SEHEMU YA 72
ufuatia agizo la rais waandishi wote
wa habari wakatolewa nje ,ukumbi
ukakaguliwa na wakaruhusiwa kuingia
mmoja mmoja huku wakikaguliwa .Baada
ya kuhakikisha ukumbi uko salama ,rais
akataarifiwa kuwa sasa anaweza
kulihutubia
taifa.Ernest
mkasa
akajitazama katika kioo akarekebisha tai
yake na kuvuta pumzi ndefu
“ I must do this.Litakalotokea na
litokee tu.” Akawaza Ernest akatoka mle
chumbani na kabla ya kuingia katika
chumba habari akaandaliwa muonekano
wake na alipokuwa tayari akaruhusiwa
kuingia katika chumba cha habari
“ Please help me God ! Help me do
the right thing for this country” akaomba
kimya kimya huku akitembea kuingia
katika chumba cha habari.karibu vituo
vyote vikubwa vya redio na televisheni
vilisimamisha matangazo yao kupisha
hotuba hii ya rais iliyokuwa inasubiriwa
sana na wananchi
Milango ya chumba cha habari
kilichokuwa na ulinzi mkali sana
ikafunguliwa na rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania akajitokea
akaenda
kuketi
katika
kiti
alichoandaliwa.Tofauti na ilivyozoeleka
kuwa hotuba ya rais huwa imeandaliwa
safari hii aliitoa karatasi mfukoni
aliyoiandaa yeye mwenyewe na kuanza
kuisoma
“ habari za usiku huu ndugu
watanzania wenzangu”
“ Awali ya yote ninapenda nichukue
nafasi hii kumshukuru mwenyezi Mungu
mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuja
mbele yenu na kuongea nanyi kuhusiana
na masuala kadhaa muhimu kwa taifa
letu.Kuna mambo kadhaa makubwa kwa
taifa letu ambayo yamenilazimu nije mbele
yenu leo”
akanyamaza halafu akaendelea
“ Kwa muda wa zaidi ya mwaka
mmoja sasa tumekuwa katika mchakato
wa kuandaa muswada wa haki za
binadamu .Uandaaji wa muswada huo
umekuwa na changamoto nyingi na kubwa
ni kupingwa kutoka kila kona na makundi
mbali mbali ya wananchi,viongozi wa dini
n.k.Ndani ya muswada huo kuna vipengele
kadhaa vinavyopigiwa kelele sana na
wananchi ambavyo vinatambua haki za
makundi ya watu wanaojihusisha na
mapenzi na ndoa za jinsia moja.Vile vile
kuna haki ya kutoa mimba pamoja na
mambo mengine kadhaa ambayo
yanakwenda kinyume kabisa na tamaduni
zetu na hata mafundisho ya dini zetu.”
Akanyamaza tena halafu akaendelea.
“ Kumekuwa na shinikizo kubwa
toka kwa nchi tajiri , zikizitaka nchi zote
za afrika kuhakikisha kwamba zinapitisha
sheria za kutambua haki kadhaa za
binadamu na hapa wanalenga makundi
hayo niliyokwisha yaeleza.Nchi nyingi za
Afrika tayari zimekwisha pitisha sheria
hiyo na chache ikiwemo Tanzania bado
hatujafanya hivyo japokuwa sisi tulikuwa
katika mchakato wa kuupeleka bungeni
muswada wa sheria hiyo ili kutimiza
matakwa hayo ya nchi tajiri.Mchakato wa
kuandaa muswada huo umekamilika na
unategemewa kuwasilishwa katika kikao
kijacho cha bunge lakini kumekuwa na
shinikizo kubwa toka kwa wanachi,wazee
kwa vijana,wake kwa waume wakipinga
muswada huo kupelekwa bungeni.Katika
kila mkoa kumeanzishwa kampeni kubwa
za kupinga muswada huu na tayari
makundi ya watu wameanza kujiandikisha