QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Acha upaka pori wewe....Lege angeibania kuileta uku ungeijua wapi? watu wengine hamnazo aise

Sent using Jamii Forums mobile app
Si Ndo maana kaileta ili na sisi badaye tujiongeze kwa kutopenda vya bure muda wote unaonjeshwa na ikifika mahali na wewe unajiongeza sio lazima huyo lege akwambie ununue vitu vingine vya kujiongeza ili na mtunzi na yeye apate ela ya kununua maji ya kunywa sio unajikunja mgongo muda wote na kwa season zote hizo afu watu hawajiongezi hata kama ni wewe huwezi fanya hivyo kwa lege anayo tayari season 8 ila anasubiri kwanza na nyie mjiongeze kidogo bhana sio vya bure muda wote kuwa na uelewa wa mbali wa kuchanganua mambo kwa jicho la tatu.
 
Ulichokifanya siyo fair kabisa, ifute hiyo thread ya hilo file....Kama kutuma ungetuma pm kwa kila muhusika.
Mkuu shusha story kama vipi!

sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
 
Nmeisoma,

Ni vyema watu wakaheshim taaluma za watu, patrick ni miongoni mwa watu wachache walio na kipaji cha pekee cha kuandika story,

Japo bado hawezi kufika kwa akina willy, ila tunaanza kupata mbadala wake taratibu....

Ikiwa ataendelea hivi na sifa zisimlevye kama wengine atakuja kuwa na mafanikio makubwa sana,

Ni vyema akaziondika story zake ktk vitabu ili kutunza kumbukumbu kwa kizazi kijacho,

Ikiwa ataruhisi, tunaweza kufanya hariri, uhakiki na tathimini, ili tuiweke story katika maudhui halisi,

Huenda tukapata vitu vzr vya kujifunza kama taifa, maana humo ndani yapo mambo mengi sana....

Kikubwa ni pongezi kwa patrick,

Wengi namna ya kuhitimisha story huwa inawashinda, na mtunzi mzr ni namna ambavyo anaimalizia story, (kwa mtazamo wangu) najua wengine hamjaisoma ufanisi uongezwe umaliziaje bado si mzr sana...

Tutahakiki wote tukimaliza

................................................

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nmeisoma,

Ni vyema watu wakaheshim taaluma za watu, patrick ni miongoni mwa watu wachache walio na kipaji cha pekee cha kuandika story,

Japo bado hawezi kufika kwa akina willy, ila tunaanza kupata mbadala wake taratibu....

Ikiwa ataendelea hivi na sifa zisimlevye kama wengine atakuja kuwa na mafanikio makubwa sana,

Ni vyema akaziondika story zake ktk vitabu ili kutunza kumbukumbu kwa kizazi kijacho,

Ikiwa ataruhisi, tunaweza kufanya hariri, uhakiki na tathimini, ili tuiweke story katika maudhui halisi,

Huenda tukapata vitu vzr vya kujifunza kama taifa, maana humo ndani yapo mambo mengi sana....

Kikubwa ni pongezi kwa patrick,

Wengi namna ya kuhitimisha story huwa inawashinda, na mtunzi mzr ni namna ambavyo anaimalizia story, (kwa mtazamo wangu) najua wengine hamjaisoma ufanisi uongezwe umaliziaje bado si mzr sana...

Tutahakiki wote tukimaliza

................................................

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unachangiaje kitu ambacho hakipo hapa.Sasa unategemea sisi ambao hatujasoma tuchangie nini?Wewe ni sawasawa na mtu anayesikiliza mziki kwenye headset halafu unatafuta maoni ya huo wimbo kwa watu wa pembeni!
 
ENDELEA………………………….
Job na Daniel Swai walihakikisha
dege lililowabeba akina Austin limepaa
na kuondoka katika uwanja wa
kimataifa wa Julius nyerere bila
matatizo yoyote.
“ Thank you God” Akasema Job na
kumuelekeza Julieth aendeshe moja
kati ya magari mawili waliyotumia
kuendea pale uwanjani.Akampigia simu
Marcelo na kumfahamisha kwamba
zoezi limekamilika hivyo wanarejea
nyumbani.Job na Daniel wakaingia
katika gari lingine na kuondoka pale
uwanjani.
“Job mpaka sasa bado siamini
kama kweli ni wewe.Pole sana kwa yale
matatizo makubwa
yaliyokupata.Binafsi nilistuka sana
nilipopata taarifa za matatizo yale
.Dunia hii imejaa watu wasio na
huruma hata kidogo” akasema Daniel
lakini Job hakuongea chochote
“vipi hali yako kwa sasa? I hope
everything is ok” akasema Daniel
“ I’m ok.” Job akajibu kwa ufupi
“Job nilisikia kuwa shemeji
alitoweka baada ya wewe kupata
matatizo.Taarifa hizi ni za kweli?
Akauliza Daniel
“Daniel can we stop talking about
me for now and concentrate on our
mission? Akasema Job ambaye
hakuonekana kupendezwa na maswali
ya Daniel
“ I’m sorry Job.Nilihitaji tu
kufahamu kuhusu maendeleo
yako.Kilichokupata kilitushangaza
wengi na ndiyo maana nilipatwa na
mstuko mkubwa baada ya kukuona leo
ukiwa mzima wa afya na unaendelea
vyema na kazi zako.Tuachane na hayo
na tujielekeze katika kazi iliyoko mbele
yetu.Nahitaji kwanza kufahamu jambo
mnaloshughulika nalo kwani Austin
aliniambia kuna jambo mnashughulikia
ambalo ni zito linalohusiana na
rais.Naweza kulifahamu ni jambo gani?
Akauliza Daniel
“Not now Daniel.Tutazungumza
baadae kwa sasa tunakwenda
kumuondoa Yule dada pale kwa Monica
na kumpeleka sehemu salama”
“ Wapi unataka tumpeleke Irene?
Daniel akauliza
“Katika makazi yangu.Pale kwa
Monica hayuko salama hata kidogo”
akajibu Job
“Job,mimi ndiye niliyempeleka
Irene pale nyumbani kwa Monica
nikiamini kabisa kwamba ni sehemu
salama sana kwa Irene kuwepo pale
kwa wakati huu” akasema Daniel
‘No ! She’s not safe there.Hakuna
ulinzi wowote wa maana pale isitoshe
tayari watu wa usalama wa taifa
wamekwisha hisi kuna kitu pale kwa
Monica kwa hiyo si sehemu salama kwa
Irene kuwepo pale” akasema Job
“ Nina wasiwasi kama Job
amepona sawa sawa ugonjwa wake wa
akili uliokuwa unamsumbua.Sina
hakika kama tutaweza kufanya kazi
pamoja lakini ngoja niendelee
kumsoma vizuri kwani ni mtu ambaye
sijawahi kufanya naye kazi yoyote zaidi
ya kufahamiana tu.Hili la kumtoa Irene
nyumbani kwa Monica na kumpeleka
katika makazi yake siliafiki sana ila
ngoja nikubaliane naye lakini endapo
nitaona usalama wa Irene uko shakani
basi itanilazimu kufanya maamuzi
magumu kwani mimi ndiye
niliyechukua dhamana ya usalama
wake” Akawaza Daniel
“Bado mpaka sasa nina mshangao
kuhusu Austin.Wote tuliamini alifariki
dunia lakini kumbe yuko hai.Ni jambo
gani linalomuhusu rais
wanalishughulikia? Wale watu
walioongozana nao kwenda Kinshasa ni
akina nani? Mbona wanaonekana
kuwalinda sana? Ngoja nivute subira na
Job akitulia atanieleza kila kitu”
akaendelea kuwaza Daniel huku safari
ikiendelea bila maongezi mengi hadi
walipowasili nyumbani kwa Monica
wakafunguliwa geti na kuingia
ndani.Julieth aliyekuwa nyuma yao
naye akawasili.Walikaribishwa
sebuleni .Irene ambaye alikuwa
chumbani anapumzika akaitwa akaja
mara moja.Macho yake yalikuwa
mekundu kwa kulia
“Unajisikiaje Irene? Daniel
akauliza
“ Bado sijielewi Daniel.Nahisi
nitakuwa mwendawazimu.Nimewaza
hadi akili yangu imefika kiwango chake
cha mwisho cha kufikiri” akasema
Irene
“ Usihofu Irene suala hili
tutalimaliza.Baada ya kujadiliana na
wenzangu tumeona tukuhamishe hapa
na tukupeleke sehemu salama zaidi
.Mimi na huyu mwenzangu anaitwa Job
tutafanya kila linalowezekana
kuhakikisha tunawapata wazazi wako”
akasema Daniel na bila kupoteza muda
wakamchukua Irene,wakaingia garini
na Julieth akakalia usukani
wakaondoka.Job alipanda piki piki
yake aliyokuwa ameicha pale nyumbani
kwa Monica .Tayari giza lilikwisha anza
kuchukua nafasi yake
“ Daniel giza linaingia na
sijawapigia wale jamaa simu kama
walivyotaka.Nina wasi wasi sana
wanaweza wakawadhuru wazazi
wangu.I wont forgive myself if anything
happens to them!! Akasema Irene na
machozi yakaanza kumtoka
“Irene naomba uniamini
.Nimekuahidi kwamba,mimi na
wenzangu tutafanya kila tuwezalo
kuhakikisha tunawakomboa wazazi
wako na pili kuwafahamu watu hao
wanaokutafuta ni akina nani.Hatutalala
usingizi hadi suala hili likamilike”
Akasema Daniel
“Vipi kuhusu rais na mkuu wa
majeshi? Hawa mtawafanya nini? Nina
uhakika mkubwa wameshiriki au kuna
kitu wanakifahamu kuhusiana na
mashambulio yale” akasema Irene
“Ni mapema mno kusema
chochote kuhusiana na rais na mkuu
wa majeshi kuhusika katika matukio
yale ila nakuahidi mimi na wenzangu
tutafanya uchunguzi na endapo
tutagundua walihusika kwa namna
yoyote ile basi hawatabaki salama”
akasema Daniel na jibu lile
halikuonekana kumridhisha Irene
“Daniel umeisikia ile rekodi na
wanasikika wazi mkuu wa mejshi na
rais wakijasiliana kuhusiana na
shambulio la hoteli.Hawa wana kitu cha
kujibu.kwa nini msiitumie rekodi ile
kama ushahidi wa kuwatia hatiani
hawa watu kwa kuhusika katika njama
ovu na kusababisha vifo vingi? Akauliza
Irene
“Ushahidi wa ile rekodi ni muhimu
sana lakini bado hautoshi.Tunatakiwa
kuchimba zaidi na kupata ushahidi wa
kutosha.Ukumbuke hapa
tunamuongelea mkuu wa nchi kwa hiyo
ushahidi mkubwa unatakiwa.Hili si
suala jepesi kama unavyodhani
Irene.Kupata ushahidi dhidi ya rais ni
jambo gumu mno lakini tutajitahidi
kufanya kadiri tutakavyoweza
kuhakikisha tunachunguza na kuupata
ukweli wa jambo hili” akasema Daniel
na safari ikaendelea
****************
 
Mkuu unachangiaje kitu ambacho hakipo hapa.Sasa unategemea sisi ambao hatujasoma tuchangie nini?Wewe ni sawasawa na mtu anayesikiliza mziki kwenye headset halafu unatafuta maoni ya huo wimbo kwa watu wa pembeni!
Mkuu mwisho nimeeleza vzr, kama ulisoma mpka mwisho..
 
QUEEN MONICA: FINAL SEASON
SEHEMU YA 1
Job na Daniel Swai walihakikisha
dege lililowabeba akina Austin limepaa
na kuondoka katika uwanja wa
kimataifa wa Julius nyerere bila
matatizo yoyote.
“ Thank you God” Akasema Job na
kumuelekeza Julieth aendeshe moja
kati ya magari mawili waliyotumia
kuendea pale uwanjani.Akampigia simu
Marcelo na kumfahamisha kwamba
zoezi limekamilika hivyo wanarejea
nyumbani.Job na Daniel wakaingia
katika gari lingine na kuondoka pale
uwanjani.
“Job mpaka sasa bado siamini
kama kweli ni wewe.Pole sana kwa yale
matatizo makubwa
yaliyokupata.Binafsi nilistuka sana
nilipopata taarifa za matatizo yale
.Dunia hii imejaa watu wasio na
huruma hata kidogo” akasema Daniel
lakini Job hakuongea chochote
“vipi hali yako kwa sasa? I hope
everything is ok” akasema Daniel
“ I’m ok.” Job akajibu kwa ufupi
“Job nilisikia kuwa shemeji
alitoweka baada ya wewe kupata
matatizo.Taarifa hizi ni za kweli?
Akauliza Daniel
“Daniel can we stop talking about
me for now and concentrate on our
mission? Akasema Job ambaye
hakuonekana kupendezwa na maswali
ya Daniel
“ I’m sorry Job.Nilihitaji tu
kufahamu kuhusu maendeleo
yako.Kilichokupata kilitushangaza
wengi na ndiyo maana nilipatwa na
mstuko mkubwa baada ya kukuona leo
ukiwa mzima wa afya na unaendelea
vyema na kazi zako.Tuachane na hayo
na tujielekeze katika kazi iliyoko mbele
yetu.Nahitaji kwanza kufahamu jambo
mnaloshughulika nalo kwani Austin
aliniambia kuna jambo mnashughulikia
ambalo ni zito linalohusiana na
rais.Naweza kulifahamu ni jambo gani?
Akauliza Daniel
“Not now Daniel.Tutazungumza
baadae kwa sasa tunakwenda
kumuondoa Yule dada pale kwa Monica
na kumpeleka sehemu salama”
“ Wapi unataka tumpeleke Irene?
Daniel akauliza
“Katika makazi yangu.Pale kwa
Monica hayuko salama hata kidogo”
akajibu Job
“Job,mimi ndiye niliyempeleka
Irene pale nyumbani kwa Monica
nikiamini kabisa kwamba ni sehemu
salama sana kwa Irene kuwepo pale
kwa wakati huu” akasema Daniel
‘No ! She’s not safe there.Hakuna
ulinzi wowote wa maana pale isitoshe
tayari watu wa usalama wa taifa
wamekwisha hisi kuna kitu pale kwa
Monica kwa hiyo si sehemu salama kwa
Irene kuwepo pale” akasema Job
“ Nina wasiwasi kama Job
amepona sawa sawa ugonjwa wake wa
akili uliokuwa unamsumbua.Sina
hakika kama tutaweza kufanya kazi
pamoja lakini ngoja niendelee
kumsoma vizuri kwani ni mtu ambaye
sijawahi kufanya naye kazi yoyote zaidi
ya kufahamiana tu.Hili la kumtoa Irene
nyumbani kwa Monica na kumpeleka
katika makazi yake siliafiki sana ila
ngoja nikubaliane naye lakini endapo
nitaona usalama wa Irene uko shakani
basi itanilazimu kufanya maamuzi
magumu kwani mimi ndiye
niliyechukua dhamana ya usalama
wake” Akawaza Daniel
“Bado mpaka sasa nina mshangao
kuhusu Austin.Wote tuliamini alifariki
dunia lakini kumbe yuko hai.Ni jambo
gani linalomuhusu rais
wanalishughulikia? Wale watu
walioongozana nao kwenda Kinshasa ni
akina nani? Mbona wanaonekana
kuwalinda sana? Ngoja nivute subira na
Job akitulia atanieleza kila kitu”
akaendelea kuwaza Daniel huku safari
ikiendelea bila maongezi mengi hadi
walipowasili nyumbani kwa Monica
wakafunguliwa geti na kuingia
ndani.Julieth aliyekuwa nyuma yao
naye akawasili.Walikaribishwa
sebuleni .Irene ambaye alikuwa
chumbani anapumzika akaitwa akaja
mara moja.Macho yake yalikuwa
mekundu kwa kulia
“Unajisikiaje Irene? Daniel
akauliza
“ Bado sijielewi Daniel.Nahisi
nitakuwa mwendawazimu.Nimewaza
hadi akili yangu imefika kiwango chake
cha mwisho cha kufikiri” akasema
Irene
“ Usihofu Irene suala hili
tutalimaliza.Baada ya kujadiliana na
wenzangu tumeona tukuhamishe hapa
na tukupeleke sehemu salama zaidi
.Mimi na huyu mwenzangu anaitwa Job
tutafanya kila linalowezekana
kuhakikisha tunawapata wazazi wako”
akasema Daniel na bila kupoteza muda
wakamchukua Irene,wakaingia garini
na Julieth akakalia usukani
wakaondoka.Job alipanda piki piki
yake aliyokuwa ameicha pale nyumbani
kwa Monica .Tayari giza lilikwisha anza
kuchukua nafasi yake
“ Daniel giza linaingia na
sijawapigia wale jamaa simu kama
walivyotaka.Nina wasi wasi sana
wanaweza wakawadhuru wazazi
wangu.I wont forgive myself if anything
happens to them!! Akasema Irene na
machozi yakaanza kumtoka
“Irene naomba uniamini
.Nimekuahidi kwamba,mimi na
wenzangu tutafanya kila tuwezalo
kuhakikisha tunawakomboa wazazi
wako na pili kuwafahamu watu hao
wanaokutafuta ni akina nani.Hatutalala
usingizi hadi suala hili likamilike”
Akasema Daniel
“Vipi kuhusu rais na mkuu wa
majeshi? Hawa mtawafanya nini? Nina
uhakika mkubwa wameshiriki au kuna
kitu wanakifahamu kuhusiana na
mashambulio yale” akasema Irene
“Ni mapema mno kusema
chochote kuhusiana na rais na mkuu
wa majeshi kuhusika katika matukio
yale ila nakuahidi mimi na wenzangu
tutafanya uchunguzi na endapo
tutagundua walihusika kwa namna
yoyote ile basi hawatabaki salama”
akasema Daniel na jibu lile
halikuonekana kumridhisha Irene
“Daniel umeisikia ile rekodi na
wanasikika wazi mkuu wa mejshi na
rais wakijasiliana kuhusiana na
shambulio la hoteli.Hawa wana kitu cha
kujibu.kwa nini msiitumie rekodi ile
kama ushahidi wa kuwatia hatiani
hawa watu kwa kuhusika katika njama
ovu na kusababisha vifo vingi? Akauliza
Irene
“Ushahidi wa ile rekodi ni muhimu
sana lakini bado hautoshi.Tunatakiwa
kuchimba zaidi na kupata ushahidi wa
kutosha.Ukumbuke hapa
tunamuongelea mkuu wa nchi kwa hiyo
ushahidi mkubwa unatakiwa.Hili si
suala jepesi kama unavyodhani
Irene.Kupata ushahidi dhidi ya rais ni
jambo gumu mno lakini tutajitahidi
kufanya kadiri tutakavyoweza
kuhakikisha tunachunguza na kuupata
ukweli wa jambo hili” akasema Daniel
na safari ikaendelea
 
QUEEN MONICA: FINAL SEASON
SEHEMU YA 2

Ndege aina ya Boening 747 -200
inayomilikiwa na rais wa jamhuri ya
kidemokrasia ya watu wa Congo,David
Zumo iliendelea kuchana anga
kuelekea jijini Kinshasa.Ndege hii ni
moja kati ya ndege za aina yake
iliyotengenezwa kwa gharama ya dola
bilioni mbili za marekani.Ni ndege ya
kwanza ya aina hii kumilikiwa na mtu
binafsi.Ndege yenye muundo sawa na
hii inamilikiwa na serikali ya Marekani
na hutumiwa na rais wa marekani
katika ziara zake za nje ya nchi.
Uwapo ndani ya dege hili kubwa la
kifahari mno utahisi upo ndani ya
jumba kubwa la kifahari na hii ndiyo
sababu ilipewa jina la kasri lipaalo
.Ndani ya dege hili uso wa mzee
Benedict mwamsole haukupungukiwa
tabasamu.Alikuwa na furaha
iliyopitiliza kwa kufanikiwa kupanda
dege lile kubwa na la aina yake.
“Maisha yana maajabu sana
.Sikuwahi hata kuota kama siku moja
nitabahatika kupanda ndege hii ya
maajabu.Hii ni historia nimeweka
katika maisha yangu kwani si mara
moja tulikuwa na wenzangu tunajadili
kuhusu dege hili katika vikao vyetu vya
kahawa lakini leo hii nimefanikiwa
kulipanda na kuushuhudia ule uzuri
wake tuliokuwa tunausoma katika
magazeti na taarifa mbali mbali.Uzuri
uliomo humu ni zaidi ya vile
tunavyofahamu kwa kusoma ama
kusikia kutoka kwa vyombo vya
habari.Monica amepata bahati kubwa
sana ya kupendwa na mtu kama David
Zumo.Kwa vyovyote vile itakavyokuwa
lazima nihakikishe ndoa kati yake na
David inafanikiwa tena haraka zaidi”
Akawaza mzee Benedict huku
akiburudika kwa mvinyo safi wakiwa
ndani ya sebule maalum ya rais .Macho
yake hayakutulia sehemu moja na mara
akawaona Austin na Amarachi
wakibadilishana mawazo.
“Pamoja na furaha niliyonayo kwa
kupanda ndege hii kubwa
duniani,lakini kuna kitu kimenikwaza”
Akawaza mzee Ben
“Ni huyu kijana Austin.Ni nani
huyu? Ana uhusiano gani na
Monica?Nimemfahamu leo asubuhi
alipokuja kuzungumza na Monica pale
nyumbani kwangu na mchana amekuja
kutuchukua tukaenda nyumbani kwa
Monica kwa ajili ya safari hii ya
Kinshasa.Nimewaona wakiwa na silaha
yeye na wenzake.Najiuliza ni akina nani
hawa? Wametumwa kumlinda Monica?
Halafu kuna wale watu wengine watatu
siwaelewi ni akina nani? Monica
amewatoa wapi na wanaelekea wapi?
Nikipata nafasi nitazungumza na
Monica na atanipa majibu .Sitaki
matatizo yoyote kwa Monica kwa
wakati huu ambao anatarajia kuolewa
na mtu mkubwa kama David Zumo.Kwa
mambo niliyoyaona toka tumeondoka
nyumbani kwake hadi tunaingia
ndegeni kuna kitu nahisi kinaendelea
hapa kuhusiana na hawa akina Austin
na Monica anakifahamu” akawaza mzee
Ben
Ndani ya ndege Yasmin na Boaz
walipata nafasi ya kuzungumza mambo
yao.Walionekana kuzama sana katika
maongezi mazito.Maria alikuwa
amejilaza sofani.Pamoja na kuzama
katika maongezi mazito lakini wote
walionekana kuwa na nyuso zenye
furaha
“They look happy” Amarachi
aliyekuwa akiwatazama akina Yasmin
akamwambia Austin
“I don’t know if I’m doing the right
thing to let them go” akasema Austin
“Austin kuwaacha waende si
uamuzi mdogo lakini ni kwa ajili ya
kupata kitu kikubwa na muhimu kwa
taifa.Hati ya muungano wetu ni kitu cha
muhimu sana kuliko hata uhuru
wao.Usijilaumu sana kwa kuwaacha
waende.It’s the right thing.Hii hutokea
duniani kote,serikali zote
hubadilishana taarifa toka kwa watu
hatari wanaowashikilia kwa
makubaliano maalum na mara nyingi
huwa ni kuwaachia huru “ akasema
Amarachi
“Nikigundua kama anatudanganya
,nitamteketeza yeye na familia yake”
akasema Austin
“Anasema kweli” Akasema
Amarachi na Austin akafumba macho
akionekana kuhisi maumivu
“Are you ok Austin? Akauliza
Amarachi na kumshika bega
“I’m ok .Nahisi maumivu katika
sehemu za kifua mahala
paliposhonwa.Ni uzembe wangu
nilisahau kunywa dawa za kunisaidia
kutuliza maumivu.” Akasema Austin
akatoa pakiti ya dawa katika mfuko
wake wa koti akachukua dawa mbili na
kumeza.
“Tafadhali usipuuze dawa
Austin.Unatakiwa upone uwe imara
kwani tunakoelekea ni kugumu
zaidi.Mapambano yamebadilika na sasa
tunapambana na mtu tunayemfahamu
na yeye anatufahamu.” Akasema
Amarachi na kukumbuka kitu
“ Austin kuna jambo ambalo
sikushirikishwa.Ni kuhusiana na Yule
jamaa tuliyemkuta nyumbani kwa
Monica”
“ Daniel? Akauliza Austin
“ Yes Daniel.Ni nani Yule.Sielewi
namna alivyojiunga nasi” akasema
Amarachi
“ Ni kweli Amarachi kuna jambio
lilitokea pale nyumbani kwa Monica
ambalo hukuhusishwa.Tutalijadili
tukishuka ndegeni ila kwa ufupi tu ni
kwamba Daniel anafanya kazi katika
idara ya siri ya ujasusi na ni mtu
ambaye tunafahamiana vyema.Sikujua
kama yeye na Monica ni marafiki na
sikutegemea kabisa kumkuta pale”
Akasema Austin na kunyamaza baada
ya mmoja wa wafanyakazi wa ndege ile
kuingia na kwenda kumnong’oneza kitu
pierre Muyeye aliyekuwa anazungumza
na Monica.Pierre Muyeye akainuka na
kumuaga Monica akatoka.Monica
akawafuata wazazi wake
“Are you comfortable? Akauwaliza
“More than comfortable” akasema
mzee Ben huku akicheka
“Sikuwahi kuota kama siku moja
na mimi nitapanda ndege hii ya kifahari
.Ahsante sana Monica kwani wewe
ndiye uliyewezesha tukaandika historia
ya kupanda ndege kama hii.By the way I
want to ask you one question?
“Uliza baba” akasema Monica
“I want to know who is that guy?
Akauliza Ben huku akimuelekezea
kidole Austin
“Austin? Monika akauliza
“Ndiyo Austin.Who is he? Mbona
simuelewi elewi? Kwa mara ya kwanza
nimemuona leo asubuhi alipokuja
nyumbani namuona kama yupo macho
juu juu kama tai.hatulii kila dakika
anageuka huku na kule.Anashughulika
na nini?
“Baba laiti ungejua Yule jamaa
alivyo muhimu kwangu na kwako pia
usingekuwa na wasiwasi naye hata
kidogo.Hata hivyo ni mapema sana
kukueleza yeye ni nani na
anashughulika na nini.Foe now just
enjoy the plane” akasema Monica na
kuwafuata akina Austin
“Monica ahsante sana kwa msaada
wako huu mkubwa uliotusaidia”
akasema Austin
“ Huu si msaada Austin.Huu ni
wajibu wetu.Kama vijana wazalendo
hatuna budi kupambana kufa ama
kupona kuhakikisha tunaikomboa nchi
yetu.Mimi sijawahi kushika silaha
lakini nitashiriki katika mapambano
haya kwa namna nyingine yoyote
nitakayoweza” akasema Monica
“ Unapaswa kupongezwa Monica
kwa maamuzi yako haya uliyoyafanya
na kuamua kujiunga nasi katika jambo
hili hatari lakini lenye manufaa
makubwa kwa taifa. Utapata misuko
suko mingi lakini nakuomba usikate
tama.Nakuhakikishia kwamba mimi na
wenzangu tutakulinda” akasema Austin
na Monica akatabasamu halafu akauliza
“Austin katika kazi zote ambazo
ungeweza kufanya why did you choose
this job? Akauliza Monica.Austin
akatabasamu na kusema
“Nilipenda kazi hii toka nikiwa
mdogo.Nilipenda sana kutazama filamu
za kijasusi na nilimwambia baba
kwamba nataka na mimi siku moja
niwe jasusi.Namshukuru baba ambaye
alielewa ni kitu gani nakihitaji hivyo
akaanza kunijenga kuipenda zaidi kazi
hii kwa kuniletea filamu na hata vitabu
mbali mbali vyote vikiwa na maudhui
ya ujasusi.Kwa ufupi naweza kusema
kwamba sikuichagua kazi hii ila
yenyewe ndiyo iliyonichagua” akasema
Austin
“That’s interesting.Umewahi hata
mara moja kufikiria kuachana na kazi
hii na kufanya kazi nyingine? Amarachi
akauliza
“Ndiyo.Nilipokutana na Maria
nilikuwa tayari kufanya chochote kwa
ajili yake na tayari nilikwisha fanya
maamuzi kwamba sintarejea tena
katika kazi hii kwani nilitaka nianze
maisha mapya.Nilitamani kuwa na
familia lakini hizo zote zilikuwa ni
ndoto za mchana .Kama nilivyosema
kwamba kazi hii ndiyo imenitafuta
mimi kwa hiyo siwezi
kuikimbia.Imenilazimu kukubali
kwamba haya ndiyo maisha yangu na
lazima niendelee kuyaishi.kazi hii iko
damuni na sina hakika kama nitaweza
kuiacha” akasema Austin halafu
akageuza shingo akamtazama Maria
aliyekuwa amejilaza sofani
“I was ready to give her the
world.Nilikuwa tayari kwa kila kitu ili
kumfanya awe na furaha lakini kumbe
yeye hakuwa na mapenzi yoyote na
mimi bali alitaka kunitumia kwa faida
zake.I don’t believe in love
anymore.Love hurts so badly” akasema
Austin huku akimtazama maria kwa
jicho kali
Pierre Muyeye aliingia katika
chumba cha marubani alikoitwa
akapewa taarifa kwamba kuna ndege
nne zimeonekana katika rada
zikiwafuata kwa kasi kubwa na tayari
ziliweka sawa makombora yake kwa
ajili ya kushambulia.Muyeye akastuka
sana
“Ni nani hawa wanaotufuata?
Akaulizia kwa woga.
“Zinaonekana ni ndege za jeshi la
anga la Tanzania” akasema kapteni
Odomba
“Inawezekana labda serikali ya
Tanzania imetuma ndege hizo
kutusindikiza baada ya kuhisi kuna
hatari inakuja .Ninahisi hivyo kwani ni
jana tu Tanzania imeshambuliwa na
magaidi kwa hiyo kuna uwezekano
mkubwa kwamba wanataka kutupa
ulinzi” akasema Muyeye
“Kama ni ulinzi kwa nini
hatukutaarifiwa kama kuna ndege
zitatumwa kutusindikiza? Kibaya zaidi
kinachotupa mashaka ni ndege zote
kuyaweka sawa makombora yake kwa
ajili ya kushambulia” Akasema
Odomba.Muyeye akaonekana
kuchanganyikiwa.
“kwa hiyo tunafanya nini?
Akauliza .
“Tumeona tukutaarifu kwanza
wewe ambaye ndiye kiongozi wa safari
kabla hatujachukua hatua
nyingine.Kitu cha kwanza ni
kuwasiliana na kikosi cha anga cha
jeshi la Tanzania na kuwauliza kama
ndege hizi ni za kwao na kama ni zao
kwa nini zinatufuata? Baada ya kupata
majibu tutawaomba waziondoe ndege
zao na endapo watakaidi basi tutajua
nini cha kufanya” akasema Odomba na
kuitisha kiko cha dharura cha
marubani wote wanaoendesha ndege
ile ambao ni wanajeshi ili kujadiliana
jambo lile la dharura lililojitokeza.
Wakati kikao cha marubani na
wafanyakazi kikiendelea Pierre
Muyeye akatoka haraka na kwenda
katika chumba walimokuwamo akina
Monica akamuita pembeni
“Monica kuna tatizo limejitokeza
ambalo nimeona ni vyema
ukalifahamu” akasema Muyeye
“Tatizo gani? akauliza Monica kwa
wasiwasi
“Kuna ndege nne zimeonekana
katika rada zinatufuata .Zinaonekana ni
za kikosi cha anga cha Tanzania .Ndege
hizo zimeweka makombora yao tayari
kwa kushambulia.Hivi sasa marubajni
wanashauriana hatua za kuchukua
hivyo nimeona ni vyema endapo
ukalifahamu suala hili ili kama kuna
chochote kitatokea basi wewe na
wenzako muwe na taarifa ila
msiogope.Ila msiogope kwani hata
kama tutashambuliwa ndege hii ina ina
mfumo mkubwa sana wa ulinzi na
hatuwezi kushambuliwa na kombora
lolote” Akasema Muyeye.Monica
akahisi baridi ya ghafla na mwili
ukaanza kumtetemeka kwa
ndani.Akamuita Austin
“Monica kuna tatizo lolote?
Akauliza Austin baada ya kumuona
Monica amebadilika
“Austin kuna tatizo
limetokea.Marubani wamegundua kuna
ndege zipatazo nne zinatufuata kwa
kasi na tayari zimeweka sawa
makombora kwa ajili ya
kushambulia.Hakuna anayejua nini
hasa dhumuni la ndege hizo lakini
marubani wa ndege hii wako katika
kikao hivi sasa kujadiliana hatua za
kuchukua kukabiliana na hatari yoyote
inayoweza kujitokeza.” Akasema
Monica
“My God !! akasema Austin
“Tayari wanafahamu tuko ndani
yandege hii na huu ni mwendelezo wa
mikakati yao ya kuhakikisha kwamba
hatufanikiwi na wamedhamiria
kufanya jambo lolote ili kuhakikisha
hatufanikiwi lengo letu”akasema Austin
na mlango ukafunguliwa.Muyeye
akaitwa.Akawaomba Austin na Monica
wamfuate hadi katika chumba cha
marubani
“Muyeye tumepokea taarifa muda
si mrefu kwamba ndege hii inatakiwa
kurejea Dar es salaam mara moja ama
sivyo itatolewa amri ya kushambuliwa
endapo tutakaidi amri hiyo.Wewe kama
kiongozi wa safari hii unatoa uamuzi
gani? turejee Dar es salaam kama
tunavyotakiwa? akauliza Odombo
.Muyeye akashindwa atoe jibu gani
akamtazama Monica ambaye mikono
yake ilikuwa inatetemeka .Monica naye
akamtazama Austin
“Hakuna kurejea Dar es
salaam.Tunaendelea na safari kuelekea
Kinshasa” akasema Austin
“Wewe ni nani? Kapteni Odomba
akauliza kwa ukali huku akimsogelea
Austin
“Ni mlinzi wangu” akasema
Monica ili kumzuia Odomba
asimkaribie Austin
“ Wakati mwingine usiingilie
maongezi yasiyokuhusu.Tuko katika
hatari kubwa hivi sasa halafu hutakiwi
kuwepo mahala hapa” akasema
Odomba kwa ukali.Maneno yale ya
Odombo yakampandsha hasira Austin
akainua mguu kutaka kumwendea
Odombo lakini Monica akamzuia
“Austin please !! akasema Monica
baada ya kugundua alichotaka
kukifanya Austin
“Monica naomba kaa pembeni!!
akasema Austin na Monica akaogopa
akasogea pembeni.Austin akamfuata
Odomba
“kapteni tafadhali naomba
msinilazimishe nifanye kile ambacho
sikuwa nimepanga kukifanya.Naomba
tafadhali ufuate maelekezo yangu na
ndege hii iendelee na safari hadi
Kinshasa na hakuna kurejea Dar es
salaam kama mlivyoamriwa.
Tunafahamu sababu ya ndege hizi
kutufuata na hili si suala gumu
tunaweza kulimaliza.Uamuzi wa
kurejea Dar es salaam ni kumuweka
Monica katika hatari kubwa na rais
David Zumo hatakuacha salama kwa
kitendo chako cha kuhatarisha usalama
wa mtu wake muhimu.Nakusihi kapteni
fuata maelekezo yangu na tutakuwa
salama” Akasema Austin .Kapten
Odomba akamtazama Muyeye
“Muyeye tumepewa dakika kumi
ndege iwe imebadili uelekeo na kurejea
Dar es salaam vinginevyo
tutashambuliwa.Una toa uamuzi gani?
Akauliza Odomba
“Wazo la Austin si baya.David
hatatuelewa kama tukimuweka Monica
katika hatari .Safari iendelee kuelekea
Kinshasa na hatutarudi Dar es
salaam.Wekeni sawa mifumo yote ya
ulinzi wa ndege kwa ajili ya tahadhari
endapo kutatokea aina yoyote ya
shambulio toka katika zile ndege.Vile
vile toeni taarifa kwa jeshi la anga la
Congo ili wakae tayari kutoa msaada
endapo utahitajika” akasema Muyeye
“ Hapana !! akasema Austin.Wote
wakageuka kumtazama
“ Wekeni sawa mfumo wenu wa
ulinzi wa ndege kama alivyoshauri
Muyeye lakini msiwasiliane kwanza na
jeshi la Congo kwani kwa kufanya hivyo
tutaweka mataifa yetu katika hatari
kubwa.Naombeni mnipe dakika chache
tumalize hili suala” Akasema
Austin.Kapteni Odomba akamtazama
Muyeye ambaye hakuwa na cha kusema
zaidi ya kukubaliana na ushauri wa
Austin
“Ahsante Muyeye.” Akasema
Austin na kumgeukia Monica
“Monica piga simu kwa rais sasa
hivi umtaarifu kuwa tunataka
kushambuliwa”
Monica akastuka na kumtazama
Austin kwa mshangao
“You want me to call president?
Akauliza
“ Yes Monica.Do it now!! Akasema
Austin lakini Monica akaonekana
kusita.
“Monica if you don’t do it now
they’ll shoot down this plane and we’ll
all die so make the call now”akasema
Austin na kumpa Monica namba za rais
na kwa kutumia simu iliyokuwemo mle
ndegeni,Monica akampigia simu rais
Ernest.
“Hallow”ikasema sauti ambayo
monica akaitambua ni ya rais.
“Shikamoo mheshimiwa
rais,Monica hapa ninaongea”
“Monica?”rais Ernest akashangaa.
“Ndiyo mzee,samahani kwa
usumbufu mzee nimekupigia kuomba
tena msaada wako”akasema Monica
“Msaada gani unahitaji Monica
?akauliza rais.Monica akavuta pumzi
ndefu na kusema,
“Niko ndani ya ndege ya rais David
zumo ninaelekea Kinshasa lakini kuna
jambo limetokea muda mfupi uliopita
“akanyamaza.
“Jambo gani limetokea
Monica?”akauliza rais Ernest.
“Kuna ndege nne za vita
zinatufuata na kwa mujibu wa
marubanmi wa ndege hii,ndege hizo
zimeweka makombora yake tayari kwa
kushambulia.Mheshimiwa rais naomba
sana msaada wako katika jambo
hili”akasema Monica.Ernest akasikika
akivuta pumzi ndefu.
“Monica unachonieleza ni kitu cha
kweli?”akauliza rais
“Mheshimiwa rais
ninachokwambia ni kitu cha kweli
kabisa na tuna wasi wasi kwamba
dakika yoyote kutoka sasa ndege hii
inaweza kulipuliwa kwa
makombora.Tafadhali naomba msaada
wako mheshimiwa rais.Nimewaomba
marubani wasitoe taarifa kwa jeshi la
Congo hadi kwanza nizungumze nawe”
akasema Monica
“ Ahsante Monica kwa taarifa
hii.Naomba unipe dakika tano
nilishughulikie hili suala na nitakupigia
tena” akasema rais na kukata
simu.Alipandwa na hasira kali.Alikuwa
amewasili ikulu akitokea mjini
Dodoma.Haraka haraka akamuita
Jenerali Lameck wakaelekea katika
chumba cha maongezi ya faragha.
“ Lameck nilikuonya mara ya
kwanza kuhusu kwenda kinyume na
maelekezo yangu lakini umeendelea
kunipuuza why Lameck? Maamuzi
yangu kama rais wa nchi kwa nini
unayapuuza na kufanya maamuzi yako
mbadala?!! akauliza rais kwa ukali
“Mheshimiwa rais kuna tatizo gani
limetokea? Akauliza Lameck
“Nataka uniambie nani katuma
ndege vita ziifuate ndege ya rais David
Zumo ? Nataka jibu haraka sana kabla
sijafanya maamuzi magumu !! akafoka
rais,Lameck akabaki kimya
“Answer me !! akafoka
“Mheshmiwa rais ni mimi lakini
kuna ufafanuzi” akasema Lameck
“ Sihitaji ufafanuzi wowote
Lameck.Nataka sasa hivi sitisha zoezi
linaloendelea dhidi ya ndege ya David
Zumo.Nataka ndege hizo zinazoifuatilia
ndege hiyo zikiwa zimejiandaa
kuishambulia kwa makombora zirudi
haraka sana !!
“Mheshimiwa rais naomba
unisikilize ninachotaka kukueleza”
akasema Lameck
“Lameck nimesema sitaki kusikia
ufafanuzi wowote toka kwako,nataka
sasa hivi ndege zinazoifuatilia ndege ya
David Zumo zirejee haraka
sana.Naomba usinijaribu Lameck.I’ll
destroy you !! akaendelea kufoka rais
“ Mheshmiwa rais listen to me !!
Lameck naye akafoka
“ I cant believe this” rais akasema
kwa sauti ndogo
“ Ndani ya ile ndege wamo pia
Yasmin na Austin.Kwa mara nyingine
tena Austin amemtumia Monica
kumtorosha Yasmin.Mheshimiwa rais
marubani tayari wamepewa amri ya
kurejea Dar es salaam na wakirejea
tutawakamata Austin na Yasmin halafu
Monica ataendelea na safari
yake.Mheshimiwa rais tafadhali
naomba uniache niendelee na
operesheni hii kwani itatusaida
kukipata kile kitu tunachokitafuta
sana.Endapo marubani watakaidi amri
waliyopewa hakutakuwa na njia
nyingine zaidi ya kuilipua ndege
hiyo.Mimi kama mkuu wa majeshi siko
tayari kuona Yasmin akitoka nje ya
mipaka ya nchi hii.Ni afadhali akafa
kulikko kutoroka na hati na kutishia
uhai wa nchi” Akasema Lameck.Rais
akamtazama kwa hasira na kusema
“Austin was wrong.Hufai kuwa
mkuu wa majeshi.How can you disobey
my order? Akasema rais huku akiuma
meno kwa hasira na kutoa simuyake
“ Kwa kuwa umekaidi amri
yangu,ninapiga simu mimi mwenyewe
kuondoa ndege hizo angani na dakika
nitakayokata simu hii utakuwa ni
mwisho wako kuwa mkuu wa majeshi”
akasema rais
“ Hapana mheshimiwa rais,usipige
hiyo simu.Nitafanya kama unavyotaka”
akasema Lameck na kuchukua simu
yake akapiga simu na kusitisha zoezi
lile lililokuwa likiendelea angani halafu
akamtazam arais
“ Done” akasema huku
akimtazama rais kwa hasira
“ Are youhappy now? Mheshimiwa
rais nimekuwa pamoja nawe katika
operesheni hii lakini kuna nyakati
nashindwa kukuelewa nini hasa lengo
lako.Tumeelekeza nguvu kubwa katika
kumtafuta Yasmin na tayari
tumefahamu mahala alipo lakini cha
ajabu unazuia operesheni ya
kumkamata isiendele na kumuacha
aende.Nini hasa lengo lako? Una nia ya
dhati ya kuiokoa nchi hii isigawanywe?
Akauliza Lameck
“ Nina mashaka kama kweli una
nia ya dhati ya kuisafisha nchi hii kwa
sababu kama kweli ungekuwa na
uchungu na nchi hii usingekubali
Yasmin aende wakati unajua kabisa ana
hati ya muungano ambayo ndiyo
chimbuko la uwepo wa
Tanzania.Tumefanya kazi kubwa
,tumeondoa uhai wa watu wengi na
wengi wasio na kosa lolote lengo la
haya yote ni kuisafisha nchi lakini
hakutakuwa na maana kama
tumewaondoa Alberto’s na kisha nchi
yetu ikagawanyika.” Akasema Lameck
“ I don’t care.Kama nchi
itagawanyika na iwe hivyo lakini siko
tayari kuuondoa uhai wa mwanangu
kwa ajili ya kitu kinaitwa hati ya
muungano.Mnaweza kutengeneza hati
nyingine lakini uhai wa Monica
ukipotea mnaweza kuutengeneza? She’
s the only daughter I have siwezi
kuruhusu jambo lolote la kuhatarisha
maisha yake.Kwa hili uliolifanya leo
Lameck umevuka mpaka na unanifanya
nifikirie upya kama unafaa kuwa mkuu
wa majeshi.Ninataka kufanya kazi na
watu ambao watatii amri zote za amiri
jeshi mkuu.Kitendo chako cha kutaka
kuishambulia ndege ya David Zumo
kingesababisha mwanangu akapotea na
vile vile kingehatarisha uhusiano wetu
na Congo na ingeweza kutokea hata vita
.Kwa sasa nchi yetu inapitia kipindi
kigumu sana ,sitaki kuongeza matatizo
zaidi kwani haya tuliyonayo
yanatosha.Lameck wewe ni mshirika
wangu lakini hiki ulichokifanya sina
hakika kama nitakusamehe
.Utajisikiaje endapo na mimi nitautoa
uhai wa mwanao? Naamini
ungenichukia milele” akasema rais
“No mr president!! Akasema
Lameck na kumfanya rais ashangae
“kama ni kwa manufaa ya taifa
siwezi kuchukia.”
“ What a devil !! akawaza rais
“ Mheshimiwa rais mimi na wewe
tulianza vizuri sana hadi tumefanikisha
jambo kubwa kwa jili ya nchi yetu na
kwa sasa idadi kubwa kama si wote ya
Alberto’s wameuawa lakini hiki
ulichokifanya jioni hii kimeharibu
mafanikio yote tuliyoyapata kwani
hakuna maana ya kuwaondoa Alberto’s
halafu nchi yetu ikagawanyika vipande
viwili.Siku moja utajutia hiki
ulichokifanya .Kuanzia sasa mimi
sintakushauri jambo lolote bali
nitakuwa natekeleza yale yote
utakayoniamuru nifanye na ukumbuke
kuwa katika operesheni hii mimi
nilikuwa mtekelezaji wa maagizo lakini
maamuzi yote umeyafanya wewe kwa
hiyo mambo yakiharibika ni wewe peke
yako utakayejibu” akasema Lameck na
rais akamtazama kwa hasira
“Kwa nini tumefika hapa Lameck?
Akauliza rais
“Wewe ndiye uliyesababisha
tukafika hapa baada ya kumchagua
Monica badala ya nchi kwa hiyo
unapaswa kujiandaa kwa athari za
maamuzi yako” akasema Lameck.Rais
akamtazama Lameck kwa hasira na
kuuliza
“ Una hakika Yasmin you katika ile
ndege? Akauliza Ernest
“Ndiyo nina uhakika.Silvanus
Kiwembe alinipigia simu na
kunihakikishia kwamba amepitia
kumbu kumbu za kamera za ulinzi pale
uwanjani na amemuona Yasmin akiwa
na akina Monica.Aliponipa maelezo
hayo nikaamua kuchukua maamuzi
yale ya kutuma zile ndege ili
kuwaogopesha na kisha kuiamuru
ndege irejee Dar es salaam na
kuwakamata Yasmin na akina
Austin.Sikutaka Yasmin atoke nje ya
Tanzania” akasema Lameck
“Lameck ulichokifanya hakikuwa
kitu kibaya lakini ulipaswa kuwasiliana
kwanza na mimi ili tujadiliane na tuone
nini tufanye.Mimi na wewe hatupaswi
kuingia katika malumbano.Tulianza
pamoja suala hili na tunapaswa
kulimaliza pamoja.Tukitengana
tutaharibu kila kitu.Endapo ungelileta
kwangu suala hilo tungekwisha lipatia
ufumbuzi .Hebu fikiria Lameck nini
kingetokea endapo ndege ya David
Zumo ingeshambuliwa? Tungezidi
kuongeza matatizo zaidi.Nakuomba
tafadhali tushirikiane katika kila jambo
hata kama ni dogo.Nafahamu hata
wewe una uchungu na nchi lakini
umakini unatakiwa sana katika kupata
ufumbuzi wa baadhi ya
mambo.Tumeelewana Lameck?
Akauliza rais
“ Nimekuelewa mheshimiwa rais”
akajibu Lameck
“ Kwa mara ya nyingine
nitakusamehe na hili pia ila sitaki
urudie tena kudharau maagizo yangu
na kufanya vile utakavyo wewe”
akasema rais
“ Ahsnate mheshimiwa rais”
“ Nitawasiliana na David Zumo
muda si mrefu na kumtaka radhi kwa
kitendo kilichotokea kwani lazima
taarifa zitamfikia vile vile nitamtaka
mara tu ndege yake itakapotua
Kinshasa Austin na Yasmin wakamatwe
mara moja.Hawataweza kutoroka hata
kama wako nje ya nchi ndiyo maana
nikakwambia ulipaswa kunitaarifu
mapema suala hili kwani nina mkono
mrefu” akasema rais Ernest na
kuzitafuta namba za David Zumo
akampigia
“Hapokei simu” akasema rais
“Unapaswa kuendelea kumtafuta
tena na tena kabla ndege haijatua
kwani ndege ile inakwenda kwa kasi
kubwa na inaweza kutumia saa nne
kufika Kinshasa kwa hiyo David Zumo
anapaswa kuwa na taarifa kabla ndege
haijatua.” Akasema Lameck
“ Inashangaza toka asubuhi
sijapokea simu yoyote toka kwa Habib
kulikoni?Alinitaka nimpigie simu
asubuhi ya leo na nimfahamishe
kuhusiana na maendeleo ya kumpata
Yasmin lakini sikufanya hivyo na
hajanipigia simu.Kuna kitu anapanga
kukifanya ? Wale jamaa si watu wa
kuingia nao katika vita kwani
mashambulizi yao hupangwa kimya
kimya.Nitawasiliana naye kesho
asubuhi kumjulisha kuhusu Yasmin ”
Sura yake ikajikunja alipomuwaza
Yasmin
“Austin tayari amekuwa adui
yangu mkubwa .Ninaapa kutumia
uwezo wangu wote kumsaka na
kuhakikisha ninampata.Hawezi kijana
mdogo kama yule kucheza na akili
yangu kiasi hiki.Tatizo ni kwamba
amejiweka karibu na Monica na
anamtumia kama ngao yake
.Anamtumia Monica kufanikisha
mipango yake kwani anafahamu siwezi
kumkatalia Monica kitu
chochote.Nilifanya kosa kubwa sana
kumshirikisha huyu kijana katika
jambo kubwa kama hili na sasa
amekwisha ujua udhaifu wangu na
anautumia kufanikisha mipango yake
lakini naapa lazima nimsake hadi
nimpate.Kitukingine cha kujiuliza
anampeleka wapi Yasmin? ” akajiuliza
rais bila kupata jibu
 
QUEEN MONICA : FINAL SEASON
SEHEMU YA 3

Dakika tano hazikuisha toka
Monica awasiliane na rais Ernest ndege
vita zilizokuwa zinawafuatilia
zikabadili muelekeo na kurejea
zilikotoka.Kitendo kile kiliwashangaza
sana marubani wakafurahi na
kupongezana kwa kitisho kile
kuondoka.Wote wakaenda pia
kuwapongeza Monica na Austin.Pierre
Muyeye akawachukua Monica na Austin
wakaenda katika chumba cha maongezi
“ Monica na Austin kwanza
ninawashukuru sana kwa msaada wenu
mkubwa mliotusaidia.Bila ninyi sijui
nini kingetokea.Hata hivyo nataka
kufahamu kuhusiana na hiki
kilichotokea kwani nitalazimika
kumtaarifu rais suala hili.Nataka kujua
ndege zile kwa nini zilitufuata na lengo
lake lilikuwa nini? Kitendo cha kuweka
makombora tayari kwa kushambulia
kilimaanisha nini? Akauliza Muyeye
“Rais David Zumo aliomba kibali
kwa rais Ernest mkasa cha kutua Dar es
salaam na akapewa.Tumetua salama na
kuondoka salama lakini ghafla
tunaanza kufuatiliwa na kuamriwa
kurejea dar es salaam.Kuna chochote
kibaya tumekifanya? Akauliza Muyeye
akionekana kuvuja jasho.
Austin na Monica wakatazamana
na Monica akataka kusema kitu Austin
akamzuia na kusema
“Pierre Muyeye tunakushukuru
kwa busara zako wakati wa tukio lile na
ukachagua kutusikiliza sisi badala ya
marubani .Pamoja na hayo nina ombi
moja kwako” akanyamaza akamtazama
Muyeye na kusema
“Hiki kilichotokea ,naomba
Monica awe wa kwanza kumueleza
mheshimiwa rais David
Zumo.Nafahamu ni wajibu wako kutoa
taarifa kwa vyombo husika lakini
endapo taarifa itakayowasilishwa
isipokuwa sahihi basi inaweza
kusababisha kutetereka kwa
mahusiano ya kindugu baina ya nchi
zetu mbili.Ni Monica pekee anaweza
akalimaliza suala hili endapo atapewa
nafasi ya kufanya hivyo na
ninakushauri umpe nafasi hiyo ya
kuzungumza kwanza na rais kabla ya
mtu mwingine yeyote hajawasilisha
taarifa ya jambo hili kwa rais” akasema
Austin
“Austin hoja yako nimeielewa na
ninamshukuru sana Monica kwa
kumpigia simu rais wa Tanzania na
ndege zile zikaondoka lakini pamoja na
hayo ningependa kufahamu kile
mnachokifahamu kuhusu ndege
zile.Najaribu tu kuwaza ni vipi endapo
rais angekuwepo ndegeni wakati ndege
zile zinatufuata zikiwa tayari na
makombora?Naamini hivi sasa
tungekuwa tunaongelea masuala
mengine kabisa.Nataka kufahamu kuna
kitu gani tumekifanya hadi tupewe
amri ya kurejea Dar es salaam?
Akauliza Muyeye.
“Muyeye suala hili ni pana lakini
nitajaribu kukupa picha japo ndogo ya
kuhusiana na kile kilichotokea.Jana
yamefanyika mashambulizi mawili
yanayodaiwa kuwa ya kigaidi katika jiji
la Dar es salaam na mjini
Dodoma.Uchunguzi wetu tulioufanya
tumegundua kwamba shambulio lile
halikufanywa na magaidi wa Alshabaab
kama walivyojitokeza na bali
limefanywa na watu wa ndani ya nchi
tena waliomo serikalini.Bado
uchunguzi wetu unaendelea ili
tufahamu ni akina nani hao waliopanga
shambulio lile.Mmoja wa watu
tuliyeambatana naye katika safari hii
ana taarifa za muhimu sana kuhusiana
na shambulo lile la jana na maisha yake
yako hatarini kwa hiyo Monica
akanisaidia usafiri wa kumuondoa
Tanzania ili aweze kutupa taarifa
alizonazo kuhusiana na mshambulio
yale.Ninahisi wale watekelezaji tayari
wamefahamu kuwa mtu huyo yumo
katika ndege hii na ndiyo maana
wakatoa amri ya kurejea Dar es salaam
ili waweze kumkamata.Wanatumia kila
nguvu waliyonayo ili kuhakikisha
kwamba siri yao haivuji na kilichotokea
muda mfupi uliopita ni jitihada zao za
kutaka kuzuia siri zao zisivuje”
akasema Austin
“Austin umeniogopesha
zaidi.Kumbe tungeweza hata
kulipuliwa kama lengo la hao jamaa ni
kuificha siri yao isivuje.Wasi wasi
wangu zaidi ni kwa Monica.Kwa
maelezo hayo ulonipa ninaona yuko
katika hatari kubwa kwani yeye ndiye
aliyefanikisha mkafanikiwa
kumuondoa huyo mtu mwenye
kufahamu siri za hao jamaa .Wataanza
kumuwinda sana wakiamini naye kuna
kitu atakuwa anakifahamu au
ameambiwa kuhus wao.Austin
tutafanya nini kumlinda Monica?
Akauliza Muyeye
“ Pierre Muyeye usihofu,Monica
hayuko katika hatari.Monica hawezi
kuguswa na mtu yeyote.Nadhani
umeshuhudia nguvu yake.Amempigia
simu rais Ernest na baada ya muda
mfupi ndege zile zikabadili uelekeo na
kurudi zilikotoka.Usiwe na wasi wasi
kabisa kuhusu Monica. Muyeye nadhani
tumeelewana na unakubaliana na ombi
langu kwamba Monica awe wa kwanza
kuzungumza na David Zumo kuhusiana
na hiki kilichotokea?” Akasema Austin
“ Hakuna shaka kuhusu
hilo.Nitahakikisha anapata nafasi ya
kukutana na na rais usiku huu”
akasema Muyeye na kutoka mle
chumbani akarejea katika chumba cha
marubani.
“Austin nini hasa lilikua lengo la
kutuma zile ndege? Monica akamuuliza
Austin baada ya Muyeye kutoka
“Kama nilivyosema awali lengo la
hawa jamaa ni kutumia nguvu zao
kuhakikisha wanampata Yasmin.Ndege
zile zilitumwa kwa kusudi maalum na
walikuwa wamejiandaa kwa lolote hata
ikibidi kuilipua ndege hii na ndiyo
maana makombora yaliwekwa
tayari.Hata hivyo nakutoa hofu
kwamba shambulio lolote
lisingefanikiwa kwa sababu ndege hii
ina mfumo mkubwa wa ulinzi .Ina
uwezo wa kujikinga dhidi ya
mashamulio yoyote ya makombora ya
adui kwa hiyo si ndege ambayo ina
weza kushambuliwa kirahisi
rahisi.Ukiwa ndani ya ndege hii
unakuwa salama zaidi. ” Akasema
Austin
“ Austin kuna kitu kingine
ambacho bado naendelea kujiuliza .Ni
kuhusiana na rais.Kwa nini amekuwa
mwepesi sana kunisikiliza na
kunisaidia yale yote ninayomuomba ?
Hata kama jambo liwe gumu kiasi gani
nikimuomba rais linafanikiwa kwa
nini? Do you know anything why he’s
doing that to me? Akauliza Monica
“I don’t know
anything.Inawezekana ni kwa sababu
ya mahusiano mazuri kati yake na
wazazi wako” akajibu Austin
“Nina wasi wasi lazima kuna
jambo lingine kwa sababu uliniambia
nimpigie simu siku ile usiku
kumuomba usafiri wa kwenda Zanzibar
na akanipa ndege ya kwenda Zanzibar
tena kama haitoshi na ulinzi juu.Leo
nimempigia simu kumtaarifu tunataka
kushambuliwa na muda mfupi baadae
ndege zile zilizotaka kutushambulia
zikaondoka.Kwa nini anafanya haya
yote?
“Usiumize kichwa kwa jambo hilo
Monica.Kitu cha msingi kwa sasa ni
kujielekeza katika kile kilichopo mbele
yetu.” Akasema Austin
“ Austin bado kuna kitu
nakitafakari.Unadhani ni rais aliyetoa
amri ndege zile zitufuate? Akauliza
Monica
“ Kama si yeye nani basi anaweza
akatoa amri ndege zile zitufuate na hata
kutishia kufanya shambulio? lazima
atakuwa ni rais kwani yeye ndiye
mwenye uwezo wa kuamuru chochote
kifanywe na jeshi.Kwa nini umeuliza
hivyo?
“Nimeuliza hivyo kutokana na
namna rais alivyoonyesha kustuka
nilipomtaarifu kwamba kuna ndege
zinataka kutushambulia.Inaonekana
hakuwa na taarifa za jambo lile”
akasema Monica
“Unahisi kwamba rais hakuwa na
taarifa zozote kuhusiana na zile ndege?
Austin naye akauliza
“ Sina hakika kama alikuwa
anafahamu chochote kuhusiana na zile
ndege kwani alistuka sana
nilipomueleza kwamba kuna ndege
zinatufuata na zinataka
kutushambulia” Akasema Monica
“Ninaweza kukubaliana na hicho
unachokisema .Rais katu asingekubali
kuruhusu ndege zile zitufuate na hata
kutishia kulipua ndege wakati akijua
kwamba umo ndani ya ndege hii kwa
hiyo nakubaliana nawe kwamba kuna
uwezekanao jambo hili limefanywa na
watu wengine bila ya rais
kufahamu.Kama ndiyo, ni nani basi
anaweza kuwa amefanya jambo hili bila
kumshirikisha rais? Inawezekana kuna
watu ambao wanamzunguka rais?
Akauliza Austin
“Hilo unalolisema linawezekana
kabisa Austin kwani rais aliponiita
ikulu aliniambia kwamba siku ile
tulipotaka kuzuiliwa uwanja wa ndege
tukitokea Zanzibar hakuwa
amefahamishwa chochote.Kuna watu
walitoa amri ya sisi kukamatwa bila ya
yeye kufahamu kwa hiyo ni wazi
kwamba kuna mambo yanafanyika bila
ya rais kufahamu.Hata hili tukio la leo
naamini lilifanywa bila rais kufahamu”
akasema Monica
“Hii haileti picha nzuri kama
wanazungukana wao kwa wao.rais
alikosea sana kuchagua kutoshirikiana
nami .Lakini mwisho wa sakata hili
lazima wote hawa wanaoshirikiana na
rais tuhakikishe tunawaweka
nguvuni.Mtu wa kwanza ambaye tayari
tumemfahamu kuwa ni mshirika wa
rais ni mkuu wa majeshi Lameck
msuba.Huyu ni mtu ninayefahamiana
naye sana na mimi ndiye
niliyempendekeza kwa rais amchague
ayaongoze majeshi yetu kwa kutumaini
ni mzalendo wa kweli na niliposikia
maongezi yake na rais katika ile rekodi
ya Irene nilistuka sana .Nitakapotulia
nitaisikiliza tena rekodi ile ili nipate
uhakika kama kweli aliyekuwa
akizungumza na rais katika ile rekodi
ni Lameck msuba ninayemfahamu
mimi.” akasema Austin
 
QUEEN MONICA : FINAL SEASON
SEHEMU YA 4

Job aliwakaribisha nyumbani
kwake Daniel na Irene.Marcelo tayari
alikwisha fika kitambo kwani yeye
alitangulia
“Kila kitu kilikwenda vizuri
hakukuwa na tatizo lolote? Marcelo
akamuuliza Job
“Hakukuwa na tatizo
lolote.Wameondoka salama” akasema
Job
“Marcelo tell Julieth to prepare
something for Daniel and Irene”
akasema Job
“No thank you Job.Ninachokihitaji
sasa hivi ni kuwapata wazazi wangu
tu.Sihitaji kitu kingine
chochote.Tafadhali naombeni mfanye
kila mnaloweza kulifanya ili niwapate
tena wazazi wangu.Namuhofia baba
yangu ni mgonjwa na anaweza
akapoteza maisha” akasema Irene
“Usijali Irene baba yako
atapatikana.Naomba sasa unipe picha
kamili ya tatizo lako kwani Austin
alinipa maelezo ya juu juu kutokana na
haraka” Akasema Job
“Job ngoja mimi nielezee kwani
Irene kwa hali yake ilivyo hataweza
kukueleza vizuri.Ni kwamba Irene
anafanya kazi ……………” akasema Daniel
lakini Job akamkatisha
“ Muache Irene anieleze yeye
mwenyewe.Irene tafadhali jikaze na
unieleze kile kilichotokea.Tell me
everything .” akasema Job.
“ I cant .Muache Daniel akueleze
kwani anafahamu kila kitu
kilichotokea” akasema Irene na
kuinamisha kichwa
“ Hapana nataka wewe unieleze
kile kilichokutokea.Tafadhali Irene
tuokoe muda” akasema Job
“ Job don’t you trust me? Kwa nini
hutaki mimi nikueleze jambo
lililomsibu Irene? Akauliza Daniel
“ Ahsante Danel najua
unafahamukila kitu lakini nataka Irene
ndiye anieleze kilichotokea.C’mon
Irene tell me” akasema Job.Irene
akainua kichwa akamtazama Job na
kusema
“Sijui hata nianzie wapi kwa
sababu akili yangu nahisi imefika
mwisho wa kufikiri” akasema Irene
“Anzia mwanzo kabisa.” Akasema
Job.Irene akakaa kimya kwa muda
akivuta kumbu kumbu na kusema
“Siku moja alinifuata mtu mmoja
ambaye ni msaidizi wa rais anaitwa
Mukasha”
“Mukasha ?!! Job akastuka
“Ndiyo.Mukasha alinifuata
akanitaka nimsaidie kudukua simu ya
rais.Aliniambia kwamba kuna jambo
baya linaweza kumtokea rais hivyo
akanitaka nidukue simu hiyo ili
afahamu rais anazungumza na akina
nani.Baada ya kuidukua simu ya rais
tulisikia maongezi kati yake na
mwanamke mmoja simkumbuki jina
lake lakini walikuwa wanaongelea kitu
kuhusiana na usalama wa Monica kuwa
mashakani.Baada ya hapo
sikuwasiliana tena na Mukasha hadi
jana aliponipigia simu na kunitaka
nidukue tena simu ya rais” akanyamaza
“Sikuwa tayari kufanya kitendo
kile tena kwani ni kitendo cha hatari
sana lakini Mukasha akanitishia
kwamba nisipofanya vile anavyotaka
atafanya kila awezalo ili kibali
nlichopewa cha kumpeleka baba yangu
nje ya nchi kwa matibabu
kifutwe.Niliogopa kitisho chake
ikanilazimu nifanye vile
anavyotaka.Nikaweka program Fulani
katika simu ya rais ambayo
iliniwezesha kusikia mazungumzo kati
ya rais na wale anaoongea nao simuni
na ndipo nikafanikiwa kunasa
mazungumzo kati ya rais na jenerali
lameck wakizungumzia kuhusu
shambulo litakalotokea.Hiyo ilikuwa ni
saa mbili kabla ya shambulio la hoteli
kutokea.Kwa bahati mbaya rekodi ile
anayo Austin ungesikiliza vizuri”
akasema Irene
“Tayari nimekwisha isikia.Austin
alinipa nikaisikia” Job akasema
“Baada ya kuipata rekodi ile
niliogopa sana nikarudi nyumbani na
nikafikiria namna ya kufanya .Katika
rekodi ile rais na Lameck
wanazungumzia kuhusu kumuua
madam Agatha mke wa rais.Huyu ni
mama ambaye ninaelewana naye sana
na ananipenda kama
mwanae.Ilinilazimu kumpigia simu na
kumtaka atoke pale katika ile
hoteli.Alinisikia na akatoka pale
hotelini na baadae hoteli
ikalipuliwa.Usiku madam Agatha
akanipigia simu akanishukuru kwa
kumsaidia akatoka salama ndani ya ile
hoteli lakini akanitaka nimueleze
nimewezaje kugundua kama kuna
shambulio litatokea? Nilimuahidi
kumjibu baadae na toka wakati huo
nikazima simu.Leo asubuhi nikaenda
kuonana na Daniel ili kumuomba
msaada wa fedha kwa ajili ya matibabu
ya baba lakini tukiwa sehemu
tunaongea nikafuatwa na watu wawili
wakanitaka niongozane nao.Nashukuru
Daniel akapambana nao na
tukafanikiwa kuondoka.Tulipofika
nyumbani tukakuta mambo ya
kusikitisha.Wazazi wangu hawakuwepo
na mfanyakazi wetu wa ndani
ameuawa.Pembeni yake kukawekwa
ujumbe ukinitaka niwasiliane na
namba zilizoandikwa katika ujumbe ule
kama ninataka kuwaokoa wazazi
wangu.Daniel aliwasiliana na watu hao
lakini waliendelea kusisitiza kwamba
wanahitaji mimi ndiye nizungumze nao
na niwarudishie kitu chao na wao
wawaachie huru wazazi
wangu.Walituma video ambayo
inaonyesha namna wanavyowatesa
wazazi wangu.Job tafadhali
nawaombeni mfanye kila muwezalo
kuwatafuta na kuwapata wazazi
wangu.Baba yangu ni mgonjwa na
endapo wataendelea kumshikilia
anaweza akapoteza maisha” akasema
Irene.Daniel akamuonyesha Job video
iliyotumwa na wale watu waliowateka
wazazi wa Irene.Job akaitazama kwa
makini sana ,akairudia zaidi ya mara
tatu halafu akasema
“Baada ya hapo hujawasiliana nao
tena?
“Hapana hatujawasiliana tena na
watu wale” akasema Daniel.Job
akachukua muda akafikiri kidogo na
kusema
“Tunatakiwa tuwatafute watu
hawa ni akina nani.Nina uhakika mke
wa rais ambaye ulimsaidia kutoka
salama katika jengo lile
lililoshambuliwa atakuwa nyuma ya
jambo hili .Kuna mtu mwingine yeyote
uliyemtaarifu suala hili zaidi yake?
Akauliza Job
“ Hapana sijamtaarifu mtu
mwingine yeyote zaidi yake.Lakini
madam Agatha hawezzi akanifanyia
kitu kama hiki.Yule ni mtu mwema
sana na zaidi ya yote mimi ndiye
niliyemuokoa toka katika
hatari.Nisingempa taarifa za kuwepo
kwa shambulio lile katika hoteli
angekuwa miongoni mwa watu
waliofariki dunia .Kwa nini anifanyie
haya?Sina hakika kama ni yeye.lazima
kuna watu wengine wanaofanya hivi na
si madam Agatha.Ninaweza kumtetea
kwa sababu ninamfahamu vyema ni
mtu mwema sana” akasema Irene
“Agatha hayuko kama
unavyomfahamu.Ni mtu mbaya zaidi ya
unavyoweza kufikiria.Agatha ni mfuasi
wa mtandao au kikundi kinajiita
Alberto’s.Hawa wana lengo la kuitawala
dunia na kueneza mambo yao machafu
kama vile mapenzi ya jinsia moja,utoaji
mimba,n.k.kwa ujumla ni watu
wanaofungamana na nguu za giza.Hapa
Tanzania tayari walikwisha simika
himaya yao na ndio waliokuwa
wanaioangoza nchi kwani rais Ernest
Mkasa ni mmoja wa watu
wao.Walimuweka madarakani ili
waweze kumtumia kufanikisha
mipango yao miovu kwa taifa.Wao ndio
wanaoliongoza taifa na rais yuko pale
kama picha tu hadi hivi majuzi Austin
alipokuja na kumtaka waanzishe
mapambano ya kuwaondoa Alberto’s
hapa nchini.Kwa kuwa hatuna muda wa
kutosha tutaongelea suala hilo wakati
mwingine. Lakini ninachotaka tu
kukufahamisha ni kwamba Agatha ni
mtu mwenye roho mbaya sana na nina
uhakika mkubwa kwamba ndiye aliye
nyuma ya haya yanayotokea kwa
familia yako.Anataka kufahamu ni jinsi
gani ulifahamu kuhusu shambulio lile
na ndiyo maana ameona njia pekee ya
kukufanya ufanye kile anachokitaka ni
kwa kuwachukua mateka wazazi
wako.Mimi na wenzangu tutajitahidi
kuhakikisha tunawapata wazazi wako
na kufahamu ni nani aliye nyuma ya
haya matukio.Ninachokuomba kwa
sasa ni wewe kuchukua simu na
kuwapigia hao jamaa kisha waambie
wanahitaji nini halafu tutajua nini cha
kufanya.” Ak asema Job
“ Job hawa jamaa wanachokihitaji
ni kitu kimoja tu.Ni kujua nilifahamu
vipi uwepo wa shambulio lile?
Ninaamini ni hicho tu na hakuna
kingine.Nikiwapigia simu watasema
niwape hicho wanachokitaka.Nitawapa
nini wakati rekodi anayo Austin?
Akasema Irene
“ Irene hakuna anayefahamu
kama unayo rekodi ile.Ni sisi
pekee.Kwa hiyo chukua simu wapigie
na uwasikilize
wanachokitaka.Usiwaeleze kama unayo
rekodi” akasema Job.Irene akamtazama
Daniel aliogopa sana
“Do it Irene” Daniel akamwambia
“Ninaogopa Daniel .Ni vipi endapo
kwa kufanya hivyo nitakuwa ninazidi
kuwaweka wazazi wangu katika hatari?
“ Irene kuendelea kukaa kimya
kunawaweka wazazi wako katika
hatari zaidi kwa hiyo Lazima tufanye
kila jitihada kuhakikisha kwamba
tunawakomboa wazazi wako.Hatua ya
mwanzo ni kama alivyosema Job
chukua simu na uzungumze na hao
watekaji na usikie wanataka nini”
akasema Daniel.Irene huku akiwa na
wasi wasi mwingi akaiwasha simu yake
na hakujali jumbe nyingi zilizoingia
akaziandika namba zile alizotakiwa
apige na kupiga halafu akaiweka simu
ile katika sauti kubwa ili kila mmoja
aweze kusikia anachokiongea na wale
watu
“ Irene.Umepiga kwa wakati
muafaka kwani ungechelewa dakika
kumi tu tayari tulikuwa katika
maandalizi ya kuwatekeza wazazi wako
na kisha tuanze kukusaka wewe!!
Ikasema sauti kali ya mwanamke
upande wa pili
“Tafadhali sana naombeni
msiwadhuru wazazi wangu.Msiwafanye
chochote!! Akasema Irene na kutaka
kuanza kulia Job akamfanyia ishara
kwamba asithubutu kulia
“Hatutawafanya chochote wazazi
wako endapo utatimiza kile
tutakachokuelekeza” akasema Yule
mwanamama upande wa pili
“ Mnahitaji nini? Semeni chochte
mnachokihitaji na mimi
ntawapatia.Kama ni pesa semeni ni
kiasi gani mnakihitaji nitawapa”
akasema Irene na kushindwa kuyazuia
machozi kudondoka
“ Irene hatuhitaji
pesa.Tunakuhitaji wewe”
“ Mnanihitaji mimi?
“ Ndiyo”
“ Mnahitaji nini toka kwangu?
Semeni mnachokitaka”
‘ Irene tunakuhitaji wewe.Subiri
baada ya dakika kadhaa utajulishwa ni
wapi unatakiwa kwenda” akasema yule
mwanamama
“Tafadhali naom…” kabla
hajamaliza sentensi yake simu
ikakatwa.Irene akaanza kulia
“Tafadhali usilie Irene.Ni muda wa
kusimama imara na kupambana kwa
ajili ya wazazi wako.Sisi tuko tayari
kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya
kuhakikisha wazazi wako
wanakombolewa lakini na wewe
lazima usimame imara katika
kupambana . We have to fight together
.Kitendo cha kudukua simu ya rais
kinanihakikishia kwamba wewe ni
mwanamke jasiri sana na unaweza
ukafanya jambo lolote lile hata kama ni
la hatari kwa hiyo hili lisikupe hofu.Sisi
tuko pamoja nawe” akasema Job na
Irene akafuta machozi
“ Sasa tayari tumefahamu
wanachokihitaji hawa jamaa.Ni kama
nilivyosema awali kwamba
wanamuhitaji Irene ili kujua amepataje
taarifa za lile shambulio? Wamesema
kwamba watampa maelekezo muda si
mrefu na maelekezo hayo wataelekeza
mahala anakotakiwa kwenda.Usiogope
wakikuelekeza sehemu ya kwenda
nenda bila hofu kwani sisi tutakuwa
nyuma yako tukifuatilia kila
kinachoendelea.” Akasema Job.
“ Mnataka niende mwenyewe kwa
hawa wauaji? Akauliza Irene
“ Irene hawa jamaa hawatakiwi
kujua kama kuna watu unashirikiana
nao na nina imani kabisa katika
maelekezo watakayokupa
watakwambia kwamba unatakiwa
uende mwenyewe.Ni watu wataalamu
na wanajua wanachokifanya hivyo
lazima watachukua tahadhari kubwa
kuhakikisha kwamba hakuna yeyote
atakayekufuata .Sisi tutakuwekea kifaa
maalum ambacho kitatusaidia
kufahamu mahala uliko na tutasikia
mazungumzo yote kati yako na hao
jamaa na tutakupa maelekezo nini cha
kufanya.” akasema Job
“ Job I’m so scared” akasema Irene
“ Usiogope tafadhali.Trust us Irene
.Tutawakomboa wazazi wako” akasema
Daniel.Job akainuka na kuelekea
chumbani kwake kisha akarejea akiwa
na sanduku alilolifungua kwa
namba.Ndani ya sanduku lile kulikuwa
na vifaa mbali mbali akatoa kiboksi
fulani akakifungua na kutoa kidude
kidogo akakiweka sikioni mwa Irene.
“ Hiki ni kifaa cha mawasiliano
ambacho kila mmoja wetu atakivaa
sikioni na kitatuwezesha
kuwasiliana.Kila tutakachokiongea
utakuwa unakisikia na sisi tutakuwa
tunasikia kila utakachokuwa
unazungumza na hao jamaa na
tutakupa maelekezo nini cha
kufanya.Hawa jamaa wanaweza
wakagundua kwamba una kifaa hiki
sikioni ingawa si rahisi sana hata hivyo
utavaa saa hii ambayo nayo
itatuwezesha sisi kufahamu mahala
uliko na hata kusikia kila
kinachoendelea kati yako na hao
jamaa.” Akasema job na mara simu ya
Irene ikaita.
“ It’s them” akasema Irene.
“ Pokea uzungumze nao” akasema
Job.Irene mikono ilikuwa
inamtetemeka.Akaipokea simu
“ Hallow “ akasema
“ Fuata maelekezo haya.Karibu na
La Sienda casino utakuta kuna gari
mbili zimeegeshwa pembeni ya
barabara mbele ya kontena
jekundu.Moja ni la rangi nyeupe na
lingine nyekundu.Utaingia katika gari
jekundu.Tafadhali uhakishe uko
mwenyewe kwani ukithubutu kufanya
jambo lolote la kipuuzi au kumwambia
mtu mwingine yeyote kuhusiana na
suala hili basi hutawaona wazazi wako
tena kwa hiyo fuata maelekezo yetu na
wazazi wako watakuwa salama.Narudia
tena usithubutu kufanya jambo lolote
ambalo haujalekezwa ulifanye”
akasema Yule jamaa aliyekuwa akimpa
maelekezo Irene
“Tafadhali naomba mnihakikishie
kwamba nikifanya haya mnayotaka
niyafanye mtawaachia wazazi wangu”
akasema Irene
“Ukifuata maelekezo uliyopewa
wewe na wazazi wako mtakuwa
salama.Hatuna lengo baya nawe au
wazazi wako.Ukionyesha ushirikiano
kwetu mtaachiwa huru nyote.Fanya
haraka uelekee mahala hapo
ulipoelekezwa” akasema Yule jamaa na
kukata simu
“Kinachofuata hapa kwa sasa ni
kujiandaa kwa ajili ya kuanza
safari.Irene wewe utatangulia mimi na
Daniel tutakuwa nyuma yako.Hawa
jamaa hawatakiwi kugundua kama
kuna atuwako nyuma yako.Vifaa hivi
tulivyokuwekea vitatupa urahisi sisi wa
kukufuatilia na kujua mahala
utakapokuwa” akasema Job halafu
akapanda chumbani kwake akarejea na
fulana isiyopenya risasi na kumpa
Daniel pamoja na basrora mbili.
“ Marcelo sisi tunaondoka kuna
kazi tunakwenda kuifanya ya muhimu
sana.Utabaki hapa nyumbani na
Julieth.”Job akamweleza Marcelo
“Tayari Yasmin amekwisha
waelekeza mahali ilipo hati ya
muungano? Marcelo akauliza
“Hapana bado.This is another
mission” akasema Job .Akamsindikiza
Irene garini halafu nao wakaingia
katika gari lingine safari ikaanza.
“ Job naomba niulize swali.Yule
jamaa pale ndani,Dr Marcelo
ulipomuaga kwamba tunaondoka
akakuuliza kama tayari umeelekezwa
mahala ilipo hati ya muungano.Alikuwa
anamaanisha nini? Daniel akauliza
“Daniel umeuliza swali zuri lakini
nitakujibu baadae kwa sasa tujielekeze
katika zoezi hili gumu.Nguvu na akili
zetu zote tuzielekeze huko.We have to
save Irene,we have to save her
family.Watu hawa baada ya kuwaeleza
kile wanachokitaka hawatamuacha hai
lazima watamuua kwa hyo tusielekze
akili zetu katika masuala mengine bali
tujielekeze katika kuhakikisha
tunawakmboa wazazi wa Irene”
akasema Job
“Job usihofu kuhusu hilo.Wazazi
wa Irene watakombolewa na
operesheni hii itakamilika.Lakini
nahitaji kufahamu kuhusiana na
operesheni nyingine zinazoendelea
kwani mimi na ninyi tayari ni timu
moja.Austin aliniambia kwamba kuna
mambo yanayoendelea ila hakupata
nafasi ya kunieleza ni mambo
gani.Unaweza ukanieleza tafadhali japo
kwa ufupi ili mimi na ninyi tuwe katika
ukurasa mmoja? Akauliza Daniel
“Fine” akasema Job
“ Niliwaeleza kuhusiana na
Alberto’s na mapambano ambayo
Austin na rais walikuwa
wameyaanza.Tukiwa katika kuandaa
mikakati ya kuwaondoa Alberto’s wote
hapa nchini Austin alipigwa risasi na
mpenzi wake anaitwa Maria na kwa
bahati nzuri tulifanikiwa kumkamata
mwanamke huyo na
kumuhoji.Tuligundua kwamba
mwanamke Yule alikuwa na mama
yake anaitwa Yasmin ambaye ni mfuasi
wa kundi la IS na ambaye alikuwa
amefungwa hapa nchini kwa miaka
kadhaa.Tulimuuliza rais kuhusiana na
Yasmin na Akakana
kumfahamu.Baadae tukagundua
kwamba rais ametundanganya kwani
alikuwa anamfahamu Yasmini na
alikuwa katika mipango ya kumuachia
huru toka kifungoni.Tuligundua tena
kwamba rais alifanya makubaliano na
Alshabaan na walikubaliana kwamba
Yasmin pamoja na mtu mwingine
anaitwa Tariq waachiwe huru.Hatujui
makubaliano hayoyalihusu nini.Pamoja
na kutaka Yasmin na Tariq waachiwe
huru Alshabaab pia walitaka wapewe
hati ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.”
“ He gave them?!! Akauliza Daniel
kwa mshangao mkubwa.Job aliyekuwa
makini katika usukani akajibu
“Yes he gave them” akajibu Job na
Daniel akamtazama kwa mshangao
akashindwa aseme nini
“Nimekosa neno la kusema.Job
niambie tafadhali hili suala ni la kweli?
“kwa nini nikudanganye Danny?
Job akasema
“Yote haya nikwambiayo ni ukweli
mtupu”
“I cant believe this.President
Ernest can do that?!! Akauliza Job
“Kwani yeye ni malaika? Ni yeye
ndiye aliyefanya haya yote.Ameitoa
hati ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar kwa magaidi.Kwa bahati nzuri
Yasmin ambaye ndiye aliyekuwa
amekabidhiwa hati hiyo alitaka tufanye
mabadilishano tumpatie mwanae
Maria na yeye atupatie hati ya
muungano na hilo ndilo zoezi
linaloendelea hivi sasa.Austin
amekwenda Kinshasa akiwa katika
harakati za kutimiza masharti ya
Yasmin ili atueleze mahala ilipo hiyo
hati” akasema Job.
“Sitaki kuamini kama kweli hati ya
muungano haiko ikulu.Kwa nini rais
afanye hivyo? Halafu kwa nini rais awe
na mawasiliano na Alshabaab ambao
wanatambulika dunia nzima kama ni
magaidi? Akauliza Daniel
“Sababu iliyopelekea akafanya
hayo aliyoyafanya hatujui lakini
tunaendelea kuitafuta.Hatutalala hadi
tuhakikishe tumefahamu kila kitu”
akasema Job
“Nadhani sasa tayari umefahamu
ni kitu gani kinachoendelea japo Austin
atakaporejea atakueleza kwa undani
zaidi” akasema Job
“Ahsante Job nimeelewa.Mwili
wote umenisisimka baada ya kusikia
habari hizi.Ni habari nzito.Kwa hiki
ulichonieleza na kwa kile nilichokisikia
toka katika rekodi ile ya Irene
ninashawishika kuamini moja kwa
moja kwamba rais anahusika katika
mashambulio ya jana” akasema Daniel
“Hatuna uhakika bado japokuwa
kuna kila dalili kwamba anahusika hadi
hapo tutakapopata ushahidi wenye
kujitosheleza kumuhusisha rais na
mashambulio yale” akasema Job na
safari ikaendelea kimya kimya
“Yasmin anahitaji nini? Akauliza
Daniel
“Anahitaji kuelekea nje ya nchi
mahala ambako atakuwa mbali na
IS.Austin analishghulikia suala hilo na
pindi likikamilika basi Yasmin
atatuelekeza mahala ilipo hiyo hati ya
muungano” akasema Job na safari
ikaendelea kimya kimya.Mkononi
Daniel alikuwa na simu kubwa
iliyokuwa inaonyesha nukta nyekundu
inayotembea ambayo ni uelekeo wa
Irene .
“ Do you know this famous rich
guy, Dogo bill? Akauliza Job na Daniel
akastuka
“ Dogo Bill?!
“ Ndiyo.Unamfahamu?
“ Yule jamaa ninamfahamu kwa
sura tu.Nimekuwa nazisoma taarifa
zake katika magazeti lakini mimi na
yeye hatuna mahusiano yoyote ya
karibu na hatujawahi hata
kusalimiana.Kwa nini umeniuliza kama
ninamfahamu?
“ Ninahitaji kumpata Yule
jamaa.Yeye ana taarifa za mahala
walipo mke wangu na mwanangu.”
“ Mke wako na mwanao?akauliza
Daniel
“ Ndiyo.Kabla ya matatizo yale
kunikuta niligundua kwamba Dogo Bill
na mke wangu walikuwa na mahusiano
kwa hiyo baada ya matatizo yale
kutokea mke wangu akatoweka na
hajulikani alipo.Baada ya kumuhoji
Mukasha ambaye ni mtu wa karibu na
Dogo Bill alisema kwamba Bill hana
mahusiano na mke wangu bali kuna
mtu mwingine anaitwa Don ambaye
ndiye mwenye mahusiano na mke
wangu na Bill alitumika kama mshenga
tu.Baada ya suala la Irene kumalizika
nataka unisaidie katika suala
hili.Nataka nimpate dogo Bill ili
anieleze huyo Don ni nani na
nitawezaje kumpata mke na
mwanangu.” Akasema Job
“Kwani bado hujapata taarifa
kuhusu huyu jamaa dogo Bill? Daniel
akauliza
“Taarifa gani? Akauliza Job
“ taarifa zenye uhakika
zimesambaa katika mitandao kwamba
Bill ni mmoja wa watu waliofariki jana
katika shambulio hotelini”
“ What? Bill amefariki? Akauliza
Job kwa mshangao
“ Taarifa hizi zina ukweli ?
akauliza Job
“ Kweli kabisa na tayari
imethibitishwa na picha zimesambazwa
katika mitandao”
“ dah !! akasema Job na kushusha
pumzi.
“ Bill alikuwa ni tegemeo kubwa la
kufahamu mahala aliko mwanangu
Millen.I’ll have to find another way to
know who is that Don” akawaza Job
“ Daniel kitengo chenu cha siri
bado kipo chiniya ofisi ya rais? Akauliza
Job
“ Ndiyo.Bado tuko chini ya ofisi ya
rais ,kwa nini? Akauliza
“ Unamfahamu Wilson Mukasha?
Akauliza Job
“ Mukasha?! Daniel akauliza kwa
mshangao kidogo
“ Ndiyo.Unamfahamu? Akauliza
Job
“ Hapana simfahamu .Ni mara ya
kwanza kumsikia leo.Who is he? Daniel
akauliza
“ Huyu ni msaidizi wa rais.Ni msiri
wake mkubwa”akasema Job
“ Simfahamu kabisa mtu huyu”
akasema Job
“ kama Bill amefariki basi lazima
Mukasha apatikane.Huyu anaweza
akanisaidia kufahamu mahala alipo
mwanangu” akawaza Job
 
Back
Top Bottom