QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Watabiri wa kujitolea wameanza kuwa wengi hapa ni kweli yasije tokea ya peniela watu wakaanza kukana ubatizo wao.
 
Dah!huyu cjui ananifahamu...maana sifa zote alizonazo austin ndo nlizonazo mimi,yan vile vile aisee.
 
SEHEMU YA 112




kumtafuta.Inaonyesha wazi hataki nije
Dar es salaam kwani toka nilipomueleza
nia yangu ya kuja Dar amekuwa akitoa
kisingizio cha usalama.Kuna kitu gani
Austin hataki nikijue? Ninahisi lazima
lazima atakuwa na mwanamke huku
Dar.Nitajua tu kinachoendelea na
ambacho hataki nikifahamu” akawaza
Maria akiwa garini akipelekwa hotelini
“ Dar es salaam imebadilika
sana.Limekuwa jiji la kisasa na la
kupendeza.Serikali ya Tanzania inastahili
pongezi kwa kulifanya jiji kuu la
kibiashara Tanzania kuwa zuri namna hii”
akaendelea kuwaza Monica huku
akitazama nje kushuhudia uzuri wa jiji la
Dar es salaam.
*********************
Tayari kiza kimeanza kutanda
angani ,rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Ernest Mkasa alipowasili katika
hoteli yake ya kifahari ya White Panda
kama ilivyo ada yake kufika hapa kila jioni
kwa ajili ya kupumzika, kupata kinywaji
pamoja na kukutana na watu mbali mbali
kwa faragha.Kwa siku nzima alikuwa
amejifungia ofisini kwake na hakutaka
kuonana na mtu yeyote.Alikuwa na kazi
ngumu ya kuchambua baadhi ya watu
anaodhani wanaweza kumfaa katika
baraza lake jipya la mawaziri
Alipofika hotelini akapitiliza hadi
katika chumba chake na mtu wa kwanza
kuwa na maongezi naye usiku huu alikuwa
ni Mukasha.
“ Mukasha nini kinaendelea huko
mtaani? Watu wanasemaje kuhusu
maamuzi niliyoyachukua? Akaanzisha
maongezi Ernest
“ Kuna mjadala mkali sana
mheshimiwa rais.Kila mahala ukipita leo
hii habari kubwa ni kuhusiana na
maamuzi uliyoyafanya.Ni maamuzi
makubwa
ambayo
hakuna
aliyeyatarajia.Wengi wanapongeza kwa
hiki ulichokifanya na wanakuunga mkono
lakini wengi wanahoji kutaka kufahamu
sababu ya wewe kufanya maamuzi
yale.Hilo limekoleza mjadala na kila
mmoja anaongea analolifahamu lakini
ukweli wote unaujua wewe mheshimiwa
rais” akasema Mukasha.Ernest akanywa
mvinyo akakohoa kidogo na kusema
“Ni kweli Mukasha.Wananchi
hawajui sababu ya mimi kuchukua
maamuzi yale makubwa.Kuvunja baraza la
mawaziri si jambo dogo.Ni jambo zito
lakini nililazimika kufanya hivyo
.Mukasha wewe ni mmoja kati ya watu
wachache ninaowaamini sana na ninataka
nikiri kwako kwamba kuna jambo kubwa
linaloendelea ndani ya serikali” akasema
Ernest akanywa tena funda mbili za
mvinyo na kuendelea
“Kuna nguvu kubwa hivi sasa
inayotaka kuibadili dunia”
“ Nguvu kubwa? Ipi hiyo? Kubadili
dunia kivipi mheshimiwa rais? Akauliza
Mukasha
“ Ni hadithi ndefu lakini nitakueleza
kwa ufupi kwa kuwa wewe ni mtu wangu
wa muhimu sana” akanyamaza
akamtazama Mukasha halafu akaendelea
 
SEHEMU YA 113


Kuna kiongozi mmoja wa kanisa
aliwahi kuasi kanisa lake kwa kuanzisha
vuguvugu la kudai mabadiliko katika
ndani ya kanisa, mabadliko ambayo
hayaendani na imani ya kanisa
hilo.Kiongozi mkuu wa kanisa hilo kwa
wakati huo hakupendezwa na kitendo cha
kiongozi Yule kutaka kuanzisha uasi ndani
ya kanisa hivyo akamvua daraja na
kumfukuza katika kanisa hilo.Baada ya
kufukuzwa akaanzisha kundi la Alberto
ambalo ndilo linataka kuibadili dunia na
kuyafanya mataifa yote yafuate imani
yao.Kundi hili lenye makao yake makuu
nchini Italia limekuwa likipata nguvu kila
uchao na kusambaa sehemu mbali mbali
duniani.Kitu kimoja ambacho unapaswa
kukifahamu ni kwamba kundi hili
linaongozwa na nguvu za giza na mambo
ambayo wanayashabikia na kutaka dunia
nzima iyafuate ni yale ambayo
yanakwenda kinyume na Mungu muumba
wa mbingu na nchi.Baadhi ya mambo hayo
ni mahusiano na ndoa za jinsia moja,kutoa
mimba,uhuru wa ngono kwa vijana
wadogo n.k.” Ernest akanyamaza na
kumtazama Mukasha kisha akaendelea
“ Ili kufanikisha mipango yao
,wamekuwa wakiwatumia wakuu wa nchi
kuhalalisha mambo hayo katika nchi
zao.Walianza kuotesha mizizi katika
mataifa makubwa ya Amerika na Ulaya na
wamefanikiwa kiasi kikubwa sana huko
kwani tayari nchi nyingi zimeyapokea na
kuyakubali mambo hayo na kuyashabikia
sana.Kwa kuyatumia mataifa hayo
makubwa wameweza kuyafikia mabara
mengine na kwa sasa wamefika bara la
Afrika.Walilifanya bara hili kuwa la
mwisho kutokana na nchi zake nyingi
kuwa masikini na kutegemea sana
misaada na mikopo toka mataifa
makubwa kwa hiyo kazi ya kuotesha
mizizi katika nchi za Afrika si ngumu.Hadi
hivi sasa sehemu kubwa ya nchi za Afrika
wameyakubali mashari yaliyotolewa na
nchi wafadhili ya kutunga sheria
kukubaliana na mapenzi ya jinsia
moja,utoaji mimba n.k.Nchi pekee ambayo
wamepata ugumu kuingia ilikuwa
Tanzania lakini baadae walifanikiwa
kuingia na kuotesha mizizi na mimi ndiye
mzizi mkuu”
Kauli ile ya Ernest ikamfanya
Mukasha ainuke na kumtazama Ernest
kwa macho ya woga
“ Mr President you are one of them??
Akauliza kwa mshangao.Ernest akavuta
pumzi ndefu na kusema
“ Mimi si mmoja wao lakini ni
sehemu yao.They are using me.......”
“ Oh my God !!! akasema Mukasha
“ Alberto’s ....” Ernest akaendelea
“ Ndio walioniweka mimi
madarakani.Walitumia nguvu yao
nikachaguliwa kugombea urais na
kuibuka
mshindi
kwa
kura
nyingi.Walinipa nafasi hiyo kubwa kwa
sharti moja kwamba wataitumia ofisi
yangu katika kufanikisha mambo
yao.Baada ya kuupata mzizi mkuu
walianza kusambaza miziz midogo midogo
katika sehemu mbali mbali ili
kutengeneza
mmea
wenye
afya.Walichokifanya kwanza ni kuliteka
bunge.Asilimia kubwa ya wabunge ni
wafuasi wao waligharamia kampeni zao
na kuwasaidia kushinda na kila mwezi
kuna kiasi kikubwa cha pesa wanakipokea
kwa siri kutoka kwa Alberto’s.Lengo la
 
SEHEMU YA 114



kuliteka kwanza bunge ni kuweka urahisi
wa kupitisha miswada mbali mbali
itakayowasilishwa mbele yao.Nilimteua
mgombea mwenza ambaye ni makamu wa
rais kwa maelekezo yao,waziri mkuu pia
walinipa maelekezo wao,na haijaishia
hapo bali hata mawaziri wote
nimewachagua kwa maelekezo yao.Kwa
ufupi ni kwamba Alberto’s wameishika
nchi hii na wanaipeleka namna
watakavyo.Mimi niko kama kivuli tu lakini
nchi inaongozwa na watu wengine
kabisa.Kuna baraza dogo la vingozi wa juu
wa Alberto hapa nchini ndio wanaofanya
kazi ya kuongoza nchi na mimi
ninatekeleza maagizo na maelekezo
yao.Alberto’s wana nguvu na kwa sasa
wanamiliki robo tatu ya dunia”
akanyamaza akanywa funda la mvinyo na
kuendelea
“ Uliandaliwa muswada wa sheria
uliotazamiwa kupelekwa bungeni ambao
unazitambua haki za wapenzi wa jinsia
moja.Endapo ungefikishwa bungeni na
kupitishwa basi mambo hayo
yangehalalishwa hapa nchini lakini kabla
hilo halijafanyika nimewahi na kuufutilia
mbali muswada huo ,na kama haitoshi
nikalivunja baraza la mawaziri,nikamteua
pia mkuu mpya wa majeshi” akasema
Ernest na ukimya ukatanda mle ndani
baada ya muda Mukasha akauliza
“ Nini hasa kilipelekea ukachukua
maamuzi hayo ya kuwageuka watu hatari
kama hawa ambao ndio waliokuweka
madarakani?Huwaogopi?
Ernest akatoa mkebe katika mfuko
wa koti akatoa sigara kubwa akaiwasha
akavuta mikupuo kadhaa na kusema
“ Mke wangu Agatha ni mmoja wa
viongozi wa Alberto’s hapa Tanzania”
“ What ??!!..Mukasha akazidi
kushangaa
“ Even First lady??? Akauliza
“ Yes.She’s one of them,” akajibu
Ernest na kuvuta tena mkupuo mmoja
akapuliza moshi na kusema
“ yeye ndiye aliyenishawishi mimi
nikubaliane nao niwe rais.Kama
nilivyokueleza awali kwama hawa jamaa
wanatumia nguvu za giza kufanya mambo
yao kwa hiyo Agatha aliwatoa kafara
watoto wetu watatu ili kunishikiniza
nikubaliane nao . Baada ya kuwazika
wanangu watatu kwa siku moja sikuweza
tena kupata mtoto mwingine.” Akanyama
na kuvuta tena sigara akanywa funda moja
la mvinyo
“ So sorry for that Mr
president.Sikujua kama umepitia mambo
magumu namna hiyo” akasema Mukasha
“ Ni kweli Mukasha,nimepitia
mambo mengi magumu latika kipindi hiki
cha urais wangu.Kwa muda mrefu
nimekuwa nikitafuta upenyo wa
kuniwezesha kuachana na watu hawa
lakini nilishindwa .Hivi majuzi niligundua
kwamba enzi za ujana wangu niliwahi
kuwa na mahusiano na mwanamke mmoja
na katika mahusiano hayo tulibahatika
kuwa na mtoto ingawa mwanamke huyo
alinificha hadi hivi majuzi alipoamua kuja
kunieleza ukweli.Nilifurah mno kwani
niliamini ningekufa bila kuwa na mrithi
wa utajiri wangu.Japokuwa hizi zilikuwa
ni taarifa njema mno kwangu lakini
sikutaka kuamini haraka haraka na ndiyo
maana nikam tafuta Austin li aweze
kunisaidia kupata sampuli toka kwa huyo
mtoto kwa dhumuni la kufanya kipimo cha
vinasaba kubaini kama kweli mtoto huyo
 
Ernest asingemueleza mukasha kuhusu Austin. Ni mapema mno wengine hawana siri.lakini lege unarusha fupi fupi.na shuhuli bado ndefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…