Rafiki yangu anataka kunipa kiwanja

Rafiki yangu anataka kunipa kiwanja

almano

Member
Joined
Dec 2, 2016
Posts
56
Reaction score
102
Habarini wana JF!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza mm naish maeneo flani ya mji sasa ninarafiki yangu yupo vizuri kidogo kwa kuwa tuna urafiki wa muda mrefu rafiki yangu kwa kuon natesek na kodi anataka kunikatia kipande kidogo cha eneo lake ili nijenge.

Sasa swali langu je, vitu gani muhimu vya kuzingatia kwenye makabidhiano ili isije kuleta changamoto hapo baadae kweny umiliki wangu na ninapo amua kujenga mana binadamu hawaeleweki( wanabadilika) na yeye ndio mwenye hatimiliki asanten.
 
Habarini wana jf! Kama kichwa cha habari kinavyojieleza mm naish maeneo flani ya mji sasa ninarafiki yangu yupo vizuri kidogo kwa kuwa tuna urafiki wa muda mrefu rafiki yangu kwa kuon natesek na kodi anataka kunikatia kipande kidogo cha eneo lake ili ni jenge sasa swali langu je vitu gani muhimu vya kuzingatia kwenye makabidhiano ili isije kuleta changamoto hapo baadae kweny umiliki wangu na ninapo amua kujenga mana binadamu hawaeleweki( wanabadilika) na yeye ndio mwenye hatimiliki asanten.
Kwahiyo unataka Kujenga kwenye kiwanja cha mtu?

Andaa legal document ikionesha kuwa amekupatia sehemu ya Ardhi yake bure na ukubwa wake isainiwe na Wakili au hakimu na kugongwa muhuri wa Wakili au hakimu shughuri imeisha.

Ila ukitumia hakimu mahakamani ni bora zaidi mawakili wamekaa kipesapesa tu.
 
Habarini wana jf! Kama kichwa cha habari kinavyojieleza mm naish maeneo flani ya mji sasa ninarafiki yangu yupo vizuri kidogo kwa kuwa tuna urafiki wa muda mrefu rafiki yangu kwa kuon natesek na kodi anataka kunikatia kipande kidogo cha eneo lake ili ni jenge sasa swali langu je vitu gani muhimu vya kuzingatia kwenye makabidhiano ili isije kuleta changamoto hapo baadae kweny umiliki wangu na ninapo amua kujenga mana binadamu hawaeleweki( wanabadilika) na yeye ndio mwenye hatimiliki asanten.
Ni kweli binadamu hatueleweki, wewe mwenyewe unaweza kumgeuka ukasema eneo lote ni lako, upande mwingine ndugu zake baadaye nao wanaweza kukutimua wakidai nyumba ni ya ndugu yao.
 
Ushataja hatimiliki

Sasa unataka tukushaurije tofauti na kumilikishwa hatimiliki?
 
Kwahiyo unataka Kujenga kwenye kiwanja cha mtu?

Andaa legal document ikionesha kuwa amekupatia sehemu ya Ardhi yake bure na ukubwa wake isainiwe na Wakili au hakimu na kugongwa muhuri wa Wakili au hakimu shughuri imeisha.

Ila ukitumia hakimu mahakamani ni bora zaidi mawakili wamekaa kipesapesa tu.mkuu kama ulikuwa hujui kimsingi hakimu haruhusiwi kushuhudia mikataba sababu ana conflict of interest. Embu jiulize umetokea mgogoro juu ya hiyo ardhi na umepelekwa mahakamani kwa hakimu aliyeshuhudia huo mkataba itakuaje. Nadhani jambo la mhimu kwa jamaa ni kwenda kwa wakili aandaliwe hati ya zawadi na katika kuandaa mkataba kama huyo jamaa anamke basi nae asaini kuridhia ardhi hiyo itolewe lasivyo baadae kunaweza kuibuka migogoro isiyo ya msingi
 
Haitakua mbali na ule msemo wa chakuazima hakisitiri.
Uwezekano wakuwa mtumwa wake ni mkubwa mno.

Endelea kulipa kodi ndugu yangu mpaka utakapo jaliwa, weka nia ya kuwa na cha kwako na si cha kupewa, Mungu huibariki na kuufanikisha nia njema.
 
Habarini wana jf! Kama kichwa cha habari kinavyojieleza mm naish maeneo flani ya mji sasa ninarafiki yangu yupo vizuri kidogo kwa kuwa tuna urafiki wa muda mrefu rafiki yangu kwa kuon natesek na kodi anataka kunikatia kipande kidogo cha eneo lake ili ni jenge sasa swali langu je vitu gani muhimu vya kuzingatia kwenye makabidhiano ili isije kuleta changamoto hapo baadae kweny umiliki wangu na ninapo amua kujenga mana binadamu hawaeleweki( wanabadilika) na yeye ndio mwenye hatimiliki asanten.
" VYA KUPEWA UVISHIBISHI UKIPEWA LAZIMA UKUMBUSHWE"

Kuwa makini na rafiki yako maana neno rafiki lina kinyume chake ila.

neno ndugu mpaka leo hii sijajua kinyume chake
 
Wewe utakuwa mvamizi tu,kujenga kwenye eneo la mtu,maana hata miliki inasoma jina lake labda akumilikishe kisheria,na ninanvyohisi ukianza kumwambia mpekekane kisheria atakuwa mzito sana
 
Alichofanya ni sawa ila kwa Mimi ningeon angeend kukununulia kiwanja nje ya eneo ambalo anamilik yeye kwasababu
Kulind utu wako
Kuepush migogor ya ki familia zenu
Anunue kwa hati ya jina lako

Usikubal ukae karbu na rafk yako hata cku moja inabd muw na umbali wa kupand ata gari
 
Tafuta mwanasheria akuandalie deed of gift, hiyo transfer inakubalika kisheria, na ye ukimwambia anaelewa...
Deed of gift ni according to love and affection so hakuhuzii anakupatia tu bure, hiyo document iwe na muhuri wa mwanasheria, wa Donor(ambae anakupatia) nw Donee (wewe unaepokea) na sahihi za mashahidi pande zote mbili. Kama upo Dar naweza kukusaidia kwa hilo
 
Ni kweli binadamu hatueleweki, wewe mwenyewe unaweza kumgeuka ukasema eneo lote ni lako, upande mwingine ndugu zake baadaye nao wanaweza kukutimua wakidai nyumba ni ya ndugu yao.
Hii ni kweli kabisa. Nina ushuhuda kuna mtu aligawiwa kiwanja ili ajenge kwa kuhurumiwa tu. Kwa kuwa mmiliki wa kiwanja alikuwa mbali (nje ya DSM) baadaye aliyegawiwa sehemu ya Kiwanja akawa anafanya ujanja ili alimiliki eneo lote. Kwa bahati nzuri document za umiliki zilikuwa vizuri na zilimsaidia Mmiliki Halali wa Kiwanja hicho.
 
Ujenzi una mavitu mengi mengi unaweza ukakata tamaa maana bajeti haijawahi kuwa sawa na makadirio ,bidhaa za ujenzi zina high inflation rate
 
Back
Top Bottom