Radio Free Afrika watakiwa kujieleza kwanini wasiadhibiwe kwa kurusha kipindi cha 'Amka na BBC' bila mizania

Radio Free Afrika watakiwa kujieleza kwanini wasiadhibiwe kwa kurusha kipindi cha 'Amka na BBC' bila mizania

Hahaha...kama uliambiwa Taifa ni wewe na mmeo ulidanganywa, hupendi kitu the majority wanapenda na huko na amani nacho dawa ni kuhama nchi, hiyo ndo demokrasia, majority rules, kama huko na uhakika sana October sio mbali, JPM hatopata chini ya 90% ya kura zote.
Ushindi ni lazima tunajua Kwa nguvu ya dola lakini mtambue tu uchaguzi huu utamtia doa rais magufuri hadi anakuja kutoka madalakani mengi tutayasikia yote aliyoyaficha Kwa kipind cha miaka 5 wanainch wanataka kuyasikia kwanini mtumie nguvu kubwa kuzuia
 
Labda wahusika wa maswala ya ulinzi wa Tanzania wamejifunza huko kwao mabeberu wanavyoweza punguza hathari zinazotokana na media kwenye kuhatarisha amani na umoja wao wakati sisi huku wanataka media zetu zifanye kazi kiholela na kuatarisha usalama wetu.

Narudia tena, madictator wote huwa wanaingilia vyombo vya habari, ili kutangaza watakayo na kuzuia washindani wao wa ukweli.
 
Issue sio kupost bali unapost kitu gani? Na outcome zake ni zipi?
Joselela, mlitaadharishwa mapema!!. Wakitumaliza sisi .......

Tanzania ya Mwl ilisimama kuyakemea mataifa yaliowafanya wananchi wao namna hii. Leo tumekuwa wa kunyoshewa. Naamini hata mashabiki wa huko hamfurahii haya .
 
BBC kwa mara ya kwanza toka nimezaliwa inakwenda kupigwa marufuku sijajua kwa nini huu utwawala licha ya kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati kabla ya wakati,kukusanya kodi kuliko serikali zote,kujenga miundombinu kuliko serikali zote,kumaliza ufisadi kuliko serikali zote bado wanakuwa waoga wa chama dhaifu na kilichojifia kama CHADEMA
Tena imehurumiwa sana vile haijafungiwa kitambo, yule kilaza wao Samwel Awami anojikuta leo Muzungu na elimu yake ya taabu ya Umoja Sekondari amekuwa akikiuka miiko kila uchao na anafanya kwa maslahi ya mabwana zake, mtafurahi.
 
TCRA imekituhumu kituo cha utangazaji cha RFA kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji kupitia kipindi cha 'amka na BBC' kwa kurusha maudhui bila kuzingatia mizania ya habari walipokuwa wanamuhoji Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu juu ya viongozi wa chama hicho kutoshiriki kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa hayati Benjamin Mkapa.

TCRA imesema mtangazaji wa kipindi aliruhusu kurushwa habari iliyoegemea upande mmoja kwa Lissu kutoa tuhuma na kulalamika kuwa serikali ilimnyima nafasi ya kutoa heshima za mwisho bila kumtafuta msemaji wa serikali ili aweze kutolea ufafanuzi tuhuma hizo.

RFA wanatuhumiwa kukiuka kanuni Na. 15(2)(b) na (c) na 16 za mawasiliano ya kielektroniki na Posta(Maudhui ya Utangazaji na Televisheni) 2018.

Saa 5 asubuhi ya tarehe 10 Agosti, 2020 itakuwa ukomo kwa uongozi wa RFA kufika ofisi za makao makuu ya TCRA zilizopo Dar es Salaam kutoa utetezi wao katika shauri dhidi yao wa kimaandishi na kufika mbele ya kamati kujieleza kwanini kituo chao kisichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka kanuni za huduma ya utangazaji.

Harafu nikisikia watu wanasema Huyu jamaa ni Raisi wa wanyonge,huwa nawaona Kama vichaa,
Vyombo vya habari vyote kadhibiti,ataki wapinzani wasikike,
 
Acha tu, inabidi wanajf tuanze kuambiana ni mtandao gani tutahamia wakitupiga pini. Nakumbuka mara ya mwisho walivyoleta mizengwe tulihamia Kenya Talk.
Tutahamia huko tena.
 
Mkumbuke tu, vyombo vya habari hasa vya nje ya nchi ndio huwa chanzo cha machafuko na kutoweka kwa amani katika mataifa mengi duniani hasa Africa, hii ni hatua nzuri kudhibiti mitafaruku inayotarajiwa kutokea...

Na tunaomba serikali ifungie na mitandao ya kijamii hasa Facebook na Twitter.

Tangu tumepata uhuru mbona havijawahi kuleta machafuko siku zote machafuko hutokana na ukandamizaji wa seriakali zilizo madarakani siyo vyombo vya nje. Wakati utaongea tu ikiwezekana wafute vyombo vyote binafsi wabakize TBC hakuna shida yoyote maisha yataendelea tu.
 
Hakuna kaburi wala ujinga gani, we unamuitaje kichaa mmoja ambaye anatapika utumbo bila mtu wa ku respond?? Huyo alisema kuna corona hawezi kufika mahakamani au kurundikana na watu, huyo huyo alipokewa na watu na wakasakata rumba na kunywa ma konyagi mpaka asubuhi, huyo huyo akataka kwenda kurundikana na sisi pale uwanjani bila kukumbuka kama alikuja na libarakoa lake akalivua, huyo huyo alitaka kiprotokali eti awe wa mwisho kuingia uwanjani baada ya mhe Rais !! Yeye ni nani nchi hii?? Hatukubali u.t.a.a..hi.r.a wake aupeleke huko, na waliompa airtime wachukuliwe hatua kali
CCM mjiandae kwa yajayo, mmefanya vibaya sana mkifikiri watu ni wajinga sasa msubiri hukumu yenu October.
 
Hii nchi iko chini ya utawala wa kishamba sana, huu ubabe peleka nyumbani kwa familia yako.
Ujinga tu! Nchi gani ambayo haina mizania ya utoaji habari? Tatizo ni watu kama wewe na wenye waandishi Kanjanja. Vijana wa BBC nao hoi kuna wakati wanakuwa mashabiki wa habari za nyumbani bila kuheshimu sheria.
 
Ushindi ni lazima tunajua Kwa nguvu ya dola lakini mtambue tu uchaguzi huu utamtia doa rais magufuri hadi anakuja kutoka madalakani mengi tutayasikia yote aliyoyaficha Kwa kipind cha miaka 5 wanainch wanataka kuyasikia kwanini mtumie nguvu kubwa kuzuia
Kitu gani tusichokijua? mnaosemea annual increment? kwani sisi watumishi hatujui maana ya kufunga mikanda? nchi hii sio yetu wafanyakazi pekee, kama hajaongeza mishahara na katuomba tufunge mikanda na tunaona pesa inakoenda kutumika ni kule ambako kunaenda kunufaisha watanzania wote ikiwemo wakulima, wafugaji na wafanyabiashara, haiendi mifukoni mwa wachache, sisi ni nani hata tusielewe kwamba haya yanayofanywa ni makubwa zaidi ya hizo nyongeza za mishahara kwa tabaka la wachache? Meli tutapanda sote, train tutapanda sote na umeme tutatumia wote, mahospitali, zahanati na vituo vya afya tutavitumia sote, keki hii ndogo ya Taifa lazima tuifaidi kwa pamoja, miaka yote hiyo hujapata sikia mkulima akiongezewa mshahara, wafanyakazi tumeelewa na tumefunga mikanda.
 
Kama unakaa nyumba ya kupanga, kwako, au kwa mtu jaribu kufuata taratibu za sehemu husika, jamii husika au wale wanao kutunza ukienda kinyume inakuwa ni uvunjaji wa taratibu za jamii husika ambazo zitapelekea kutokuwa na imani na wewe..

Always fata sheria na taratibu popote pale ulipo, ndio maana unavyodrive unafuata lami hauchepuki kuendesha korongoni, kwenye mchepuo unafuata,kuliko nyoka vivyo hivo sasa na katika serikali fuata sheria uishi kwa furaha na amani.
 
TCRA imekituhumu kituo cha utangazaji cha RFA kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji kupitia kipindi cha 'amka na BBC' kwa kurusha maudhui bila kuzingatia mizania ya habari walipokuwa wanamuhoji Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu juu ya viongozi wa chama hicho kutoshiriki kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa hayati Benjamin Mkapa.

TCRA imesema mtangazaji wa kipindi aliruhusu kurushwa habari iliyoegemea upande mmoja kwa Lissu kutoa tuhuma na kulalamika kuwa serikali ilimnyima nafasi ya kutoa heshima za mwisho bila kumtafuta msemaji wa serikali ili aweze kutolea ufafanuzi tuhuma hizo.

RFA wanatuhumiwa kukiuka kanuni Na. 15(2)(b) na (c) na 16 za mawasiliano ya kielektroniki na Posta(Maudhui ya Utangazaji na Televisheni) 2018.

Saa 5 asubuhi ya tarehe 10 Agosti, 2020 itakuwa ukomo kwa uongozi wa RFA kufika ofisi za makao makuu ya TCRA zilizopo Dar es Salaam kutoa utetezi wao katika shauri dhidi yao wa kimaandishi na kufika mbele ya kamati kujieleza kwanini kituo chao kisichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka kanuni za huduma ya utangazaji.

ukisikia "impunity" ndiyo hii sasa.

so very sad.

sidhani amani ya nchi hii itakuja kutoweshwa na fujo za barabarani au watu kuingia msituni au wapinzani au mabeberu.

amani ya nchi itatoweshwa na sheria mbovu na kandamizi kama hizi ambapo itafika mahala zitawachosha hata wananchi wa kawaida, na ndiposa lawlessness itakapofyatuka kama jini lililoachiliwa kutoka katika kichupa!
 
Tangu tumepata uhuru mbona havijawahi kuleta machafuko siku zote machafuko hutokana na ukandamizaji wa seriakali zilizo madarakani siyo vyombo vya nje. Wakati utaongea tu ikiwezekana wafute vyombo vyote binafsi wabakize TBC hakuna shida yoyote maisha yataendelea tu.
Serikali haingozwi kwa historia bali kwa kila kiashiria ambacho kinaweza kuhatarisha usalama na amani ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom