John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Wazazi wako tu waliokuleta duniani ndio Marafiki wa kweli kwa mtu yoyote yule.Hii iko wazi kabisa kuwa Marafiki wengi husalitiana Mume kwa Mke.
Malalamiko ya marafiki kugeukana yamekuwa mengi kipindi hiki.
Hata mahakamani kesi nyingi ni za watu ambao waliwahi kuwa marafiki wakubwa wakashirikiana katika baadhi ya mambo mwisho wa siku wakagombana na kupelekana mahakamani.
Lakini pia unapopata tatizo mtu wa kwanza kutafutwa ni rafiki yako wa karibu kuulizwa uko wapi na unafanya nini ama kwa nini umebadilika.
Je una rafiki unayemuamini na kumpa siri zako zote?
Tujuze rafiki wa kweli ana sifa zipi?