Rafiki wa mume wangu ananitaka

Rafiki wa mume wangu ananitaka

mkuu, it is the truth and nothing but the truth

inauma sana uchungu

Nimeisoma yote! Jamaa wametuchana sana.....hebu angalia issue ya Radar...na JF inavyoendeshwa ....pathetic....Back to the topic....unajua waandishi wa tamthilia wamekuwa wengi sana JF...I dont buy this piece of commedy
 
Hivi rafiki wa mume wako inakuwaje awe anakupigia wewe simu?

Kwangu haimake sense hata kidogo. Rafiki wa mume ni rafiki yake yeye na ibaki hivyo. Na rafiki zako wewe mwanamke wasiwe na mawasiliano na mume wako na ibaki hivyo
 
Mimi hapo nimepapenda, kumbe asingekuwa mtu wa karibu ungemkubalia? Duh! kazi ipo kwenye ndoa zetu

loooo naona watu mmekomaa sana na hili. kinachokushinda kuelewa hapo nini. nimesema hivo kwa maana kwamba angekua mtu wa mbali asiejua kama ni mke wa mtu basi ningemfahamisha ili akomage. sasa hapa namshangaa huyu kwani anajua fika kua niko na mume tena anaejidai rafikie.
 
Jichunguze kama kuna indicator uliwasha iliyopelekea hayo kutokea. Kama ipo izime mapema maana imemu invite huyo na ita invite wengine pia. Next time usikubali miadi bila mumeo kuwa na taarifa hata kama ni dharura mwambie we si kitengo cha dharura ampigie rafiki yake.
 
Hivi rafiki wa mume wako inakuwaje awe anakupigia wewe simu?

Kwangu haimake sense hata kidogo. Rafiki wa mume ni rafiki yake yeye na ibaki hivyo. Na rafiki zako wewe mwanamke wasiwe na mawasiliano na mume wako na ibaki hivyo

Hii ni Tamthilia ...do not take it seriously!
 
Personally, huwa sipendi kabisa mke wangu anambie habari za nani amemtongoza au anamtaka. Maana kwanza inanipa mashaka kama kweli jamaa hajala. Maana anaweza kuwa ananambia kama sehemu ya kujilinda yeye binafsi, pili inaweza kuwa ni kinga, ili siku nyingine ukiona message mbaya kutoka kwa jamaa usiwe na la kusema, maana ukimuuliza atakwambia "si nilikwambia kwamba ananitongoza?" I hate it! Mke wangu ni mtu mzima, afanye maamuzi yake mwenyewe, wala asinihusishe mimi juu ya yale anayojibizana au wanayokubaliana na dume lake huko. Hata mimi nina madada wanaonitaka na simwambii yeye. So kama mme wake ni wa aina kama yangu, ni bora kutokusema kabisa. otherwise timbwili linaanza!!
zingatia ushauri huu haraka dada,usipende kushtakshtak utakuja jutia,lakin pamoja na hayo kunajinsi unavomtega huyo jamaa...either kwa kumkalia vibaya,kumlegezea macho lakin kama yana mvuto,kmbania pua,kumkonyeza au kumponda mmeo huku akiwepo..si bure.
 
Kisasangwe

Na utakuwaje na miadi ya kukutana na rafiki wa mumeo bila ya mumeo kuwa na taarifa?
 
zingatia ushauri huu haraka dada,usipende kushtakshtak utakuja jutia,lakin pamoja na hayo kunajinsi unavomtega huyo jamaa...either kwa kumkalia vibaya,kumlegezea macho lakin kama yana mvuto,kmbania pua,kumkonyeza au kumponda mmeo huku akiwepo..si bure.

none of the above mr. Naona tu mhaya huyu ana lake.
 
Sasa majuzi alinicall akasisitiza nimwone ana shida sana ya kuongea na mie. nikamwambia tungekwenda na Mr weekend, akakataa akadai shida yake ni siku hiyo hiyo. mi kwa heshima kabsaaa nkakubali nikijua ni shida ya kweli. nikajitoa job mapeema ili nikamwone.
Kufika alikosema nimkute nikakuta mwenzangu ashaanza kuutwika mtungi, kwa vile mi si mnywaji wa pombe nikaagiza maji yangu. Nkamuliza Shem kulikon? hakyanani mi sikuamini kama alimaanisha manake mshenzi yule eti na chumba alishalipia ili .... jamani jamani mi hata sijui nimwambie mume wangu au nifaneje manake nimekwazika sana kwa kweli. sina hata raha mie manake mtu bora hata angekua simjui au hana ukaribu na familia sasa huyu wako marafiki na ni mtu tunaemvalue kama rafiki kumbe ajenda zake mbovu.

kwa hali hii yani duuh sijui kwa kweli.

kisasangwe..

Kama unaweza kumfuata mwanamume asiye mume wako baa, likelyhood ya kuingia "guest house" na huyo mwanamume au mwanamume mwingineo ni kubwa - that means lazima siku hiyo either mli-do na sasa unajuta au unam-feel huyo jamaa na hiyo post is mere guilty consciousness..

So, mnaweza mkapeana na shemeji yako as long as kila kitu kinabaki SIRI!!!
 
Kweli kabisa,Lazma alishapiga mahesabu yake, na jinsi unavyobehave kwake akajua lazma utakubal tu, vinginevyo asingethubutu hata kukutongoza tena alipie na chumba kabisa mhhhh miamekudharau sana sana.Wala usimwambie mumeo, jipange mwenyewe ulimalize.
Duh kwahiyo wale viwembe wanaofata kila mtu na kudhani kila mtu atawakubali siku hizi hawapo???, tena ukizingatia alishapiga kinywaji.., hapa naona.... We are blaming the Gun instead of the Shooter
 
Kisasangwe

Na utakuwaje na miadi ya kukutana na rafiki wa mumeo bila ya mumeo kuwa na taarifa?


hili mwalimu nadhani linawezekana kutegemeana na mazingira husika,
tatizo linaweza kuwa kwenye hiyo mada itakayozungumzwa tu..........................
 
Kisasangwe

Na utakuwaje na miadi ya kukutana na rafiki wa mumeo bila ya mumeo kuwa na taarifa?
If this story is true....
je huwezi kumsikiliza rafiki ya mume wako akikuita ili aombe ushauri..? maybe anataka ushauri ambao mwanamke ndio anaweza akautoa hususan kama hio issue inahusu mke wake.., au anakutafuta hili mumfanyie surprise mume wako ya birthday.. Hivi kweli tumefikia wakati wa kutokumuamini mtu yeyote na kuomba ruhusa ya kila tunachofanya?
 
Duh hapa kuna shida kubwa. Inaelekea mmekuwa na mgongano wa 'mawasiliano' (ya alama) kwa muda mrefu na huyo shemejio. Most likely kuna signals kutoka kwao alikuwa anazitafsiri ndivyo sivyo au pengine hukuwa umemaanisha kuzituma signal hizo kwake.

Kama mpaka aliandaa na chumba maana yake alikuwa amekusoma kama 'maji mara moja' au wengine wanasema 'maharage ya mbeya' (if you know what I mean!). Ni vema ukajitizama upya jinsi unavyo behave mbele yake au mbele za watu. Lakini inawezekana everything is fine with you isipokuwa huyo mwanaume ni mkware tu.
.

Bwana
smu, umesema nililotaka sema, mara nyingi the way women behave ndio anatafsiriwa, Inaonesha kunauchangamfu uliopitiliza ambao umekuwa ukimuonyesha mfano kuhagi, au kusema tumekumis na kujichekesha sana au kujishaua kwa jamaa pia kumsifia kila wati,umependeza sana leo au gari lako zuri, umepuliza pafume nzuri na mambo mengi kama hayo. hata kama haukuwa na jambo lolote katika moyo wako, mara nyingi hili hutokea kwa mwanaume ambae ana uwezo kiuchumi kuzidi mumeo. SASA kwa mwanaume mzaifu moja kwa moja anaingia kwenye taamaa.
Kosa ulilofanya nikama wengine walivyo changia, kukubali kukutana naye bila kutoa taarifa kwa mumeo, chukulia mfano hata kama asingekutaka kimapenzi lakini mumeo akakukuta katika mazingira kama hayo bila ya yeye kuwa na taarifa bado ingekuwa ngumu kutoa maelezo.

Sasa Muonye jamaa, akiendelea fanya kama
afrodenzi alivyo shauri
 
hili mwalimu nadhani linawezekana kutegemeana na mazingira husika,
tatizo linaweza kuwa kwenye hiyo mada itakayozungumzwa tu..........................

Mkuu Bacha kama unamuachia wife wako atende hilo, ndio unaanza kuwajengea mazingira rafiki zako wafanye wayapendayo kwa mwandani wako.

Sijaona mantiki hata kidogo.

Kama alikupigia simu uko kazini kuwa lazima leo tuonane, unatakiwa kumuandikia japo msg mume kumwambia kuwa ukitoka kazini utapita kuonana na rafiki yake kwa vile amepiga simu ana shida mno. As simple as that. Kutofata hizi kanuni za kimaadili ndio zilikomfikisha mtoa mada hapo alipo
 
hii iliwahi kumkuta wife.....alikuja kuniambia......nikasema isiwe tabu..nikamwita yule jamaa yeye na mkewe....tukapata chakula cha mchana pale kwangu...baada ya hapo agenda kuu ikaanza....nikamuuliza pale pale na nikamwambia jinsi tulivyoheshimiana...na baada ya hapo nikavunja urafiki nae na nikampiga marufuku kukanyaga kwangu.....sikufichi alihama mji kwa aaibu na ninasikia hata mkewe waliachana huko mbele..........
 
Nimeisoma yote! Jamaa wametuchana sana.....hebu angalia issue ya Radar...na JF inavyoendeshwa ....pathetic....Back to the topic....unajua waandishi wa tamthilia wamekuwa wengi sana JF...I dont buy this piece of commedy
Moja ya makosa makubwa ambayo tunayafanya wanadamu ni kuamini unachohisi,fahamu na kumbuka unachofikiri ni mawazo yako na hayana uhusiano na ukweli,unapofanya maamuzi kutokana na unachofikiri kikawa wrong sijui utafanya nini!Kuwa makini sana na unayofanya na kuamua!
 
Hivi rafiki wa mume wako inakuwaje awe anakupigia wewe simu? Kwangu haimake sense hata kidogo. Rafiki wa mume ni rafiki yake yeye na ibaki hivyo. Na rafiki zako wewe mwanamke wasiwe na mawasiliano na mume wako na ibaki hivyo
Nakubaliana nawe..kuna dada hapa JF ameshauri wanawake watumie akili zao kufikiria sio vinginevyo..haingii akilini kuwa mwanaume anashida badala kuomba msaada toka kwa rafikiye aombe kwa mke wa rafikiye...ok imeshatoke na iwe fundisho kwa wote. Recipe ya tatizo imeanza na mawasiliano ambayo supposedly yalikuwa honest kati ya familia mbili...shida ni channels iliyokuwa ikitumika...kwa mawasiliano yenye tija ni lazima head of the house ashirikishwe and not otherwise.
 
If this story is true....
je huwezi kumsikiliza rafiki ya mume wako akikuita ili aombe ushauri..? maybe anataka ushauri ambao mwanamke ndio anaweza akautoa hususan kama hio issue inahusu mke wake.., au anakutafuta hili mumfanyie surprise mume wako ya birthday.. Hivi kweli tumefikia wakati wa kutokumuamini mtu yeyote na kuomba ruhusa ya kila tunachofanya?

hii ni kweli na imetokea si muda mrefu. kwa kweli kwa mazingira aliyoyaweka hata kama mtu ukiwa mbishi ungekwenda. hasa ukizingatia nimeshasema kuna wakati nilikua msaada kwake na mkewe walipohitilafiana. so kwa mazingira kama haya tena baada ya kumwambia kwamba tungekwenda na Mr weekend ye akasisitiza shida haiwezi ngoja hivo niende, kwa ustaarabu tu nilikwenda nikijua pengine ni kama wakati ule walipokosana na mkewe.

wengi wanadai ilikua kosa kwenda, ila hebu mtu ajiweke kwenye nafasi hiyo. ikiwa suala ni kuomba ruhusa basi itajafikia wakati hata mtu anakufa mtu ushindwe msaidia kumpeleka hata hosp kisa hujaomba ruhusa
 
JF...I dont buy this piece of commedy
Mkuu ikija kwenye issue ya authenticity ya habari humu JF I can guarantee you that 80% ni Fiction; lakini uzuri wa mambo ushauri unaoweza kutoa hapo unaweza kumsaidia mwingine.....
 
Mnyime huyo, anataka kukuchakachua huyo. Hako kawowowooo kaka kamemtega jamaa teh!
 
Back
Top Bottom