QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Lege
Lege

Lege
L e g e
L E G E.
L. E. G. E
Legezaaaaaaàaa[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
daa wakuu sifanyi kusudi natamani nifanye kama wengi mtakavyo mm nimdau mkubwa sana wa kusoma story huwa nami pia napata taabu sana na maumivu na machungu myapatayo nayafaham.hivyo siwafanyii kusudi tokea jana sijaingia JF mpaka now mida hii ndio naingia jf saa 2 hii bado kuna wadau mnanilaum natakiwa kupumzika na then kesho kwenye majukum kama kawa
 
daa wakuu sifanyi kusudi natamani nifanye kama wengi mtakavyo mm nimdau mkubwa sana wa kusoma story huwa nami pia napata taabu sana na maumivu na machungu myapatayo nayafaham.hivyo siwafanyii kusudi tokea jana sijaingia JF mpaka now mida hii ndio naingia jf saa 2 hii bado kuna wadau mnanilaum natakiwa kupumzika na then kesho kwenye majukum kama kawa

Pamoja Mkuu Ila hii Mida ya Haki za Watu
Au uko single bro
 
SEHEMU YA 36


kubwa kama uliyonipata wewe na mkeo
Pauline.Ahsanteni sana” akasema Monica
“ Monica wewe ni mgeni wetu wa
heshima kwa hiyo ni jukumu letu
kuhakikisha kwamba unafurahi na
nimefarijika kusikia umefurahi.Naomba
uwe na amani na ujisikie uko
nyumbani.Muda wowote kama kuna
chochote unahitaji usisite kutueleza.”
Akasema David
“ Ahsante David” akajibu Monica
“ Leo asubuhi nimewasiliana na
wazazi wako nikawafahamisha kwamba
umefika salama na kuwatoa hofu .Wazazi
wako wanakupenda sana Monica”
akasema David na Monica akatabasamu
“ Vipi kuhusu Yule rafiki yako
aliyepigwa risasi anaendeleaje?
“ Anaendelea vizuri lakini bado
hajaanza kuzungumza “ akajibu Monica
“ Pole sana.Waliofanya unyama huo
tayari wamekamatwa?
“ Hapana bado hawajakamatwa
mpaka leo”
“ Ninahisi lazima atakuwa
anawafahamu.Laiti kama angeweza
kuzungumza basi angewataja ili
wakamatwe na kuchukuliwa hatua”
“ David suala hili lina utata
mwingi.Jana mchana nilimtembelea Dr
Marcelo hospitali na akaniandikia ujumbe
wa kunitaka nimsaidie kumtorosha pale
hospitali kuna watu wanataka kumuua”
“ Una hakika hajapatwa na tatizo
lolote la kiakili? Watu wanaotamka
maneno kama hayo mara nyingi huwa
wana matatizo ya akili”Akauliza David
“ Hapana hana tatizo la akili.Anazo
akili zake timamu na hata madaktari
wamethibitsha hivyo”
“ Kama anawafahamu watu
wanaotaka kumuua basi suala hili
linatakiwa kuwasilishwa katika vyombo
husika ili vilishughulikie”
“ Ningeweza kufanya hivyo lakini
katika ujumbe alioniandikia alinieleza
kuwa suala hili ni la siri na hapaswi mtu
mwingine yeyote kufahamu kwa hiyo
siwezi kumueleza mtu yeyote hata
polisi.Endapo angetaka niliwasilishe
jambo hili polisi basi angenielekeza hivyo
lakini hakutaka nifanye hivyo.” akasema
Monica
“Monica nakushauri achana kabisa
na suala hilo.Watu hao wanaotaka
kumuua huyo rafiki yako wakibaini kuwa
unajihusisha na jambo hilo unaweza
ukajikuta katika matatizo”
“ Hapana David,siwezi kuacha
kumsaidia Dr Marcelo kwani ni rafiki
yangu.Anahitaji mno msaada wangu na
hana
mwingine
wa
kumkimbilia.Nisipomsaidia
anaweza
akauawa” akasema Monica.David
akamtazama kwa makini kisha akasema
“ Monica wewe ni mtu mwenye moyo
wa aina yake.Uko tayari hata kuyaweka
hatarini maisha yako kwa sababu ya rafiki
yako.Pamoja na hayo sitaki ujiingize
katika suala hili la hatari.Naomba uniachie
mimi jambo hili nilishughulikie .Rais wa
Tanzania ni rafiki yangu na nitaongea
naye kumuomba alishughulikie suala
hili.Yeye ana watu wengi wanaoweza
kuifanya kazi hiyo kwa weledi
mkubwa.Nitajie jina la mgonjwa wako na
mahala alipo ili nimuombe rais wa
Tanzania
anisaidie
kwenda
kumuondoa.Niambie vile vile unahitaji
huyo rafiki yako apelekwe wapi baada ya
kutolewa hospitali? Akauliza David
“ Ahsante sana David na sijui
nitakushukuruje kwa msaada huu
mkubwa.Mgonjwa anaitwa Dr Marcelo na
amelazwa hospitali ya mtakatifu Lucia
wodi za watu maalum chumba namba
tatu.Nataka akishatolewa hapo hospitali
apelekwe sehemu salama hadi hapo
nitakaporejea .Naomba umsisitize rais
kwamba jambo hili ni la siri na watu
watakaotumwa kwenda kumtoa Marcelo
hospitali wasithubutu kumuhoji chochote”
“ sawa Monica nimekuelewa na
maelekezo yako yatazingatiwa” akasema
David akachukua simu na kumpigia rais
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Ernest Mkasa
 
SEHEMU YA 37


DAR ES SALAAM - TANZANIA
Ernest Mkasa alistushwa na simu
toka kwa David Zumo.Hakuwa
ametegemea kabisa kama David Zumo
angeweza kumpigia usiku ule.Akabonyeza
kitufe cha kupokelea
“ Hallow David” akasema
“ hallow Ernest,habari za usiku huu?
“ habari nzuri sana.habari za
Kinshasa?
“ Huku kwema kabisa” akasema
David
“ Mheshimiwa rais umenistua kidogo
kwa simu yako ya usiku huu “ akasema
Ernest
“ Samahani sana kwa hilo
mheshimiwa rais lakini nimelazimika
kukupigia kutokana na kuhitaji sana
msaada wako”
“ Sawa David nakusikiliza”
“ Mheshimiwa rais kuna kijana
mmoja anaitwa Marcelo ni daktari
alipigwa risasi hivi karibuni na watu
wasiojulikana amelazwa hospitali ya
mtakatifu Lucia chumba namba tatu.Mtu
huyu bado yuko katika hatari ya
kuuawa.Ninaomba msaada wako
mheshimiwa rais utume vijana wako
wamuondoe hapo hospitali kwa siri na
kumuweka sehemu salama na baadae
nitakupa maelekezo mengine.Ninaomba
sana unisaidie kwa hilo mheshimiwa rais”
akasema David Baada ya sekunde kadhaa
Ernest akasema
“ Huyo kijana ni raia wa Congo?
“ Hapana si raia wa Congo .Ni
mtanzania ila ananihusu sana na ndiyo
maana ninaomba msaada wako katika
suala hili.Tafadhali mheshimiwa rais
naomba unisaidie”
Ukapita ukimya mfupi kisha Ernest
akasema
“ Sawa David nitakusaidia lakini
naomba mtu huyo asiwe amejihusisha na
jambo lolote la kihalifu”
“ Ahsante sana mheshimiwa
rais.Nakuhakikishia kijana huyo ni safi na
hana rekodi yoyote ya uhalifu”
‘” Vizuri.Nitakutaarifu suala hili
likikamilika” akasema Ernest wakaagana
na kukata simu
 
SEHEMU YA 38


KINSHASA – DRC
Alipomaliza kuzungumza na Ernest
simuni,David Zumo akamgeukia Monica
“ Monica usihofu tena.Suala hili
limemalizika na rafiki yako atakuwa
salama.Rais wa Tanzania ameahidi
kulishughulikia
haraka
iwezekanavyo.Kuwa na amani” akasema
David
“ Ahsante sana David.Mungu
akubariki sana” akasema Monica
“ Usijali Monica.Kuna ule msemo
unaosema kuwa ukikaa karibu na uaridi
basi utanukia harufu ya uaridi kwa hiyo
ukikaa karibu a watu wakubwa hata
mambo yako yatakuwa makubwa na
rahisi.Simu moja tu na kila kitu kinakaa
sawa” akasema David halafu akamuomba
Monica waelekee katika chakula.Waliingia
katika chumba kikubwa cha chakula David
akabonyeza kitufe chini ya meza
wakaingia wahudumu sita wakiwa na
nyuso zenye tabasamu na waliovalia
nadhifu sana.Wakaandaa meza na baada
ya dakika kumi meza ikawa tayari
wahudumu wakatoka wakamuacha David
Zumo na Monica peke yao mle chumbani
“ Monica chakula hiki kimeandaliwa
maalum kwa ajili yako” akaanzisha
maongezi David wakiwa mezani wakipata
chakula.Monica akatabasamu na kusema
“ Ahsante David nashukuru
sana.Siwezi kuelezea furaha yangu kwa
namna wewe na mkeo mlivyonipokea na
kunijali”
“ Monica ni kawaida yetu kuwapokea
wageni wengi wanaokuja kututembelea
lakini nakuhakikishia kwamba katika
wageni wote tuliowahi kuwapokea hakuna
ambaye ana umuhimu mkubwa kwetu
kama wewe.Upekee wako ndio
uliosababisha hadi muda huu uko humu
ndani ya kasri hili ambalo si kawaida kwa
mtu ambaye hana ukaribu na rais
kuingia.” Akanyamaza kwa muda kisha
akasema
“ Monica siku ile nilipowakaribisha
wazazi wako kwa chakula na kufahamiana
,halafu ukaondoka baada ya kupata taarifa
za rafiki yako kupigwa risasi ,mimi na
baba yako tuliongea mambo mengi
makubwa na ya msingi sana” akanyamaza
tena akamtazama Monica na kusema
“ Nina imani mzee Benard tayari
amekwisha kueleza yale yote
tuliyoyaongea” akasema David na Monica
akatikisa kichwa ishara ya kukubali kile
alichokisema David
“ Vizuri.” Akasema David na baada ya
sekunde chache akaendelea.
“ Nafahamu sikufanya vizuri
kuongea suala kama lile na baba yako
kabla ya kuzungumza nawe
kwanza.Nilikwenda nje ya utaratibu na
ninaamini utakuwa umekwazika
.Nisamehe sana kwa hilo lakini nilifanya
vile kutokana na umuhimu wa suala
lenyewe kwangu.Nilitaka kupata msaada
toka kwa wazazi wako .Kuna msemo
usemao when it comes to love,smart
people becomes idiots.Hicho ndicho
kilichonitokea mimi na kujikuta nikifanya
mambo kinyume na taratibu na
kuzungumza na baba yako badala ya w
ewe.lakini nashukuru pamoja na
mzunguko huo mrefu nilioutumia ,ujumbe
wangu umefika” akasema David na wote
wakaangua kicheko.David akaendelea
“ Monica nilichomueleza baba yako
ni kitu cha kweli na kinatoka hapa
moyoni” akasema na kunyamaza
akamtazama
Monica
aliyekuwa
anamsikiliza kwa makini
“ Kutwa nzima ya leo umekuwa na
mke wangu Pauline.Amekueleza mambo
 
SEHEMU YA 39


mengi na kubwa ni suala lile nililomueleza
baba yako.Nilitaka upate kwanza nafasi ya
kuonana na kuongea na Pauline na
ninaamini alikueleza kwa kirefu sana
kuhusuana na suala hilo kwa hiyo sina
haja ya kurudia tena.Monica nakiri kwako
kwamba ninakupenda sana zaidi ya
ninavyoweza kukueleza.Nakiri sikuwahi
kukufahamu hapo kabla hadi pale jarida la
The Face lilipokutangaza kuwa ni
mwanamke mrembo zaidi kuliko wote
barani Afrika lakini mara tu nilipoiona
picha yako katika ukurasa wa mbele wa
jarida lile nilisikia sauti ndani mwangu
ikiniambia kwamba huyu ndiye.Naamini
Pauline alikueleza historia yetu na mambo
gani tunayapitia katika ndoa yetu.Ni
kutokana na changamoyo hizo ndipo
Pauline kwa upendo aliponitaka nitafute
mwanamke mwingine nioe ili atuzalie
watoto ambao watakuwa ni warithi wetu
.Pauline ni mwanamke mwenye upendo
wa kipekee kabisa .Sikuwa tayari kwa hilo
na hakuchoka kunisisitiza kuwa nitafute
mwanamke nioe.Imepita miaka mitatu
sasa toka aliponipa ruhusa hiyo na sikuwa
tayari kwa sababu moyo wangu ulimpenda
yeye pekee.Nilipokuona kwa mara ya
kwanza katika jarida ,nilihisi kama vile
moyo wangu unataka kusimama.Nilipatwa
na mstuko mkubwa.Nilitokea kukupenda
ghafla mno kabla hata ya kuonana nawe
ana kwa ana.Japokuwa nilikuja Dar es
salaam kikazi lakini lengo kuu la safari ile
ya kuja Dar ilikuwa kuonana
nawe.Ninashukuru sana Monica kwa
uelewa wako na ukaitika wito pale
nilipokuomba tuonane na ninashukuru
kwa kuwa leo hii niko nawe hapa ana kwa
ana kwa uhuru zaidi kuliongelea suala hili
” akanyamaza tena halafu akaendelea
“ Monica ninarudia tena
kukuhakikishia kwamba toka katika
sakafu ya moyo wangu ninakupenda mno
na nina nia ya dhati ya kutaka kukuoa uwe
mke wangu wa pili.” Akanyamaza kwa
sekunde kadhaa akaendelea
“ Nafahamu kwako hili si suala rahisi
hata kidogo .Tumefahamiana katika
kipindi kifupi ambacho hakijaziti hata
wiki moja na tayari ninatanganza ndoa
,hili si jambo jepesi.Ndoa ni jambo kubwa
na ili ukubali kuingia katika ndoa na mtu
Fulani inafaa uwe tayari unamfahamu
vyema mtu huyo nje na ndani na umpende
pia.Kwa upande wangu japokuwa
nimekufahamu katika kipindi kifupi
nimejitafakari sana na ninaongea kwa
ujasii mkubwa kuwa ninakupenda na niko
tayari kuwa nawe.Nafahamu kila mmoja
katika maisha yake ana ndoto zake juu ya
mwenzi amtakaye na ninafahamu
yawezekana sina vigezo vya mwanaume
Yule wa ndoto zako lakini nakuahidi
kufanya kila niwezalo kuwa mwanaume
bora kwako.Sina wasi wasi nawe kwani
naamini wewe ni mwanamke bora kabisa
ambaye kila mwanaume anaota kukupata
kwa hiyo nakuomba Monica tafadhali
kubali ombi langu .Nitakuweka juu zaidi
ya wanawake wote wa dunia hii.” Akasema
David Zumo.Ilimchukua Monica zaidi ya
dakika mbili kufungua mdomo wake na
kutamka
“ David ninaomba nikiri kwako kuwa
toka nilipopata taarifa za suala hili toka
kwa
baba
nimekuwa
silali
nikilitafakari.Mkeo Pauline naye
amenieleza kwa kirefu kabisa na
nimemuelewa lakini moyo wangu
unakuwa mzito kufanya maamuzi kwa
 
SEHEMU YA 40


haraka.Nashindwa nikujibu nini David ila
naomba ufahamu kuwa wewe ni
mwanaume bora kabisa.Haihitaji nguvu
kubwa kufahamu namna ulivyo mkarimu
na mwenye moyo wa huruma.Pauline
amenieleza mambo mengi kuhusu wewe
namna unavyompenda na kujali na
nimemuamini alichonieleza.Pamoja na
hayo yote lakini nasikitika kukueleza
David kuwa bado sina hisia zozote za
mapenzi nawe.Sitaki nikudanganye David
labda unipe muda zaidi wa kulitafakari
jambo hili” akasema Monica
David akaivua kofia yake yenye
manyoya ya Simba na kujifuta jasho
kichwani
“ Monica sina maneno mazuri na
matamu ya kuulainisha moyo wako au
laiti ningekuwa na uwezo wa kuyawezesha
macho yako yaweze kuona namna moyo
wangu unavyoteseka juu yako ungenionea
huruma na kulikubali ombi langu.Monica
sihitaji unipende.Ninachohitaji mimi ni
kuwa nawe tu.Nipe nafasi Monica
nikuonyeshe namna ninavyokujali na
kukupenda.Najua hauna mchumba bado
kwa hiyo tafadhali naomba usininyime
nafasi hii.Yawezekana labda unaogopa
kuwa mke wa pili lakini naomba
usiogope.Tutafunga ndoa halali serikalini
na utakuwa mke wangu wa halali.Hakuna
tatizo kwa upande wa Pauline na tayari
amekwisha kuthibitishia hilo.” Akasema
David akainuka na kumshika mkono
Monica wakatoka katika chumba cha
chakula wakaelekea sebuleni wakaketi
sofani.Mapigo ya moyo wa Monica
yalikuwa yanakwenda kwa kasi ya ajabu
“ Monica ninapokutazama machoni
najiona
mimi.Ninaiona
kesho
yangu.Ninaiona kesho ya Congo.Kesho
yangu iko juu yako Monica kwa hiyo
naomba usininyime nafasi ya kuiona
kesho yangu.Nikubali nikuoe Monica
nikuonyeshe namna ulivyo muhimu
kwangu,namna ulivyo muhimu kwa Congo
.Nchi yote ya Congo itakusujudu kama
malkia wao.Niruhusu nikupe nafasi hii ya
kuwa malkia wa Congo kwani naamini
kutokea kwako atazaliwa mtawala mpya
wa Congo baada yangu kwa hiyo wewe ni
mtu muhimu sana kwa nchi hii.Ufungue
moyo wako Monica na niruhusu niingie
kama niivyoufungua wa kwangu na
kukuruhusu uingie na utawale.” David
Zumo akatamka maneno yale kwa hisia
kubwa akiwa ameishika mikono ya
Monica.Walikuwa wamekaribiana sana na
maneno yale ya David yakaonekana
kumuingia .
“ Kuna sauti kubwa ninaisikia ndani
mwangu
inaniambia
nimkubali
David.Tayari nimekwisha pata picha ya
maisha nitakayoishi nitakapokubali
kuolewa na David.Ni maisha ya kifahari
mno.Hakuna mwanamke katika dunia hii
ambaye hataki kuishi kama
malkia.Nitapoteza kitu gani nikimkubali
David hata kama bado hajaniingia moyoni
mwangu? Akajiuliza Monica
“ Hakuna chochote nitakachopoteza
nikikubali kuolewa na David Zumo.Ngoja
tu nikubali kwani nafasi kama hizi
hutokea
mara
chache
sana
duniani.Imekuwa ni kama bahati
imeniangukia mimi,sipaswi kufanya
mzaha katika jambo hi.................” Mara
Monica akaondolewa mawazoni baada ya
kuhisi kitu kama mkono ukipapasa na
kuyatomasa matiti yake.Alistuka
 
SEHEMU YA 41

sana.Hakuwahi kutomaswa matiti yake na
mwanaume yeyote
“ David !!! akasema na kutaka
kumsukuma lakini mikono yeye nguvu ya
David ikamshika bara bara
“ Monica tafadhali naomba
usihamaki.Nimeshindwa kuvumilia.Najua
umekwisha fahamu ninachokihitaji kwako
na ninafahamu hata wewe unahitaji pia
jambo hili kwa hiyo naomba Monica unipe
heshima hii” akasema David kwa sauti ya
kubembeleza huku akihema haraka
haraka.Monica akashindwa afanye nini
kwani tayari David alikwisha onyesha
dhamira ya wazi ya kutaka kufanya
ngono.David aliendelea na kuyapapsa
maungo ya Monica na kumfanya ahisi
msisimko wa aina yake
“ Ni mara ya kwanza ninachezewa
hivi na mwanaume.Nahisi raha ya aina
yake.David ananigusa katika sehemu zile
ambazo zinanifanya nipagawe.oh my gosh
!!.Leo nimepatikana sina ujanja tena.I have
to do it.Ngoja tu nimuachie afanye kile
anachokitaka lakini ukweli utabaki pale
pale kuwa I’m so weak and
stupid.Nimejitunza kwa kipindi kirefu
lakini leo nimenasa kwenye mtego kama
kinda na siwezi kujinasua.” Akawaza
Monica wakati David akiendelea
kumfanyia utundu wa kila aina na
kumfanya atoe migumo kwa raha
aliyokuwa anaipata.Alihisi kuhamishwa
dunia.Alilainika na hakuweza kufumbua
hata ukope.
 
SEHEMU YA 42


DAR ES SALAAM – TANZANIA
Rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Ernest Mkasa alipomaliza
kuzungumza na David Zumo katika simu
akamgeukia Austin
“Austin sasa naomba unisikilize
vizuri.” Akasema Ernest.Akatulia kidogo
akamtazama Austin kwa makini na
kusema
“ Nina kazi mbili ambazo nataka
unifanyie.Kazi ya kwanza kuna mtu Fulani
anaitwa Dr Marcelo amelazwa hospitali ya
mtakatifu Lucia.Nataka ukamtoe hapo
hospitali kwani kuna watu wanataka
kumuua.Nataka atolewe kimya kimya bila
ya mtu yeyote kufahamu na baada ya
kumtoa utamleta hapa kwako atakaa hapa
hadi hapo nitakapokupa maelekezo
mengine.” Akasema Ernest na kunyamaza
“ Ni nani huyo Marcelo? Nani
wanataka kumuua? Akauliza Austin
“ Austin umepewa kazi ya kufanya
tafadhali naomba uifanye.Sihitaji maswali
katika jambo hili.” Akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais ,nimekuuliza
maswali hayo kwa lengo la kutaka
kufahamu kwa kina kuhusu jambo
hili.Nataka kufahamu ni akina nani
wanaotaka kumuua na kwa nini ili
ninapokwenda huko niwe tayari
ninafahamu nguvu ya hao wanaotaka
kumuua Marcelo.Hata hivyo unataka lini
kazi hiyo ifanyike?
“ Soon as possible” akajibu Ernest
kwa haraka
“ kama kungekuwa na uwezekano
hata usiku wa leo ungeifanya kazi hiyo
lakini naomba uifanye kesho.Kama kuna
chochote utakachohitaji utanitaarifu”
akasema Ernest
“ kazi ya pili ambayo ni kubwa”
akaendelea
“ Kuna msichana mmoja anaitwa
Monica benedict mwamsole ambaye hivi
majuzi ametajwa na jarida moja kubwa la
mitindo la The Face kuwa ndiye mrembo
kuliko wote Afrika.Enzi za ujana wangu
niliwahi kuwa na mahusiano na
mwanamke mmoja ambaye ni mke wa
rafiki yangu na hivi karibuni mwanamke
huyo amekuja kwangu akanieleza
kwamba wakati ule tukiwa katika
mahusiano aliwahi kupata mimba yangu
ila akanificha.Mwanamke huyo akadai
kwamba Monica ni mwanangu.Hapa nilipo
sina mtoto hata mmoja kwani watoto
wangu wote wamekwisha tangulia mbele
za haki na nilipopewa taarifa hizi nilistuka
sana na sijataka kuziamini moja kwa moja
kwa hiyo nataka nifanya uchunguzi wangu
wa siri kubaini kama kweli Monica ni
mwanangu.Ninataka kufanya kipimo cha
vinasaba ambacho kitanipa jibu kama
kweli Monica ni mwanangu .Jambo hili ni
la siri kubwa na sitaki mtu mwingine
yeyote alifahamu zaidi yako.Nimekuamini
na ndiyo maana nikafanya kila lililo ndani
ya uwezo wangu kuhakikisha ninatimiza
 
SEHEMU YA 43


masharti yako ili unifanyie kazi hii”
akanyamza na baada ya muda akaendelea.
“ Nataka kupata sampuli kwa siri
toka kwa Monica kwa hiyo basi nataka
ujenge urafiki wa karibu naye .Nataka
kuutumia ukaribu huo wako na yeye
kumfahamu vizuri Monica ili hata kama
ikitokea akawa kweli ni mwanangu iwe
rahisi kujenga mahusiano mazuri naye.”
Akanyamaza tena kidogo, akaendelea
“ Tukisha ipata sampuli hiyo ,kipimo
kitakwenda kufanyika nje ya nchi.Sitaki
kipimo kifanyike hapa nchini kwa
kuogopa
udanganyifu.Austin
nimekukabidhi jukumu hili lote
ulisimimamie wewe mwenyewe na
mwisho unipatie majibu .Nakuomba
ufanye kila linalowezekana kufanikisha
jambo hili.Chochote utakachokihitaji
katika
saula
hili
niambie
nitakupatia.Kama nimeweza kumtoa
ndugu yako kifungoni China siwezi
kushindwa jambo lingine lolote.kwa hiyo
Austion kaa na utafakari namna
utakavyoweza kulifanikisha suala
hili.Narudia
tena
chochote
utakachokihitaji katika jambo hili
utakipata na yale yote niliyokuahidi
kuhusu dada yako yatatekelezwa.Natumai
umenielewa Austin”
Ukimya ukatanda wa takribani
dakika mbili kisha Austin akasema
“ Nimekuelewa mheshimiwa
rais.Nitakufanyia kazi yako ila nina
mambo mawili ya kukwambia kabla
sijafanya kazi zako” akanyamaza kidogo
na kusema
“ Kwanza nataka kukuweka wazi
kwamba baada ya kumaliza kazi zako
mbili mkataba wangu na wewe utakuwa
umemalizika na sintapokea tena kazi
nyingine yoyote kwa hiyo kama una
mawazo ya kunipa kazi nyingine baada ya
hizi yafute kabisa mawazo hayo.”
Akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Jambo la pili nilikuuliza kuhusu
Alberto’s ukakiri kuwafahamu japo wewe
si mmoja wao.Nimefurahi kusikia hivyo
kwani kuna jambo nataka ulifanye.”
Akanyamaza akameza mate na kuendelea
“ Nimekuwa nikifuatilia habari za
Tanzania.Ni siku ya tatu leo katika kila
mkoa hapa Tanzania kuna makundi ya
watu wake kwa waume ,wazee kwa vijana
wanajiandikisha kwa ajili ya kufanya
maandamano makubwa kuelekea bungeni
mjini Dodoma ambako kunatarajiwa
kuwasilishwa muswada wa kutetea haki
za binadamu katika kikao kijacho cha
bunge kitakachoanza hivi karibuni.Katika
muswaada huo kuna vipengele ambavyo
vinataja kutambua haki za baadhi ya
makundi kadhaa ya watu wakiwamo watu
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia
moja.Muswada huu unazitambua pia ndoa
za jinsia moja na kama haitoshi musaada
huu pia unatambua haki ya mwanamke
kutoa mimba.Miswada ya aina hii tayari
imekwisha pitishwa kuwa sheria katika
nchi zaidi ya ishirini barani afrika.Lengo
ni kuhakikisha nchi zote za Afrika
zinakubaliana na mambo hayo .Imetumika
nguvu kubwa kuufikisha muswada huu
hapa ulipofika na toka maandalizi ya
muswaada huu yalipoanza kumekuwa na
kelele nyingi toka kwa wananchi
wakiupinga lakini viongozi na wewe
ukiwemo ,mmeziba masikio na
mmeendelea na mchakato wake kwa
kigezo cha manufaa kwa nchi.Mheshimiwa
rais ninakueleza haya yote lakini
 
SEHEMU YA 44



unafahamu kila kitu kwani umeshiriki pia
katika kuubariki muswada huu uende
kujadiliwa bungeni na nina hakika uko
tayari kuweka saini yako ili uwe sheria
pindi utakapofikishwa katika ofisi yako
baada
ya
kujadiliwa
na
bunge.Mheshimiwa rais wewe na wenzako
hamuwezi mkawa sababu ya Tanzania
kulaaniwa kwa mambo mnayotaka
kuyafanya kwa hiyo utaitisha mkutano wa
dharura wa watendaji wako kesho na
utatangaza kuufutilia mbali muswada huo
,usipelekwe bungeni na wala usijadiliwe
sehemu yoyote ile.”
“ Austin.....!!! Ernest akataka kusema
kitu Austin akamzuia
“ Naomba usubiri nimalize
mheshimiwa rais.” Akasema Austin
“ Kesho hiyo hiyo baada ya kuufuta
muswada huo wa haki za binadamu ,jioni
utalihutuba taifa na kuwataarifu
wananchi kuwa hakutakuwa tena na
muswada huo na utaitumia nafasi hiyo
kuitangazia dunia kuwa Tanzania haiko na
haitakuwa tayari kukubaliana na masharti
toka kwa taifa lolote kubwa au dogo na
utamke wazi wazi kuwa mapenzi au ndoa
ya jinsia moja ni marufuku nchini
Tanzania.Mr president are you readuy for
that? Akauliza Austin.Bila kukawia Ernest
akasema
“ Austin that’s impossible.Hilo ni
jambo lisilowezekana na ninaomba
tusiliongelee hilo kabisa !! akasema Ernest
kwa hamaki
“ Mheshimiwa rais naomba
nikuweke wazi kwamba utimilifu wa kazo
zako utategemea sana na wewe
utakavyolipokea suala hili.Endapo
utafanya
kama
nilivyokueleza
nitakufanyia kazi yako tena kwa muda
mfupi sana lakini endapo hautakuwa
tayari kutekeleza hayo maagizo yangu basi
sintoifanya kazi yako na nitaamini wewe
ni mfuasi wa Alberto’s ambao ni maadui
zangu kwa hiyo na wewe utakuwa mmoja
wa maadui zangu.” Akasema Austin.Ernest
akamtazama kwa macho makali na
kusema
“ Austin ninakuamini sana na ndiyo
maana niko tayari kufanya kila lililo ndani
ya uwezo wangu ili unifanyie kazi yangu
vizuri.Nitafanya lolote utakaloniamuru
nifanye lakini hili unalotaka nilifanye
kesho ni jambo ambalo lipo nje ya uwezo
wangu na sina mamlaka nalo kwa hiyo
siwezi
kulifanya”
Akanyamaza
akamtazama Austin halafu akasema
“ Austin ninaamini mpaka hapa
tayari unawafahamu Alberto’s ni watu wa
namna gani.”
“ Ndiyo mheshimiwa rais
ninawafahamu”
“ Basi naomba nikuweke wazi kuwa
wao ndio walioniweka madarakani.”
Sura ya Austin ikabadilika
akapandwa na hasira .
“ You lied to me.You are one of
them!! Akasema Austin kwa hasira
“I’m not one of them,ila walinisaidia
nikaingia madarakani kwa makubaliano
ya kuwasaidia katika mambo yao Fulani
Fulani.Sikutegemea kama siku moja
wangeweza kuja na muswada kama
huu.Siwezi kuufuta muswada huu kwa
sababu tayari nimekwisha weka
makubaliano nao kuitumia ofisi yangu
kufanikisha mambo yao na moja ya
mambo hayo ni huu muswada unaotarajia
kuwasilishwa
bungeni
hivi
karibuni.Nitakapokwenda kinyume nao
 
SEHEMU YA 45

I’m dead.These people are powerfull and
mosters.I can’t betray them.Naomba
mambo haya tuyaache kama yalivyo na
tuongelee kuhusu yale yanayohusiana na
kazi yetu” akasema Ernest
“ Hata hili linanihusu pia.” Akasema
Austin na kumkazia macho Ernest kisha
akasema
“ Alberto’s are my enemies mr
President.If you want me to do your job
then they should be your enemies too.”
Macho ya Ernest Mkasa yalionyesha
woga mkubwa
“ Austin hutakiwi kuweka uadui na
hawa watu.Kama nilivyokueleza they are
powerfull and monsters.Wako kila
sehemu .Wamekita mizizi katika sehemu
zote za muhimu za serikali na hivyo ni
vigumu sana kupambana nao.Nakushauri
Austin tafadhali achana kabisa na watu
hawa kijana wangu” akasema Ernest
“Mzee naomba nikuweke wazi kitu
kimoja .Mimi kutaka kuuawa kule Somalia
ulikuwa ni mpango wao na walitaka
kuniua baada ya kuifahamu mipango yao
miovu hapa Tanzania.Niliponusurika kifo
niliamua kuachana kabisa na kazi hizi na
sikutaka
kujishughulisha
nao.Nilichukizwa mno na kitendo kile na
ndiyo maana nikaichukia Tanzania na
sikutaka tena kurejea nikaamua kuchukua
uraia wa Afrika kusini ambako ninaishi
kwa amani.Uliponimbia nije Tanzania
nilikubali kwa sababu ya mambo mawili
kwanza kumkomboa dada yangu na pili
niliamua kuja kuwakomboa watanzania
wenzangu dhidi ya mambo machafu
wanayofanyiwa na Alberto’s kupitia
viongozi walioweka maslahi yao mbele na
kusahau
kuwahudumia
wananchi.Mheshimiwa rais nimekuja
kupambana na Alberto’s na ninaomba
uniunge mkono.Macho yako yanaonyesha
wazi kwamba hufurahishwi na mambo
yanayofanywa na Alberto’s lakini huna
namna ya kuweza kuwakatalia kwa
sababu ya makubaliano yenu.Mheshimiwa
rais imetosha sasa na umefika wakati wa
kuachana nao.Wakati wako ni huu wa
kufanya maamuzi yenye kufaa kwa
mustakabali wa taifa letu.Nakuhakikishia
mheshimiwa rais ukishindwa kufanya
maamuzi leo na ukakubali taifa
likatumbukia katika laana hii kubwa,siku
ukifa kaburi lako litapigwa mawe .Liokoe
taifa hili lisilaaniwe” akasema Austin
.Ernest akainamisha kichwa akafikiri kwa
sekunde kadhaa akasema
“ Austi sina la kusema zaidi ya
kurudia ushauri wangu kuwa achana na
mambo hayo.Kama hutaki ushauri wangu
na ukaamua kuendelea na hicho
unachokiita mapambano dhidi ya
Alberto’s naomba usinishirikishe tafadhali
na nina wasiwasi sintakuwa na namna
nyingine ya kukusaidia.Ninakushauri tena
kama kijana wangu,fanya kazi zangu
nilizokuagiza halafu urejee zako afrika ya
kusini ukaendelee na maisha yako ya
amani .Usitake kuyaharibu maisha yako
kwa kutafuta ushujaa.” Akasema Ernest
.Austin akamtazama kwa makini sana na
kusema
“ Mheshimiwa rais ,utajisikiaje
iwapo ungekuwa na mtoto wa kiume
ambaye umemlea kwa mapenzi makubwa
na ukiwa na mategemeo kuwa atakuletea
wajukuu lakini badala yake akageuzwa
mke na mwanaume mwenzake? Au
utajisikiaje iwapo ikatokea Monica akawa
kweli ni mwanao halafu ukagundua
 
Nimezifumua zinatupiwa nafikiri mchezo unaendelea
 
SEHEMU YA 47


kwamba ameolewa na mwanamke
mwenzake?
Ernest akainamisha kichwa akafikiri
na kusema
“ Ni wazi nitajisikia vibaya na
ninaomba usiku na mchana laana hiyo
ipite mbali na familia yangu.Siwezi
kuvumilia upuuzi kama huo!!! Akasema
Ernest
“ Jinsi utakavyojisikia ndivyo
watakavyojisikia vibaya wazazi ambao
watoto wao watafanywa wenzi na wenzao
wa jinsia moja pale tu utakaporuhusu
muswada huo ukaingia bungeni na baadae
ukatia saini kuufanya sheria.Tafadhali
mheshimiwa rais usikubali jambo
hili.Unazo nguvu za kuhakikisha muswada
huu haupelekwi bungeni .Tumia
madaraka yako kama rais” akasema
Austin.Ernest akatumia zaidi ya dakika
saba kutafakari kisha akasema
“ Austin maneno uliyoyasema ni
mazitoi na yameniingia barabara.Ninakiri
kwako kuwa nilifanya kosa kubwa sana
kukubali kutumiwa na watu hawa .Ni
tamaa ya urais iliniponza.Kuna mambo
mengi mabaya yamefanywa na watu hawa
kwa wananchi ambao niliapa
kuwatumikia na ninaumia sana kila
ninapoona taarifa za habari na kusikia
kasi ya saratani ya kizazi inaongezeka kila
uchao kwa wanawake kutokana na
madawa mengi yanayoingizwa kwa
makusudi yanayosababisha saratani ya
kizazi.Lengo hapa ni kupunguza idadi ya
watu barani Afrika ili baadae kusiwe na
nguvu kazi na wazungu waje waitawale
tena Afrika.Kundi kubwa la vijana nguvu
kazi ya taifa limeathirika na dawa za
kulevya.Ninatamani nifanye kitu lakini
mikono yangu tayari imefungwa
.Nimekuwa rais kivuli ambaye ninatumiwa
na watu wengine.I cant fight these people
so do you.” Akasema Ernest kwa unyonge
“ Mr President nimefarijika kuona
kuwa una umizwa na mambo
haya.Naomba usiogope tafadhali.Kuwa
jasiri na ufanye leo maamuzi makubwa
ambayo yatakufaya ukumbukwe na vizazi
vingi vijavyo.Kuwa rais wa mfano na
ufanye nchi hii iwe nzuri na salama kuishi
kwa watoto wa watoto wetu” akasema
Austin.Ilimchukua dakika zaidi ya tatu
Ernest kuongea
“Austin narudia tena kusema kuwa
mambo uliyoyaongea ni mazito na yenye
manufaa makubwa.Nimekuelewa kijana
wangu na niko tayari kufanya maamuzi
makubwa na magumu lakini ukae ukijua
kuwa nitakapofanya hivyo unavyotaka
nifanye basi tayari mimi na wewe
tutakuwa katika hatari kubwa.Sitaki
kukuingiza katika matatizo.Sitaki niwe
chanzo cha maisha yako kuharibika tena”
akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais umesoma faili
langu na tayari umefahamu mambo mengi
kuhusu mimi.Siogopi kuingia katika
matatizo na wala maisha yangu
kuvurugika.Kwa hiyo usihofu kuhusu
usalama wangu na wako” akasema
Austin.Ernest akafikiri tena kwa muda
kidogo na kusema
“ Austin nitafanya hivyo unavyotaka
nifanye lakini kwa sharti moja”
“ Sharti gani mheshimiwa rais?
Akauliza Austin
“ Nataka unihakikishie kwamba
hautarejea tena Afrika kusini bali utabaki
hapa hapa nchini.Austin I need you here to
protect me”
 
SEHEMU YA 48


Mheshimiwa rais unao ulinzi wa
kutosha kwa hiyo sioni sababu ya mimi
kubaki Tanzania”
“ Ni kweli Austin ninao ulinzi
mkubwa lakini hakuna kati ya walinzi
wangu mwenye uwezo mkubwa kama
wewe.Umepata mafunzo ya hali ya juu
katika nchi tofauti tofauti .Ni mtanzania
pekee kati ya 10 uliyemaliza na kuhitimu
mafunzo ya operesheni maalum katika
chuo cha Navy seal nchini
Marekani.”akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais nipe muda wa
kulitafakari suala hili kwani siwezi
kukupa jibu la haraka haraka kama
ninaweza kulikubali ombi lako ama vipi”
“ Austin ni wewe ambaye
umenishawishi kuingia katika hii vita kwa
hiyo lazima tupambane wote wawili.You
are going to stay here for good.Nitakupatia
kila unachokihitaji na utakuwa mlinzi
wangu wa siri.Austin kazi hii huwezi
kuikimbia ,haya ndiyo maisha
yako.Yakubali na uyaishi.Mimi kesho
nitafanya kama tulivyokubaliana na nina
imani na wewe utatekeleza kwa upande
wako” akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais ,ahsante kwa
kunisikiliza na kunielewa.Kesho nitaanza
kufanya kazi zako.Nitakupa orodha ya vitu
nitakavyovihitaji kwa ajili ya kuikamilisha
kazi hizo.Natumai tutakuwa tena na
kikao kingine cha kuzungumzia kwa
undani kuhusu vita hii tunayokwenda
kuianza.Kwa sasa naomba uende
ukapumzike na mimi uniache nitafakari
namna nitakavyofanya kazi zako”
akasema Austin akaagana na Ernest
akaondoka
“ hatimaye ninarejea tena rasmi
katika kazi ambayo sikuwa ninataka
kuifanya katika kipindi cha maisha yangu
yote yaliyobakia lakini kama alivyosema
rais kuwa this is my life ,this is my job,this
is where I belong.Ni muda muafaka sasa
umefika wa kupambana na Albertos na
kuung’oa kabisa mzizi wake hapa
Tanzania.Watu hawa walinifanya
nikaichukia nchi yangu na hata kuapa
kutokurudi tena,ninasema safari hii ni
ama zao ama zangu.Siwaogopi
tena.Nitapambana nao hadi mwisho
wangu.Nashukuru kwa rais kuamua
kuniunga mkono .Endapo kesho atafanya
kama nilivyomuelekeza basi litakuwa ni
pigo kubwa kwa Alberto’s.Hawataamini
kilichotokea.Wakati wakiwa katika
mshangao wakijiuliza juu ya kilichotokea
nitawaondoa mmoja baada ya mwingine.Si
kazi nyepesi hii lakini nitajitahidi kwa
nguvu zangu zote na pale itakapobidi
nitaomba msaada.Lazima nipambane nao
,lazima waondoke Tanzania.Hii ni nchi
pekee ambayo wamehangaika kwa miaka
mingi kuotesha mizizi yao na walifanikiwa
baada ya kumsaidia Ernest Mkasa kuingia
madarakani.Toka hapo nchi imebadilika
sana na wamekuwa wakifanya yale
ambayo wameyafanya katika nchi
nyingine za afrika na dunia. Lakini ngoja
kwanza niachane na mawazo hayo kuhusu
vita na Alberto’s kwa sasa na nielekeze
akili yangu katika kutafuta namna ya
kuweza kumtoa Marcelo hospitali na
namna nitakavyojenga ukaribu na Monica”
akawaza Austine na mara akamkumbuka
mpenzi wake Maria
“ Natakiwa kuwasiliana na Maria
nijue maendeleo yake.Nimekuwa
namuwaza
kutwa
nzima
ya
leo.Ninampenda sana na moyo unaiuma
 
Back
Top Bottom