SEHEMU YA 4
ayari ni usiku mwingi na
hakukuwa na magari barabarani hii
ilimpa Amarachi nafasi ya kuendesha
gari kwa mwendo mkali mno
.Ilimchukua dakika kumi na mbili
kuwasili hospitali waliyoelekezwa na
rais.Tayari taarifa za ujio wa Austin
zilikwisha fika na madaktari na wauguzi
tayari walikwisha jiandaa
kumpokea.Haraka haraka akashushwa
garini na kukimbizwa katika chumba
cha upasuaji.
Akiwa nje ya chumba cha
upasuaji,Amarachi akampigia simu Job
“Hallo Job” akasema Amarachi na
kukawa kimya
“Job !! akaita Amarachi
“Amarachi mikono inanitetemeka
ninaogopa hata kupokea simu yako
nikihofia pengine kuna taarifa isiyo
nzuri.Tayari umefika hospitali?
“Usihofu Job.Tayari nimefika
hospitali na tayari Austin amekimbizwa
katika chumba cha
upasuaji.Kinachohitajika hivi sasa ni
maombi.Austin amepoteza damu nyingi
lakini anao nafasi ya
kupona.Anaonekana ni mpambanaji.Hii
ni hospitali kubwa,rais na viongozi wote
wakubwa waserikali hutibiwa hapa kwa
hiyo uhakika wa kupona ni
mkubwa.Tusimame katika maombi na
tumuachie Mungu suala hili
ikimpendeza asimchukue Austin kwa
sasa.Kwa hali aliyokuwa nayo Austin
wakati namfikisha hapa hospitali lolote
linaweza kutokea.Mimi si muoga kabisa
lakini kwa mara ya kwanza nahisi
kuingiwa na woga” akasema
Amarachi.Job akasikika akivuta pumzi
ndefu na kusema
“Austin is strong and he can fight
this.Austin hapaswi kufa.Operesheni hii
yote inamtegemea yeye.Kama
ulivyoshauri tuungane katika maombi
kumuombea.Naamini Mungu ana
makusudi yake kwa jambo kama hili
kutokea .Kama angekuwa hana mipango
mizuri na Austin basi usingetokea kwa
wakati ule” akasema Job
“Hata mimi naamini ni mpango wa
Mungu kwani uliponipigia simu usiku
na kunieleza kwamba tuonane kuna
jambo zito sikutaka kusubiri hadi
kesho.Tayari nilikuwa nimelala lakini
niliamka na kuelekea kwako bila ya
kukutaarifu kuwa ninakuja.Nilipofika
nilifungua geti na kuingia ndani
,nikaelekea katika mlango na nilipotaka
kuufungua nilistuka baada ya kuona
kupitia katika kioo cha mlango jamaa
mmoja anamfungua mwanamke
aliyekuwa ameketi sofani amefungwa
mikono.Baada ya tu ya kumfungua Yule
mwanamke akaongea kitu na Yule
jamaa na mara tu alipogeuka akampiga
pigo moja zito jamaa akaanguka na
kupoteza fahamu.Yule mwanamke
akachukua bastora iliyokuwa mezani
akaelekea mlangoni akashika kitasa cha
mlango ili aufungue atoke mara
akatokea Austin toka ghorofani na
kumuamuru aweke chini silaha
yake,Yule mwanamke akatii na
kubonyea ili kutii amri aliyopewa lakini
ghafla aligeuka kama upepo na kumpiga
risasi Austin akaanguka.Akamfuata pale
chini alipoanguka na kutaka kummaliza
kabisa kwa risasi ndipo nilipomuwahi
risasi ya kiganjani akaanguka chini.Ni
nani yule mwanamke? Anaonekana ni
mtu hatari sana kwa namna alivyo kuwa
mwepesi katika kucheza na silaha.Huyu
Austin ni nani? Akauliza Amarachi.
“Nakubaliana nawe Amarachi
mwanamke huyu ni hatari mno zaidi ya
tunavyodhani.Austin,ni rafiki
yangu,amewahi kufanya kazi katika
idara ya ujasusi ya taifa lakini kwa sasa
anaishi nchini Afrika ya kusini na
amekuja nchini Tanzania kwa mwito wa
rais kuna kazi anamfanyia.Austin na
Yule mwanamke ni wapenzi.”
“Wapenzi?!! Amarachi akashangaa
“Ndiyo ni wapenzi.Suala hili
linaonekana kuwa pana na ndiyo maana
inatubidi tumuombee Aus.