QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEASON 7: SEHEMU YA 4

Inakaribia saa kumi na mbili
za asubuhi,Silvanus Kiwembe
mkuu wa idara ya usalama wa taifa
alipowasili ikulu kuonana na
rais.Walielekea katika chumba cha
maongezi ya faragha.
“ Silvanus nililazimika
kusitisha lile zoezi la kumtafuta
Yasmin kule Zanzibar baada ya
kupata taarifa zenye uhakika
kwamba Yasmin tayari yuko jijini
Dar es salaam.”
“ Amekuja Dar es salaam?!!
Akauliza Silva
“ Ndiyo yuko hapa Dar es
salaam”
“ Amewezaje kutoka
Zanzibar? Njia zote za kuingilia na
kutokea Zanzibar zilifungwa na
ulinzi ni mkali sana” akasema
Silva.
“ Silva kuna kitu ambacho
unatakiwa ukifahamu.Ninaye binti
yangu mmoja niliyempata enzi za
ujana wangu .Binti huyo ana
mahusiano ya karibu na kijana
mmoja anaitwa Austin January.”
“ Austin January?! Silva
akastuka
“ Ndiyo.Unamfahamu?
“ Hapana nimewahi kuzisikia
habari zake.Yuko hapa
nchini?akauliza Silva
“ Austin yuko hapa nchini”
akasema rais na kumtazama
Silvanus ambaye alionekana
kustushwa na taarifa zile za Austin
kuwapo Tanzania
“ Jana usiku nilipigiwa simu
na Monica ambaye ndiye
mwanangu akaniambia kwamba
amepata safari ya ghafla kwenda
Zanzibar kwa hiyo akaniomba
nimsaidie apate
usafiri.Nilishindwa kumkatalia
japokuwa kulikuwa na katazo la
kutoruhusu ndege yoyote kutua au
kupaa,ilinilazimu kutoa maelekezo
Monica apelekwe Zanzibar kwa
ndege maalum na kurudishwa
baada ya kumaliza shughuli
zake.Sikuishia hapo nikatoa na
vijana wawili wamlinde hadi
atakaporudi.Nilikupigia
nikakuomba uongeze vijana wawili
pia kule Zanzibar ili ulinzi wa
Monica uwe madhubuti lakini cha
kushangaza walinzi wote hawa
walikutwa katika magari yao
hawana fahamu.Hili ni jambo la
kushangaza sana.Bila ruhusa
yangu,jenerali lameck alitoa amri
Monica na wenzake waliokuwamo
katika ndege wakamatwe mara tu
watakapotua dar es salaam
wakitokea Zanzibar.Monica na
wenzake waligundua mtego
uliowekwa uwanja wa ndege ili
wakamtwe kwa hiyo ikawalazimu
kwenda kutua katika daraja la
Nyerere Kigamboni.Hili ni jambo la
hatari sana.Ilinilazimu kumuita
Monica hapa ikulu usiku huo huo
nikamuhoji na akanieleza ukweli
kwamba Austin ndiye aliyemfuata
nyumbani kwake akamtaka
anipigie simu na kuniomba usafiri
kwa kunidanganya kwamba
amepata dharura.Anasema
kwamba Austin alikuwa na
wenzake wawili na wakawapoteza
fahamu wale walinzi niliotoa
wamsindikize kisha wakawaficha
garini na kuelekea Zanzibar” Rais
akanyamaza na kupiga mwayo
ishara ya uchovu halafu akasema
“ Huwezi kuamini Silva lakini
ukweli ni kwamba Austin
alikwenda Zanzibar kumchukua
Yasmin Esfahani”
“ Austin amefahamu vipi
kuhusu Yasmin? Akauliza Silva
kwa mshangao
“ Hata mimi sijui Austin
amefahamuje kuhusu
Yasmin.Mpaka hivi sasa
tunavyoongea Austin na wenzake
wanaye Yasmin na sifahamu
wamemchukua kwa malengo
yapi.Kitu ambacho ninataka
ukifanye wewe na idara yako ya
usalama wa taifa ni kutumia kila
aina ya uwezo mlio nao kumtafuta
Austin.Tukimpata Austin
tutakuwa tumempata pia Yasmin”
akasema rais.Silva aliyekuwa
akisikilza kwa makini akauliza
“ Mheshimiwa rais kuna
jambo linanitatiza kidogo.Naomba
kufahamu kwa nini tunamtafuta
Yasmin wakati ulikuwa
umemuachia huru?
Ilimchukua rais sekunde
kadhaa za kutafakari kabla ya
kulijibu swali lile la Silva
“ It was a mistake.Kumuachia
huru Yasmin lilikuwa ni kosa
kubwa sana na ndiyo maana kwa
kila namna nataka Yasmin
apatikane na arudishwe kule
gerezani.”
“ Austin anaishi wapi? silva
akauliza
“ Kwa sasa hakuna
anayefahamu ni wapi anaishi
Austin lakini kuna mtu mmoja tu
ambaye anaweza akatusaidia
kumpata Austin.Huyu ni
Monica.Niliongea naye jana usiku
na kumuomba awasiliane na
Austin asubuhi na aombe kuonana
naye baada ya hapo anitaarifu ni
wapi watakutana ili tukamchukue
Austin.” Akasema rais
“ Mheshimwa rais hilo ni wazo
zuri lakini sina hakika kama
linaweza kutusaidia.Ni vipi iwapo
Monica hatampigia simu Austin?
Silva akauliza
“ Ndiyo maana nimekuita hapa
Silva ili na wewe unipe mchango
wa mawazo kwani kwa sasa
kichwa changu kimevurugwa
kabisa na sielewi nianzie wapi
niishie wapi.Please help me”
akasema rais
“ Nionavyo mimi wazo la
kumtumia Monica kumpata Austin
ni sahihi lakini si kwa kumuacha
Monica ampigie simu Austin.kama
ulivyosema kwamba wawili hawa
wana mahusiano ya karibu kuna
uwezekano Monica asiwasiliane na
Austin au amtaarifu kuwa
anatafutwa.Tunachotakiwa
kufanya ni kummulika Monica kila
mahala.Kudukua mawasiliano
yake,kufahamu kila mahala
anakokwenda .tukifanya hivyo
tutagundua kitu.” Akashauri
Silva.Rais akafikiri kwa muda
halafu akasema
“ Silva nakukabidhi jukumu
hilo ufanye unavyoona inafaa ili
mradi Monica asipate madhara
yoyote.”
“ Mzee kazi zetu tunazifanya
kitaalamu sana na sisi lengo letu ni
kumpata Austin pekee na si
Monica.”
“ Good.Ukiacha hilo kuna
suala lingine pia ambalo nataka
ulipe uzito mkubwa.” Akasema rais
akanyamaza kidogo
“ Ni kuhusu mke wangu
Agatha.Tuliamini kwamba
aliwemo katika hoteli ile
iliyolipuliwa lakini kwa bahati
nzuri hakuwemo katika hoteli
ile.Kwa hiyo mke wangu yuko hai”
akanyamaza tena na kuinamisha
kichwa akafikiri kidogo na kusema
“ Amenipigia simu jana usiku
akanitaarifu kwamba yuko hai
lakini hakutaka kunieleza mahala
aliko.Nataka ufanye uchunguzi
mkubwa kufahamu mahala alipo
mke wangu.Nilijaribu kumpigia
simu kwa namba zile alizotumia
kunipigia lakini nikaambiwa
kwamba namba zile si
sahihi.”akasema rais
“ Mzee hili suala
linanishangaza kidogo.Kwa nini
asiweke wazi mahali aliko?Kwa
nini anajificha ? Akauliza Silva
“ Silva hilo ndilo swali ambalo
nataka ulijibu .Nataka utafute
mahala alipo .Nimekupa
majukumu haya mawili mazito
kwa hiyo tumia kila rasilimali
uliyonayo na endapo kuna kitu
chochote kinahitajika usisi…” Rais
akanyamaza baada ya lango
kugongwa.Akainuka na kwenda
kuufungua akakutana na Jenerali
Lameck Msuba akamuomba
amsubiri kwa dakika moja amalize
mazungumzo yake na Silva
“ Silva kuna mtu nahitaji
kuzungumza naye kwa hiyo
naomba uyafanyie kazi hayo
mambo niliyokuambia.Chochote
utakachohitaji nieleze
tafadhali.Tumia nguvu yote
uliyonayo kuhakikisha kabla ya
jua kuzama siku ya leo Austin na
wenzake wawe
wamepatikana.Naomba taarifa za
mara kwa mara” akasema rais na
kumpa Silva namba za simu za
Monica ili wawasiliane kisha Silva
akaondoka na akaingia Jenerali
Lameck
“Lameck nipe ripot.Nini
kimeendelea? Akauliza rais
“ Mzee mambo yanakwenda
vizuri na kabla ya mapambazuko
leo ,ndege zetu za vita
zimeshambulia kambi mbili za
Alshabaab na kuziharibu
kabisa.Tulifanya mashambulio
hayo katika zile kambi
tulizoelekezwa na wao
wenyewe.Kwa hiyo dunia
itaamshwa na habari mpya siku ya
leo na hii itapunguza hasira za
watanzania kwa kuona kwamba
tayari serikali yao imeanza
kuchukua hatua dhidi ya
Alshabaab waliomwaga damu ya
watanzania.Ni hatua nzuri
tumepiga.” Akasema Lameck
“ Good Job lameck” Akasema
rais na kuvuta pumzi ndefu .
“ Lameck naona kama kichwa
changu kinataka
kupasuka.Asubuhi ya leo Habib
anahitaji majibu kama tayari
nimefanikiwa kumpata
Yasmin.Nilimuahidi kumpa jibu
zuri asubuhi na sina cha
kumueleza kwani bado Yasmin
sijampata na hata kama
ningekuwa nimempata sina
mpango wa kumpa Habib ile hati
ya muungano.Nishauri nifanye
nini?
“ Relax Mr President.Huu ni
wakati unaohitaji utulivu mkubwa
na kufanya mambo kwa utulivu na
akili kubwa.Kama Habib
atakupigia simu tell him anything
good just to buy time.Baadae
baada ya mambo kutulia utaongea
naye na kumuomba alipwe kitu
kingine badala ya hati ile ya
muungano anayoitaka.Nafikiri hilo
ndilo jambo pekee zuri la kufanya
kwa sasa kuhusu Habib”akasema
Lameck
“ It’s a good idea.Itanibidi
nifanye hivyo” akajibu rais
“Vipi kuhusu ripoti ya vifo na
majeruhi ,tayari umeipata ili
tufanye tathmini ya kazi
tuliyofanya kama imezaa
matunda? Akauliza Lameck
“Mpaka sasa bado sijapokea
ripoti yoyote ila nategemea kupata
taarifa asubuhi hii ya leo kwani
kazi ya kufukua vifusi na kutafuta
maiti katika majengo
yaliyolipuliwa imeendelea
kufanywa usiku kucha.Katika
kikao cha asubuhi ya leo tutapata
taarifa rasmi na hapo baadae
nategemea kwenda katika hoteli
iliyolipuliwa kisha nitakwenda
Dodoma na kule nitatembelea
jengo la bunge lililolipuliwa halafu
nitahutubia taifa kutokea pale pale
katika eneo la bunge.Nina ratiba
ndefu sana siku ya leo na
ninaomba uambatane nami kila
mahala nitakapokwenda siku ya
leo kwani nahitaji sana mtu wa
karibu wa kunishauri.Kitu kingine
ni kwamba nimemkabidhi Silva
jukumu la kuwatafuta Austin na
wenzake na vile vile kufahamu
mahala aliko Agatha.” Akasema
rais na ukimya mfupi ukatawala
mle chumbani
“ Mheshimiwa rais bado
najiuliza imewezekanaje Agatha
akanusurik…….” Kabla Lameck
hajamaliza sentensi yake simu ya
rais ikalia akaitoa mfukoni
akatazama mpigaji halafu
akamuomba Lameck atoke nje ili
aweze kuzungumza na simu ile.
“ hallow sweetheart” akasema
rais baada ya kuipokea simu ile
“ hallo my love” ikasema sauti
laini ya mwanamke upande wa pili
“ Nashukuru umenipigia
mpenzi wangu Monalisa.Habari za
Arusha? Akauliza rais
“Huku si kwema
mpenzi.Nimeshindwa kupata
usingizi kutokana na tukio
lililotokea jana.Nilitaka kukupigia
usiku nikajua utakuwa katika hali
mbaya nikaona ni vyema nikupigie
asubuhi ya leo ili nijue maendeleo
yako.Pole sana mpenzi wangu kwa
mambo yaliyotokea
jana.Nimeogopa mno” akasema
Monalisa.
“Mona usihofu mimi ni mzima
kabisa japokuwa nilipata mstuko
kidogo lakini ninaendelea vyema
na sina tatizo lolote.Kwa sasa
tunaendelea na uchunguzi
kuhusiana na jambo hili lakini
hawa magaidi hawataweza
kutuchezea ,tutuwafundisha
adabu” akasema rais
“Naomba uwe makini sana
mpenzi wangu katika kazi yako
hiyo imekuwa na hatari
nyingi.Maadui wanaokutafuta ni
wengi.Mimi na Millen
tunakuombea sana uweze kuwa
salama”
“msiwe na hofu yoyote
nitakuwa salama kabisa” Akasema
rais
“Nimepata taarifa nyingine
asubuhi ya leo imenistua sana.Ni
kwamba Bill naye ni miongoni
mwa watu waliokuwamo katika
hoteli hiyo iliyoshambuliwa Dar es
salaam.Naye amefariki dunia”
akasema Monalisa
“ Umepata wapi taarifa hizi?
Mbona mimi bado
sijazipata?akauliza rais
akionekana kustuka
“Nimepigiwa simu na rafiki wa
karibu na Bill akaniambia kwamba
Bill alimpigia simu jana jioni akiwa
hapo hotelini akamwambia
kwamba alikuwa anakusubiri
wewe na baada ya muda mfupi
likatokea hilo shambulio.”
Akasema Mona
“Ni kweli Mona nilikuwa na
miadi ya kukutana na Bill jana pale
hotelini.Nitafuatilia katika taarifa
nitakayopewa ili nijue kama Bill ni
mmoja wa watu
waliofariki”akasema rais
“Hakuna haja ya kufuatilia,
kwani tayari marafiki zake
wamekwisha fuatilia na
kuhakikisha kweli Bill amefariki
dunia” Akasema Mona na kuanza
kulia
“Pole sana Monalisa hata mimi
jambo hili limenigusa mno.Bill
alikua mtu wetu wa karibu sana”
Akasema rais
“Mona ninakuomba kitu
kimoja,hali ya usalama kwa sasa si
nzuri kwa hiyo ile safari ya
kuelekea ulaya inatakiwa iwe
mapema zaidi na mterejea pale
hali ya usalama itakapokuwa
imekaa vizuri.”
“Hapana sweetheart.Ile safari
lazima tuiahirishe kwa
muda.Lazima nihudhurie msiba wa
Bill.Yule ni mtu wangu wa karibu
sana na siwezi kuondoka bila
kuhudhuria mazishi yake.Yeye ni
sababu ya mimi na wewe kuwa
pamoja”akasema Monalisa na rais
akastuka
“Unamaanisha unataka kuja
dar es salaam?
“Ndiyo.kama msiba wa Bill
utakuwa Dar es salaam lazima
nihudhurie”
“Mona hapana usije Dar es
salaam.Hali si shwari kwa
sasa.Nakuomba Mona endelea na
safari ya ulaya na mimi
nitakuwakilisha katika mazishi
hayo ya Bill”
“Hapana siwezi kukosa
kuhuduria msiba kama huu
unaonihusu sana.Hiyo safari
itasubiri kwanza hadi pale msiba
utakapomalizika .Isitoshe hakuna
kitu chochote cha kuhofia”
akasema Monalisa
“Mona nakuomba tafadhali
usije Dar kwa sasa.Hali ya usalama
bado si nzuri” akasema rais
“Darling wewe ni mkuu wa
nchi kwa hiyo fanya kila uwezavyo
kuhakikisha kwamba mimi na
Millen tunakuwa salama
tutakapokuwa Dar.” Akasema
Monalisa
“Mona tafadhali naomba
tusiweke mjadala katika suala
hili.Unafahamu fika hali uliyoiacha
huku kwa hiyo nakushauri Mona
usije Dar”akasema rais
“Darling ni miaka imepita sasa
na isitoshe Job ni kichaa na hawezi
kunitambua tena kwa hiyo hakuna
chochote cha kuogopa.Ninakuja
kuhudhuria msiba na kuondoka ili
tuendelee na ratiba nyingine hizo
za kwenda ulaya.Tafadhali
niruhusu japo mara moja mpenzi
wangu nije Dar niwaslimu hata
ndugu zangu kwani sijawahi
waeleza niko wapi” Akasema
Monalisa.Rais akafikiri kwa muda
halafu akasema
“Nipe muda nilifikirie suala
hilo Mona nitakupa jibu baadae.”
Akasema rais na kuagana na
Monalisa akakata simu.
“Siku imeanza vibaya
.Monalisa anataka kuja Dar !!
akawaza rais.
“Nimeshindwa kumueleza
kama Job si kichaa na
anamtafuta.Hata hivyo nimefurahi
kusikia kwamba Bill tayari
amekufa.Yule pekee ndiye
aliyekuwa anafahamu kuhusu
mimi na Monalisa na Job alikuwa
anamuwinda ili amueleze mahala
alipo mkewe na mwanae
Millen.Pamoja na Bill kuondoka
nina wasi wasi ujio wa Monalisa
hapa Dar unaweza kusababisha
mambo mengine endapo ataonana
na Job au watu wanaweza
wakamuona na kumtaarifu Job”
Akawaza
“Hakuna namna
nitakayofanya kumzuia Mona asije
Dar .Kitu pekee ni kuhakikisha
kwamba anakuwa na ulinzi mkali
muda wote na hakuna mtu yeyote
anayemkaribia.Vile vile anatakiwa
abadili muonekano wake ili
asitambuliwe kirahisi” akaendelea
kuwaza rais
 
SEASON 7: SEHEMU YA 5

Wakati Monica akiendelea
kumsubiri Austin afike simu yake
ikaita.Zilikuwa ni namba ngeni
.Akapokea.
“ hallow” akasema Monica
“ hallow Monica.Naitwa
Silvanus Kiwembe mkurugenzi wa
idara ya usalama wa
taifa.Nimepewa namba zako na
rais.”akasema Silva.Monica
akastuka na kuogopa.
“ Nini unahitaji mr Silvanus?
Akajikaza na kuuliza
“ Ni kuhusiana na yale
mazungumzo yako na rais jana
usiku.Ana shughuli nyingi siku ya
leo kwa hiyo amenipa namba yako
ya simu na utakuwa unawasiliana
nami kuanzia sasa.” Akasema Silva
“Tayari umekwisha wasiliana
na Austin asubuhi hii? Silva
akauliza
“Hapana bado sijawasiliana
naye” Akajibu Monica kwa kifupi
“Sawa hakuna
tatizo.Ninawatuma vijana wangu
watakufuata mahala ulipo ili
wakati unawasiliana na Austin wao
watafanyakazi ya kutafuta mahala
simu ya Austin inapotokea na
itakuwa ni kazi rahisi kwetu
kumpata” akasema Silva
“Mr Silva ,nilimuahidi rais
kwamba nitafanya kama
alivyoniomba nifanye yaani
kumpigia simu Austin lakini
naomba suala hili lisinifanye
nikashindwa kuwa huru na
kutekeleza majukumu mengine
yanayonikabili.Nina mambo mengi
ya kufanya na sitaki kuzungukwa
na watu wa usalama wa taifa kila
dakika.Baada ya kupiga simu na
mkajua mahala alio Austin nataka
mniache niendelee na majukumu
yangu mengine” akasema Monica
“Monica samahani kama
tumekukwaza kwa namna yoyote
ile .Nafahamu una shughuli zako
nyingi za kufanya lakini hili
tunalokuomba utusaidie ni
muhimu sana hasa kwa wakati huu
ambao taifa linapitia katika
kipindi kigumu.Wewe
unachotakiwa kufanya ni kumpigia
simu Austin na halafu tutakuacha
uende zako na hatutakusumbua
tena.Tusaidie tafadhali” akasema
Silva.Monica akafikiri kidogo na
kusema
“Kwa sasa siko nyumbani
kwangu.Nitakupigia baada ya
muda ili nikueleze mahala
nitakapokutana na hao watu
wako”akasema Monica
“ Ahsante Monica ila naomba
isichukue muda mrefu
sana.Tunahitaji kuanza kumtafuta
Austin asubuhi hii” akasema Silva
na kukata simu
“ Nilifanya kosa kubwa
kumkubalia rais kwamba
nitamsaidia kumtafuta Austin na
sasa tayari wamenza kunisumbua
na wataendelea kunisumbua kwa
sababu wanajua mimi pekee ndiye
mwenye mawasiliano naye.Silva
anasema kwamba kumpata Austin
ni muhimu kwa ajili ya usalama wa
nchi inawezekana Austin ni mtu
hatari kiasi cha kuhatarisha
usalama wa nchi? Nimeanza
kuogopa sana.Sikutegemea kama
siku moja nitajikuta nimebanwa
sahemu kama hii.Ngoja kwanza
nimsubiri Austin ili nizungumze
naye na anielez….” simu ya Monica
ikaita alikuwa ni David Zumo
“Hallo mpenzi” akasema
Monica baada ya kupokea simu
“Malaika wangu umeamkaje
leo?
“Nimeamka salama
kabisa.Vipi maendeleo yako?
“Maendeleo yangu
mazuri.Nimekupigia kujua hali
yako malaika wangu” akasema
David
“Nashukuru David .Mmi
naendelea vizuri
sana.Kinachonisumbua ni
kukuwaza wewe tu” akasema
Monica na david akatoa kicheko
kidogo
“Monica huwezi jua maneno
hayo uliyoyatamka yamenipa
faraja gani ndani ya moyo
wangu.Sauti yako laini ambayo
hupenya ndani kabisa mwa moyo
wangu imekuwa ni kitulizo
kikubwa sana kwa wakati huu
mgumu nilionao.Pauline kaondoka
lakini imekuja zawadi nyingine
ambayo ni wewe. Monica
namshukuru sana Mungu kwa
kunishushia malaika kama wewe.”
Akasema David
“Hata mimi nashukuru sana
David kwa mapenzi makubwa
unayonionyesha.Ni bahati sana
kuwa na mwanaume kama wewe
katika maisha yangu”akasema
Monica
“Monica tuna mengi tutaongea
pale tutakapoonana ila kwa sasa
naomba nikujulishe kwamba muda
si mrefu tutaanza safari ya
kuelekea Kinshasa kuupeleka
mwili wa Pauline na jioni ya leo
nitatuma ndege yangu binafsi kuja
kukuchukua na kukuleta Congo
kuhudhuria mazishi hapo kesho.”
Akasema David.
“Ahsante sana David.Tayari
tunajiandaa mimi na wazazi wangu
na baadhi ya watu kadhaa
watakaotusindikiza kuja msibani.”
“Monica naomba nikutakie
siku njema tutaonana usiku wa leo
utakapowasili Kinshasa.” Akasema
David na kukata simu
“ Afadhali niende zangu
Kinshasa nikapunguze
mawazo.Mambo yaliyotokea jana
na yanayoendelea kutokea hapa
dar es salaam yananiumiza mno
kichwa changu.” Akawaza na mara
mlango wake ukagongwa akaenda
kuufungua akakutana na mama
yake aliyemtaarifu kwamba
wageni wake tayari
wamefika.Monica akaenda
sebuleni akawakuta Austin na
Amarachi wakizungumza na mzee
Ben.Akawasalimu na kuwataka
waelekee chumbani kwake.
“ Karibuni sana Austin na
Amarachi .Hapa ni nyumbani kwa
wazazi wangu.Hapa ndipo
nilipokulia na hiki ni chumba
changu nilichoishi toka nikiwa
mdogo .Austin vipi hali yako?
Akauliza Monica
“Hali yangu ni
nzuri.Ninaendelea vyema.Vipi
wewe unaendelea je?
“Sijaweza kupata usingizi
kabisa,kila nikifumba macho tukio
la jana usiku linanijia kichwani.Ni
tukio baya kuwahi kunitokea
katika maisha yangu” akasema
Monica
“Pole sana” akasema Austin
.Monica akamtazama Amarachi na
kusema
“Amarachi naomba
nizungumze na Austin peke yake
kwa dakika kadhaa.Is that ok with
you sweetheart?
“Hakuna tatizo” akasema
Amarachi.Monica akampeleka
katika sebule yake halafu
akamuita mtumishi na kumuomba
amuhudumie Amarachi kwa chai
wakati akiendelea kuzungumza na
Austin
“Austin” akaanzisha maongezi
Monica
“Kwanza samahani sana kwa
mambo yote yaliyotokea
jana.Nilikutamkia maneno makali
kutokana na hasira na sikuwa
nikifikiri sawa sawa” akasema
Monica
“Usijali Monica.Hata mimi
nilifahamu hilo” akasema Austin
“Nashukuru
Austin.Nimelazimika kukuita hapa
ili tuzungumze mimi na wewe
kama marafiki na watu wa karibu
kuhusiana na tukio lile la
jana.Sijaweza kulala usiku
nikiwaza juu ya tukio
lile.Nilijilazimisha kuiaminisha
akili yangu kwamba ile ilikuwa ni
ndoto lakini ukweli utasimama
kuwa ile haikuwa ndoto bali ni kitu
cha kweli.Austin mimi na wewe
tumefahamiana katika ipindi
kifupi na katika muda huo mfupi
tumekuwa marafiki
wakubwa.Naomba tutumie muda
huu mchache tulioupata asubuhi
hii kuongea kama marafiki,kama
ndugu na tuelezane ukweli.Nataka
nikufahamu Austin wewe ni nani?
Unashughulika na nini? Sitaki
uniambie kwamba wewe ni meneja
sijui wa kampuni gani na unataka
kushirikiana name katika miradi
ya kijamii.Nieleze ukweli
nikufahamu Austin.Baada ya
kunijibu hilo ndipo tutaendelea na
mambo mengine” akasema
Monica.Austin akamtazama
Monica ambaye macho yake
aliyakaza kumtazama halafu
akasema
“Monica kabla ya kukueleza
chochote ,napenda nitumie nafasi
hii kukushukuru sana sana kwa
msaada wako mkubwa ulionisaidia
jana usiku.Vile vile samahani sana
kwa kukuingiza katika matatizo
makubwa .Haikuwa dhamira
yangu kufanya vile lakini sikuwa
na sehemu nyingine ya kuomba
msaada zaidi yako” akasema
Austin na kunyamaza
kidogo.Monica hakujibu
chochote.Austin akaendelea
“Umetaka kufahamu mimi ni
nani.Nitakueleza kwa ufupi.Jina
langu halisi ni Austin January
.Mimi ni mtanzania lakini kwa sasa
makazi yangu ni Afrika kusini na
nina uraia wa Afrika kusini.Kuna
hadithi ndefu kidogo hapa
iliyonifanya hadi niamue
kuchukua uraia wa Afrika
kusini.Wazazi wangu wote wawili
wamekwisha tangulia mbele za
haki .Ninaye mdogo wangu
anaitwa Linda ambaye kwa sasa
yuko nje ya nchi” Austin
alipomkumbuka Linda akasikia
kama mapigo ya moyo yanaanza
kumuenda mbio
“Linda atakuwa katika hatari
kubwa hivi sasa.Rais anaweza
akamtumia kama chambo ili
kunilazimisha nifanye kitu
anachotaka kwani anajua niko
tayari kufanya kitu chochote kwa
ajili ya mdogo wangu…”
“ Austin !! akaita Monica
baada ya kumuona Austin
amezama katika mawazo ghafla
“Sorry kuna kitu kilikuwa
kimenijia akilini kuhusiana na
mdogo wangu.Tuendelee”
akasema Austin
“ kazi yangu ni ujasusi”
Sura ya Monica ikabadilika na
kuonyesha woga aliposikia
maneno yale ya Austin
“Nimewahi kufanya kazi
katika idaraya ujasusi wa taifa
hadi pale nilipoamua kuachana na
kazi hiyo na kuanza maisha
mengine.Nimerudi Tanzania hivi
karibuni baada ya rais kuniita na
kuniomba nije kumfanyia kazi
yake binafsi.Ilinilazimu kukubali
kuifanya kazi ya rais kwa ajili ya
kumsaidia mdogo wangu
aliyekuwa amefungwa nchini
China kwa kujihusisha na biashara
ya dawa za kulevya.Nilikubaliana
na rais kumfanyia kazi yake na
yeye anisaidie kumtoa mdogo
wangu gerezani.Kwahiyo hayo ni
maelezo mafupi kuhusu mimi”
akasema Austin.Sura ya Monica
ikaonyesha kukasirika
“You lied to me !! akasema
“Nilipokuja hospitali
nikamkuta rais nikakuuliza kama
unafahamiana na rais ukasema
kwamba ni mtu wako wa karibu
kwani alikuwa anafahamiana na
wazazi wako.Kwa nini hukunieleza
ukweli Austin? Kwa nini
ukanidanganya? Akauliza Monica
“Sorry Monica.Ni kweli
nilikudanganya.Nisingeweza
kukueleza ukweli kwani sisi
tunaojihusisha na kazi hizi huwa
hatuweki wazi kuhusu kazi yetu na
ndiyo maana katika kazi hizi wapo
hadi makasisi lakini ni majasusi
.Ukweli sikuwa nikifahamiana na
rais hadi aliponitafuta yeye
mwenyewe na kuniomba
nimfanyie kazi yake.Hiyo pekee
ndiyo sababu ya ukaribu wangu na
yeye” akasema Austin
Monica akamtazama ,akameza
mate na kusema
“I want to know one
thing.Ulipokuja kwangu
ukajitambulisha kwamba wewe ni
meneja wa kampuni kubwa ya
utalii na unataka kushirikiana na
kampuni yangu katika miradi ya
kijamii.Nini hasa lilikuwa lengo
lako? Ni kweli ulihitaji
kushirikiana nami au ulikuwa na
lengo lingine? Akauliza Monica.
“Ni kweli ninasimamia
kampuni kubwa ya utalii
inayomilikiwa na mtanzania
anaitwa Boaz ambaye ni baba wa
aliyekuwa mpenzi wangu Maria,
lakini kuja kwangu kwako
kulikuwa na lengo lingine zaidi ya
kutaka kushirikiana nawe katika
miradi ya kijamii.Ile ilikuwa ni
namna ya kutafuta ukaribu mimi
na wewe ili lengo langu litimie.”
Akasema Austin na sura ya Monica
ikaonyesha hasira
“Nini hasa lilikuwa lengo lako?
Ulikuwa unanichunguza? Akauliza
Monica kwa ukali
“Monica kuna jambo ambalo
unapaswa kulifahamu lakini wapo
wahusika ambao wanatakiwa
kukujulisha jambo hilo na si mimi”
akasema Austin
“Austin wewe ni rafiki yangu
na ninakuthamini sana na ndiyo
maana kila siku lazima nifahamu
maendeleo yako.Kama kweli na
wewe unanithamini na kunijali
naomba unieleze hicho ambacho
unakifahamu kinanihusu mimi ”
akasema Monica
“Monica kama nilivyokueleza
kwamba wapo watu ambao
wanapaswa kukufahamisha
kuhusu suala hilo na si mimi.Subiri
muda muafaka utakapofika
utafahamishwa kila kitu”
Monica akaendelea
kumtazama Austin halafu akasema
“Jana usiku kuna jambo
ulitaka kunieleza ni jambo gani?
Au uliokuwa unanidanganya ili
nikusaidie katika tatizo lako?
“Nilichotaka kukueleza jana
ndicho hicho ninachokwamba
kwamba wapo watu maalum
watakaokueleza .Nilikuwa tayari
kukueleza jana lakini baadae
baada ya kujitafakari nikaona
haitakuwa busara kama nitaingilia
majukumu ya watu
wengine.Monica ulinieleza simuni
kwamba una jambo unataka
kuzungumza nami.Naomba
tujielekeze katika jambo uliloniitia
hapa na hayo mengine tuyaweke
pembeni” akasema Austin
“Austin nilikuita hapa ili
nikufahamu vyema kwani usiku
mzima nimekuwa nikitafakari
wewe ni nani .Mambo niliyoyaona
ukiyafanya jana yalinistua
mno.Nashukuru kwa kuamua
kuwa muwazi na kunieleza kuhusu
wewe lakini lipo jambo la muhimu
nililokuitia hapa”akanyamaza
kidogo na kuendelea
“Jana baada ya kurejea
nyumbani kutoka Zanzibar,mama
alinifuata akaniambia kwamba
ninahitajika ikulu.Rais anataka
kuniona.Niliongozana na mama
pamoja na walinzi wawili wa ikulu
nikaenda kuonana na rais.”
“Ulienda ikulu usiku ule?
Austin akauliza
“Ndiyo nilikwenda baada ya
kuitwa na rais.Tulingia katika
chumba cha maongezi ya faragha
tukiwa mimi na rais pekee.Rais
alinihoji kilichowatokea wale
walinzi waliotumwa kunipeleka
Zanzibar ambao walikutwa katika
gari lao wamefungwa na hata wale
wa Zanzibar waliokutwa hawana
fahamu katika gari lao.Akataka
kufahamu nini kilichotokea?
Nilikuwa na hasira sana
ikanilazimu kumueleza ukweli
wote kuwa ni wewe ndiye
uliyeniomba niwasiliane naye na
wewe na wenzako ndio
mliowapoteza fahamu wale walinzi
wa Dar es salaam na kule
Zanzibar.Rais alistuka sana na
hasa pale nilipomweleza kwamba
mlikwenda Zanzibar kumchukua
yule mwanamke niliyesikia
mkimtaja kwa jina moja la
Yasmin.Rais alinihakikishia
kwamba suala lile atalimaliza na
hakutakuwa na tatizo lolote kwa
upande wangu lakini akanitaka
nimsaidie kitu kimoja.Akataka
niwasiliane nawe asubuhi ya leo
halafu niombe tuonane kisha
nimjulishe mimi na wewe
tumepanga tuonane wapi ili atume
vijana wake waje
wakuchukue.Niliporejea nyumbani
nilitafakari sana suala hili
nikajiuliza kwa nini rais anitumie
mimi kukupata wewe wakati wewe
na yeye ni watu wa karibu? Kama
lengo lake ni zuri kama anavyodai
kwa nini asikupigie simu yeye
mwenyewe mkaonana? Kitu
kingine kilichonishangaza ni jana
uliponifuata na kunitumia mimi
kuwasiliana na rais.Nimejiuliza
kwa nini mimi? Kwa nini
msiwasiliane nyie wenyewe? Kuna
tatizo gani hapa?Nimeona
ninataka kujingiza katika hatari
kubwa nisiyoifahamu ndiyo maana
nikaamua nikuite asubuhi hii ili
tuzungumze na nifahamu nini
hasa kinachoendelea kati yako na
rais? Kwa nini mniweke mimi kati
kati? Kitu kingine ninachotaka
kufahamu yule mwanamke Yasmin
ni nani hadi ukahatarisha maisha
yako na yetu namna ile? Kwa nini
rais alipomsikia Yasmin alistuka
na kuogopa sana? Hayo ndiyo
mambo niliyokuitia hapa.Nataka
kuufahamu ukweli” akasema
Monica
“Monica sipati neno zuri la
kukushukuru kwa hiki
ulichokifanya.Nimeamini kweli
unanithamini na kunijali.Kwa hili
ulilolifanya nakuahidi baadae
nitakueleza kile nilichotaka
kukueleza jana.Jambo ulilolifanya
ni kubwa sio kwangu tu bali kwa
nchi.Ahsante sana Monica”
akasema Austin
“Kuna mambo mazito
yanaendelea hapa nchini bila watu
kuyafahamu.Ili twende sawa
itanilazimu nikueleze ukweli wote”
Akasema Austin na kumsimulia
Monica kuhusiana na Alberto’s na
yeye kutaka kuuawa Somalia hadi
alivyokombolewa na kwenda
kuishi Afrika kusini.
“Baada ya kikwazo
kuondolewa ambacho kilikuwa ni
mimi,Alberto’s waliendela na
mikakati yao ya kujimarisha hapa
nchini na walifanikiwa kuusimika
utawala wao na Ernest Mkasa
akiwa ni kiongozi wa kwanza wa
Tanzania kuwa chini yao.Rais
Ernest amechaguliwa na wananchi
kwa kura nyingi lakini amekalia
kiti cha urais kama sanamu.Hana
maamuzi yoyote bali nchi
inaongozwa na Alberto’s.Wao ndio
wenye kupanga kila kitu kiende
vipi hapa nchini na Ernest ni
mtekelezaji tu wa maelekezo
yao.Alberto’s tayari wamekwisha
imarisha mizizi yao hapa
nchini.Tayari wana mzizi wao
mkuu ambaye ni rais ,pia yupo
makamu wa rais,waziri
mkuu,wanayo pia idadi kubwa ya
wabunge wafuasi wao bungeni
.Wamejiimarisha katika sehemu
zote za muhimu ili kusitokee
kukwama katika sehemu yoyote na
ndiyo maana hivi karibuni ulitaka
kupelekwa muswada bungeni wa
haki za binadamu ambao ndani
yake una vipengele vinavyotamka
kuwatambua watu wanaojihusisha
na mapenzi ya jinsia moja,utoaji
mimba nk.Nadhani mpaka hapo
tayari umepata picha namna hawa
jamaa wanavyoliharibu taifa letu.”
Akasema Austin baada ya muda
akaendelea
“Nilipoonana na rais kwa
mara ya kwanza siku aliyokuwa
ananikabidhi kazi yake nimfanyie
nilimuuuliza kama na yeye ni
mfuasi wao akanijibu kuwa yeye si
mfuasi bali ameshinikizwa na wale
jamaa awe rais lakini hapendezwi
na kitendo cha yeye kuwekwa
kama sanamu bila kuwa na nguvu
yoyote kama rais.Nilimshauri
kama kweli anachukizwa na
Alberto’s basi tuunganishe nguvu
na tuwaondoe hapa nchini.Rais
akakubali na nikampa maelekezo
yangu namna ya kuanza
kupambana na
Alberto’s.Nilimshauri kwanza
kuufutilia mbali muswada ule wa
haki za binadamu uliokuwa
unatarajia kuwasilishwa
bungeni.Kama hiyo haitoshi
nilimshauri pia kumuondoa waziri
mkuu katika nafasi yake na
kulivunja baraza lote la
mawaziri.Nikamshauri pia
amuondoe mkuu wa majeshi ili
awe na uhakika kwamba Alberto’s
hawatatumia jeshi
kumuangusha.Yote haya
aliyatekeleza bila tatizo na
mliyasikia”
“Austin haya unayonieleza ni
mambo ya kweli? Akauliza Monica
“Don’t you trust me? Austin
naye akauliza
“Ofcourse I do trust you.Ila
mambo uliyonieleza ni makubwa
na mazito.”
“Ni kweli Monica mambo haya
ni makubwa na yanaogopesha
ukiyasikia lakini ndiyo hali
halisi.Nchi yetu imefikia hapo”
akanyamaza tena kidogo halafu
akasema
“Rais alinipa kazi mbili
nimfanyie.Kazi ya kwanza ilikuwa
ni kumtoa hospitali rafiki yako
Marcelo” akasema Austin na kuzidi
kumshangaza Monica.
“Ni wewe ndiye ulimtoa
Marcelo hospitali?!! Akauliza
Monica.Alishangaa sana
“Ndiyo ni mimi.Rais alipokea
ombi toka kwaDavid Zumo na
akanipa mimi kazi ya kwenda
kumtoa Marcelo hospitali.”
Monica akajikuta akiinuka na
kwenda kumkumbatia Austin
“Austin sikujua kama u mtu
muhimu namna hii.Jana
nilikuchukia na sikutaka hata
kukuona tena lakini kumbe
nilifanya kosa kubwa” Akasema
Monica na kama ilivyo kawaida
yake machozi yake yako karibu
sana akashindwa kuyazuia.Austin
akatabasamu halafu akaendelea
“Makubaliano yangu na rais
yalikuwa kuanza operesheni ya
kuwaondoa Alberto’s baada ya
kuzikamilisha kazi zake zote mbili
na wakati nikiwa katika harakati
za kuikamilisha kazi yake ya pili
likatokea lile tukio la kupigwa
risasi na Maria na mambo
yakaanza kuharibikia
hapo.Tuligundua kwamba Maria ni
mfuasi wa kikundi cha kigaidi cha
IS na hapa nchini alikuja kwa lengo
la kumtafuta mama yake anaitwa
Yasmin Esfahani.Huyu Yasmin ni
mfuasi wa IS aliyekuwa
amefungwa mahala pa siri hapa
nchini kwa zaidi ya miaka
kumi.Tulianza kumtafuta Yasmin
na ilinilazimu kumuuliza rais
kama ana taarifa zozote za
kuhusiana na Yasmin akasema
kwamba hana taarifa zozote na
akaomba nimpe muda ili alifanyie
kazi suala hilo.Baade aliomba
kuzungumza na Maria na ghafla
Maria akabadili lugha akaanza
kuzungumza kiarabu lugha
ninayoifahamu vyema.Niligundua
kwamba alikuwa anazungumza na
mama yake ambaye ni Yasmin
.Baadae rais akanipigia simu na
kuniambia kwamba anamuhitaji
Maria jana saa nne asubuhi .Mimi
na wenzangu tulijiuliza maswali
mengi kuhusiana na hiki
alichokifanya rais.Alikiri
kutomfahamu Yasmin lakini
baadae akampa simu Yasmin
azungumze na
mwanae.Tulishangaa sana na
kuweka alama ya kiulizo.Jana
ilinilazimu kutumia mbinu
kuzungumza na Yasmin na
tukafikia makubaliano kwamba
nitakapompatia mwanae atanipa
kitu kikubwa.Usiku wa jana
akanipigia simu na kuniomba
nikamchukue Zanzibar kwani
alikuwa katika hatari na ndiyo
maana nikalazimika kuja kwako
kukuomba msaada.Sikutaka rais
afahamu chochote kuhusu mimi
kwenda Zanzibar kwani angejua
lazima ninakwenda kumchukua
Yasmin. Nashukuru ulinisaidia
sana na tukafanikisha kumpata
Yasmin ambaye tunaye mikononi
mwetu.Yasmin kama
nilivyokueleza kwamba ni mfuasi
wa kikundi cha kigaidi cha IS na
alikuwa amefungwa hapa Tanzania
baada ya kukamatwa akiwa katika
harakati za kueneza kikundi cha IS
Afrika mashariki, amenieleza
kwamba aliachiwa huru na rais
baada ya kufanyika makubaliano
kati ya rais na Alshabaab.”
“Alshabaab?!! Monica
akashangaa
“Ndiyo.Rais amefanya
makubaliano na Alshabaab na
katika makubaliano hayo
waliafikiana kwamba Yasmin na
mtu mwingine ambaye amekuwa
mpangaji mkubwa wa
mashambulio mbali mbali ya
Alshabaab anaitwa Tariq
waachiwe huru.Rais alitekeleza
makubaliano yao na kuwaachia
huru Yasmin na Tariq.Wakiwa
Zanzibar Yasmin alimuua Tariq na
akanipigia simu kunitaka
nikamchukue na lengo hasa la
kumleta Dar es salaam ni
kukamilisha makubaliano kati
yetu na yeye.Kuna mambo ambayo
tunayataka toka kwake na yeye
kuna mambo anayataka toka
kwetu” akasema Austin
“Austin umenistua sana kwa
haya mambo uliyonieleza.Rais
wetu anawezaje kuwa na
makubaliano au hata mawasiliano
na Alshabaab watu ambao ni jana
tu wametushambulia na kuua watu
wengi wakiwemo viongozi
wakubwa? Monica akashangaa
“Mpaka sasa hatufahamu ni
kitu gani hasa kilichopelekea rais
aingie katika makubaliano na
Alshabaab kiasi cha kuwaachia
huru watu wale wawili hatari”
akasema Austin
“Austin nimeogopa
sana.Sikuwahi hata kuota kama
rais wetu anaweza akafanya
mambo kama haya.”
“Monica mimi na wenzangu
tuko kazini hivi sasa
kutakakufahamu ni kitu gani
ambacho rais alikubaliana na
Alshabaab hadi akafikia hatua ya
kuwaachia watu wale wawili.Kitu
kingine ambacho huwezi ukaamini
na ambacho naomba ibaki kuwa
siri yako ni kwamba Alshabaab
pamoja na kuachiwa watu wao
wawili walitaka pia hati ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar”
“ What ?!! Akasema Monica
kwa mshangao akainuka na
kushika kiuno.
“Alshabaab wametaka nini?
“Katika makubaliano hayo
Alshabaab walitaka pia wapewe
hati ya muungano wa Tanganyika
na Zanzibar”
“Austin that’s a lie.It’s not
true.Alshabaab hawawezi kutaka
kitu kama hicho ambacho ni
ngumu kukipata.Kwa nini kwanza
watake kitu kama hicho? Akauliza
Monica
“Lengo kuu ni kuigawa nchi hii
vipande vipande.” Akasema Austin
Monica akamtazama Austin
halafu akasema
“Tafadhali Austin usiniambie
kwamba rais tayari amewapa
Alshabaab hati ya muungano wetu”
akasema Monica
“Usistuke Monica lakini tayari
rais amekwisha itoa hati hiyo na
alimkabidhi Yasmin” akasema
Austin
“Jesus Christ !! akasema
Monica na kuweka mikono
kichwani
“Nini kimeikumba nchi
yangu?? Akasema kwa sauti
ndogo.Ulipita ukimya wa sekunde
kadhaa halafu Monica akasema
“Austin tayari mnaye Yasmin
.Ichukue hiyo hati ya muungano na
ufanyike utaratibu wa kuiorejesha
mahala inakohifadhiwa ikulu
halafu huyu rais anatakiwa
kushtakiwa kwa hili alilolifanya la
kucheza na muungano wetu kiasi
hiki !! akasema Monica kwa hasira
“It’s not that easy Monica.Ni
kweli Yasmin anayo hati lakini ili
kuipata hati hiyo kuna mambo
ambayo Yasmin anayataka
tumfanyie kwanza ndipo
atuonyeshe mahala alipoificha
hiyo hati”
“Hayuko nayo mkononi?
Akauliza Monica
“Hapana hayuko nayo
mkononi.Anadai kuna mahala
ameificha na atatuelekeza mahala
hapo endapo tutamtimizia mambo
anayoyataka.”
“Mungu wangu !! Monica
akahisi kuchanganyikiwa.
“Kwa nini nchi yetu
inachezewa kiasi hiki? Austin hati
hiyo ndiyo chimbuko la kuzaliwa
Tanzania.Usithubutu tafadhali
kuacha kitu muhimu kama hiki
kikachezewa namna hii.Wazee
wetu waliitunza hati hiyo kwa kila
uwezo waliokuwanao lakini leo hii
inatolewa kama vile si kitu
chochote.Tafadhali fanya kila
unaloweza kufanya ili kuipata hati
hiyo.Kwani huyo Yasmin anataka
kitu gani? Akauliza Monica
“Thank you Lord.Hapa ndipo
nilipokuwa napatafuta.Amefika
mwenyewe” akawaza Austin.
“Kwa maelezo yake,amekiri
kwamba baada ya kukaa muda
mrefu gerezani ameamua kuacha
na IS kwa hiyo anataka kwenda
kuishi mbali yeye na mwanae
ambako hawataweza kutambuliwa
na IS.Tukilifanikisha hilo
atatueleza mahala alikoificha hiyo
hati ya muungano” akasema Austin
“Mmekubali kumtekelezea
jambo hilo? Akauliza Monica
“Hatuna namna ya kuweza
kuipata hati hiyo zaidi ya kukubali
kutekeleza anachotaka” akasema
Austin.Monica akamtazama kisha
akasema
“Doyou believe her?
“Yes I do” akajibu Austin
“Kwa hiyo mtalitekelezaje
ombi lake?Monica akauliza
“Utekelezaji wake ni mgumu
kwa sababu anatakiwa kupata pasi
mpya za kusafiria yeye na
mwanae,vile vile tunatakiwa
kupata nchi ambayo itakubali
kuwapokea na kuwahifadhi na hii
lazima iwe ni katika nchi za ulaya
au Amerika.Hatuwezi kumpeleka
katika nchi za kiarabu au
Asia.Anajulikana sana huko na ni
rahisi kugundulika na IS.Jambo la
tatu linalofanya jambo hili liwe
gumu ni kiasi kikubwa cha fedha
kinachohitajika ili
kulikamilisha.Endapo mahusiano
yangu na rais yangekuwa mazuri
basi suala hili lingemalizika kwa
urahisi sana lakini mimi na rais
kwa sasa hatupikwi chungu
kimoja”
“What are you going to do?
akauliza Yasmin
“I need your help”
“My h elp?!! Monica akauliza
“NdiyoMonica nahitaji sana
msaada wako.Hata kama
usingenitafuta ,mimi
ningekutafuta kwani kwa sasa ni
wewe tu ambaye unaweza
kutusadia” Akasema Austin
“Austin mambo uliyonieleza
yamenistua na kuniogopesha mno
lakini sina namna yoyote ya
kukusaidieni.Jana nilikusaidia
lakini ona yaliyonitokea.Nusura
tungepoteza uhai baada ya
kupeleka ndege kutua katika
daraja la nyerere.Siwezi kulisahau
tukio lile baya kabisa katika
maisha ” akasema Monica
“Monica ulihitaji nikueleze
ukweli na nimekueleza
ukweli.Hakuna mtu mwingine
ukiacha mimi na wenzangu
anayelifahamu suala hili zaidi
yako.Tafadhali naomba
utusaidie.You’re not doing this for
me but for your country.Juhudi
zetu zote tulizozifanya hadi kufikia
hapa haziwezi kuwa na maana
endapo tutashindwa kutimiza
mahitaji ya Yasmin na hivyo
kuikosa hati ya muungano”
Monica aliyekuwa
amesimama akaketi sofani
akazama katika tafakari halafu
akasema
“Unahitaji nikusaidie kitu gani
Austin?
“Msaada mkubwa ninaouhitaji
ni kuwaondoa Yasmin na mwanae
hapa nchini na kisha tuwatafutie
nchi ya kwenda kuishi pamoja na
namna watakavyoyaendesha
maisha yao.”akasema Austin
“How do you want me to
help,call president again and ask
for help? No I wont do that.Siwezi
kumuomba msaada tena shetani
kama Yule!! Akasema Monica kwa
ukali.Akatazamana na Austin
halafu akasema
“Lakini kuna kitu tunaweza
tukafanya” Akanyamaza na
kushika kichwa
“I didn’t want to do this but I
have to” akawaza Monica kisha
akasema.
“Austin kuna jambo moja
tunaweza kulifanya.Ninasema
tunaweza kulifanya kwa sababu
tayari na mimi nimo katika suala
hili” Akanyamaza tena halafu
akasema
“Nilikueleza kwamba niko
katika mahusiano na David Zumo
ambaye mke wake amefariki na
kesho anazikwa.Jioni ya leo David
atatuma ndege yake kubwa kuja
kunichukua mimi na familia yangu
kwenda kuhudhuria mazishi hapo
kesho.Tunaweza kuitumia ndege
hiyo kuwaondoa akina Yasmin
hapa nchini tukawapeleka Congo
tukifika kule nitaubeba mimi
mzigo na kumuomba David
anisaidie kuwatafutia nchi ya
kwenda kuishi.Yule ni mtu
mkubwa na suala kama hili
haliwezi kumshinda.Nadhani huo
ni msaada mkubwa ambao
ninaweza kuufanya ili kukusaidia
katika suala hili” Akasema
Monica.Austin akainuka na
kwenda kumshika mkono
“Monica ahsante
sana.Ninakushukuru mno kwa
kujitolea katika jambo hili.”
Akasema Austin
“Austin nimejitolea kufanya
hivi baada ya kuziona juhudi zako
katika kuipigania nchi yako kwa
hiyo lazima nikuunge mkono lakini
naomba uwe na uhakika kwamba
Yasmin anayo hiyo hati na si
kutuchezea akili zetu.Japokuwa
tutamuondoa hapa Tanzania lakini
hatakwenda kokote,ataendelea
kuwa chini ya ulinzi hadi
tuhakikishe kwamba tumeipata
hati yetu” akasema Monica
“Monica nina uhakika
mkubwa Yasmin anayo hati hiyo
na endapo tutamtimizia hicho
anachokitaka basi tutaipata”
akasema Austin
“Austin ninaomba uniahidi
kitu kimoja”akasema Monica.
“Endapo tukifanikiwa kuipata
hati ya muungano ,niahidi kwamba
rais lazima afikishwe mbele ya
sheria.Lazima akajibu shtaka la
kuichezea nchi yetu kiasi hiki”
Akasema Monica
“Monica lazima rais afikishwe
mbele ya sheria kwa kuuchezea
muungano ambao aliapa
kuulinda.Hata hivyo kuna kitu cha
muhimu ambacho unapaswa
kukifahamu kuhusu rais
kwan….”Monica hakutaka kumpa
nafasi Austin ya kumaliza kile
alichotaka kukisema akamkatisha
“Austin sitaki kusikia
chochote kuhusiana na yule
rais.Hakuna sababu yoyote
inayoweza kumsaidia asifikishwe
mbele ya sheria kujibu kosa la
kuichezea nchi yetu kiasi hiki.Yeye
na wenzake wote lazima
waadhibiwe na liwe fundisho kwa
wengine wote watakaokuja
kutothubutu kucheza na nchi
yetu.Austin yule mzee ni
shetani.Laiti ungenieleza toka
mapema mambo haya
nisingemkubalia kitu
alichoniomba jana .Najuta sana
kwa kumuahidi kumsaidia
kukupata wewe.Leo hii asubuhi
nimepigiwa simu na mkuu wa
idara ya usalama wa taifa anaitwa
Silvanus nani sijui anasema
kwamba amekabidhiwa na rais
jukumu la kukutafuta na alikuwa
anauliza kama tayari nimekupigia
simu.Nilimjibu bado akaniambia
kwamba kuna vijana wake
atawatuma ili nipige simu nikiwa
nao waweze kufahamu mahala
ulipo na wakuvamie.Rais anatumia
nguvu kubwa sana kukutafuta
kumbe anafahamu tayari
unafahamu madhambi yake”
Akasema Monica
“Monica hawa jamaa
watakuandama kwani wanajua
kabisa kwamba wewe una
mawasiliano nami kwa hiyo
umakini mkubwa sana
unahitajika.Sintoitumia tena ile
simu yangu bali mawasiliano yote
yatafanywa kwa kutumia ile simu
ya Amarachi.halikadhalika wewe
usitumie simu yako kuwasiliana
name kwani wanaweza wakawa
wanafuatilia mawasiliano yako
kujua kama unawasiliana nami
kwa siri”
“Kuhusu simu hakuna tatizo
kwani nina simu zaidi ya tatu
nitakupa moja kwa ajili ya
kuwasiliana.Ile simu yenye namba
aliyonayo Silvanus sintoitumia
kuwasiliana nawe bali itakuwa ni
kwa ajili ya mawasiliano na David”
“Good. Saa ngapi unategemea
kuondoka kueleka Kinshasa.?
“Saa kumi za jioni.”
“Sawa .Tutawasiliana mambo
yanavyokwenda.Mimi na
wenzangu tunakwenda kuandaa
mpango namna ya kuweza
kuwaondoa akina Yasmin hadi
ndani ya ndege .Tutawasiliana
baadae nitakujulisha kila kitu
kitakavyokwenda” Akasema
Austin
“Monica haya niliyokueleza
usithubutu kumueleza mtu yeyote
yule.Hii ni siri yangu mimi na
wewe” akasema Austin
“ Usihofu Austin.” Akasema
Monica na kabla Austin
hajaondoka akampatia simu moja
halafu Austin na Amarachi
wakaeleka katika gari na
kuondoka kurejea nyumbani
kwao.
Baada ya Austin na Amarachi
kuondoka,Monica akampigia simu
Silvanus Kiwembe na kumuelekeza
sehemu ambako atakutana na wale
watu wa usalama wa Taifa ili
awasiliane na Austin.
“Dah ! mambo niliyoyasikia
toka kwa Austin ni mazito
mno.Sasa nimefahamu kwa nini
rais anatumia nguvu kubwa
kumsaka Austin.Kumbe ni kwa
sababu ya mambo ya kishenzi
anayoyafanya.Anathubutuje kuwa
na mahusiano na Alshabaab ambao
wameua watu wengi wasio na
hatia jana? Anathubutuje kuitoa
hati ya muungano wetu kwa
magaidi hawa? Lengo lao ni nini
hasa? Halafu kuna hawa
Alberto’s.Nchi yetu imekumbwa na
balaa gani? Nawasifu sana Austin
na wenzake kwa ujasiri
walionao.Wameyatoa maisha yao
kupigania nchi.Lazima niwasaidie
na tuhakikishe tunawaondoa wale
wote wasiotutakia mema.Mtu
yeyote mwenye mapenzi mema na
nchi yake hatathubutu kuvumilia
uchafu huu unaofanywa na rais na
genge lake.Mwisho wao uko karibu
sana na watafahamu kwamba
wapo vijana wazalendo ambao
hawaogopi kumwaga damu kwa
ajili ya nchi yao”akawaza Monica
“How did it go? Amarachi
akamuuliza Austin wakiwa garini
baada ya kutoka nyumbani kwa
wazazi wa Monica
“Ni mambo mazito lakini
Mungu amenyoosha mkono wake
na mambo yanakwenda
vyema.Jana usiku Monica aliitwa
na rais ikulu”
“Aliitwa ikulu?!! Amarachi
akashangaa
“Ndiyo.Rais alimtaka aende
ikulu na akamuhoji kuhusiana na
kilichokuwa kimetokea.Alipata
taarifa za wale wanausalama
tuliowapoteza fahamu ndiyo mana
wakaweka vikosi pale uwanja wa
ndege watukamate watuhoji na
wajue nini kilichotokea.Bahati
nzuri tulistuka mapema na
kwenda kutua
darajani.Tusingefanya vile
tungekuwa ndani hivi sasa na
tungeharibukila kitu.Monica
alimueleza rais kila kitu
kilichotokea na rais akamuahidi
akamuomba amsaidie kuweza
kunipata.Alimuomba asubuhi ya
leo anipigie simu na aombe
kukutana nami na baada ya hapo
amtaarifu mahala tulikopanga
kukutana halafu angewatuma
vijana wake kuja
kutukamata.Lengo kubwa la rais ni
kumpata Yasmin ili aweze kuipata
ile hati.”Austin akanyamaza
“The situation is geting ugly”
akasema Amarachi
“Rais anatumia uwezo wake
wote kuhakikisha kwamba
anatupata kwani tayari tumekuwa
hatari kwake.Nimemueleza Monica
kila kitu na amestuka
sana.Hakutegemea kabisa kusikia
mambo makubwa kama yale.”
“Ulimueleza kama rais ni baba
yake? Amarachi akauliza
“Hapana.Sikuweza kufanya
hivyo kwa namna alivyoonyesha
hasira kwa rais.Baada ya
kumueleza kila kitu nilimuomba
atusaidie na amekubal
kutusaidia.Leo saa kumi ndege ya
rais wa Congo itakuja kumchukua
yeye na familia yake kwa ajili ya
kwenda Kinshasa katika msiba wa
mke wa David Zumo.Tutaongozana
na Monica hadi Congo na kufika
kule Monica atamuomba David
Zumo amsaidie kumtafutia Yasmin
na mwanae makazi katika nchi ya
mbali ambako hataweza
kujulikana na IS.Mimi na wewe
tutaongozana na akina Yasmin
kwenda Congo, Job atabaki hapa ili
Yasmin akituelekeza mahala ilipo
hati akaichukue na kuiifadhi
.Hatutamuachia Yasmin hadi hapo
atakapotuelekeza mahala
alikoiweka hati hiyo.Bado tuna
mlima mrefu wa kupanda.Lazima
tuhakikishe rais Ernest
anafikishwa mbele ya sheria kwa
mambo maovu aliyoyafanya kwa
nchi hii” akasema Austin
“Vipi kuhusu Boaz yeye
tutamfanya nini? Amarachi
akauliza
“Nilikuwa na hasira naye sana
kwa mambo aliyomfanyia mdogo
wangu Linda lakini nafikiria
kumpa nafasi nyingine na
kumuunganisha na akina Yasmin
kwenda kuanza maisha
mapya.Ninauthamini mchango
wake wa kuniokoa toka katika
mikono ya Alshabaab kwa hiyo
nitamshawishi Yasmin aongozane
naye kama atakuwa tayari”
akasema Austin
 
SEASON 7: SEHEMU YA 6
Habari kubwa iliyotawala
vyombo vingi vya habari duniani
bado ilikuwa ni ile ya
mashambulio mawili ya kigaidi
yaliyotokea Tanzania na kupoteza
maisha ya mamia ya watu
wakiwamo viongozi.Vyombo vingi
vya habari vya ndani na nje
vilijitahidi kutangaza au kuandika
habari hii kwa kila namna
walivyoweza.Viongozi wa mataifa
mbali mbali duniani waliendelea
kutuma salamu za pole kwa rais
wa Tanzania kwa tukio lile la
kusikitisha.Wengi waliahidi
msaada mkubwa kwa ajili ya
kuhakikisha wale wote
waliohusika na tukio lile
wanaadhibiwa vikali.
Asubuhi hii Tanzania
iliamshwa na habari mpya ambapo
jeshi la wananchi wa Tanzania
lilikuwa limeshambulia na
kuzisambaratisha kabisa kambi
mbili za Alshabaab mapema
alfajiri.Wananchi wengi
waliupongeza uamuzi ule wa
haraka wa kuwashambulia
Alshabaab na kutaka nguvu kubwa
zaidi iongezwe ili kuhakikisha
kundi hilo linamalizwa kabisa.
Saa mbili za asubuhi rais
alikutana na viongozi wa juu wa
vyombo vya ulinzi na usalama
ambapo alitaarifiwa kwamba kazi
ya kufukua vifusi na kutafuta miili
ya waliopoteza maisha katika
majengo yaliyolipuliwa ilikamilika
usiku .Idadi ya waliopoteza maisha
katika shambulio la Dar es salaam
ilikuwa ni watu mia tatu na ishirini
na saba.Mjini Dodoma waliopotea
maisha walikuwa ni mia nne
thelathini na tisa.Watu ambao
tayari walikwisha tambuliwa kuwa
miongoni mwa waliofariki dunia ni
makamu wa rais,waziri mkuu
aliyevuliwa madaraka na wengine
ni wafanya biashara wakubwa na
wote walikuwemo katika hoteli ile
iliyolipuliwa.Miili mingine
iliharibika vibaya na waliendelea
kuitambua kwa vipimo vya
vinasaba.
Mkuu wa majeshi Jenerali
Lameck msuba alitoa taarifa ya
shambulio lililofanywa na kikosi
cha anga na kuziharibu vibaya
kambi mbili za wapiganaji wa
Alshabaab na kuahidi
mashambulizi zaidi kwa kundi hili
kubwa
Wakati kikao kikiendelea
ikulu kati ya rais na wakuu wa
vyombovya usalama ,mkuu wa
idara ya usalama wa taifa Silvanus
Kiwembe na vijana wake walikuwa
katika operesheni nzito ya
kuhakikisha wanampata Austin
kwa namna yoyote ile.Tayari
Monica alikwisha kutana na watu
wawili toka usalama wa taifa
akampigia simu Austin mbele yao
lakini simu hiyo haikuwa
ikipatikana.Pamoja na simu ya
Austin kutopatikana bado
waliendelea na mikakati ya
kumfuatilia Monica kwani ndiye
hasa anayewasiliana na Austin
.Tayari walipafahamu nyumbani
kwake na kikatumwa kikosi cha
watu nane wakiwa na magari
mawili kumfuatilia Monica kila
anakokwenda na kuchunguza kila
anachokifanya.
Pembeni ya nyumba ya
Monica kulikuwa na shamba lenye
minazi na mikorosho.Mtu mmoja
aliyejifunga msuli akiwa na panga
mkononi huku akitafuna muwa
aliwasili katika shamba lile na
kuzunguka zunguka na baada ya
dakika tano akatokea mwanamke
mmoja aliyevaa mavazi kuu kuu
akaungana na Yule jamaa
wakaendelea kuzunguka katika
shamba lile.Watu wale hawakuwa
wakulima wala wamiliki wa lile
shamba bali ni wapelelezi
waliotumwa kufanya uchunguzi
katika nyumba ya Monica.Yule
mwanaume alipanda mnazi mmoja
mrefu na alipofika juu alitega
kamera ambayo aliielekeza
nyumbani kwa Monica ambayo
iliunganishwa na kompyuta
iliyokuwa katika gari lao mita
kadhaa toka nyumba ya Monica na
kuwawezesha kutazama kila
kilichokuwa kinaendelea pale
ndani katiak nyumba ya
Monica.Baada ya kukamilisha kazi
yake akashuka na kuongozana na
Yule mwanamke aliyeonekana
kama mke wake wakaondoka.
Mita kadhaa toka nyumbani
kwa Monica gari mbili zilikuwa
zimeegeshwa zikiwa na timu ya
wapelelezi waliokuwa wakifuatilia
nyendo za Monica.Baada tu ya
kamera ile kutegwa walianza
kupata picha moja kwa moja
kutoka ndani ya nyumba ya
Monica.
“Mkuu kila kitu kinakwenda
vizuri na tayari tumefunga kamera
tunaweza kuona kila
kinachoendelea pale
ndani.Tunawaunganisha makao
makuu ili muweze kushuhudia kila
kinachoendelea hapa” Akasema
kiongozi wa timu ile akimtaarifu
Silvanus
“Good.Nataka muwe na
mawasiliano ya karibu sana na
timu nyingine zilizo sehemu mbali
mbali zinazoendelea na zoezi hili
na endapo kuna timu itagundua
jambo lolote ambalo si la kawaida
taarifa ya haraka inatakiwa”
Akasema Silvanus akiwasiliana na
vijana wake aliowapanga karibu
na nyumba ya Monica.
SEASON 7: SEHEMU YA 7
Saa nne za asubuhi kikao kati
ya rais na wakuu wa vyombo vya
usalama kilimalizika na rais
akatoka ikulu akaelekea kwanza
hospitali kuhakiki kama kweli
makamu wa rais amefariki
dunia.Baada ya hapo akaelekea
katika eneo la hoteli
iliyoshambuliwa. Toka hapo
akaelekea nyumbani kwa makamu
wa rais kutoa pole. Na kusaini
kitabu cha maombolezo.Kwa kuwa
alikuwa na ratiba ndefu siku hii
hakukaa sana hapo nyumbani kwa
makamu wa rais akaelekea uwanja
wa ndege kwa ajili ya safari ya
kuelekea Dodoma katika viwanja
vya bunge ambako angelihutubia
taifa kutokea pale.Katika safari hii
alikuwa ameambatana na mkuu
wa majeshi Jenerali Lameck Msuba
“ Kuna taarifa zozote toka kwa
Silva? Akauliza rais wakiwa
ndegeni
“Mpaka sasa hakuna taarifa
yoyote.Nimewasiliana na Silva
kabla yakupanda ndegeni
amenielza kwamba bado
wanaendelea na zoezi lakini
mpaka sasa hakuna chochote
walichokipata”
“Lameck simamia zoezi hili
kwa karibu sana na hakikisha ka
namna yoyote kabla ya jua kuzama
siku ya leo Austin na Yasmin wawe
wamepatikana.Tukiwakosa leo
itakuwa vigumu sana kuwapata
tena ” Akasema Rais

SEASON 7: SEHEMU YA 8

Austin na Amarachi walirejea
katika makazi yao .Tayari
watuwote walikwisha
amka.Akawaeleza Job na Marcelo
kila kitu alichoelezwa na Monica
halafu akamfuata Yasmin
aliyekuwa chumbani kwake.
“Umeamkaje Yasmin?
Akauliza Austin
“Mimi niko salama
Austin.Sijapata usingizi nikiwaza
namna mwanangu anavyoteseka
.Austin tafadhali naomba
umfungue Shamim awe
huru.Hatakwenda sehemu
yoyote.Niko tayari nifungwe mimi
badala yake” akasema Yasmin
“Yasmin usijali mambo haya
yatakwisha si muda mrefu
sana.Leo jioni tutaondoka
kuelekea Kinshasa na kutokea pale
kila kitu unachokihitaji
kitakamilika.Nina rudia tena
kukuonya Yasmin tafadhali usiwe
unatuambia uongo.Endapo
utakuwa unatudanganya
nakuhakikishia nitakuua wewe na
mwanao.Maisha yetu tunayaweka
rehani kwa ajili ya kuipata hiyo
hati na tukifika Kinshasa
tutaendelea kukushikilia wewe na
mwanao hadi pale
utakapotuonyesha ilipo hati ndipo
tutakapo waachia muende”
akasema Austin
“Austin usiwe na hofu.Siwezi
kukudanganya.Yote niliyokuambia
ni ya kweli kabisa.Nchi gani
umepanga kunipeleka? Akauliza
Yasmin
“Utachagua wewe mwenyewe
unataka kwenda nchi gani lakini ni
hadi tufanikiwe kufika Kinshasa
salama.” Akasema Austin na
kugeuka kutaka kutoka Yasmin
akamuita
“Austin naomba tafadhali
uniruhusu nionane na Boaz.Ni
miaka mingi sijaonana naye”
“Boaz utaonana naye hapo
baadae kwani utaongozana naye
kwenda huko mbali unakotaka
kwenda.Nimeamua kumsamehe ili
aende zake kutokana na wema
aliowahi kunitendea” Akasema
Austin na kutoka akaenda sebuleni
kuendelea na majadiliano na
wenzake
Mjadala uliokuwa mezani ni
namna watakavyoweza kufika
salama uwanja wa ndege .
“Kama nilivyowapa taarifa
niliyoipata toka kwa Monica,rais
amewekeza nguvu kubwa
kutusaka.Tayari anafahamu kuwa
tunaye Yasmin na mpaka muda
huu tayari atakuwa ametueleza
kila kitu kwa hiyo basi kila aina ya
nguvu itatumika kuhakikisha
tunapatikana ili mambo yake
yaendelee kuwa siri.Monica
alimuahidi rais kumsaidia
kunipata na kwa sasa ndiye
tegemeo lao kuu kwa hiyo lazima
wamfuatilie bila yeye
kufahamu.Zoezi hili la kuambatana
na Monica halitaweza kuwa rahisi
sana lakini lazima tuhakikishe
Yasmin anafikishwa uwanja wa
ndege na kuelekea
Congo.Nitaongozana na Amarachi
kwenda Congo.Job na Marcelo
mtabaki hapa.Yasmin
atakapoelekeza mahala ilipo hati
Job utakwenda kuichukua na sisi
ndipo tutakapomuachia Yasmin
aende zake” akasema Austin kisha
wakaendelea kujadiliana kuhusu
jambo lile.
 
Back
Top Bottom