Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Rafiki yangu wa siku nyingi Salvanus Kamugisha ni mtu tuliyeshibana.
Licha ya sote kutoka kanda ya ziwa lakini misimamo yetu kimaisha ilikuwa inalingana.
Kwa miaka mingi tatizo la Salva lilikuwa langu na la kwangu lake.
Hivyo basi jana jumamosi jioni nilipomkuta anakata bia mbimbili za mnyama Serengeti nikamuuliza kulikoni.
Siku mbili kabla, alinitonya kuwa harusi ya mpwawe imeahirishwa ghafla, nami nilimchangia vizuri kama rafiki.
Pale bar, Serengeti Lager chupa kubwa zilikuwa zimeadimika hivyo akawa anabugia tule tu emolo Serengeti lager(tule tudogo).
"Omwami" nilikuwa nimezoea kumwita
"Mbona unatumeza tu emolo kama unafukuzwa" nili muuliza.
Salva akachukua kale kaserengeti ka pili na kukanywa koote kwa mafundo makubwa makubwa hadi kumaliza.
Alipovuta pumzi ndio akaanza kuniambia stori.
Yule Mpwawe kawaingiza mjini.
Alianzia mbali kwanza.
Jumapili iliyopita walifanya kikao cha mwisho cha ndoa ya mpwawe Gregory, naye Salva Kamugisha ndio mwenyekiti wa shughuli.
Mpwawe Gregory ni kijana wa mujini hivyo kuamua kutulia kwa kuoa ndugu walifurahi sana.
Wengi wachanga michango ingawaje midogo midogo maana familia yao si watu wenye uwezo sana hivyo shughuli ilikuwa sanasana ni ya wanandugu.
Mpaka wiki iliyipita zilikuwa zimepatikana cash milioni 12.
Gregory akiwa anaaminika kama mjuaji town , akaaminiwa kumtafuta MC-msema chochote, ukumbi, Chef wa kujua vyakula vya kihaya na hata vinywaji.
Hata mtu wa mapambo Gregory aliwaaminisha kuwa mchumba wake anamjua mama mmoja wa uhakika.
Hivyo basi mweka hazina akatuma jumapili 50% ya fedha za shugguli kwa watoa huduma on condition kwamba jumatano wamaliziwe jumatano.
Gregory akawaambia wana kamati wakutane ukumbini alhamisi ili kuona jinsi matayarisho yalipofikia.
Kweli wanakamati walikubaliana, na ukumbi ule wanaufahamu vizuri.
Mimi nikaanza kumtazama Salva Kamugisha na kumwuliza sasa tatizo lenu nini?
Salva akaniambia brother tulia tu nimalize.
Basi ikafika siku ya alhamisi na Salva akaamua kuwahi ukumbini.
Akakagua na kumuuliza mhudumu kama anaijua shughuli ya jumamosi.
Mhudumu ukumbini akasema ndiyo, ile shughuli ya kina Massawe?
Kamugisha akamsahihisha akamwambia hapana ni ile yetu kina Kamugisha na Byarugaba.
Mhudumu akakana katakata kuwa shughuli hiyo hajaisikia, pengine ukumbi mwingine.
Kwa kuchanganyikiwa Salva Kamugisha akaanza kumtafuta Gregory kwenye simu.
Akaipiga simu zaidi ya mara kumi.....yenyewe ikawa inaimba tu kuwa simu hii haipatikani.
Wajumbe wengine wa kamati sasa wakawa wamefika na kuuliza kulikoni.
Salva Kamugisha akawaambia Gregory hapatikani kwa simu zake zote.
Wajumbe baada ya kikao kifupi wakakubaliana wawapigie serce providers wote na walichogundua kikawashitua.
MC na muziki....hapatikani!
Chef wa vyakula ....hapatikani!
Mtu wa vinywaji....hapatikani!
Mtu wa matenti na mapambo .....hapatikani!
Kamugisha akapanick, akaamua mchana huo huo kumfuata Gregory nyumbani kwake alikopanga, Mbezi Luis.
Kule Mbezi Luis mwenye nyumba ambaye naye alikuwa anaishi hapo hapo alimwambia Gregory alihama jumatatu!
Na hajui kahamia wapi.
Kwa kuchanganyikiwa Salva Kamugisha akawa na jambo moja tu la kufanya-kutoa taarifa polisi.
Lakini ndugu wakamsihi avute subira pengine kesho yake ataonekana.
Wakati huo huo Kamugisha akawa na kazi nzito ya kuwaeleza waliochanga kuwa shughuli imeahirishwa hadi pale hali itakaporuhusu na kuwa Gregory anaumwa sana!
Siku ya pili ijumaa bado si Gregory au watoa huduma walikuwa wanapatikana kwa simu.
Ilibidi waende polisi.
Baada ya kutoa taarifa polisi , polisi waliwaomba warudi mchana wapate kufuatilia suala zima.
Mchana waliporudi polisi waliwaambia wamepata fununu lakini warudi tu jumamosi watakuwa wamepata picha nzima.
Sasa leo jumamosi ndio polisi wamefuatilia simu zote.
Gregory bado kazima simu ila walimpata usiku wa manane ijumaa.
Zile simu za service providers zote zilikuwa ni za Gregory mwenyewe.
Hela yote ya shughuli kaikusanya mwenyewe Gregory.
Kati ya 12 zilizokusanywa Gregory alitumiwa milioni 11(1 million) alikusanya mwenyewe..
Na yayari alisha zitumia, kanunua Mark II ya zamani kwa milioni 5, kanunua samani na tayari anaishi na kakidosho supa nyumba nyingine ya kupanga.
Mimi nilimwonea huruma Salva Kamugisha lakini naadaye nilicheka mpaka machozi yakanitoka.
Na bado nikiifikiria mkasa nikaendelea kucheka mpaka nikaangusha glasi yangu ya Serengeti...!!!
Salva Kamugisha naye ikabidi aanza kucheka tu baada ya kumwambia , ndugu yangu, hii ni bijampora no. 2.