mno kwa taifa na
historia itakukumbuka kwamba
uliweza kudukua simu ya rais na
kufanikiwa kugundua jambo kubwa na
la muhimu sana.Mpaka hivi sasa tuna
hakika kwamba rais na Lameck kuna
jambo wanalifahamu kuhusiana na
mashambulio yale lakini tumeligundua
hilo kutokana na ile rekodi.Kwa hiyo
usijilaumu sana kwa jambo
ulilolifanya.Nakuhaikishia kwamba
mtaishi hapa wakati tukiendelea
kutafuta namna ya kumsaidia mzee
wako aweze kupelewka nje ya nchi kwa
matibabu na ninakuahdi kwamba
hatutashindwa kwa hilo naomba
uniamini.Kuhusu kutafutwa na polisi
mambo hayo yasikupe shida na wala
usiyawaze kabisa ni mambo madogo tu”
akasema Job wakatoka kule juu
ghorofani wakaenda kumtazama baba
yake Irene aliyekuwa anapatiwa
matibabu na Marcelo
“Anaendeleaje mgonjwa? Job
akauliza
“Anaendelea vyema” akasema
Marcelo kisha wakatoka nje kwa ajili ya
maongezi
“Marcelo,Irene na familia yake
wataishi hapa kwa muda hadi hapo
mambo yao yatakapotulia.Ni watu wetu
kwa hiyo lazima tuwahudumie kwa kila
kitu.Baba yake ni mgonjwa na
anatakiwa apelekwe nje ya nchi kwa
matibabu ila kwa sasa kwa kuwa bado
hali ya mambo haijakaa sawa italazimu
kusubiri lakni kwa wakati huo
nakuomba ufanye kila linalowezekana
ili kuhakikisha mzee Maboko anakuwa
salama” akasema Job
“Sawa Job nimekuelewa.Nini
kimetokea huko mlikokwenda? Yule
jamaa Daniel yuko wapi? Akauliza
Marcelo
“He was a traitor.I killed him”
akasema Job na kumstua Marcelo
“You killed him?
“Yes I killed him.Tutazungumza
baadae lakini kwa sasa nataka nitoke
kuna kazi nakwenda kuifanya ya
muhimu” akasema Job na marcelo
akamtazama kwa wasi wasi
“ Unakwena kuifanya mwenywe?
“ Ndiyo ninakwenda kuifanya
mwenyewe.Dont you trust me?
“Si hivyo Job ila nimeingiwa na
hofu kidogo kwani wakati ule
uliondoka mwenyewe na yakakukuta
matatizo na leo tena unataka kwenda
mwenyewe.Kwa hizi kazi zenu hupaswi
kwenda mahala peke yako.Unatakiwa
uwe na mtu wa kukusaidia” akasema
Marcelo
“Usihofu Marcelo I’ll be fine”
akasema Job
“Endapo sintarejea hadi asubuhi
utawaeleza akina Austin hali halisi
endapo watapiga simu” Akasema Job na
kuelekekea chumbani kwake akakaa
kitandani akaitazama simu ile ya Daniel
kisha akazitafuta namba za Mukasha na
kuandika ujumbe mfupi wa maandishi
“Tayari nimemaliza operesheni
yangu.Nielekeze mahala ulipo ili nije
hapo sasa hivi”
Baada ya sekunde kadhaa
ukaingiaujumbe wa simu Job
akaufungua na kuusoma ulitoka kwa
Mukasha.Alimuelekeza mahala ambako
anataka wakutane.Job akabadili nguo
akachukua baadhi ya silaha zake
akaondoka
 
Back
Top Bottom