Rafiki yangu kamfumania mkewe gesti

Rafiki yangu kamfumania mkewe gesti

Nawasalimia wadada mliopo kwenye ndoa.

Wale wachepukaji kama dada tajwa hapo juu. Mtasalimiwa na wauza chips
 
Kitu ameumbiwa mtu kwa mapenzi yake anampa mwingine atumie na si kuondoka nacho unakuta kuna mtu anaumia wengine kujinyonga du!
 
Nimetumia masaa karibu 8 siku ya jumamosi tarehe 25/1/2020 kumpa ushauri wa kisaikolojia, rafiki yangu ambaye ijumaa ya tar 24/1/2020 alimfumania mkewe Gesti majira ya saa 1 jioni hapa Morogoro.

Mkewe aliaga anakwenda msibani amefiwa na mtoto wa binamu yake, hivyo siku ya kwanza alishinda humo mpk jioni. Ila siku ya pili yake ambayo ni ijumaa, mkewe aliaga anaenda kusaidia shughuli msibani lkn kumbe alifika asubuhi na kuzuga kufanya vishughuli vya hapa na pale kisha akaenda kwa jamaa fulani hiv ambaye ni mchepuko wake.

Mke wa jamaa alionekana akiwa anaingia gesti iliyopo mitaa ya Kihonda hapa Morogoro hivyo inasemekana kuna mtu aliyekuwa anamfahamu alivujisha taarifa kwa mumewe. Jamaa mwenye mke alikuwa mbali wilaya nyingine hivyo alichelewa kufika eneo la tukio mida ya saa 1jioni. Alipofika gesti alikuta jamaa ameshaondoka na mkewe alikuwa anamalizia kuvaa nguo.

Hivyo jamaa alimpiga sana mkewe mpk watu waliopo karibu walivamia chumbani na kuamua ugomvi. Hivyo jambo hili limemuuma sana jamaa kwani mpaka sasa amekuwa ni mtu wa mawazo na kulewa sana. Mke wake hajulikani alipokimbilia.

Wanawake tafadhalini sana heshimuni ndoa zenu!

Sent using Jamii Forums mobile app
mwanamke ni mtu mzima kama anacheat ni kumpa nafasi tu afanye anayotaka si kumpiga.
 
Mimi nilishamwambia wife ikiwa nimembamba na mchepuko iwe kwa njia ya SMS, Fb au popote pale muda huohuo ndio mwisho wa ndoa yetu, simpigi. Wife ananiogopa kama ukoma.
Huyo sasa ana mawazo ya nini huku mke kakimbia ndoa yeye mwenyewe?
Umtendee mwenzako upendavyo kutendewa naye...

Jipe moyo maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom