Radio Free Afrika watakiwa kujieleza kwanini wasiadhibiwe kwa kurusha kipindi cha 'Amka na BBC' bila mizania

Radio Free Afrika watakiwa kujieleza kwanini wasiadhibiwe kwa kurusha kipindi cha 'Amka na BBC' bila mizania

Dawa ni kumwomba Mungu atuepushe na utawala huu aisee kwa style hii tutakuja kuwa na hali mbaya kwa kila nyanja
 
Wameambiwa na TCRA ni marufuku kwa vituo vya Radio na Tv za ndani kujiunga na hayo mashirika ya nje bila kupata kibali. Kazi kweli kweli, yaani ni pini kwa kwenda mbele kuelekea uchaguzi.
Huyu mtu atakumbukwa kwa lipi akifariki?
 
Mkumbuke tu, vyombo vya habari hasa vya nje ya nchi ndio huwa chanzo cha machafuko na kutoweka kwa amani katika mataifa mengi duniani hasa Africa, hii ni hatua nzuri kudhibiti mitafaruku inayotarajiwa kutokea...

Na tunaomba serikali ifungie na mitandao ya kijamii hasa Facebook na Twitter.
Sawa kabisa wafunge na ubalozi wa Marekani maana ndio washenzi kabisa wafunge pia misikiti na makanisa
 
Mkumbuke tu, vyombo vya habari hasa vya nje ya nchi ndio huwa chanzo cha machafuko na kutoweka kwa amani katika mataifa mengi duniani hasa Africa, hii ni hatua nzuri kudhibiti mitafaruku inayotarajiwa kutokea...

Na tunaomba serikali ifungie na mitandao ya kijamii hasa Facebook na Twitter.
Ndio tunakoelekea.
 
TCRA imekituhumu kituo cha utangazaji cha RFA kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji kupitia kipindi cha 'amka na BBC' kwa kurusha maudhui bila kuzingatia mizania ya habari walipokuwa wanamuhoji Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu juu ya viongozi wa chama hicho kutoshiriki kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa hayati Benjamin Mkapa..
Kura kwa Lisu tu
 
Zilitungwa na bunge Wakati Lisu akiwa mbunge na chadema wakiwa wabunge kwenye kipindi Cha Bunge la 2015-2020

Hapa CDM nawatetea huwa wanapinga kila kitu bungeni wasinge kubali sema wengi walisema ndiooo ikapita ili itunyoooshe wanyonge dah
 
Ee Mungu fanya jambo ili nchi uliyoiumba iwe na amani halisi.
 
Nani kakwambia wanadhibiti??? Ushawai jifungia ndani na paka alafu ukaanza kumpiga????

Ndo wanachokifanya magufuli na vyombo vyake. Majibu watayapata siku si nyingi.
Kwani wewe umenielewa vipi.? Naona umeniattack tu.
 
Hebu jiulize, hivi wakati Jiwe anawatuhumu wapinzani kuwa watavunja madaraja aliyojenga yeye iwapo wananchi watawapa kura na kuingia madarakani, je vyombo vya habari vilikwenda kuwahoji viongozi wa upinzani kabla ya kuzitangaza?

Hii nchi inakokwenda kwa sasa ni kubaya sana!
Narudia tena kwa msaada wa wale msioelewa, balancing ni kwenye mahojiano tu, narudia tena ni kwenye mahojiano tu siyo kwenye NEWS jamani!
 
Mkuu Tanzania si nchi ya kishamba Ila washamba ni hawa viongozi wetu wa awamu hii and we have all the power ya kuwatoa either kwa kura au kwa nguvu
Kabisa mkuu.... Umenena vema ila ushamba wetu ni pale tunapofumbia macho mambo yote machafu......

Lazima tuchukue hatua stahiki October 28
 
Korea kaskazini hii hapa... habari ziwe zakumsifu mwenye nyumba!!
 
Sasa sie wasikiliza BBC tutakuwa tunajiunga through which station?
Mamaee awamu ngumu
Wameambiwa na TCRA ni marufuku kwa vituo vya Radio na Tv za ndani kujiunga na hayo mashirika ya nje bila kupata kibali. Kazi kweli kweli, yaani ni pini kwa kwenda mbele kuelekea uchaguzi.
 
Back
Top Bottom