Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,715
Mungu hahusiki jamani, hebu someni vizuri kitabu cha Ayub mtaelewa alisema maneno hayo bila ujuzi bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea kati ya Mungu na Shetani na isitoshe katika Ayub sura za 42 alitengua usemi huo na yale yote akidhani Mungu ndiye alikuwa akimtendea. Wachungaji walitudanganya, tukafikiri Mungu anahusika katika vifo vinavyotokea. Wengine wanasema "Tulimpenda marehemu lakini Mungu kampenda sana au Mungu anavuna alichopanda. Lakini unaweza kuangalia matokeo ya vifo kwa mfano. Unaaenda kutembeza umalaya unakumbana na virus vya ukimwi baada ya muda unakufa, Mungu ndiye aliyekutuma ufanye umalaya??? si alisema mzinzi hataurithi ufalme wa Mungu sasa atakutumaje. Jambo tunapaswa kujifunza ni kwamba Mungu karuhusu kifo cha mwanadamu lakini hasababishi kifo hicho, kuna tofauti kati ya kurusu na kusababisha. Ukitaka maelezo zaidi soma kitabu cha Mhubiri.
Hivyo usemi huo tunaendelea kuutumia kimakosa. Mimi namuomba Mungu aipe nguvu za familia ya mzee Remmy kukabiliana na msiba huu kwani ni kipindi kigumu kwao cha kumpoteza mpendwa wao. Na aiangalie familia hiyo ili iendelee kupata mahitaji yake ya kila siku. Amen.
Duuuuu!
Huyo Mungu unayemwamini ni mkali kweli!!!!!
Ni namna tu ya kuongea kuwa Mungu anawaita kwake watu toka Dunia hii. Wala kifo mbele ya Mungu si adhabu bali ni kuhamisha watu toka Maisha ya Duniani na kuwaweka kwenye umilele, kadiri ya matendo yetu hapa duniani: ama raha ya milele au kuangamia.
Hawajakosea hata kidogo waliosema hivyo kwani Maisha yetu yamo mikononi mwa Mungu. Mungu ndiye mtoa uhai naye pia ndiye huturejesha kwake.