SEHEMU YA 114
kuliteka kwanza bunge ni kuweka urahisi
wa kupitisha miswada mbali mbali
itakayowasilishwa mbele yao.Nilimteua
mgombea mwenza ambaye ni makamu wa
rais kwa maelekezo yao,waziri mkuu pia
walinipa maelekezo wao,na haijaishia
hapo bali hata mawaziri wote
nimewachagua kwa maelekezo yao.Kwa
ufupi ni kwamba Alberto’s wameishika
nchi hii na wanaipeleka namna
watakavyo.Mimi niko kama kivuli tu lakini
nchi inaongozwa na watu wengine
kabisa.Kuna baraza dogo la vingozi wa juu
wa Alberto hapa nchini ndio wanaofanya
kazi ya kuongoza nchi na mimi
ninatekeleza maagizo na maelekezo
yao.Alberto’s wana nguvu na kwa sasa
wanamiliki robo tatu ya dunia”
akanyamaza akanywa funda la mvinyo na
kuendelea
“ Uliandaliwa muswada wa sheria
uliotazamiwa kupelekwa bungeni ambao
unazitambua haki za wapenzi wa jinsia
moja.Endapo ungefikishwa bungeni na
kupitishwa basi mambo hayo
yangehalalishwa hapa nchini lakini kabla
hilo halijafanyika nimewahi na kuufutilia
mbali muswada huo ,na kama haitoshi
nikalivunja baraza la mawaziri,nikamteua
pia mkuu mpya wa majeshi” akasema
Ernest na ukimya ukatanda mle ndani
baada ya muda Mukasha akauliza
“ Nini hasa kilipelekea ukachukua
maamuzi hayo ya kuwageuka watu hatari
kama hawa ambao ndio waliokuweka
madarakani?Huwaogopi?
Ernest akatoa mkebe katika mfuko
wa koti akatoa sigara kubwa akaiwasha
akavuta mikupuo kadhaa na kusema
“ Mke wangu Agatha ni mmoja wa
viongozi wa Alberto’s hapa Tanzania”
“ What ??!!..Mukasha akazidi
kushangaa
“ Even First lady??? Akauliza
“ Yes.She’s one of them,” akajibu
Ernest na kuvuta tena mkupuo mmoja
akapuliza moshi na kusema
“ yeye ndiye aliyenishawishi mimi
nikubaliane nao niwe rais.Kama
nilivyokueleza awali kwama hawa jamaa
wanatumia nguvu za giza kufanya mambo
yao kwa hiyo Agatha aliwatoa kafara
watoto wetu watatu ili kunishikiniza
nikubaliane nao . Baada ya kuwazika
wanangu watatu kwa siku moja sikuweza
tena kupata mtoto mwingine.” Akanyama
na kuvuta tena sigara akanywa funda moja
la mvinyo
“ So sorry for that Mr
president.Sikujua kama umepitia mambo
magumu namna hiyo” akasema Mukasha
“ Ni kweli Mukasha,nimepitia
mambo mengi magumu latika kipindi hiki
cha urais wangu.Kwa muda mrefu
nimekuwa nikitafuta upenyo wa
kuniwezesha kuachana na watu hawa
lakini nilishindwa .Hivi majuzi niligundua
kwamba enzi za ujana wangu niliwahi
kuwa na mahusiano na mwanamke mmoja
na katika mahusiano hayo tulibahatika
kuwa na mtoto ingawa mwanamke huyo
alinificha hadi hivi majuzi alipoamua kuja
kunieleza ukweli.Nilifurah mno kwani
niliamini ningekufa bila kuwa na mrithi
wa utajiri wangu.Japokuwa hizi zilikuwa
ni taarifa njema mno kwangu lakini
sikutaka kuamini haraka haraka na ndiyo
maana nikam tafuta Austin li aweze
kunisaidia kupata sampuli toka kwa huyo
mtoto kwa dhumuni la kufanya kipimo cha
vinasaba kubaini kama kweli mtoto huyo