Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Sura 36:37-40 inasema, "Na ishara yao ni usiku: Tulijitoa pale toka mchana, na tazama wakazamishwa kwenye giza; 38 na jua linafuata mkondo wake wa kawaida kwa muda liliopangiwa; hii ni amri yake (yeye), aliyeinuliwa kwenye nguvu, yeye ajuaye vyote
Hiyo Aya uliyotaja ni hii hapa
وَآيَةٌ لَّهُمُ اللَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ النَّهَارَ فَإِذَا هُم مُّظْلِمُونَ
Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani.
وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ
Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua.
وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ
Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe.
لَا الشَّمْسُ يَنبَغِي لَهَا أَن تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ
Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.
Sasa niliyoandika ndio sahihi zaidi
Sasa niambie tatizo ni nini,au unataka kuelewa nini mkuu