Radio Wasafi vs. Clouds FM...

Safi sana mkuu
 
We jamaa huwa una akili sana!
 
Watu gani wananyanyaswa na Clouds..?? Au wao ndo mnawanyanyasa kwa kuwavamia usiku na silaha.?? Halafu kesho mnasifiana "PIGA KAZI". Nadhani ingekuwa wananyanyasa wangeshakamatwa siku nyingi.

Au ni watu gani hao unaozungumzia..??
Eti redio inayonyanyasa watu na wasanii ndo inazidi kuwa juu... kuna watu hata hawafikirii mbali
 
Samahani unaishi Tz hasa Dar au?!
Unafuatilia wasanii wanavyoilalamikia clouds media group?!

Kama hujafuatilia basi kaa kimya Maana utaonekana kituko mbele ya jamii
Kama inawaboa si waende Radio nyingine? Au ipo redio moja?

Mbona WCB wana shutuma kibao?

Watu wanamlaumu hadi Mungu sembuse Clouds!
 
Kumbuka nyuma ya wasafi kuna babu tale na said fela je hao jamaa wamewai kulalamikiwa na wasanii wangapi??
Well said mkuu! WCB wenyewe shutuma kibao, inayotrend sasa ni kutaka kumshusha Aslay so shutuma lazima ziwepo tu
 
Azam Fc ni ya lini na Simba Fc pamoja na Yanga Fc ni za lini lakini bado Azam inatisha?

Kikubwa ni uwekezaji tu.
Clouds pia wamefanya uwekezaji mkubwa na ndo kilichowafikisha hapo
 
Kuna East Africa Radio, kuna E FM, Kuna Radio One Sterio, kuna TBC FM na TBC Taifa na kadhalika... Hao wanaolalamika waende Radio nyingine.

Mbona hawailalamikii EATV/Radio ambayo nayo haipigi nyimbo za Dai?
 
Nilisikia kipindi kile kabla ya beef walikuwa ni mwendo kumfunua mtoto wa watu sasa hiv nasikia nandy ndiyo kipozeo cha mkurugenzi
Anawabaka? Nadhani mapenzi ni makubaliano Kati ya watu wawili na kuwa boss haimaanishi hupaswi kupenda.
 
Kabisa mkuu. Eti mtu na akili zake anajitokeza wazi eti Clouds ife kwa sababu inakuja WCB Radio /TV [emoji15] . Hizo ni akili?
 
Wenzio wanapiga pesa, mambo ya Wadada ni km accident
 
Teh teh teh..

Walikuja Times Fm,Wakaja Efm mkasema hvyohvyo..kwahyo sahv tumaini lenu ni Wasafi Radio na tv..
Mwisho wa siku weledi ktk kazi ndo kila kitu, Ruge anachukiwa sana coz ndo mastermind wa pale na clouds inasonga.

Kuja na sababu eti inawanyanyasa wasanii ndo kuishushe wakati wasanii wenyewe ndo wanaikimbilia ni kukosa hoja.
 
Nimekusoma mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…