hiyo ni presumption of marriage, kama mume na mke wamekaa miaka miwili, hata kama sio nyumba moja, na jamii inayowazunguka ( sio lazima wawe wazazi) ikaamini kuwa hao ni mke na mume, hapo dhana ya ndoa inakuwepo. kutokutoa mahali hakuathiri uhalali wa ndoa, ndugu hapo anaweza kudai fidia kutokana na uzinzi wa mkewe na wadaiwa wakawa mke pamoja na huyo bwana, au anaweza kudai talaka, suala la mtoto itategemea na ushahidi lakini mahakama huangalia maslahi ya mtoto, mahakama mara nyingi zinataka mtoto aishi na wazazi wake, kama huyo mama anatangatanga, kisheria anapata negative impression ya mahakama hasa ukichukulia ameshaolewa, mtoto atafata mila na tamaduni zipi? matunzo? jinsi gani ni rahisi kila mzazi kumuona mtoto na mengineyo
mheshimiwa, unajua essence ya 'PRESUMPTION OF MARRIAGE"?, iko pale kwaajili ya nini? na inaibuliwa wakati gani? hata katika mazingira haya?...well, kama unasema talaka itatolewa hapo, itatokaje talaka kwa mahusiano ya watu ambayo hayakuwa registered?
kwa kukusaidia ni kwamba, dhana ya kuchukulia ndoa ni exception tu ya general rule inayosema kuwa bila kuwepo registration ya marriage hakuna ndoa. sheria haiutambui muunganiko kati ya mwanaume na mwanamke wanaoishi pamoja bila kusajili muunganiko huo kama ndoa.
kwa kifupi ni kwamba, hata kama mahari imetolewa au labda ndoa imefungwa kimila wanandoa wanalazimika kuisajili ndoa hiyo ili waingizwe kwenye register kule kwa msajili mkuu. pindi talaka inapotamkwa na mahakama msajili huwa ana delete ndoa hiyo kwenye register ya ndoa. sasa kama hakuna usajili mahakama itatoa talaka gani, talaka kwa kitu kisichotambulika?
msimamo wa kisheria ni kwamba, ndoa inatambulika tu pale inapokuwa imesherehekewa na kusajilia, lakini exception yake ni kwamba, kama kuna tatizo kwa watu waliokuwa wakiishi pamoja kwa miaka si chini ya miwili mfululizo, jamii inayowazunguka imewachukulia kama mume na mke, wako katika umri unaoruhusiwa kisheria, na wana ndoa wote hawana ndoa inayoendelea(no existing marriage to either of them) basi, inaweza kudhaniwa kuwa watu hao ni mume na mke kama rungu la kuokoa maslahi ya yule anayetaka kudhulumiwa, akipata haki yake msimamo uko palepale, hakuna ndoa hapo. dhana hii inaibuliwa tu kwa nia ya kutetea maslahi ya yule anayetaka kudhulumiwa, kama hakuna kudhulumiwa muunganiko huu hautambuliki kabisa kama ni ndoa.
mfano pekee ni pale mwanaume na mwanaume wameishi miaka miwili au zaidi bila kusajili muunganiko huo kuwa ndoa, wamechuma mali pamoja, ikafika kipindi mmoja akapata mwanamke/mwanaume mwingine hivyo wakatakiwa kuachana, hapo dhana ya ndoa inaingilia ili wagawane mali bila dhuluma.
mfano mwingine mwanamke ameishi na mwanaume kwa miaka miwili au zaidi, wamechuma mali, mwanamme akafariki. kwenye mirathi, dhana ya ndoa inaweza kuingia ili mwanamke huyu hata kama hakuwa amesajili ndoa na marehemu, adhaniwe kuwa alikuwa mkewe ili apate shea kwenye mirathi.
kwenye mazingira kama haya, wameishi na mwanamke kwa miaka miwili au zaidi bila kusajili ndoa/kufunga ndoa, mmoja ameamua kumpenda mwingine akaenda kuolewa na kusajili kabisa ndoa, hapo yule aliyekuwa akiishi kihawara hawezi kuibua dhana ya ndoa, kwani anaibua ili imsaidia kuondoa dhuluma gani? kama ni huyo mtoto anaweza kumchukua bila hata kutumia rungu la dhana ya ndoa. labda kama anahisi amesababishiwa hasara fulani kwa kusalitiwa na huyo mwanamke aende akafungue kesi ya madai adai. ila kwasababu huyo mwanamke ameshafunga ndoa huyu hawara wa zamani ambaye hakufunga ndoa akilala naye kisheria anayezini ni huyu ambaye hakusajili ndoa na anaweza kufunguliwa kesi ya madai ya uzinzi kama kuna madhara yeyote kwake yaliyotokea.
katika kesi ya
HOKA MBOFU V PASTORY MWIJAGE 1983 TLR 286(HC) iliamriwa kuwa, kama dhana ya ndoa haitaibuliwa na upande unaodhani unadhulumiwa, muungano huo hauwezi kutambuliwa ksawababu tu watu walikuwa wanaishi kihawara.lengo la sheria kuitambua dhana si kuhalalisha muungano huu usio rasmi kuwa ndoa lalali, lengo ni kupata haki kwa yule anayetaka kudhulumiwa (my emphasis added) .
pia katika kesi ya
ZAINA ISMAIL V SAID MKONDO 1985 TLR 239 kesi ambayo mwanaume na mwanamke walikaa kinyumba miaka mitano bila kusajili ndoa, iliamriwa kuwa, pamoja na kwamba kifungu cha 160 kinatambua dhana ya kuchukulia ndoa, dhana ambayo inakanushika, lengo kuu la kifungu hiki sio kuunda utaratibu/njia mbadala wa kufunga ndoa, lengo lake kuu hapa ni kuitambua dhana hii ili kuokoa maslahi ya yule anayetaka kudhulumiwa tu.
kwa kifupi ni kwamba, kwasababu hao watu hawakuwa wamefunga ndoa, hawatambuliwi kisheria kuwa walikuwa kwenye ndoa. hapo hakutakuwa na talaka kwasababu huwezi kutoa talaka kwenye kitu ambacho hakikuwepo/hakikusajiliwa. ila kama huyo mwanaume ataona ameathirika kwa namna moja ama nyingine ambayo itabidi aithibitishie mahakama kuwa kweli ameathirika kutokana na kusalitiwa, anaweza kufungua shauri la madai tu. issue ya mtoto, kinachozingatiwa zaidi ni maslahi bora ya mtoto. kama maslahi ya mtoto yanaweza kuathirika kwa kuwa kwa huyo mama jamaa anaweza kwenda kumchukua. kama mtoto inaonekana ataishi vizuri tu, kisheria mtoto aliye chini ya miaka 7 anatarajiwa kuwa anatakiwa kuishi na mama yake. wishes za mtoto pia zitapimwa kama atakuwa na uwezo wa kujiexpress.