R.I.P mwanaJF!

R.I.P mwanaJF!

Kwa kweli yanatisha haswa, kuna umuhimu wa watu tunaofahamiana kuwa tunajuliana hali,ili linapotokea la kutokea unakuta mtu mmoja ana taarifa za huyo mtu, ulijaribu kumwuliza crashwise kama alikua anajua jina alilokuwa anatumia huku JF?
Crashwise pia alikuwa anafahamiana sana na huyu member kimtaani, na anasema alikuwa ni mtu wa mabandiko sana, karibu kila siku yuko online!..Lakini anasema hawakuwahi kuulizana ishu ya ID kwa matumaini ya kuwa huenda watajuana baadaye!. Chelewa chelewa......!
 
Mmhh hivi mods hawawezi kutusaidia tujue ID yake?
 
Kila nafsi itaonja mauti, Inna Lillah Wainnailaih Raj'un, R.I.P Abuu
 
Mheshimiwa Regia,
Kwa sisi tunaojuana hakuna aliyeenda kunako mazshi yake, labda basi kama kuna aliyeshiriki amekalia kimya jambo zito hili!
Nawasifu sana watu kama wewe ambao mnatumia majina yenu halisi...Kuna advantage ambayo wengi wetu tunakuwa wazito kupokea kutokana na aidha kurithi tu hali hiyo, au kutokuwa na uhakika WA source za yale tunayobandika hapa...

Hii kitu imenigusa sana ?Mwenzetu mezikwa bila wanafamilia wa JF kuwa na habari.Tunapata habari wiki tatu baadaye.Inahuzunisha.Kuna mtu aliwahi kuanzisha sredi huko nyuma akishauri watu kuwaeleza rafiki zetu wa karibu ID zetu ili linapotokea lolote basi tupashane habari.Lolote laweza kuwa zuri ama baya mfano harusi,au shughuli yeyote ile,kuugua kama ilivyotokea kwa Lunyungu na hata msiba.Hii inasaidia sana kwa kweli.Si lazima utumie jinalako halisi lakini angalau watu kadhaa wakufahamu kama baadhi yetu tunavyofahamina.

Ila ni kwakuwa jina lake halisi linafahamika basi itabidi uongozi JF utake trouble ya kuagalia emailadress yake na kufahamu alikuwa natumia jina gani.With teknolojia tuliyonayo tutapata tu habari..
 
Crashwise pia alikuwa anafahamiana sana na huyu member kimtaani, na anasema alikuwa ni mtu wa mabandiko sana, karibu kila siku yuko online!..Lakini anasema hawakuwahi kuulizana ishu ya ID kwa matumaini ya kuwa huenda watajuana baadaye!. Chelewa chelewa......!

Hivi bro kuna yule member ulienda kumwona njiro wakati fulani alikua mgonjwa hivi yupo au nae alishatangulia mbele ya haki?
 
Rest in Peace Mkuu. Kwa kweli hili ni tatizo kubwa sana na linahitaji ufumbuzi. Bado sijaona jinsi gani hili tatizo linaweza kupatiwa ufumbuzi. nafikiri itakuwa juu ya individuail member mwenyewe kama anataka kutumia username au jina kamili. Labda wakati wakati wa kujisajili members wajulishwe faida na hasara za kutumia usernames au majina kamili? Ni suala gumu kwa kweli.

Kama alivyosema dada Regia hapo juu kama mtu wa karibu akijua ID yako, itasaidia kwa kiasi fulani. Lakini still hili linategemea unamtrust vipi huyo mtu. Na jinsi sie wanadamu tunavyobadilika kama upepo, unaweza ukamtrust mtu leo, kesho kutwa anakugeuka. But we still need to think how to overcome this problem.
 
yeye mbele sisi nyuma, mungu aiweke roho yake mahalim pema peponi
 
Sababu ambayo inatufanya watu kutumia ID za anonym ni kubandika hapa habari ambazo hazina ukweli au uchunguzi, au za ugombanishi, au za kuwasema watu tunaokaa nao nyumba moja etc!

Ongea ukweli mtupu uweke jina lako!
 
Hivi wakati ule mnafanya vikao vya safari hakuwahi kuja? Sasa kaka tufanyeje kwenye hili swala la usiri? hivi wakati mtu anajiunga na JF si kuna mahali information zake zinakuwepo au?

Poleni Msindima kwa msiba huu.
Vp taratibu za mazishi?
 
Poleni Msindima kwa msiba huu.
Vp taratibu za mazishi?

Mazishi sikushiriki mimi mwenyewe nimepata taarifa leo tena baada ya kusoma huku Jf ikabidi nimwulize PJ nani alimpa hizi taarifa, nikawasiliana na huyo jamaa ndo akaniambia ni kweli jamaa alipatwa na mauti tar 24, kuuliza ofisini nao wananiambia kuwa walipata taarifa tar 24.
 
Ok poleni jamani
 
Sababu ambayo inatufanya watu kutumia ID za anonym ni kubandika hapa habari ambazo hazina ukweli au uchunguzi, au za ugombanishi, au za kuwasema watu tunaokaa nao nyumba moja etc!

Ongea ukweli mtupu uweke jina lako!

Lakini pia wapo wale wanaopenda kuongea ukweli bila kutumia majina yao halisi. Actually, wanaongea ukweli wanaweza kuwa victims zaidi ya wale wanaobandika habari ambzo sio za ukweli. Kama ukinizushia habari za uongo unafikiri nitamind? Ila ukiweka za ukweli ndio pale watu wanapoanza kutafutana.
 
Sababu ambayo inatufanya watu kutumia ID za anonym ni kubandika hapa habari ambazo hazina ukweli au uchunguzi, au za ugombanishi, au za kuwasema watu tunaokaa nao nyumba moja etc!

Ongea ukweli mtupu uweke jina lako
!

RIP
Mkuu wewe hilo ni Jina Lako?
 
Ooh! Habari ya huzuni sana! Roho yake ipumzishwe kwa amani!
 
Back
Top Bottom