SEASON 7: SEHEMU YA 5
Wakati Monica akiendelea
kumsubiri Austin afike simu yake
ikaita.Zilikuwa ni namba ngeni
.Akapokea.
“ hallow” akasema Monica
“ hallow Monica.Naitwa
Silvanus Kiwembe mkurugenzi wa
idara ya usalama wa
taifa.Nimepewa namba zako na
rais.”akasema Silva.Monica
akastuka na kuogopa.
“ Nini unahitaji mr Silvanus?
Akajikaza na kuuliza
“ Ni kuhusiana na yale
mazungumzo yako na rais jana
usiku.Ana shughuli nyingi siku ya
leo kwa hiyo amenipa namba yako
ya simu na utakuwa unawasiliana
nami kuanzia sasa.” Akasema Silva
“Tayari umekwisha wasiliana
na Austin asubuhi hii? Silva
akauliza
“Hapana bado sijawasiliana
naye” Akajibu Monica kwa kifupi
“Sawa hakuna
tatizo.Ninawatuma vijana wangu
watakufuata mahala ulipo ili
wakati unawasiliana na Austin wao
watafanyakazi ya kutafuta mahala
simu ya Austin inapotokea na
itakuwa ni kazi rahisi kwetu
kumpata” akasema Silva
“Mr Silva ,nilimuahidi rais
kwamba nitafanya kama
alivyoniomba nifanye yaani
kumpigia simu Austin lakini
naomba suala hili lisinifanye
nikashindwa kuwa huru na
kutekeleza majukumu mengine
yanayonikabili.Nina mambo mengi
ya kufanya na sitaki kuzungukwa
na watu wa usalama wa taifa kila
dakika.Baada ya kupiga simu na
mkajua mahala alio Austin nataka
mniache niendelee na majukumu
yangu mengine” akasema Monica
“Monica samahani kama
tumekukwaza kwa namna yoyote
ile .Nafahamu una shughuli zako
nyingi za kufanya lakini hili
tunalokuomba utusaidie ni
muhimu sana hasa kwa wakati huu
ambao taifa linapitia katika
kipindi kigumu.Wewe
unachotakiwa kufanya ni kumpigia
simu Austin na halafu tutakuacha
uende zako na hatutakusumbua
tena.Tusaidie tafadhali” akasema
Silva.Monica akafikiri kidogo na
kusema
“Kwa sasa siko nyumbani
kwangu.Nitakupigia baada ya
muda ili nikueleze mahala
nitakapokutana na hao watu
wako”akasema Monica
“ Ahsante Monica ila naomba
isichukue muda mrefu
sana.Tunahitaji kuanza kumtafuta
Austin asubuhi hii” akasema Silva
na kukata simu
“ Nilifanya kosa kubwa
kumkubalia rais kwamba
nitamsaidia kumtafuta Austin na
sasa tayari wamenza kunisumbua
na wataendelea kunisumbua kwa
sababu wanajua mimi pekee ndiye
mwenye mawasiliano naye.Silva
anasema kwamba kumpata Austin
ni muhimu kwa ajili ya usalama wa
nchi inawezekana Austin ni mtu
hatari kiasi cha kuhatarisha
usalama wa nchi? Nimeanza
kuogopa sana.Sikutegemea kama
siku moja nitajikuta nimebanwa
sahemu kama hii.Ngoja kwanza
nimsubiri Austin ili nizungumze
naye na anielez….” simu ya Monica
ikaita alikuwa ni David Zumo
“Hallo mpenzi” akasema
Monica baada ya kupokea simu
“Malaika wangu umeamkaje
leo?
“Nimeamka salama
kabisa.Vipi maendeleo yako?
“Maendeleo yangu
mazuri.Nimekupigia kujua hali
yako malaika wangu” akasema
David
“Nashukuru David .Mmi
naendelea vizuri
sana.Kinachonisumbua ni
kukuwaza wewe tu” akasema
Monica na david akatoa kicheko
kidogo
“Monica huwezi jua maneno
hayo uliyoyatamka yamenipa
faraja gani ndani ya moyo
wangu.Sauti yako laini ambayo
hupenya ndani kabisa mwa moyo
wangu imekuwa ni kitulizo
kikubwa sana kwa wakati huu
mgumu nilionao.Pauline kaondoka
lakini imekuja zawadi nyingine
ambayo ni wewe. Monica
namshukuru sana Mungu kwa
kunishushia malaika kama wewe.”
Akasema David
“Hata mimi nashukuru sana
David kwa mapenzi makubwa
unayonionyesha.Ni bahati sana
kuwa na mwanaume kama wewe
katika maisha yangu”akasema
Monica
“Monica tuna mengi tutaongea
pale tutakapoonana ila kwa sasa
naomba nikujulishe kwamba muda
si mrefu tutaanza safari ya
kuelekea Kinshasa kuupeleka
mwili wa Pauline na jioni ya leo
nitatuma ndege yangu binafsi kuja
kukuchukua na kukuleta Congo
kuhudhuria mazishi hapo kesho.”
Akasema David.
“Ahsante sana David.Tayari
tunajiandaa mimi na wazazi wangu
na baadhi ya watu kadhaa
watakaotusindikiza kuja msibani.”
“Monica naomba nikutakie
siku njema tutaonana usiku wa leo
utakapowasili Kinshasa.” Akasema
David na kukata simu
“ Afadhali niende zangu
Kinshasa nikapunguze
mawazo.Mambo yaliyotokea jana
na yanayoendelea kutokea hapa
dar es salaam yananiumiza mno
kichwa changu.” Akawaza na mara
mlango wake ukagongwa akaenda
kuufungua akakutana na mama
yake aliyemtaarifu kwamba
wageni wake tayari
wamefika.Monica akaenda
sebuleni akawakuta Austin na
Amarachi wakizungumza na mzee
Ben.Akawasalimu na kuwataka
waelekee chumbani kwake.
“ Karibuni sana Austin na
Amarachi .Hapa ni nyumbani kwa
wazazi wangu.Hapa ndipo
nilipokulia na hiki ni chumba
changu nilichoishi toka nikiwa
mdogo .Austin vipi hali yako?
Akauliza Monica
“Hali yangu ni
nzuri.Ninaendelea vyema.Vipi
wewe unaendelea je?
“Sijaweza kupata usingizi
kabisa,kila nikifumba macho tukio
la jana usiku linanijia kichwani.Ni
tukio baya kuwahi kunitokea
katika maisha yangu” akasema
Monica
“Pole sana” akasema Austin
.Monica akamtazama Amarachi na
kusema
“Amarachi naomba
nizungumze na Austin peke yake
kwa dakika kadhaa.Is that ok with
you sweetheart?
“Hakuna tatizo” akasema
Amarachi.Monica akampeleka
katika sebule yake halafu
akamuita mtumishi na kumuomba
amuhudumie Amarachi kwa chai
wakati akiendelea kuzungumza na
Austin
“Austin” akaanzisha maongezi
Monica
“Kwanza samahani sana kwa
mambo yote yaliyotokea
jana.Nilikutamkia maneno makali
kutokana na hasira na sikuwa
nikifikiri sawa sawa” akasema
Monica
“Usijali Monica.Hata mimi
nilifahamu hilo” akasema Austin
“Nashukuru
Austin.Nimelazimika kukuita hapa
ili tuzungumze mimi na wewe
kama marafiki na watu wa karibu
kuhusiana na tukio lile la
jana.Sijaweza kulala usiku
nikiwaza juu ya tukio
lile.Nilijilazimisha kuiaminisha
akili yangu kwamba ile ilikuwa ni
ndoto lakini ukweli utasimama
kuwa ile haikuwa ndoto bali ni kitu
cha kweli.Austin mimi na wewe
tumefahamiana katika ipindi
kifupi na katika muda huo mfupi
tumekuwa marafiki
wakubwa.Naomba tutumie muda
huu mchache tulioupata asubuhi
hii kuongea kama marafiki,kama
ndugu na tuelezane ukweli.Nataka
nikufahamu Austin wewe ni nani?
Unashughulika na nini? Sitaki
uniambie kwamba wewe ni meneja
sijui wa kampuni gani na unataka
kushirikiana name katika miradi
ya kijamii.Nieleze ukweli
nikufahamu Austin.Baada ya
kunijibu hilo ndipo tutaendelea na
mambo mengine” akasema
Monica.Austin akamtazama
Monica ambaye macho yake
aliyakaza kumtazama halafu
akasema
“Monica kabla ya kukueleza
chochote ,napenda nitumie nafasi
hii kukushukuru sana sana kwa
msaada wako mkubwa ulionisaidia
jana usiku.Vile vile samahani sana
kwa kukuingiza katika matatizo
makubwa .Haikuwa dhamira
yangu kufanya vile lakini sikuwa
na sehemu nyingine ya kuomba
msaada zaidi yako” akasema
Austin na kunyamaza
kidogo.Monica hakujibu
chochote.Austin akaendelea
“Umetaka kufahamu mimi ni
nani.Nitakueleza kwa ufupi.Jina
langu halisi ni Austin January
.Mimi ni mtanzania lakini kwa sasa
makazi yangu ni Afrika kusini na
nina uraia wa Afrika kusini.Kuna
hadithi ndefu kidogo hapa
iliyonifanya hadi niamue
kuchukua uraia wa Afrika
kusini.Wazazi wangu wote wawili
wamekwisha tangulia mbele za
haki .Ninaye mdogo wangu
anaitwa Linda ambaye kwa sasa
yuko nje ya nchi” Austin
alipomkumbuka Linda akasikia
kama mapigo ya moyo yanaanza
kumuenda mbio
“Linda atakuwa katika hatari
kubwa hivi sasa.Rais anaweza
akamtumia kama chambo ili
kunilazimisha nifanye kitu
anachotaka kwani anajua niko
tayari kufanya kitu chochote kwa
ajili ya mdogo wangu…”
“ Austin !! akaita Monica
baada ya kumuona Austin
amezama katika mawazo ghafla
“Sorry kuna kitu kilikuwa
kimenijia akilini kuhusiana na
mdogo wangu.Tuendelee”
akasema Austin
“ kazi yangu ni ujasusi”
Sura ya Monica ikabadilika na
kuonyesha woga aliposikia
maneno yale ya Austin
“Nimewahi kufanya kazi
katika idaraya ujasusi wa taifa
hadi pale nilipoamua kuachana na
kazi hiyo na kuanza maisha
mengine.Nimerudi Tanzania hivi
karibuni baada ya rais kuniita na
kuniomba nije kumfanyia kazi
yake binafsi.Ilinilazimu kukubali
kuifanya kazi ya rais kwa ajili ya
kumsaidia mdogo wangu
aliyekuwa amefungwa nchini
China kwa kujihusisha na biashara
ya dawa za kulevya.Nilikubaliana
na rais kumfanyia kazi yake na
yeye anisaidie kumtoa mdogo
wangu gerezani.Kwahiyo hayo ni
maelezo mafupi kuhusu mimi”
akasema Austin.Sura ya Monica
ikaonyesha kukasirika
“You lied to me !! akasema
“Nilipokuja hospitali
nikamkuta rais nikakuuliza kama
unafahamiana na rais ukasema
kwamba ni mtu wako wa karibu
kwani alikuwa anafahamiana na
wazazi wako.Kwa nini hukunieleza
ukweli Austin? Kwa nini
ukanidanganya? Akauliza Monica
“Sorry Monica.Ni kweli
nilikudanganya.Nisingeweza
kukueleza ukweli kwani sisi
tunaojihusisha na kazi hizi huwa
hatuweki wazi kuhusu kazi yetu na
ndiyo maana katika kazi hizi wapo
hadi makasisi lakini ni majasusi
.Ukweli sikuwa nikifahamiana na
rais hadi aliponitafuta yeye
mwenyewe na kuniomba
nimfanyie kazi yake.Hiyo pekee
ndiyo sababu ya ukaribu wangu na
yeye” akasema Austin
Monica akamtazama ,akameza
mate na kusema
“I want to know one
thing.Ulipokuja kwangu
ukajitambulisha kwamba wewe ni
meneja wa kampuni kubwa ya
utalii na unataka kushirikiana na
kampuni yangu katika miradi ya
kijamii.Nini hasa lilikuwa lengo
lako? Ni kweli ulihitaji
kushirikiana nami au ulikuwa na
lengo lingine? Akauliza Monica.
“Ni kweli ninasimamia
kampuni kubwa ya utalii
inayomilikiwa na mtanzania
anaitwa Boaz ambaye ni baba wa
aliyekuwa mpenzi wangu Maria,
lakini kuja kwangu kwako
kulikuwa na lengo lingine zaidi ya
kutaka kushirikiana nawe katika
miradi ya kijamii.Ile ilikuwa ni
namna ya kutafuta ukaribu mimi
na wewe ili lengo langu litimie.”
Akasema Austin na sura ya Monica
ikaonyesha hasira
“Nini hasa lilikuwa lengo lako?
Ulikuwa unanichunguza? Akauliza
Monica kwa ukali
“Monica kuna jambo ambalo
unapaswa kulifahamu lakini wapo
wahusika ambao wanatakiwa
kukujulisha jambo hilo na si mimi”
akasema Austin
“Austin wewe ni rafiki yangu
na ninakuthamini sana na ndiyo
maana kila siku lazima nifahamu
maendeleo yako.Kama kweli na
wewe unanithamini na kunijali
naomba unieleze hicho ambacho
unakifahamu kinanihusu mimi ”
akasema Monica
“Monica kama nilivyokueleza
kwamba wapo watu ambao
wanapaswa kukufahamisha
kuhusu suala hilo na si mimi.Subiri
muda muafaka utakapofika
utafahamishwa kila kitu”
Monica akaendelea
kumtazama Austin halafu akasema
“Jana usiku kuna jambo
ulitaka kunieleza ni jambo gani?
Au uliokuwa unanidanganya ili
nikusaidie katika tatizo lako?
“Nilichotaka kukueleza jana
ndicho hicho ninachokwamba
kwamba wapo watu maalum
watakaokueleza .Nilikuwa tayari
kukueleza jana lakini baadae
baada ya kujitafakari nikaona
haitakuwa busara kama nitaingilia
majukumu ya watu
wengine.Monica ulinieleza simuni
kwamba una jambo unataka
kuzungumza nami.Naomba
tujielekeze katika jambo uliloniitia
hapa na hayo mengine tuyaweke
pembeni” akasema Austin
“Austin nilikuita hapa ili
nikufahamu vyema kwani usiku
mzima nimekuwa nikitafakari
wewe ni nani .Mambo niliyoyaona
ukiyafanya jana yalinistua
mno.Nashukuru kwa kuamua
kuwa muwazi na kunieleza kuhusu
wewe lakini lipo jambo la muhimu
nililokuitia hapa”akanyamaza
kidogo na kuendelea
“Jana baada ya kurejea
nyumbani kutoka Zanzibar,mama
alinifuata akaniambia kwamba
ninahitajika ikulu.Rais anataka
kuniona.Niliongozana na mama
pamoja na walinzi wawili wa ikulu
nikaenda kuonana na rais.”
“Ulienda ikulu usiku ule?
Austin akauliza
“Ndiyo nilikwenda baada ya
kuitwa na rais.Tulingia katika
chumba cha maongezi ya faragha
tukiwa mimi na rais pekee.Rais
alinihoji kilichowatokea wale
walinzi waliotumwa kunipeleka
Zanzibar ambao walikutwa katika
gari lao wamefungwa na hata wale
wa Zanzibar waliokutwa hawana
fahamu katika gari lao.Akataka
kufahamu nini kilichotokea?
Nilikuwa na hasira sana
ikanilazimu kumueleza ukweli
wote kuwa ni wewe ndiye
uliyeniomba niwasiliane naye na
wewe na wenzako ndio
mliowapoteza fahamu wale walinzi
wa Dar es salaam na kule
Zanzibar.Rais alistuka sana na
hasa pale nilipomweleza kwamba
mlikwenda Zanzibar kumchukua
yule mwanamke niliyesikia
mkimtaja kwa jina moja la
Yasmin.Rais alinihakikishia
kwamba suala lile atalimaliza na
hakutakuwa na tatizo lolote kwa
upande wangu lakini akanitaka
nimsaidie kitu kimoja.Akataka
niwasiliane nawe asubuhi ya leo
halafu niombe tuonane kisha
nimjulishe mimi na wewe
tumepanga tuonane wapi ili atume
vijana wake waje
wakuchukue.Niliporejea nyumbani
nilitafakari sana suala hili
nikajiuliza kwa nini rais anitumie
mimi kukupata wewe wakati wewe
na yeye ni watu wa karibu? Kama
lengo lake ni zuri kama anavyodai
kwa nini asikupigie simu yeye
mwenyewe mkaonana? Kitu
kingine kilichonishangaza ni jana
uliponifuata na kunitumia mimi
kuwasiliana na rais.Nimejiuliza
kwa nini mimi? Kwa nini
msiwasiliane nyie wenyewe? Kuna
tatizo gani hapa?Nimeona
ninataka kujingiza katika hatari
kubwa nisiyoifahamu ndiyo maana
nikaamua nikuite asubuhi hii ili
tuzungumze na nifahamu nini
hasa kinachoendelea kati yako na
rais? Kwa nini mniweke mimi kati
kati? Kitu kingine ninachotaka
kufahamu yule mwanamke Yasmin
ni nani hadi ukahatarisha maisha
yako na yetu namna ile? Kwa nini
rais alipomsikia Yasmin alistuka
na kuogopa sana? Hayo ndiyo
mambo niliyokuitia hapa.Nataka
kuufahamu ukweli” akasema
Monica
“Monica sipati neno zuri la
kukushukuru kwa hiki
ulichokifanya.Nimeamini kweli
unanithamini na kunijali.Kwa hili
ulilolifanya nakuahidi baadae
nitakueleza kile nilichotaka
kukueleza jana.Jambo ulilolifanya
ni kubwa sio kwangu tu bali kwa
nchi.Ahsante sana Monica”
akasema Austin
“Kuna mambo mazito
yanaendelea hapa nchini bila watu
kuyafahamu.Ili twende sawa
itanilazimu nikueleze ukweli wote”
Akasema Austin na kumsimulia
Monica kuhusiana na Alberto’s na
yeye kutaka kuuawa Somalia hadi
alivyokombolewa na kwenda
kuishi Afrika kusini.
“Baada ya kikwazo
kuondolewa ambacho kilikuwa ni
mimi,Alberto’s waliendela na
mikakati yao ya kujimarisha hapa
nchini na walifanikiwa kuusimika
utawala wao na Ernest Mkasa
akiwa ni kiongozi wa kwanza wa
Tanzania kuwa chini yao.Rais
Ernest amechaguliwa na wananchi
kwa kura nyingi lakini amekalia
kiti cha urais kama sanamu.Hana
maamuzi yoyote bali nchi
inaongozwa na Alberto’s.Wao ndio
wenye kupanga kila kitu kiende
vipi hapa nchini na Ernest ni
mtekelezaji tu wa maelekezo
yao.Alberto’s tayari wamekwisha
imarisha mizizi yao hapa
nchini.Tayari wana mzizi wao
mkuu ambaye ni rais ,pia yupo
makamu wa rais,waziri
mkuu,wanayo pia idadi kubwa ya
wabunge wafuasi wao bungeni
.Wamejiimarisha katika sehemu
zote za muhimu ili kusitokee
kukwama katika sehemu yoyote na
ndiyo maana hivi karibuni ulitaka
kupelekwa muswada bungeni wa
haki za binadamu ambao ndani
yake una vipengele vinavyotamka
kuwatambua watu wanaojihusisha
na mapenzi ya jinsia moja,utoaji
mimba nk.Nadhani mpaka hapo
tayari umepata picha namna hawa
jamaa wanavyoliharibu taifa letu.”
Akasema Austin baada ya muda
akaendelea
“Nilipoonana na rais kwa
mara ya kwanza siku aliyokuwa
ananikabidhi kazi yake nimfanyie
nilimuuuliza kama na yeye ni
mfuasi wao akanijibu kuwa yeye si
mfuasi bali ameshinikizwa na wale
jamaa awe rais lakini hapendezwi
na kitendo cha yeye kuwekwa
kama sanamu bila kuwa na nguvu
yoyote kama rais.Nilimshauri
kama kweli anachukizwa na
Alberto’s basi tuunganishe nguvu
na tuwaondoe hapa nchini.Rais
akakubali na nikampa maelekezo
yangu namna ya kuanza
kupambana na
Alberto’s.Nilimshauri kwanza
kuufutilia mbali muswada ule wa
haki za binadamu uliokuwa
unatarajia kuwasilishwa
bungeni.Kama hiyo haitoshi
nilimshauri pia kumuondoa waziri
mkuu katika nafasi yake na
kulivunja baraza lote la
mawaziri.Nikamshauri pia
amuondoe mkuu wa majeshi ili
awe na uhakika kwamba Alberto’s
hawatatumia jeshi
kumuangusha.Yote haya
aliyatekeleza bila tatizo na
mliyasikia”
“Austin haya unayonieleza ni
mambo ya kweli? Akauliza Monica
“Don’t you trust me? Austin
naye akauliza
“Ofcourse I do trust you.Ila
mambo uliyonieleza ni makubwa
na mazito.”
“Ni kweli Monica mambo haya
ni makubwa na yanaogopesha
ukiyasikia lakini ndiyo hali
halisi.Nchi yetu imefikia hapo”
akanyamaza tena kidogo halafu
akasema
“Rais alinipa kazi mbili
nimfanyie.Kazi ya kwanza ilikuwa
ni kumtoa hospitali rafiki yako
Marcelo” akasema Austin na kuzidi
kumshangaza Monica.
“Ni wewe ndiye ulimtoa
Marcelo hospitali?!! Akauliza
Monica.Alishangaa sana
“Ndiyo ni mimi.Rais alipokea
ombi toka kwaDavid Zumo na
akanipa mimi kazi ya kwenda
kumtoa Marcelo hospitali.”
Monica akajikuta akiinuka na
kwenda kumkumbatia Austin
“Austin sikujua kama u mtu
muhimu namna hii.Jana
nilikuchukia na sikutaka hata
kukuona tena lakini kumbe
nilifanya kosa kubwa” Akasema
Monica na kama ilivyo kawaida
yake machozi yake yako karibu
sana akashindwa kuyazuia.Austin
akatabasamu halafu akaendelea
“Makubaliano yangu na rais
yalikuwa kuanza operesheni ya
kuwaondoa Alberto’s baada ya
kuzikamilisha kazi zake zote mbili
na wakati nikiwa katika harakati
za kuikamilisha kazi yake ya pili
likatokea lile tukio la kupigwa
risasi na Maria na mambo
yakaanza kuharibikia
hapo.Tuligundua kwamba Maria ni
mfuasi wa kikundi cha kigaidi cha
IS na hapa nchini alikuja kwa lengo
la kumtafuta mama yake anaitwa
Yasmin Esfahani.Huyu Yasmin ni
mfuasi wa IS aliyekuwa
amefungwa mahala pa siri hapa
nchini kwa zaidi ya miaka
kumi.Tulianza kumtafuta Yasmin
na ilinilazimu kumuuliza rais
kama ana taarifa zozote za
kuhusiana na Yasmin akasema
kwamba hana taarifa zozote na
akaomba nimpe muda ili alifanyie
kazi suala hilo.Baade aliomba
kuzungumza na Maria na ghafla
Maria akabadili lugha akaanza
kuzungumza kiarabu lugha
ninayoifahamu vyema.Niligundua
kwamba alikuwa anazungumza na
mama yake ambaye ni Yasmin
.Baadae rais akanipigia simu na
kuniambia kwamba anamuhitaji
Maria jana saa nne asubuhi .Mimi
na wenzangu tulijiuliza maswali
mengi kuhusiana na hiki
alichokifanya rais.Alikiri
kutomfahamu Yasmin lakini
baadae akampa simu Yasmin
azungumze na
mwanae.Tulishangaa sana na
kuweka alama ya kiulizo.Jana
ilinilazimu kutumia mbinu
kuzungumza na Yasmin na
tukafikia makubaliano kwamba
nitakapompatia mwanae atanipa
kitu kikubwa.Usiku wa jana
akanipigia simu na kuniomba
nikamchukue Zanzibar kwani
alikuwa katika hatari na ndiyo
maana nikalazimika kuja kwako
kukuomba msaada.Sikutaka rais
afahamu chochote kuhusu mimi
kwenda Zanzibar kwani angejua
lazima ninakwenda kumchukua
Yasmin. Nashukuru ulinisaidia
sana na tukafanikisha kumpata
Yasmin ambaye tunaye mikononi
mwetu.Yasmin kama
nilivyokueleza kwamba ni mfuasi
wa kikundi cha kigaidi cha IS na
alikuwa amefungwa hapa Tanzania
baada ya kukamatwa akiwa katika
harakati za kueneza kikundi cha IS
Afrika mashariki, amenieleza
kwamba aliachiwa huru na rais
baada ya kufanyika makubaliano
kati ya rais na Alshabaab.”
“Alshabaab?!! Monica
akashangaa
“Ndiyo.Rais amefanya
makubaliano na Alshabaab na
katika makubaliano hayo
waliafikiana kwamba Yasmin na
mtu mwingine ambaye amekuwa
mpangaji mkubwa wa
mashambulio mbali mbali ya
Alshabaab anaitwa Tariq
waachiwe huru.Rais alitekeleza
makubaliano yao na kuwaachia
huru Yasmin na Tariq.Wakiwa
Zanzibar Yasmin alimuua Tariq na
akanipigia simu kunitaka
nikamchukue na lengo hasa la
kumleta Dar es salaam ni
kukamilisha makubaliano kati
yetu na yeye.Kuna mambo ambayo
tunayataka toka kwake na yeye
kuna mambo anayataka toka
kwetu” akasema Austin
“Austin umenistua sana kwa
haya mambo uliyonieleza.Rais
wetu anawezaje kuwa na
makubaliano au hata mawasiliano
na Alshabaab watu ambao ni jana
tu wametushambulia na kuua watu
wengi wakiwemo viongozi
wakubwa? Monica akashangaa
“Mpaka sasa hatufahamu ni
kitu gani hasa kilichopelekea rais
aingie katika makubaliano na
Alshabaab kiasi cha kuwaachia
huru watu wale wawili hatari”
akasema Austin
“Austin nimeogopa
sana.Sikuwahi hata kuota kama
rais wetu anaweza akafanya
mambo kama haya.”
“Monica mimi na wenzangu
tuko kazini hivi sasa
kutakakufahamu ni kitu gani
ambacho rais alikubaliana na
Alshabaab hadi akafikia hatua ya
kuwaachia watu wale wawili.Kitu
kingine ambacho huwezi ukaamini
na ambacho naomba ibaki kuwa
siri yako ni kwamba Alshabaab
pamoja na kuachiwa watu wao
wawili walitaka pia hati ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar”
“ What ?!! Akasema Monica
kwa mshangao akainuka na
kushika kiuno.
“Alshabaab wametaka nini?
“Katika makubaliano hayo
Alshabaab walitaka pia wapewe
hati ya muungano wa Tanganyika
na Zanzibar”
“Austin that’s a lie.It’s not
true.Alshabaab hawawezi kutaka
kitu kama hicho ambacho ni
ngumu kukipata.Kwa nini kwanza
watake kitu kama hicho? Akauliza
Monica
“Lengo kuu ni kuigawa nchi hii
vipande vipande.” Akasema Austin
Monica akamtazama Austin
halafu akasema
“Tafadhali Austin usiniambie
kwamba rais tayari amewapa
Alshabaab hati ya muungano wetu”
akasema Monica
“Usistuke Monica lakini tayari
rais amekwisha itoa hati hiyo na
alimkabidhi Yasmin” akasema
Austin
“Jesus Christ !! akasema
Monica na kuweka mikono
kichwani
“Nini kimeikumba nchi
yangu?? Akasema kwa sauti
ndogo.Ulipita ukimya wa sekunde
kadhaa halafu Monica akasema
“Austin tayari mnaye Yasmin
.Ichukue hiyo hati ya muungano na
ufanyike utaratibu wa kuiorejesha
mahala inakohifadhiwa ikulu
halafu huyu rais anatakiwa
kushtakiwa kwa hili alilolifanya la
kucheza na muungano wetu kiasi
hiki !! akasema Monica kwa hasira
“It’s not that easy Monica.Ni
kweli Yasmin anayo hati lakini ili
kuipata hati hiyo kuna mambo
ambayo Yasmin anayataka
tumfanyie kwanza ndipo
atuonyeshe mahala alipoificha
hiyo hati”
“Hayuko nayo mkononi?
Akauliza Monica
“Hapana hayuko nayo
mkononi.Anadai kuna mahala
ameificha na atatuelekeza mahala
hapo endapo tutamtimizia mambo
anayoyataka.”
“Mungu wangu !! Monica
akahisi kuchanganyikiwa.
“Kwa nini nchi yetu
inachezewa kiasi hiki? Austin hati
hiyo ndiyo chimbuko la kuzaliwa
Tanzania.Usithubutu tafadhali
kuacha kitu muhimu kama hiki
kikachezewa namna hii.Wazee
wetu waliitunza hati hiyo kwa kila
uwezo waliokuwanao lakini leo hii
inatolewa kama vile si kitu
chochote.Tafadhali fanya kila
unaloweza kufanya ili kuipata hati
hiyo.Kwani huyo Yasmin anataka
kitu gani? Akauliza Monica
“Thank you Lord.Hapa ndipo
nilipokuwa napatafuta.Amefika
mwenyewe” akawaza Austin.
“Kwa maelezo yake,amekiri
kwamba baada ya kukaa muda
mrefu gerezani ameamua kuacha
na IS kwa hiyo anataka kwenda
kuishi mbali yeye na mwanae
ambako hawataweza kutambuliwa
na IS.Tukilifanikisha hilo
atatueleza mahala alikoificha hiyo
hati ya muungano” akasema Austin
“Mmekubali kumtekelezea
jambo hilo? Akauliza Monica
“Hatuna namna ya kuweza
kuipata hati hiyo zaidi ya kukubali
kutekeleza anachotaka” akasema
Austin.Monica akamtazama kisha
akasema
“Doyou believe her?
“Yes I do” akajibu Austin
“Kwa hiyo mtalitekelezaje
ombi lake?Monica akauliza
“Utekelezaji wake ni mgumu
kwa sababu anatakiwa kupata pasi
mpya za kusafiria yeye na
mwanae,vile vile tunatakiwa
kupata nchi ambayo itakubali
kuwapokea na kuwahifadhi na hii
lazima iwe ni katika nchi za ulaya
au Amerika.Hatuwezi kumpeleka
katika nchi za kiarabu au
Asia.Anajulikana sana huko na ni
rahisi kugundulika na IS.Jambo la
tatu linalofanya jambo hili liwe
gumu ni kiasi kikubwa cha fedha
kinachohitajika ili
kulikamilisha.Endapo mahusiano
yangu na rais yangekuwa mazuri
basi suala hili lingemalizika kwa
urahisi sana lakini mimi na rais
kwa sasa hatupikwi chungu
kimoja”
“What are you going to do?
akauliza Yasmin
“I need your help”
“My h elp?!! Monica akauliza
“NdiyoMonica nahitaji sana
msaada wako.Hata kama
usingenitafuta ,mimi
ningekutafuta kwani kwa sasa ni
wewe tu ambaye unaweza
kutusadia” Akasema Austin
“Austin mambo uliyonieleza
yamenistua na kuniogopesha mno
lakini sina namna yoyote ya
kukusaidieni.Jana nilikusaidia
lakini ona yaliyonitokea.Nusura
tungepoteza uhai baada ya
kupeleka ndege kutua katika
daraja la nyerere.Siwezi kulisahau
tukio lile baya kabisa katika
maisha ” akasema Monica
“Monica ulihitaji nikueleze
ukweli na nimekueleza
ukweli.Hakuna mtu mwingine
ukiacha mimi na wenzangu
anayelifahamu suala hili zaidi
yako.Tafadhali naomba
utusaidie.You’re not doing this for
me but for your country.Juhudi
zetu zote tulizozifanya hadi kufikia
hapa haziwezi kuwa na maana
endapo tutashindwa kutimiza
mahitaji ya Yasmin na hivyo
kuikosa hati ya muungano”
Monica aliyekuwa
amesimama akaketi sofani
akazama katika tafakari halafu
akasema
“Unahitaji nikusaidie kitu gani
Austin?
“Msaada mkubwa ninaouhitaji
ni kuwaondoa Yasmin na mwanae
hapa nchini na kisha tuwatafutie
nchi ya kwenda kuishi pamoja na
namna watakavyoyaendesha
maisha yao.”akasema Austin
“How do you want me to
help,call president again and ask
for help? No I wont do that.Siwezi
kumuomba msaada tena shetani
kama Yule!! Akasema Monica kwa
ukali.Akatazamana na Austin
halafu akasema
“Lakini kuna kitu tunaweza
tukafanya” Akanyamaza na
kushika kichwa
“I didn’t want to do this but I
have to” akawaza Monica kisha
akasema.
“Austin kuna jambo moja
tunaweza kulifanya.Ninasema
tunaweza kulifanya kwa sababu
tayari na mimi nimo katika suala
hili” Akanyamaza tena halafu
akasema
“Nilikueleza kwamba niko
katika mahusiano na David Zumo
ambaye mke wake amefariki na
kesho anazikwa.Jioni ya leo David
atatuma ndege yake kubwa kuja
kunichukua mimi na familia yangu
kwenda kuhudhuria mazishi hapo
kesho.Tunaweza kuitumia ndege
hiyo kuwaondoa akina Yasmin
hapa nchini tukawapeleka Congo
tukifika kule nitaubeba mimi
mzigo na kumuomba David
anisaidie kuwatafutia nchi ya
kwenda kuishi.Yule ni mtu
mkubwa na suala kama hili
haliwezi kumshinda.Nadhani huo
ni msaada mkubwa ambao
ninaweza kuufanya ili kukusaidia
katika suala hili” Akasema
Monica.Austin akainuka na
kwenda kumshika mkono
“Monica ahsante
sana.Ninakushukuru mno kwa
kujitolea katika jambo hili.”
Akasema Austin
“Austin nimejitolea kufanya
hivi baada ya kuziona juhudi zako
katika kuipigania nchi yako kwa
hiyo lazima nikuunge mkono lakini
naomba uwe na uhakika kwamba
Yasmin anayo hiyo hati na si
kutuchezea akili zetu.Japokuwa
tutamuondoa hapa Tanzania lakini
hatakwenda kokote,ataendelea
kuwa chini ya ulinzi hadi
tuhakikishe kwamba tumeipata
hati yetu” akasema Monica
“Monica nina uhakika
mkubwa Yasmin anayo hati hiyo
na endapo tutamtimizia hicho
anachokitaka basi tutaipata”
akasema Austin
“Austin ninaomba uniahidi
kitu kimoja”akasema Monica.
“Endapo tukifanikiwa kuipata
hati ya muungano ,niahidi kwamba
rais lazima afikishwe mbele ya
sheria.Lazima akajibu shtaka la
kuichezea nchi yetu kiasi hiki”
Akasema Monica
“Monica lazima rais afikishwe
mbele ya sheria kwa kuuchezea
muungano ambao aliapa
kuulinda.Hata hivyo kuna kitu cha
muhimu ambacho unapaswa
kukifahamu kuhusu rais
kwan….”Monica hakutaka kumpa
nafasi Austin ya kumaliza kile
alichotaka kukisema akamkatisha
“Austin sitaki kusikia
chochote kuhusiana na yule
rais.Hakuna sababu yoyote
inayoweza kumsaidia asifikishwe
mbele ya sheria kujibu kosa la
kuichezea nchi yetu kiasi hiki.Yeye
na wenzake wote lazima
waadhibiwe na liwe fundisho kwa
wengine wote watakaokuja
kutothubutu kucheza na nchi
yetu.Austin yule mzee ni
shetani.Laiti ungenieleza toka
mapema mambo haya
nisingemkubalia kitu
alichoniomba jana .Najuta sana
kwa kumuahidi kumsaidia
kukupata wewe.Leo hii asubuhi
nimepigiwa simu na mkuu wa
idara ya usalama wa taifa anaitwa
Silvanus nani sijui anasema
kwamba amekabidhiwa na rais
jukumu la kukutafuta na alikuwa
anauliza kama tayari nimekupigia
simu.Nilimjibu bado akaniambia
kwamba kuna vijana wake
atawatuma ili nipige simu nikiwa
nao waweze kufahamu mahala
ulipo na wakuvamie.Rais anatumia
nguvu kubwa sana kukutafuta
kumbe anafahamu tayari
unafahamu madhambi yake”
Akasema Monica
“Monica hawa jamaa
watakuandama kwani wanajua
kabisa kwamba wewe una
mawasiliano nami kwa hiyo
umakini mkubwa sana
unahitajika.Sintoitumia tena ile
simu yangu bali mawasiliano yote
yatafanywa kwa kutumia ile simu
ya Amarachi.halikadhalika wewe
usitumie simu yako kuwasiliana
name kwani wanaweza wakawa
wanafuatilia mawasiliano yako
kujua kama unawasiliana nami
kwa siri”
“Kuhusu simu hakuna tatizo
kwani nina simu zaidi ya tatu
nitakupa moja kwa ajili ya
kuwasiliana.Ile simu yenye namba
aliyonayo Silvanus sintoitumia
kuwasiliana nawe bali itakuwa ni
kwa ajili ya mawasiliano na David”
“Good. Saa ngapi unategemea
kuondoka kueleka Kinshasa.?
“Saa kumi za jioni.”
“Sawa .Tutawasiliana mambo
yanavyokwenda.Mimi na
wenzangu tunakwenda kuandaa
mpango namna ya kuweza
kuwaondoa akina Yasmin hadi
ndani ya ndege .Tutawasiliana
baadae nitakujulisha kila kitu
kitakavyokwenda” Akasema
Austin
“Monica haya niliyokueleza
usithubutu kumueleza mtu yeyote
yule.Hii ni siri yangu mimi na
wewe” akasema Austin
“ Usihofu Austin.” Akasema
Monica na kabla Austin
hajaondoka akampatia simu moja
halafu Austin na Amarachi
wakaeleka katika gari na
kuondoka kurejea nyumbani
kwao.
Baada ya Austin na Amarachi
kuondoka,Monica akampigia simu
Silvanus Kiwembe na kumuelekeza
sehemu ambako atakutana na wale
watu wa usalama wa Taifa ili
awasiliane na Austin.
“Dah ! mambo niliyoyasikia
toka kwa Austin ni mazito
mno.Sasa nimefahamu kwa nini
rais anatumia nguvu kubwa
kumsaka Austin.Kumbe ni kwa
sababu ya mambo ya kishenzi
anayoyafanya.Anathubutuje kuwa
na mahusiano na Alshabaab ambao
wameua watu wengi wasio na
hatia jana? Anathubutuje kuitoa
hati ya muungano wetu kwa
magaidi hawa? Lengo lao ni nini
hasa? Halafu kuna hawa
Alberto’s.Nchi yetu imekumbwa na
balaa gani? Nawasifu sana Austin
na wenzake kwa ujasiri
walionao.Wameyatoa maisha yao
kupigania nchi.Lazima niwasaidie
na tuhakikishe tunawaondoa wale
wote wasiotutakia mema.Mtu
yeyote mwenye mapenzi mema na
nchi yake hatathubutu kuvumilia
uchafu huu unaofanywa na rais na
genge lake.Mwisho wao uko karibu
sana na watafahamu kwamba
wapo vijana wazalendo ambao
hawaogopi kumwaga damu kwa
ajili ya nchi yao”akawaza Monica
“How did it go? Amarachi
akamuuliza Austin wakiwa garini
baada ya kutoka nyumbani kwa
wazazi wa Monica
“Ni mambo mazito lakini
Mungu amenyoosha mkono wake
na mambo yanakwenda
vyema.Jana usiku Monica aliitwa
na rais ikulu”
“Aliitwa ikulu?!! Amarachi
akashangaa
“Ndiyo.Rais alimtaka aende
ikulu na akamuhoji kuhusiana na
kilichokuwa kimetokea.Alipata
taarifa za wale wanausalama
tuliowapoteza fahamu ndiyo mana
wakaweka vikosi pale uwanja wa
ndege watukamate watuhoji na
wajue nini kilichotokea.Bahati
nzuri tulistuka mapema na
kwenda kutua
darajani.Tusingefanya vile
tungekuwa ndani hivi sasa na
tungeharibukila kitu.Monica
alimueleza rais kila kitu
kilichotokea na rais akamuahidi
akamuomba amsaidie kuweza
kunipata.Alimuomba asubuhi ya
leo anipigie simu na aombe
kukutana nami na baada ya hapo
amtaarifu mahala tulikopanga
kukutana halafu angewatuma
vijana wake kuja
kutukamata.Lengo kubwa la rais ni
kumpata Yasmin ili aweze kuipata
ile hati.”Austin akanyamaza
“The situation is geting ugly”
akasema Amarachi
“Rais anatumia uwezo wake
wote kuhakikisha kwamba
anatupata kwani tayari tumekuwa
hatari kwake.Nimemueleza Monica
kila kitu na amestuka
sana.Hakutegemea kabisa kusikia
mambo makubwa kama yale.”
“Ulimueleza kama rais ni baba
yake? Amarachi akauliza
“Hapana.Sikuweza kufanya
hivyo kwa namna alivyoonyesha
hasira kwa rais.Baada ya
kumueleza kila kitu nilimuomba
atusaidie na amekubal
kutusaidia.Leo saa kumi ndege ya
rais wa Congo itakuja kumchukua
yeye na familia yake kwa ajili ya
kwenda Kinshasa katika msiba wa
mke wa David Zumo.Tutaongozana
na Monica hadi Congo na kufika
kule Monica atamuomba David
Zumo amsaidie kumtafutia Yasmin
na mwanae makazi katika nchi ya
mbali ambako hataweza
kujulikana na IS.Mimi na wewe
tutaongozana na akina Yasmin
kwenda Congo, Job atabaki hapa ili
Yasmin akituelekeza mahala ilipo
hati akaichukue na kuiifadhi
.Hatutamuachia Yasmin hadi hapo
atakapotuelekeza mahala
alikoiweka hati hiyo.Bado tuna
mlima mrefu wa kupanda.Lazima
tuhakikishe rais Ernest
anafikishwa mbele ya sheria kwa
mambo maovu aliyoyafanya kwa
nchi hii” akasema Austin
“Vipi kuhusu Boaz yeye
tutamfanya nini? Amarachi
akauliza
“Nilikuwa na hasira naye sana
kwa mambo aliyomfanyia mdogo
wangu Linda lakini nafikiria
kumpa nafasi nyingine na
kumuunganisha na akina Yasmin
kwenda kuanza maisha
mapya.Ninauthamini mchango
wake wa kuniokoa toka katika
mikono ya Alshabaab kwa hiyo
nitamshawishi Yasmin aongozane
naye kama atakuwa tayari”
akasema Austin