Radio Free Afrika watakiwa kujieleza kwanini wasiadhibiwe kwa kurusha kipindi cha 'Amka na BBC' bila mizania

Ushindi ni lazima tunajua Kwa nguvu ya dola lakini mtambue tu uchaguzi huu utamtia doa rais magufuri hadi anakuja kutoka madalakani mengi tutayasikia yote aliyoyaficha Kwa kipind cha miaka 5 wanainch wanataka kuyasikia kwanini mtumie nguvu kubwa kuzuia
 

Narudia tena, madictator wote huwa wanaingilia vyombo vya habari, ili kutangaza watakayo na kuzuia washindani wao wa ukweli.
 
Issue sio kupost bali unapost kitu gani? Na outcome zake ni zipi?
Joselela, mlitaadharishwa mapema!!. Wakitumaliza sisi .......

Tanzania ya Mwl ilisimama kuyakemea mataifa yaliowafanya wananchi wao namna hii. Leo tumekuwa wa kunyoshewa. Naamini hata mashabiki wa huko hamfurahii haya .
 
Tena imehurumiwa sana vile haijafungiwa kitambo, yule kilaza wao Samwel Awami anojikuta leo Muzungu na elimu yake ya taabu ya Umoja Sekondari amekuwa akikiuka miiko kila uchao na anafanya kwa maslahi ya mabwana zake, mtafurahi.
 
Harafu nikisikia watu wanasema Huyu jamaa ni Raisi wa wanyonge,huwa nawaona Kama vichaa,
Vyombo vya habari vyote kadhibiti,ataki wapinzani wasikike,
 
Acha tu, inabidi wanajf tuanze kuambiana ni mtandao gani tutahamia wakitupiga pini. Nakumbuka mara ya mwisho walivyoleta mizengwe tulihamia Kenya Talk.
Tutahamia huko tena.
 

Tangu tumepata uhuru mbona havijawahi kuleta machafuko siku zote machafuko hutokana na ukandamizaji wa seriakali zilizo madarakani siyo vyombo vya nje. Wakati utaongea tu ikiwezekana wafute vyombo vyote binafsi wabakize TBC hakuna shida yoyote maisha yataendelea tu.
 
CCM mjiandae kwa yajayo, mmefanya vibaya sana mkifikiri watu ni wajinga sasa msubiri hukumu yenu October.
 
Hii nchi iko chini ya utawala wa kishamba sana, huu ubabe peleka nyumbani kwa familia yako.
Ujinga tu! Nchi gani ambayo haina mizania ya utoaji habari? Tatizo ni watu kama wewe na wenye waandishi Kanjanja. Vijana wa BBC nao hoi kuna wakati wanakuwa mashabiki wa habari za nyumbani bila kuheshimu sheria.
 
Kitu gani tusichokijua? mnaosemea annual increment? kwani sisi watumishi hatujui maana ya kufunga mikanda? nchi hii sio yetu wafanyakazi pekee, kama hajaongeza mishahara na katuomba tufunge mikanda na tunaona pesa inakoenda kutumika ni kule ambako kunaenda kunufaisha watanzania wote ikiwemo wakulima, wafugaji na wafanyabiashara, haiendi mifukoni mwa wachache, sisi ni nani hata tusielewe kwamba haya yanayofanywa ni makubwa zaidi ya hizo nyongeza za mishahara kwa tabaka la wachache? Meli tutapanda sote, train tutapanda sote na umeme tutatumia wote, mahospitali, zahanati na vituo vya afya tutavitumia sote, keki hii ndogo ya Taifa lazima tuifaidi kwa pamoja, miaka yote hiyo hujapata sikia mkulima akiongezewa mshahara, wafanyakazi tumeelewa na tumefunga mikanda.
 
Kama unakaa nyumba ya kupanga, kwako, au kwa mtu jaribu kufuata taratibu za sehemu husika, jamii husika au wale wanao kutunza ukienda kinyume inakuwa ni uvunjaji wa taratibu za jamii husika ambazo zitapelekea kutokuwa na imani na wewe..

Always fata sheria na taratibu popote pale ulipo, ndio maana unavyodrive unafuata lami hauchepuki kuendesha korongoni, kwenye mchepuo unafuata,kuliko nyoka vivyo hivo sasa na katika serikali fuata sheria uishi kwa furaha na amani.
 
ukisikia "impunity" ndiyo hii sasa.

so very sad.

sidhani amani ya nchi hii itakuja kutoweshwa na fujo za barabarani au watu kuingia msituni au wapinzani au mabeberu.

amani ya nchi itatoweshwa na sheria mbovu na kandamizi kama hizi ambapo itafika mahala zitawachosha hata wananchi wa kawaida, na ndiposa lawlessness itakapofyatuka kama jini lililoachiliwa kutoka katika kichupa!
 
Serikali haingozwi kwa historia bali kwa kila kiashiria ambacho kinaweza kuhatarisha usalama na amani ya nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…