QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEASON 7: SEHEMU YA 13
Daniel Swai na Irene
wakawasili katika makazi ya
Monica wakashuka katika taksi
wakaingia ndani.Monica
akataarifiwa kufika kwao
“ karibuni sana” akasema
Monica na kukumbatiana na
Daniel kisha akasalimiana na Irene
“ Daniel kimya chako
kimenishangaza sana.Si kawaida
yako kukaa kimya namna hiyo bila
hata kunijulia hali.Kuna tatizo
lolote? Akauliza Monica
“ Hakuna tatizo
Monica.Nilikuwa na vijisafari vya
hapana pale ndiyo maana umeona
kimya namna hii.”
“ Simu nayo ilikuwa safari?
Monica akauliza na wote
wakacheka
“I’m sorry for that Monica.It
wont happen again” akasema
Daniel
“ Haya niambie.Naona
umeniletea mrembo leo” akasema
Monica na kwa mbali Irene
akajilazimisha kutabasamu
“ Anaita Irene maboko ni
rafiki yangu anafanya kazi ikulu.”
Akasema Daniel
“ Irene huyu anaitwa Monica
benedict ni rafiki yangu
mkubwa.Tumekuwa marafiki toka
tukiwa watoto wadogo na hadi
sasa tuko pamoja.Ni mtu wangu wa
karibu sana na ndiyo maana
umeona analalama kwa nini
sijawasiliana naye kwa siku
kadhaa.” Akasema Daniel.Monica
akainuka na kwenda kumpa
mkono Irene
“Karibu sana Irene.Nafurahi
kukufahamu” akasema Monica
“ Monica nimekuja kwako
nina shida nahitaji msaada wako.”
“ Sema shida yako Daniel.”
“ Irene ana matatizo na
anahitaji sehemu salama ya
kujihifadhi kwa muda mfupi
wakati tatizo lake likitafutiwa
ufumbuzi.Kwa kuwa ni rafiki
yangu na mimi ndiye tegemeo lake
nimeona nije hapa nikuombe Irene
akae hapa kwako kwani ni sehemu
salama na kuna ulinzi wa kutosha
hadi hapo suala lake litakapokuwa
limetatuliwa.Naomba sana Monica”
akasema Daniel.Monica
akatabasamu na kusema
“ Daniel hapa ni nyumbani
kwako na hupaswi kuomba.Irene
karibu sana utaishi hapa.Nyumba
hii ni kubwa na bado ninahitaji
watu wa kuishi nao humu.Ulinzi
hapa ni wa uhakika na hupaswi
kuwa na hofu yoyote.Daniel
amekuleta sehemu sahihi”
akasema Monica na wote
wakacheka.Irene akainuka na
kwenda kumpa mkono Monica
akamshukuru
“Monica nashukuru sana kwa
msaada wako huu.Ahsante kwa
kunikaribisha niishi hapa kwako
kwa muda” akasema Irene
“Baada ya kulikubali ombi
lako ni wakati sasa wa kulifahamu
tatizo la Irene” akasema Monica
“ Monica tatizo la Irene ni
binafsi kwa hiyo itoshe tu
kumsaidia sehemu ya kukaa.Hayo
mengine sidhani kama yana
umuhimu ” akasema Daniel
“ Daniel hili si tatizo binafsi
tena.Tayari limekuwa tatizo letu
sote.Nimekubali kumsaidia Irene
kwa moyo mmoja kwa hiyo
nitahitaji kufahamu Irene ana
tatizo gani? Akauliza Monica
“ Monica tatizo la Irene ni
kubwa na tayari ninalishughulikia
kwa hiyo nitakufahamisha pale
ufumbuzi wake utakapokuwa
umepatikana” akasema Daniel
“ Daniel haijawahi kutokea
ukanificha kitu chochote hata zile
siri zako kubwa umekuwa
unanieleza.Thats because you trust
me.Kama umeniamini ukanieleza
mambo yako yote,niamini pia
katika hili” Akasema
Monica.Daniel akatazamana na
Irene halafu akamwambia
“I trust her with my life.Hana
tatizo hata akifahamu” Irene
akatikisa kichwa kukubaliana na
Daniel
“ Kama nilivyokueleza awali
kwamba Irene anafanya kazi
ikulu.Ndiye anayehusika na mfumo
wote wa ulinzi wa mtandao wa
kompyuta wa ikulu.Katika
shughuli zake hizo alifanikiwa
kuyanasa maongezi ya simu kati ya
rais na mkuu wa majeshi
wakizungumzia kuhusu shambulio
lile lililotokea jana.Mazungumzo
hayo aliyanasa kabla shambulio
hilo halijatokea na hii inatoa picha
kwamba rais na mkuu wa majeshi
walifahamu kuhusu kutokea kwa
shambulio hilo kabla .Mapema leo
nikiwa na Irene pale Tiger hotel
walikuja watu wawili wakamtaka
Irene aongozane nao lakini
nilipambana nao kisha
tukafanikiwa kuondoka.Tulipofika
nyumbani kwao tukakuta nyumba
imevurugwa mno,mfanyakazi wa
ndani amepigwa risasi na
wazaziwake hawajulikani
walipo.Tukiwa pale wakatokea
wau wawili tukapambana nao na
kufanikiwa kutoroka ndipo Irene
aliponieleza kila kitu kilichotokea”
Akasema Daniel halafu
akamuomba Irene amuwekee
Monica rekodi ile aisikilize.Monica
akaisikiliza na kuwatazama Daniel
na Irene kwa mshangao
“ Is this true?!! Akauliza akiwa
haamini alichokisikia
“ Yes .Its true” akajibu Irene
“ Jesus Christ !! akasema
Monica
“ Irene una hakika hawa
wanaozungumza humu ni rais
Ernest na mkuu wa majeshi? Siyo
kwamba kuna watu wametumia
teknolojia wakatengeneza sauti
hizi? Akauliza Monica
“Hiki si kitu cha kutengeneza
Monica.Hizi ni sauti za kweli za
rais na mkuu wa
majeshi.Niliyanasa mimi
mwenyewe kwa kutumia simu
yangu.”akasema Irene
“ Dah ! nimeishiwa nguvu”
akasema Monica
“Pembeni ya maiti ya
mfanyakazi wa ndani wa akina
Irene kuliachwa karatasi hii” Danel
akaitoa karatasi ile akampa
Monica akaisoma
“Nilipiga namba hizo za simu
nikaongea na hao jamaa
wakasisitiza kwamba wanataka
kuzungumza na Irene na si mtu
mwingine kisha wakatuma video
hii” akasema Daniel na
kumuonyesha Monica video ile ya
mama yake Irene akilia akimtaka
Irene amsaidie.Monica
akashindwa kujizuia akainuka na
kwenda kumkumbatia Irene wote
wawili wakilia
“ Pole sana Irene.Hili ni tatizo
kubwa lakini nakuahidi kwamba
litakwisha.Utawapata tena wazazi
wako” Akasema Monica na kufuta
machozi halafu akasema
“ Nina safari ya kuelekea
Congo kwa ajili ya kuhudhuria
mazishi ya mke wa rais wa Congo
na kama isingekuwa hivyo
ningeahirisha safari hiyo kwa ajili
ya suala hili lakini si muda mrefu
toka sasa atakuja hapa mtu mmoja
anaitwa Austin January.Huyu ni
mpele..”
“ Monica hebu subiri
kidogo.Umesema Austin January?!
Akauliza Daniel
“ Ndiyo.Do you know him?
‘ Yes but that man is dead!!
Akasema Daniel
“ He’s not dead.He’s alive na
muda sio mrefu sana toka sasa
atafika hapa.” Akasema
Monica.Daniel alionekana
kushangaa sana
“ Monica hayo unayosema ni
ya kweli?
“ Ni kweli kabisa Danny”
akajibu Monica
“ he must be a ghost.Austin
January ninafahamiana naye na
alifariki nchini Somalia miaka
kadhaa iliyopita.Nashangaa
kuniambia kwamba yuko hai na
yuko hapa Tanzania.”
“ Daniel niamini
nikwambiavyo kwamba Austin
yupo na atakuja hapa utaonana
naye.Austin ni mpelelezi
mashuhuri na atalishughulikia
suala hili .Irene usijali suala hili
litakwisha na wazazi wako
utawapata.” Akasema Monica na
kuwaomba akina Daniel
wamsubiri pale akamalizie
kujiandaa kwa ajili ya safari.
“ Irene,huyo Austin January
aliyemsema Monica ni mtu hatari
sana .Amewahi kufanya kazi katika
idara ya ujasusi na sote tuliamini
kwamba alifariki nchini Somalia
kumbe yuko hai.Haya ni maongozi
ya Mungu kwani suala hili sasa
limefika katika mikono salama na
litashughulikiwa ipasavyo” Daniel
akamwambia Irene
“ Thanx Daniel.Huyu rafiki
yako Monica anafahamu kama
wewe ni mpelelezi? Akauliza Irene
“ Hafahamu chochote.Hakuna
miongoni mwa marafiki zangu
anayefahamu suala hili ni wewe tu
ambaye nimekueleza ukweli.Ila
Austin ananifahamu vyema”
akasema Daniel
“Daniel kuna jambo limekuwa
linaniumiza sana kichwa
changu.Unadhani rais anahusika
katika lile tukio? Akauliza
“ Ni mapema mno kusema
chochote kwa sasa hadi hapo
uchunguzi utakapofanyika
tutafahamu kila kitu” akasema
Daniel
Monica aliingia chumbani
kwake kwa dhumuni la kumalizia
kujiandaa kwa safari lakini
akajikuta akikaa kitandani
kutokana na mawazo mengi
aliyokuwa nayo
“ Ernest Mkasa .Is this the
president I voted? Kwa ushahidi
huu alionao Irene ni wazi rais
anahusika na mashambulio haya
mawili.Oh my Gosh ! huyu mtu
anaipeleka wapi nchi hii?
Ningekuwa na uwezo kama wa
akina Austin ningehakikisha
anafikishwa mbele ya sheria na
anahukumuwa kifo.Ameua watu
wengi wasiona hatia.I hate him so
much” akawaza Monica
 
SEASON 7: SEHEMU YA 14
“Mkuu kuna watu wawili
wameshuka katika taksi na
wameingia nyumbani kwa
Monica.Ni mwanamke na
mwanaume lakini hawa
wanaonekana ni watu wake wa
kawaida.Hawana wasifu wowote
unaoshabihiana na wale
tunaowatafuta” Mmoja wa watu wa
usalama wa taifa waliokuwa mita
chache toka nyumbani kwa Monica
wakifuatilia kila kilichokuwa
kinaendelea alimtaarifu Silvanus
Kiwembe.
“ Sawa endeleeni
kufuatiliakila kinachojiri hapo
ndani na mnipe taarifa,mimi
nimepata dharura kidogo”
akasema Silva
Baada ya dakika ishirini
kupita toka wale jamaa wawili
walipoingia nyumbani kwa Monica
gari mbili zikaingia pale ndani na
wakashuka watu watu nane.Wote
wakiwa na mavazi meusi.
“ Mkuu kuna gari mbili
zimeingia hapa ndani na watu
nane wameshuka.Naona kuna
wanawake watano na wanaume
watatu.Wote wamevaa mavazi
meusi”
Silvanus Kiwembe
akataarifiwa na vijana wake
wanaoendelea kumfuatilia Monica
“ Inawezekana ni ndugu zake
anaoambatana nao kwenda
kwenye msiba.Kwa hapo mlipo
mnaweza kuwavuta kuona sura
zao?
“ Kuna ugumu kidogo kwa
sababu kamera imewekwa juu ya
mnazi mrefu na kuna kuti la mnazo
limeanza kuifunika kwa hiyo
inatuwia ugumu kuona vizuri”
“ Sawa.Endeleeni kuwafuatilia
watakapotoka watafuatiliwa na
watu wetu njia watakayopita
halafu tutawasiliana na polisi
walio katika kizuizi watawazuia ili
tuwakague” Silvanus akatoa
maelekezo.
Monica akawapokea wageni
wake akawakaribisha
sebuleni.Austin akabaki nje akatoa
simu na kuwasiliana na Job
“ Tuko nyumbani kwa Monica
sasa.Kuna chochote umekiona
huko njiani? kuna mtu yeyote
aliyekuwa anatufuatilia? Akauliza
Austin
“ Mpaka hapa hakuna hatari
yoyote.Marcelo tayari amefika
mahala tulikompangia ” akasema
Job
“ Good.Kama huko njiani
hakuna tatizo lolote tunatakiwa
tujiridhishe kwamba hata hapa
nyumbani kwa Monica hakuna
tatizo lolote kabla hatujatoka.Sasa
unaweza kuja hapa ili tufanye
uhakiki wa mwisho kabla ya
kuondoka.Monica ni mtu
wanayemtegemea sana
kuwaongoza niliko kwa hiyo
lazima tujiridhishe kwamba
hakuna mtu yeyote aliyewekwa
kumfuatilia .Lazima tuhakikishe
njia ni safi kabla ya kuwatoa watu
humu ndani kuelekea uwanja wa
ndege.Come quick we don’t have
much time here” akasema Austin
akakata simu na kuingia
ndani.Akavua miwani na mara
akakutana na kitu ambacho
hakuwa amekitegemea.
“Daniel !! akasema kwa
mshangao
“ Austin !! Is that you? Daniel
naye akasema kwa mshangao
asiyaamini macho yake.Akainuka
na kwenda kumkumbatia Austin
“ Is that you brother ? akauliza
Daniel kwa mshangao.
“ Yes its me” akajibu Austin
huku akitoa kicheko kidogo
“ You must be a ghost.”
Akasema Daniel na wote
wakacheka
“What are you doing here?
Austin akauliza
“ Mimi hapa ni kama
nyumbani.Monica ni rafiki yangu
toka tukiwa wadogo.Mzee Ben na
mama Janet hawa ni wazee wangu
wananifahamu vyema sana.Monica
aliniambia kuhusu wewe
nikashangaa na sikumuamii hadi
nilipokuona kwa macho yangu
mwenyewe.”akasema Daniel
“ Nimefurahi sana kukuona
tena Daniel.Ni muda mrefu
umepita” akasema Austin na mara
mlango ukagongwa Monica
akaenda kuufungua akakutana na
Job.
“ Job karibu sana” akasema
Monica.Daniel akastuka na
kugeuka aliposikia Monica
akimkaribisha ndani Job
“ Oh my God is this true?!!
Akasema kwa mshangao baada ya
kumuona Job akiwa na begi kubwa
mgongoni.Job naye akastuka baada
ya kumuona Daniel
“ Daniel ? akasema Job.
“ Job !! akasema Daniel na
kwenda kukumbatiana na Job
“ Leo ni siku ya muujiza
mkubwa kwangu.Siamini
ninayoyaona.” Akasema Daniel
.Monica akabaki anashangaa
“ Do you know each other?
Akauliza
“ Yes .We do know each other”
akajibu Daniel.
“ Good to see you Daniel.We’ll
talk later but for now I have a job
to do” akasema Job .Kabla ya
kufanya chochote Monica
akawaomba Austin ,Job Daniel na
Irene wakaongee kidogo
pembeni.Kabla ya kutoka pale
sebuleni Austin akamfuata
Amarachi akamnong’oneza sikioni
“ Kuwa macho sana.Don’t give
them a chance.Yeyote
atakayethubutu kuleta ujinga
wowote mmalize mara moja”
akasema Austin na kutoka mle
sebuleni akawafuata akina Monica
walioingia katika chumba
kingine.Benedict mwamsole na
mkewe Janet walibaki
wanashangaa kwa mambo
yalivyokuwa yanakwenda na
hawakuelewa kilichokuwa
kinaendelea.
“Austin ahsanteni kwa
kufika.Tayari nimetaarifiwa ndege
imekwisha tua na inatusubiri kwa
hiyo kilichobaki hapa ni ninyi
kukamilisha mambo yenu ya
usalama ili tuweze kuondoka
hapa”akasema Monica
“ Tunachotaka kukifanya kwa
sasa ni kufanya uhakiki kama
hakuna mtu yeyote aliyewekwa
hapa maeneo ya nyumbani kwako
kukuchunguza .Job utapanda juu
ghorofani .Rusha drone na
tuchunguze kama kuna mtu yeyote
anayetufuatilia kabla
hatujaondoka.” Akasema
Austin.Monica akamuonyesha Job
njia ya kuelekea juu.Job akiwa na
begi lake kubwa lililokuwa na vifaa
mbalimbali akapanda ghorofani.
“Austin naomba kwa dakika
chache kuna suala nataka
tulizungumze” akasema Monica na
kumgeukia Daniel.
“Daniel huyu ndiye yule rafiki
yangu Austin niliyekwambia na
kwa bahati nzuri unafahamiana
naye.Austin huyu mwanadada
mrembo anaitwa Irene ni
mfanyakazi wa ikulu.”
Akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“ Si muda mrefu sana Daniel
na Irene wamekuja kwangu na
kuna jambo wamenieleza ambalo
limenistua mno.Daniel unaweza
ukamueleza Austin ilivyokuwa?
Akasema Monica.Daniel
akamueleza Austin kila kitu na
kumpa ile rekodi akaisikia na
mwisho akampa ile video ambayo
waliituma watu waliowateka nyara
wazazi wa Irene akaitazama na
kuvua miwani akafuta jasho usoni
na kumtazama Irene kwa macho
makali
“Irene are you sure this is
real? Akauliza
“ Yes I’m sure” akasema Irene
“ Good job.Ulifanya jambo la
hatari lakini zuri na kubwa sana
.Usiwe na wasi wasi wazazi wako
watapatikana wakiwa
hai.Nakuomba nenda kapumzike
sebuleni niache mimi na hawa
wenzangu tujadili jambo hili”
akasema Austin na Irene akarejea
sebuleni.
“ This is what we’ve been
looking for.Nilikuwa natafuta sana
kitu cha kuweza kumuunganisha
rais ana matukio yale ya jana na
sasa kimepatikana.Ni wazi rais na
Jenerali Lameck wanahusika
katika mashambulio ya
jana.Rekodi hii ni mwanga mzuri
tumepata but we have to dig
deeper.Tunatakiwa tupate
ushahidi wa kutosha
kutuhakikishia kwamba ni kweli
rais na mkuu wa majeshi
wanahusika na jambo hili.Daniel
are you active? Akauliza
Austin.Daniel akamtazama Monica
na kisha akasema
“ Yes I am”
“ Wait ! akasema Monica
“Unamaanisha nini
unapomuuliza kama yuko
active?Akauliza Monica
“ Monica kuna kitu ambacho
hukifahamu na sijawahi kukueleza
na si wewe tu watu wengi
hawafahamu hata wazazi wangu
hawajui.Ninafanya kazi katika
idara ya siri sana ya ujasusi.”
“ What ?! Monica akashangaa
“ Monica I’m sorry for hidding
this .Tutazungumza baadae ila kwa
sasa tuongelee suala lililko mbele
yetu” akasema Daniel
“ Oh my God ! I cant believe
this !! All these years and you
didn’t even tell me ? akauliza
Monica.
“ Monica tutaliongelaa baadae
suala hilo.Daniel welcome to the
team” akasema Austin
“Thank you Austin.Ni furaha
yangu kufanya kazi nawe”
akasema Daniel
“ Daniel kuna jambo kubwa
ambalo mimi na wenzangu
tunaendelea nalo linalomuhusu
huyo huyo rais na kutokana na
suala hilo jioni hii mimi na
mwenzangu mmoja tunasafiri
pamoja na Monica kuelekea
Kinshasa na tutarejea kesho au
kesho kutwa.Job atabaki hapa kwa
pamoja mtahakikisha mnawapata
wazazi wa Irene .Hii rekodi
ninaondoka nayo.It’ll be safe with
me.Huu ni ushahidi mkubwa sana
na siwezi kuuacha kwa mtu
yeyote” Mara mlango wa kile
chumba ukafunguliwa akaingia
Job.
“ I found something” akasema
Job akiwa ameshika kompyuta
yake ndogo.
“Umepata kitu gani Job?
Akauliza Austin
“ Nimerusha drone nimepata
picha hizi.Mita kadhaa toka hapa
kuna gari mbili zimeegeshwa na
kuna watu kadhaa wengine wako
nje wamesimama wakipiga soga na
wengine wako ndani ya
gari.Mwanzo nilidhani labda ni
watu wa ardhi wanapima lakini
baada ya kuchunguza kwa makini
nimegundua si watu wa
ardhi.Mmoja wao amevaa miwani
kama hii ambayo ina kamera
ambayo wapelelezi huitumia
sana.” Akasema Job.Austin
akazitazama picha zile halafu
akampa Daniel.
“ Hawa ni watu wa usalama wa
taifa.Nimegundua namba za
magari wanayotumia”akasema
Daniel
“ So I was right.Watu hawa
wamewekwa pale kwa lengo moja
tu la kumchunguza Monica kwani
wanaamini kabisa kwamba ana
mahusiano na mimi.” Akasema
Austin
“ Wait” akasema Monica kwa
woga
“ Kama watu hawa ni usalama
wa taifa na wamewekwa hapa kwa
ajili ya kunichunguza mimi mbona
wamekaa mbali,kwa nini
wasingekuwa maeneo ya karibu?
Akauliza Monica
“Teknolojia inafanya
kazi.Wanafanya kazi hata wakiwa
mbali.Wanasaidiwa na kamera au
satelaiti .”
“ Lazima kuna kamera
imewekwa mahala ambayo
inaweza kuchukua picha na
kurusha moja kwa moja mahala
walipo” akasema Daniel
“ Tunawafanya nini hawa
jamaa? Hatuna muda wa kutosha”
akasema Job
“ Tuwaondoe maeneo haya ili
tupate nafasi ya kuondoka.”
Akasema Austin kisha wakapanda
wote juu ghorofani.Job akalifungua
begi lake kubwa akatoa sanduku
fulani akalifungua na kuanza
kuunganisha bunduki yenye
uwezo wa kulenga kwa umbali
mrefu.Kwa kutumia kiona mbali
kilichokuwa katika bunduki ile,Job
akaachia risasi moja iliyopiga kioo
cha mbele cha gari moja na
kuwastua wale jamaa.Wakiwa
hawana hili wala lile risasi
zikaendelea kuvuma na kuvunja
vioo vya magari yao.Job hakuwa na
lengo la kumuua hata mmoja wao
bali alitaka kuwaondoa eneo lile
kama alivyoelekezwa na Austin.
Watu wote waliokuwa katika
magari yale mawili wakatimua
mbio kujiokoa wakayatelekeza
magari yao na Job akayatoboa
matairi yote kwa risasi
“Huu ni wakati wa kuondoka
kabla wale jamaa hawajarejea
tena” akasema Austin na kumpa
Job maelekezo ashirikiane na
Daniel katika suala lile la Irene
wakati yeye akiwa Kinshasa
Watu wote waliingia katika
magari mawili na safari ya
kuelekea uwanja wa ndege ikaanza
huku Irene akiachwa pale
nyumbani apumzike.
Walifika uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere bila kupata
matatizo yoyote na wakapokewa
na Pierre Muyeye msaidizi wa
David Zumo na kwa kuwa taarifa
tayari zilikuwepo kwa uongozi wa
uwanja ,Monica na watu wake wote
wakaongozwa na Muyeye hadi
ndegeni.
Jenerali Lameck Msuba akiwa
bado mjini Dodoma alipokea simu
toka kwa Silvanus Kiwembe
akamtaarifu kwamba vijana wake
wameshambuliwa na watu
wasiowafahamu na kwa muda wa
daika kadhaa walipoteza
mawasiliano na makao makuu kwa
hiyo hawakupata nafasi ya
kufuatilia kilichokuwa
kinaendelea nyumbani kwa
Monica
“ Wilson,unataka kuniambia
mmeshindwa kuwafuatilia akina
Monica? Akauliza Lameck kwa
ukali
“ Kama nilivyokwambia
Jeneral kwamba vijana wangu
walishambuliwa na watu
wasiowafahamu wakatawanyika
na kupoteza mawasiliano na
makao makuu .Magari na vifaa
vyao vimeharibiwa vibaya kwa
risasi hivyo iliwabidi kukimbia
kunusuru maisha yao kwani kwa
eneo walilokuwepo hawakujua
wanashambuliwa toka
wapi.Waliporejea tayari Monica na
familia yake walikwisha
ondoka.Tulipowasiliana na vijana
waliokuwepo uwanja wa ndege
tulikuwa tumechelewa kwani
tayari Monica na watu wake
walikwisha ingia ndegeni na hivi
tuongeavyo ndege tayari imepaa
kama dakika nne
zilizopita.Nimetumiwa picha za
kamera za usalama pale uwanjani
na nimejiridhisha kwamba mmoja
wa watu wale walioongozana na
Monica ni Yasmin Esfahani.”
“ Silva how could you miss
her? Huu ni uzembe mkubwa sana
na laiti ungekuwa karibu yangu
ningekuchapa kibao.Athari za hiki
ulichokifanya ni kubwa mno”
Akasema Lameck na kukata simu
kwa hasira
“ Stupid !! akasema kwa hasira
.Akafikiri kidogo halafu
akazitafuta namba fulani katika
simu yake na kupiga akatoa
maelekezo
“ Afande nahitaji
kuhakikishiwa kwa mara ya
mwisho.Are you sure Sir? Akauliza
mtu aliyekuwa anazungumza na
Jenerali Lameck simuni
“ I’m sure.Take down that
plane!! Akasema Lameck kwa
hasira.
“ I don’t have a choice.Yasmin
hatakiwi kutoka nje ya Tanzania.Ni
bora akafariki dunia kuliko
kuvuka mpaka na kutokomea na
hati ya muungano.Monica yuko
ndani ya ile ndege lazima naye
ateketee hakuna namna nyingine
ya kufanya.Huyu amekuwa ni
kikwazo kikubwa sana katika
kufanikisha mipango yetu.Ni kwa
kupitia yeye Austin alimtorosha
Yasmin kutoka Zanzibar.Kama
haitoshi leo tena huyu huyu
Monica anatumika kumuondoa
nchini Yasmin mtu muhimu
ambaye tunamuhitaji mno.Austin
na wenzake tayari wanafahamu
mambo mengi waliyoambiwa na
Yasmin kwa hiyo itakuwa jambo
zuri nao pia wakipotea
kabisa.Jambo hili litasababisha
mgogoro mkubwa kati yangu na
rais akigundua kwamba mimi
ndiye niliyetoa amri ndege
aliyopanda mwanae ilipuliwe na
mgogoro mwingine utakuwa nikati
ya Tanzania na Congo.Lolote
litakalotokea nitakabiliana nalo
lakini ndege lazima ilipuliwe.!!
Akawaza .
Dakika kadhaa baada ya dege
la rais wa Congo kuondoka katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere,marubani
waligundua kitu
kilichowastua.Ndege nne za vita
zilikuwa zinawaelekea na
kilichowastua zaidi ni mfumo wa
kutambua makombora ya adui
kuwaonyesha kwamba
makombora katika ndege zile
yaliwekwa tayari kwa
kushambulia.
TUKUTANE SEHEMU
IJAYO………………………
 
Back
Top Bottom