Duuuuu!
Huyo Mungu unayemwamini ni mkali kweli!!!!!
Ni namna tu ya kuongea kuwa Mungu anawaita kwake watu toka Dunia hii. Wala kifo mbele ya Mungu si adhabu bali ni kuhamisha watu toka Maisha ya Duniani na kuwaweka kwenye umilele, kadiri ya matendo yetu hapa duniani: ama raha ya milele au kuangamia.
Hawajakosea hata kidogo waliosema hivyo kwani Maisha yetu yamo mikononi mwa Mungu. Mungu ndiye mtoa uhai naye pia ndiye huturejesha kwake.
Kidogo kidogo
Kidogo kidogo bwana wewe eeeeee
Kidogo kidogo baba
Kidogo kidogo
Pole pole
Pole pole mume wangu wee
Saa nane za usiku bwana wewe watoka wapi?
Saa nane za usiku mume wangu nambieeeee
Kama ni marumba, mbona peke yako?
Kama ni maraha, ulikuwa na nani bwana
Pole pole
Pole pole mume wangu wee
Nikikuulliza ulikuwa wapi Bazo
Nikikuuuliza unatoka wapi mume wangu baba watoto?
Wanijia juu kwa mateke na mangumi(x2)
Haina ujanja hiyo
Haina dawa
Haina Kinga
Haina sindano.....WAFWA
''Orchestra Makassy, the brainchild of Mzee Makassy himself, has taken audiences all over East Africa by storm. Their blend of pure Kiswahili and Zairois rhythms have captured the hearts of music lovers who have constantly demanded this set of Makassy's greatest hits.
The popularity of the group has not come without its share of disappointments and it has entailed great work from Mzee Makassy. The group would perhaps have been a household name sooner had it not been for the unexpected and tragic knifing of the lead singer Isiak Baharia, alias Gobby. This sad event caused great turmoil but from the ashes of the former group Mzee Makassy moulded his present band with the considerable help of Rammy Ongara and Fan Fan from OK Jazz. These were then supplemented with Aimala Mbutu, Simaroo on Solo guitar, Kadesi on Bass, Batty on Rhythm and Adam Seye on Trumpet (also formerly with OK Jazz) amongst the others in the group.Thus the Orchestra Makassy, whose emblem of the elephant and drum has become famous in such a short space of time, has brought some of the finest musicians together from the brink of disaster to the top of the charts. Here now are Makassy's greatest hits - the first set of many from this fine band."
source; worldservice: The brink of disaster
Mkuu hata mimi nasubiri kwahamu hizi taarifa! MwanaVillage tafadhali naomba tuzibitishie hizi habari kama ni za kweli!
Halafu kuna kibwagizo cha AMISA ambacho kila ninapokisikia hujikuta nikitabasamu mwenyewe:
(Remmy) Hodi hodi jamani humu ndani hodiii,
(Binti) kariibu,
(Remmy) Wewe ni mke wa nani kwenye nyumba hii,
(Binti) mimi mke wa fundi koroboi pale muembeni,
(Remmy) yule mwenye anakaa banda la uani huku,
(Binti) mmmmmm!
(Remmy) Mume wako ameenda wapi?
(Binti) Mume wangu ameenda gerezani kutafuta makopo,
(Remmy) Hivi we mtoto unajua mi ni nani?
(Binti) hivi we ndio nani?
(Remmy) Mi ndio baba mwenye nyumba hii!
(Binti) mmmmmm, Shikamooo!
(Remmy) Marahaba marahaba,mpaka nikuambie mi ndio mwenye nyumba ndio unaniamkia? haya mama marahaba!
(Remmy) Hivi we mtoto umetoka wapi
(Binti) mimi nimetoka Dodoma
(Remmy) umetoka Dodoma? we Mgogo?
(Binti)Aka! Mi sio Mgogo mi Mkaguru
(Remmy) Sasa we mtoto!
(Binti) mmmm?
(Remmy) Unajua ukifika Darisalamu ni lazima utuone watu kama sisi utapata kila kitu bure! Au Vipi?
(Binti) basi nitasubiri mume wangu akija nimuambie tumepata chumba cha bure!
(Remmy) Utasubiri mume wako akija umumbie ya kwamba Mzee Chumaulete ametupa chumba cha bure? basi akija fungasheni na ondokeni, Ondokeeni!
(Binti) Baaasiii!
Huu ulikuwa ni Ubunifu mkubwa wa Dr Remmy kueleza kwa kifupi tu matatizo yaliyokuwa yanawapata wapangaji wenye wake na vipato vidogo kutoka kwa baadhi ya wababa wenye nyumba. Sikumbuki yule binti aliyekuwa aliyemuitikia Dr Remmy aliishia wapi kwenye ulimwengu wa Muziki.