R.I.P. Dr. Remmy Ongara

R.I.P. Dr. Remmy Ongara


MWANAIDI

nimetokea kumpenda binti Mwanaidi
nimeridhishwa na tabia yake
nikaamua tufunge nae pingu za maisha
urithi ulioacha baba niliutumia
ili kuneemesha ukoo wake
nilianza kuuza mifugo
hatimaye shamba
ili kumtosholeza mahitaji yake ehhh

baada ya miezi michache nikapata barua kutoka kwa Mwanaidi
..... .. kuwa yeye hanitaki tena
tena hawezi kuolewa na mimi

(wote)
mimi najuta eh najuta mama
gharama nilizogharamia
ameona bure
sijui la kufanya .. nasikitika oh
sababu yako ....... Mwanaidi x 3
 
Duuuuu!

Huyo Mungu unayemwamini ni mkali kweli!!!!!

Ni namna tu ya kuongea kuwa Mungu anawaita kwake watu toka Dunia hii. Wala kifo mbele ya Mungu si adhabu bali ni kuhamisha watu toka Maisha ya Duniani na kuwaweka kwenye umilele, kadiri ya matendo yetu hapa duniani: ama raha ya milele au kuangamia.

Hawajakosea hata kidogo waliosema hivyo kwani Maisha yetu yamo mikononi mwa Mungu. Mungu ndiye mtoa uhai naye pia ndiye huturejesha kwake.


Kasome kitabu cha Ayub ndio utajua chanzo cha usemi huo na kitabu cha Muhubiri. Mungu afurahii kifo cha mtu na huwa anasikitika hata kwa maovu yanayowapata wanadamu, hivyo siwezi kumuhusisha na jambo lolote ovu au kifo. Nikutoelewa Bible tu ndio sababu na kutofikiri jinsi anvyotenda ndio maana wengi humsingizia kuwa ni muhusika katika vifo vinavyowapata wanadamu. Nikupe mfano mmoja. Wewe umeweka dawa ya kuua panya nyumbani na ukawaambia watoto wasijekula dawa hiyo maana wakila itawazuru, akatokea jirani mwenye roho mbaya akasema kuleni hiyo dawa ni tamu kweli. Mkila alafu mkifa mtasema ni Baba ndiye kaua watoto wake au ni yule jirani aliyewadanganya? Mungu kwakuwa ni mwenye nguvu (sifa yake kuu) angeweza kuzuia Adam na Hawa wasife, ndio maana tunasema "aliruhusu" kifo lakini hakukisababisha, aliyesababisha ni shetani.

Huyo ndio chanzo cha yote na anapaswa kulaumiwa, Mungu alituumba tuishi milele katika paradiso duniani hakuwa natarajio la sisi tufe. Revise your bible reading !
 
Mwanza

Mwanza oooh Mwanza eeeh,
Mwanza mji mzuri eeh,
Mwanza nitarudi Mwanza,
Mwanza nitakuja tena! x2

Mji wa Mwanza umezungukwa na milima ya mawe,
Milima ya alimasi,
Milima ya dhahabu,


Mji wa Mwanza umezungukwa na Lake Victoria,
Lenye maji bariiiidi,
Na samaki watamu wazuri,
Mwanza ooh,

Nalia Mwanza,
Wakazi wa Mwanza ni Wasukuma ooh,
Kabila Wasukuma,
Sukuma waaa!
Sukuma waaa!


Kutoka Mwanza tulielekea Bukoba,
Bukoba tulipokewa vizuri eeh,
Matoke kwa wingi,

Wakazi wa Bukoba wanasema Kihaya,
Mwabonaki waitu,
Mmmmh waitu eeeh


Mwanza oooh Mwanza eeeh

 
Kidogo kidogo

Kidogo kidogo bwana wewe eeeeee
Kidogo kidogo baba
Kidogo kidogo
Pole pole
Pole pole mume wangu wee

Saa nane za usiku bwana wewe watoka wapi?
Saa nane za usiku mume wangu nambieeeee

Kama ni marumba, mbona peke yako?
Kama ni maraha, ulikuwa na nani bwana

Pole pole
Pole pole mume wangu wee

Nikikuulliza ulikuwa wapi Bazo
Nikikuuuliza unatoka wapi mume wangu baba watoto?
Wanijia juu kwa mateke na mangumi(x2)
Haina ujanja hiyo
Haina dawa
Haina Kinga
Haina sindano.....WAFWA
 
Kidogo kidogo

Kidogo kidogo bwana wewe eeeeee
Kidogo kidogo baba
Kidogo kidogo
Pole pole
Pole pole mume wangu wee

Saa nane za usiku bwana wewe watoka wapi?
Saa nane za usiku mume wangu nambieeeee

Kama ni marumba, mbona peke yako?
Kama ni maraha, ulikuwa na nani bwana

Pole pole
Pole pole mume wangu wee

Nikikuulliza ulikuwa wapi Bazo
Nikikuuuliza unatoka wapi mume wangu baba watoto?
Wanijia juu kwa mateke na mangumi(x2)
Haina ujanja hiyo
Haina dawa
Haina Kinga
Haina sindano.....WAFWA

Lete utamu Ngongo
 
Asante mkuu MBU, niwekee Mwanza aiseeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, halafu na ule wa Dodoma, walahi leo sifanyi kazi nasikiliza on line nyimbo zote.
 
Hivi sasa namuomboleza Dr kwa kusikiliza nyimbo zake murua,Mariam eh,kwenye mapenzi kiwete hupakatwa,mambo kwa soksi,congas zinasikika kwa utamu RIP Dr,kwa sisi wakazi wa Sinza tutakukumbuka sana kwani nyumbani pako tulipafanya" kijiwe" cha kupata menu free ,kuangalia TV ,kujifunza muziki,kupata vijisenti,wasela walikuwa wanashinda from asubuhi kwa kupata break fast hadi jioni mpaka wapate "sapa" na tulikuwa tunafurahi sana kwa kupewa mastori ya majuu na kuangalia photo /cd za mtoni.Ulitoka kwa udongo utarudi kwa udongo
 




...R.I.P Remmy Ongala...:rip:
 
Last edited by a moderator:
...Nakumbukia miaka ya 1977 Orch Makassy walifanya show za mwanzo mwanzo pale Diamond Jubilee na Dr Remmy ambaye walimleta kuziba pengo la marehemu Isiak Baharia aka Gobby aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu. Wenye kumbukumbu, watamkumbuka Gobby katika wimbo wake wa Kuzaliwa kwa Chama kipya, tar 5/2/77.

''Orchestra Makassy, the brainchild of Mzee Makassy himself, has taken audiences all over East Africa by storm. Their blend of pure Kiswahili and Zairois rhythms have captured the hearts of music lovers who have constantly demanded this set of Makassy's greatest hits.
The popularity of the group has not come without its share of disappointments and it has entailed great work from Mzee Makassy. The group would perhaps have been a household name sooner had it not been for the unexpected and tragic knifing of the lead singer Isiak Baharia, alias Gobby. This sad event caused great turmoil but from the ashes of the former group Mzee Makassy moulded his present band with the considerable help of Rammy Ongara and Fan Fan from OK Jazz. These were then supplemented with Aimala Mbutu, Simaroo on Solo guitar, Kadesi on Bass, Batty on Rhythm and Adam Seye on Trumpet (also formerly with OK Jazz) amongst the others in the group.
Thus the Orchestra Makassy, whose emblem of the elephant and drum has become famous in such a short space of time, has brought some of the finest musicians together from the brink of disaster to the top of the charts. Here now are Makassy's greatest hits - the first set of many from this fine band."

source; worldservice: The brink of disaster

...nahitimisha na nyimbo hii. Wimbo ambao mashairi yake nayakumbukia mara kwa mara maishani mwangu.
Nyimbo nyingi za Remmy Ongala zimeacha mark kwenye maisha yangu. Ikiwemo "NARUDI NYUMBANI", ambayo ukiwa ughaibuni inafariji sana, hasa inapopigwa kwenye kumbi za burudani.

 
Last edited by a moderator:
RIP Dr. Remmy,
Utakumbukwa kwa mengi katika tasnia ya music. Mimi binafsi nilipendezwa na uwazi aliouonesha katika kupiga vita ukimwi (Wimbo wa mambo kwa soksi) katika kipindi ambacho watanzania tulikuwa tunaogopa kuongelea ngono hadharani.
 
Last edited by a moderator:
GC....Jamaa kanikumbusha mbali sana,mwaka 1990 wakati Dk.Remmy kwa kushirikiana na Cosmas Chidumule na kundi zima la wana Talakaka 'Bongo Beats' Super Matimila walipotoa kibao kilicholeta mtafaruku cha 'Mambo kwa soksi' ambacho kilikuwa kinalenga kuwahimiza watu kutumia condom kujikinga na ukimwi lakini kikaonekana kama kinachochea ngono zaidi....Siukumbuki vizuri huu wimbo ila nayakumbuka baadhi ya maneno kama:

'E bwana leo kuna mechi,mechi inachezwa wapI?,inachezwa uwanja wa kitandani,ni mechi kati ya timu baba na timu mama,timu baba inacheza na soksi na timu mama inacheza pekupeku'............Dah

Kiitikio cha wimbo huu nakumbuka kilikuwa hivi:

'Ukimwi ni hatari jama,ukimwi ni hatari jama........Naogopa mambo,mambo mambo(kwa soksi),jamani mambo(kwa soksi),ya siku hizi(kwa soksi)...................Dude hilo(kwa soksi),likuvaa(kwa soksi),utaondoka(kwa soksi),na kil mbili(kwa soksi)......Haya maneno ya kwenye mambano kwenye kiitikio yaliimbwa na Dk.Remmy na mengine yaliimbwa na Chidumule............

Nakumbuka wimbo mwingine uliokuwamo kwenye albamu hii iliyozua utata mwaka 1990 ni nyimbo ambayo nimesahau jina lake ila ulikuwa na maudhui ya mtoto kumlalamikia baba yake ambaye ametelekeza familia na kwenda TANDALE kwa nyumba ndogo......Baadhi ya maneno ya wimbo huo ni haya hapa chini

'Amepata mama mwingine tena mama huyo(yupo Tandale),fundi wa kupika ugimbi(na Gongo) mama huyo na wangoni kwa ugimbi(ndio wenyewe) si mnawajua jama,baba ameshapotea'......Haya maneno ya kudakia ya kwenye mabano pia yaliimbwa na Dk.Remmy...............

Hakika kati ya watu watakaomkumbuka sana Dk.Remmy mmojawapo ni swahiba wake Cosmas Thobias Chidumule
 
My most favorite songs of Dr Remmy are these Two. Ni miaka mingi kidogo kuna baadhi ya maneno nitakuwa nimechanganya ama kusahau:

Dunia

Yote utakayofanya ukimtendea mwenziox2
ubaya ee utalipwa hapa ulimenguni,
Kwa mungu hatuonani,
Kwa Mungu hatupajui,
Kwa Mungu kuna Giza,
aee dunia, jamani dunia, inasikitisha dunia, wandugu dunia,

Ukinipiga leo kesho utapigwa na wengine,
ukinitukana nawe utatukanwa,
ukilangua jua utakamatwa,
kuna wengine watu hudhulumu wenzio wao,
kwa uongo wao, kwa maneno yao, kwa rushwa zao, kwa vyeo vyao kazini, kwa ujanja wao oo dunia,
jamani dunia, inasikitisha dunia, wandugu dunia,

Anakukopa pesa na anakuahidi nitakulipa siku fulani,
siku ikifika humuoni,
na siku ukimuona anakueleza matatizo ya uongo, matatizo ya uongo, ya uongo,matatizo ya uongo,
kukopa harusi kulipa matanga,
kukopa asali kulipa shubiri

jamani dunia, wandugu dunia,
dunia kwa nini waleta vifoo, dunia kwa nini haupendi walimwengu,
Kwa nini nife x2 dunia,
niache mke wangu,
niache mali yangu,
niache nyumba yangu,
aeee dunia oo ooooooooo,

hii ni miongoni mwa nyimbo Classic za Dr Remmy.
 
Halafu kuna hii Classic nyingine:


Tembea Ujionee

Natembea popote unapokwenda,
iwe usiku ama mchana mbele yetu kuna mwanga wa maisha,
Natembea popote lakini wajua pa kula pa kulala,
maisha ya mtu tumefautiana na tumezaliwa mahali mbali mbali,

Mtu anaweza kufanana na nduguye sio shangazi wala mjomba,
labda pengine rafiki yake,
mkifanana kwa sura mwendo tofauti,
mkifanana kwa mwendo sura tofauti,
mawazo mbali mbali,
tabia mbali mbali,
mavalio mbali mbali,

Tumefikiria kuimba hivi kutokana na kutembea sehemu mbali mbali,
kutofautisha tabia na vitendo vya huyu vipi na kile vipi,
huyu bwana vipi na yule bibi vipi,
Hii shati vipi na suruwali vipi,
hii soksi vipi na kiatu vipi,

Kila mtu na kila sehemu vinatofautiana,
hauwezi kufananisha Morogoro na Darisalama,
tembea ujionee usingoje kuambiwa,

(chorus ya akina Skassy kasambaula na wenzake)
Tembea ujionee usingoje kuambiwa,
Duniani kuna mengi yote yanakusubiri x2

(Dr Remmy)
Tembea mama tembea bibi ii,
Tembea uone mambo,
tembea ushangae,
tembea upande mabasi,
tembea tembea tembea mama tembea bibi oo x2
oo tembea oo mama,

tembea oo mama
(oo tembea bibi oo)
tembea oo bibi oo
(oo tembea uone mambo)
tembea uone mambo



tembea oo mama
 
Halafu kuna kibwagizo cha AMISA ambacho kila ninapokisikia hujikuta nikitabasamu mwenyewe:


(Remmy) Hodi hodi jamani humu ndani hodiii,
(Binti) kariibu,
(Remmy) Wewe ni mke wa nani kwenye nyumba hii,
(Binti) mimi mke wa fundi koroboi pale muembeni,
(Remmy) yule mwenye anakaa banda la uani huku,
(Binti) mmmmmm!
(Remmy) Mume wako ameenda wapi?
(Binti) Mume wangu ameenda gerezani kutafuta makopo,

(Remmy) Hivi we mtoto unajua mi ni nani?
(Binti) hivi we ndio nani?
(Remmy) Mi ndio baba mwenye nyumba hii!
(Binti) mmmmmm, Shikamooo!
(Remmy) Marahaba marahaba,mpaka nikuambie mi ndio mwenye nyumba ndio unaniamkia? haya mama marahaba!


(Remmy) Hivi we mtoto umetoka wapi
(Binti) mimi nimetoka Dodoma
(Remmy) umetoka Dodoma? we Mgogo?
(Binti)Aka! Mi sio Mgogo mi Mkaguru


(Remmy) Sasa we mtoto!
(Binti) mmmm?
(Remmy) Unajua ukifika Darisalamu ni lazima utuone watu kama sisi utapata kila kitu bure! Au Vipi?
(Binti) basi nitasubiri mume wangu akija nimuambie tumepata chumba cha bure!
(Remmy) Utasubiri mume wako akija umumbie ya kwamba Mzee Chumaulete ametupa chumba cha bure? basi akija fungasheni na ondokeni, Ondokeeni!
(Binti) Baaasiii!

Huu ulikuwa ni Ubunifu mkubwa wa Dr Remmy kueleza kwa kifupi tu matatizo yaliyokuwa yanawapata wapangaji wenye wake na vipato vidogo kutoka kwa baadhi ya wababa wenye nyumba. Sikumbuki yule binti aliyekuwa aliyemuitikia Dr Remmy aliishia wapi kwenye ulimwengu wa Muziki.
 
RIP Remmy. My favorite was Sauti ya Mnyonge (The voice of the underdog). Wimbo umejaa ujumbe mzito sana, hasa hasa kwa watu waliyopewa dhamana.
 
R.I.P
Wadau kesho mjitokeze atazikwa makaburi ya sinza yako karibu na kituo cha kwa REMMY
 
Halafu kuna kibwagizo cha AMISA ambacho kila ninapokisikia hujikuta nikitabasamu mwenyewe:


(Remmy) Hodi hodi jamani humu ndani hodiii,
(Binti) kariibu,
(Remmy) Wewe ni mke wa nani kwenye nyumba hii,
(Binti) mimi mke wa fundi koroboi pale muembeni,
(Remmy) yule mwenye anakaa banda la uani huku,
(Binti) mmmmmm!
(Remmy) Mume wako ameenda wapi?
(Binti) Mume wangu ameenda gerezani kutafuta makopo,

(Remmy) Hivi we mtoto unajua mi ni nani?
(Binti) hivi we ndio nani?
(Remmy) Mi ndio baba mwenye nyumba hii!
(Binti) mmmmmm, Shikamooo!
(Remmy) Marahaba marahaba,mpaka nikuambie mi ndio mwenye nyumba ndio unaniamkia? haya mama marahaba!


(Remmy) Hivi we mtoto umetoka wapi
(Binti) mimi nimetoka Dodoma
(Remmy) umetoka Dodoma? we Mgogo?
(Binti)Aka! Mi sio Mgogo mi Mkaguru


(Remmy) Sasa we mtoto!
(Binti) mmmm?
(Remmy) Unajua ukifika Darisalamu ni lazima utuone watu kama sisi utapata kila kitu bure! Au Vipi?
(Binti) basi nitasubiri mume wangu akija nimuambie tumepata chumba cha bure!
(Remmy) Utasubiri mume wako akija umumbie ya kwamba Mzee Chumaulete ametupa chumba cha bure? basi akija fungasheni na ondokeni, Ondokeeni!
(Binti) Baaasiii!

Huu ulikuwa ni Ubunifu mkubwa wa Dr Remmy kueleza kwa kifupi tu matatizo yaliyokuwa yanawapata wapangaji wenye wake na vipato vidogo kutoka kwa baadhi ya wababa wenye nyumba. Sikumbuki yule binti aliyekuwa aliyemuitikia Dr Remmy aliishia wapi kwenye ulimwengu wa Muziki.

Dah Babadesi umemaliza kila kitu mkuu mwenzangu...
 
Back
Top Bottom