R.I.P. Dr. Remmy Ongara

R.I.P. Dr. Remmy Ongara

Siku ya kufa, KIFO, Narudi nyumbani
...mambo kwa soksi (ulipigwa stop)
But the guy was Genius R.I.P
 
kifo ndio mwimbo ambao naukumbuka, ulikuwa mzuri na umepangika,RIP DR REMMY ONGARA
 
Namkumbuka kwa wimbo wa Mwanza na Nalia Mume.
Mimi na Mume wangu tulianza nae Mwanza,
Harusi ikafanyika Mwanza
Baada ya siku chache, tukaja nao ko Darsalama
Naacha kwetu kwa baba na mama na furaha yote....
......
Baada ya siku chache, simwoni mume nyumbani...
......
Wanaume wa sasa hawana uaminifu,
Huwadanganya wana wa wenzao

mkuu umenikuna mnooooo huo wimbo ukipigwacbeats zake ni km umetungwa leoooo
 
Ameimba nyimbo nyingi sana nzuri ila KIFO HAKINA HURUMA jamani umefunika
 
KIFO OOH KIFO HAKINA HURUMA!!!!!!

Kifo kifo siku yangu ikifika kifo nitaarifu mapema , niage familia, wanangu,
Mke wangu, pesa zangu nizigawanye zilizobaki nizile mwenyewe, kifo nakusubiri kwa hamu,
Kifo nakwenda dukani kariakoo nanunua shati jipya, suruali mpya, koti jipya, tai mpya, soksi mpya,
Kiatu kipya, kifo nitanunua sanda yangu mwenyewe, kifo nitawalipia watu wanichimbie kaburi yangu ningali hai
Sipendi kuzikwa na mtu nitajizika Mwenyewe kwangu hakuna matanga, hakuna kilio, hakuna uji.

Kifo nakwenda breweries nanunua kreti 20, mwarubaini kwa wingi,
Michemsho kwa wingi, migebuo kwa wingi, wanzuki kwa wingi chimpumu kwa wingi,
Kaya kwa sela, kifo nitafanya pati nitaita watu binafsi wote, marafiki zangu wote,
Kifo niambie tukutane wapi hata Muhimbili ntakwenda mwenyewe kwa miguu
 
Muziki asili yake wapi? is among the best for me
 
naukumbuka wimbo wa mambo kwa socks.
sukari yetu imeingia sumu
sukari imeingia mafuta ya taaa
RIP
 
KIFO OOH KIFO HAKINA HURUMA!!!!!!

Kifo kifo siku yangu ikifika kifo nitaarifu mapema , niage familia, wanangu,
Mke wangu, pesa zangu nizigawanye zilizobaki nizile mwenyewe, kifo nakusubiri kwa hamu,
Kifo nakwenda dukani kariakoo nanunua shati jipya, suruali mpya, koti jipya, tai mpya, soksi mpya,
Kiatu kipya, kifo nitanunua sanda yangu mwenyewe, kifo nitawalipia watu wanichimbie kaburi yangu ningali hai
Sipendi kuzikwa na mtu nitajizika Mwenyewe kwangu hakuna matanga, hakuna kilio, hakuna uji.

Kifo nakwenda breweries nanunua kreti 20, mwarubaini kwa wingi,
Michemsho kwa wingi, migebuo kwa wingi, wanzuki kwa wingi chimpumu kwa wingi,
Kaya kwa sela, kifo nitafanya pati nitaita watu binafsi wote, marafiki zangu wote,
Kifo niambie tukutane wapi hata Muhimbili ntakwenda mwenyewe kwa miguu

Dah kweli kifo ni kiboko yao
 
athumani eeeh vipi mambo valuvalu

Umenioa bado ningali kijana
Ukipata chungu kipya usitupe cha zamani
Aathumani eeeeeh


Athumani eeh samaki hapiti chambo
Kila apitae Athumani ashangai
Kusemasema sijui kupigana sintoweza
Athumani eeeeh
 
Duh! jamaa ana wimbo mmoja sijui jina lake lakini ni wa promotion ya condom, baadhi ya maneno yake " mambo mambo kwa soksi....shangazi na mjomba kwa soksi...." humo ni kufuru tu....

Hapo ndio sura halisi ya huyu mkongo utaielewa
 
Namkumbuka kwa wimbo wa Mwanza na Nalia Mume.
Mimi na Mume wangu tulianza nae Mwanza,
Harusi ikafanyika Mwanza
Baada ya siku chache, tukaja nao ko Darsalama
Naacha kwetu kwa baba na mama na furaha yote....
......
Baada ya siku chache, simwoni mume nyumbani...
......
Wanaume wa sasa hawana uaminifu,
Huwadanganya wana wa wenzao

Heshima kwako Pasco,

Duh umenikumbusha mbali sana enzi za radio mkulima.Dr aliimba nyimbo zenye hisia kali sana ebu fikiria muda aliotunga hadi leo unatamani kuusikiliza tofauti na muziki wa kizazi kipya.
 
NALILIA MTOTO

Nakulilia Mola wangu weee,
Nakuwaza Mola wangu wee,
Yalonipata makubwa naona balaa,
Wala hamu sina x2

Wenzangu wana watoto,
Mimi sina hata wa dawa eeeh,
Niwatumapo wana wa wenzangu,
Mama zao hunisimanga x2

Nalia nasikitika bahati sina,
Kwa waganga wa kila namna nimefika ni bure tuuuu,
Hospitali za kila namna nimekenda ni bure tuuuu,
Mola nimemuomba na sadaka nimetoa ni bure tuuuu,

Mola, Mola, Molaaa eeeh,
Mola eeeh nataka mtoto,

Mola Mola, Molaa eeh,
Mola eeh, nalilia mtoto

Mtoto angelikuwa ni nguo ningenunua,
Mtoto ni mtoto kwa mama hakui,
Hata angelikuwa kilema au mbaya kama Remmy ni mtoto tu!

Mola Mola, Mola eeeh....
 
ndugu muacici, nina neno kidogo na ile comment ya kitabu cha ayubu. tafadhari zingatia kuwa kitabu cha ayubu si cha historia au mambo ya nyakati (matukio/chronicles).......... ni kitabu cha utenzi kinachokusudia kuibua asili, sifa na tabia ya Mungu.......... simulizi la shetani kama ulivyolinukuu liko katika prologe ya hicho kitabu (3-42:6). ........ na kibwagizo chake kiko kwenye epilogue yake (42:7 hadi mwisho)............ ila maudhui ya kitabu chenyewe yako sura za 3-42:6 na yameandikwa katika mtindo wa utenzi unawahusu ayubu na marafiki zake watatu (elifaaz, zofari na bildad) mwishonimwishoni anaibuka kijana mmoja mdogo lakini mwenye hekkima kubwa (elihu) kushinda hata ya ayubu na rafiki zake wote. anaongea mambo yanayokaribia kufanana na ya Mungu mwenyewe na hatimaye anasababisha ayubu akiri alipopotoka na kutubu.......... tafadhari soma taratibu na Mungu akusaidie kuelewa nasema nini na kama utapata tatizo, nitafurahi kukusaidia........... unaweza kutumia PM........... ubarikiwe..........

RIP Dr Remmy..............

Akili Kichwani nashukuru kuwa umekiri kuwa Ayub alikiri alichokuwa akikizungumza mwanzoni. Lingine unapaswa kufikiri Mungu ni Upendo hivyo hawezi kukuulia kijana wako. Tusimsingizie sio muuaji. Nitamtetea hadi mwisho kwa kuwa nimejifunza sifa kuu za Mungu. Kasome kitabu cha Muhibiri kitakupa insight.
 
Mariamu


ataka yote akosa yote
apita ahangaika asijue la kufanya ... asijue la kufanya
mshika mawili yote yamponyoka
apita akebakeba asijiue la kujitetea
mmmhhh mapenzi yawaka moto
naitika nilikukosea sasa nihurumie
si ninafikiri zaidi kuliko wewe
nakonda kama mnazi kwa mapenzi nilionayo
nilalapo nakuota mchana kutwa sili
moyo wanichechemea mwili damu hukauka
penzii eh ..... mmmh penzi eh x 2

nasumbuka kwako unionavyo moyo wangu
wewe ndio dawa yangu
Maraimu wangu
Tanga mbali
waja leo wondoka leoo
waja leo warudi leo

Mariamu bibi
mwenzenu sina pumuzi kujizuwia siwezi ohhh
mwanaume barabara kazi ya mume kwa mke
neno ya mke chumvi kwa mumewe
neno ya muke kachumbari kwa mumewe
penzi oh penzi likamung'uma he heh heh

likamung'uma hen heh heh .... mmhhhh
mdundiko, mdundiko ........ waaaaaa
mdundiko ...... waaaa
 
Muziki asili yake wapiie eh
Muziki ni wa nani eeh
Muziki hakuna mwenye, muziki ni amani moyoni eeeh!
Usinione nikiimba ukazani ninayofuraha, kumbe ninayo huzuni moyoniii eh
 
Back
Top Bottom