rafiki yangu anaomba msaada wa kisheria

rafiki yangu anaomba msaada wa kisheria

mshana org

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2012
Posts
2,091
Reaction score
619
habari wakuu polen namajukumu.kuna rafiki yangu alikua na mke na mtoto 1 huyu mwanamke alimuoa baada ya kupata mimba inamaana walikua marafikitu kabla.na walikutana huku mjini jamaa mchaga mke mjaluo sasa jamaa kutokana na kipato kua
duni alishindwa kwenda kwao kwa mudahuo.ila aliongea na wazazi kwa njia ya cm na wakamkubalia waishtu ili badae akipata uwezo ndipo aende.sasa kilichotokea baada ya miaka 2 kupita akiwa anaendelea kujikusanya aweze kwenda mwanamke alipata
msiba kwao jamaa wakapanga na mkewake kwakua hawana pesa yakutosha mke aende yeye kufika kwao akagoma kurudi mpaka jamaa aende akalipe mahari jamaa kabembeleza ikashindikana akaambiwa kamahawezi kwend atume mahari kwa mpesa.wakati anaendelea kujipanga baada ya mwezi akambiwa mke ameolewa namtumwingine kibaya zaidi mtoto wajamaa kalipiwa mahari namume mpia jamaa kaambiwa hana chake amechanganyikiwa anaomba ushauri afanyeje ampate mtoto wake?naamini hapa wapowajuzi namsaada asante sana.kama kuna sehemu
nimekosea naomba radh
 
nimetanguliza samahani lakn nilijua nitakosea coz hapa natumia cm na nimeandika kwaharaka sana kwakua nilikua nimebanwa na ishu nyingine.ila tuachane na mwandiko tumsaidie kijana mwenzetu.
 
Eh,mbona me naona muandiko ni mzuri tuu waungwana!
 
lengo nikumpa mongozo mjia anayoweza kutumia kumpata mtoto wake

Afu we nawe hutaki kujishughulisha kha,ushawekewa link hiyo hapo unataka muongozo gani tena?!..Kama vp pandeni gari muende mkamchukue mtoto.
 
Nashukuru waku nilikua sijagundua kua hiyo ni link
 
hapo kaka angu huyo rafk yko anahaki zte cz kwanza wao wawili walishardhia kuendlea na maisha,pili wazaz walirdhia,tatu wameshaish takriban miaka miwili ki2 ambacho kisheria 2naita presumption of marriage kwenye Sheria ya ndoa
kifungu cha 160(1&2) .mwambie aende mahakaman akafungue kesi ya madai ya ndoa juu ya ma2nzo ya mtoto ktk mahakama ya mwanzo,na akiona mambo yanazngua aappeal district court kwa ground kuwa hana uaminifu na maamuz ya mahakama ilyopta.
 
nashukuru mkuu nimemfikishia ujumbe.alienda ustawi wa jamii wakamzingua eti kwakua mtoto yuko musoma na yeye yuko arusha hawawezi kumsaidia labda atoe hela ili waweze kumfuata mtoto huko.
 
habari wakuu polen namajukumu.kuna rafiki yangu alikua na mke na mtoto 1 huyu mwanamke alimuoa baada ya kupata mimba inamaana walikua marafikitu kabla.na walikutana huku mjini jamaa mchaga mke mjaluo sasa jamaa kutokana na kipato kua
duni alishindwa kwenda kwao kwa mudahuo.ila aliongea na wazazi kwa njia ya cm na wakamkubalia waishtu ili badae akipata uwezo ndipo aende.sasa kilichotokea baada ya miaka 2 kupita akiwa anaendelea kujikusanya aweze kwenda mwanamke alipata
msiba kwao jamaa wakapanga na mkewake kwakua hawana pesa yakutosha mke aende yeye kufika kwao akagoma kurudi mpaka jamaa aende akalipe mahari jamaa kabembeleza ikashindikana akaambiwa kamahawezi kwend atume mahari kwa mpesa.wakati anaendelea kujipanga baada ya mwezi akambiwa mke ameolewa namtumwingine kibaya zaidi mtoto wajamaa kalipiwa mahari namume mpia jamaa kaambiwa hana chake amechanganyikiwa anaomba ushauri afanyeje ampate mtoto wake?naamini hapa wapowajuzi namsaada asante sana.kama kuna sehemu
nimekosea naomba radh
hapo hamna mke kisheria hata kama aliishi naye kwa miaka miwili na zaidi. alikuwa hawara tu ambaye hatambuliki moja kwa moja kisheria, labda kwa exeption tu, huyo kisheria hakuwa mke na hawezi kumdai kuwa alikuwa mke wake kwasababu hawakufunga ndoa/hawana cheti cha usajili wa ndoa. presumption of marriage in exception pia. hiyo presumption of marriage/dhana ya ndoa inaweza kutumika tu kwa mshikaji kudai fidia kama kwa miaka hiyo aliyokaa naye, au kwa mwanamke kuolewa na mwanaume mwingine yeye mwanaume ameathirika na kutendwa huko na amepata hasara fulani. na presumption hiyo imewekwa na sheria kama rungu la kupatia haki upande unaotaka kudhulumiwa tu, kama hakuna upande unaodhulumiwa basi presumption of marriage haihalalishi uhawara kuwa ndoa, na sheria haiutambui.

vilevile, unatakiwa kuelewa kuwa, issue ya kuishi na mtoto kwa wazazi wasioishi pamoja ipo kisheria; nayo ni, mtoto yeyote mwenye umri chini ya miaka saba anatakiwa kuishi na mama yake labda kama ikithibitika kuwa kuishi na mama yake huyo kutaathiri maslahi bora ya mtoto. hivyo mtoto huyo kama anakaa na mama yake kule alikoolewa upya baba hawezi kwenda kumchukua labda kama atathibitisha kuwa kuishi na mama yake huyo kutamuathiri mtoto katika maslahi bora ya mtoto.

sasa, jamaa afanyeje ili apate mtoto? asubiri mtoto afike miaka saba halafu akamchukue kisheria.(hata hivyo maslahi ya mtoto na hata wishes za mtoto mwenyewe zitakuwa considered wakati huo), its not guaranteed kwamba atampata labda mamake aamue; manake wamama wengine wanaweza kumlisha mtoto maneno ya sumu akamchukia kabisa babake na siku unaenda kumchukua basi mtoto anaonekana kabisa kuathirika kisaikolojia na kukataa kabisa hivyo wishes of the child zinaheshimiwa na unashindwa kumpata mtoto. Nimeandika haraka kwasababu niko safarini, nimesimama tu hapa kwa muda mfupi, unaweza kutuma maswali yako kwenye email hii then nikisettle nitakuelezea na kukupatia vifungu. mishpachabrucha@gmail.com

pia, hiyo link nimeweka hapo juu, unaweza kubonyeza SHERIA KWA KISWAHILI ndani yake utakuta kuna "contacts" utapata email na simu. pia ubonyeza kwenye "products" utaona kuna sehemu unaweza kupata vitabu na utadownload pia sheria mbalimbali bure. bofya SHERIA KWA KISWAHILI
 
hiyo ni presumption of marriage, kama mume na mke wamekaa miaka miwili, hata kama sio nyumba moja, na jamii inayowazunguka ( sio lazima wawe wazazi) ikaamini kuwa hao ni mke na mume, hapo dhana ya ndoa inakuwepo. kutokutoa mahali hakuathiri uhalali wa ndoa, ndugu hapo anaweza kudai fidia kutokana na uzinzi wa mkewe na wadaiwa wakawa mke pamoja na huyo bwana, au anaweza kudai talaka, suala la mtoto itategemea na ushahidi lakini mahakama huangalia maslahi ya mtoto, mahakama mara nyingi zinataka mtoto aishi na wazazi wake, kama huyo mama anatangatanga, kisheria anapata negative impression ya mahakama hasa ukichukulia ameshaolewa, mtoto atafata mila na tamaduni zipi? matunzo? jinsi gani ni rahisi kila mzazi kumuona mtoto na mengineyo
 
mheshimiwa, unajua essence ya 'PRESUMPTION OF MARRIAGE"?, iko pale kwaajili ya nini? na inaibuliwa wakati gani? hata katika mazingira haya?...well, kama unasema talaka itatolewa hapo, itatokaje talaka kwa mahusiano ya watu ambayo hayakuwa registered?

kwa kukusaidia ni kwamba, dhana ya kuchukulia ndoa ni exception tu ya general rule inayosema kuwa bila kuwepo registration ya marriage hakuna ndoa. sheria haiutambui muunganiko kati ya mwanaume na mwanamke wanaoishi pamoja bila kusajili muunganiko huo kama ndoa.

kwa kifupi ni kwamba, hata kama mahari imetolewa au labda ndoa imefungwa kimila wanandoa wanalazimika kuisajili ndoa hiyo ili waingizwe kwenye register kule kwa msajili mkuu. pindi talaka inapotamkwa na mahakama msajili huwa ana delete ndoa hiyo kwenye register ya ndoa. sasa kama hakuna usajili mahakama itatoa talaka gani, talaka kwa kitu kisichotambulika?

msimamo wa kisheria ni kwamba, ndoa inatambulika tu pale inapokuwa imesherehekewa na kusajilia, lakini exception yake ni kwamba, kama kuna tatizo kwa watu waliokuwa wakiishi pamoja kwa miaka si chini ya miwili mfululizo, jamii inayowazunguka imewachukulia kama mume na mke, wako katika umri unaoruhusiwa kisheria, na wana ndoa wote hawana ndoa inayoendelea(no existing marriage to either of them) basi, inaweza kudhaniwa kuwa watu hao ni mume na mke kama rungu la kuokoa maslahi ya yule anayetaka kudhulumiwa, akipata haki yake msimamo uko palepale, hakuna ndoa hapo. dhana hii inaibuliwa tu kwa nia ya kutetea maslahi ya yule anayetaka kudhulumiwa, kama hakuna kudhulumiwa muunganiko huu hautambuliki kabisa kama ni ndoa.

mfano pekee ni pale mwanaume na mwanaume wameishi miaka miwili au zaidi bila kusajili muunganiko huo kuwa ndoa, wamechuma mali pamoja, ikafika kipindi mmoja akapata mwanamke/mwanaume mwingine hivyo wakatakiwa kuachana, hapo dhana ya ndoa inaingilia ili wagawane mali bila dhuluma.

mfano mwingine mwanamke ameishi na mwanaume kwa miaka miwili au zaidi, wamechuma mali, mwanamme akafariki. kwenye mirathi, dhana ya ndoa inaweza kuingia ili mwanamke huyu hata kama hakuwa amesajili ndoa na marehemu, adhaniwe kuwa alikuwa mkewe ili apate shea kwenye mirathi.

kwenye mazingira kama haya, wameishi na mwanamke kwa miaka miwili au zaidi bila kusajili ndoa/kufunga ndoa, mmoja ameamua kumpenda mwingine akaenda kuolewa na kusajili kabisa ndoa, hapo yule aliyekuwa akiishi kihawara hawezi kuibua dhana ya ndoa, kwani anaibua ili imsaidia kuondoa dhuluma gani? kama ni huyo mtoto anaweza kumchukua bila hata kutumia rungu la dhana ya ndoa. labda kama anahisi amesababishiwa hasara fulani kwa kusalitiwa na huyo mwanamke aende akafungue kesi ya madai adai. ila kwasababu huyo mwanamke ameshafunga ndoa huyu hawara wa zamani ambaye hakufunga ndoa akilala naye kisheria anayezini ni huyu ambaye hakusajili ndoa na anaweza kufunguliwa kesi ya madai ya uzinzi kama kuna madhara yeyote kwake yaliyotokea.

katika kesi ya HOKA MBOFU V PASTORY MWIJAGE 1983 TLR 286(HC) iliamriwa kuwa, kama dhana ya ndoa haitaibuliwa na upande unaodhani unadhulumiwa, muungano huo hauwezi kutambuliwa ksawababu tu watu walikuwa wanaishi kihawara.lengo la sheria kuitambua dhana si kuhalalisha muungano huu usio rasmi kuwa ndoa lalali, lengo ni kupata haki kwa yule anayetaka kudhulumiwa (my emphasis added) .

pia katika kesi ya ZAINA ISMAIL V SAID MKONDO 1985 TLR 239 kesi ambayo mwanaume na mwanamke walikaa kinyumba miaka mitano bila kusajili ndoa, iliamriwa kuwa, pamoja na kwamba kifungu cha 160 kinatambua dhana ya kuchukulia ndoa, dhana ambayo inakanushika, lengo kuu la kifungu hiki sio kuunda utaratibu/njia mbadala wa kufunga ndoa, lengo lake kuu hapa ni kuitambua dhana hii ili kuokoa maslahi ya yule anayetaka kudhulumiwa tu.

kwa kifupi ni kwamba, kwasababu hao watu hawakuwa wamefunga ndoa, hawatambuliwi kisheria kuwa walikuwa kwenye ndoa. hapo hakutakuwa na talaka kwasababu huwezi kutoa talaka kwenye kitu ambacho hakikuwepo/hakikusajiliwa. ila kama huyo mwanaume ataona ameathirika kwa namna moja ama nyingine ambayo itabidi aithibitishie mahakama kuwa kweli ameathirika kutokana na kusalitiwa, anaweza kufungua shauri la madai tu. issue ya mtoto, kinachozingatiwa zaidi ni maslahi bora ya mtoto. kama maslahi ya mtoto yanaweza kuathirika kwa kuwa kwa huyo mama jamaa anaweza kwenda kumchukua. kama mtoto inaonekana ataishi vizuri tu, kisheria mtoto aliye chini ya miaka 7 anatarajiwa kuwa anatakiwa kuishi na mama yake. wishes za mtoto pia zitapimwa kama atakuwa na uwezo wa kujiexpress.
 
usajli wa ndoa si kigezo cha uhalali wa ndoa, zile mahakama za mwanzo vijijini mbon zinatoa talaka na hata za wilaya bila kuwa na proof ya registration? hata mahakama za mjini, presumption ina cover mazingira hayo ndio maana mahakama hutoa reliefs za kindoa, inaa-assume watu hao wameoana hata kama hawana vyeti,
 
mind you, definition ya ndoa haiongelei vyeti wala sherehe, ndoa ni muungano wa watu wawili, wa hiari, mengine ni umaliziaji wa taratibu ambao si wa lazima kwa mfano katika ndoa za kimila
 
further,kuna tofauti ya cohabitation na ndoa, people who cohabit can not, by way of evidence reach the burden of proof required in presumption of marriage, hao ni mahawara hata jamii ikiletwa kutoa evidence itasema ivo, they call it presumption of marriage because it need evidence to prove its existence in case there are doubts. THEN WHAT HAPPENS WHEN ONE PROVES THAT THERE IS A MARRIAGE, Can you still presume? you presume when you are waiting for proof. Law has a lot of presumption such as presumption of death, presumption of innocence e.t.c let's assume you enjoy presumption of innocence, the prosecution come with evidence, you are found guilty, the presumption will no longer protect you , the same is in presumption of marriage, if one proves that it is a marriage, then it is. Then the court will issue reliefs as per the marriage Act, 1971,if there Is cohabitation, th law of marriage will not apply coz the parties failed to meet the criterias set out in the LAW OF MARRIAGE ACT
 
mheshimiwa, unajua essence ya 'PRESUMPTION OF MARRIAGE"?, iko pale kwaajili ya nini? na inaibuliwa wakati gani? hata katika mazingira haya?...well, kama unasema talaka itatolewa hapo, itatokaje talaka kwa mahusiano ya watu ambayo hayakuwa registered?

kwa kukusaidia ni kwamba, dhana ya kuchukulia ndoa ni exception tu ya general rule inayosema kuwa bila kuwepo registration ya marriage hakuna ndoa. sheria haiutambui muunganiko kati ya mwanaume na mwanamke wanaoishi pamoja bila kusajili muunganiko huo kama ndoa.

kwa kifupi ni kwamba, hata kama mahari imetolewa au labda ndoa imefungwa kimila wanandoa wanalazimika kuisajili ndoa hiyo ili waingizwe kwenye register kule kwa msajili mkuu. pindi talaka inapotamkwa na mahakama msajili huwa ana delete ndoa hiyo kwenye register ya ndoa. sasa kama hakuna usajili mahakama itatoa talaka gani, talaka kwa kitu kisichotambulika?

msimamo wa kisheria ni kwamba, ndoa inatambulika tu pale inapokuwa imesherehekewa na kusajilia, lakini exception yake ni kwamba, kama kuna tatizo kwa watu waliokuwa wakiishi pamoja kwa miaka si chini ya miwili mfululizo, jamii inayowazunguka imewachukulia kama mume na mke, wako katika umri unaoruhusiwa kisheria, na wana ndoa wote hawana ndoa inayoendelea(no existing marriage to either of them) basi, inaweza kudhaniwa kuwa watu hao ni mume na mke kama rungu la kuokoa maslahi ya yule anayetaka kudhulumiwa, akipata haki yake msimamo uko palepale, hakuna ndoa hapo. dhana hii inaibuliwa tu kwa nia ya kutetea maslahi ya yule anayetaka kudhulumiwa, kama hakuna kudhulumiwa muunganiko huu hautambuliki kabisa kama ni ndoa.

mfano pekee ni pale mwanaume na mwanaume wameishi miaka miwili au zaidi bila kusajili muunganiko huo kuwa ndoa, wamechuma mali pamoja, ikafika kipindi mmoja akapata mwanamke/mwanaume mwingine hivyo wakatakiwa kuachana, hapo dhana ya ndoa inaingilia ili wagawane mali bila dhuluma.

mfano mwingine mwanamke ameishi na mwanaume kwa miaka miwili au zaidi, wamechuma mali, mwanamme akafariki. kwenye mirathi, dhana ya ndoa inaweza kuingia ili mwanamke huyu hata kama hakuwa amesajili ndoa na marehemu, adhaniwe kuwa alikuwa mkewe ili apate shea kwenye mirathi.

kwenye mazingira kama haya, wameishi na mwanamke kwa miaka miwili au zaidi bila kusajili ndoa/kufunga ndoa, mmoja ameamua kumpenda mwingine akaenda kuolewa na kusajili kabisa ndoa, hapo yule aliyekuwa akiishi kihawara hawezi kuibua dhana ya ndoa, kwani anaibua ili imsaidia kuondoa dhuluma gani? kama ni huyo mtoto anaweza kumchukua bila hata kutumia rungu la dhana ya ndoa. labda kama anahisi amesababishiwa hasara fulani kwa kusalitiwa na huyo mwanamke aende akafungue kesi ya madai adai. ila kwasababu huyo mwanamke ameshafunga ndoa huyu hawara wa zamani ambaye hakufunga ndoa akilala naye kisheria anayezini ni huyu ambaye hakusajili ndoa na anaweza kufunguliwa kesi ya madai ya uzinzi kama kuna madhara yeyote kwake yaliyotokea.

katika kesi ya HOKA MBOFU V PASTORY MWIJAGE 1983 TLR 286(HC) iliamriwa kuwa, kama dhana ya ndoa haitaibuliwa na upande unaodhani unadhulumiwa, muungano huo hauwezi kutambuliwa ksawababu tu watu walikuwa wanaishi kihawara.lengo la sheria kuitambua dhana si kuhalalisha muungano huu usio rasmi kuwa ndoa lalali, lengo ni kupata haki kwa yule anayetaka kudhulumiwa (my emphasis added) .

pia katika kesi ya ZAINA ISMAIL V SAID MKONDO 1985 TLR 239 kesi ambayo mwanaume na mwanamke walikaa kinyumba miaka mitano bila kusajili ndoa, iliamriwa kuwa, pamoja na kwamba kifungu cha 160 kinatambua dhana ya kuchukulia ndoa, dhana ambayo inakanushika, lengo kuu la kifungu hiki sio kuunda utaratibu/njia mbadala wa kufunga ndoa, lengo lake kuu hapa ni kuitambua dhana hii ili kuokoa maslahi ya yule anayetaka kudhulumiwa tu.

kwa kifupi ni kwamba, kwasababu hao watu hawakuwa wamefunga ndoa, hawatambuliwi kisheria kuwa walikuwa kwenye ndoa. hapo hakutakuwa na talaka kwasababu huwezi kutoa talaka kwenye kitu ambacho hakikuwepo/hakikusajiliwa. ila kama huyo mwanaume ataona ameathirika kwa namna moja ama nyingine ambayo itabidi aithibitishie mahakama kuwa kweli ameathirika kutokana na kusalitiwa, anaweza kufungua shauri la madai tu. issue ya mtoto, kinachozingatiwa zaidi ni maslahi bora ya mtoto. kama maslahi ya mtoto yanaweza kuathirika kwa kuwa kwa huyo mama jamaa anaweza kwenda kumchukua. kama mtoto inaonekana ataishi vizuri tu, kisheria mtoto aliye chini ya miaka 7 anatarajiwa kuwa anatakiwa kuishi na mama yake. wishes za mtoto pia zitapimwa kama atakuwa na uwezo wa kujiexpress.

wakuu ndoa ilikuepo ya kiislam tatizo ilikua mwanaume hajafika kwa wakwe na mahari alikua hajalipa
 
Back
Top Bottom