QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEASON 7: SEHEMU YA 9
Imetimu saa nne za asubuhi
na harakati za kujitafutia mkate
wa kila siku zilikuwa zinaendelea
kama kawaida katika jiji la Dar es
salaam.Ulinzi ulikuwa mkali katika
kila kona ya jiji.Magari ya jeshi na
polisi yaliranda randa mitaani
kuhakikisha usalama
unaimarishwa.Katika nyumba
moja eneo la mikokoni msichana
mmoja mrembo alikuwa amejilaza
kitandani.Nywele zake zilikuwa
zimevurugika na alionekana kuwa
na mawazo mengi sana.Akiwa
bado amejilaza kitandani,mlango
wa chumba chake ukafunguliwa
akaingia mama yake
“Irene.Una tatizo gani
leo,unaumwa? Akauliza
“Hapana mama siumwi ila
sijisikii kwenda kazini leo” akajibu
Irene
“Unaogopa yale mashambulio
ya jana? Akauliza mama yake
“Mama sina hamu kabisa ya
kwenda kazini siku ya leo.Nataka
nikae hapa hapa ndani.Vipi baba
anaendeleaje?” Akauliza Irene
“ Baba yako anaendelea
vyema.Amepata matumaini mapya
baada ya kibali cha kwenda nje ya
nchi kwa matibabu
kupatikana.Mipango yote ya safari
inakwenda vyema na kilichobaki
ni kupata kiasi cha fedha
kinachotakiwa .Tukifanikisha hilo
basi baba yako atasafiri haraka
sana kwenda ulaya kwa matibabu”
Akasema mama yake Irene na
Irene aliyekuwa amejilaza
kitandani akainuka na kukaa
akaweka mikono kichwani .
“Irene !! mama yake
akaita.Irene akainua kichwa
akamtazama mama yake
“Kuna jambo nataka
kukufahamisha.Nimepigiwa simu
na mjomba wako ambaye
tulitegemea atuazime shilingi
milioni saba ili tuongezee na kile
kiasi tulichonacho kwa ajili ya
kufikia kiasi kinachohitajika kwa
matibabua ya baba yako, amesema
kwamba mahala alikotegemea
kupata kiasi alichoahidi kutuazima
amekosa.Nimempigia simu mama
yako mdogo ili naye atusaidie
katika suala hili na ninasubiri jibu
lake ila sina uhakika kama
tutafanikiwa” akasema mama
yake Irene
“Mama tafadhali usiendelee
kuumiza kichwa kuhusu suala la
fedha.Nitafanya mpango na
nitapata hizo fedha
zilizobaki.Lazima baba aende
kutibiwa” akasema Monica na
kumtaka mama yake amuache
aendelee kupumzika.
“ Sitaki wazazi wafahamu
nilichokifanya ili kufanikisha
kibali cha matibabu ya
baba.Wakigundua jambo la hatari
nililolifanya wataumia
sana.Kichwa changu nahisi
kinataka kupasuka kwa mawazo
.Lakini yote haya yamesababishwa
na Mukasha.” Akawaza na kuanza
kukumbuka mambo aliyoyafanya
MASAA MAWILI KABLA YA
SHAMBULIO LA KIGAIDI JIJINI DAR
ES SALAAM
Irene maboko akiwa ametulia
katika meza yake akiendelEa na
kazi zake za kawaida simyake
ikaita.Zilikuwa namba
ngeni,akaipokea
“halow” akaita
“hallow Irene ni mimi
Mukasha ninaongea.Tafadhali
usilitamke jina langu na kama uko
karibu na watu toka uende mahala
kusikokuwa na watu kuna jambo
nataka kuzungumza nawe”
akasema Mukasha na Irene
akatoka akaelekea katika sehemu
kusikokuwa na mtu
“Hallo” akasema
“ Irene naomba
unisikilize.Nahitaji tena msaada
wako.Kabla sijakwambia chochote
vipi ulifanikiwa kupata kile kibali
cha kumpeleka mzee wako kwa
matibabu nje ya nchi?
“Ndiyo nilifanikiwa”Irene
akajibu
“Mzee wako tayari
amekwenda kutibiwa?
“Hapana bado tunakusanya
fedha zinazohitajika.Sisi tulidhani
kwa kupata kibali kile
hatutagharamia kitu chochote
kumbe tunatakiwa kuchangia
gharama hizo.Tumetakiwa kutoa
kiasi cha shilingi milioni kumi na
moja.Hivi sasa tunaendelea
kukusanya kwa ndugu na watu
mbali mbali” akasema Irene
“ Pole sana Irene lakini
usiwaze sana hilo ni suala dogo
pesa hiyo utaipata.Nitakusaidia
kiasi cha shilingi milioni ishirini
ambazo zitasaidia kwa matibabu
ya baba yako na zitakazobaki
zitakusaidia katika mambo
mengine”
“Ahsante sana Mukasha.Sijui
nitakushuruje kama ukinisaidia
kupata kiasi hicho .Nini unahitaji
nikusaidie mzee? Akauliza Irene
“Irene unakumbuka
ulinisaidia kudukua simu ya
rais.Nataka ufanye tena
hivyo.Tumia uwezo wako wote
uweze kuidukua tena simu ya
rais.Nahitaji kujua kwa siku nzima
ya leo amewasiliana na akina nani?
Nataka unitumie mazungumzo yao
katika barua pepe yangu” akasema
Mukasha halafu kukawa kimya.
“Irene” akaita Mukasha
“Mzee umenipa mtihani
mgumu sana.Nilidhani kwamba
hatutarudia tena lile jambo
tulolifanya,ni kosa kubwa na
tukigundulika adhabu yake ni
kubwa.Nasikitika mzee sintaweza
kukusaidia safari hii” akasema
Irene
“Irene tafadhali naomba
unisaidie.Nilikusaidia na bado
ninaendelea kukusaidia ili uokoe
uhai wa baba yako.Endapo
hautakuwa tayari kunisaidia basi
kibali kile kitafutwa na baba yako
atapoteza uhai.Utajisikiaje baba
yako akifariki wakati uwezo wa
kumsaidia unao? Tafadhali Irene
nisaidie nami nikusidie.”
Irene akawa kimya
akitafakari halafu akasema
“Mzee naomba unipe muda
kidogo nione namna
nitakavyoweza kufanya kwani
kompyuta yangu iko katika
matumizi mengine ya kiofisi na
siwezi kufanya zoezi lile bila kuwa
na kompyuta yangu ile. Nipe muda
halafu nitakupigia” akasema Irene
“ Nitakupigia baada ya saa
moja.Naomba ndani ya muda huo
uwe umefanikisha suala hilo.”
Akasema Mukasha na kukata
simu.Irene akahisi
kuchanganyikiwa.Jambo
aliloombwa alifanye na Mukasha ni
jambo la hatari kubwa
“ What am I going to do?
Akajiuliza akiwa ameziba uso kwa
mikono yake.Akarejea ofisini
akatafakari kwa muda hali ya baba
yake ilivyo
“Ngoja nifanye
atakavyo.Litakalotokea na litokee
tu” akawaza halafu akafanya kitu
Fulani katika kompyuta yake na
ujumbe ukasambaa katika
kompyuta zote pale ikulu halafu
akatoka mle ofisini kwake
harakaharaka kuelekea katika
ofisi ya rais.Hakuna aliyemzuia
kuingia katika ofisi hii kwani
anafahamika kama ndiye
mtaalamu mkuu wa ulinzi wa
mfumo wote wa kompyuta katika
ofisi ya rais kwa hiyo alikuwa na
uwezo wa kuingia ofisi yoyote
muda wowote.
“ Irene” akasema rais baada ya
Irene kuingia mle ofisini kwake.
“ Shikamoo mzee” akasema
Irene
“ Marahaba.Sijakuona ofisini
kwangu kwa siku kadhaa”
“Nipo mzee.Ni kazi zimekuwa
nyingi” akasema Irene na
kumuomba rais ampe dakika tano
katika kompyuta yake kuna kitu
anataka kukifanya
“ Kuna tatizo lolote Irene?
Nimeona umetuma ujumbe kwa
watu wote kwamba kuna tatizo la
kiufundi”
“ Kuna tatizo dogo
mzee.Baada ya dakika tano kila
kitu kitakuwa tayari” akasema
Irene na kuichukua ile kompyuta
ya rais
“Mzee kwa nini usinyooshe
miguu na unipe dakika tano nikae
katika hicho kiti chako nimalize
tatizo katika kompyuta yako?
Umekuwa ofisini toka
asubuhi.Zunguka uwasalimie
wafanyakazi wako wakati
ninarekebisha mambo” akasema
Irene huku akicheka.Amezoea
sana kutaniana na rais
“ Unataka kuweka nini katika
kiti changu? Akauliza rais huku
naye akicheka
“Nitakuwekea nini wewe mzee
uliyechoka na nguvu huna tena?
Subiri muda wako ufike uende
zako ukapumzike na mkeo”
akasema Irene
“Una hakika kwamba sina
nguvu? Jaribu kunipa siku moja
uone kama hukuzungumza kireno”
Akasema rais na wote wakacheka.
“Nenda zako mzee usije
ukanifia kifuani.” Akasema Irene
na rais akainuka akatoka mle
ofisini kwake akaingia katika ofisi
nyingine.Juu mezani rais aliiacha
simu yake.Haraka haraka Irene
akaichukua akaifungua akatoa
kadiya kuhifadhia kumbu
kumbuya rais akweka kadi nyingie
ndogo halafu akaiwasha
akabonyeza bonyeza namba
kadhaa kwa muda halafu akaitoa
ile kadi yake akairudisha simu ya
rais kama ilivyokuwa .Akabonyeza
bonyeza kompyuta ya rais na
kuirejesha katika hali yake kisha
akatoka na kumfuata rais katika
ofisi aliyokuwa ameingia
akamtaarifu kwamba kompyuta
iko tayari kisha akatembea
kuelekea ofisini kwake.Miguu
ilikuwa inajigonga kwa woga
aliokuwa nao.Alichukua mkoba
wake akaelekea bafu la wanawake
akajitazama katika kioo.Alikuwa
na jasho usoni.Akanawa uso na
kurekebisha poda usoni halafu
akarejea ofisini kwake.Mapigo ya
moyo yalikuwa yanamwenda mbio
“Naomba Mungu anisaidie rais
asigundue chochote kuhusu hiki
nilichokifanya.Hii ni kesi kubwa
sana .Kudukua simu ya rais si kesi
ndogo.Mukasha anataka kuniweka
katika matatizo makubwa.Endapo
nitakamatwa basi baba yangu ndio
utakuwa umefika mwisho wake
kwani hatapata msaada
wowote.Mtoto pekee
anayenitegemea ni mimi.Natakiwa
kuwa makini sana na haya mambo
ninayoyafanya”akawaza
Dakika arobaini baadae simu
yake ikalia lakini kwa mlio tofautio
na ule aliouzoea akatoka mle
ofisini na kusikiliza maongezi kati
ya rais na mtu mwingine.Irene
aliiunganisha simu ya rais na simu
yake na hii ilimuwezesha kusikia
simu zote ambazo rais atakuwa
anapiga au kupigiwa.Hii ni
teknolojia mpya ambayo
hutumiwa sana na majasusi
kudukua simu za viongozi au watu
wanaotaka kupata taarifa zao.
“Mheshimiwa rais” ikasema
sauti ya upande wa pili
“ Jeneral Lameck muda
unasogea sana .Vipi maendeleo?
Mambo yanakwenda vizuri?
“ Mambo yanakwenda vizuri
mzee na kila kitu tayari
kimeandaliwa.Ndege ziko angani
hivi sasa vijana wanasubiri muda
ufike wafanye kazi yao.Kilichobaki
ni upande wako kuhakikisha kuwa
muda huo ukifika Alberto’s wote
wanakuwa ndani ya ukumbi na
ninakuhakikishia mzee mabomu
tutakayotumia ni mazito
yaliyotengenezwa kisasa kwa ajili
ya kumchakaza adui aliyejificha
katika majengo makubwa kama
maghorofa kwa hiyo hakuna
atakayekuwemo ndani ya ukumbi
huo atatoka hai” akasema Lameck
“ Kwa upande wangu mambo
yanakwenda sawa.Nimepokea
simu muda si mrefu kutoka kwa
Agatha akinitaarifu kwamba tayari
wajumbe wameanza kuingia ndani
ya ukumbi na akanisisitiza
nisikose .I think that was her last
call to me.Lameck I hate that
woman.Ni yeye ndiye aliyeniingiza
katika matatizo haya.Bila yeye
nisingefanya haya ninayofanya
kwa hiyo hakuna msamaha lazima
na yeye aondoke leo” Akasema rais
“ Vipi kuhusu
Habib.Mmewasiliana?
“Habib tayari tumemalizana
na kila alichokitaka
amekipata.Hivi tuongeavyo watu
wake wako angani wakielekea
Mogadishu.Hakuna tatzo lolote na
yeye” akasema rais
“ Good.Nitafika hapo saa kumi
na moja za jioni ili tuelekee
hotelini kwani shambulio
linatakiwa lifanyike wakati
msafara wako umekaribia kufika
hotelini hapo.Lazima watu
wafahamu kwamba shambulio hilo
lilikulenga wewe.Usihofu mzee
hautadhurika japo utapata mstuko
kidogo kutokana na kishindo cha
bomu ila utakuwa salama”
“ That’s a good plan
Lameck.Endelea na maandalizi
tutaonana baadae” akasema rais
na kukata simu
Irene alibaki ameishikilia
simu yake asiamini kile
alichokisikia.
“Hii si ndoto.Hiki ni kitu cha
kweli kabisa.Nimesikia kwa
masiko yangu rais na jenerali
Lameck kuna jambo baya
wanalipanga.” Akawaza Irene na
kuchomeka spika za masikioni
akayasikiliza tena maongezi yale
kati ya rais na lameck
ambayotayari yalirekodiwa katika
ile kadi ya simu
“Something bad is going to
happen.Kuna shambulio
linakwena kufanyika leo ambalo
linapangwa na rais na
lameck.Halafu kilichonistua zaidi
mke wa rais naye ni mlengwa
katika shambulio hilo.”akawaza
Irene na kuhisi mwili wote
ukimtetemeka
“Mwili wote unanitememeka
kwa woga.Masikio yangu
hayakuwahi hata mara moja
kusikia jambo zito kama hili
nililosikia leo.”
Irene alishindwa kuendelea
na kazi ikamlazimu kutoka na
kwenda nje kupunga upepo.Alihisi
kama vile akili yake haikuwa
ikifanya kazi sawa sawa.Aliwaza
mambo mengi sana lakini
alishindwa kupata ufumbuzi
afanye nini.
“ Ee Mungu niangazie nini
nifanye baada ya kuyasikia mambo
haya mazito.watu wako wengi
wasio na hatia wanakwenda
kuangamia.” Akaomba kimya
kimya na kuendelea kutafakari
“Nimtaarifu Mukasha kuhusu
jambo hii? Lakini Yule ni mtu wa
karibu sana na rais na anaweza
akamueleza kuhusu suala hili na
ikafuatiliwa nikagundulika kuwa
ni mimi ndiye niliyedukua simu ya
rais na kufuatilia maongezi yake
na Lameck” Akashindwa kupata
jibu ikamlazimu kuondoka
kuelekea nyumbani akajifungia
chumbani kwake.Mukasha alipiga
simu zaidi ya mara nne lakini Irene
aliitazama bila kupokea.
Muda ulikwenda kwa kasi
hadi ilipofika saa kumi na moja na
nusu bado hakuwa amepata jibu
afanye nini.Mwishowe akaamua
afanye kitu kimoja.
“I must save the first
lady.She’s a good woman na hana
tatizo lolote.Hajawahi kunifanyia
jambo lolote baya na isitoshe
watumishi wote wa ofisi ya rais
anatupenda sana kama watoto
wake.Aliwahi kunizawadia mkufu
mzuri wa dhahabu
nilipomtengenezea kompyuta
yake.Kama kweli kuna shambulio
limepangwa kufanyika I must save
her.Litakalokuwa na liwe”
akachukua simu na kuzitafuta
namba za mke wa rais akampigia
Agatha akapokea simu
“ Irene my daughter .leo
umenikumbuka mama yako”
akasema Agatha
“ Madam first lady,samahani
kwa kukusumbua muda huu lakini
naomba kufahamu mahala uliko
hivi sasa” akasema Irene.Agatha
akasita kidogo halafu akasema
“ Kuna sehemu nimekuja
kujumuika na wenzangu nina
kikao.”
“ Ni hotelini? Akauliza
“ Ndiyo ni hotelini.Kwa nini
umeuliza Irene?
“ Madam naomba unisikilize
na ufanye
nitakavyokuelekeza.Naomba utoke
hapo katika hiyo hoteli sasa hivi
bila ya mtu yeyote kufahamu
unakwenda wapi.Kuna jambo baya
linakwenda kutokea hapo”
“ jambo gani Irene? Akauliza
Agatha
“ madam naomba unisikie na
uondoke hapo mara
moja.Something bad is going to
happen there.Believe me”
akasema Irene
“Irene unanichanganya
nashindwa kukuelewa.Kitu gani
kinakwenda kutokea hapa?
“ Hoteli hiyo inakwenda
kulipuliwa muda si mrefu.tafadhali
ondoka hapo mara moja” akasema
Irene.Agatha akahisi
kuchanganyikiwa
“ Irene una uhakika na hayo
unayoyasema? Akauliza Agatha
“Nina uhakika madam .Ninao
ushahidi kwamba hoteli hiyo
inakwenda kulipuliwa.Tafadhali
ondoka hapo mara moja” akasema
Irene.Ulipita muda kidogo Agatha
akasema
“ Irene thank you so
much.Nitakupigia baadae kidogo”
akasema Agatha na kukata simu.
Kumbu kumbu ile ya namna
mambo yalivyokuwa ikamfanya
Irene atoe machozi
“kwa nini rais ameua watu
wote wale?Wamemkosea nini?
Akajiuliza
“Nilifanikiwa kumuokoa
madam Agatha peke yake ,kwa nini
sikuokoa maisha ya watu wengine
? Nilifanya kosa kubwa kwani
nilikuwa na uwezo wa kuwaokoa
pia watu wengine.Ningeweza kutoa
taarifa hii katika vyombo vya
usalama na wangeweza kuchukua
hatua mara moja.Kwa sasa
nimekwisha chelewa ,shambulio
limefanyika na watu
wamekufa.Taarifa yangu haina
maana tena.” Akawaza
“ Nimemchukia sana rais na
sitaki kufanya kazi tena
ikulu.Siwezi kuvumilia nikiiona
sura yake shetani mkubwa
Yule.Laiti kama ningekuwa na
uwezo ningemfikisha mbele ya
sheria lakini uwezo sina.Hata
kama nikisema nikashitaki mahala
kwa kutumia ushahidi huu
nilionao nitajiweka matatizoni
mimi mwenyewe na kuiacha
familia yangu inateseka.Nitafanya
nini basi? Nikae kimya? Akajiuliza
“Madam Agatha alinipigia
simu jana usiku akanishukuru
kwa kumuokoa .Alitaka nimueleze
nimefahamuje taarifa ya
shambulio lile lakini nilimuomba
anisubiri hadi hapo nitakapokuwa
nimetulia ndipo nimueleze kila
kitu.Je nikimueleza kwamba ni
mume wake ndiye aliyepanga
shambulio lile nini
kitatokea?Ataniamini? Sina hakika
kama ataniamini.Kitu cha msingi
ni kuendelea kumkwepa nisionane
naye tena.Sitaki kurejea tena ikulu
.Sitaki kuendelea kufanya kazi na
watu ambao mikono yao imeloa
damu.Lakini nikiacha ghafla tu bila
taarifa zozote ninaweza kuzua
maswali na wakanifuatilia
wakanigundua.Halafu nikiacha
kazi ghafla nitamuhudumiaje baba
yangu ambaye anahtaji msaada
wangu? Mukasha aliahidi
kunisaidia pesa kwa ajili ya
kumpeleka baba ulaya lakini sitaki
kuwasiliana naye tena kwani
sikumpa majibu ya kazi
aliyonituma niifanye.Nikisema
nimuombe madam Agatha msaada
atataka nimueleze nilikopata
taarifa za shambulizi lile .What am
I going to do? Akajiuliza na kuzama
mawazoni
“ Ngoja nimpigie simu Daniel
nimuombe msaada.Japokuwa
tumeachana muda mrefu lakini
bado tunaendelea kuwasiliana
vizuri.Huyu nikimueleza tatizo
langu hatasita kunisaidia.Ana pesa
za kutosha tatizo lake ni mwingi
wa wanawake” akawaza Irene
akainuka kitandani akafungua
simu yake akatoa laini ya simu
ambayo ameiweka kama akiba
akaiweka katika simu nyingine
akazitafuta namba za Daniel
akampigia
“ Princess Irene” akasema kwa
furaha Daniel baada ya kupokea
simu
“ halo Daniel” akasema Irene
“ Irene ! You sound so cool
today.Are you ok? Akauliza Daniel
“ Daniel can we meet? I want
to talk to you.”Akasema Irene
“ Irene una tatizo
limekutokea? Akauliza Daniel
“ Daniel kweli nina tatizo
nahitaji kuzungumza nawe.Uko
ofisini kwako?
“ Hapana siko ofisini.Naomba
tukutane Tiger hotel” akasema
Daniel na kukata simu.Irene
akaenda kuoga haraka haraka na
kuaga wazazi wake akaingia katika
gari lake na kuondoka kuelekea
mahala alikopanga akutane na
Daniel Swai.Barabarani alikutana
na askari wengi wakizunguka
kulinda usalama akahisi kuumia
moyoni.
“Nilikuwa na uwezo wa kuzuia
shambulio lile na laiti kama
ningefanya kitu haya yasingetokea
jana kwani nilikuwa na taarifa
kuhusiana na shambulio lile na
nikafanikiwa kumuokoa mtu
mmoja pekee.jambo hili litaniuiza
moyo hadi siku naingia kaburini.”
Akawaza na kuigusa simu
aliyokuwa ameiweka mfukoni
“ Simu hii yenye ushahidi ule
wa maongezi ya rais na Lameck
nitatembea nayo kila mahala
nitakapokwenda kwani siku moja
ushahidi huu unaweza ukanisaidia
sana.Nilifanya kosa niliposeti
kunasa maongezi ya rais kwa msaa
mawili.Ningejua kama kuna
mambo kama haya yanaendelea
ningeseti hata ninase maongezi
yake kwa wiki nzima.Ningepata
mambo mengi sana anayoyafanya
rais.Kumbe hawa viongozi
wanaishi na siri nyingi
sana.Nilidhani viongozi wengi ni
wasafi lakini kwa haya yaliyotokea
imenilazimu kuwatazama viongozi
hawa kwa jicho la tatu.” Akawaza
Irene
Aliwasili Tiger hotel
akamkuta tayari Daniel amefika
akimsubiri
“ Irene leo kulikoni
umejitanda namna hiyo kiasi ni
vigumu hata kutambulika?
Akauliza Daniel.Irene akavua
miwani mikubwa aliyokuwa
amevaa na kumstua Daniel
“ Irene una tatizo gani mbona
macho yako yamevimba” Daniel
akashangaa
“ Daniel kwanza kabla ya yote
vipi hali yako? Muda kidogo
umepita hatujawasiliana.”
“ Ninaendelea vizuri sana.Sijui
wewe.”
“ Hata mimi ninaendelea
vyema.Bado unafanya kazi ikulu?
Akauliza Daniel
“ Ndiyo bado niko ikulu.”
Akasema Irene.Muhudumu akafika
wakaagiza vinywaji
“ Niambie Irene una tatizo
gani? Daniel akauliza.
“ It’s my dady” akasema Irene
“ Ana tatizo gani mzee
maboko?
“ Anaumwa sana.Ana tatizo la
ini kwa hiyo anatakiwa apelekwe
nje ya nchi kwa matibabu.Kibali
tumepata lakini kunatakiwa pia
fedha za kufanikisha matibabu
hayo ambazo ni zaidi ya milioni
kumi.Tumehangaika sana mpaka
sasa tumepata kiasi kidogo cha
fedha na tumebakiza kama milioni
saba.Nimekuja kukuomba
unikopeshe kiasi hicho cha fedha
na mimi nitaendelea kukulipa
kidogo kidogo.Nimekwama kabisa
na wewe ndiye tegemeo langu la
mwisho.” Akasema Irene.Daniel
akamtazama Irene kwa muda
halafu akasema
“ Irene nitakusaidia kutatua
tatizo lako.Nitakupatia kiasi hicho
cha fedha unachokihitaji kwa ajili
ya matibabu ya mzee wako.Siwezi
kukukopesha fedha hizo kwani
baba yako ni sawa na baba
yangu.Ondoa shaka nitakusaid…”
Irene na Danie wakastuka baada
ya watu wawili waliovalia suti
nyeusi kusimama mbele ya meza
yao .
“ Irene maboko.Tunakuhitaji
tafadhali.” Akasema mmoja wa
wale jamaa.
“ Who are you people
!!..akauliza Daniel akionyesha
kukerwa na kitendo cha wale
jamaa kuwavamia na kumtaka
Irene
“Samahani kaka tunashida na
huyu mwenzako”
“ Mnashida gani naye? Halafu
ninyi ni akina nani ?Kwa nini
mnakuja kutuvamia bila
kujitambulisha? Akauliza Daniel
kwa ukali kidogo
“Ndugu samahani hatuna
muda wa kupoteza hapa.Irene
naomba uongozane nasi kwa hiari
yako tafadhali.” Akasema mmoja
wao.Irene alikuwa anatetemeka
mwili alishindwa afanye
nini.Akamtazama Daniel
“ Irene nadhani umetusikia
.Usitake tutumie nguvu.Inuka
tafadhali na uongozane nasi”
“ Irene don’t go!! akasema
Daniel na kusimama.Mmoja wa
wale jamaa akafunua koti lake na
kuishika bastora.Ghafla kukatokea
kitu ambacho hawakuwa
wamekitarajia.Daniel swai alishika
meza akaruka juu na kujitanua
msamba akawapiga mateke wale
jamaa wakaanguka chini.Jamaa
mmoja alipotua chini akaichomoa
bastora yake haraka na kumlenga
Daniel lakini tayari alikwisha
kiona kitendo kile akaruka kama
nyani na kumpiga teke mkono
uliokuwa umeshika bastora ile
ambayo ilianguka mita kadhaa
toka pale halafu akampiga teke
kali la mbavuni na kumfanya atoe
ukelele.Yule mwenzake alipoona
mambo yaliyotokea akainuka na
kutimua mbio.Tayari watu
walianza kujaa eneo lile
kushuhudia ule ugomvi.
“ Irene twende tuondoke
mahala hapa ,tayari watu
wameanza kujaa” akasema Daniel
na kumshika mkono Irene
wakaelekea katika gari la Daniel
na kuondoka kwa kasi wakiacha
umati wa watu ukimiminika eneo
lile kushuhudia ugomvi ule.Daniel
akamtazama Irene alikuwa
anatetemeka
“ Unajisikiaje Irene?
“ I don’t know.Sijielewi.Wale
ni akina nani? Akauliza
“ Sifahamu ni akina
nani.Sikupata nafasi ya
kuwachunguza kujua ni akina nani
lakini wanaonekana ni watu wenye
uzoefu katika mapambano.Kwa
nini walikufuata wewe? Akauliza
Daniel
“ Hata mimi sifahamu watu
wale wamenifahamuje.Au ni
mapolisi? Akauliza
“ Hata mimi nahisi hivyo
.Kama ni polisi wamekufahamu
vipi? Kuna tatizo limetokea kiasi
cha kuwafanya polisi wakutafute ?
Please tell me” Akauliza Daniel
“ Daniel hapa nilipo
nimechanganyikiwa na sielewi
chochote.Watu wale siwafahamu
na sina tatizo lolote la kutafutwa
na polisi.Wewe mwenyewe
unanifahamu mimi nikitoka zangu
kazini ninarudi nyumbani na sina
ugomvi wowote na
mtu.Ninashangaa kwa watu wale
kunifuata moja kwa moja na
kutamka jina langu kana kwamba
ni watu wanaonifahamu.Daniel
what am I going to do? Akauliza
Irene
“ Relax Irene.Tutajua baadae
watu wale ni akina nani na nini
lengo lao”akasema Daniel na
kukawa kimya
“ Tayari nimeanza kuingia
katika matatizo.Watu wale
watakuwa wamtumwa aidha na
rais,mke wake madam Agatha au
Mukasha.lakini nahisi hawa watu
wawili rais au mke wake.Hapa
ninatafutiwa kuhusiana na
kufahamu kuhusu mlipuko
ule.Ninashawishika kuamini
kwamba watu wale wanaweza
kuwa wametumwa na
Agatha.Nadhani lengo lake ni
kutaka kufahamu nilifahamu vipi
kuhusu mlipuko ule.Natakiwa
kuificha sana hii simu yenye
ushahidi.Itanisaidia katika wakati
huu ambao naona ninaanza
kuingia katika hatari
kubwa.Mukasha ndiye
aliyesababisha maisha yangu
yakaingia mashakani namna hii
aliponishawishi nikubali kuidukua
simu ya rais na kufahamu mambo
haya makubwa”
“Irene !! akaita Daniel. Na
Irene akageuka
“Unawaza nini?
“I don’t know what I’m
thinking.Nimechanganyikiwa na
sijielewi.Watu wale
wamenichanganya mno” akajibu
Irene
“ Daniel umejifunza wapi
kupigana? Sikutegemea kama
ungeweza kupigana namna
ile.Umenishangaza mno.Niliogopa
sana Yule jamaa alipokuelekezea
silaha lakini hukuogopa
ukamuwahi na kuipiga silaha yake
kwa namna ya ajabu kisha
ukamuadhibu kwa teke kali.”
akasema Irene na Daniel akatoa
kicheko
“ Nina rafiki yangu anatoka
China ndiye amekuwa
ananifundisha mbinu mbali mbali
za kupigana.Itakulazimu kuanza
kuhudhuria mafunzo kwa ajili ya
kujihami pindi ukutanapo na watu
kama hawa waliokufuata leo.”
Akasema Daniel na wote
wakacheka
“Watu wale nimewatazama
vizuri wanatoka idara ya usalama
wa taifa.Sitaki kumwambia Irene
asije akaanza kuogopa.Irene ana
tatzo gani na hawa jamaa? Kuna
jambo amelifanya hadi afuatwe na
usalama wa taifa? Nahisi kuna kitu
anaogopa
kuniambia.Ninamfahamu Irene
vizuri ndiyo maana nilipomuona tu
nilijua ana tatizo.Itanibidi
nimdadisi taratibu sana ili anieleze
ana tatizo gani.Watu wale wa
usalama wa taifa hawawezi
wakakufuata hivi hivi lazima kuna
jambo” Akawaza Daniel
“Irene unaonaje tukipita
mahala tukapumzika tuendelee na
maongezi yetu? Akauliza Daniel
“ Daniel please take me
home.Sihitaji kwenda sehemu
yoyote kwa sasa.Kichwa changu
tayari kimevurugika” akasema
Irene
“Usihofu Irene hakuna tena
tatizo lolote.Usiwahofu wale jamaa
hawatarudi tena.”
“Daniel siku nyingine
tutaendelea na maongezi kwa sasa
naomba unirudishe nyumbani
nikapumzike.Kichwa changu
kimejaa mawazo mengi na mwili
wote unanitetemeka” akasema
Irene.
Walifika nyumbani kwa akina
Irene geti lilikuwa wazi
wakaingiza gari ndani.Sauti kubwa
ya muziki ilisikika toka
ndani.Akaingia sebuleni hakukuwa
na mtu yeyote .Sebule ilikuwa
imevurugwa sana.Irene
akashangazwa na hali ile
“ Flora !! akaita Irene kwa
sauti kubwa akimuita mfanyakazi
wa ndani.Akaita zaidi ya mara tatu
lakini Flora hakuitika.Akamuomba
Daniel amsubiri pale sebuleni
.Akagonga katika chumba cha
wazazi wake lakini
hakujibiwa.Akakinyonga kitasa
mlango ukafunguka akachungulia
ndani hakukuwa na mtu.
“wazee wamekwenda wapi?
Wamekwenda hospitali?
Akajiuliza.Akaenda chumbani
kwake na kukuta kila kitu
kimetupwa chini.Akaanza
kuogopa.Akaenda katika chumba
ambacho hulala mtumishi wa
ndani .Alipofika mlangoni
akastuka baada ya kuona matone
ya damu
Daniel akiwa sebuleni
akitazama baadhi ya picha
zilizokuwa zimetupwa chini ghafla
akawaona watu wawili
wakichomoza toka katika kichaka
cha maua.Walitembea kwa
kunyata na walipokaribia mlango
wa sebule kila mmoja akatoa
bastora.Taa nyekundu
ikamuwakia Daniel akanyata na
kujibanza pembeni ya mlango.
Watu wale wakapeana ishara na
mmoja wao akatangulia kuingia
ndani akiwa ameunyoosha mkono
wake uliokuwa na bastora.Ghafla
bila kutarajia Daniel akaruka na
kuupiga teke ule mkono uliokuwa
na bastora ikaanguka chini.Wakati
jamaa akijiuliza kilichotokea
akapigwa ngumi nzito
iliyompeleka chini .Daniel akarudi
nyuma ya mlango baada ya yule
jamaa mwingine aliyekuwa nje
kuanza kuvurumisha risasi.Mara
akasikia Irene akipiga
ukelele.Akawaacha wale jamaa
akatoka mbio kumfuata kule
chumbani.Mlango wa chumba cha
mtumishi wao wa ndani ulikuwa
wazi na alikuwa amelala katika
dimbwi la damu.Irene alikuwa
analia kwa sauti kubwa.Daniel
akamfuata akamuinua na kumziba
mdomo
“Shhhhh!!!..usipige kelele
kuna watu wako hapa wana silaha
” akasema Daniel na mara juu ya
meza ndogo pembeni na maiti ya
Flora kulikuwa na karatasi
imeandikwa ujumbe akaichukua
na kuiweka mfukoni
“ Irene listen to me..kuna
mlango wowote wa kutokea nje?
“ Ndiyo kuna mlango wa
jikoni” akasema Irene na kwa
tahadhari kubwa akamuongoza
Daniel wakatoka nje .Huku
wakikimbia kwa tahadhari Irene
akamuongoza Daniel hadi katika
mlango mdogo uliokuwa nyuma ya
nyumba wakatoka nje.
“Daniel I cant walk.Sina nguvu
za kutembea .Where are my
parents? I want to get back to find
my parents” akasema Irene
“Irene no ! the’ll kill you.These
people are dangerous” akasema
Daniel na kumshika mkono Irene
akamsaidia kutembea.
“Twende tuondoke eneo hili”
akasema Daniel .Bado Irene
aliendelea kumwaga
machozi.Walipanda bajaji
iliyowapeleka hadi Sameni Bar
wakachukua taksi kuelekea
nyumbani kwa Daniel.Wakiwa
garini Daniel akaufungua ule
ujumbe ulioandikwa kwa kalamu
nyekundu
“Tunao wazazi wako.Ili
kuwakomboa piga namba hizo za
simu chini.Ukipeleka taarifa hizi
polisi au ukimwambia mtu yeyote
utawapoteza wazazi wako wote”
Daniel akaukunja uso
hakutaka kumuonyesha Irene
ujumbe ule kwani alikuwa
ameinama akilia.
“What’s going on? Nani
kawachukua wazazi wa Irene? Kwa
kusudi gani? Wale jamaa pale
nyumbani kwa akina Irene mbona
wanafanana na wale usalama wa
taifa waliomfuata Irene kule Tiger
hotel? Hapa kuna jambo kubwa na
Irene anatakiwa anieleze ukweli
wote kabla mambo hayajawa
magumu.Kama nisingekuwepo
angekwisha chukuliwa na wale
jamaa.” Akawaza Daniel
 
SEASON 7: SEHEMU YA 10
Rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzani Ernest Mkasa aliwasili
mjini Dodoma.Akapokelewa na
viongozi wa mkoa wa Dodoma
kisha akaelekea katika ikulu ya
Dodoma akapata taarifa fupi toka
kwa uongozi wa mkoa kuhusiana
na hatua zilizochukuliwa na
usalama ulivyoimarishwa toka
lilipotokea shambulio katika
ukumbi wa bunge.Baada ya
kupokea taarifa fupi toka uongozi
wa mkoa rais na msafara wake
wakaelekea katika viwanja vya
bunge kwa ajili ya kuangalia
uharibifu uliofanywa na vile vile
kulihutubia taifa.Watu walikuwa
ni wengi sana katika viwanja vya
bunge na ulinzi ulikuwa
mkali.Ukiacha vikosi vya askari wa
miguu kulikuweo pia na askari wa
farasi,mbwa na angani kulikuwa
na helkopta za polisi zikipiga
doria.
Rais alifika katika viwanja vya
bunge akaongozwa na mkuu wa
mkoa .Kwa kawaida rais akifika
bungeni mwenyeji wake huwa ni
spika wa bunge lakini siku hii
mwenyeji wake alikuwa ni mkuu
wa mkoa kwani spika wa bunge na
wasaidizi wake wote ni miongoni
mwa watu waliopoteza maisha
katika shambulio lile.Baada ya
kumaliza kukagua uharibifu
uliotokea rais akaelekea eneo
aliloandaliwa .Vongozi wa dini
toka madhehebu mbalimbali
wakatoa maombi na kisha
zikafuata salamu toka kwa watu na
makundi mbalimbali wakiwemo
baadhi ya mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao hapa
nchini ambao walitoa salamu za
pole kwa wananchi wa Tanzania
kwa niaba ya mataifa
wanayoyawakilisha.Zoezi la
salamu ilipomalizika rais wa
jamhuriya muungano wa Tanzania
akapewa nafasi ya kuhutubia taifa.
“ Vizazi na vizazi
vijavyo,vitaikumbuka tarehe ya jana
kama tarehe mbaya kabisa katika
historia ya nchi yetu baada ya ndugu
zetu,wapendwa wetu,baba,mama
kaka na dad zetu kuuawa kikatili
katika shambulio la kigaidi.”
Ndiyo alivyoanza hotuba yake.
“Ndugu zangu watanzania
,nimesimama hapa na sijui
nizungumze kitu gani kwa tukio hili
ambalo itafaa likiitwa ni unyama
uliopitiliza.Sioni neno la kuzunguma
kuipa faraja mioyo yenu kwani kila
mmoja ameumizwa vibaya sana na
jambo hili.Itoshe kusema poleni sana
ndugu zangu watanzania.”
Jana majira ya saa kumi na mbili
za jioni wakati watanzania
wakiendelea na shughuli zao za kila
siku ghafla walistushwa na taarifa
mbaya baada ya kufanyika kwa
mashambulio makubwa mawili.Moja
ni katika hoteli jijini Dar es salaam na
lingine ni katika jengo la bunge hapa
Dodoma.Mashambulio yote haya
mawili yamefanywa na watu
wasiotutakia mema ,watu
wasiopendezwa na maendeleo na
ustawi wa nchi yetu,wasiopenda
amani iliyotamalaki katika kila pembe
ya nchi yetu.Ni tukio lililoushangaza
ulimwengu wote kwani Tanzania
inajulikana kwa amani na utulivu
wake na hatuna ugomvi na majirani
zetu.
Vikosi vya majeshi yetu
vimefanya kazi usiku kucha kufukua
maiti zilizokuwa katika vifusi na vile
vile kujaribu kutafuta kama kuna
majeruhi au manusura na leo asubuhi
nimekabidhiwa ripoti inayoonyesha
katika shambulio la Dar es salaam
watu wapatao mia tatu na ishirini na
saba wamepoteza maisha .Mjini
Dodoma waliopoteza maisha
walikuwa ni mia nne thelathini na tisa
na idadi kubwa ikiwa ni wabunge
wetu waliokuwa wakitekeleza
majukumu yao waliyotumwa na
wananchi wao.Vile vile ndani ya
ukumbi wa bunge kulikuwa na wageni
mbalimbali waliotembelea bunge na
wengi kati yao walikuwa wanafunzi
waliokuwa katika ziara za
kimasomo.Adui huyu katili
amezikatisha ndoto za vijana wetu
hawa ambao miongoni mwao
tungewapata viongozi.Amekatisha
ndoto walizokuwa nazo wabunge
wetu za kuwatumikia wananchi
wao.Machozi gani tutalia kwa ukatili
huu mkubwa tuliofanyiwa?
Watu wote walikuwa kimya
wakimsikiliza rais.Hotuba hii
ilirushwa katika vituo vyote vya
runinga nchini ,ilitangazwa pia na
redio mbalimbali.Rais akaendelea.
Adui aliyetushambulia
amejitokeza hadharani na kutamba
kwamba ataendelea kumwaga damu
ya watanzania hadi pale serikali yetu
itakapoondoa vikosi vyetu vilivyoko
nchini Somalia vinavyosaidia
kuliojenga upya jeshi la Somalia.Adui
huyu ni mwoga, mpinga amani na sisi
kama nchi hatutaweza kumvumilia
aendeleze unyama wake katika ardhi
ya Tanzania.Hakuna damu ya
mtanzania mwingine itakayomwagwa
tena na Alshabaab .
Nimetoa maelekezo kwa vikosi
vyetu kuanza mara moja kumchakaza
adui huyu na tayari amekwisha anza
kufunzwa adabu. Alfajiri ya leo vikosi
vyetu vimeshambulia kambi mbili za
Alshabaab na kuziharibu vibaya
.Tutaendelea na mashambulio hadi
tuhakikishe tumemchakaza vibaya
adui huyu kama si kummaliza
kabisa.Huu ni ujumbe tunatuma kwa
wale wengine wote wenye kutaka
kuichezea nchi yetu kwamba sisi tuko
imara na tutapambana na adui yeyote
yule awe mkubwa au mdogo na
tutamchakaza vibaya.Tuko tayari
hata kwa vita na mtu,kikundi au taifa
lolote lile lenye kutishia amani na
ustawi wetu.Ujumbe huu ufike kwa
mitandao,vikundi au mataifa yote
yenye kutaka kuingilia uhuru wa nchi
yetu kwa kisingizo cha misaada na
kuharibu tamaduni zetu.Hatutaruhusu
nchi yetu kuwa kichaka au jalala la
tamaduni ovu.Tamaduni kama za
mapenzi ya jinsi moja,utoaji mimba
nk.hazina nafasi katika nchi yetu na
hatutazikubali.Tutazifungia asasi zote
zinazoshabikia tamaduni hizo za
kijinga zisithubutu kufanya kazi
katika ardhi yetu.
Ndugu watanzania nchi yetu
inapita katika kipindi
kigumu.Nawaomba shambulio hili
lililofanywa na adui mwoga lisitugawe
kwa misingi ya rangi wala dini
zetu.Tuungane pamoja kupambana na
adui huyu.Siku zote watanzania ni
wamoja hata pale linapotokea jambo
baya kama hili.Tukatae utumwa
mambo leo,tuzikatae tamaduni za
kigeni tukumbatie tamaduni
tulizorithi toka kwa wazee wetu kwa
manufaa ya nchi yetu na vizazi vyetu.
Ndugu zangu sina maneno mengi
ya kusema siku hii ya majonzi
makubwa kwa nchi
yetu.Mtatangaziwa siku na tarehe ya
kuaga miili ya wapendwa wetu na siku
ya mazishi ya kitaifa.Natangaza siku
saba za maombolezo ya kitaifa na siku
hizo zote bendera yetu itapepea nusu
mlingoti.Nawasihi tuwe watulivu na
tuendelee na shughuli zetu kama
kawaida.Licha ya kushambuliwa
lakini nchi yetu bado ni
salama.Tushirikiane na vyombo vya
dola kufichua njama zote ovu kwa
taifa letu
Narudia tena kuwapa pole na
kuwaomba tuendelee kuiombea nchi
yetu amani.
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Rais wa jamhuri ya muugano
wa Tanzania Ernest Mkasa
akamaliza hotuba yake fupi kisha
akaenda kuketi mahala
pake.Nyimbo za dini zikaimbwa
toka katika kwaya mbali mbali
zilizokuwepo halafu rais na
viongozi wengine wakaelekea
ikulu kwa ajili ya kikao na uongozi
wa mkoa.Wakati rais akiwa katika
kikao na uongozi wa mkoa
wakijadili mambo mbalimbali
kuhusiana na shughuli za kuwaaga
wabunge waliopoteza maisha
,simu yake ikatetema.Toka
amefika Dodoma hakukumbuka
kabisa simu yake.Mpigaji alikuwa
David Zumo.Akatoka nje ya kile
chumba cha mikutano akaipokea.
“Hallow mheshimiwa rais”
akasema Ernest
“Mheshimiwa rais pole sana
kwa matukio makubwa
yaliyotokea nchini kwako
jana.Nchi yangu iko nawe bega kwa
bega na endapo kuna chochote
tunachoweza kusaidia tuko
tayari.Tanzania ni ndugu zetu wa
damu.Tumeguswa sana tukio hili
baya kutokea katika ukanda huu
wetu” akasema David Zumo
“ Ahsante sana mheshimiwa
rais” akasema David Zumo
“Mheshmiwa rais,pamoja na
salamu nyingi za pole kwa
watanzania nina ombi moja
kwako.Nimefiwa na mke wangu
Pauline Zumo”
“ Pauline amefariki?!! Ernest
akashangaa
“ Ndiyo amefariki.Mazishi
yake ni kesho kwa hiyo kuna watu
wangu wa karibu toka Tanzania
ambao watafika kuhudhuria
mazishi.Nitatuma ndege yangu
binafsi kuja kuwachukua watu hao
kwa hiyo ninaomba kibali cha
ndege yangu kutua katika uwanja
wa ndege wa Julius Nyerere leo saa
kumi kuwachukua wageni wangu”
“Hakuna tatizo katika hilo
suala nitatoa maelekezo kwa
maafisa wangu ambao
watawasiliana na maafisa wako ili
kufahamu ni akina nani
wanaotakiwa kuondoka ili kusiwe
na mkwamo wowote kwani kama
unavyojua kwa sasa kiwanja cha
ndege kimefungwa na hakuna
ndege inayoruhusiwa kuingia wala
kutoka ”
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais.Ndege inakuja kuichukua
familia ya Benedict
mwamsole.Nina hakika
unamfahamu mzee huyu ambaye
ni mmoja wa wafanya biashara
wakubwa hapo Tanzania.Yeye na
familia yake ndio wanakuja
kuungana nasi katika mazishi ya
Pauline” Akasema David Zumo
akaagana na rais akakata simu
“David amenichafua sana
.Hana taarifa kama mimi ndiye
baba yake na Monica.Ninaapa
kwamba hatafanikiwa mpango
wake wa kumuoa Monica.Siko
tayari Monica akaolewa na
David.Ngoja nimalize kwanza
mambo haya ya hapa nchini kisha
nitalishughulikia suala la David”
Akawaza rais halafu akamuita
jenerali Lameck
“Lameck muda mfupi
uliuopita nimezungumza na rais
David Zumo wa Congo.Amepatwa
na msiba ,mke wake amefariki
dunia na mazishi ni kesho kwa
hiyo kuna watu ambao ni rafiki wa
familia wanakwenda Congo
kuhudhuria mazishi .Atatuma
ndege yake binafsi kuja
kuwachukua watu hao na
kuwapeleka Kinshasa hivyo
alikuwa anaomba kibali cha ndege
yake kutua na nimemkubalia
.Utawasiliana na vikosi vilivyoko
uwanja wa ndege ili kusiwe na
tatizo lolote na watu hao
wanaokwenda Congo wapite bila
matatizo yoyote.Hili ni agizo la
rais” akasema rais Ernest
“ Nimekuelewa mheshimiwa
rais.Nitafanya hivyo.Tayari
amekueleza ni akina nani ambao
wanatakiwa kwenda huko Congo?
Akauliza Lameck
“ Ni Monica na familia yake”
“ Monica?!! Lameck
akashangaa
“ Ndiyo.Monica na familia yake
ni watu wa karibu na David
Zumo.Kuna tatizo lolote? Akauliza
rais
“ Hakuna tatizo mheshimiwa
rais” akajibu Lameck
“ Kuna maendeleo yoyote hadi
hivi sasa kuhusiana na kuwapata
Austin naYasmin? Rais akauliza
“ Nimekuwa na mawasiliano
ya karibu na Silvanus lakini mpaka
sasa bado hakuna chochote
kilichopatikana ila juhudi
zinaendelea
kufanyika.Nakuhakikishia
mheshimiwa rais kwamba
tutampata Austin leo .Jua
halitazama kabla Austin na Yasmin
hawajapatikana” akasema Lameck
“ Sawa Lameck.Endelea
kufuatilia suala hili mimi naenda
kuendelea na kikao bado nina
ratiba ndefu” akasema rais na
kuingia ndani kuendelea na
kikao.Lameck akampigia simu
Silvanus Kiwembe
“Kiwembe kuna taarifa zozote
nzuri hadi sasa? Kuna muelekeo
wowote wa kumpata Austin?
Akauliza Lameck
“ Mpaka sasa hakuna taarifa
zozote nzuri.Vijana wangu wako
kazini na tumeelekeza nguvu
kubwa kumtafuta Austin lakini
mpaka sasa hakuna mwelekeo
wowote.This man knows how to
hide.Ni mtu anayeifahamu vyema
kazi yake.”
“Kiwembe Austin si mtu wa
mchezo mchezo.Ninamfahamu
vyema ni mtu mwenye akili nyingi
na anaifanya vyema kazi yake kwa
hiyo vijana wako wanatakiwa
kutumia akili ya ziada
kumtafuta.Nina uhakika bado yuko
hapa hapa Dar es salaam.Vipi
kuhusu Monica mnapata
ushirikiano wowote toka kwake
kama alivyomuahidi rais?
“ Monica alitupa ushirikiano
asubuhi alimpigia simu Austin
lakini simu yake haikuwa
ikipatikana na baada ya hapo
aliomba tumuache kwani
anashghuli nyingi leo.Mpaka sasa
hatujapata simu yoyote toka
kwake.Tumekuwa tukimfuatilia
kwa ukaribu sana kuanzia
nyumbani kwake,na hadi
mawasiliano yake ya simu na
mpaka sasa hatujasikia
akiwasiliana na Austin.Ila
tunaendelea kumfuatilia kwa
karibu na tunaamini ndiye njia kuu
ya kutufikisha mahala alipo
Austin.ifahamu kuhusu Austin japo
hatakikuweka wazi”akasema Silva
“Kazi nzuri Silva endeleeni
kumfuatilia.Chochote
mtakachokipata nitaarifu mara
moja.Tukiachana na hayo kuna
maelekezo nimepewa na rais
.Alasiri ya leo Monica na familia
yake wataondoka kuelekea
Kinshasa kuhudhuria mazishi ya
mke wa rais wa Congo hapo
kesho.Rais David Zumo tayari
amemuomba kibali rais Ernest cha
ndege yake binafsi kutua Dar es
salaam kuwachukua akina Monica
na familia yake.Nataka ufuatilie
suala hili kwa ukaribu sana
japokuwa rais amesema kwamba
tuhakikishe hawapati kikwazo
chochote lakini kitu alichokifanya
yeye na wenzake jana kinanifanya
nisiwe na imani sana na huyu
Monica.Akina Austin wanaweza
wakamtumia kama
walivyomtumia jana kwa kuwa
wanafahamu ukaribu wake na
rais.Nataka wafuatiliwe na
wachunguzwe ili katika safari hiyo
wasiwepo na watu wengine
wasiotakiwa kuwepo.Endapo
utahisi kuna jambo lolote lisilo la
kawaida nijulishe tafadhali.”
“ Sawa Jeneral lameck
.Nitakujulisha kila kitu”akasema
Silvanus Kiwembe .Lameck
akazungumza na makamanda
wake wa vikosi sehemu mbali
mbali nchini kujua hali ya usalama
halafu akarejea katika chumba cha
mikutano.
 
SEASON 7: SEHEMU YA 11
Taksi waliyokodi akina Daniel
iliwafikisha nyumbani kwa Daniel
wakaingia ndani.Kibarazani
alikuwepo mwanamke mmoja
aliyekuwa akitengeneza kucha
zake.
“Baby mbona umerudi
mapema leo?akauliza mwanamke
Yule lakini Daniel hakumjali
akamkaribisha ndani Irene
ambaye bado alikuwa
analia.Kitendo cha Daniel
kumtomjali yule mwanamke
kilimuudhi akaingia ndani akiwa
amefura kwa hasira
“ Daniel can we talk? Akasema
akiwa amesimama akimtazama
Daniel kwa hasira
“ Not now Angela.” Akasema
Daniel
“ Now ! akasema Angela kwa
ukali.Uso wa Daniel ukabadilika
kwa hasira ,Akainuka na kumshika
mkono Angela wakaenda
chumbani.
“ Ninakwambia kwa mara ya
mwisho don’t disrespect me
again!! Umenisikia Angela?
Akauliza Daniel akiwa amemkaba
Angela shingoni
“ Daniel lini utaacha tabia
yako chafu ya kubadili wanawake
kama nguo? Ninajiheshimu sana
nikitegemea na wewe
utajiheshimu lakini bado
haubadiliki.Kila siku unakuja na
makahaba ndani.Wewe ni
mwanaume wa aina gani? Ulidhani
nimeondoka na ukaamua kumleta
kahaba wako asubuhi yote hii?
Daniel akamnasa Angela
kibao kikali akaanguka kitandani
“ Yule si kahaba.Ni mwanamke
mwenye heshima zake na wewe
huwezi kujifananisha naye hata
kidogo.Inuka chukua mizigo yako
ondoka nisikuone tena hapa
kwangu.!! Akafoka Daniel
“ Daniel nisamehe sintarudia
tena darling!!
“ Dakika tano nakupa ondoka
hapa haraka sana” akasema Daniel
na Angela akaanza kuvaa kisha
akachukua begi lake akaondoka
.Daniel akarejea sebuleni
alikomuacha Irene
“ Irene samahani kwa
kukuacha peke yako.Nyamaza
kulia ili tujadili na tujue nini
kimetokea? Akasema Daniel
“ Daniel wazazi wangu nani
kawachukua? Wamewapeleka
wapi? Akauliza Irene huku
akimwaga machozi
“Irene usilie tafadhali
.Nyamaza ili tulijadili suala hili na
tulipatie ufumbuzi.Kulia
hakutasaidia chochote .” akasema
Daniel na kumfuta Irene machozi
“ Niambie Irene una tatizo
gani? Nini kimetokea? Tukiwa kule
baa walikufuata wale jamaa
wakataka uongozane nao na kwa
bahati nzuri nilikuwepo
nikakusaidia.Tumerejea nyumbani
na kuikuta hali kama ile.Nyumba
imevurugwa hovyo,mtumishi wa
ndani ameuliwa na mbaya zaidi
wazazi wako wamechukuliwa.Nani
amefanya hivi? Kuna nini
wanakitafuta? Akauliza Daniel
“ Sifahamu Daniel.Siwafahamu
hao jamaa wanaonifauta ni akina
nani na wanataka nini
kwangu”Akasema Irene.Daniel
akautoa ujumbe ule aliouchukua
chumbani kwa Flora akampatia
Irene akausoma na kuanza tea
kulia
“ Daniel nisaidie niwapate
wazazi wangu!! Akasema
“ Irene usilie tafadhali.Hili si
suala dogo.Unatakiwa uwe jasiri
sana kwani haya ni
mapambano.watu hawa
wanaokutafuta kuna kitu
wanakitaka aidha toka kwako au
kwa mmoja wa ndugu zako na
ndiyo maana wamevuruga nyumba
yote kutafuta hicho
wanachokihitaji na walipokikosa
wakaondoka na wazazi wako”
Daniel akanyamaza na kumtazama
Irene kwa makini
“Irene kama kuna kitu
unakifahamu au kama kuna tatizo
lolote lile niambie tafadhali.Niko
hapa nitakusaidia.Endapo kuna
kitu unakifahamu halafu
unakificha kinaweza kusababisha
suala hili likawa baya zaidi au hata
wazazi wako wakapata
madhara.Niambie ukweli tafadhali
kuna tatizo lolote katika familia
yako limetokea? Akauliza Daniel
“ Daniel nimekwambia
sifahamu chochote.Mimi na familia
yangu hatuna ugomvi na mtu na
sielewi kwa nini wale jamaa
wanatufuata na kutuletea matatizo
haya yote.Nisaidie tafadhali Daniel
kuwapata wazazi wangu kama
unao uwezo .Baba yangu ni
mgonjwa na anatakiwa apelekwe
nje ya nchi kwa
matibabu.wakiendelea
kumshikilia atakufa” akasema
Irene na kuanza tena kulia
“ Irene ninatamani sana
kukusaidia lakini sielewi nitaanzia
wapi kukusaidia kwani sielewi
chochote .Hawa jamaa wameacha
namba zao hapo chini.Piga namba
hizo halafu tusikie watasema nini”
akasema Daniel.Irene akaonekana
kusita
“ Irene muda unakwenda
wapigie simu hawa jamaa usikie
wanataka kitu gani.” Daniel
akasisitiza
“ Hapana Daniel sitaki
kuzungumza na hawa jamaa.Kama
unataka zungumza nao usikie ni
akina nani na wanataka
nini”akasema Irene.Daniel
akaziandika katika simu yake
namba zile zilizoachwa kwenye
ujumbe akapiga na simu ikaita
“ Simu inaita” Daniel
akamwambia Irene
“ Hallo” ikasema sauti ya
mwanamke upande wa pili
“ Hallow” akasema Daniel
“ Wewe ni nani na unataka
nini? Akauliza Yule mwanamke
kwa ukali
“ Nimepiga simu kwa niaba ya
Irene maboko ambaye nyumbani
kwao kumevamiwa ,yakafanyika
mauaji na wazazi wake wakatekwa
na mkaacha ujumbe kuwa
awapigie.Ninyi ni akina nai?
Mnataka nini kwake? Wazazi wake
mmewapeleka wapi?
“ Tafadhali kijana naomba
usiingie katika mambo
yasiyokuhusu.Simu hii alitakiwa
kupiga Irene mwenyewe na si mtu
mwingine yeyote.Kwa kitendo hiki
ulichokifanya unazidi kuwaweka
hatarini wazazi wake.”
“ Tafadhali naomba
msiwafanye chochote wazazi wa
Irene.Semeni ni kitu gani
mnakitaka ? Kama mnataka pesa
semeni ni kiasi gani mnakitaka?
Niko tayari kulipa kiasi chochote
cha pesa mnachokitaka” akasema
Daniel
“ Shida yetu sisi si
pesa.Tunamtaka Irene.Muonyeshe
video tutakayoituma hivi punde na
hadi kufika leo jioni apige simu na
bila kufanya hivyo ataletewa miili
ya wazazi wake wakiwa
wamekufa.” Akasema Yule
mwanamke na kukata simu.Baada
ya muda ikatumwa video
waliyoisema Daniel
akaifungua.Katika video hiyo
walionekana wazazi wa Irene
wakiwa wamefungwa katika viti
huku baba yake akiwa anavuja
damu mdomoni.Mama yake Irene
huku akilia akasema
“Irene mwanangu nakuomba
sana wape hawa jamaa kitu
wanachokitaka ama sivyo
watatuua.Hali ya baba yako inazidi
kuwa mbaya .Tafadhali tuokoe
mwanangu.Wape kitu chao” Video
ile ikaishia hapo.Irene aliangua
kilio kikubwa
“ Irene hebu nyamaza.Kulia
hakutakusaidia kitu chochote”
akasema Daniel kwa ukali na Irene
akanyamaza akafuta machozi
“ Irene kuna kitu
unanificha.Tafadhali naomba
unieleze ukweli.Hawa jamaa
wanatafuta kitu gani toka kwako?
Kitu gani ambacho mama yako
anakutaka uwape hawa jamaa ili
wawaachie? Tell me the truth
Irene” akasema Daniel
“Daniel sifahamu kitu
chochote.Siwafahamu watu hawa
na wala sifahamu wanataka nini
kwangu.Tafadhali kama unaweza
kunisaidia kuwapata wazazi
wangu nisaidie Dany.Nitakupa kitu
chochote kile ukinisaidia
kuwapata wazazi wangu”
“Irene kama nilivyokueleza
kwamba natamani sana
kukusaidia katika suala hili lakini
nashindwa nitaanzia wapi
.Ningekuwa ninaufahamu ukweli
ningejua nini nifanye lakini hutaki
kunieleza ukweli.Narudia tena
kukuomba kwa mara ya mwisho
kama kuna chochote unakifahamu
kuhusu wale jamaa nieleze.Wale si
wajinga wakakufuata wewe na
kufikia hatua ya kuwateka wazazi
wako.Lazima kuna kitu
wanakitaka toka kwako.Niambie
ni kitu gani hicho? Akasema Daniel
Irene hakujibu kitu akabaki
kimya
“ Irene muda unakwenda na
usalama wa wazazi wako uko
shakani.Nieleze tafadhali kama
una kitu chochote unakifahamu
kuhusu hawa jamaa ili tuone
namna ya kuwaokoa wazazi
wako.Umeona mwenyewe hali zao
si nzuri na baba yako ni mgonjwa
na hawa jamaa wanaonekana
wamempiga.Tukichelewa anaweza
akapoteza maisha .Is that what you
want? Akauliza Daniel.Irene
akainamisha kichwa.
“ Nafahamu wale jamaa
wanachokitaka.Hii ni siri yangu na
siko tayari kuwapa.Huu ni mchezo
unachezwa aidha na rais au
madam Agatha.Wanachokitaka
toka kwangu ni kujua nimefahamu
vipi kuhusu shambulio lile la
jana.Lazima nitafute namna ya
kuwaokoa wazazi wangu lakini siri
hii siwezi kuitoa kamwe kwa hawa
jamaa.Lakini kwa nini nisimueleze
Daniel ukweli labda anaweza
akanisaidia” akawaza Irene halafu
akainua kichwa akamtazama
Daniel
“ Daniel” akaita Irene
“ Kuna kitu nataka nikwambie
.Nafahamu hawa jamaa
wanachokitafuta toka kwangu.”
“ Niambie Irene ili nione
namna ya kukusaidia” akasema
Daniel.Irene akafuta machozi na
kusema
“ I have a record”
“ A record? Akauliza Daniel
“ Ndiyo.Ninayo rekodi ya
maongezi ya simu kati ya rais na
mkuu wa majeshi,jenerali lameck
msuba.Katika maongezi hayo
walikuwa wanaongelea kuhusiana
na shambulio lililotokea
Dar.Nilirekodi maongezi yao kabla
ya shambulio kutokea”
“ Hebu subiri kidogo
Irene.Umesema uliwarekodi rais
na jenerali lameck wakiongelea
kuhusu shambulio lililotokea Dar
es salaam jana?Uliwarekodi vipi?
“ Nilidukua simu ya rais”
“ You did what ?!!! Daniel
akashangaa
“ Nilidukua simu ya rais”
“ How? Akauliza Daniel akiwa
katika mshangao mkubwa
“ Niliingiza program Fulani
katika simu ya rais ambayo
iliniwezesha kusikia simu zote
anazopiga au kupigiwa.”
Daniel akamtazama Irene kwa
mshangao mkubwa
“ kwa nini ulifanya hivyo?
“ Ni hadithi ndefu nitakueleza
siku nyingine lakini naomba tu
ufahamu kwamba nilidukua simu
ya rais nikanasa maongezi yake na
Lameck wakiongelea kuhusu
shambulio litakalotokea”
‘ Umesema maongezi
hayoyalikuwa kabla ya shambulio?
Daniel akauliza
“ Ndiyo.Ni saa mbili hivi kabla
ya shambulio kutokea.” Akajibu
Irene
“ Unataka kuniambia kwamba
rais na mkuu wa majeshi
walifahamu kuhusu uwepo wa
shambulio hilo? Akauliza Daniel na
Irene akatikisa kichwa kukubali.
“ No ! that’s not true
Irene.Please don’t lie to me”
akasema Daniel
“ Daniel huu si uongo.Hiki ni
kitu cha kweli na ushahidi ninao”
“ Nitakuamini endapo utanipa
huo ushahidi wa hayo maongezi
nisikilize” akasema Daniel
“ Daniel huwezi kuniamini
hadi nikupe ushahidi?Unadhani
ninaweza kukudanganya kwa
jambo kama hili?
“ Irene hili unalolisema ni
jambo kubwa sana kwamba rais
alifahamu kuhusiana na shambulio
lile hata kabla halijatokea.Hili si
jambo linaloweza kutamkwa
kirahisi namna hii.Kama una
matatizo yako binafsi na rais
tafadhali usijaribu kumsingizia
katika jambo baya kama hili.You’ll
destroy him” akasema Daniel
“ Daniel sina sababu yoyote ya
kutunga uongo kumuhusu rais
kwani kwa muda wote amekuwa ni
mtu mwema kwangu lakini
niamini nikwambiacho kwamba
nina ushahidi huo wa kumuhusu
rais na jenerali lameck”
“ I don’t believe you
Irene.Kama hautanionyesha huo
ushahidi sintaweza kukuamini na
kukusaidia” akasema Daniel.Irene
akachukua simu yake aliyoizima
akaifungua na kutoa kadi ya
kuhifadhia kumbu kumbu
akaiweka katika simu anayotumia
kisha akatafuta rekodi ile akampa
Daniel aisikilize.
“ Oh my God !! akasema Daniel
kwa mshangao.
“ I cant believe this” akasema
na kuicheza tena rekodi ile
akaisikiliza kwa makini halafu
akamtazama Irene
“ Kuna mtu yeyote
uliyemueleza kuhusiana na rekodi
hii? Akauliza
“ Wewe ni mtu wa kwanza
kuisikiliza.Ila kama ulivyosikia
maongezi yao walikuwa
wanamlenga madam Agatha hivyo
ikanilazimu kumpigia simu na
kumtaka atoke haraka ndani ya
hilo jengo kwani kuna kitu kibaya
kinakwenda kutokea.Alifanikiwa
kutoka salama katika hoteli ile
kabla ya mlipuko kutokea na
baadae akanipigia simu
kunishukuru kwa kumuokoa
.Alitaka nimueleze nilikopata
taarifa za mlipuko ule nikamuahidi
kwamba nitampigia simu baade
kumfahamisha kila kitu na toka
hapo nimeizima simu hiyo na
sijaitumia tena.” Akasema
Irene.Daniel akainuka na
kuchungulia nje kama kuna mtu
yeyote pale karibu
“Do you believe me now?
Akauliza Irene
“I do.But are you sure this is
real?
“ Yes it is real”akajibu Irene
Daniel akavuta pumzi ndefu
akamtazama Irene na kusema
“ Irene sasa nimepata picha
kamili kwa nini unatafutwa.Hili si
jambo dogo .Ni jambo la hatari
sana umelifanya lakini lenye
manufaa makubwa kwa nchi.Watu
hawa watakuandama usiku na
mchana hadi wahakikishe
wamekutia mikononi kwani
inaonekana tayari wamekwisha
fahamu kwamba kuna kitu
unakifahamu” Akasema Daniel
“ How are you going to help
me? Akauliza Irene
“ Irene kwa hapa ilipofika
kuna kitu nalazimika
nikufahamishe ambacho wengi
hawakifahamu” Daniel
akanyamaza kidogo halafu
akasema
“Ninafanya kazi katika idara
ya siri sana ya ujasusi.Hii ni idara
ya siri mno na ina watuwachache
sana na watu kama sisi
hatufahamiki kirahisi.Mfumo huu
wa maisha yangu ninaoishi nikiwa
na wanawake mbalimbali si
kwamba ninapenda bali
ninalazimika kuishi hivi ili kujenga
taswira tofauti katika
jamii.Ninakuomba uniachie suala
hili nitakusaidia lakini kabla ya
yote ninapaswa kukutafutia
sehemu salama utakayoishi
mahala ambako hawa jamaa
hawataweza kukupata” akasema
Daniel
“ Daniel wewe ni mpelelezi?!!
Akauliza Irene kwa mshangao
“ Ndiyo” Akajibu
“ How come I didn’t know
about this? akasema Irene.Daniel
hakumjibu kitu.Akachukua simu
na kuzitafuta namba Fulani
akapiga.
“ Hallow Monica” akasema
Daniel
“ Daniel ! how’re you? Umepoa
sana hadi najiuliza kuna tatizo
gani?
“Nimetingwa na shughuli
nyingi Monica ndiyo maana
nimepotea.Uko wapi sasa hivi?
“ Niko hapa nyumbani
ninajiandaa nina safari ya
kuelekea Kinshasa baadae jioni”
“ Kuna nini Kinshasa?
“ Naenda kuhudhuria mazishi
ya mke wa rais wa Congo” akasema
Monica
“Monica nina shida nataka
unisaidie.Ninakuja hapo kwako
sasa hivi” akasema Daniel na
kukata simu akamchukua Irene
wakatoka pale ndani wakatembea
mita kadhaa na kukodi taksi
kuelekea kwa Monica.
 
SEASON 7: SEHEMU YA 12
Austin na wenzake
waliizunguka meza kubwa
sebuleni ambayo juu yake
kulikuwa na ramani kubwa ya jiji
la Dar es salaam.walikuwa katika
mjadala kuhusiana na namna
watakavyoondoka kuelekea
uwanja wa ndege.Ilipata saa tisa na
dakika ishirini na nane.Baada ya
kujadiliana kwa kirefu na kufikia
makubaliano namna zoezi la
kuwaondoa Yasmin na mwanae
jijini Dar es salaam litakavyokuwa
Austin akamuelekeza Amarachi na
Marcelo wakamuandae Maria
kwani muda wa kuondoka
ulikaribia sana.
“ Vipi kuhusu Boaz? Akauliza
Job
“ Hatima ya Boaz itategemea
kama Yasmin atakuwa tayari
kuongozana naye.Kama hatakuwa
tayari atabaki hapa na huo
utakuwa mwisho wake ingawa sina
nia ya kumpoteza kwani
amenifanyia mengi mazuri”
Akasema Austin,wakaelekea
chumbani kwa Yasmin
“ Yasmin,muda unakaribia
sana.Dakika chache zijazo tutaanza
safari yetu.Haitakuwa safari rahisi
kwani tayari unafahamika uko
hapa Dar kwa hiyo tutakutana na
vikwazo vingi njiani.Hata hivyo
mimi na wenzagu tutawalinda na
mtaondoka salama hapa
nchini.Narudia kukusisitiza tena
kwamba kama una hakika hiyo
hati haipo,usiache mimi na
wenzangu tukasumbuka
bure.Ukitudanganya I swear I’m
going to kill you.!! Akasema Austin
“Sikudanganyi
Austin.Niamini” akasema Yasmin
kwa kujiamini”
“Umefikia maamuzi gani
kuhusu Boaz? Kama
nilivyokwambia pamoja na yote
aliyoyafanya lakini kuna baadhi ya
mema alinitendea kwa hiyo
ninataka kumpa nafasi ya pili ya
kubadilika lakini ni endapo tu
utakuwa tayari kwenda naye
kuishi mbali na asikanyage tena
Afrika.Uko tayari kwa hilo?
Akauliza Austin
“ Nitaondoka na Boaz.Nataka
tuwe familia moja huko tuendako”
akasema Yasmin
“ Good.” Akasema Austin kisha
wakatoka mle chumbani
“ Job muandae Boaz tayari
kwa safari” akasema Austin kisha
akaenda kumpigia simu Monica
akamfahamisha namna
walivyojipanga.Wakitoka pale
wataelekea nyumbani kwa wazazi
wa Monica watawachukua mzee
Benedict na mkewe na wataelekea
kwa Monica na kutokea pale
itaanza safari ya kuelekea uwanja
wa ndege.Monica alimfahamisha
kwamba amepigiwa simu ndege
iko karibu kutua katika uwanja wa
ndege wa Julius Nyerere.
Maria alitolewa katika kile
chumba akisaidiwa kutembea na
Amarachi akapelekwa
sebuleni.Maandalizi
yalipokamilika wote
wakakutanika sebuleni.
“ Jamani wakati
umefika.Safari inaanza na
ninaomba niwaweke wazi kwamba
haitakuwa safari
nyepesi.Tunaweza kukutana na
vikwazo vingi lakini chochote
kitakachotokea kila mmoja atulie
na afuate maelekezo
atakayopewa.Atakayejaribu
kwenda kinyume au kufanya
jambo lolote la kijinga utakuwa
ndiyo mwisho wake ”akasema
Austin halafu wote wakaelekea
garini.Amarachi akakaa katika
usukani,pembeni yake akakaa
Julieth.Kiti cha kati kati walikaa
Boaz,Yasmin na Maria,nyuma
alikaa Austin akiwa na bunduki
ndogo mbili zilizosheheni risasi
kwa ajili ya kukabiliana na hatari
yoyote ile itakayojitokeza. Marcelo
aliingia katika gari lingine akiwa
peke yake.Gari hili liliwekwa kwa
ajili ya dharura yoyote
itakayojitokeza.Job yeye alikuwa
wa mwisho kutoka pale nyumbani
akiwa na piki piki .Alivaa koti jeusi
ambalo ndani yake alikuwa na
bunduki ndogo na mgongoni
alikuwa na begi kubwa lililokuwa
na vitu mbali mbali mbali ambavyo
wangevihitaji.
“ Please Lord be with us”
Austin akaomba kimya kimya
 
Back
Top Bottom