QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 49


kwa kitendo nilichokifanya cha
kumdanganya kuhusu kazi iliyonileta Dar
es salaam.Itanilazimu nimueleze ukweli
wa kila kitu ili asije huku kwani mambo
yanayokwenda kutokea siku si nyingi ni ya
hatari sana kwa usalama wake na siko
tayari kuyaweka maisha yake hatarini.”
Akawaza Austin na kwenda kuchukua
kompyuta yake akamtafuta Maria
mtandaoni akampigia.Maria akapokea
simu
“ How’re you my love.Huwezi jua ni
kwa namna gani nimeisubiri simu hii
leo.Sijui kama ningeweza kulala bila
kuisikia sauti yako nzuri.Nakupenda sana
Austin na ndiyo maana ninakuwaza mno
kuliko kitu kingine chochote.” Akasema
Maria na kumfanya Austin atabasamu
“ Hello malaika wangu, umeshindaje
leo? Nisingeweza kulala bila kujua hali
yako “
“ Nimeshinda salama mpenzi wangu
na hali yangu ni njema sana.Leo
nimeshindwa kusaini ule mkataba
,wanasheria wa Alnoor wanaweka sawa
baadhi ya vipengele ila kesho nina
uhakika tutasaini mkataba na baada ya
hapo sintopoteza hata dakika moja
,nitapanda ndege kuja Dar es salaama
kukutana nawe mfalme wangu” Akasema
Maria na Austin akajikuta akikosa neno la
kusema
“ Mbona umekuwa kimya ghafla
Austin? Hutaki nije Dar es salaam?
Akauliza Maria.Austin akakohoa kidogo na
kusema
“ Uhhmm ! Maria bado unasisitiza
kutaka kuja Dar es salaam?
“ Ndiyo ninasisitiza Austin.Mbona
unaonekana hujapendezwa na mimi
kutaka kuja Dar es salaam?Kuna nini
unanificha Austin? Tafadhali kuwa
muwazi”
akasema
Maria.Austin
akatabasamu na kusema
“ Hakuna chochote ninachokificha
Maria ila nina wasi wasi na usalama”
“ Kama huna unachokificha basi
hupaswi kuwa na wasi wasi.Nitakuja Dar
es salaam mara tu baada ya kumalizana na
Alnoor.Austin siogopi hatari yoyote kama
kuna lolote baya basi litufike sote kwa
hiyo ujiandae kunipokea kesho
kutwa.Nitakutaarifu kesho ni ndege gani
nitapanda ili unipokee uwanja wa ndege”
akasema Maria wakaendelea na maongezi
mengine na baada ya saa nzima
wakaagana
“ Nimeshindwa kumueleza Maria
ukweli na hii ina maana lazima aje Dar es
salaam.What can I do? Nifanye nini
kumzuia asije? Ulimi umekuwa mzito
kumueleza ukweli na endapo atakuja Dar
lazima atagundua nimemdanganya na
ataumia sana kwani mimi ni mtu
anayeniamini kuliko hata baba yake
mzazi.Nitaongea na baba yake pengine
anaweza akanisaidia kwa namna yoyote
ile kumfanya Maria asije Dar es salaam”
akawaza Austin na kuanza kuwaza tena
juu ya majukumu yaliyoko mbele yake
“ Monica Benedict Mwamsole ,who is
this woman? Kwa bahati mbaya mimi si
mfuatiliaji sana wa habari za mambo haya
ya urembo ndiyo maana simfahamu huyo
Monca ni nani hadi kutangazwa kuwa
mwanamke mrembo kuliko wote
Afika.Haiwezekani atokee mwanamke
mmoja awe mzuri kuliko mamilioni ya
wanawake wa Afrika,awe mzuri
kumshinda hata mpenzi wangu
Maria.Mimi naamini Maria ni mwanamke
 
SEHEMU YA 50


mzuri kuliko wote Afrika na dunia “
akawaza Austin na kuanza kupekua
mtandaoni kutafuta t aarifa za Monica.
Alipata picha nyingi za Monica
alizoweka mtandaoni na akabaki mdomo
wazi
“ What a beautiful woman.!!! She’s an
angel..I was wrong,huyu anastahili kabisa
kuwa mrembo kuliko wote afrika.” Austin
akajikuta akiongea mwenyewe kwa sauti
ndogo na kuendelea kupitia picha za
Monica moja baada ya nyingine halafu
akajiegemeza kitini
“ Monica Benedict !!..akasema kwa
suti ndogo
“ Nilidhani labda ni mwanamke
mwenye uzuri wa kawaida tu lakini
kumbe ni mwanamke mwenye uzuri
usioweza
kuelezeka
kwa
maneno.Nawapongeza watu wa jarida la
The Face walifanya kazi kubwa ya
kusakanya na kumpata mtu sahihi kuwa
malkia wa urembo Afrika.” Akawaza
Austin huku akiendelea kuzitazama picha
za Monica
“ Mpenzi wangu Maria ni mzuri sana
lakini nakiri hawezi kufikia uzuri wa
Monica” Bado picha za Monica zilionekana
kumsisimua mno
“ Japokuwa kazi nimekubali kuifanya
lakini nathubutu kukiri ina majaribu
makubwa .Mara nyingi huwa sipendi
kufanya kazi ambazo ndani yake
kunakuwa na wanawake warembo kama
Monica.Binadamu siku zote ni dhaifu na
unaweza
ukajikuta
umeanguka
kishawishini na kushindwa kuitekeleza
kazi yako ipasavyo.Nitajitahidi sana hilo
lisitokee.Nakumbuka nliwahi kutumwa
kazi na rais aliyetangulia kabla ya Ernest
kuwasaka watu waliotaka kumuua Boaz
na nikajikuta nimezama mapenzini na
mtoto wake Maria.Sitaki kilichotokea
wakati ule kinitokee sasa na kusababisha
kutetereka kwa mahusiano yangu na
Maria.Ninampenda sana na sitaki
kumuumiza.Yeye ndiye sababu ya mimi
kuendelea kuwa hai hadi sasa.Yeye ndiye
aliyemshawishi baba yake akalipa kiasi
kikubwa cha pesa walichokitaka
wanamgambo wa Alshabaab wakaniachia
huru.Ninamuheshimu sana Maria na siku
zote atabaki kuwa mwanamke wa pekee
kabisa katika maisha yangu” akawaza
Austin akainuka na kuelekea chumba cha
kulaa.tayari umekwisha kuw ausiku
mwingi
 
SEHEMU YA 51

wa sekunde kadhaa sasa David
Zumo alikuwa amepiga magoti pembeni ya
mwanamke mrembo kuliko wote Afrika
Monica Benedict Mwamsole aliyekuwa
amelala kifudi fudi huku wote wakiwa
watupu sebuleni .David alikuwa anahema
kwa kasi kubwa na jasho jingi
likimtiririka.Macho yake aliyaelekeza kwa
mwanamke aliyelala pembeni yake
ambaye alikuwa analia kwa kwikwi
“ Ni vigumu kuamini lakini ni
kweli.Monica
hajawahi
kumjua
mwanaume na mimi ndiye mwanaume
wake wa kwanza.Huyu ni mwanamke wa
kipekee kabisa .Wanawake wanaotunza
bikira zao hadi umri kama huu wa Monica
ni wachache mno katika ulimwengu wa
sasa.Laiti ningejua Monica bado ni bikira
ningesubiri hadi tutakapofunga ndoa
kwani naamini kabisa hawezi kukataa”
akawaza David
“ Najisikia fahari kubwa kuwa
mwanaume wa kwanza kumjua Monica.Hii
ni heshima kubwa kwangu na lazima
niitunze.Nitamuweka Monica katika nafasi
ya juu mno.Nitampa heshima ya kipekee
kabisa mwanamke huyu wa pekee ambaye
sikuwahi kuota kama nitaweza kumpata
katika maisha yangu.” Akawaza David
huku akiendelea kumtazama Monica
aliyekuwa amejilaza kitandani akilia kwa
kwikwi.Akamuinua na kumfuta machozi
“ Pole Monica.Tafadhali nyamaza
kulia” akasema David akimfuta Monica
machozi
“ Najua umeumia Monica lakini
nakuomba usiendelee kulia malaika
wangu.” Akasema David Zumo.Monica
akamtazama na kusema
“ Umenishawishi tukafanya mapenzi
na umeniondolea bikira yangu ambayo
ilikuwa ni zawadi kwa mwanaume wa
maisha yangu” akasema Monica na
kuendelea kumwaga machozi
“ Monica malaika wangu usilie
tafadhali.Hata mimi ninajilaumu sana kwa
hiki kilichotokea.Laiti kama ningejua
mapema ningejitahidi kujizuia lakini
tayari imeshatokea kwa hiyo nakuomba
unifanye mimi niwe mwanaume wako wa
kwanza.Nifanye mimi niwe mfalme
wako.Monica wewe ni mwanamke wa
pekee kabisa kuwahi kukutana nawe.Ni
nadra sana kwa zama hizi kukutana na
mwanamke aliyetunza usichana wake hadi
kufikia umri kama wa kwako.Unastahili
pongezi na heshima ya kipekee
kabisa.Mimi kama mwanaume wako wa
kwanza ninaomba unipe nafasi Monica ili
nikupe heshima unayostahili mwanamke
kama wewe.Naomba nikuonyeshe namna
ninavyokupenda .Nipe ruhusa nikuinue
juu ya wanawake wote wa dunia hii.Kubali
kuolewa nami Monica “ akasema David
Monica akaupeleka mkono sirini
akautazama,
ulikuwa
na
damu,akamtazama David na kusema
“ Umenitoa bikira yangu ambayo
nimeitunza kwa miaka hii yote kwa ajili ya
mwanaume Yule ambaye atakuwa wa
pekee kwangu,mwanaume ambaye
nitamkabidhi moyo wangu autunze zaidi
ya mboni ya jicho lake.Bikira hiyo
imekuwa ikinipa ujasiri na subira ya
kumsubiri mwanaume wa ndoto zangu .Ni
 
SEHEMU YA 52

kitu nilichojivunia na kukithamini mno
lakini kwa sasa baada ya kuiondoa
nimekua mtu wa kawaida nisiye na
thamani tena.Kwa kuwa wewe ndiye
uliyenitoa usichana wangu siwezi
kulikataa tena ombi lako la kutaka
kunioa.Ninakubali kuolewa nawe ila
nomba yale yote uliyoniahidi yawe ya
kweli.” Akasema Monica.David hakumpa
nafasi ya kuendelea zaidi akapagawa kwa
jibu lile la Monica akajikuta
amemkumbatia kwa nguvu na kuanza
kumporomoshea mabusu katika sehemu
mbali mbali za mwili
“ Ahsante Monica.Ahsante malaika
wangu kwa kukubali ombi langu.Sijui
nikwambie nini Monica kuhusu furaha
niliyonayo kwa kulikubali ombi
langu.Nakuahidi hautajutia uamuzi wako
.Nakuahidi nitakupenda zaidi ya upendo
wenyewe.” Akasema David na kumbusu
Monica
“ Sasa twende chumbani ukapumzike
malaika wangu,siku yetu imekuwa nzuri
na njema sana .Kesho tutakuwa na
maongezi mengi zaidi kuhusiana na
maisha yetu.” akasema David akambusu
Monica na kumshika mkono akamuinua
wakaelekea katika chumba cha kulala.
“ Hiki ni chumba chako cha kulala
malkia wa Congo.Panda kitandani
upumzike ewe mzuri wa wazuri” akasema
David Zumo akambusu Monica na kutoka
mle chumbani.Monica akaingia bafuni
kuoga.Kwa dakika kadhaa alikuwa
amesimama bafuni akitafakari
“ Sielewi nini kimenitokea hadi
nikajikuta kwa hiari yangu nikimvulia
nguo David.Nahisi huyu jamaa anatumia
uchawi kwani mimi ni mtu mwenye
msimamo mkali linapokuja suala la haya
ya mapenzi lakini najishangaa kwani leo
nimejikuta mwenyewe nikichojoa nguo na
kufanya mapenzi.I’m so weak and
stupid...” akawaza Monica huku akijipiga
vibao shavuni
“ So this is it.Bikira yagu
imeondolewa na sina tena cha
kujivunia.Imenilazimu nikubali kuolewa
na David Zumo .Hata hivyo nikimtazama
David anaonekana ananipenda kwa dhati
ya moyo wake na hata mke wake pia
amenikubali .Ngoja tu niolewe na David
japokuwa nitakuwa mke wa pili lakini
 
SEHEMU YA 53


hakuna tatizo kwani Pauline mke wa
David ameridhia jambo hilo “ akaendelea
kuwaza Monica huku akioga

David
anaonekana
kuchanganyikiwa kabisa na mimi .Sijui
amechanganyikiwa na nini lakini nahisi
lengo lake kubwa yeye na mke wake ni
kupata mtoto kutoka kwangu.Sipati picha
hiyo harusi yetu itakuaje.Mhh ..!! mwili
wote unanisisimka.Halafu kuna jambo
ambalo bado sijapata muafaka
wake.Nikiolewa na David najua atanitaka
niishi hapa Congo karibu naye lakini kama
nitakubali kuishi hapa nitaendeshaje
program zangu? Hapana sitaki kuishi
Kinshasa ,nitaishi Tanzania” akawaza
Monica.Picha nyingi za haraka haraka
zikamjia kuhusiana na maisha
atakayoyaishi baada ya kuolewa na David
Zumo.Akatabasamu
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Kijua tayari kimekwisha chomoza
kuashiria mwanzo wa siku nyingine
.Austin tayari alikuwa katika chumba cha
mazoezi akiweka mwili sawa kuikabili
siku.Alipomaliza kufanya mazoezi akatoka
akaelekea jikoni akafungua mojawapo ya
kabati
akatoa
kitu
Fulani
alichokitengeneza mara tu alipoamka
asubuhi akakichunguza kwa makini halafu
akakiweka katika boksi na kuliingiza
boksi lile katika begi la mgongoni
“ I’m back to work
again.Sikutegemea kabisa kama nitarejea
tena katika mambo haya” akawaza na
kutoka mle jikoni akaenda bafuni akaoga
halafu akarejea tena jikoni akaandaa
stafstahi.Alikunywa chai kwa haraka
akiwa amesimama na alipomaliza
akachukua begi lake la mgongoni
alimoweka lile boksi lenye kifaa Fulani
ndani yake .Akaenda tena chumbani
akafungua sanduku kubwa na ndani yake
akatoka sanduku lingine la kadiri
akalifungua.Lilikuwa limesheheni silaha
ndogo ndogo.Akachukua bastora mbili
pamoja na vifaa vingine vichache ambavyo
vingeweza kumsaidia.Kabla hajatoka
alihakikisha kamera tatu za ulinzi
alizofunga zinafanya kazi vizuri.Kamera
 
SEHEMU YA 54


zile ndogo lakini zenye uwezo mkubwa
ziliunganishwa na mfumo wa kompyuta
ambao uliweza kutuma picha za kila
kilichokuwa kinaendelea moja kwa moja
katika miwani maalum aliyoivaa.Mara tu
anapoivaa miwani hiyo na kugusa sehemu
Fulani yenye kitu mfano wa doa jeusi
sehemu moja ya miwani hiyo hubadilika
na kuanza kupokea picha toka katika
kamera zilizoko nyumbani kwa hiyo
kumuwezesha kujua kinachoendelea .Hii
ilikuwa teknolojia ya hali ya juu sana
“ It’s perfect.” Akasema na kutoka
akafunga nyumba na kuelekea katika
maegesho zilikoegeshwa gari tatu mpya
.Akachagua moja ambalo aliona lingemfaa
kwa shughuli anayokwenda kuifanya
kisha akaondoka
“ Filimbi tayari imepulizwa sasa
kinachofuata ni kuingia vitani.” Akawaza
akiwa garini na mara akamkumbuka
mpenzi wake Maria.
“ Leo atasaini mkataba na Alnoor na
kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba
mara tu atakapomaliza masuala
yaliyompelekea Dubai ,moja kwa moja
atapanda ndege kuja Tanzania.Ni wiki ya
tatu sasa hatujaonana na imekuwa ni
kama miezi mitatu kwetu .She loves me a
lot na hata mimi ninampenda mno zaidi
ya ninavyoweza kueleza lakini suala la
yeye kuja dar es salaam bado siliafiki
kabisa kwani ni hatari mno kwake.mambo
yatakayotokea ndani ya siku chache zijazo
ni mambo ya hatari na sitaki mwanamke
nimpendaye kuliko wote aingie katika
hatari.Nasikitika kwamba sina cha
kufanya
kumzuia
asije
Tanzania.Nilishindwa kumueleza ukweli
kwa hiyo lazima atakuja dar es slaam”
akaendelea kutafakari akiwa amesimama
katika taa za kuongozea magari.
“ Kuna kitu kimoja ninachoweza
kufanya ili kumzuia Monica asije dar .Ni
kuacha kuwasiliana naye.Nikifanya hivyo
hata kama akija Dar hatajua namna ya
kunipata na ataondoka kurejea afrika ya
kusini.Ni bora nikafanya hivyo kwa ajili ya
usalama wake yeye mwenyewe ingawa
najua ataumia na atanichukia sana lakini
sina ujanja.Nitamuelewesha huko mbele
ya safari naamini atanielewa.” Akaendelea
kuwaza Austin na sura ya Monica ikamjia
 
SEHEMU YA 55

Sura ya binti malaika huyu inanijia
kichwani kila mara.Ngoja kwanza
nishughulikie kazi ya kwanza ya
kumuondoa hospitali Marcelo na baada ya
hapo nitajipanga wa ajili ya Monica.”
Lango la kuingilia hospitali ya Mt
Lucia lilikuwa wazi,watu na magari
walikuwa wakipita bila kikwazo
chochote.Hakukuwa na ukaguzi wowote
japokuwa walikuwepo walinzi waliovalia
sare za kampuni binafsi ya ulinzi
.Kulikuwa na magari mawili mbele ya
Austin yakiingia mle hospitali .Austin kwa
haraka haraka akachunguza ulinzi ulivyo
pale getini akatabasamu
“ Hakuna ulinzi wowote wa maana
hapa getini.Hawa walinzi wako hapa
kutangaza kampuni yao tu” akawaza
wakati akivuka geti na kukutana na kibao
kilichomuelekeza sehemu ya kuegesha
gari.Ilipata saa tatu na dakika ishirini na
tayari eneo la maegesho lilisheheni
magari .Austin akachukua kofia nyeusi
akavaa pamoja na miwani ile ya
kielektroniki yenye kuweza kufanya
mambo kadhaa kwa wakati
mmoja.Akahakikisha bastora zake
zimekaa vizuri kisha akachukua begi
akashuka.Ilikuwa ni mara yake ya kwanza
kufika katika hospitali hii kubwa
iliyokuwa na bango kubwa lenye ramani
ya hospitali ikielekeza namna ya kufika
katika sehemu mbali mbali za hospitali ile
.Taratibu huku akiyasoma mazingira
Austin akakamata njia iliyoelekea ziliko
wodi za kulaza wagongwa..
“ Hospitali ya kisasa sana hii.Ina
miundo mbinu mizuri lakini kuna kasoro
moja tu kubwa,hakuna usalama” akawaza
Austin akiwa amezifikia wodi . akakutana
na bango lingine lililoelekeza namna
mpangilio wa wodi ulivyo ukianzia na zile
wodi za watu maalum.Kwa kufuata
maelekezo ya lile bango akafika katika
wodi za watu maalum.Kulikuwa na pilika
pilika nyingi eneo hili hivyo hakuna
yeyote aliyekuwa na muda wa kumfuatilia
Austin.Alichunguza eneo la chumba
alimolazwa Dr Marcelo na kuondoka
akaelekea
katika
jengo
la
mapokezi.Lilikuwa ni jengo kubwa la
ghorofa nne.Watu walikuwa wengi katika
jengo hilo na Austin akajumuika nao huku
akiyasoma mazingira ya mle ndani
 
SEHEMU YA 56

yalivyo.Alitoka mle ndani akaelekea
katika bustani nzuri iliyokuwa karibu na
jengo la mapokezi.Begi lake akaliweka
pembeni na alioneka kama mtu aliyekuwa
akisubiria huduma.Akapita kijana muuza
magazeti akanunua gazeti moja akaanza
kusoma huku akichunguza mazingira
yalivyokaa.Alipohakikisha hakukuwa na
mtu yeyote aliyekuwa anamtilia shaka
akalifungua begi lake na katika lile boksi
lililokuwa na kifaa ndani yake akabonyeza
kidude Fulani kilichokuwa mithili ya saa
kikaanza kuandika namba kwa haraka
haraka,akalifunga begi na kuliweka
pembeni na kwa kutumia mguu wake
akalisogeza katika maua halafu
akaangaza tena pande zote lakini
hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa
anamfuatilia.Taratibu akainuka akaingia
tena katika jengo la mapokezi halafu
akatoka na kuanza kuelekea ziliko
wodi.Alipokaribia chumba cha Marcelo
akatoa kitu Fulani mithili ya simu
akabonyeza namba kadhaa na mara
ukatokea mlipuko mkubwa karibu na
jengo la mapokezi.Kizaa zaa kikubwa
kikaibuka hapo hospitali watu wakaanza
kukimbia hovyo kunusuru maisha yao.
Taharuki ile ndiyo aliyokuwa
anaihitaji Austin ili afanikishe kazi
yake.Akachomoka kama mshale hadi
katika chumba cha Marcelo.Hakukuwa na
daktari yeyote mle chumbani ,alikuwemo
Dr Marcelo pekee akiwa hajui afanye
nini.Marcelo akastuka sana kwa namna
Austin alivyoingia mle chumbani
“ Are you Marcelo? Akauliza Austin
“ yes “ akajibu Marcelo kwa wasiwasi
“ Good.My name is Austin and I’m
here to take you out of here.Naomba
ufuate maelekezo yangu” akasema Austin
“ Wewe ni nani? Umetumwa na nani?
“ Marcelo ninao muda mchache sana
wa kufanikisha zoezi la kukutoa hapa kwa
hiyo nahitaji ushirikiano wako.” Akajibu
Austin huku akimshika mkono Marcelo na
kumtaka ainuke
“ Siendi kokote bila kufahamu ni
nani aliyekutuma” Marcelo akagoma
“ What ??..akauliza Austin
“ Najua umetumwa uje unichukue
ukaniue.Naomba uniulie hapa hapa ila
 
SEHEMU YA 57

huko unakotaka kunipeleka siendi”
akasema Marcelo.
Austin akavua kofia na kumtazama
Marcelo
“ Nisikilze kaka.Kazi yangu ni
kukuondoa hapa na kukupeleka sehemu
salama kwa hiyo sina muda wa mabishano
na wewe.Kuna mambo mawili ya
kuchagua ,aidha ufuate maelekezo yangu
nikutoa hapa au nikutoe humu kwa
nguvu” akasema Austin kwa sauti ya ukali
wakaendelea kutazamana
“ Are we going or you want me to use
force? Akauliza Austin.Marcelo akatikisa
kichwa ishara ya kukubaliana na Austin
Haraka haraka Austin akamuinua
Marcelo akamuweka begani na
kuchungulia nje ambako bado taharuki
ilikuwa imetanda na watu wakikimbia
hovyo kunusuru maisha yao.Akaangaza
pande zote kuhakiki usalama
“ It’s clear” akasema taratibu na
kuingia katika gari lake akaondoka eneo
lile akipishana na magari mawili ya zima
moto yaliyofika kwa haraka sana huku
magari matatu ya polisi yaliyosheheni
askari yakifika kwa haraka
“ Nini kimetokea hapa? Nimesikia
kishindo kikubwa kama mlipuko na watu
wakaanza kukimbia huku wakipiga
makelele na ghafla ukatokea chumbani
kwangu.Who are you? Nani kakutuma uje
unitoe hapa hospitali? Unahusika na
kilichotokea hapa? Akauliza Marcelo
lakini Austin hakumjibu kitu akaendelea
kuendesha gari kwa umahiri kuhakikisha
hakuna mtu anayemfuatilia
“ C’mon brother I deserve to know
who are you? Who sent you and where are
you taking me? Akauliza Dr Marcelo .Bado
Austin hakumjibu chochote
“ Huyu mtu ni nani? Ametumwa na
nani aje anitoe pale hospitali?Ananipeleka
wapi? Maswali haya yalimuumiza sana
Kichwa Dr Marcelo
“ Kuna mtu mmoja tu ambaye
nilimueleza tatizo langu na nikamuomba
anisaidie ambaye ni Monica.Inawezekana
huyu jamaa ametumwa na Monica au
ametumwa na wale jaama wanaotaka
kuniua? Lakini nikimtazama kwa makini
haonyeshi kama ana lengo la kuniua.Kama
ni Monica ndiye aliyemtuma sijui
nitamshukuruje kwani nisingemaliza siku
 
SEHEMU YA 58


mbili bila kuuawa.Asubuhi ya leo
niliwaona watu wao wawili wakiongea na
daktari na baada ya hapo daktari akaja
akanipima na kuondoka.Kilichoniweka hai
hadi sasa ni kwa sababu nilijifanya siwezi
tena kuongea.Natakiwa niikimbie nchi
kwani endapo nitaendelea kukaa humu
nchini lazima watanisaka na kuniua.”
Akawaza Dr Marcelo wakati gari likikata
mitaa ya jiji huku akiwa hajui ni wapi
alipokuwa anapelekwa.
“ Nimewastua na mlipuko ule wa
fataki
wamechanganyikiwa
kabisa.Kimetokea kizaa zaa cha kutisha
pale hospitali” akawaza Austin huku
akitabasamu kwa mbali
“ Kazi ya kwanza kati ya mbili za rais
nimeimaliza.Imekuwa ni kazi nyepesi mno
zaidi ya nilivyotazamia japokuwa
nimetumia nguvu kubwa kidogo lakini
nimefanya vile ili kuwapoteza lengo watu
waliokuwa na nia ya kumuua
Marcelo.Ninaamini kabisa kama kweli
huyu jamaa alikuwa anataka kuuawa basi
lazima kuna watu waliowekwa pale
hospitali kumfuatilia na nisingeweza
kumtoa pale kirahisi bila ya kuonekana
lakini kwa njia hii niliyoitumia naamini
hata wao kama walikuwepo lazima
walikimbia
kunusuru
maisha
yao.Nasikitika kishindo kile cha mlipuko
kinaweza kuwa kimesababisha madhara
kwa baadhi ya wagonjwa hasa wenye
matatizo ya moyo lakini sikuwa na namna
nyingineya kufanya ili kumuokoa
Marcelo.”akawaza Austin
 
SEHEMU YA 59


KINSHASA – DRC
Muziki wa ala uliosikika kwa sauti ya
chini ulimfanya Monica aote ndoto nzuri
.Alikuwa katika uwanda mpana wenye
nyasi nzuri za kijani.Vijito vya maji
vikitiririka katika kila kona ya uwanda
huu wa kuvutia mno.Ndege wa rangi mbali
mbali wakubwa wa wadogo walikuwa
wanaruka .Upande wa juu watu waliovalia
nadhifu walikuwa wamejipanga katika
mstari wakiimba na wengine walikuwa
pembeni wakipiga vyombo vya
muziki.Ulikuwa ni muziki mtamu
ulioburudisha.Pembeni na pale alipokuwa
amekaa kulikuwa na wanawake zaidi ya
sita wakiwa tayari kumuhudumia kwa
chochote
akitakacho.Tabasamu
halikukauka .Alikuwa amevaa taji la
dhahabu pamoja na vito vingi vyenye
kung’aa vya thamani kubwa.Alikuwa
anameremeta .Ghafla akastushwa na
kengele iliyolia akakurupuka toka
usingizini.Kulikuwa
na
mtu
mlangoni.Haraka haraka akajifunga taulo
na kwenda kuufungua mlango akakutana
na sura yenye tabasamu ya mwanamama
mmoja wa makamo akamsalimiana
kujitambulisha.
“ naitwa Anna.Ni muhudumu mkuu
wa rais katika jumba hili.Nimefurahi
kukuona malkia wa wangu.Kuna chochote
unahitaji asubuhi hii?
“ hata mimi nimefurahi kukufahamu
Anna.Nitakujulisha baadae endapo
nitahitaji chochote” akajibu Monica na
Anna akaondoka kwenda kuendelea na
shughuli zake.Monica Akakaa kitandani na
kuanza kutafakari kilichotokea usiku
uliopita.”
“Nilifanya ujinga mkubwa sana
jana.Nilimkubalia David kirahisi kufanya
 
SEHEMU YA 60


mapenzi bila hata kutumia kinga.Oh my
gosh ni vipi kama ana magonjwa?
Akawaza na kushika kichwa
“ Lakini hapana David ni mtu
muungwana asingeweza kukubali kufanya
nami mapenzi bila kinga hali akifahamu
kuwa ana matatizo.” Akajipa moyo na
kutabasamu baada ya kuikumbuka ndoto
ile nzuri aliyoiota.
“ Ilikuwa ndoto nzuri ajabu.Sijawahi
kuota ndoto nzuri kama ile katika maisha
yangu.Je ndoto ile inaashiria maisha yangu
yatakavyokuwa huko mbeleni? Kama
nilichokiota katika ndoto ndivyo maisha
yangu yatakavyokuwa basi sikufanya
makosa kukubali kuolewa na David
Zumo.” Akawaza Monica halafu
akamkumbuka Marcelo
“ Marcelo..Hali yake ikoje sasa
hivi?Jana David aliongea na rais wa
Tanzania na akamuahidi kumsaidia
kumtoa pale hospitali.Natamani kujua
kama zoezi hilo limekwisha fanyika au
vipi.Nikionana na David nitamuuliza
kuhusu jambo hili”
Akiwa bado amekaa kitandani huku
akiwaza mambo mengi kengele ya mlango
ikalia akaenda kufungua na kukutana na
David Zumo
“U hali gani Monica? Akauliza David
Zumo aliyekuwa amesimama mlangoni
akiwa amevaa mavazi yale aliyokuwa
ameyavaa usiku yaani ngozi ya chui na
kofia ya manyoya ya Simba.
“ Hallow David” akasema Monica
huku akitabasamau na kuona aibu kwa
mbali.David akaingia ndani
“ Umeamkaje malaika wangu?
Akauliza
“ Nimeamka salama kabisa ,sijui
wewe”
“ Hata mimi nimeamka salama
kabisa.Vipi maendeleo yako?Una hali
yoyote ya maumivu nimuite daktari?
“ Ninahisi maumivu kwa mbali lakini
nitatumia dawa za kutuliza maumivu tu na
nitapona.” Akasema Monica
“ Samahani sana Monica.”
“ Usiogope David.Jambo hili
limeshatokea na limepita kwani hata
kama isingekuwa ni wewe basi angefanya
mwanaume mwingine.Kwa sasa tuachane
na suala hilo tuangalie mengine ya msingi
 
Sehemu ya 46 kama sijaiona hivi, au wenzangu mmeiona mnisaidie?
 
Lege ahsante umekata kiu yetu. Endelea na majukumu sasa ya kikazi. Lakini usiwe unatusahau mda mrefu.
 
Back
Top Bottom