Radio Wasafi vs. Clouds FM...

Radio Wasafi vs. Clouds FM...

Kwan bongo kuna radio ngap? Si muende huko kwingne kwanini mkimbilie clouds. Mi naona sometimes ni ujinga, inakuaje mtu unapiga kelele eti mlimani city vitu bei mbaya wakat maduka yapo tu mengi mjini hapa ila shobo zako mwenyew ndio unakimbilia mlimani city.
Safi sana mkuu
 
Nawapongeza hao Wasafi kwa ujio wao huu wa kuwa na Media yao kwani wataongeza ushindani na hata kuleta ushindani katika Tasnia nzima ya Habari, Utangazaji na Mawasiliano ila tu wasijidanganye na hata Sisi Wadau tusijidanganye kwani kwa ' mizizi ' iliyojingea Clouds Media Group na kwa sifa yao ya kuwa ' Wabunifu ' kila uchao itawachukua miaka hata 10 ijayo kwa Wasafi Media kuwakaribia na siyo kuwafikia Clouds Media Group ' Kiubora '. Hata Efm Redio ambayo Watu wengi ilipoanzishwa walikuwa wakiisifia na kudhani kuwa itaipiku na kuleta ' ushindani ' wa Kitija bado haijaweza kufanikiwa katika hilo na bado tu wanapambana kama siyo kujitutumua.

Clouds Media Group naifananisha na Chama cha CCM na hizo Redio zingine nazifananisha na Vyama vya CHADEMA, CUF na ACT ambapo vinajitahidi kupambana lakini bado havijajizatiti kuweza kushindana.

Yangu ni hayo tu.
We jamaa huwa una akili sana!
 
Watu gani wananyanyaswa na Clouds..?? Au wao ndo mnawanyanyasa kwa kuwavamia usiku na silaha.?? Halafu kesho mnasifiana "PIGA KAZI". Nadhani ingekuwa wananyanyasa wangeshakamatwa siku nyingi.

Au ni watu gani hao unaozungumzia..??
Eti redio inayonyanyasa watu na wasanii ndo inazidi kuwa juu... kuna watu hata hawafikirii mbali
 
Samahani unaishi Tz hasa Dar au?!
Unafuatilia wasanii wanavyoilalamikia clouds media group?!

Kama hujafuatilia basi kaa kimya Maana utaonekana kituko mbele ya jamii
Kama inawaboa si waende Radio nyingine? Au ipo redio moja?

Mbona WCB wana shutuma kibao?

Watu wanamlaumu hadi Mungu sembuse Clouds!
 
Kumbuka nyuma ya wasafi kuna babu tale na said fela je hao jamaa wamewai kulalamikiwa na wasanii wangapi??
Well said mkuu! WCB wenyewe shutuma kibao, inayotrend sasa ni kutaka kumshusha Aslay so shutuma lazima ziwepo tu
 
Azam Fc ni ya lini na Simba Fc pamoja na Yanga Fc ni za lini lakini bado Azam inatisha?

Kikubwa ni uwekezaji tu.
Clouds pia wamefanya uwekezaji mkubwa na ndo kilichowafikisha hapo
 
Yap, nakaa Dar. Lakini pia hata mikoani Clouds inasikika. Au hao wasanii wanaolalamika huwa mnakutana vijiweni...???

Sio kila anayelalamika basi anaonewa kweli. Muda mwingine tunashindwa kukubali kutokukubaliana au tunashindwa kuwa na makubaliano chanya na demands wanazotaka wao kama service providers, so tunaishia kulalamika tu.

Hata watoto wa kambo muda mwingine huwa tunawaonea huruma kwa kudhani kweli wanaonewa kweli, bila hata kupima tabia zao binafsi. Yawezekana akawa mtoto ni pasua kichwa na full mibangi, ila tunawatetea tu.
Kuna East Africa Radio, kuna E FM, Kuna Radio One Sterio, kuna TBC FM na TBC Taifa na kadhalika... Hao wanaolalamika waende Radio nyingine.

Mbona hawailalamikii EATV/Radio ambayo nayo haipigi nyimbo za Dai?
 
Nilisikia kipindi kile kabla ya beef walikuwa ni mwendo kumfunua mtoto wa watu sasa hiv nasikia nandy ndiyo kipozeo cha mkurugenzi
Anawabaka? Nadhani mapenzi ni makubaliano Kati ya watu wawili na kuwa boss haimaanishi hupaswi kupenda.
 
Ni kitu ambacho kipo japo sisi watanzania tunatabia ya kutaka kuona wenzetu wakifeli mfano team kiba leo mnafurahia diamond
kugombana na clouds lkin mjue clouds wakisha malizana na diamond watamgeukia kina ivyo huu ndo wakati wa wasanii kusimama pamoja na kupigania masilahi yao maana clouds imewaumiza watu wengi sana kuliko mfano na list ni kubwa sana ya wasanii waliopoteza na clouds kisa wao waliamua kupambania maslahi yao mfano watu kama banana zoro kigwema mapacha sugu wakina juma nature wakina h baba k sal abby skilz mpaka sasa yupo kwa studio ya nas b Anahangaika kuangalia kama atashine tena nas b ingawa yeye Mungu amemsaidia akafungua ofisi yake kwa maana recording studio watu kama Wachuja nafaka watu kama bigdog poz watu kama pig black watu kama sam wa kwel watu kama chelea man watu kama dullayo watu kama nako 2 nako na wengine wengiiiiiii orodha ni kubwa mno kifupi clouds wanautumia na pale unapokuja kujitambua kuwa unaibiwa na ukaamua kudai maslahi yako ndo wanapo anza kukuzushia maskendo kibao lengo lao ikiwa ni kukumbusha chini namaanish kukupoteza kabisa kwenye ramani ya muziki
Kabisa mkuu. Eti mtu na akili zake anajitokeza wazi eti Clouds ife kwa sababu inakuja WCB Radio /TV [emoji15] . Hizo ni akili?
 
Clouds media LAZIMA wafanye vil kwa sababu wamefanya ile kuwa mtego wao kuwanasa wadada wa mjini wasiojitambua. Binafsi sidhani kama Wasafi radio itafika mbali, kwa sababu ukiangalia wasanii walionao hakuna hata mmoja mzuri including Diamond mwenyewe.
Wenzio wanapiga pesa, mambo ya Wadada ni km accident
 
Teh teh teh..

Walikuja Times Fm,Wakaja Efm mkasema hvyohvyo..kwahyo sahv tumaini lenu ni Wasafi Radio na tv..
Mwisho wa siku weledi ktk kazi ndo kila kitu, Ruge anachukiwa sana coz ndo mastermind wa pale na clouds inasonga.

Kuja na sababu eti inawanyanyasa wasanii ndo kuishushe wakati wasanii wenyewe ndo wanaikimbilia ni kukosa hoja.
 
Binafsi siyo mshabiki wa muziki, lakini clouds kwangu mimi ni zaidi ya radio, sasa hebu niambieni mtu kama mimi nisiyependa miziki mkaleta redio kwa ajili ya wanamuziki mnawezaje kunipata? Au hiyo wasafi radio inakuja na lipi jipya ambalo halipo clouds?

Suala la wao clouds kunyanyasa wasanii wala halina uhusiano na mimi kusikiliza sports xtra au jahazi au power breakfast, hao wasanii kama wananyanyaswa ni lini watafika mahakamani kwenda kudai kukiukwa kwa MKATABA kati yao na clouds? Ni lini wasanii wamekubaliana na clouds kwamba katika fiesta arusha tutakulipa kadhaa halafu hajalipwa?

Wananyanyaswa au wanakubaliana? Isijekuwa wanakubaliana halafu wakitoka wakakutana na fulani anamuambia umelipwa kidogo sana halafu anakasirika anasahau walikubaliana.....

Radio ya kuifunika clouds haitozaliwa na watajwa.
Nimekusoma mkuu
 
Back
Top Bottom