SEHEMU YA 109
David naomba usisumbuke kuhusu suala
hilo la ulinzi”
“ Monica mpenzi wangu,wewe ni
malkia mtarajiwa wa Congo kwa hiyo
unahitaji ulinzi wa hali ya juu lakini kama
una uhakika uko salama hakuna tatizo”
“ Ahsante David kwa kunielewa”
“ Usijali Monica ,siku zote neno lako
ni amri kwangu.Halafu kuna jambo
lingine” akasema David na kunyamaza
kidogo
“ Jambo gani David? Monica
akaulliza.David akasikika simuni akivuta
pumzi ndefu kisha akasema
“ Wakati akikusindikiza uwanja wa
ndege ,Pauline kuna jambo alikueleza”
“ Ndiyo David.Kuna jambo alinieleza
limenistua na kunitoa machozi mengi”
“ Ndiyo hivyo Monica.Hilo ni jambo
ambalo tunajitahidi kukabiliana nalo.Si
jambo jepesi kwangu lakini naamini
utakuwa pamoja nami kwani nahitaji
nguvu ya kulikabili suala hili.”
“ David niko pamoja nawe katika
jambo hili lakini nakuomba tusikate
tamaa.Tunatakiwa
kufanya
kila
linalowezekana kuhakikisha Pauline
anapona.Ni mapema mno kukata tamaa”
“ Monica suala hili la Pauline ni suala
ambalo tumeshughulika nalo kwa muda
mrefu na tumejaribu kila tiba bila
mafanikio.Laiti kama kuna mahali
ningeweza kupata tiba kwa ajili ya
Pauline,niko tayari kutumia utajiri wangu
wote kupata tiba hiyo lakini hakuna tiba
hiyo.Madaktari wamekwisha kata tamaa
na wanaamini kuwa Monica hawezi
kupona tena.Tumeliweka suala hili katika
mikono ya Mungu .Ni yeye pekee atakaye
amua hatima ya Pauline.Hata hivyo
atafanyiwa upasuaji wa mwisho ingawa
madaktari wana wasi wasi mkubwa
kwamba yawezekana Pauline asiamke
tena na huo ukawa ndio mwisho
wake.Kwa hiyo Monica lazima tujiweke
tayari kwa lolote litakalotokea.”akasema
David
“Nimekuelewa David,kitu cha
muhimu kwa sasa ni kuzidisha
maombi.Tukiachana na suala hilo David
ninataka kushughulikia suala la Marcelo
kwa hiyo nahitaji kufahamu mahala alipo
ili nikamchukue na kumpeleka sehemu
salama zaidi.unaweza kunisaidia
kumuuliza rais Ernest mahala alipo
Marcelo?”
“Sawa Monica,nitaongea naye
anielekeze mahala aliko hifadhiwa
Marcelo halafu nitakujulisha”Akasema
David,wakaongea
kidogo
kisha
wakaagana.
“Huyu Marcelo ni nani kwa
monica ?anaonekana ni mtu mwenye
umuhimu mkubwa sana kwake hadi
akafikia hatua ya kutaka kuhatarisha
maisha yake kumuokoa dhidi ya watu
wanaotaka kumuua.Inawezekana wakawa
na mahusiano ya kimapenzi?”akawaza
David zumo baada ya kumaliza kuongea
na Monica .
“ Kuna uwezekano mkubwa
Marcelo na Monica wakawa na mahusiano
ya kimapenzi .Japokuwa nimemkuta
Monica akiwa bado bikira lakini
nashawishika kuamini kwamba lazima
ana mahusiano na Marcelo.Hainingii
akilini eti mwanamke mzuri kama Yule
asiwe na mpenzi.Ninampenda sana Monica
na kwa ajili yake niko tayari kufanya
jambo lolote hata kama ni baya na kwa