Vyovyote vile....Kwa nini utoe taarifa kama mtu unajiamini na unaamini kwamba shemeji yako ni mtu genuine? Au ina maana kwamba kwenye ndoa zetu siku hizi wa wanaishi kimachale machale?? Bado sielewi!
wewe unaonaje? hafai kuwa mpango wa kando? chukua ngoma bana.. watakucheka!!Jamani mi hata sielewielewi huyu kiumbe anataka nini. ni rafiki wa karibu sana na mume wangu. Amekua na tabia ya kutaka sana kunijulia khali.
nami kama shemeji namsabahi na namheshimu sana.
Mwenyewe kaoa, ana mtoto mmoja.
Sasa majuzi alinicall akasisitiza nimwone ana shida sana ya kuongea na mie. nikamwambia tungekwenda na Mr weekend, akakataa akadai shida yake ni siku hiyo hiyo. mi kwa heshima kabsaaa nkakubali nikijua ni shida ya kweli. nikajitoa job mapeema ili nikamwone.
Kufika alikosema nimkute nikakuta mwenzangu ashaanza kuutwika mtungi, kwa vile mi si mnywaji wa pombe nikaagiza maji yangu. Nkamuliza Shem kulikon? hakyanani mi sikuamini kama alimaanisha manake mshenzi yule eti na chumba alishalipia ili .... jamani jamani mi hata sijui nimwambie mume wangu au nifaneje manake nimekwazika sana kwa kweli. sina hata raha mie manake mtu bora hata angekua simjui au hana ukaribu na familia sasa huyu wako marafiki na ni mtu tunaemvalue kama rafiki kumbe ajenda zake mbovu.
kwa hali hii yani duuh sijui kwa kweli.
Tuko pamoja kabisa. Mimi na unoko wangu wote kuna watu wakiniita sijuhi hata kama nitakumbuka kumtaharifu hubby kwani they are our friends na mume wangu hana right ya kunihisi vibaya akinikuta nao. Mume wangu ni mtu mwenye bonge la wivu ila kuna rafikiye ambaye ni best huyo hata tukikutana (mbele ya hubby) yeye lazima anipe hug ya nguvu na mume wangu na wivu wake wote ha mind kabisa kwa sababu ni rafiki yake na anamuamini 100% na ndiyo staili yake ya kunisalimia tangu sijaolewa up to now 8 years na hajawahi kunitaka. Na he is the only person ambae nikigombana na hubby naenda kumshtaki. Kweli nyie wenzetu ina maana hamna watu mnaowaamini maishani??? If so you have problems. Na tatizo si kuwa hamuamini marafiki ila hamuwaamini wenza wenu pia.
Yaani nitoe taharifa kila niendako??? Hapo nitakuwa tayari nimesha utilia shaka huo wito. Haa. SIjauza uhuru wangu kiasi hicho. Naenda popote nitakako nitatoa feedback jioni tukikutana home. Hata yeye anakata mitaa na he might share with me where he was the whole day (kama kuna something worth sharing) au asinambie. Kuoa au kuolewa si jela jamani eeh. Yaani nimwambie marafiki zangu ofisini wa kike na wa kiume wameandaa suprise party somewhere. Afu aniambie usiende. Tunapendaga wenyewe kuchungwa sometimes. Ukianza kuomba ruhusa jua maisha yako yote utakuwa treated like a child!!! And you will never ever enjoy marriage life.
Kuna vitu siwezi fanya yes, kama kutoka home bila kuaga; ila safari za juu kwa juu. Sorry siombi ruhusa wala nini!
Kuoa au kuolewa haina maana huna authority at all.
umeona eeh! watu wanajudge sana kwamba nilifanya kosa sana kwenda. ila hawataki kukubaliana na uhalisia kwamba kuna wakati mtu ukiwa huna mashaka utaenda. sipendi kuishi kwa wasiwasi kwamba kila saa naripoti kwa mume, vilevile yeye anajua kwamba nina akili timamu hivo kuchungwa si poa. mtu hachungwi bwana. ikifikia hatua ya kuchungana itafikia hata mtu kwenda kwa daktari utasubiri ruhusa, dk yupi ok kukutibu na yupi noo..
wanawake wengi hawawezi kubisha kwamba hata kama wameolewa mara kibao wanazukiwa na wanaume wakware, ambao hata ukisema umeolewa watasumbua tu. wako wanaojidai eti mwanaume kumtokea mwanamke kunakua na dalili za mapenzi kwanza... mh huu unafki bana. mara ngapi mtu unakua hata umekaa kwenye semina siku moja tu mtu anaanza habari hizi sasa hizo dalili unakua umezionesha sa ngapi. Wengine wanadhani na kushauri kwa kufikirika tu madhali hayajakukuta. aaaaagrgh mi kinachonikera ni hili kwamba huyu ni mtu niliekua namheshimu sana.
Am just thinking kwa imani hii what if ingetokea bahati mbaya akakubaka!? Najua ulishasema mlikutana open space but supposed, supposed ingetokea akakubaka kwa nguvu........what will that be!! Just thinking, Kumbuka pia kuna tofauti kati ya kuripoti na kujulisha/kumweka mwenzako 'in the know' situation!
umeona eeh! watu wanajudge sana kwamba nilifanya kosa sana kwenda. ila hawataki kukubaliana na uhalisia kwamba kuna wakati mtu ukiwa huna mashaka utaenda. sipendi kuishi kwa wasiwasi kwamba kila saa naripoti kwa mume, vilevile yeye anajua kwamba nina akili timamu hivo kuchungwa si poa. mtu hachungwi bwana. ikifikia hatua ya kuchungana itafikia hata mtu kwenda kwa daktari utasubiri ruhusa, dk yupi ok kukutibu na yupi noo..
wanawake wengi hawawezi kubisha kwamba hata kama wameolewa mara kibao wanazukiwa na wanaume wakware, ambao hata ukisema umeolewa watasumbua tu. wako wanaojidai eti mwanaume kumtokea mwanamke kunakua na dalili za mapenzi kwanza... mh huu unafki bana. mara ngapi mtu unakua hata umekaa kwenye semina siku moja tu mtu anaanza habari hizi sasa hizo dalili unakua umezionesha sa ngapi. Wengine wanadhani na kushauri kwa kufikirika tu madhali hayajakukuta. aaaaagrgh mi kinachonikera ni hili kwamba huyu ni mtu niliekua namheshimu sana.
MJ1....Please...huwezi kuwa Shekh Yahya ku-predict magnetude ya kila risk...Na mbaya zaidi kama mtu mwenyewe una imani naye.
Nadhani tukifika mahali ambapo kila mtu tunadhani atabaka basi itabidi wanawake wote wafungiiwe ndani kama kuku wa kisasa. Utapenda hayo yatokee??