SEASON 7: SEHEMU YA 10
Rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzani Ernest Mkasa aliwasili
mjini Dodoma.Akapokelewa na
viongozi wa mkoa wa Dodoma
kisha akaelekea katika ikulu ya
Dodoma akapata taarifa fupi toka
kwa uongozi wa mkoa kuhusiana
na hatua zilizochukuliwa na
usalama ulivyoimarishwa toka
lilipotokea shambulio katika
ukumbi wa bunge.Baada ya
kupokea taarifa fupi toka uongozi
wa mkoa rais na msafara wake
wakaelekea katika viwanja vya
bunge kwa ajili ya kuangalia
uharibifu uliofanywa na vile vile
kulihutubia taifa.Watu walikuwa
ni wengi sana katika viwanja vya
bunge na ulinzi ulikuwa
mkali.Ukiacha vikosi vya askari wa
miguu kulikuweo pia na askari wa
farasi,mbwa na angani kulikuwa
na helkopta za polisi zikipiga
doria.
Rais alifika katika viwanja vya
bunge akaongozwa na mkuu wa
mkoa .Kwa kawaida rais akifika
bungeni mwenyeji wake huwa ni
spika wa bunge lakini siku hii
mwenyeji wake alikuwa ni mkuu
wa mkoa kwani spika wa bunge na
wasaidizi wake wote ni miongoni
mwa watu waliopoteza maisha
katika shambulio lile.Baada ya
kumaliza kukagua uharibifu
uliotokea rais akaelekea eneo
aliloandaliwa .Vongozi wa dini
toka madhehebu mbalimbali
wakatoa maombi na kisha
zikafuata salamu toka kwa watu na
makundi mbalimbali wakiwemo
baadhi ya mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao hapa
nchini ambao walitoa salamu za
pole kwa wananchi wa Tanzania
kwa niaba ya mataifa
wanayoyawakilisha.Zoezi la
salamu ilipomalizika rais wa
jamhuriya muungano wa Tanzania
akapewa nafasi ya kuhutubia taifa.
“ Vizazi na vizazi
vijavyo,vitaikumbuka tarehe ya jana
kama tarehe mbaya kabisa katika
historia ya nchi yetu baada ya ndugu
zetu,wapendwa wetu,baba,mama
kaka na dad zetu kuuawa kikatili
katika shambulio la kigaidi.”
Ndiyo alivyoanza hotuba yake.
“Ndugu zangu watanzania
,nimesimama hapa na sijui
nizungumze kitu gani kwa tukio hili
ambalo itafaa likiitwa ni unyama
uliopitiliza.Sioni neno la kuzunguma
kuipa faraja mioyo yenu kwani kila
mmoja ameumizwa vibaya sana na
jambo hili.Itoshe kusema poleni sana
ndugu zangu watanzania.”
Jana majira ya saa kumi na mbili
za jioni wakati watanzania
wakiendelea na shughuli zao za kila
siku ghafla walistushwa na taarifa
mbaya baada ya kufanyika kwa
mashambulio makubwa mawili.Moja
ni katika hoteli jijini Dar es salaam na
lingine ni katika jengo la bunge hapa
Dodoma.Mashambulio yote haya
mawili yamefanywa na watu
wasiotutakia mema ,watu
wasiopendezwa na maendeleo na
ustawi wa nchi yetu,wasiopenda
amani iliyotamalaki katika kila pembe
ya nchi yetu.Ni tukio lililoushangaza
ulimwengu wote kwani Tanzania
inajulikana kwa amani na utulivu
wake na hatuna ugomvi na majirani
zetu.
Vikosi vya majeshi yetu
vimefanya kazi usiku kucha kufukua
maiti zilizokuwa katika vifusi na vile
vile kujaribu kutafuta kama kuna
majeruhi au manusura na leo asubuhi
nimekabidhiwa ripoti inayoonyesha
katika shambulio la Dar es salaam
watu wapatao mia tatu na ishirini na
saba wamepoteza maisha .Mjini
Dodoma waliopoteza maisha
walikuwa ni mia nne thelathini na tisa
na idadi kubwa ikiwa ni wabunge
wetu waliokuwa wakitekeleza
majukumu yao waliyotumwa na
wananchi wao.Vile vile ndani ya
ukumbi wa bunge kulikuwa na wageni
mbalimbali waliotembelea bunge na
wengi kati yao walikuwa wanafunzi
waliokuwa katika ziara za
kimasomo.Adui huyu katili
amezikatisha ndoto za vijana wetu
hawa ambao miongoni mwao
tungewapata viongozi.Amekatisha
ndoto walizokuwa nazo wabunge
wetu za kuwatumikia wananchi
wao.Machozi gani tutalia kwa ukatili
huu mkubwa tuliofanyiwa?
Watu wote walikuwa kimya
wakimsikiliza rais.Hotuba hii
ilirushwa katika vituo vyote vya
runinga nchini ,ilitangazwa pia na
redio mbalimbali.Rais akaendelea.
Adui aliyetushambulia
amejitokeza hadharani na kutamba
kwamba ataendelea kumwaga damu
ya watanzania hadi pale serikali yetu
itakapoondoa vikosi vyetu vilivyoko
nchini Somalia vinavyosaidia
kuliojenga upya jeshi la Somalia.Adui
huyu ni mwoga, mpinga amani na sisi
kama nchi hatutaweza kumvumilia
aendeleze unyama wake katika ardhi
ya Tanzania.Hakuna damu ya
mtanzania mwingine itakayomwagwa
tena na Alshabaab .
Nimetoa maelekezo kwa vikosi
vyetu kuanza mara moja kumchakaza
adui huyu na tayari amekwisha anza
kufunzwa adabu. Alfajiri ya leo vikosi
vyetu vimeshambulia kambi mbili za
Alshabaab na kuziharibu vibaya
.Tutaendelea na mashambulio hadi
tuhakikishe tumemchakaza vibaya
adui huyu kama si kummaliza
kabisa.Huu ni ujumbe tunatuma kwa
wale wengine wote wenye kutaka
kuichezea nchi yetu kwamba sisi tuko
imara na tutapambana na adui yeyote
yule awe mkubwa au mdogo na
tutamchakaza vibaya.Tuko tayari
hata kwa vita na mtu,kikundi au taifa
lolote lile lenye kutishia amani na
ustawi wetu.Ujumbe huu ufike kwa
mitandao,vikundi au mataifa yote
yenye kutaka kuingilia uhuru wa nchi
yetu kwa kisingizo cha misaada na
kuharibu tamaduni zetu.Hatutaruhusu
nchi yetu kuwa kichaka au jalala la
tamaduni ovu.Tamaduni kama za
mapenzi ya jinsi moja,utoaji mimba
nk.hazina nafasi katika nchi yetu na
hatutazikubali.Tutazifungia asasi zote
zinazoshabikia tamaduni hizo za
kijinga zisithubutu kufanya kazi
katika ardhi yetu.
Ndugu watanzania nchi yetu
inapita katika kipindi
kigumu.Nawaomba shambulio hili
lililofanywa na adui mwoga lisitugawe
kwa misingi ya rangi wala dini
zetu.Tuungane pamoja kupambana na
adui huyu.Siku zote watanzania ni
wamoja hata pale linapotokea jambo
baya kama hili.Tukatae utumwa
mambo leo,tuzikatae tamaduni za
kigeni tukumbatie tamaduni
tulizorithi toka kwa wazee wetu kwa
manufaa ya nchi yetu na vizazi vyetu.
Ndugu zangu sina maneno mengi
ya kusema siku hii ya majonzi
makubwa kwa nchi
yetu.Mtatangaziwa siku na tarehe ya
kuaga miili ya wapendwa wetu na siku
ya mazishi ya kitaifa.Natangaza siku
saba za maombolezo ya kitaifa na siku
hizo zote bendera yetu itapepea nusu
mlingoti.Nawasihi tuwe watulivu na
tuendelee na shughuli zetu kama
kawaida.Licha ya kushambuliwa
lakini nchi yetu bado ni
salama.Tushirikiane na vyombo vya
dola kufichua njama zote ovu kwa
taifa letu
Narudia tena kuwapa pole na
kuwaomba tuendelee kuiombea nchi
yetu amani.
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Rais wa jamhuri ya muugano
wa Tanzania Ernest Mkasa
akamaliza hotuba yake fupi kisha
akaenda kuketi mahala
pake.Nyimbo za dini zikaimbwa
toka katika kwaya mbali mbali
zilizokuwepo halafu rais na
viongozi wengine wakaelekea
ikulu kwa ajili ya kikao na uongozi
wa mkoa.Wakati rais akiwa katika
kikao na uongozi wa mkoa
wakijadili mambo mbalimbali
kuhusiana na shughuli za kuwaaga
wabunge waliopoteza maisha
,simu yake ikatetema.Toka
amefika Dodoma hakukumbuka
kabisa simu yake.Mpigaji alikuwa
David Zumo.Akatoka nje ya kile
chumba cha mikutano akaipokea.
“Hallow mheshimiwa rais”
akasema Ernest
“Mheshimiwa rais pole sana
kwa matukio makubwa
yaliyotokea nchini kwako
jana.Nchi yangu iko nawe bega kwa
bega na endapo kuna chochote
tunachoweza kusaidia tuko
tayari.Tanzania ni ndugu zetu wa
damu.Tumeguswa sana tukio hili
baya kutokea katika ukanda huu
wetu” akasema David Zumo
“ Ahsante sana mheshimiwa
rais” akasema David Zumo
“Mheshmiwa rais,pamoja na
salamu nyingi za pole kwa
watanzania nina ombi moja
kwako.Nimefiwa na mke wangu
Pauline Zumo”
“ Pauline amefariki?!! Ernest
akashangaa
“ Ndiyo amefariki.Mazishi
yake ni kesho kwa hiyo kuna watu
wangu wa karibu toka Tanzania
ambao watafika kuhudhuria
mazishi.Nitatuma ndege yangu
binafsi kuja kuwachukua watu hao
kwa hiyo ninaomba kibali cha
ndege yangu kutua katika uwanja
wa ndege wa Julius Nyerere leo saa
kumi kuwachukua wageni wangu”
“Hakuna tatizo katika hilo
suala nitatoa maelekezo kwa
maafisa wangu ambao
watawasiliana na maafisa wako ili
kufahamu ni akina nani
wanaotakiwa kuondoka ili kusiwe
na mkwamo wowote kwani kama
unavyojua kwa sasa kiwanja cha
ndege kimefungwa na hakuna
ndege inayoruhusiwa kuingia wala
kutoka ”
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais.Ndege inakuja kuichukua
familia ya Benedict
mwamsole.Nina hakika
unamfahamu mzee huyu ambaye
ni mmoja wa wafanya biashara
wakubwa hapo Tanzania.Yeye na
familia yake ndio wanakuja
kuungana nasi katika mazishi ya
Pauline” Akasema David Zumo
akaagana na rais akakata simu
“David amenichafua sana
.Hana taarifa kama mimi ndiye
baba yake na Monica.Ninaapa
kwamba hatafanikiwa mpango
wake wa kumuoa Monica.Siko
tayari Monica akaolewa na
David.Ngoja nimalize kwanza
mambo haya ya hapa nchini kisha
nitalishughulikia suala la David”
Akawaza rais halafu akamuita
jenerali Lameck
“Lameck muda mfupi
uliuopita nimezungumza na rais
David Zumo wa Congo.Amepatwa
na msiba ,mke wake amefariki
dunia na mazishi ni kesho kwa
hiyo kuna watu ambao ni rafiki wa
familia wanakwenda Congo
kuhudhuria mazishi .Atatuma
ndege yake binafsi kuja
kuwachukua watu hao na
kuwapeleka Kinshasa hivyo
alikuwa anaomba kibali cha ndege
yake kutua na nimemkubalia
.Utawasiliana na vikosi vilivyoko
uwanja wa ndege ili kusiwe na
tatizo lolote na watu hao
wanaokwenda Congo wapite bila
matatizo yoyote.Hili ni agizo la
rais” akasema rais Ernest
“ Nimekuelewa mheshimiwa
rais.Nitafanya hivyo.Tayari
amekueleza ni akina nani ambao
wanatakiwa kwenda huko Congo?
Akauliza Lameck
“ Ni Monica na familia yake”
“ Monica?!! Lameck
akashangaa
“ Ndiyo.Monica na familia yake
ni watu wa karibu na David
Zumo.Kuna tatizo lolote? Akauliza
rais
“ Hakuna tatizo mheshimiwa
rais” akajibu Lameck
“ Kuna maendeleo yoyote hadi
hivi sasa kuhusiana na kuwapata
Austin naYasmin? Rais akauliza
“ Nimekuwa na mawasiliano
ya karibu na Silvanus lakini mpaka
sasa bado hakuna chochote
kilichopatikana ila juhudi
zinaendelea
kufanyika.Nakuhakikishia
mheshimiwa rais kwamba
tutampata Austin leo .Jua
halitazama kabla Austin na Yasmin
hawajapatikana” akasema Lameck
“ Sawa Lameck.Endelea
kufuatilia suala hili mimi naenda
kuendelea na kikao bado nina
ratiba ndefu” akasema rais na
kuingia ndani kuendelea na
kikao.Lameck akampigia simu
Silvanus Kiwembe
“Kiwembe kuna taarifa zozote
nzuri hadi sasa? Kuna muelekeo
wowote wa kumpata Austin?
Akauliza Lameck
“ Mpaka sasa hakuna taarifa
zozote nzuri.Vijana wangu wako
kazini na tumeelekeza nguvu
kubwa kumtafuta Austin lakini
mpaka sasa hakuna mwelekeo
wowote.This man knows how to
hide.Ni mtu anayeifahamu vyema
kazi yake.”
“Kiwembe Austin si mtu wa
mchezo mchezo.Ninamfahamu
vyema ni mtu mwenye akili nyingi
na anaifanya vyema kazi yake kwa
hiyo vijana wako wanatakiwa
kutumia akili ya ziada
kumtafuta.Nina uhakika bado yuko
hapa hapa Dar es salaam.Vipi
kuhusu Monica mnapata
ushirikiano wowote toka kwake
kama alivyomuahidi rais?
“ Monica alitupa ushirikiano
asubuhi alimpigia simu Austin
lakini simu yake haikuwa
ikipatikana na baada ya hapo
aliomba tumuache kwani
anashghuli nyingi leo.Mpaka sasa
hatujapata simu yoyote toka
kwake.Tumekuwa tukimfuatilia
kwa ukaribu sana kuanzia
nyumbani kwake,na hadi
mawasiliano yake ya simu na
mpaka sasa hatujasikia
akiwasiliana na Austin.Ila
tunaendelea kumfuatilia kwa
karibu na tunaamini ndiye njia kuu
ya kutufikisha mahala alipo
Austin.ifahamu kuhusu Austin japo
hatakikuweka wazi”akasema Silva
“Kazi nzuri Silva endeleeni
kumfuatilia.Chochote
mtakachokipata nitaarifu mara
moja.Tukiachana na hayo kuna
maelekezo nimepewa na rais
.Alasiri ya leo Monica na familia
yake wataondoka kuelekea
Kinshasa kuhudhuria mazishi ya
mke wa rais wa Congo hapo
kesho.Rais David Zumo tayari
amemuomba kibali rais Ernest cha
ndege yake binafsi kutua Dar es
salaam kuwachukua akina Monica
na familia yake.Nataka ufuatilie
suala hili kwa ukaribu sana
japokuwa rais amesema kwamba
tuhakikishe hawapati kikwazo
chochote lakini kitu alichokifanya
yeye na wenzake jana kinanifanya
nisiwe na imani sana na huyu
Monica.Akina Austin wanaweza
wakamtumia kama
walivyomtumia jana kwa kuwa
wanafahamu ukaribu wake na
rais.Nataka wafuatiliwe na
wachunguzwe ili katika safari hiyo
wasiwepo na watu wengine
wasiotakiwa kuwepo.Endapo
utahisi kuna jambo lolote lisilo la
kawaida nijulishe tafadhali.”
“ Sawa Jeneral lameck
.Nitakujulisha kila kitu”akasema
Silvanus Kiwembe .Lameck
akazungumza na makamanda
wake wa vikosi sehemu mbali
mbali nchini kujua hali ya usalama
halafu akarejea katika chumba cha
mikutano.