Radio Safina this is too much

shetani kazini, nenda na wewe kaanzishe wakwako kama unazani ni kazi rahisi
 
Kwa aliyeanzisha huu Uzi, na kila aliyechangia (Nikiwemo Mimi), Tujiulize Swali hili la Bonny Mwaitege...

"Utanitambuaje Kama nimeokoka?"
No one on earth anapaswa kusema ameokoka na bado anaishi, kuokoka ni pale itakopewa hesabu yako na mwingi wa rehema kwa huruma yake akaona unafaa kuingia peponi,
/mbinguni. Hii ndo definition ya kuokoka kwa upande wangu. Yani umeepuka kuingia motoni na kiungia peponi.
Lakn bado unaishi, unamkosea Mungu kwa mawazo, maneno na matendo bado hujaokoka
 
sasa kama ni uongo, mbona ninyi kina mama na wanawake ndo mnaongoza kudondoka kwa mapepo, makanisani mwao? na ndo huwa mnajaza makanisa yao.
 
Wajinga hawawezi kuisha Nchi hii,mwenzenu yupo kazini ninyi mnakesha bila sababu.
 
Acha kujitafutia laana bure wewe na kizazi chako chote kwa kuandika usivyovijua. Kwenye haya mambo ya rohoni wewe ni kipofu, so mengine yakupite tu.
 
Wokovu si dini, wala si Jambo jipya.

Wokovu ni Kuuacha utu wa zamani (Matendo yasiyo mpendeza Mungu, mfano Ulevi, Uzinzi, Uongo, Uuaji, Wizi, Lugha mbaya n.k), na Kumrudia Mungu na kuanza kufanya yaliyo kadiri ya maelekezo ya Mungu.

Wokovu ni neema tuipatayo kwa njia YA IMANI KUPITIA YESU KRISTO WA NAZARETH.. Sasa Kama mtu Hamuamini Yesu Kristo wa Nazareth Basi ni wazi kuwa bado hujafikiwa/hujaipata Neema hii..

UAMUZI unabaki kwako Sasa, Kuifuata neema hii tuipatayo kwa njia ya imani kupitia KRISTO Bwana wetu au Kubakia huko uliko (Ambako wewe unaona kunakufaa).. Ukiichagua neema hii Sawa, Ukibaki Uliko Pia Sawa.

Kuipata neema hii na kuiishi kikamilifu kimwili na kiroho basi wewe unayo nafasi ya kuurithi ufalme wa Mungu, lakini kuipata na kuyarudia maovu au kutoiishi sawasawa (Yani nusu kwa Yesu nusu unafuataa matendo na tamaa za Mwilini) Basi ni wazi kuwa huna nafasi katika ufalme wa Bwana, maana Mungu hapendi vuguvugu.. Chagua Sasa, Kuwa Moto au Baridi.

UAMUZI NI wako, njoo kwa Yesu au Ubaki huko uliko, Hakuna atakayekulazimisha.

Nisamehe Sana nimeandika mambo mengi, lakini yote ni katika kukuelezea juu ya wokovu/kuokoka... Sasa Basi naomba nitoe mjumuisho wa nilicho andika.

Ili uokoke, kwanza inakupasa kumuamini Mungu na Mwanaye Yesu Kristo ambaye kupitia huyo ndio utapata huo wokovu... Sasa Kama humwamini Kristo huwezi kuuamini wokovu.

Asante na Kwaheri.
 
Wewe huwezi kumzuia mwanamke kwenda kusali ataenda tu
Mimi nilimuona siku moja wife kwenye tv ya mchungaji moja uko kawe anamshukuru Mungu kwa kumaliza ujenzi nikanyamaza tu
Acha masihara bro
 
hv Shetani mmoja ndiye anafanya mishe mishe dunia nzima na hachoki au halali ?

kama ana wasaidizi wake anawaamrisha cha kufanya akiwa wapi ?
 
Haya makanisa ya Arusha yanawasulubisha Sana wa wanawake..
 
Ninamuamini aliyemuumba mimi na wewe na yesu (pbuh) . Ninamshukuru sana Mungu alienitoa nilipokua na kuniongoza kwenye njia sahihi na zaidi naomba aniongoze mimi wewe na wengine wote kwenye njia ya wale anayowaridhia na wala sio wale aliowakasirikia..
Audhubillah, ametakasika mno kuliko chchote na hana mwana.
 
Haya makanisa ya Arusha yanawasulubisha Sana wa wanawake..
Wengin watakuambia chuki za dini, lkn hukuti wakiwaambia hawa wanawake wa waheshimu waume zao kutwa kukaa huko safina j4 alhamis na jmos na wakirudi majumbani wanasikiliza redio usiku kucha huku wao wanaingiza pesa za hawa.
 
Aiseeee, we ni mkongwe. Mara nyingi huduma huanza vizuri ila baadaye huamka roho ya tamaa na hiyo ndio huwa mwisho wa huduma. Mungu awasaidie
Kwasasahivi hawamtumikii Mungu tena

Juzi walisema kuwa wana sadaka za getini na za ndani ya ukumbi na wataweka wanazoita ''Sanduku la Agano'' huko

Kweli haya ni maneno sahihi?

Wanauza mpaka maji, Fruto, vitambaa na kalamu eti wanasema kalamu ni za Israel na zina upako tofauti na kalamu za Tanzania.

SAFINA RADIO SASA MNATIA AIBU, MNAMWAIBISHA YESU KRISTO.
 
Acha kujitafutia laana bure wewe na kizazi chako chote kwa kuandika usivyovijua. Kwenye haya mambo ya rohoni wewe ni kipofu, so mengine yakupite tu.
Hahaha, haya matisho ndio huwa mnawapa wanawake na wengine wadhaifu wa kiroho ili mpate pesa zao.

Mimi nilihusika kuanzisha Safina Radio, nimehudumu pale for years ukitaka ushahidi utapata

Kuna mambo mengine sitaki kuyaweka wazi hapa kuhusu Daniel Lema na mama Hellen Lema kwa kuwastahi tu

Ila mkiendelea hivi nitaanza kuanika maovu yao.
 
Kiukweli mimi ni muumini mkubwa wa safina sasa hivi biashara imetawala jaman etii nunua CD hata kama huna tv etc ghaii??
Neno linahubiriwa na pesa inatafutwa so akili kumkichwa watu wasimame na neno ya mafundisho ya neno mambo mengine ya bongo movie waachane nayoo
 
Nilijua mtakuwepo na si bure nawewe in mnufaika wa sadaka za Safina.

Acheni wizi, mmegeuza ibada kuwa mradi wenu wa kupata pesa

Mnatangaza shuhuda za UONGO KABISA na kuigiza kunena kwa lugha

Mimi ninawafahamu sana ninyi tangu Safina inaanza
hayo umesema wewe,

mimi natoa shuhuda kwamba, nilishawahi kusali na kuomba pale safina na nilifanikiwa.

chamsingi waombapo na kusali huomba kwa jina la Mungu na hutumia neno takatifu

kilichobakia ni wewe na imani yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…