QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 106


ungu wangu !! akasema Monica
kwa mshangao
“ Polisi wametoa taarifa gani hadi
hivi sasa? Akauliza
“ Mpaka sasa jeshi la polisi
wanaendelea na uchunguzi wao na bado
hawajatoa taarifa yoyote kuhusiana na
tukio hilo.Familia yake wako kimya nao
wanasubiri taarifa toka polisi.Nimeongea
na Julieth asubuhi ya leo na ameniambia
kwamba mpaa sasa hawana taarifa zozote
kuhusiana na Marcelo.Hilo ndilo jambo
lililotokea wakati ukiwa safarini
Monica.By the way nimefurahi umerudi
salama Monica.Karibu tena nyumbani.”
“ Ahsante Daniel.Nikipata nafasi
nitakutafuta kuna mambo ambayo nahitaji
kuzungumza nawe” akasema Monica
akaagana na Daniel kisha akamgeukia
Linah
“ Kuna tatizo lolote Monica?
Nimesikia unazungumzia ripoti ya jeshi la
polisi” akauliza LInah
“ Kuna rafiki yangu mmoja alipigwa
risasi hivyo nilitaka kujua kuhusu ripoti
ya uchunguzi ya jeshi la polisi kama
wamefanikiwa kuwabaini waliofanya
kitendo hicho .Tuachane na hayo ,mambo
yamekwendaje kwa hizi siku mbili
ambazo sikuwepo? Akauliza Monica
“ Mambo yamekwenda vizuri hakuna
tatizo lolote lililojitokeza.Hata hivyo kuna
mgeni alikuja kukutafuta leo asubuhi.Gosh
! he’s super handsome.Kijana huyo
ameacha gumzo pale ofisini kwani kila
mtu anamzungumzia.” Akasema Linah
huku akitabasamu
“ Anaitwa nani huyo kijana mzuri
?Anahitaji nini? Akauliza Monica huku
akitabasamu
“ Anaitwa Austin .Ni mtanzania
mwenye makazi yake afrika ya kusini
.Monica huyo kijana ni mzuri mno.”
“ Mhh ! leo Linah umemsifia
mwanaume basi lazima atakuwa ni kijana
mzuri haswa.Alikuwa na shida gani na
mimi?
“ Monica lazima nimsifie naamini
hata wewe ukimuona utakubaliana nami
kwamba Austin ni kijana wa kipekee
sana.Ana sura nzuri ya kuvutia,ana umbo
zuri la kiuana mitindo.Ana sautio nzuri, ni
mcheshi,mstaarabu,dah ! ana sifa nyingi
Yule kijana itoshe tu kusema ni wa
kipekee” akasema Linah na Monica
akaangua kicheko kisha akasema
“ Mhh ! Linah usiniambie tayari
umekufa kwa huyo kijana kwa sababu
namna unavyomsifia dah ! “
“ Monica wewe ni msiri wangu na
sijawahi
kukuficha
jambo
lolote.Nakuambia ukweli nilipomuona tu
Austin nilihisi kama moyo wangu unataka
kusimama.Nilihisi kama ninataka
kupagawa
kwa
msisimko
nilioupata.Monica usinione mjinga lakini
naomba niwe wazi kwamba Yule kijana
amenitikisa na nimetokea kumpenda.”
Akasema LInah
“ C’mon baby girl,give me a break
usiseme tayari umempenda mtu ambaye
umekutana naye kwa dakika kumi tu”
akasema Monica
“ It’s true Monica.Hata mimi
mwenyewe najishangaa kwa hali hii
iliyonitokea.”
Monica akamtazama Linah kisha
akatabasamu.
“ Austin alikuwa anahitaji nini?
“ Austin ni mkurugenzi wa kampuni
ya utalii inaitwa AA safaris ambao
 
SEHEMU YA 107


wamekuwa wakifadhili miradi mbali
mbali ya kijamii katika sehemu zile mbali
mbali.Kwa sasa wana mpango wa
kufungua ofisi nchini Tanzania kwa hiyo
wanataka kushiriki pia katika kufadhili
miradi kadhaa ya kijamii.AA safaris
wanataka kushirikiana na sisi katika
jambo hilo na hicho ndicho kilichomleta
Austin ofisini kwetu” akasema Linah
“ Ni jambo zuri sana.Mliafikiana
mambo gani?
“ Hatukuafikiana chochote kuhusu
suala hilo nilimueleza kwamba mtaongea
kwa kirefu utakaporejea.Aliahidi kufika
ofisini kila siku kufahamu kama
umerudi”
“ Sawa Linah endapo mtafanikiwa
kuwasiliana mueleze nimekwisha rejea na
aje tuonane”
“ It’s your turn now.Nieleze ulikuwa
wapi na ikawaje ukarudi na ndege ya rais
wa Congo? Akauliza Linah kama kawaida
yae Monica akatabasamu na kusema
“ Ni hadithi ndefu kidogo lakini kama
nilivyokuahidi kwamba nitakueleza kila
kitu ila kwa sasa nitakupa kwa kifupi tu”
akasema Monica akanyamaza kidogo
halafu akasema
“ Nilikwenda Congo DRC.Nilialikwa
na rais David Zumo kuhudhuria
kongamano la umoja wa vijana wa Congo”
“ Hebu subiri kwanza Monica.Wewe
na David mmefahamiana kwa muda gani?
Akauliza Linah
“ Mimi na David tumefahamiana siku
ya zile mbio.Kama unakumbuka wewe
ndiye uliyempokea Jean Pierre Muyeye
msaidizi wa David Zumo.Siku ile alitumwa
na David kuniletea ujumbe kuwa David
anahitaji kuonana nami kwa sababu
amevutiwa na juhudi zangu za kusaidia
jamii masikini.Nilikwenda kuonana naye
hotelini kwake tukaongea mambo mengi
na
akanipa
mchango
wake
mkubwa.Alipoondoka kurudi Congo
akanialika
niende
kuhuduhuria
kongamano la vijana wa Congo .Alituma
ndege yake binafsi kuja kunichukua na
kunipeleka Congo.Nilipokewa vizuri na
mke wa rais wa Congo aitwaye Pauline
Zumo.Nilipelekwa katika jumba kubwa la
kifahari.Ndani ya jumba hilo hadi vijiko ni
vya dhahabu.Nashindwa nikuelezeaje
uzuri wa jumba hilo na maisha ya kifahari
niliyoshi Congo.Linah katika dunia hii
kuna watu wanaishi kama vile wako
peponi.Kila nilipopita magari yaliwekwa
pembeni .Sikuwahi kuota hata siku moja
kama ningeweza kupewa heshima kubwa
kiasi kile.Anyway tuachane na hayo
maisha ya kifahari,kuna jambo kubwa
ambalo David Zumo aliniitia Congo
ukiacha hilo ” akasema Monica
“ Jambo gani hilo Monica?
Monica akamtazama Linah kwa
sekunde kadhaa ,akatabasamu na kusema
“ David Zumo anataka kunioa”
“ What ?? akasema Linah kwa
mstuko mkubwa na kusimama akajishika
kiuno
“ David Zumo anataka kufanya
nini?!!
“ David Zumo anataka kunioa “
Linah akamtazama Monica kwa
macho makali na kusema
“ Tafadhali Monica usifanye utani
katika jambo kubwa kama hilo “
“Siwezi kuweka utani Linah katika
suala kama hili.Ni kweli ninachokwambia”
 
SEHEMU YA 108



inah akashusha pumzi ndefu na
kuendelea kumtazama Monica kisha
akasema taratibu
“ What a suprise”
“ Ni kweli Linah jambo hili
litawashangaza wengi “
“ Monica mimi sishangazwi na David
kutangaza ndoa nawe bali nashangazwa
na muda mfupi toka mlipofahamiana.”
“ Uko sahihi Linah.Muda umekuwa
mfupi sana ambao mimi na David
tumekutana hadi kufikia hatua ya David
kutangaza kutaka kunioa”
“ kwa hiyo uelipokeaje ombi la
david? Akaulzia Linah.Bila kupepesa
macho Monica akasema
“ I said yes!!
Linah akainuka na kumkumbatia
Monica
“ Oh ! Monica thank you.You did
good.Hata kama ningekuwa mimi
nisingekubali kutamka hapana kwa mtu
kama Yule tajiri namba moja
Afrika.Monica una bahati ya kupata fursa
nyingi na unajua kuzitumia .Hii ni fursa
kubwa umeipata na umeitumia vyema.”
Akasema LInah
“ Linah hii si fursa kama
unavyodhani.hya ni maamuzi ya kutoka
moyoni.kwa hiari yangu nimekubali
kuolewa na David na si kwa sababu ya
utajiri wake.Ni kweli ni muda mfupi sana
tumkutana na kufikia makubaliano ya
kufunga ndoa lakini hicho si kigezo.hata
masaa mawili yanatosha sana kutangaza
ndoa.Ni kama wewe ulivyochanganyikiwa
na Austin baada ya kuonana naye kwa
muda usiozidi nusu saa.Tuachane na hilo
suala tutaliongelea siku nyingine kwani
nahitaji kupumzika “ akasema Monica
wakaagana Linah akaondoka
“ Suala la ndoa yangu na David
litatengenza vichwa vya habari kwa muda
mrefu pindi likiwekwa wazi lakini sintajali
chochote.Nimekwisha amua kuolewa na
David Zumo na hakuna wa kunibadilisha
mawazo.Kwa sasa ninachotakiwa kufanya
ni kujua mahala alipo Marcelo ili
nikamjulie hali.Ngoja niwasiliane na David
nimtaarifu kuwa nimefika salama na
nimuulize mahala alipo Marcelo”
Monica akachukua simu akaandika
namba za David Zumo akapimpigia
“ Hallow malaika wangu habari gani
Monica? Natumai umefika salama Dar es
salaam”

Nimefika
salama
David.Nimekupigia kukushukuru mno
wewe na mkeo Pauline kwa ukarimu wenu
mkubwa.Mungu amewajalia mioyo iliyojaa
upendo wa aina yake .Sipati neno zuri la
kuwashukuru
kwa
namna
mlivyonipokea.Nazidi kuwaombea kwa
Mungu aendelee kuwaongoza na kuwapa
mafanikio mengi” akasema Monica
“ Ahsante sana Monica malkia
mtarajiwa wa Congo.Halafu kuna kitu
nilisahahu kukueleza .Ninafikiria
kukuletea walinzi nane kutoka Israel kwa
ajili ya kukulinda.Nataka uwe salama
malkia wangu.” Akasema David
“ David ahsante sana kwa kunijali na
kuthamini usalama wangu lakini kwa
wakati huu nadhani bado sihitaji ulinzi
wowote. Huku kwetu amani imetawala na
kingine ni kwamba mimi ni mtu wa watu
kwa hiyo hata kama nina mahusiano na
rais au mfalme sitaki kubadlika.Nataka
niendelee kuwa mtu wa kawaida kwa hiyo
 
SEHEMU YA 109



David naomba usisumbuke kuhusu suala
hilo la ulinzi”
“ Monica mpenzi wangu,wewe ni
malkia mtarajiwa wa Congo kwa hiyo
unahitaji ulinzi wa hali ya juu lakini kama
una uhakika uko salama hakuna tatizo”
“ Ahsante David kwa kunielewa”
“ Usijali Monica ,siku zote neno lako
ni amri kwangu.Halafu kuna jambo
lingine” akasema David na kunyamaza
kidogo
“ Jambo gani David? Monica
akaulliza.David akasikika simuni akivuta
pumzi ndefu kisha akasema
“ Wakati akikusindikiza uwanja wa
ndege ,Pauline kuna jambo alikueleza”
“ Ndiyo David.Kuna jambo alinieleza
limenistua na kunitoa machozi mengi”
“ Ndiyo hivyo Monica.Hilo ni jambo
ambalo tunajitahidi kukabiliana nalo.Si
jambo jepesi kwangu lakini naamini
utakuwa pamoja nami kwani nahitaji
nguvu ya kulikabili suala hili.”
“ David niko pamoja nawe katika
jambo hili lakini nakuomba tusikate
tamaa.Tunatakiwa
kufanya
kila
linalowezekana kuhakikisha Pauline
anapona.Ni mapema mno kukata tamaa”
“ Monica suala hili la Pauline ni suala
ambalo tumeshughulika nalo kwa muda
mrefu na tumejaribu kila tiba bila
mafanikio.Laiti kama kuna mahali
ningeweza kupata tiba kwa ajili ya
Pauline,niko tayari kutumia utajiri wangu
wote kupata tiba hiyo lakini hakuna tiba
hiyo.Madaktari wamekwisha kata tamaa
na wanaamini kuwa Monica hawezi
kupona tena.Tumeliweka suala hili katika
mikono ya Mungu .Ni yeye pekee atakaye
amua hatima ya Pauline.Hata hivyo
atafanyiwa upasuaji wa mwisho ingawa
madaktari wana wasi wasi mkubwa
kwamba yawezekana Pauline asiamke
tena na huo ukawa ndio mwisho
wake.Kwa hiyo Monica lazima tujiweke
tayari kwa lolote litakalotokea.”akasema
David
“Nimekuelewa David,kitu cha
muhimu kwa sasa ni kuzidisha
maombi.Tukiachana na suala hilo David
ninataka kushughulikia suala la Marcelo
kwa hiyo nahitaji kufahamu mahala alipo
ili nikamchukue na kumpeleka sehemu
salama zaidi.unaweza kunisaidia
kumuuliza rais Ernest mahala alipo
Marcelo?”
“Sawa Monica,nitaongea naye
anielekeze mahala aliko hifadhiwa
Marcelo halafu nitakujulisha”Akasema
David,wakaongea
kidogo
kisha
wakaagana.
“Huyu Marcelo ni nani kwa
monica ?anaonekana ni mtu mwenye
umuhimu mkubwa sana kwake hadi
akafikia hatua ya kutaka kuhatarisha
maisha yake kumuokoa dhidi ya watu
wanaotaka kumuua.Inawezekana wakawa
na mahusiano ya kimapenzi?”akawaza
David zumo baada ya kumaliza kuongea
na Monica .
“ Kuna uwezekano mkubwa
Marcelo na Monica wakawa na mahusiano
ya kimapenzi .Japokuwa nimemkuta
Monica akiwa bado bikira lakini
nashawishika kuamini kwamba lazima
ana mahusiano na Marcelo.Hainingii
akilini eti mwanamke mzuri kama Yule
asiwe na mpenzi.Ninampenda sana Monica
na kwa ajili yake niko tayari kufanya
jambo lolote hata kama ni baya na kwa
 
SEHEMU YA 110



hiyo nitahakikisha Monica na Marcelo
hawaonani tena.Nitaongea na rais wa
Tanzania na kumsisitizia Marcelo
aendelee kuhifadhiwa mahala salama na
ikiwezekana nitafanya mpango wa
kumuhamisha na kumleta Congo
atahifadhiwa mahala ambako hatatoka
hadi kifo chake au kama nitalazimika
kumtoa uhai nitafanya hivyo.Kwa ajili ya
Monica nitajifunza kuwa mkatili.Monica ni
wangu peke yangu”akawaza David na
kumpigia simu Ernest Mkasa rais wa
jamuhuri ya muungano wa Tanzania
wakaongea akamuomba Ernest eandelee
kumuhifadhi Marcelo mahlala alikofichwa
na asiruhusiwe kutoka hadi hapo
atakapotoa
maelekezo
mengine.Alipomaliza kuzungumza na
Ernest Mkasa akampigia Monica
“Monica nimezungumza na rais wa
Tanzania amesema kwamba atanipa
maelekezo baadae ya mahala alipo
Marcelo ili umtembelee”
“ Ahsante sana David kwa msaada
wako huu mkubwa” akasema Monica
wakaagana tena
“ Ngoja nipumzike kidogo nahisi
uchovu
mwingi.Sintakwenda
kuwatembela wazazi leo nataka
nipumzike hadi kesho asubuhi ndipo
nitawatembelea” akawaza Monica.
*******************
Saa tisa na nusu za alasiri ndege ya
shirika la ndege la Emirates iliwasili
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius nyerere jijni Dar es salaam ikitokea
Dubai na miongoni kwa abiria walioshuka
katika ndege hiyo ni Maria mpenzi wa
Austin
Alikamilisha taratibu za uhamiaji
hapo uwanjani kisha akatoka nje ya
uwanja na kwa kuwa hakukuwa na mtu
yeyote aliyekuja kumpokea uwanjani
ikamlazimu akodishe teksi kuelekea
hotelini
“ Austin yuko ndani ya jiji hili na
ndiye aliyepaswa kuja kunipokea hapa
uwanjani leo lakini toka jana hakunitafuta
kama
tulivyokuwa
tumekubaliana.Ameniumiza sana lakini
kwa kuwa ninampenda sina budi
kumtafuta.Inaonyesha wazi hataki nije
Dar es salaam kwani toka nilipomueleza
nia yangu ya kuja Dar amekuwa akitoa
kisingizio cha usalama.Kuna kitu gani
Austin hataki nikijue? Ninahisi lazima
lazima atakuwa na mwanamke huku
Dar.Nitajua tu kinachoendelea na
ambacho hataki nikifahamu” akawaza
Maria akiwa garini akipelekwa hotelini
“ Dar es salaam imebadilika
sana.Limekuwa jiji la kisasa na la
kupendeza.Serikali ya Tanzania inastahili
pongezi kwa kulifanya jiji kuu la
kibiashara Tanzania kuwa zuri namna hii”
akaendelea kuwaza Monica huku
akitazama nje kushuhudia uzuri wa jiji la
Dar es salaam.
 
shikrani..LEGE...[emoji1] [emoji1] ..kwa episode zenye mfumo wa andunje...!!...
huko mbeleni hakuna ndoa kati ya zumo na monnie.....kwa mawazo ya kijinga aliyojiwazisha...!!.kitakachofuata ni butwaa la monnie atalapokutana na marcelo kwa austin.....
 
shikrani..LEGE...[emoji1] [emoji1] ..kwa episode zenye mfumo wa andunje...!!...
huko mbeleni hakuna ndoa kati ya zumo na monnie.....kwa mawazo ya kijinga aliyojiwazisha...!!.kitakachofuata ni butwaa la monnie atalapokutana na marcelo kwa austin.....
Umetabiri vyema mkuu
 
Back
Top Bottom