QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Jamani Naomba nitoe Ushauri kwa Sote tulokwisha Isoma

Haifai Kuwatamanisha watu humu kwa Kuwaelezea kilichomo ikiwa huna Uwezo wa Kuibandika hapa Basi Tutulie Mpaka ikishushwa humu na wenZetu wakaisoma Mpaka mwisho
Hapo sasa tutakuwa huru kuijadili na kuyajadili matukio yote yaliyomo

Vinginevyo tutakuwa na VIHERE HERE
Ndo mnunue sasa haiwezekani season zote uletewe humu ndani bila hata ya kumchangia mtunzi kununua hata moja huo ni ubahiri wa kiwango cha lami.
 
Ahsante Sana kwa wote mlioshiriki kuandaa hadithii hii mpk kutufikia, mkuu lege big up sana.....

Imeishia pazuriii siyo kwa couples zile...... Austin[emoji7] [emoji7] [emoji7]
 
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Jenerali Lameck Msuba akiwa
bado mjini Dodoma alipokea simu toka
kwa Silvanus Kiwembe akamtaarifu
kwamba vijana wake wameshambuliwa
na watu wasiowafahamu na kwa muda
wa daKika kadhaa walipoteza
mawasiliano na makao makuu kwa
hiyo hawakupata nafasi ya kufuatilia
kilichokuwa kinaendelea nyumbani
kwa Monica
“ Wilson,unataka kuniambia
mmeshindwa kuwafuatilia akina
Monica? Akauliza Lameck kwa ukali
“ Kama nilivyokwambia Jeneral
kwamba vijana wangu walishambuliwa
na watu wasiowafahamu
wakatawanyika na kupoteza
mawasiliano na makao makuu .Magari
na vifaa vyao vimeharibiwa vibaya kwa
risasi hivyo iliwabidi kukimbia
kunusuru maisha yao kwani kwa eneo
walilokuwepo hawakujua
wanashambuliwa toka
wapi.Waliporejea tayari Monica na
familia yake walikwisha
ondoka.Tulipowasiliana na vijana
waliokuwepo uwanja wa ndege
tulikuwa tumechelewa kwani tayari
Monica na watu wake walikwisha ingia
ndegeni na hivi tuongeavyo ndege
tayari imepaa kama dakika nne
zilizopita.Nimetumiwa picha za kamera
za usalama pale uwanjani na
nimejiridhisha kwamba mmoja wa
watu wale walioongozana na Monica ni
Yasmin Esfahani.”
“ Silva how could you miss her?
Huu ni uzembe mkubwa sana na laiti
ungekuwa karibu yangu ningekuchapa
kibao.Athari za hiki ulichokifanya ni
kubwa mno” Akasema Lameck na
kukata simu kwa hasira
“ Stupid !! akasema kwa hasira
.Akafikiri kidogo halafu akazitafuta
namba fulani katika simu yake na
kupiga akatoa maelekezo
“ Afande nahitaji kuhakikishiwa
kwa mara ya mwisho.Are you sure Sir?
Akauliza mtu aliyekuwa anazungumza
na Jenerali Lameck simuni
“ I’m sure.Take down that plane!!
Akasema Lameck kwa hasira.
“ I don’t have a choice.Yasmin
hatakiwi kutoka nje ya Tanzania.Ni
bora akafariki dunia kuliko kuvuka
mpaka na kutokomea na hati ya
muungano.Monica yuko ndani ya ile
ndege lazima naye ateketee hakuna
namna nyingine ya kufanya.Huyu
amekuwa ni kikwazo kikubwa sana
katika kufanikisha mipango yetu.Ni
kwa kupitia yeye Austin alimtorosha
Yasmin kutoka Zanzibar.Kama haitoshi
leo tena huyu huyu Monica anatumika
kumuondoa nchini Yasmin mtu
muhimu ambaye tunamuhitaji
mno.Austin na wenzake tayari
wanafahamu mambo mengi
waliyoambiwa na Yasmin kwa hiyo
itakuwa jambo zuri nao pia wakipotea
kabisa.Jambo hili litasababisha
mgogoro mkubwa kati yangu na rais
akigundua kwamba mimi ndiye
niliyetoa amri ndege aliyopanda
mwanae ilipuliwe na mgogoro
mwingine utakuwa nikati ya Tanzania
na Congo.Lolote litakalotokea
nitakabiliana nalo lakini ndege lazima
ilipuliwe.!! Akawaza .
Dakika kadhaa baada ya dege la
rais wa Congo kuondoka katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere,marubani waligundua kitu
kilichowastua.Ndege nne za vita
zilikuwa zinawaelekea na
kilichowastua zaidi ni mfumo wa
kutambua makombora ya adui
kuwaonyesha kwamba makombora
katika ndege zile yaliwekwa tayari kwa
kushambulia.

ENDELEA………………………….

Job na Daniel Swai walihakikisha
dege lililowabeba akina Austin limepaa
na kuondoka katika uwanja wa
kimataifa wa Julius nyerere bila
matatizo yoyote.
“ Thank you God” Akasema Job na
kumuelekeza Julieth aendeshe moja
kati ya magari mawili waliyotumia
kuendea pale uwanjani.Akampigia simu
Marcelo na kumfahamisha kwamba
zoezi limekamilika hivyo wanarejea
nyumbani.Job na Daniel wakaingia
 
Back
Top Bottom