SEHEMU YA 48
Mheshimiwa rais unao ulinzi wa
kutosha kwa hiyo sioni sababu ya mimi
kubaki Tanzania”
“ Ni kweli Austin ninao ulinzi
mkubwa lakini hakuna kati ya walinzi
wangu mwenye uwezo mkubwa kama
wewe.Umepata mafunzo ya hali ya juu
katika nchi tofauti tofauti .Ni mtanzania
pekee kati ya 10 uliyemaliza na kuhitimu
mafunzo ya operesheni maalum katika
chuo cha Navy seal nchini
Marekani.”akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais nipe muda wa
kulitafakari suala hili kwani siwezi
kukupa jibu la haraka haraka kama
ninaweza kulikubali ombi lako ama vipi”
“ Austin ni wewe ambaye
umenishawishi kuingia katika hii vita kwa
hiyo lazima tupambane wote wawili.You
are going to stay here for good.Nitakupatia
kila unachokihitaji na utakuwa mlinzi
wangu wa siri.Austin kazi hii huwezi
kuikimbia ,haya ndiyo maisha
yako.Yakubali na uyaishi.Mimi kesho
nitafanya kama tulivyokubaliana na nina
imani na wewe utatekeleza kwa upande
wako” akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais ,ahsante kwa
kunisikiliza na kunielewa.Kesho nitaanza
kufanya kazi zako.Nitakupa orodha ya vitu
nitakavyovihitaji kwa ajili ya kuikamilisha
kazi hizo.Natumai tutakuwa tena na
kikao kingine cha kuzungumzia kwa
undani kuhusu vita hii tunayokwenda
kuianza.Kwa sasa naomba uende
ukapumzike na mimi uniache nitafakari
namna nitakavyofanya kazi zako”
akasema Austin akaagana na Ernest
akaondoka
“ hatimaye ninarejea tena rasmi
katika kazi ambayo sikuwa ninataka
kuifanya katika kipindi cha maisha yangu
yote yaliyobakia lakini kama alivyosema
rais kuwa this is my life ,this is my job,this
is where I belong.Ni muda muafaka sasa
umefika wa kupambana na Albertos na
kuung’oa kabisa mzizi wake hapa
Tanzania.Watu hawa walinifanya
nikaichukia nchi yangu na hata kuapa
kutokurudi tena,ninasema safari hii ni
ama zao ama zangu.Siwaogopi
tena.Nitapambana nao hadi mwisho
wangu.Nashukuru kwa rais kuamua
kuniunga mkono .Endapo kesho atafanya
kama nilivyomuelekeza basi litakuwa ni
pigo kubwa kwa Alberto’s.Hawataamini
kilichotokea.Wakati wakiwa katika
mshangao wakijiuliza juu ya kilichotokea
nitawaondoa mmoja baada ya mwingine.Si
kazi nyepesi hii lakini nitajitahidi kwa
nguvu zangu zote na pale itakapobidi
nitaomba msaada.Lazima nipambane nao
,lazima waondoke Tanzania.Hii ni nchi
pekee ambayo wamehangaika kwa miaka
mingi kuotesha mizizi yao na walifanikiwa
baada ya kumsaidia Ernest Mkasa kuingia
madarakani.Toka hapo nchi imebadilika
sana na wamekuwa wakifanya yale
ambayo wameyafanya katika nchi
nyingine za afrika na dunia. Lakini ngoja
kwanza niachane na mawazo hayo kuhusu
vita na Alberto’s kwa sasa na nielekeze
akili yangu katika kutafuta namna ya
kuweza kumtoa Marcelo hospitali na
namna nitakavyojenga ukaribu na Monica”
akawaza Austine na mara akamkumbuka
mpenzi wake Maria
“ Natakiwa kuwasiliana na Maria
nijue maendeleo yake.Nimekuwa
namuwaza
kutwa
nzima
ya
leo.Ninampenda sana na moyo unaiuma