Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Nina rafiki ninayefanya naye kazi, sasa kutokana na ubize wa kazi pamoja na mkewe, waliamua kufunga kamera kwenye nyumba yao ili waweze kujua kinachoendelea wanapokuwa nje ya nyumba.
Nyumba yao ni ya vyumba vitatu, ambapo kimoja anatumia msaidizi wa kazi za ndani ambaye pia analala na mtoto wao mwenye miaka mitatu, na anasema lengo la kufunga ni kwa ajili ya ulinzi wa binti yao huyo.
Binafsi nimemwambia kuwa anazingua kwani kufanya hivyo ni kuvunja faragha ya dada. Nimemuuliza endapo na yeye angekuwa huru kubadili nguo na kulala chumba ambacho anajua kina kamera za ufuatiliaji, akajibu hapana.
Nimemueleza kuweka kamera za ufuatiliaji kwenye chumba cha mfanyakazi wa ndani ni suala nyeti la kisheria na kimaadili, ingawa ana haki kulinda bintiye na mali zao, lakini kufunga kamera mahali pa faragha kama chumba cha kulala au choo ni ukiukaji wa haki za faragha.
Ni bora zaidi kuweka kamera katika maeneo ya wazi ya nyumba ili kuhakikisha usalama wa watoto na mali bila kuingilia faragha ya mfanyakazi wa ndani.
Pia soma Kamera (CCTV Camera) ndani vyumba vya kujaribishia nguo ktk duka la Mr. Price, ni sahihi?